"Mchungaji" huyu anasakwa kwa uhusika na mauaji ya albinoTafsiri: 

Mimi sishangazwi hata kidogo. Viongozi wa Kanisa na wanasiasa wakubwa wanashiriki katika mila hii ya kishetani. Kiongozi mmoja mkubwa wa kanisa mwenye usharika mkubwa jijini Dar es Salaam, anayemiliki benki, alikamatwa akiwa na albino amefungwa nyuma ya gari lake. Alitoroka eneo la tukio na kesi yake haikuripotiwa kwa sababu alitoa rushwa. Yeye pia ni muuza madawa ya kulevya mkubwa na mtakasaji fedha haramu. Kwahiyo tunatarajiwa Umoja wa Mataifa utaanza kuwafungulia watu hawa mashtaka ya ukatitili dhidi binadamu ili Watanzania walichukulie suala hili kwa makini.

Kwa umoja wetu na upendo wetu kwa ndugu zetu albino, tuunganishe kumsaka mwanaharamu huyu anayejiita mchungaji ilhali anafanya matendo ya kishetani.

Mie ni muumini katika nguvu ya umma. Na nguvu ya umma si kuandamana tu bali hata katika kufichua maovu katika jamii. Ni na imani ya asilimia 100 kuwa kuna mtu au watu flani, sehemu flani wanamfahamu 'mchungaji' huyu. Kadhalika ninaamini kuna mtu au watu flani wanamfahamu mwanasiasa au mfanyabiashara au mganga au muuaji anayejihusisha na mauaji ya albino. Sasa pengine hofu ya kumripoti inachangiwa na kuchelea matokeo hasa ikizingatiwa kuwa polisi wetu hawaaminiki.

Tutumie nguvu ya umma. Kama una taarifa ya uhakika (ikiwa na uthibitisho itakuwa vema zaidi) basi ninaomba uwasiliane nami kwa barua-pepe CHAHALI at ABOUT dot ME au nitumie meseji Facebook evarist.chahali.1 au nenda kwenye tovuti hii swarmsecret.com kisha tweet kwa @chahali nami sio tu nitaweka hadharani suala hilo bali nitatumikia kila tone la nguvu zangu kuhakikisha mtu huyo anachukuliwa hatua za kisheria, ndani au nje ya Tanzania yetu.

Vinginevyo, ukifanikiwa kupata taarifa za mchungaji huyo au mtu yeyote anayejihusisha na unyama huo,

Kwa pamoja tunaweza katika hili

SHUKRANI: Asante Ndugu Alfred Kiwuyo kwa kutufahamisha kuhusu habari husika.

Lori lavunja tena daraja la Kinyerezi


Mitandao ya kijamii imebeba habari kuwa daraja linalounganisha Kinyerezi na Majumba Sita jijini Dar es Salaam limevunjika tena baada ya kupita lori lililokuwa limebeba zege. Daraja hilo lilivunjika pia Juni mwaka jana baada ya lori lililokuwa limebeba kontena kupita eneo hilo.

[video] Is this Calgary's worst driver?The video uploader included this text in the description: The man in green top is the owner of red car. He helped the driver of silver BMW without knowing that she damaged his car before he arrived. She drove away without saying anything.

You may click here to see the damage on the red car.

Barua ya Maaskofu Tanzania kuhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa

BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA 

BARUA YA KICHUNGAJI

“Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu” (Lk. 21: 19)

Sisi Maaskofu wenu tulikutana kusali na kutafakari pamoja huko Arusha tarehe 16 – 17 Februari 2015. Moja ya mambo tuliyoyazingatia ni suala lililo mbele yetu, la kupigia Kura ya Maoni Katiba Inayopendekezwa.

Tunazidi kuendelea kukumbusha kwamba Katiba ni chombo kitakatifu, kinacholenga kufikia maridhiano kama taifa juu ya namna tunavyotaka kuishi pamoja kwa amani na utulivu.

Tunapotafakari kipindi chote cha mchakato wa kuunda Katiba, tunaona mazuri mengi yamefanyika. Lakini yapo mambo mengine ambayo yamefanyika na yametugusa na kutufanya tuhofie namna mambo yanavyoweza kujengeka na kuleta madhara katika nchi yetu. Hali hiyo inatulazimu kujiuliza kwa tafakari: Je, tutaweza kuendelea kudumisha amani na utulivu?

1. Mashaka yetu

Hadi sasa Katiba Inayopendekezwa haijawafikia watu wengi.
Hatua muhimu mno ambayo ni kuelimisha watu juu ya Katiba Inayopendekezwa haijafanyika, kwahiyo wananchi wengi hawana ufahamu wa kutosha juu ya maudhui na misingi yake.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapigakura halijafikia hatua yenye mwelekeo wa kulikamilisha. Hii inatupa mashakama kubwa sana na hatuwezi kuamini kuwa zoezi hilo litakamilika kabla ya tarehe ya kupiga kura ya maoni.

Katika hali hii tunabaki na mahangaiko na mashaka makubwa ya kutakiwa kupigia Kura Katiba Inayopendekezwa ambayo hawaielewi kikamilifu wala kujua matokeo yake kwa mustakabali wa Taifa letu.

Tunajiuliza, katika mazingira kama haya amani haitatetereka? Bahati mbaya sana wanasiasa viongozi wa nchi wanaendelea kutoa maelezo ya kisiasa yanayotoa majibu mepesi kwa maswali magumu, kwa lengo la kufanikisha malengo yao binafsi ya kisiasa. Huu siyo muda wa kufanya hivyo!

Pamoja na mahangaiko na mashaka juu ya suala la Katiba, bado yapo mambo mengi mazito yanayoleta fadhaa kwa jamii yetu:

  • Mfululizo wa matukio ya mauaji na/au kunyofolewa viungo ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (Maalbino).
  • Kuibuka kwa makundi ya wezi na vibaka wakijigamba na kujipachika majina kama panya road, mbwamwitu.
  • Uvamizi wa vituo vya polisi ambapo watu hujeruhiwa wakiwemo askari, na hata kuuawa na silaha kuporwa.
  • Matumizi ya nguvu kupita kiasi yafanywayo na vyombo vya sheria na vyombo vya ulinzi dhidi ya mikusanyiko ya watu.
  • Hali ya wasiwasi na hofu inayoendelea kujengeka miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali, ambayo inaonekana matokeo yake ni kuligawaTaifa.
  • Mifumo ya kutoa haki inakwama mno kutokana na mienendo ya kifisadi inayozidi kuota mizizi.
  • Taasisi za Serikali zinashindwa kuwapatia wananchi wengi haki zao za msingi.

2. Msimamo wetu juu ya Mpango wa Kura ya Maoni.

Tuangaliapo hali ya nchi yetu leo, tunapata hofu kwamba uharakishwaji wa zoezi hili unaongeza fadhaa na mpasuko ambao tayari upo katika jamii yetu. Watu watawaka hasira kwasababu wanaelewa maoni yao waliyotoa na kuzingatiwa na Rasimu II (ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba) hayakuheshimiwa. Badala yake matakwa ya kisiasa ya watu wachache ndio yamepewa uzito mkubwa katika KatibaInayopendekezwa. Katika muktadha huu msimamo na Ushauri Wetu ni:

Zoezi la kupitisha KatibaInayopendekezwa lipewe muda zaidi/liahirishwe, na kufanyika baada ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2015.

Tuonavyo sisi, sio jambo la busara kuendelea kuwataka watu kupigia kura kitu wasichokijua. Ikiwa watawala wataendelea kulazimisha, basi wananchi wajitokeze na kupiga kura ya kuikataa Katiba Inayopendekezwa.

Bado tunakumbuka vizuri, jinsi mchakato wa kupata Katiba mpya ulivyoendeshwa kupitia Bunge Maalum la Katiba. Kwa ufupi, uadilifu ulikosekana, dhamiri za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ziliingiliwa na wengi wao kulazimishwak utenda kwa hofu na unafiki, uwazi ulikosekana, sheria haikuzingatiwa na roho ya sheria yenyewe haikupewa tafakari stahiki.

Tunabaki kujiuliza motisha wa viongozi wa kisiasa na serikali kulazimisha maoni yao ulitokana na nini? Je, walisukumwa na moyo wa uzalendo ama matakwa ya kibinafsi? Bado tunaamini kuwa walisahau kwa makusudi kwamba suala hilin linadai uwajibikaji mkubwa kwa ajili yaTaifa letu.

Hitimisho

Tunawasihi waumini wetu kuendelea kuombea amani taifa letu na kufanya kila linalowezeka ili kuimarisha na kudumisha amani.

Tunaiomba Serikali kutumia mamlaka yake na vyombo vyake vya sheria na vya ulinzi na usalama kujenga amani na kuhimiza ushiriki wa watu wote katika masuala yanayolihusu Taifa letu.

Tunawasihi viongozi wa dini zote na kuwatia moyo watambue kwamba wao ni wadau wa kwanza katika kujenga umoja na moyo wa kupokeana kwa stahamala bila kujali tofauti zetu za kidini.

Tunaendelea kukazia UTAKATIFU wa mchakato wa kuunda Katiba ambayo lazima iwe chombo cha kulinda tunu na matakwa/matamanio ya watu wote, na sio ya wachache tu.

Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, name nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta, nakuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote (Yer 29: 12 – 13).

Imetolewa na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki – Tanzania
Tarcisius Ngalalekumtwa
RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA

After collapsing on podium, Zambia's Pres. Lungu will have treatment abroad

Edgar Lungu

ZAMBIA’s leader Edgar Lungu will have treatment abroad for throat surgery, the presidency said Monday, only a day after he was diagnosed with malaria after falling in public.

Lungu collapsed on the podium while presiding over a Women’s Day celebration in Lusaka Sunday, and an official statement later said he was receiving treatment for malaria and there was no need for concern.

“I am feeling much better and have been told I have high levels of fatigue and should take some rest,” Lungu was quoted saying, adding: “There is nothing to worry about.

He later told a press briefing at the hospital: “I am looking forward to going home. Doctors have done their tests and they have found traces of malaria, but they are doing further tests and they will let me know what next after before the end of the day.

The latest statement on Monday said he was suffering from a narrowing of the oesophagus which needed “high-tech medical procedure which is currently unavailable in Zambia”.

“There he has been referred for specialised treatment abroad,” it said, but did not specify when he would have the operation.

It added that this was a recurrence of a condition for which he was treated 30 years ago.

In another country, a bout of presidential ill-health and the shifting diagnoses might have been shrugged off easily. Not Zambia.

Lungu came to power in January after the death in office of president Michael Sata, then 77, in October.

Read more: mgafrica.com

Mbowe akihutubia Kahama jioni ya leo...


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wakazi wa Kahama jioni hii


Sending money to Kenya? M-Pesa it!

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania, March 9, 2015 : Over 7 million M-Pesa customers in Tanzania and over 18 million Safaricom customers in Kenya can now send and receive money from each other. This revolutionary service allows for mobile wallet to wallet transfers between the two largest telecom operators in East Africa. Now, customers can transfer funds across the border at the same rate as sending money locally.

Speaking in Dar es Salaam, Vodacom Tanzania’s Managing Director said available statistics indicate that over TZS 200 billion is sent from Tanzania to Kenya annually , while the latter sends over 26 billionto Tanzania. “Statistics from the World Bank, (2013) indicate that Tanzania sent approximately TZS 200 billion to Kenya through formal channels. Estimates would indicate that more than twice that amount was transacted via informal channels including bus drivers, friends and family” stated Meza.

“We have looked into the hurdles that our customers need to overcome in order to send and receive money across to our neighbors in Kenya and have come up with a safe, secure and convenient way to do so. From today one doesn’t need to send money by suka wa basi au konda or incur hefty charges to transfer school fees, buy goods or settle business payments, he or she can do so directly from their M-Pesa wallet and… from the comfort of their home, anytime the need arises , ” says Meza.

For his part, Safaricom’s Chief Operating Officer Bob Collymore said “We believe that we have launched a new chapter in the continuing growth story of M-Pesa Enabling transactions between Kenya and Tanzania will make it ever-more convenient for businesses and individuals to transact across borders and unleash the transformative power of a first of its kind cross-border payment system.”

“Vodacom customers will from today be able to send and receive money to and from Kenya through the same process that they are already used to. Their experience is the same as that of sending money nationally, the only difference is that a customer can now choose option 3 - send money to M-Pesa Kenya- and enter the mobile number beginning with the +254…prefix,” added Meza. “Even before the money is sent, the customer will be shown the Kenyan Shillings equivalent value of the money that the customer in Kenya will receive. The currency conversion will happen immediately and the money will be available instantly for withdrawal or making bill payments, buying airtime or any other services on M-Pesa” he added.

M-Pesa is offered by Vodacom Tanzania Limited and Safaricom in Kenya – the region’s two biggest telecom operators. Vodacom has approximately 65% market share of mobile financial services in Tanzania whereas Safaricom commands over 80% share in Kenya. Meza further says, “Our combined distribution of over 150,000 agents in Tanzania and Kenya will ensure that our customers continue to enjoy the many benefits that M-Pesa offers them today. This groundbreaking service in the evolution of mobile financial services as we know it today is supported by a fully-fledged customer service unit that is reachable 24 hours every day.”

“Kenya is Tanzania’s largest trading partner and it was therefore logical that we activate the service there first. This is our own way of further cementing the ties that bind the people of the EAC region,” says Meza. He goes on to say that communication is about connecting people and communities regardless of the geographical barriers that stand between them – something that Vodacom does only too well across the countries where it has a presence around the world.

Tanzania is home to approximately 300,000 Kenyans who remit funds to their home country via informal ways and channels including bus drivers, friends and family. There is also a sizeable part of the Tanzanian population that has chosen to educate their children in Kenya and rely on the very same means to transfer money. “This service will now empower a trader or a small business owner in Kariakoo or any other part of Tanzania to transact with his customers or suppliers in Kenya. For the parents whose children go to school in Kenya, settlement of school fees has been simplified because of this service. Gone are the days that bus drivers, friends and family had to carry cash across the border to settle such dues For all Kenyans who reside in Tanzania today, M-Pesa now makes it easier for them to send and receive money home” added Meza.

“This service will also eradicate the need for people to carry large amounts of money in physical cash. For, it is CONVENIENT, SECURE and DIRECT and reaches the intended person INSTANTLY. This is what Making Life Better is all about. ” says Meza.

Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Dadi (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Isack Nchunda wakimsikiliza jambo Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu Tanzania, James Masoy (katikati) wakati wa uzinduzi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Dadi (katikati) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) baada ya uzinduzi rasmi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu Tanzania, James Masoy.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kulia) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Dadi (katikati) na Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu Tanzania, James Masoy, mara baada ya uzinduzi rasmi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Rais Kikwete aongoza sherehe za Siku ya Mwanamke Duniani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mabanda ya maonesho uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mabanda ya maonesho uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha alipowasili uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 kuongoza kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo

Rais Kikwete akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo


Rais Kikwete akipokea maandamano ya kinamama katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo


Rais Kikwete akiongea na mtoto Miriam Edward mwenye ulemavu wa jicho ambaye alitoa burudani katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo

Rais Kikwete akiongea na mtoto Miriam Edward mwenye ulemavu wa jicho ambaye alitoa burudani katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo

Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba akimkabidhi Rais Kikwete tuzo maalum ya Wanawake kwa mchango wake mkubwa wa kujali maslahi ya kinamama katika jamii katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 katika kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo.

Mama Maria Nyerere azungumza na TBC kwa kuzushiwa kifoMama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amezungumza na kituo cha runinga cha Taifa, TBC na kukanusha uvumi ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameaga dunia.

Akizungumza na mwandishi, Mama Nyerere amemwuliza, "ukiniangalia unanionaje?" ambapo wmandishi alijibu, "nakuona mzima!" huku wakitabasamu.

Mama Maria amesema ni mwaka wa uchauguzi huu kwa hivyo mambo haya ya uzushi si ya ajabu.

Kwa taarifa zaidi, tizama taarifa za TBC.

Kabla ya uvumi wa kizushi kuhusu Mama Maria, juzi kupigia WhatsApp ulikuwa ukitumwa ujumbe mwingine wa kumzushia kifo Reginald Mengi, Mwenyekiti wa makampuni ya IPP.


Taarifa ya Julius Mtatiro ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge Segerea

Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.

Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.

Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.

Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.

Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.

Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0

Julius Mtatiro, +255 787 536 759, 0755 855 144, [email protected]

Julius Mtatiro,
Cert in Linguistics (Nairobi), B.A (Hons) - Dar, M.A(Hons) - Dar, LLB (Candidate) - Dar,
Freelance Translator and Private Consultant in
Administration, Education and Political Science.
P.O Box 10979,
Dar Es Salaam,

Phone; +255717536759, +255787536759

Email; [email protected]

Mapato yaliyopatikana katika mechi ya Simba vs Yanga

Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.

Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.

Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.

Wakati huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.

Siku ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Azam FC.

Aidha mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)