Pres. Obama's answer on finding success...

Barack Obama, 44th USA President
Barack Obama, 44th USA President

When asked, “When is the time you felt most broken?” his reply was...

“I first ran for Congress in 1999, and I got beat. I just got whooped. I had been in the state legislature for a long time, I was in the minority party, I wasn’t getting a lot done, and I was away from my family and putting a lot of strain on Michelle. Then for me to run and lose that bad, I was thinking maybe this isn’t what I was cut out to do. I was forty years old, and I’d invested a lot of time and effort into something that didn’t seem to be working. But the thing that got me through that moment, and any other time that I’ve felt stuck, is to remind myself that it’s about the work. Because if you’re worrying about yourself—if you’re thinking: ‘Am I succeeding? Am I in the right position? Am I being appreciated?’ — then you’re going to end up feeling frustrated and stuck. But if you can keep it about the work, you’ll always have a path. There’s always something to be done.”

FRIDAY 6 FEBRUARY 2015

Quote source: humansofnewyork.com

Poem: If I Could Be Someone Else


If I could be someone else

If I thought less
If I felt less

Less of you

Would it matter
Would it shatter

The lock in your heart

If I can be someone else

If I think more
If I feel more

More of me

Will you care
Will you dare

To open your eyes

If we could be somewhere else

If we thought more or less
If we felt more or less

More or less of us

Shall we prop
Shall we stop

To close our minds

If we can be somewhere else

If we think more and more
If we feel more and more

More and more of you and I

Shouldn't we rally
Shouldn't we try

To live happily ever after

Poem shared by CHAMBI CHACHAGE

Mwekezaji achomewa mali kwa mara ya tatu Babati

Mjengwa: Nimepokea kwa masikitiko kufukuzwa kwa Zitto

Nimepokea kwa masikitiko taarifa kuwa ndugu yangu Zitto Kabwe amefukuzwa kwenye chama cha Chadema. Ni habari ya kusikitisha unapotafakari demokrasia tunayojitahidi kuijenga.

Zitto amekuwa mwanachama wa Chadema tangu akiwa kijana mdogo. Mwenyekiti wa chama hicho , Freeman Mbowe, amenukuliwa mara kadhaa akikumbushia jinsi alivyoshirikiana na Zitto kuhamasisha vijana wengine waliokuwa vyuoni kujiunga na Chadema.

Kwenye siasa za vyama kuna kutofautiana kifikra na kimitazamo. Na mara nyingine migongano huwa inahusu kugombania nafasi za uongozi. Haya ni mambo ya kawaida kwa chama cha siasa. Hayapaswi kuwa sababu za viongozi wa vyama kuwafukuza wanachama.


Kwenye siasa tofauti humalizwa kwa hoja, kwenye vikao. Na anayekiuka taratibu za chama kumfukuza kwenye chama ni adhabu kubwa na kali kama ya kifo. Maana, anayejiunga na chama hufanya hivyo kwa mapenzi. Anapokosea anaweza kuonywa au kuadhibiwa, lakini, kufukuzwa kwa misingi ya kutofautiana kifikra na kimitazano si hulka njema.

Zitto Kabwe ni mwanasiasa kijana na mahiri. Chadema ilipaswa imvumilie na ishindane nae kwa hoja, lakini, si kumtupa nje kwa staili tuliyoishuhudia.

Chadema, kama chama cha siasa, isijiandalie mazingira ya wanachama wake kuwa na hofu ya kufukuzwa pindi wanapotofautiana na viongozi wa juu. Itapoteza kisiasa.

Na hili la Zitto Kabwe linatukumbusha kile ambacho binafsi nimeandika mara kadhaa, juu ya udhaifu kwenye Katiba yetu. Kwamba Mbunge aliyechaguliwa na Wananchi anaishi kwa hofu ya rungu la chama.

Kwamba leo Wananchi wa Kigoma Kaskazini wanampoteza Mbunge wao waliyemchagua kwa maamuzi ya Chama anachotoka Mbunge wao. Haya ni mapungufu makubwa. Wananchi hapaswi kuadhibiwa kwa maamuzi ya vyama.

Nachukua fursa hii kumtakia kila la heri ndugu yangu Zitto Kabwe, nikimuasa asikate tamaa, akipata fursa nyingine, aendelee na siasa na hususan uongozi wa uwakilishi wa wananchi. Aendelee kuwa sauti ya wasio na sauti, popote pale.

Maggid Mjengwa,

Dar Es Salaam.

[video] Marando aeleza walivyomgundua 'mlinzi jasusi pandikizi' wa Dk Slaa

NHC now selling Victoria Place apartments in Kijitonyama


Greetings from National Housing Corporation.

Please be informed that VICTORIA PLACE apartments located at Kijitonyama along New Bagamoyo road are now selling. For further details please visit www.nhctz.com/victoriaplace

Below are payment options:

1.      Mortgage Payment Plan(MPP)
·        The home buyer, after completing house application form and depositing at least 10% of the Purchase price, will be given
·        Letter of Offer-extending 90days for looking for Bank loan/Mortgage
·        Agreement of Sale will be issued after the Bank has paid into NHC account the Balance Purchase Price.
·        Other steps towards obtaining Unit Title (multiple steps)
2.      Progressive Payment Plan(PPP)
·        The home buyer, after completing house application form and depositing at least 10% of the Purchase price, will be given
·        Letter of Offer-which requires the buyer to:
ü  Pay 20% after 3 months
ü  Pay the remaining 65% in a number of installments covering the whole construction period(depending on kind of project))
ü  Pay 5% after project completion/before handover.
·        Other steps towards obtaining Unit Title (multiple steps)

In case you wish to deposit full amount cash, we appreciate and welcome you as well.

Please feel free to contact me on 0786 563 017 should you require more clarifications on the above. You may as well forward this to your colleagues, family and friends who might be interested too.

We thank you for choosing NHC as your housing developer.

Barua ya mkwara wa Maseneta wa Marekani kwa uongozi wa juu wa Iran


Ni barua waliyoitia saini Maseneta 47 wakiionya Iran kuhusu mazungumzo ya kutafuta muafaka kuhusu utengenezaji wa bomu la nyuklia, wakionya kuwa maamuzi yoyote yatakayofanywa baina yao na Rais Barack Obama yatahitaji kupitia katika Seneti kabla na yanaweza kufutwa mara moja na Rais atakayemrithi aliyeko madarakani wakati huu.

Barua hii imeamsha hisia za kukerwa kwa baadhi ya viongozi wa chama cha Democratic huku baadhi ya Wabunge na Maseneta wa Republican wakikwepa kuweka saini zao kuidhinisha kilichoandikwa.

Baadhi ya wananchi wanaona hii ni dharau kwa Rais aliyeko madarakani, ingawaje wengine wanaona ni sawa na hatua sahihi.IS watoa video inayoonesha mtoto akimuua mtuhumiwa ujasusi wa Israel


Kundi la Dola la Kiislam (IS) limefyatua video inayomwonesha mtoto wa umri wa miaka 12 akimwuua jasusi wa taifa la Israel aliyekiri kufanya kazi katika shirika la ujasusi la nchi hiyo, Mossad.

Video iliyochapishwa na kundi hilo kwenye tovuti ya Twitter siku ya Jumanne jioni inamwonesha mwanaume aliyeketi na kutambuliwa na familia yake kuwa ni Muhammad Said Ismail Musallam mwenye umri wa miaka 19 akikiri kuwa aliajiriwa na shirika hilo la ujasusi la taifa la Kiyahudi. Alitamka pia kiwango cha fedha alizokuwa analipwa.

Inasadikiwa kuwa Musallam aliyekuwa akiishi Mashariki mwa mji wa Yerusalemu, ndiye ambaye IS walidai mwezi uliopita kuwa wamemkamata jasusi wa Mossad.

Musallam anaonekana kwenye video akidai kuwa aliandikishwa na jirani yake ambaye ni afisa Polisi, ili kufanya kazi hiyo.

"He came one day and asked me to work with Israeli intelligence," "I told him I would think about it, and then went and asked my father and brother what they thought. They both encouraged me to do it and told me that it was a very good job. They told me there was a lot of money in it, and that you could advance to higher positions. I knew at that point that they themselves were working as spies." 

amekaririwa akisema, Musallam.


Anadai alitumwa na Mossad kujiingiza katika kundi la IS na kutoa taarifa za maeneo ambapo silaha zinahifadhiwa, kambi na majina ya Wapalestina waliopo katika kundi hilo.

Anasema iliwezekana kukamatwa kwa kuwa mwenendo wake ulianza kutofautiana na ile ya wanamgambo wengine, licha ya mafunzo aliyopewa na Mossad.

Baba yake Musallam anadai kuwa mwanaye hakuwa jasusi ila alijiunga na IS kwa mapenzi yake miezi michache iliyopita. 

Watafiti wa masuala haya wanahisi huenda Musallam alifanya jaribio la kuitoroka IS na alipogundulika njama zake ndipo alipotuhumiwa kuwa jasusi na kupewa adhabu ya kuuawa.

Labda cha kuacha hofu zaidi ni pale kwenye video hiyo inapotamkwa orodha ya majina, anwani na ramani za makazi ya mawakala wa Mossad katika lugha ya Kiingereza na Kiarabu.

Vitisho kama hivyo vimetolewa pia kwa marubani wa nchi ya Jordan.

Karibu na mwisho wa video hiyo pia Wayahudi wanaoishi nchini Ufaransa wametishiwa.

Hii ni mara ya pili kwa kundi hilo kufyatua video inayomwonesha mtoto akiua. Mara ya kwanza, mtoto wa Kazakhstan alionekana akiua Warusi wawili ambao nao walituhumiwa kufanya ujasusi.

“In this video, ISIS appeals to the Palestine people saying ‘we haven’t forgotten your plight’ and issues a call to French speaking fighters, saying ‘Your voice is powerful within the state, and your foreign fighters hold key glamorous positions.’ To the English speaking audience, they seek potential recruits and political leaders. To Israel, they say “You are not safe, we know who you are and where you live.”
“Since 2015, Islamic State has been pushing hard its “cub” training program and we’ve seen a significant up tick in ‘graduation’ photo journals, training facilities and one other foreign fighter child executioner,” “The use of a child executioner is significant because ISIS is demonstrating the “growing” Caliphate and that they are raising their next generation of warriors now.”

 amenukuliwa akisema Veryan Khan, editorial director of the Florida-based Terrorism Research & Analysis Consortium

Zitto, CHADEMA failed to capitalize on dividends of law of concentration - Kadulyu

Zitto Kabwe’s case against his party (CHADEMA) has been quashed by the high court...

This will cast a controversial landscape in our politics and a transient of events at this critical time, especially complicated by the fact that after successful delivery on #TegetaEscrow scandle I was expecting Zitto and Chadema to quickly iron out their differences.

Many of us have different views on this matter perhaps we wait and see what this will lead up to. I have a strong conviction that leaders can sometime subdue their interests for the sake of national interest. 

To me I think both Zitto on one side and Chadema on the other have failed us. What would be of utmost importance for the alternative political force in Tanzania was to ensure they steer up the second liberation of our country, whatever follows thereafter is trivial and can be suppressed for this grand purpose. 

Take an example of South Africa, I know there were other heroes more than Mandela who relatively paid the same price as him. Yet these guys (the leaders of anti-apartheid movement) were focused. They all decided to unite and agreed to symbolize their resistance through Madiba. Madiba became the epicenter of change where all all energies were concentrated upon. It doesn't mean that there were no other political prisoners in South Africa, there were many but people like Oliver Tambo and the rest realized the importance of THE LAW OF CONCENTRATION and fully capitalized on it. It finally paid its dividend. Opposition leaders in Tanzania need to understand this law too and use it to the advantage of the citizens of Tanzania.

There is no dispute that Zitto is a formidable politician, he is effective in addressing and dealing with the menaces of the political creed. He carries with him some potential to tackle the most intriguing challenges of our time. 

His success for example in the previous #TegetaEscrow scandle was not by virtual of himself alone rather by the input and contribution from PAC team, members of opposition including Chadema and the support from some of the CCM MPs who have realized that change is inevitable and have accepted to adapt to the direction of the wind. 

His contribution in politics is still important but in my view it will be much more pronounceable within the confines of Chadema, his political birthplace. Many Tanzanians who want change have cultivated their trust on Chadema not only because Zitto was in there but the sum total of all youthful and promising cadres and the consistent message of change. 

Politicians have to learn to live with their differences. Starting a new political party is not a panacea to addressing differences of individual party members as the law of divergence tells that humans are different, that there aren’t two humans who perfectly resemble in everything. 

To me that is Political Entrepreneurship and not health for our young democracy. We expected Chadema to exercise maturity in accommodating each other and especially in addressing those issues Zitto and the rest are complaining about, we too expected Zitto to weigh his ambitions at this material time and exercise wisdom of timing and exploit the advantages of the LAW OF CONCENTRATION.

Kadulyu
via blog

The NEW "Old MacDonald" (in light of GMO products)

Nauli za treni ya Deluxe itakayosafiri Dar - Kigoma, Mwanza

Shirika la Reli Tanzania (TRL) limetangaza nauli ya treni mpya ya Deluxe, zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), zitakazoanza kutumika mapema Aprili, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TRL iliyotolewa jana, nauli hizo ni kutoka vituo vya Dar es Salaam kwenda Kigoma, Kigoma kwenda Dar es Salaam na Mkoa wa Mwanza.

Nauli hizo ni kati ya Sh 77,800 kwa daraja la kwanza ambalo ni la kulala.

Kwa kituo cha Dar es Salaam kwenda Kigoma, nauli zilizoidhinishwa ni kwenda Morogoro daraja la kawaida nauli itakuwa Sh 10,900, daraja la pili nauli itakuwa Sh 14,600 na daraja la kwanza nauli itakuwa Sh 24,300.

Nauli kwenda Dodoma itakuwa Sh 18,500 kwa daraja la kawaida, Sh 24,700 kwa daraja la pili na Sh 41,200 kwa daraja la kwanza, huko nauli kwenda Tabora kutoka Dar nauli ni Sh 25,400 kwa daraja la kawaida, Sh 33,900 daraja la pili na Sh 56,500 kwa daraja la kwanza.

Nauli kwenda Kigoma daraja la kawaida ni Sh 35,700 daraja la pili ni Sh 47,600 na daraja la kwanza ni Sh 79,400 na kwa kituo cha Kigoma kwenda Dodoma nauli ni Sh 23,600 daraja la kawaida, daraja la pili ni Sh 31,400 na daraja la kwanza ni Sh 52,400.

Aidha, nauli kutoka Kigoma kwenda Morogoro ni kati ya Sh 30,900 hadi Sh 68,600 kulingana na daraja na kwamba kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam nauli ni kati ya Sh 6,200 hadi 77,800 kulingana na umbali na daraja.

Mfano, kutoka Mwanza kwenda Malampaka nauli daraja la kawaida ni Sh 6,200 daraja la pili ni Sh 8,300 na daraja la kwanza ni Sh 13,800 na nauli kutoka Mwana kwenda Dodoma nauli ni kati ya Sh 22,800 hadi Sh 50,600 kulingana na daraja.

Na nauli kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam nauli Sh 35,00 kwa daraja la kawaida, daraja la pili Sh 46,700 na daraja la kwanza Sh 77,800.

Awali akizungumzia usafiri huo, Meneja Biashara wa Kampuni ya Deluxe, Charles Ndenge alisema usafiri wa treni hizo ni wa kasi na utatumia saa 30, kufika katika mikoa mbalimbali ambayo reli ya TRL inapita na kusimama kwenye vituo vikubwa 14, kati ya vituo 54, vilivyopo.

Alisema treni hiyo ya Deluxe itafanya safari zake mara moja kwa wiki kwa kupokezana na mikoa ya Kigoma na Mwanza na kuwa itatumia mabehewa yenye ubora na kupunguza msongamano.

“Kutakuwa na behewa moja zuri la huduma za chakula na vinywaji na mawasiliano”, alisema Ndenge.

Akizungumzia muundo wa treni hiyo ya Deluxe, alisema itakuwa na mabehewa 10 ya daraja la tatu, ambapo kila moja litabeba abiria 80, mabehewa manne ya daraja la pili kila moja litabeba abiria 60, wa kukaa na mabehewa sita ya kulala ya daraja la kwanza kila moja litabeba abiria 36.

Aidha aliongeza vichwa vya treni vimejengwa upya na kuwekewa teknolojia mpya na kutengenezwa makochi mapya.

  • via HabariLeo

How Tsh 80/= billion went missing from TanRoads - The Citizen
A total of Sh47 billion out of Sh77 billion deposited at the Bank of Tanzania (BoT) for the purpose of paying road contractors is either missing or cannot be accounted for.

The Controller and Auditor General (CAG) says over Sh33 billion that was set aside for road projects in the 2011/2012 financial year also cannot be accounted for.

This means that a total of Sh80billion is either missing or cannot be traced as there is no proof of payment purportedly made to contractors.

In a special audit, the CAG reveals that Parliament was lied to about the expenditure of Sh252 billion earmarked for the construction of new roads.

The amount was instead diverted to pay road contractors and consultants, according to the January 2015 CAG report.

Impeccable sources told The Citizen in Dar es Salaam yesterday that Sh3,048,365,229 was not accounted for from the total amount of Sh252,975,000,000.

The sources further revealed that after the Ministry of Works released the Sh3,048,365,229 to the Tanzania National Roads Agency (Tanroads), the sum was diverted without the knowledge of the ministry.

“And documents that were used by Tanroads to reallocate this amount (Sh3,048,365,229) were not submitted to relevant authorities for auditing,” said the sources.

In another development, the CAG report said the BoT governor denied to have paid Sh30,599,193,960.28 to Strabag International Gmbh and China Geo-Engineering Corporation Company Ltd.

“This amount was part of Sh77,695,571,182 which was deposited with the Bank of Tanzania as payments to road contractors and various consultants,” said the sources.

They added that the CAG special audit had failed to establish whether Sh47,096,377,221.72 was paid to relevant road contractors and consultants after the BoT governor had refused to give information, saying the law did not allow him to disclose banking information about his clients.

The sources said although the major task of Tanroads was to oversee, construct and improve trunk roads and regional roads, the CAG report had shown that Sh13,385,089,124 was used to pay for private roads and roads under district councils.

“Construction of roads under district councils is done using money from the Road Fund Board,” said the sources.

The sources said the CAG report has also revealed massive misappropriation of funds budgeted for construction of trunk and regional roads during the 2010/2011 financial year.

“In the 2010/2011 financial year some road projects were allocated tiny budgets, but Tanroads spent huge amounts of money to pay for such projects without stating the source of the money,” said the sources.

In another development, said the sources, CAG investigators found that payments totalling Sh36,638,175,000 were not indicated in monthly progress reports by consultants and contractors handling various road projects.

The CAG report further revealed that payment of Sh6,175,786,959 was made to contractors who were not in the list submitted to the Ministry of Works.

“This amount was paid to constructors whose names were not in the list submitted to the Ministry of Works by the chief executive officer of Tanroads,” said the sources.

The CAG report recommended to the Ministry of Works and Tanroads to strengthen their accounts departments in order to be able to establish genuine contractors and consultants that were supposed to be paid certain amounts.

It also recommended the ministry to direct contractors and consultants to make monthly financial progress reports that could do away with controversies when it comes to payments.

The CAG report also recommended that the government enter into new road construction projects agreements and pay all outstanding arrears to contractors and consultants.

The CAG report also recommended to the government to ensure that new road construction tendering should stick on the budget released by the government on yearly basis.

Kuhusu watoto 18 waliokuwa wamefungiwa katika nyumba MoshiSiku mbili baada ya jeshi la polisi kuvamia nyumba moja katika Kata ya Pasua katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, iliyotumika kuhifadhi zaidi ya watoto 18 kinyume cha utaratibu, mmiliki wa nyumba hiyo yenye vyumba vinne na choo kimoja, ameibuka na kujitetea licha ya kwamba anashikiliwa na polisi.

Mmiliki huyo, Abdulnasir Abdulrahman amesema aliwakusanya watoto hao wenye umri wa kati ya miaka miwili na 16 ili kuwafundisha masomo ya dini ya Kiislamu na kuwakuza katika imani hiyo wakiwa wadogo.

Pamoja na utetezi huo, alisema watoto hao wameletwa hapo na wazazi wao kupata elimu ya dini, na wazazi wao wanajua na wanachangia vitu mbalimbali, ikiwemo vyakula ili kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ya dini ya kiislamu,

“Watoto wote tunaoishi nao hapa wana wazazi wao, ambapo wamekubaliana na sisi waaendelee kupata elimu hiyo hapa chini ya uangalizi wetu na wazazi wao wamekubaliana niwalee,” alisema Abdulrahman jana baada ya kukamatwa majira ya saa 5 asubuhi, tukio lililovutia umati wa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika katika nyumba hiyo na hata Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Moshi.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na pia baadhi ya wazazi wa watoto hao kwa uchunguzi zaidi.

Katika nyumba waliyohifadhiwa watoto hao, polisi wenye silaha walilazimika kutumia nguvu na mabomu kudhibiti umati wa wananchi waliojitokeza kushuhudia kukamatwa kwa mmiliki na watoto.

Baada ya kufikishwa polisi, walirudishwa katika nyumba waliyokuwa wamehifadhiwa wakiwa chini ya ulinzi, huku mmiliki na wazazi wakiendelea kubaki polisi.

Jeshi la polisi linawashikilia baadhi ya wazazi na mmiliki wa nyumba hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ambapo baada ya watuhumiwa hao kukamatwa bado mamia ya wananchi hao waliongozana hadi kituo cha polisi. Hadi gazeti hili linaenda mitamboni, bado wananchi walikuwa wamefurika nje ya geti hilo la kituo cha polisi.

Akizungumza na wananchi katika eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga alisema walipata taarifa kuwa eneo la Pasua, kuna mtu mwenye kituo amehifadhi watoto kinyume na taratibu, na ndiyo kamati ya ulinzi na usalama ilifika eneo la tukio na kukuta watoto hao katika nyumba hiyo.

Alisema taarifa ya kuwepo kwa watoto hao waliipata wiki moja iliyopita, lakini juzi Machi 7, mwaka huu, ndiyo jeshi la polisi liliizingira nyumba hiyo kuanzia majira ya saa 12:05 jioni kutokana na kukosa sehemu ya kuwahifadhi watoto hao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwakusanya watoto sehemu moja bila kibali ni kinyume cha sheria, ambapo mmiliki wa nyumba hiyo alipaswa kuomba kibali lakini pia mafunzo anayoyatoa kwa watoto hao hata kama ni masuala ya dini ni lazima yafuate taratibu za nchi.

“Sheria zipo unapokusanya watoto mahala pamoja kunatakiwa kuweje kuanzia mazingira hadi eneo lenyewe, na kama una taasisi unaendesha mafunzo, je, kituo kimesajiliwa na ndiyo maana tumeagiza watoto warudishwe kwa wazazi wao,” alisema Makunga.

  • via HabariLeo

-------------

Jeshi la Polisi wilayani Moshi Mjini, limedai kuwa watoto waliokutwa ndani ya nyumba katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi siyo wakazi wa Kilimanjaro na walikuwa wakiishi kwenye mateso makubwa.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela imeeleza kuwa hayo yalibainika katika mahojiano baina ya watoto na askari wa dawati la jinsia.

Alisema watoto hao wanatoka mikoa mbalimbali ikiwamo Tanga, Mara, Kagera, Mbeya na Dodoma.

Kamanda Kamwela alisema pia wamegundua kuwa watoto walikuwa wakiishi kwenye mazingira magumu ikiwamo kulala chini katika chumba kidogo.

Alisema polisi linawashikilia watu wawili (mume na mke) ambao wanatuhumiwa kuwahifadhi watoto hao.

Kamanda huyo alisema watoto hao wana umri wa kwenda shule, lakini walikuwa hawasomi.

Alisema polisi wanachunguza aina ya masomo ya dini waliyokuwa wakifundishwa.

“Lazima tuchunguze uhalali wa masomo ya dini waliyokuwa wakisoma ili tujue kama kweli watoto hawa walipelekwa na wazazi wao au la, kwa kuwa watoto hao walipaswa kuwa shuleni” alisema Kamanda Kamwela.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga alisema watoto hao walikuwa wakiishi kwenye mazingira magumu, huku wakipewa adhabu kali ikiwamo kubeba matofali mgongoni pindi wanapokosea.

“Maelezo ya watoto yanaonyesha walikuwa wakiteswa, adhabu hizi kwa watoto ni kubwa, bado tunawachunguza ili tujue kila kitu na walichukuliwaje huko majumbani kwao,” alisema Makunga.

Alisema kwa wazazi watakaowatambua watoto wao, wanapaswa kwenda na uthibitisho ikiwamo cheti cha kuzaliwa au uthibitisho mwingine utakaoonyesha ni mzazi halisi.

Makunga alisema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa, watuhumiwa hao wana kituo kingine kinachohifadhi watoto.

Alisema kwa sasa hawezi kueleza zaidi hadi polisi watakapomaliza upelelezi wao.

Majirani 

Aisha Mohamed na Marsela Minja ambao ni majirani wa watuhumiwa walidai kuwa awali nyumba hiyo ilikuwa na mmiliki mwingine, lakini alijinyonga miaka michache baada ya kuuza eneo hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walidai kuwa mmiliki wa kwanza wa nyumba hiyo alikuwa na ujirani mwema na wakazi wa eneo hilo.

Marsela alisema mmiliki wa sasa tabia yake ni tofauti kwa kuwa anawazuia watu kuchota maji na pia kajenga ukuta mrefu kuzingira nyumba hiyo.

Alisema tangu mmiliki huyo ahamie katika nyumba hiyo miaka mitatu iliyopita, hawakuwa na mazoea na jirani yeyote.

Wananchi hao walidai wiki mbili zilizopita mmiliki huyo alifunga ndoa na wao walishuhudia magari mawili ya kifahari yakiingia kwenye geti na baada ya muda yaliondoka.

“Sisi hatuwafahamu sana kwa sababu hutoka na magari wakiwa wamejifunika hadi usoni, hivyo siyo rahisi kuwafahamu...hatujawahi kuwaona watoto wakienda shule wala dukani,” alisema Marsela.

“Ukipita kwa huku nyuma ndiyo utawasikia wakifundishwa masuala ya dini, lakini wakikosea wanapewa adhabu ya kupanda ukuta , lakini hata ukiwasemesha hawajibu zaidi ya kulia,” alisema Aisha.

Mtaalamu azungumza

Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Chris Mauki alisema kitendo cha watoto hao kukosa uhuru na mazingira ya kuchangamana na watu wa aina mbalimbali kitawaathiri kisaikolojia.

“Wasiposaidiwa kuendana na mazingira hata wakitoka watakuwa na matatizo, kwa sababu walishakosa baadhi ya hatua muhimu katika makuzi yao, kwa sababu mtoto anapopelekwa shule siyo kwa ajili ya kusoma tu bali kuchangamana,” alisema Dk Mauki.

Chanzo
Sakata la watoto hao liligundulika Machi 7 mwaka huu, saa 12.00 jioni baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa mzazi mmoja mkazi wa Kata Pasua aliyedai watoto wake watatu kutoroshwa.

Mzazi huyo aliwaambia polisi kuwa alipata taarifa kuwa watoto wake wamehifadhiwa katika nyumba hiyo, ndipo askari walipofuatilia na kuwakuta watoto 18.

Juzi saa tatu asubuhi, mamia ya wakazi wa Moshi walifika katika nyumba hiyo, huku wakiimba kutaka kuwaona watoto wao baada ya kuwakuta askari kanzu wakilinda eneo hilo.

Askari hao walizidiwa nguvu na kukiita Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwenda kuwatawanya wananchi ili watoto hao watolewe na kupelekwa kituoni kwa mahojiano.

Baadaye Mkuu wa Kituo cha Polisi Moshi, Deusdedit Kasindo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Norvatus Makunga walifika katika nyumba hiyo na kuzungumza na mmiliki.

Mmiliki huyo alidai watoto hao walipelekwa na wazazi wao kwa lengo la kufundishwa dini. Polisi waliwachukua watoto hao na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano.

[audio, video] Taarifa ya Lissu kuhusu kesi, hatima ya uanachama na Ubunge wa Zitto

Tundu Lissu akitoa taarifa kwa wanahabari (picha via GPL)


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeifutilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe dhidi ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kukubali mapingamizi yaliwasilishwa na chama hicho.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Richard Mziray baada ya kupitia hoja za pande zote mbili kuhusu mapingamizi ya CHADEMA.

Mapema Saa 3:20 asubuhi Jaji Mziray alisoma uamuzi huo mbele ya wanaodaiwa kuwa wanachama huku upande wa Zitto akiwa hana mwakilishi na alikuwepo wakili wa utetezi Peter Kibatala.

Alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili mahakama imeona Zitto alikosea kuifungua kesi hiyo katika Masijala Kuu ya Mahakama Kuu badala ya Masijala ya Kanda ya Dar es Salaam ya mahakama hiyo.

Pia, Zitto hakuonyesha kwa sababu gani alifungua kesi hiyo ya madai Mahakama Kuu badala ya Mahakama ya Hakimu Mkazi kama Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai.

Awali mahakamani hapo CHADEMA kupitia mawakili wake kiliwasilisha kwa njia ya maandishi mapingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Zitto.

Katika pingamizi la kwanza, CHADEMA ilidai kwamba haikuwa sahihi kesi kufunguliwa Mahakama Kuu kwa sababu ilipaswa kufunguliwa Mahakama ya Wilaya/ Hakimu Mkazi kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Kesi za madai.

Pingamizi jingine, kesi hiyo ilikosewa kufunguliwa Mahakama Kuu, Masijala Kuu badala ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Jaji alikubali mapingamizi hayo kwamba yako sahihi na kuitupilia mbali kesi hiyo.

“Mahakama inaamuru Zitto kukilipa CHADEMA gharama zote za kesi hii” alisema Jaji Mziray.

Mapema Januari 2, mwaka 2014 Mahakama Kuu, iliyoketi chini ya Jaji John Utamwa, ilitoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya CHADEMA, kutojadili uanachama wa Zitto katika kikao cha chake kilichofanyika Januari 3, mwaka jana.

Hata hivyo, Januari 3, mwaka 2014 mahakama hiyo ilisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo mbele ya Jaji John Utamwa.

Januari 7, mwaka 2014, mahakama hiyo pia ilitoa amri kwamba Zitto asijadiliwe uana chama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Zitto alikuwa anatetewa na wakili msomi, Albert Msando na CHADEMA walikuwa wanawakilishwa na Tundu Lisu na Peter Kibatala.

Katika kesi ya msingi, Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Willbrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.

Katika maombi yake, Zitto anaiomba mahakama kuiamuru kamati kuu na chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chama.

Kadhalika, anaoimba mahakama imwamuru, Dk. Slaa kumkabidhi nakala za taarifa na mwenendo mzima wa vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa katika ngazi ya juu ya chama hicho.

Zitto kupitia wakili wake Msando aliomba mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu na vikao vingine vya chama kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Akiwasilisha hoja zake wakili Msando aliomba zuio hilo litolewe hadi Zitto atakapopata nafasi ya kuwasilisha rufaa yake ya kupinga uamuzi wa kumvua uongozi katika chama, uliotolewa katika kikao kilichofanyika Novemba 12 mwaka 2013.

Wakili alidai endapo amri hiyo haitatolewa na Kamati Kuu ikamvua uanachama, Zitto atapata athari kubwa kuliko chama chenyewe kwa kuwa atapoteza nafasi yake ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua.

Pia, mwanasheria huyo alidai athari nyingine ni kwamba iwapo atafukuzwa uanachama, Zitto atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alisisitiza kuwa, Zitto haizuii CHADEMA kufanyakazi zake za kisiasa kama wao wanavyodai katika hati ya kiapo kinzani, bali anaomba Kamati Kuu isijadili suala lake la uanachama mpaka uamuzi utakapotolewa.

Akijibu hoja hizo Wakili wa CHADEMA, Lissu alidai kuwa katika kutoa zuio la muda mahakama inatakiwa iangalie maslahi ya walio wengi na si faida ya watu wachache.

Alidai katika hati ya kiapo, Zitto anadai hakuna tarehe ya kikao cha Baraza Kuu la chama kilichopangwa, pia asipokata rufaa hatotendewa haki na atapata madhara lakini dawa ya woga na hofu yake ni kuomba mahakama iamuru kikao cha Baraza Kuu kifanyike na siyo kuomba zuio.

Lissu alidai kuvuliwa uanachama kwa Zitto hakutakuwa na athari kubwa kama anavyodai, athari ataipata yeye kwa kukosa posho na mishahara.

  • Taarifa ya sauti via BBC Swahili
  • Taarifa ya maandishi via Michuzi blog
  • Taarifa ya video via AzamTv (credit: SimuTv channel)

Taarifa ya Waziri kuhusu habari ya gazeti la NIPASHE “Mwakyembe atajwa Kashfa ya TRL”JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

JOTO la uchaguzi mkuu limezidi kupanda baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe kusema tuhuma zinazotolewa dhidi yake ni porojo na uzushi kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi. Mwakyembe alisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuhusu mabehewa ya TRL na kumhusisha yeye wakati alikwisha agiza hatua za kuchukuliwa kwa wahusika tangu waziri wa uchukuzi.

Imeandika habari yenye kichwa cha habari “Mwakyembe atajwa Kashfa ya TRL”. Napenda kutoa ufafanuzi kuwa habari hiyo iliyoandikwa ni uzushi mtupu wa kutaka kunichafua. Nachelea kusema habari hii ni uzushi na porojo za kisiasa haswa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kunihusisha kwenye mchakato wa zabuni ya TRL ambao Waziri hana mamlaka nao kikanuni na kisheria.

Kama Waziri mwenye dhamana na Wizara baada ya kupokea malalamiko kuhusu mabehewa yaliyonunuliwa na TRL kutokuwa na viwango vinavyokubalika, nilichukua hatua za awali za kuunda tume ambayo ilanza mara moja kuchunguza suala hili ili kujiridhisha na kutafuta ukweli wa jambo hilo. Baada ya kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi uliofanywa na tume hiyo, nilichukua uamuzi wa kuiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TRL kuivunja Bodi ya Zabuni.

Baada ya bodi hiyo zabuni kuvunjwa, niliagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TRL iwasimamishe kazi maafisa waandamizi wote wa TRL waliohusika katika mchakato wa manunuzi wa mabehewa hayo ili kupisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea kufanywa na tume. Aidha, niliiagiza Wizara na Bodi ya Wakurugenzi ya TRL kuiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)ifanye uchunguzi wa kina wa mkasa mzima, kazi ambayo nafahamu inaendelea kufanyika hadi sasa.

Kwa msingi huo habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo (NIPASHE) vyombo hivyo (si hili) ya kunihusisha na kashfa ya sakata hilo imenishtua na kunishangaza kwa kuwa kama ningekuwa nahusika kwa namna moja au nyingine nisingeweza kuchukua hatua nilizozieleza hapo juu. Gazeti la NIPASHE pia limehusisha suala la mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yalyofanywa na Mhe. Rais, ambayo mimi nimehamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwamba ni kwa sababu ya kuniepusha na kadhia ya kashfa hiyo ya ununuzi wa mabehewa feki.

Hilo ni jambo la kushangaza na uelewa mdogo wa mwandishi wa kutoelewa namna Serikali inavyofanya kazi. Uamuzi wa kunihamisha Wizara umefanywa na Rais kwa sababu tofauti kabisa na hizo za kusadikika zilizoandikwa na gazeti la NIPASHE. Kama Rais aliona nina dosari, hakuwa na sababu kabisa kuniteua kumsaidia kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kipindi hiki ambacho nchi yetu imepata fursa ya kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya. Hivi karibuni Mhe.

Waziri Mkuu, alifanya ziara katika Mkoa wa Mbeya na wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kyela, Waziri Mkuu alitoa ufanunuzi mzuri wa uamuzi uliochukuliwa na Mhe. Rais wa kuniamisha kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenda Wizara ya Ushirikano wa Afrika Mashariki, maelezo ambayo sina haja ya kurudia kuyaeleza kwa sababu yalishatolewa kwenye vyombo vya habari.

Nimalizie kwa kusema kuwa Watanzania tuamke kwani hakuna dosari yoyote ya mimi kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kupelekwa kwangu Afrika ya Mashariki ambako nilianzia Ubunge, ni mkakati mzuri tu wenye tija. Wenye nia njema na nchi yetu wataafiki”. Naomba ifahamike kwamba sehemu kubwa ya nguvu ya fedha ya washiriki wetu wa maendeleo sasa inapitia kwenye Jumuiya za kanda kama Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo kwa sasa Mhe. Rais ni Mwenyekiti wa Marais wa Jumuiya na mimi ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri.

Hivi sasa niko njiani natokea Marekani ambako niliongoza ujumbe mkubwa wa Mawaziri wan nchi tano (5) za Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadiliana na Serikali ya Marekani, pamoja na mambo mengine, kuongeza muda wa sheria inayozipa fursa nchi za EAC kupeleka bidhaa za biashara Marekani bila ushuru (AGOA).

Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb)
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
9 Machi, 2015

Hali halisi ya chumba cha wazazi hospitalini Dar


 Uhaba wa jengo na Vitanda ndiyo chanzo cha kuwalaza watoto watano kitanda kimoja.


via GSengo blog: MKUU WA WILAYA KINONDONI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA PALESTINA

Hofu ya Serikali dhidi ya ugaidi yaleta neema ya ajira kwa vijana

Nchi ya Cameroon imelenga kuzuia mauaji ya kundi la Boko Haram kwa kutoa ajira kwa vijana 2,000 kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri wa Uchumi na Mipango Emmanuel Nganu Djumessi amearifu kuanzishwa kwa mpango mpya utakaowahakikishia nafasi za kazi vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 – 35.

Djumessi alisema kwamba mpango huo mpya utaanza kutekelezwa katika eneo la kaskazini, eneo la karibu na mpaka wa Nigeria na baadhi ya maeneo yanayokumbwa na mashambulizi ya Boko Haram.

Djumessi alisisitiza kwamba vijana hao wataajiriwa hasa katika sehemu zinazohusika na upandaji wa miti na maua kwenye bustani.

Viongozi wa serikali za mitaa walibainisha kwamba kundi la Boko Haram limekuwa likiwatumia vijana wasiokuwa na ajira wanaoishi maeneo ya kaskazini mwa nchi kama magaidi kwa ushawishi wa fedha na pia kwa kuwalazimisha.

Uingereza yajadili muswada wa sheria ya kuzuia baadhi ya wasafiri

Bunge la Uingereza limejadili muswada utakaolazimu mashirika ya ndege kutoa taarifa kuhusu wasafiri wake kabla ya ndege zao kutua nchini Uingereza.

Hii ni moja kati ya hatua zilizochukuliwa na bunge la Uingereza katika kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi. 

Muswada huu, iwapo utaidhinishwa, utayapa mashirika ya ndege uwezo wa kuwazuia wasafiri kupanda ndege zao iwapo watashukiwa kuhusika na makundi ya kigaidi.

Waziri msaidizi katika wizara ya mambo ya ndani, James Brokenshire anayehusika na masuala ya usalama na uhamiaji alisema, "Sheria hii itaweza kuwazuia watu wanaokwenda kupigana katika nchi za nje, kurudi nchini humu."

Raia wa Uingereza zaidi ya 500 wamesafiri kwa ajili ya kushiriki katika vita nchini Iraq na Syria. Raia takriban 200 wametiwa mbaroni wakirejea nchini humo baada ya kushukiwa kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi.

Miss Tanzania aongoza Wanadaresalama kuchangia damu

Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo. 

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,mrembo Doris Mollel ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kwa mwaka 2014 ameongoza mamia ya watanzania katika zoezi la kizalendo la kuhamasisha kuchangia damu kwa watanzania kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali,zoezi ambalo limefanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Zoezi hilo ambalo lilikuwa linaongozwa na mpango wa taifa wa damu salama kwa udhamini wa kampuni ya METL lilikuwa na lengo la kupata damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwani matatizo ya damu katika hospitali za Tanzania yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,jambo lililompelekea mrembo huyo kuamua kujitoa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Zoezi hilo lilifanyika Machi 8 mwaka huu katika maeneo ya Buguruni Chama kwa muda wa siku nzima,ambapo jumla ya uniti 65 za damu zimepatikana kiwango ambacho kimetajwa kuwa kinatia matumaini kwa mrembo huyo kufanikiwa katika kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi.

Akizungumza na wanahabari kuhusu kitu kilichomsukuma kuendesha zoezi hilo,Doris alisema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kugundua kuwa wakina mama wengi pamoja na watoto hufariki dunia wakati wa kujifungua kutokana na kukosa damu ya kuongezewa,jambo ambalo amesema ni lazima watanzania kuungana kwa pamoja kutafuta damu ya kutosha katika kila hospitali ili kuiondoa hali hiyo ambayo inaweka hatarini maisha ya mama na mtoto wa kitanzania.

Amesema kuwa swala la kujitolea damu ni swala la kizalendo zaidi na moyo wa kujitoa kwa kuwa kila mtanzania anaweza kuwa na uhitaji wa damu muda wowote hivyo ni lazima watanzania wawe na utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara kwani itasaidia endepo kutatokea uhitaji wa damu katika mahospitali yetu.

Aidha amewataka watanzania wengine ambao wanauwezo wa kuhamasisha watu wengine kuchangia damu wafanye hivyo kwani kuna uhitaji mkubwa sana wa damu katika mahospitali ya kitanzania na kufanya hivyo ni kuokoa maisha ya watanzania wengi wenye uhitaji wa damu hiyo.

Doris Mollel alijizolea umaarufu mwaka 2014 baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya tatu katika shindano la Miss Tanzania mwaka huo ambapo aliwashinda warembo wengine waliokuwa wanawania taji hilo.Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick,Bi Mariam Meck Sadick akiungana na wananzania wengine kwenye zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mrembo Doris Mollel.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishiliki zoezi la uchangiaji damu katika kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Mpiga Picha wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,John Dande akipima uzito tayari kwa kushiriki zoezi la uchangiaji damu,ikiwa ni sehemu kuunga mkono sherehe za Siku ya wanawake Duniani.zoezi hilo lilifanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Picha na John Dande.