You can lose weight without exercise, But...
I don’t recommend exercising when starting ‘The Virgin Diet’. Great for the short term, unlike the long term where not exercising sets you up to be TOFI (thin on the outside, fat on the inside). 

Initially, the way to lose weight is to change what’s at the end of your fork. To do that, uncover your hidden food intolerances as I’ve discussed in my book, ‘The Virgin Diet’, and drop your sugar impact.

Exercise maintains muscle and bone. Think of muscles as metabolic Spanx, holding everything tighter so you’re going to look better naked. That’s important, right? First, move more! Get an hour’s worth of movement a day, about 6,000 steps. 

Also, there are two types of exercise I want you to do each week. One is burst training to blast fat three times a week for 12 to 20 minutes. Pick full body exercises: walk, run, swim. Warm up; go all out for 60 seconds, then take twice as long to recover. 

Repeat, reaching 8 total minutes a burst. Next is resistance training, lifting heavy, hard and fast twice a week; with at least 48 hours of recovery. The best time to exercise? I always say, “When you will.”

Visit: jjvirgin.com/blog for more.

USA cracks down on 'birth tourism'


In the largest operation of its kind, early Tuesday morning federal officials in Southern California served warrants at "Chinese birthing houses" or "maternity hotels," where wealthy Chinese nationals paid up to $80,000 for the sole purpose of giving birth in the U.S. to obtain citizenship for their children, earning in-state tuition to U.S. universities for them and permanent U.S. residency for the parents.

Birth tourism is big business. An estimated 40,000 babies are born to couples posing as tourists each year. The U.S. is one of the few countries in the world that automatically grants citizenship to any child born here, regardless of the parents’ nationality. While it is not against the law, lying to obtain a visa to enter the U.S. under false pretense is illegal. Companies offering to help foreign nationals give birth in the U.S. operate openly on the Internet, promising a U.S. passport, birth certificate and Social Security number for their newborn. Prices range from $8,000 to $80,000, depending on the services. Wealthy couples from China, the Middle East, Africa and South Korea predominate the trade.

Kerry says lawmakers won't be able to change terms of any nuclear agreement


USA Secretary of State John Kerry said on Wednesday that U.S. lawmakers won't be able to change the terms of any nuclear agreement with Iran because it won't be legally binding.

Kerry said the senators' letter "erroneously asserts that this is a legally binding plan. It's not, that's number one. Number two, it's incorrect when it says that Congress could actually modify the terms of an agreement at any time. That's flat wrong. They don't have the right to modify an agreement reached executive to executive between leaders."

No side has emphasized the need for a legally binding deal because each has stronger forms of leverage. If Iran cheats, the Obama administration has spoken of re-imposing suspended sanctions. The U.S. has also held out the prospect of military action if Iran makes progress toward a nuclear weapon.

Similarly, if the U.S. doesn't live up to its side of the bargain, the Iranians can ramp up enrichment levels of uranium, taking them closer to nuclear weapons capacity.

Congress, too, wields a threat: new forms of economic punishment of Iran that would be forbidden in the agreement. But such a move would almost surely require overriding a presidential veto and could pin a diplomatic collapse on the United States.

Negotiators from the United States, Britain, China, France, Germany and Russia hope to seal a framework with Iran by month's end and a comprehensive agreement by July. Kerry scoffed at the notion that Obama's successor would discard a deal reached between so many powerful governments and adhered to by Iran.

"I'd like to see the next president, if all of those countries have said this is good and it's working, turn around and just nullify it on behalf of the United States," he said. "That's not going to happen."

---

PAC yamwelekeza CAG achunguze ziliko milioni 699/= zilizotoka Nishati na Madini kwenda TANESCO

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Zitto Kabwe akiongoza kikao cha kamati hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishi wa hesabu za Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) lilipowasilisha ,kulia ni Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage. 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) kufanya uchunguzi wa Sh milioni 699 zinazodaiwa kutolewa na Wizara ya Nishati na Madini kwenda Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambazo zinaonekana kuyeyuka katika mazingira yasiyoeleweka.

Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam wakati wa Hesabu za TANESCO.

Kabwe alisema katika ripoti ya ukaguzi wa hesabu wa shirika hilo inaonekana wizara imetoa Sh milioni 699 kwenda TANESCO, lakini shirika hilo limeeleza kuwa halijawahi kupokea fedha hizo, jambo ambalo linaleta utata na kuhoji ni wapi fedha hizo zimekwenda.

“Kamati inamtaka CAG afanye ukaguzi maalum, kwa kushirikiana na TANESCO na Wizara na kisha ilete taarifa ni wapi fedha hizo zimekwenda,” alisema.

Awali akitoa maelezo kuhusu fedha hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dk Mighanda Manyihi alisema Tanesco haijawahi kupokea fedha hizo na kumuomba Mwenyekiti wa PAC na kamati kufanya kila linalowezekana ili fedha hizo zipatikane kwani zitakuwa msaada kwa shirika.

“Mwenyekiti, hizo fedha hata siye tunazihitaji sana kuna miradi mingi sana ambayo imekwama, kama fedha hizo zikipatikana zitatufaa sana,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dk. Mighanda Manyihi akijitambulisha kwa wajumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika kikao cha kuwasilisha hesabu za shirika hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi. Felchesmi Mramba.

Naye Kaimu Ofisa Mkuu wa Fedha, Anetha Chengula akitolea ufafanuzi suala hilo mbele ya Kamati alisema TANESCO haijawahi kupewa fedha hizo na kwamba walishafuatilia hadi wizarani kwa wahasibu wa wizara na kushindwa kutoa vielelezo kuthibitisha kutoa fedha hizo.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imeagiza Bodi ya TANESCO kuhakikisha ifikapo Aprili 30, mwaka huu nafasi zote za ngazi ya Menejimenti kuwa zimejazwa na hakuna tena suala la kukaimu kwani bodi ina mamlaka kisheria kufanya hivyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Anetha Chengula ambaye alijitambulisha kama Kaimu Ofisa Mkuu wa Fedha ambapo Mwenyekiti alihoji Bodi na Menejimenti kwa nini ofisa huyo anaendelea kukaimu wakati Bodi ina mamlaka ya kuteua na kupanga menejimenti kwa mujibu wa Sheria.

Kamati ikitoa uamuzi kuhusu suala hilo, iliagiza Bodi kujaza nafasi zote zilizo wazi katika menejimenti ifikapo Aprili 30 na itakapokamilisha ipeleke taarifa kwa Katibu wa Bunge, pamoja na kuitaka bodi mpya kupitia mikataba yote na kisha kupeleka taarifa kwa Katibu wa Bunge badala ya kusubiri kuitwa tena katika kamati.

---

Picha: Blogu ya Serikali ya Tanzania
Taarifa: Gazeti la HabariLeo

Zaidi ya bilioni 65/= za mikopo ya Elimu ya juu zimerejeshwa

L-R: Juma Chagonja, Cosmas Mwaisobwa
L-R: Juma Chagonja, Cosmas Mwaisobwa
(picha via blogu ya Serikali ya Tanzania)

IMANI potofu kuwa mikopo itolewayo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), ni ruzuku na hawapaswi kuirejesha ni moja ya changamoto ambazo bodi hiyo inakabiliana nazo katika ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika.

Wakizungumza katika mutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo maofisa kutoka HESLB wamesema makusanyo yamekuwa yakisua sua kutokana na wakopaji kutofanya marejesho na kukaa kimya hata wanapo andikiwa.

Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, amesema kuwa jumla ya shilingi Bilioni 123.8 zilipaswa kuwa zimerejeshwa lakini hadi sasa bodi imekusanya Bilioni 65.2 pekee.

Bodi ya mikopo imekopesha wanafunzi kiasi cha shilingi Trilioni 1.8 tangu mwaka wa masomo 1994/95 hadi Juni mwaka 2014 kati ya fedha hizo bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Mwaisobwa alisema jumla ya wadaiwa 136,198 sawa na asilimia 76.94 ya wadaiwa wote 177,017 ambao mikopo yao imeiva wametambuliwa na wanaendelea na marejesho ya mikopo.

“Hadi sasa mikopo yote inayotolewa na Bodi kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 inabeba tozo la utunzaji wa thamani ya mikopo kwa asilimia sita kwa mwaka kwa kiasi chote cha mkopo ambacho hakijarejeshwa” alisema.

Alisema bodi hiyo inaendelea kuongeza kasi ya urejeshaji wa mikopo kwa kubuni mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kurejesha mikopo na kuongeza matumizi ya mitandao ya simu katika kukusanya madeni.

Aidha njia mbadala za utumiaji wa huduma za kifedha za mitandao ya simu kama M Pesa na Airtel Money nazo zimeanza kutumika ili kuwarahisishia wakopaji namna ya kurejesha fedha hizo badala ya kwenda kupanga folebni benki.

Pia alisema wamezidisha ushirikiano zaidi na wadau muhimu hasa Mifuko ya Hifadhi ya Jamiii, Mamlaka ya Mapato, Waajiri, Sekta isiyo rasmina Wanufaika wa mikopo ambapo pia wamechukua hatua za kisheria dhidi ya wanufaika wanaokaidi kurejesha mikopo yao ambapo hadi sasa kuna kesi 18 zimefunguliwa mahakamani dhidi ya wadaiwa sugu.

Mtizamo na ushauri wa wasomi kuhusu Zitto kuvuliwa CHADEMA

Wasomi na wachambuzi wa masuala ya siasa nchini, wamekishauri Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumsamehe Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto kwa kuwa bado anahitajika kujenga chama hicho.

Mmoja wa wasomi wa chuo cha Diplomasia, Mhadhiri Mwandamizi wa chuo hicho, Balozi Charles Sanga alisema kuwa pamoja na umuhimu wa kuheshimu katiba ya chama, ameshauri chama hicho kingefanya uvumilivu na sio kuchukua hasira.

Alisema ni vyema uvumilivu ukatumika katika kukijenga chama hicho na sio kufanya maamuzi ya hasira ambayo yanaweza kupunguza nguvu ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

“Kujenga chama cha siasa sio jambo jepesi na la siku chache, ni kitu kinachochukua muda mrefu na huko ndani kuna watu tofauti sasa ni vyema jambo kama hili, Chadema ingefanya uvumilivu, ujenzi wa chama sio lele mama,” alisema na kuongeza:

“Nchi za Kiafrika bado zinajaribu kujenga vyama vyao, kwani ni changa, tunahitaji kuvilea, tuvumiliane, ila pia sheria mama za vyama zisivunjwe, ila pia sheria za kawaida ziangaliwe tuvumiliane kidemokrasia na sio kuchukua hasira”.

Alisema suala ya Zitto linapaswa kuangaliwa kwa mapana yake na kuangalia pia wananchi wa jimbo lake kwani athari zake ni kuwanyima wananchi uwakilishi kupitia jimbo hilo.

“Wananchi wa jimbo lake wataathirika, mara nyingi hatuangalii maslahi ya wananchi tunaangalia maslahi ya vyama, na hii sio sahihi kidiplomasia, tupime mizani je, aliyoyafanya kwa chama chake miaka yote na taifa kwa ujumla yana uzito kiasi gani ukilinganisha na adhabu aliyopewa?” Alihoji.

Alisema maamuzi ya Chadema yanaweza kukibomoa chama badala ya kukijenga kwani uamuzi wa kumfukuza Zitto, unaweza unakifanya kugawanyika kwani wapo wanachama watakaomuunga mkono Zitto hivyo kukibomoa chama, jambo ambalo sio jema.

Alisema jambo hilo liwekwe mizani, na kwamba ni vyema vyama vinapofanya maamuzi visifanye kwa hisia na kushauri kama kuna nafasi nyingine zaidi ya hapo Zitto aitumie kukata rufaa.

Msomi mwingine, Benson Bana ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mchambuzi wa masuala ya siasa za Tanzania, pamoja na Robert Mkosamali, msomi na mchambuzi pia wa siasa hizo walisema, kwa nyakati tofauti pia kuwa, kwa kumvua uanachama Zitto Kabwe, Chadema atajibomoa kwa kupunguza wanachama.

Akizungumzia kipengele cha katiba ya Chadema, kinachokinzana na Katiba ya nchi ya mwaka 1977, pamoja na haki za binadamu, Bana alisema;

"Msajili wa vyama vya siasa ana kila sababu ya kufanya mapitio ya katiba zote za vyama vya siasa kuhakikisha hazina vipengele vinavyomzuia mwanachama au kiongozi wa chama kwenda mahakamani kutafuta haki anayoamini kuwa hawezi kuipata ndani ya chama chake".

Alisema, katiba ya chama hicho inaposema kuwa Zitto amevuliwa uanachama kwa sababu amekwenda kukishitaki chama mahakamani, inakuwa imekwenda kinyume cha katiba ya nchi na haki za binadamu, zinazoelekeza kuwa chombo cha mwisho cha kutoa haki kwa mtu yeyote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mahakama.

Alisema, katiba ya nchi ya mwaka 1977 ndio sheria mama inayobeba katiba zote, zikiwemo za vyama vya siasa, kwa hiyo, kuwepo kwa sentensi inayokinzana na katiba mama ni kasoro pia inayoweza kusababisha udhaifu kama huo wa kufukuzana katika vyama.

Alieleza; "Wakati inasemwa kuwa mahakama ndio sehemu pekee ambayo mtu anaweza kukimbilia kupata haki yake ya msingi, wanachama katika vyama vyenye katiba zisizozingatia misingi ya haki za binadamu wanang'ang'ana kufukuzana kwa kosa la mtu kwenda kutafuta haki yake mahakamani.

"...Ni katiba ipi iko juu kimamlaka kati ya hiyo ya Chadema na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Jaji Mutungi ategue kitendawili hiki ili wanachama wasioneane na wasikomoane kwa sababu tu ya chuki, wivu na uadui unaosababishwa na hofu za kuzidiana 'kete' katika uongozi ndani ya vyama".

Aliongeza kuwa, tatizo lililotokea kwa Zitto halipaswi kuwatingisha Watanzania kwa kuwa, nafasi ya kutekeleza majukumu aliyoyaanza kwenye chama hicho ataipata kwingine kokote atakakojiunga kwa sababu ya uwezo wake wa kufanya kazi, mvuto na umaarufu wa kisiasa aliouonesha.

Bana anasisitiza kuwa hatima ya Zitto kisiasa bado ipo juu tofauti na ilivyo kwa CHADEMA ambacho, bila kutarajia kitakuwa kimepoteza watu wote waliokuwa wakimuunga mkono Zitto, ambao ni wengi.

Kwa upande wake, Mkosamali alisema, mahakama ndicho chombo pekee kinachotajwa na katiba ya nchi kuwa ndipo mtu yeyote anapoweza kukimbilia kupata haki yake ya msingi.

"Ni kweli Ibara ya 71 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara ndogo ya 1 (e) inasema; "Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika bunge itokeapo mambo yafuatayo;

(f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama chake na iwapo chama chake kitakuwa kimemvua uanachama.

Kwa maelezo ya Mkosamali, kulingana na maelezo hayo ya katiba, Zitto amevuliwa uanachama, lakini bado chama chake kupitia mikutano ya ndani, kinaweza kumpa nafasi nyingine kwa kuyajadili mambo hayo kwa uvumilivu ndani ya mikutano yake.

"Kazi ya Zitto katika PAC (Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali) imeonekana, mchango wake katika kukuza demokrasia na siasa nchini nayo imeonekana kwa hiyo kuondolewa kwake katika chama kunaweza kuiathiri kamati hiyo kwa sababu ukali wake na usimamizi wake madhubuti wa majukumu aliyokuwa akiyatekeleza hautakuwepo tena".

Bana na Mkosamali wanamshauri Zitto asikimbilie kuanzisha chama kipya cha siasa sasa hivi, kwa sababu, muda uliopo hadi kufikia uchaguzi mkuu Oktoba ni mfupi usiotosha kukijenga na kukiimarisha chama.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Julius Malaba alisema jana kuwa, ofisi yake itaipokea barua hiyo na kuifanyia kazi, endapo itawasilishwa kwa kufuata taratibu zinazostahili.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, amebainisha kuwa endapo Bunge litapata taarifa rasmi ya Chadema kumvua uanachama Zitto, lazima Bunge hilo lifanye kwanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ndipo litoe uamuzi.

Pia amesema sakata la mbunge wa Bunge hilo kuvuliwa uanachama na chama chake si la kwanza, kwani tayari kuna mbunge aliyevuliwa uanachama na chama chake lakini Bunge hilo halikumvua uanachama wake baada ya kumaliza uchunguzi wake. Hata hivyo hakumtaja mbunge huyo.

Akizungumza na mwandishi Dar es Salaam, Katibu huyo, alikiri kusikia habari za Zitto kuvuliwa rasmi uanachama wake na chama chake, lakini alisisitiza kuwa bado ofisi yake haijapokea barua rasmi kutoka kwa chama chake kwa ajili ya kupatiwa taarifa hizo.

“Utaratibu ulivyo, chama huliandikia Bunge kuhusu kumvua uanachama mbunge na Bunge kabla ya uamuzi wowote hufuatilia kwanza sababu za kuvuliwa uanachama huo, ili kujiridhisha kama zilikuwa halali au la,” alisema Kashililah.

Alisema baada ya hapo Bunge hilo huwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili ofisi hiyo ya msajili iweze kupitia Katiba ya chama husika na kupitia sababu za chama husika zinazoweza kumvua uanachama mwanachama wake na kama kweli zimekiukwa.

“Baada ya suala hilo kupelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, Spika wa Bunge, hutoa uamuzi baada ya kuchunguza na uamuzi huo, hupelekwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi,” alisisitiza.

Aidha alisisitiza: “Si lazima Spika atoe uamuzi wa kutengua ubunge wa mbunge husika kwani kama haikuwa halali kwa mbunge huyo kuvuliwa uanachama, Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika,” alisema.

Alisema Spika Anne Makinda katika kipindi chake alishawahi kutoa uamuzi wa kubatilisha mbunge fulani kuvuliwa ubunge hata baada ya chama chake kumvua uanachama.

Akizungumzia suala hilo, Zitto, alisema kwa upande wake bado ni mbunge na anaendelea na kazi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) hadi pale atakapopatiwa taarifa rasmi ya kuvuliwa uanachama na ubunge wake.

“Naendelea na kazi kama vile hakuna kilichotokea, sina taarifa yoyote ya kuvuliwa uanachama wangu wala ubunge, habari hizi nimezisikia kwenye vyombo vya habari, sijaitwa na Mahakama kuambiwa kinachoendelea,” alisema Zitto.

Alisema kwa sasa anaendelea kuongoza kamati hiyo na jana alikutana na menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), leo kamati yake inatarajia kukutana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pia watakutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwanasheria Mkuu kuhusu mapato ya akaunti za madini.

Aidha alisema pamoja na kuendelea kama kawaida na shughuli zake za kibunge bungeni, pia anatarajia kesho kwenda Kigoma kwa ajili ya shughuli za maendeleo jimboni kwake, kabla ya kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza rasmi Machi 17, mwaka huu.

Alisema kwa upande wake, anachukulia suala hilo kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika medani za siasa nchini na duniani kote.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema chama hicho kinajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zote, ikiwemo kuandaa na kuiwasilisha wakati wowote barua inayomvua uanachama Zitto, ili suala hilo lifanyiwe uamuzi mapema.

“Kwa sasa suala hili la Zitto limewaingia Watanzania wengi, sasa sisi tunataka tulifanyie kazi mapema, ili uamuzi ufanywe mapema na suala hili liishe. Kuna mambo mengi ya maana yanahitaji kujadiliwa kitaifa kama vile masuala ya uandikishaji katika Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa BVR,” alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye juzi alitangaza kuwa chama hicho kimemvua uanachama mbunge huyo, jana alimwambia mwandishi kuwa, jopo la wanasheria wa chama hicho litaifikisha taarifa ya Zitto kuvuliwa uanachama kwa Kamati Kuu ya chama ifikapo Mei, mwaka huu.

Alisema, "Kutokana na utaratibu uliopangwa wa Kamati Kuu kukutana kila baada ya miezi mitatu, suala la Zitto litasubiri kikao kingine cha kawaida cha kamati hiyo kitakachokaa mwezi Mei. Kikao kilichopita kilikaa Februari mwaka huu".

Kwa maelezo ya Lissu, baada ya hapo ndipo wataiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuijulisha kuwa Zitto si mwanachama wa chama hicho tena au la.

--

Taarifa: Gazeti la HabariLeo

5 behaviors you never see in happy, successful people


It’s not intrinsic characteristics or good fortune that have the greatest influence on whether or not you’re happy and successful in the long run. It’s your behavior.

What do I mean by “behavior?” How you react under stress. Whether you decide to meet your commitments or not. How you communicate and interact with loved ones. Your attitude toward bosses, colleagues, employees, and customers. How hard you’re willing to work to do a job right. Whether you’re focused and disciplined or scattered-brained and distracted.

If you want to thrive over the long-term, you might want to take a look and see if any of these behaviors describe you.

1. Your default belief is that life is too hard. 

– The truth is, it's just as easy to create good habits as it is to create bad ones. It's just a matter of how you spend your time. You can spend it doing the things that bring you closer to your dreams, or you can spend it seeking immediate comfort. People complain that “it’s too hard to exercise every day.” But exercise and movement are joyful, natural conditions that make us feel incredible. It’s not hard – it’s just that people get in the habit of not exercising. So what about you? You are where you are because of the choices you’ve made in the past. Your future depends on the choices you make today. You can choose to sit, or you can choose to run. You can choose to watch another sitcom, or you can choose to read another chapter in a great book. You can choose to act on an opportunity, or you can choose to sleep in. There’s nothing hard or complicated about it, other than the way you’re thinking about it.

2. You place blame on others for your life situation. 


– Sigmund Freud once said, “Most people do not really want freedom, because freedom involves responsibility, and most people are frightened of responsibility.” Don’t let this be you. When you blame others for what you’re going through, you deny responsibility – you surrender full power over that part of your life. In reality, the price of happiness and success IS responsibility. And no one else is responsible for you. You are in full control of how you choose to deal with the current state of your life. Through the grapevine, you may have learned that you should blame your parents, your teachers, your mentors, the public education system, the government, etc., but never to blame yourself. Right? It’s never, ever your fault… WRONG! It’s always your fault, because if you want to change – if you want to grow and move on with your life – the only person who can make it happen is YOU.

3. You act as though most people can't be trusted. 


– I won't argue that healthy discernment is important, but the happiest, most successful people are reasonably trusting of their fellow humans. They believe in the good in others, versus assuming everyone is out to get them. This helps them foster a sense of community around themselves and their ambitions. Unhappy people, on the other hand, are suspicious of everyone they meet and assume that strangers can't be trusted. This behavior gradually closes the door on every connection outside of their inner-circle and thwarts all chances of meeting new people capable of helping them grow. So keep in mind that trust is the foundation for cultivating growth and connectedness. When you choose to see the best in others, you end up finding the best in yourself.

4. You compare yourself to others and harbor envy. 


– Unhappy people believe someone else's good fortune steals from their own. They believe there's not enough goodness to go around. This leads to envy and resentment. Don’t let envy (or jealously) get the best of you. Envy is the art of counting someone else’s blessings instead of your own – there’s nothing attractive or admirable about this behavior. So stop comparing your journey with everyone else’s. Your journey is YOUR journey, NOT a competition. You are in competition with one person and one person only – yourself. You are competing to be the best you can be. If you want to measure your progress, compare yourself to who you were yesterday.

5. You expect (and need) everything to go as planned. 


– Life is often unpredictable. Some of the great moments in your life won’t necessarily be the things you do; they’ll be things that happen to you. That doesn’t mean you can’t take action to affect the outcome of your life. You have to take action, and you will. But don’t forget that on any day, you can step out the front door and your whole life can change in an instant – for better or worse. To an extent, the universe has a plan that’s always in motion. A butterfly flaps its wings and it starts to rain – it’s a scary thought, but it’s part of life’s cycle. All these little parts of the machine, constantly working – sometimes forcing you to struggle, and sometimes making sure you end up exactly in the right place at the right time.

Angel Chernoff

Image credit imgkid.com

Tahadhari ya Baraka Shelukindo kuhusu tapeli anayetumia jina lakeDear Friends

Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na tapeli mmoja ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook accounts kwa majina mbali mbali kama Justin Stan,James Brown,Onesmo,Felister Julius, Anthony Yohana au Yohana Anthony na mengineyo mengi.

Mtu huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika mtandao wa kijamii wa Facebook

Urafiki ukiwa umekamilika kwa maana ya friends request kutoka kwake and acceptance kutoka kwa victim amekuwa akiwaambia marafiki zake hawa wa Facebook kuwa yeye ni muajiriwa sehemu mbali mbali tofauti katika kila account hizi za facebook kama kwa mfano kwingine akidai anafanya Vodacom Mlimani City, kwingine akidai anafanya Tanesco Makao Makuu,PPF na sehemu nyingine kadhaa na amekuwa akiwaahidi kwamba ana watu wenye uwezo wa kuwaunganishia kazi sehemu hizo kwa sharti la wanaotaka kazi kujikusanya na kufikia idadi ya watu watano na wakilipa kiasi cha shilingi 50,000 kila mmoja basi watapata nafasi za kazi hizo.

Wakati mwingine amekuwa akiwa wadanganya baadhi ya watu kuwa yupo mkoani kikazi au akihudhuria semina na kwamba mdogo wake anashida ya dharura ya pesa kama shilingi 25,000 au 30,000 na kuomba marafiki wamtumie na kuwaahidi atawarudishia mara atakapokua free, amekuwa akitoa namba mbali mbali za simu mojawapo zikiwa hizi 0785412653 na 0688081032. Wale walioshtuka amekuwa akiwatukana matusi makubwa ya nguoni bila uoga.

Natoa tahadhari kwa watu wote kujihadhari na kufanya urafiki na watu msio wajua, kuzingatia umakini haswa katika mambo ya pesa, pia kujua watu wa namna hii ni wengi sana online haswa kwenye social media. Nashauri uki suspect mtu wa design hii basi wasiliana na polisi na ikibidi kumtengenezea mtego wa kumnasa.

Vijana tunatakiwa tuchape kazi kwa nguvu na sio kutafuta njia za mikato. Hakuna hadithi yeyote niliyowahi kuisikia ya aliyefanikiwa katika maisha kwa njia ya mkato. Mwana fundi ni kusoma kwa bidii ili elimu yako ikupatie ajira.

Mwisho naomba marafiki zangu wooote mnisaidie kurepost message hii kwani naamini itawaokoa wengi (vulnerable) ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa hawajui utapeli huu wa online.

Picha hiyo hapo juu ni yangu na ndio amekuwa akiitumia kwenye account nyingi za facebook.

Mimi ninaamini Mungu na hivyo huyu bwana Siku zake 40 zipo karibu. Napenda pia kwa namna ya kipekee nawashukuru wale wote (zaidi ya 10) waliotumia muda wao kunitafuta na kunipa taarifa hizi muhimu walipomshtukia Tapeli huyu.

Mwenyezi Mungu awabariki saana.

Japan yachangia shule alikosoma Waziri Mkuu, Pinda shilingi milioni 160/=

Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga akisoma risala fupi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
(picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

*Waziri Mkuu aomba Watanzania wamuunge mkono

SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa dola za Marekani 90,286 sawa na sh. milioni 160/- kusaidia ujenzi wa shule ya awali kwenye shule ya msingi Kakuni, iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi.

Japan imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada huo uliofanyika (Ijumaa, Machi 6, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni na kushuhudiwa na Waziri Mkuu mwenyewe, Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga alisema Serikali yake imeamua kutoa msaada huo kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 inayosema elimu ni haki ya kila mtoto.

Alisema sera ya elimu iliongezewa uzito na Mpango wa Kuendeleza Elimu ya Msingi Awamu ya Pili (PEDP II) ambao unasisitiza kwamba kila shule ya msingi ni lazima iwe na shule yake ya awali kama njia thabiti ya kuhimiza upatikanaji wa elimu ya awali hapa nchini.

“Mojawapo ya changamoto inayoikabili sekta ya elimu hapa Tanzania ni kukosekana kwa mazingira mazuri ya shule katika hatua za mwanzo za makuzi ya watoto wengi. Kwa mfano, kata ya Kibaoni ina shule tatu za msingi ambazo ni Kakuni, Ilalangulu na Milumba lakini hakuna shule ya awali hata moja, jambo ambalo hufanya watoto wote walundikane kwenye darasa mojawapo kwenye shule ya msingi Kakuni,” alisema.

Alisema anaamini mchango walioutoa utasaidia kuboresha viwango vya elimu ya awali katika kata ya Kibaoni. Mchango huo wa sh. milioni 160/- unatarajiwa kutumika kujenga madarasa mawili ya awali, ofisi ya walimu wa shule hiyo, eneo la michezo, bwalo dogo la chakula na jiko. “Natambua kuwa ujenzi wa shule peke yake hauinui kiwango cha elimu, bali kuongeza uandikishaji wa watoto, kuongeza walimu na kuboresha maslahi yao ni chachu nyingine muhimu katika kuinua kiwango cha elimu,” alisema.

Baadhi ya watendaji ofisi ya Waziri Mkuu waliohudhuria hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada na Ubalozi wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.

Utiaji saini huo ulifanywa na Kaimu Balozi huyo pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mlele, Bw. William Mwakalambile. Wengine waliokuwepo ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Ibrahim Msengi na Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu Pinda aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.

“Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha jana.

“Niliwaza pia kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani idadi ya wanafunzi waliopo ni kubwa kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao 770. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” alisema.

Alisema alipeleka maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65 kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla katika kuisimamia ndoto hiyo.

Alisema aliishirikisha Halmashauri kuandaa michoro inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI, na kuwataka waandae mapendekezo ya bajeti kwa kuzingatia taratibu za kiuhandisi na ujenzi na makisio ya awali yalikuwa sh. bilioni 1.3/-.

Alisema alipeleka barua kuomba michango kwa watu binafsi, mashirika ya umma, taasisi, mabenki na balozi mbalimbali ambao hadi sasa wamekwishamchangia sh. milioni 816.6 na dola za Marekani 210,000 na kwamba hadi sasa kwenye akaunti ya ujenzi amebakiza kiasi cha sh. milioni 182 na dola za Marekani 60,189.

“Katika kuanza zoezi la kukusanya fedha mwaka 2013, Ubalozi wa China ulikuwa wa kwanza kuitikia maombi yetu na ulitoa Dola za Marekani 200,000 ambazo zilikuwa sawa na sh. milioni 320. Pia ubalozi ukamteua mkandarasi wa barabara ya kutoka Nkasi – Kibaoni – Mpanda asaidie katika ujenzi wa shule ili kupunguza gharama,” alisema.

Hadi sasa majengo yaliyokamilika ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili (wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja, ukumbi mdogo na ofisi ya mwalimu na jengo moja la choo lenye matundu 48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua ya msingi. Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Waziri Mkuu aliwaomba Watanzania watakaoguswa na jambo hili wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba nane za walimu, choo kingine chenye matundu 48, bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, vitabu na TABLETS za wanafunzi, kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba mbili za walinzi na uzio wa shule.

Alitaja vitu vingine ambavyo bado vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo – shule ya msingi na shule ya awali.Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi (wa kwanza kushoto) akiwa na watendaji wa mkoa wa Katavi na wilaya ya Mlele alioambatana nao kwenye hafla hiyo fupi. Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William Mwakalambile (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mipango wa wilaya ya Mlele, Seif Mohamed Makome (kulia).Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia utiaji saini mkataba wa msaada wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam baina ya Kaimu balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William Mwakalambile (kulia). Waliosimama nyuma yao kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo na Kulia ni Afisa Mipango wa wilaya ya Mlele, Seif Mohamed Makome.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia tukio la kubadilishana hati za mkataba wa msaada baina ya Kaimu balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William Mwakalambile (kulia).Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Japan mara baada ya hafla ya utiaji saini wa mkataba wa msaada huo.Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifanya 'Power Point Presentation' ya hatua ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni aliyoijenga kutokana na michango ya wadau wa maendeleo kama kurudisha fadhila kwa jamii yake iliyomsomesha kijijini kwake.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kulia kwake) baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa msaada wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi na wapili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele, William Mwakalambile.

[update] Majeruhi wa basi lililoua 42 wazungumzia ukaidi wa dereva


MAJINA YALIYOPATIKANA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO HADI SASA NI:

Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule Dominick Mashauri na Omega Mwakasege.

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule,

Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37.Watu arobaini na wawili wamefariki dunia huku ishirini na wawili wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya ajali ya barabarani iliyotokea asubuhi ya Jumatano, Machi 11, 2015 huko katika eneo la Changarawe, Mafinga wilaya ya Mufindi katika mkoa wa Iringa.

Ajali hiyo iliyotokea baada ya basi la abiria la kampuni ya Majinja Express lililokua likitokea Iringa likielekea Dar es Salaam liligongana uso kwa uso na lori lililokua likitokea Dar es Salaam likielekea Iringa.

Mkuu wa polisi katika mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya watu 41 walioaga dunia, wanaume ni 33, wanawake 5 na watoto watatu.

Taarifa zaidi kutoka kwa watu walio katika eneo hilo zinasema kuwa miili ya maiti 32 bado haijatambuliwa na ndugu ama jamaa.

Mkuu wa polisi katika mkoa wa Iringa, ameelezea chanzo cha ajali hiyo akibaini kwamba dereva wa lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara suala lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo na kusababisha kugongana na basi hilo la kampuni ya Majinja Express.

Moja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Jackson Manga alisema kama dereva wa basi hilo angezingatia ishara za taa kali alizokuwa akiwashiwa na dereva wa lori hilo kwa vyovyote vile ajali hiyo isingetokea. Manga alisema katika eneo hilo lenye mteremko wa wastani, lori lilikuwa likipandisha na basi lilikuwa likishuka.

Alisema ukaidi wa dereva wa basi ulisababisha dereva wa lori aingie katika shimo kubwa katika eneo hilo hali iliyosababisha ashindwe kulimudu gari hilo kabla ya kuvaana uso kwa uso na basi hilo.

“Baada ya kuvaana, kontena la futi 40 lililokuwa limepakiwa katika loli hilo liliruka juu na kwa kishindo kikubwa, kubamiza na kufunika basi,” alisema.

Mmoja wa majeruhi wa basi hilo, Kevin Humphrey ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi alisema; “tulisikia mshindo mkubwa baada ya basi letu kugongana na lori hilo na mshindo huo ulisababisha na kontena iliyotoka kwenye lori hilo na kupiga juu ya basi letu.”

Ajali za barabarani zimekithiri nchini Tanzania. Mwaka 2014 watu zaidi ya 200 walifariki kutokana na ajali za barabarani. Ajali nyingi husababishwa na dharau na mwendo wa kasi wa madereva.

Magige naye aliniambia anataka kugombea urais - Mama Maria Nyerere

MTOTO mwingine wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Magige Nyerere, amejitokeza na kuonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Magige ni mtoto wa pili wa Mwalimu Nyerere kuonyesha nia ya kuwania uras baada ya hivi karibuni Makongoro Nyerere, kutajwa kuwa ni miongoni mwa watu wanaowania nafasi hiyo. 

Mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere amebariki watoto hao kuwania nafasi hiyo na kusema ni raia halali wa Tanzania na wanayo haki ya kufanya wapendavyo bila ya kuvunja sheria za nchi.

Mama Maria yaliyasema hayo jana nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ili kuwaondoa hofu wananchi juu ya uzushi kuwa amefariki dunia.

“Makongoro ni mtanzania, naye ameamua kujitosa, anayo haki ya kufanya apendavyo bila ya kuvunja sheria. Magige naye aliniambia anataka kugombea urais nikasema vema,” alisema.

Hata hivyo, alikiri kuwa suala la kuwania urais si jambo dogo, hasa kwa nchi change kwa sababu kuna mambo mengi muhimu ya kuzingatiwa.

Aliyekuwa mlinzi wa Dk Dlaa anayetuhumiwa kutaka kumuua, azungumza

Khalid Kangezi akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari

Aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Khalid Ahmada Kangezi amekanusha taarifa iliyotolewa na viongozi wa chama chicho kwamba alitaka kumuua bosi wake, Dk. Wilbroad Slaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema siku ya kifo cha marehemu Kapteni John Komba alikuwa akitokea nyumbani kwake Mwenge akielekea kazini nyumbani kwa Dk. Slaa ambapo baada ya kufika getini aliambiwa na mlinzi wa geti hilo kuwa haruhusiwi kuingia ndani na alipouliza sababu alijibiwa kuwa taarifa imetoka kwa mke wa Dk. Slaa.

Alipoendelea kuhoji alipewa majibu kwamba hapaswi kuendelea kumuuliza maswali ndipo aliamua kurudi tena nyumbani kujipanga kwa siku ambayo ingefuatia huku akiendelea kufanya juhudi za kumpata Dk. Slaa ili aweze kumuuliza sababu kuu ya kuzuiwa kuingia ndani.

Siku iliyofuatia ambayo ilikuwa Jumatatu ambapo Komba alikuwa anatakiwa kuagwa rasmi, alidamka asubuhi na mapema kuelekea nyumbani kwa Dk. Slaa kwani alijua kuwa naye angetakiwa kuungana na viongozi wengine kuuaga mwili wa marehemu. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kumkuta nyumbani japokuwa alizuiwa tena kuingia ndani ila majibu aliyopewa na Slaa ni kuwa aongee na mkewe wamalizane mgogoro wao na yeye akasema hakutaka kuingilia mgogoro huo.

Kangezi aliongeza kuwa hakutarajia kama mke wa Slaa angekuwa na mgogoro naye kwani walikuwa wakiitana mtu na kaka yake kwa vile wanatoka Mkoa wa Kagera.

Kangezi aliendelea kuelezea kuwa hakuamini kama kweli angeweza kufungiwa nje ya geti la nyumba kutokana na jinsi alivyokuwa akihangaika katika kuhakikisha ulinzi wa Dk. Slaa kwa nguvu ya hali ya juu kutokana na masuala ya vyama na ameishi naye kwa muda wa zaidi ya miaka 14 bila shida wala tuhuma yoyote.

Baada ya kukosa maelewano nyumbani kwa Dk. Slaa, aliamua kwenda katika ofisi za chama hicho zilizoko Kinondoni kwa ajili ya kuonana na kiongozi wake ambapo baada ya kufika alidai alizuiwa na viongozi wa chama hicho tena wakimtaka kuingia katika chumba maalumu kwa ajili ya kuchukua mahojiano naye ambapo alifanya kama alivyotakiwa.


Aliwataja viongozi wa chama hicho aliowakuta humo ambao tayari walimwamuru kuvua nguo zake zote na kubakia kama alivyozaliwa huku akitishiwa kuuawa. Humo alitakiwa kueleza mahusianao yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula, na watu wa usalama wa taifa ambapo alisema alisulubiwa kwa muda wa saa sita na akitakiwa kuandika katika karatasi kukiri kuwa kweli anawasiliana nao na kutokana na kipigo alichokuwa akikipata, akihofia kuuawa, aliamua kutii matakwa yao.

Siku hiyohiyo majira ya usiku alipelekwa katika hoteli iliyoko maeneo ya Sinza–Madukani ambapo alipakizwa katika gari lililokuwemo mwanasheria wa chama chicho, Mabere Malando, hadi kwenye hoteli waliyokuwa wamechukua vyumba na kumwingiza ndani ambako walianza tena kumsulubu hadi akaishiwa nguvu na akitakiwa tena aandike kuwa alikuwa na mpango wa kumdhuru Dk. Slaa kwa kumpa sumu,

Kutokana na uchovu aliokuwa nao aliamua kukiri kufanya hivyo huku akirekodiwa.

Alimalizia kwa kusema kuwa hajawahi kufanya jambo lolote la kutaka kumdhuru Slaa, na hata kiasi cha fedha kilichotajwa kuingiziwa na watu wa usalama wa taifa si kweli na hawezi kutunza fedha katika simu. Alieleza pia kwamba amefanya mambo mengi kwa Dk. Slaa na hivyo hawezi kumdhuru licha ya kufahamu siri zake nyingi.

via GPL