Google yatambulisha Android 5.1: HD, multi SIM, itakuwa na usalama kwa simu zitakazoibwa


Today we are rolling out Android 5.1 - an update to Lollipop that improves stability and performance and offers a few new features like support for multiple SIM cards, Device Protection and high definition (HD) voice on compatible phones.

Whether you want to share your phone with a family member or better manage your mobile costs, Android Lollipop 5.1 now lets you use more than one SIM card on a device with multiple SIM slots.

With Device Protection, your lost or stolen device will remain locked until you sign in with your Google account - even if someone resets your device to factory settings. This feature will be available on most Android phones and tablets shipped with Android 5.1 in addition to Nexus 6 and Nexus 9.

High Definition voice calling is now on your mobile phone. Get crystal clear calling with HD Voice between compatible Android 5.1 devices like the Nexus 6 on T-Mobile or Verizon.

Android 5.1 Lollipop also provides enhancements such as the ability to join Wi-Fi networks and control of your paired Bluetooth devices directly from Quick Settings.
We hope you enjoy these tasty additions to Android Lollipop as you get more out of your Android phone and tablet.Kampuni ya Google imetangaza kutoa Android 5.1 katika mradi wake wa Android itakayokuwa kwenye mfumo wa HD, SIM na usalama zaidi.

Madai hayo ambayo hayakutangazwa rasmi na Google kuhusiana na Android 5.1 yalivujishwa hapo awali na baadaye yakathibitishwa rasmi kwenye Blog ya Android.

Baadhi ya maelezo kuhusiana na utendaji kazi wa Android 5.1 pia yalitolewa. Android 5.1 itakayokuwa na uwiano wa matumizi ya SIM Card katika vifaa vya mawasiliano kama vile simu, utawawezesha watumiaji kufanya mawasiliano ya katika mfumo wa HD.

Hata hivyo kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa matatizo kati ya Android mpya na zile za zamani, watumiaji wa simu zenye Android 5.1 pekee ndio watakaofaidika na huduma hii ya mawasiliano ya mfumo wa HD.

Android 5.1 pia inaarifiwa kuboreshwa kwa mfumo wa usalama wa hali ya juu. Endapo vifaa vyenye Android 5.1 vitapotea au kuibiwa, basi vitajifunga na kuzuia utumiaji wake.

Google itahakikisha usalama kikamilifu kwa kufungua akaunti maalum kwa mtumiaji ili baadaye kusaidia kuuliza kithibitisho kupitia akaunti hiyo iwapo vifaa vilivyoibiwa vitathubutu kuchakachukuliwa.

Three Malawi players join Tanzanian club on loan


via The Nyasa Times — Thunder Queens coach Mary Waya and three players Joana Kachilika, Martha Dambo and Sheiraz Kaiche left Malawi last week to join a Tanzanian club Uhamiaji Sports Club on loan.

Waya confirmed of the deal before departure but declined to shed more light saying it is a private issue.

“What I can say is that I am going to Tanzania with three MTL players. There’s no need for the public to know that about,” Waya said.

Netball Association of Malawi (NAM) President Rosy Chinunda confirmed saying Waya and the three players were hired on a short loan.

“I can confirm that the coach and the three players were cleared to join the Tanzanian team on a short term,” Chinunda said.

“I am not aware of the specific agreements as regards terms but suffice to say that the two teams [Thunder Queens and Uhamiaji Sports Club] have a mutual working relationship. As for the terms and conditions the Thunders coach herself can shed more light.”

Chinunda however said the coach and the players move would affect the national and their clubs as there are no major activities soon.

“It’s just a short term loan deal. We expect that they will back soon even before the Airtel National netball tournament reaches the national stage. We feel it is a good move as the players stand to gain in terms of international exposure.”

Kachilika and Dambo are also national team players.

Thunders Queens spokesperson Christina Mkwanda confirmed the development but declined to divulge more information about the deal.

Chuo Kikuu cha Kiislamu chawa cha kwanza kutambuliwa Marekani


Chuo Kikuu cha Zaytuna kimekuwa chuo cha kwanza cha Kiislamu kutambuliwa nchini Marekani

Chuo Kikuu cha Zaytuna kilianza katika mwaka wa 2010 katika mji wa Berkeley katika jimbo la Carlifornia kama chuo kikuu cha Kiislamu. Mwaka huu chuo hicho kimeandikisha historia kwa kuwa chuo kikuu cha kwanza cha Kiislamu kuidhinishwa na tume ya kuidhinisha vyuo ya Muungano wa Magharibi wa shule na vyuo (WASC).

Muungano wa WASC ni moja ya miungano 6 inayoidhinisha vyuo nchini Marekani.

Chuo Kikuu cha Zaytuna kilichoanza kutoa huduma mwezi Septemba mwaka wa 2010 hutoa mafunzo katika vitengo vya Sheria ya Kiislamu, Theolojia na Kiarabu.

Chuo hichi kiliundwa katika mwaka wa 1996 na Hamza Yusuf ambaye alisimu pamoja na Zaid Shakir.

Vyuo vingine vya kidini nchini Marekani ni kama chuo cha Kikatoliki cha Notre Dame (Indiana),Yeshiva (New York) cha Mayahudi na Wheaton (Massachusetts) cha Wainjilisti.

Balaa! Pombe kuuzwa katika mfumo wa unga yamkera Seneta

Imenukuliwa kutoka NPR.org: Powdered Alcohol Faces Hurdles After Regulatory Approval


Two days after a federal regulator approved powdered alcohol, there's already an attempt to ban it.

Sen. Charles Schumer, D-N.Y., said today he is introducing legislation in the Senate to make the production, sale and possession of Palcohol illegal.

"I am in total disbelief that our federal government has approved such an obviously dangerous product, and so, Congress must take matters into its own hands and make powdered alcohol illegal," he said. Underage alcohol abuse is a growing epidemic with tragic consequences and powdered alcohol could exacerbate this."

Palcohol got the green light this week from the Alcohol and Tobacco Tax and Trade Bureau for its powdered versions of a cosmopolitan, a margarita, rum and vodka. Another product, Lemon Drop, is expected to be approved soon, The Associated Press reported.

The Alcohol and Tobacco Tax and Trade Bureau had approved the product last year – before quickly reversing that decision.

As NPR's Michaeleen Doucleff reported at the time:

"The idea behind Palcohol is simple: dehydrated vodka or rum inside a little air-tight package.

"Tear open the package, sprinkle the powder into tonic water and voila! You've got a vodka tonic with an alcohol concentration about the same as a regular cocktail (about 20 proof but the exact alcohol concentration will depend on how much liquid you add).

"In other words, it's like an adult version of Kool Aid or Country Time Lemonade."

Palcohol says on its website that it hopes to be on shelves by this summer.

Schumer's proposed legislation is not the only roadblock the product faces. Several states have already banned powdered alcohol, and other states are considering bans amid fears that minors and others will abuse the product. But Palcohol says the reason for the bans is the liquor industry's desire to "squash competition and protect their market share." And, it says, it will be sold where regular alcohol is sold and with the same rule: You can't legally buy it if you're under 21.

And if you're wondering whether you can snort the powder, Palcohol says:

"Listen, people can snort black pepper....so do we ban it? No, just because a few goofballs use a product irresponsibly doesn't mean you ban it. But even the goofballs won't snort Palcohol due to the pain the alcohol would cause. It really burns. Imagine sniffing liquid vodka. Second, it's impractical. It takes approximately 60 minutes to snort the equivalent of one shot of vodka. Why would anyone do that when they can do a shot of liquid vodka in two seconds?"

Habari ya Dk Slaa kutoa maelezo Polisi ilivyotambulishwa na magazeti
Sarafina Lidwino na Deusdedit Kahangwa via MwanaHALISI OnlineDk. Slaa afichua mauaji dhidi yake; awataka TISS, Kikwete waachie ngazi

KIONGOZI mkuu wa upinzani nchini, Dk. Willibroad Slaa, amekoleza moto kuhusu madai ya kutokomeza maisha yake.

Dk. Slaa amelieleza jeshi la polisi jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi) kuwapo mpango wa kumuua uliokuwa unasukwa na baadhi ya viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Katibu mkuu huyo wa Chadema, ameiambia MwanaHALISI Online, muda mfupi baada ya kusajili maelezo yake kituo cha Polisi cha Kati, “Mungu bado ananipenda na anakipenda Chadema.”

Alisema, “Tumepata ushahidi usio na shaka kuhusu mpango wa kutaka kuniua. Kumekuwa na mawasiliano mazito sana kati ya maafisa usalama, viongozi wakuu wa CCM na mlinzi wangu. Mawasiliano haya yalilenga kudhuru maisha yangu.”

Amesema, “Tumebaini kwamba Idara ya Usalama wa Taifa walikuwa wanafanya ujasusi dhidi ya Chadema. Walikuwa wanatoa fedha kwa mlinzi wangu binafsi ili kumshawishi kuvujisha siri za chama. Jambo hili ni kinyume cha sheria ya kuanzishwa idara ya usalama wa taifa.

Amesema, kutaka kufanya au kutishia kuua, ni kosa la jinai, hivyo analitaka jeshi la polisi kuhakikisha mhalifu huyo, anakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Taarifa zinasema, aliyekuwa anashirikiana na TISS na viongozi wa CCM kutokomeza maisha ya Dk. Slaa, ametajwa kuwa ni Khalid Kagenzi.

Kwa mujibu wa mawasiliano katika simu ya Kagenzi, aliyekiri kushiriki njama za kumuua Dk. Slaa, waliokuwa wanawasiliana na Kagenzi, ni pamoja na Philiph Mangula, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara; Gwamaka Mwang’onda na wengine kadhaa, ambao watachapishwa katika mtandao huu katika toleo lake la Jumamosi.

Akizungumza kwa uchungu na mwandishi wa gazeti hili, Dk. Slaa amesema, “Idara ya usalama wa taifa imepoteza heshima katika jamii na kuwataka viongozi wake wajiuzulu.”

Ametoa mfano wa nchini Marekani, kwamba “…ilipothibitika Rais Nixon na chama chake cha Republican walikuwa wamefanya ujasusi dhidi ya chama cha democrats, Rais Nixon alilazimika kujiuzulu. Hata CCM na idara yao ya usalama wa taifa wanafanya kosa kama hilo.”

Mwenyekiti wa CCM na ambaye ni Rais wa Jamhuri, ni Jakaya Kikwete.

Dk. Slaa amesema yeye alifika polisi kama mlalamikaji. Alitoa maelezo yake ili kuwawezesha kufanya kazi yao ya uchunguzi.

Amesema, “Sikuhojiwa kama baadhi ya watu wanavyofikiri. Mimi sio mtuhumiwa. Mimi ni mlalamikaji.”

Amesema haki zake zote zimezingatiwa alipokuwa polisi. Aliongozana na wanasheria watatu wa Chadema, Prof. Abdallah Safari, Nyaronyo Kicheere na John Mallya.

Prof. Safari, pia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara.

Zoezi la kuandika maelezo yake, lilitanguliwa na majadiliano kati yake na polisi ili kujenga picha ya pamoja kuhusu jambo litakalo andikwa.

Anasema, polisi waliuliza kama nataka waandike maelezo yangu wao au nataka kuyaandika mwenyewe. Nilichagua kuyaandika mwenyewe. Sheria inaruhusu hili pia.

Malalamiko yake yana kurasa tisa.

Akizungumzia wanachama watatu wa Chadema wanaoshikiliwa na polisi, Ahmed Sabula, Benson Mramba na Jacob Boniface (Diwani wa Ubungo), Dk. Slaa amesema, “Ni jambo la kusikitisha, muuaji yuko nje na waliozuia mauaji ndiyo wanaoshikiliwa.”

Habari ambazo zimepatikana baadaye zinasema, jeshi la polisi limeahidi kuwapa dhamana “makachero” hao wa Chadema kesho.

BoT yajieleza PAC kuhusu biashara haramu ya fedha na 'walioficha' fedha nje

Kushamiri kwa fedha haramu nchini kunakofanywa na baadhi ya Watanzania wasio waaminifu ndani na nje ya nchi, kumeisababishia taifa hasara ya bilioni 590/- (dola milioni 328) kila mwaka, imeelezwa.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Rished Bade wakati akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Akitoa ufafanuzi, Dk Bade alisema zipo taarifa mbalimbali zilizofanywa na mashirika ya nje zinazoonesha kuna tatizo la fedha haramu nchini, jambo ambalo hatua zimechukuliwa na utafiti wa jambo hilo unaendelea kubaini ukweli wake, lakini hilo linawezekana kwani wapo watanzania wanaofanya biashara na kukwepa kulipa kodi.

“Ripoti ya Benki ya Kimataifa ya HBSC yenye makao yake Uingereza, ilitoa taarifa za akaunti zenye fedha haramu zinazofanywa na makundi mbalimbali, na Tanzania imetajwa kuwepo, sasa hawa watu wanatumia mbinu nyingi kuhakikisha wanaikosesha nchi mapato”, alisema Dk Bade.

Alisema kiwango hicho cha dola milioni 328, ni kikubwa na kwamba matukio hayo yanafanywa na watanzania wasio waaminifu, ambao hutumia mbinu nyingi za biashara kudanganya kiwango halali cha fedha walichokipata kwenye biashara husika.

Awali akizungumza mbele ya kamati hiyo, Dk Bade alisema fedha haramu zinatokana na baadhi ya wafanyabiashara au watu wengine kufanya biashara nje ya nchi au kuingiza, lakini hawatoi takwimu sahihi, jambo ambalo wanakwepa kulipa kodi.

“Unakuta mtu amefanya biashara nje ya nchi, na hatoi takwimu sahihi, anaweza kuwa ameuza tani mfano laki mbili, ila anasema ameuza tani laki moja sasa hiyo tani laki moja nyingine iliyouzwa haikatwi kodi, na ndiyo fedha haramu zenyewe hizo,” alisema Dk Bade.


Alifafanua kuwa kwa kutambua tatizo hilo, hivi sasa nchi imesaini Mkataba wa Kimataifa wa kupata taarifa za kodi kutoka mataifa mbalimbali duniani, ili kupata takwimu sahihi za watanzania wanaofanya biashara nje na kukwepa kodi.

“Jambo hili ni baya kwa ukuaji wa uchumi wetu, ila tumesaini Mkataba wa Kimataifa wa kupata taarifa za kodi, tumesaini mkataba huo Februari mwaka huu, utatusaidia kupata taarifa za watu wanaofanya biashara nje, na wasiolipa kodi halali,” alisema Dk Bade.

Wakati huo huo, Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT), Juma Reli alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kubanwa na kamati hiyo iliyomtaka kueleza Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 na Waraka uliotoka mwaka 1998, unaoelekeza ufunguaji wa akaunti nje ya nchi.

Katika maswali ya kamati hiyo, BoT ilihojiwa iwapo inatoa vibali vya watu kufungua akaunti nje ya nchi.

Akijibu hoja hiyo, Gavana huyo alisema benki haitoi vibali kwa Watanzania waishio nchini, kufungua akaunti kwenye benki zilizo nje ya nchi, kwa kuwa sheria hairuhusu, ila kampuni za madini zinaruhusiwa, baada ya benki hiyo kuzipa vibali.

Kadhalika, pia watanzania waishio nje wanaweza kufungua akaunti kwa kuwa hawaishi nchini na pia kwa watumishi wa mashirika ya kimataifa waishio nje au kufanya kazi nje ya nchi.

Aliongeza kuwa hadi sasa hawana taarifa za watu binafsi wenye akaunti nje ya nchi, kwa kuwa kama wapo wamefanya hivyo bila vibali na ni kosa, lakini njia za kuwafuatilia ni ngumu kwa kuwa hawana mfumo wa kupata taarifa kutoka benki hizo.

Jibu hilo lilisababisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kabwe Zitto kuishauri serikali kuomba kupewa taarifa kutoka nchi za Uswisi na Uingereza za Watanzania wenye akaunti nje ya nchi.

Aidha, Zitto alihoji kwa gavana, iwapo benki ya HBSC, ina kibali cha kuja kuwafungulia akaunti wateja wa kitanzania na kama sio hatua gani zimechukuliwa.

Akijibu hoja hiyo, Gavana alisema, sheria hairuhusu benki hiyo kuja kufanya shughuli za kibenki nchini na kwamba kama benki hiyo imefanya hivyo, imevunja sheria ila BoT haina taarifa.

“Hatuna taarifa kama HSBC wamekuja Tanzania kukutana na wateja wake, na kama wamekuja wamevunja sheria,” alisema Reli.

Pamoja na hayo, kamati ilitoa maagizo kwa vyombo hivyo viwili, yaani BoT na TRA kuhakikisha wanakuwa na utaratibu baina yao wa kufuatilia walipa kodi ili wajulikane na kuondoa tatizo la ukwepaji kodi, unaosababisha uwepo wa fedha haramu nyingi.

Aidha BoT, imeagizwa kufuatilia benki hiyo ya HSBC, na kuichukulia hatua kwa kuvunja sheria za kufanya biashara na wateja wa hapa nchini kinyume na utaratibu, ili mabenki mengine yafahamu kuwa Tanzania sio nchi ya kuichezea.

Hata hivyo, Gavana Reli alisema mwishoni mwa mwaka huu kamati inayosimamia utafiti kuhusu fedha haramu nchini Tanzania, iliyoundwa mwaka 2012, ikiwashirikisha wadau kutoka nje ya nchi itapokea taarifa ya suala hilo, na itawekwa wazi kwa umma.

Hivi karibuni ripoti ya mtandao wa Swiss Leaks chini ya Waandishi wa Habari za Uchunguzi wa Kimataifa (ICIJ), ulifichua kuwepo kwa Watanzania 99, wenye akaunti za siri nchini Uswisi zenye mabilioni ya fedha.

Taarifa ya Swiss Leaks ilionesha kuwa Watanzania hao, wana akaunti za siri zenye Dola za Marekani milioni 114, ambazo ni sawa na Sh bilioni 199.6.

Ripoti hiyo ilitokana na aliyekuwa mfanyakazi wa Benki ya Kimataifa HSBC, Hervé Falciani, kuvujisha siri za akaunti za wateja baada ya yeye kuacha kazi.


Taarifa ya Ofisi ya W/Mkuu ya idadi ya Katiba Inayopekendekezwa zilizokwishasambazwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

*Nakala zaidi ya 650,000 kusambazwa kwenye taasisi

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema hadi kufikia Februari 26, mwaka huu, Serikali imekwishasambaza jumla ya nakala 1,341,300 za Katiba Inayopendekezwa Kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, jana jioni (Jumatano, Machi 11, 2015) Waziri Mkuu alisema Zanzibar imepatiwa nakala 200,000 na kuongeza kuwa nia ya Serikali ya kuchapisha nakala milioni mbili iko palepale.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alibainisha kwamba nakala 658,700 zilizobakia zitagawanywa Kwenye wizara zote za Tanzania Bara na Zanzibar, Mahakama, Bunge, Baraza la Wawakilishi, taasisi za Serikali, Tume zote, taasisi za dini, asasi za kiraia, vyombo vya sheria, vyuo vya elimu ya juu, vyama vya siasa na na taasisi zinazojitegemea ili kuongeza wigo wa usambazaji kwa wananchi wengi zaidi.

“Lazima nikiri kwamba kuzisambaza na kuzifikisha kwa walengwa ni jambo moja na kuhakikisha kwamba zinasomwa ni jambo jingine. Wito wangu kwa Watanzania wote ni kuhakikisha wanasoma na kuielewa Katiba Inayopendekezwa ili wanapokuja kupiga kura waelewe ni nini wanafanya,”
alisema.

“Niwasihi sana Watanzania wenzangu, wasikubali kurubuniwa juu ya kilichoandikwa Kwenye Katiba Inayopendekezwa, na tena mtu asikubali kuombwa kuomba auze nakala yake. Tusikubali watu warubiniwe kirahisi. Kila mmoja ahakikishe anaisoma na kuielewa, na wenye mitandao na blogs watumie fursa hii kuusambazia umma nakala za Katiba hii ili watu wengi zaidi waweze kuisoma,” alifafanua.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM
ALHAMISI, MACHI 12, 2015.

Skimu ya mpunga Kiroka

Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla, akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi walipofanya ziara ya kugagua miradi yao ya maendeleo mkoani Morogoro.(picha: Zainul Mzige wa modewjiblog)

Morogoro — BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi ametembelea skimu ya umwagiliaji ya Kiroka na kusema kwamba atahakikisha kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali wataendelea kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.

Akiwa katika skimu hiyo inayosaidiwa na Shirika la Chakula duniani (FAO) ametaka miradi ya maendeleo nchini kutowaacha nyuma wanawake na watoto kwani wao ndio msingi wa maendeleo ya kijamii kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

Balozi huyo ambaye anatarajiwa kurejea Ulaya mwaka huu baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini amesema kwamba kuwapo kwa asilimia 60 ya wafaidika na mradi huo wa Mpunga kuwa wanawake kumesaidia sana kuamsha maendeleo ambayo yanatakiwa kuendelea kusimamiwa.

"Wanawake wamefanikiwa kupeleka watoto wao shuleni. kuwapatia chakula kinachostahiki na kupata kipato na katika hili ni vyema wasiachwe nyuma kimaendeleo" alisema balozi huyo.

Alisema kwamba amefurahishwa sana na mradi huo na kusema kwamba Umoja wake utaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha kwamba mwananchi wa kawaida wa Tanzania anapata maisha bora.

Mradi wa Kiroka ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya FAO na benki ya NMB ikishirikiana na RaboBank umelenga kuboresha kilimo cha Mpunga na pia kuwawezesha wakulima hao kuwa na nafasi ya kupata fedha za kuendeleza majukumu yao.

Ili kufanikisha hilo wakulima wanapatiwa elimu ya fedha na pia utunzaji wa nafaka wa pamoja na mikakati ya mauzo.

Mradi huo ulioanza 2004 na kutarajiwa kuisha Juni mwakani unatekelezwa 2018 umelenga kufungua fursa kwa wanawake na wanaume na kuongeza uzalishaji, kusaka masoko, kupata njia ya kupata mikopo na kujenga uwezo wa kufanikisha shughuli za maendeleo kwenye skimu.

Mradi huo unatarajiwa kutumia dola za Marekani 737,000 hadi utakapokamilika.

Wakizungumza na balozi huyo kuelezea mazingira yao wakulima walishukuru msaada unaotoka katika mashirika ya kimataifa na kuwaomba kusaidia kuwapatia fursa zaidi za maendeleo kwa elimu wanayoipata.

Wamesema mabadiliko yaliyosababishwa na elimu yamewafanya wazalishe Mpunga kwa wingi katika eneo dogo na kufungua fursa za masoko kwa hifadhi na utafutaji masoko wa pamoja.

Mradi huo ambao ulianza na Watu wa Sua kama watoa elimu sasa wanapigwa msasa na Taasisi ya maendeleo mjini na Vijijini (RUDI) kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanatumia mfumo wa Asia wa ulimaji wa Mpunga kwa kutumia maji kidogo huku wakihifadhi ghalani kusubiri bei nzuri.

Katika ziara hiyo ya karibuni ya Balozi huyo akiambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, viongozi hao walipata nafasi ya kusikiliza changamoto za wakulima katika mradi huo ambapo uzalishaji sasa umeongezeka kutoka gunia tano kwa eka kufikia gunia 25 kwa kulima kitaalamu.

Katibu wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu alisema mradi huo ambao ulianza Februari 21,2012 umewajengea uwezo wakulima wa mlimani kutengeneza makinga maji huku wakulima wa kwenye skimu wakilima kilimo cha mashadidi.

Alisema wanawashukuru wahisani kwa kuwawezesha kurejesha uoto wa kijani ikiwa na pamoja na kuwa na kilimo cha matunda.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe amesema skimu imewasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.

Aidha wakulima wamefanikiwa kununua vyombo vya usafiri vya moto kama Pikipiki na kuachana na Baiskeli.Hata hivyo amesema pamoja mafanikio hayo wanachangamoto hasa ya masoko na elimu ambayo wanadhani wanaihitaji zaidi huku akisisitiza zaidi kwamba elimu inatakiwa hata kama wamemaliza mradi na wahisani kuondoka.

Mradi bado ambao haujakamilika kwani kati ya hekta 147 za mradi ni kama hekta 40 zinazotumuka kwa kuwa miundombinu haijatawanyika vya kutosha katika hekta zote.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akizungumza na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wanaofadhiliwa na FAO wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo ambapo mradi wa Kiroka unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la FAO huku mradi wa makazi mapya kwa waathirika wa mafuriko Kilosa ukifadhiwa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya. Kushoto kwake ni Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.


Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akifafanua jambo wakati akitoa salamu kwa wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI). Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.


Katibu wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu akielezea mafanikio waliyoyapata tangu walipoanza kupewa mafunzo ya kilimo bora yanayofadhiliwa na Shirika la FAO mbele ya ugeni huo.


Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe akielezea jinsi skimu ilivyowasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.


Mwanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), mkoani Morogoro, Bi. Asha Bogasi akitoa ushuhuda jinsi maisha yao yalivyobadilika mpaka wanaweza kusaidia na waume zao kusomesha watoto wao kutokana na skimu ya mradi huo.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na kuwapa pongezi za kuweza kubadilisha maisha yao kupitia kilimo cha kisasa kinachofadhiliwa na FAO kwa wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) alipofanya ziara ya kukagua mradi huo kijijini hapo.


Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wakiwa wamekusanyika kwenye shule ya msingi Kiroka wakati wa ugeni wa Shirika la Umoja wa mataifa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya ulipowatembelea kukagua miradi yao.
Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Balozi wa Umoja wa Ulaya wakiondoka kijijini hapo mara baada ya kukutana na kuzungumza na Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI).

Kauli ya CCM kwa CHADEMA kuhusu tuhuma za jaribio la kumwua Dk Slaa

The 10 Best Universities in the World in 2015


The U.S. has 43 of the top 100 schools in an annual list of the world’s most prestigious universities.

This year the number one school in The Times Higher Education World Reputation Rankings 2015 is Harvard University, followed by Cambridge University. The U.S. and the UK are the best represented nations on the list – this year the U.S. claims 43 schools on the list, down from 46 last year and the UK boasts 12, up from 10 in 2014. While the order has changed, the top six schools always remain constant, according to The Times Higher Education

Here is this year’s top ten:

  1. Harvard University
  2. Cambridge University
  3. University of Oxford
  4. Massachusetts Institute of Technology
  5. Stanford University
  6. University of California, Berkeley
  7. Princeton University
  8. Yale University
  9. California Institute of Technology
  10. Columbia University

For methodology, analysis, ranking and more, please visit: TimesHigherEducation.co.uk - 

World Reputation Rankings 2015 results

Picha za Rais Kikwete alipoketi leo na kuwafariji walioathiriwa na mvua ya mawe Kahama

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12, 2015.

Maelefu ya Wakazi wa Kahama wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia mara baada ya kutembelea na kujionea athari ya Mvua ya Mawe kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo Machi 12, 2015.

Dk Slaa atoa maelezo Polisi; Makala ya Ndimara kuhusu watu waliouawa kwa sumu

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (kulia) akitoka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo huku akiambatana na wanasheria wake, John Mallya (kushoto) na Nyaronyo Kicheere ambapo aliandika maelezo na kuhojiwa na Polisi kwa saa sita kuhusiana na tuhuma za kutaka kuuwawa na mlinzi wake, Khalid Kagenzi.
(picha: Francis Dande)

SIKU mbili baada ya kuwachiwa mtuhumiwa Khalid Kagenzi anayedaiwa kutaka kumuuwa kwa sumu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hatimaye Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa, naye ametoa maelezo yake Polisi leo.

Dk Slaa alifika Kituo Kikuu cha Kati majira ya saa nne asubuhi na kuandika maelezo kuhusu tishio la kutaka kuuawa kwa kulishwa sumu.

Dk Slaa aliongozana na wanasheria wake Nyoronyo Kicheere na John Mallya na kwa muda na saa sita alitoa maelezo huku baadhi ya wananchama waliombatana naye wakimsubiri nje.

Baadhi ya viongozi aliyoongozana nao walikuwa ni Profesa Abdallah Safari ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Godbless Lema na John Heche.

Akizungumza na wandishi wa habari, Dk Slaa, alisema kuwa maelezo hayo yatumika katika ushahidi kuhusu tukio hilo.

Aidha, Diwani Ubungo (CHADEMA), Jacob Boniface alikuwa akihojiwa hata hivyo hadi waandishi wanaondoka katika eneo hilo alikuwa hajotoka kituoni hapo.

Kufikishwa katika kituo hicho kumetokana na sakata CHADEMA kutoa tarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kulikuwa na mpango wa mlinzi wake Kagenzi kutaka kumuua kwa sumu.

Tishio kwa maisha ya Dk. Slaa lisipuuzwe

Ndimara Tegambwage

MAISHA ya Dk. Willibrod Slaa yametajwa kuwa hatarini. Chama chake kinasema kuna “mradi” wa kuzimisha maisha yake kwa kutumia sumu.

Dk. Slaa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mbunge kwa miaka 15. Mgombea urais mwaka 2010; na bado kuna uwezekano wa kumtuma tena mwaka huu.

Kinachoshangaza wengi ni kutosikia taratibu za kupima afya ya Dk. Slaa ili kuona kama tayari amedhurika.

Kama kuna taarifa za kutaka kumuua kwa sumu, ina maana anaweza kuwa amelishwa sumu tayari ambayo inaua taratibu.

Félix-Roland Moumié
Tishio kwa maisha siyo jambo la kudharau. Félix-Roland Moumié wa Cameroon aliuawa kwa kula sumu aina ya thallium aliyowekewa katika chakula, mjini Geneva, Uswisi tarehe 3 Novemba 1960. Taarifa zilitaja maofisa wa Idara ya Usalama ya Ufaransa (SDECE) kuhusika na kifo hicho.

Moumié aliauwa miaka miwili baada ya kuchukua uongozi wa chama cha kizalendo cha nchi hiyo – Union du Peuple Camerounais. Aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, Ruben Um Nyobe aliuawa kwa njama hizohizo Septemba 1958. Ni mazingira hayahaya.

William Bechtel anayetajwa kutumia sumu hiyo kumuua Moumié, alifahamika kuwa mwanachama wa kikundi cha kishushushu kilichoitwa Main Rouge (mkono mwekundu); kilichokuwa na jukumu la kuua wazalendo Afrika ambao walipingana na utawala uliokuwapo; na ulioungwa mkono na Ufaransa.

Alexander Litvinenko wa Urusi alifia mjini London, Uingereza, Novemba 2006, wiki tatu baada ya kulishwa sumu iitwayo polonium-210.

Alifariki akidai kuwa kilichomkumba kwa wiki tatu za mahangaiko, kina mkono wa rais wa sasa wa Urusi,Vladimir Putin; madai ambayo yalileta tetemeko katika uhusiano wa Urusi na Uingereza.
Alexander Litvinenko

Litvinenko, aliyekuwa ofisa katika idara ya ushushushu nchini Urusi (FSB) na shrikika la kijasusi la nchi hiyo (KGB), alikimbia mashitaka katika mahakama za Urusi.

Akiwa nchini Uingereza alifanya kazi katika idara za kishushushu – za MI5 kwa mambo ya ndani ya nchi; na MI6 kwa ushushushu nje ya nchi. Alikufa.

Georgi Markov wa Bulgaria alifariki tarehe 7 Septemba 1978 kutokana na sumu iitwayo ricin. Mmoja wa wapinzani wa serikali, Markov alifia mjini London alikokuwa mkimbizi.

Markov alivuka daraja la Waterloo. Akasimama kwenye kituo cha mabasi ili aende shrika la utangazaji la Uingereza, BBC. Mara akasikia mchomo kwenye paja lake la kulia. Alipogeuka alikuta mwanaume mmoja akiokota mwavuli.

Georgi Markov
Mwanaume huyo alimwambia, “Oh, samahani!” iliyosikika katika lafudhi ya kigeni na siyo ile ya London. Halafu mwanaume huyo akasimamisha teksi na kuondoka. Siku nne baadaye, Markov alifariki.


Kilichomuua Markov ni mwavuli ambao ncha yake ilikuwa na sumu. Kwa mara nyingine, Urusi ilitajwa; mara hii kwa kushirikiana na Bulgaria “kuua mpinzani.” Hata ndani au nje ya nchi, watakuwinda!

Daktari alipokata kipande cha nyama pajani ambako Markov alichomwa na kukichunguza, alikuta kitu kama kidonge chenye ukubwa wa milimita 1.52 kilichotengenezwa kwa kemikali za platinum na iridium.

Ndani ya kidonge hicho chenye matundu mawili yaliyozibwa kwa nta, ndiko ilikuwa imemwagwa sumu ipatayo moja ya tano ya milimita (1/5).

Nta hiyo iliyeyuka kutokana na joto la mwili na kuachia sumu iitwayo ricin kumiminika mwilini mwa Markov; kushambulia tezi la limfu, kusababisha damu kuvuja mwilini; na katika siku ya nne, figo na moyo kushindwa kufanya kazi. Alikufa.

Victor Yushchenko, rais wa sasa wa Ukraine aliponea chupuchupu mwaka 2004. Alilishwa sumu aina yadioxin. Uchunguzi katika jaribio hili la kutaka kumuua, ulianza mwaka 2007, lakini hakuna hata mshukiwa aliyewahi kufikishwa mahakamani.

Daktari wake, Mykola Korpan anasema rais anaendelea vizuri na sura yake iliyokuwa imepotea katikati ya vipele na msinyao, sasa inaanza kurejea kwa kasi.

Mwendesha mashitaka mkuu wa Ukraine amekuwa akidai kuwa ni nchi tatu tu ambazo zinaweza kuwa zimefanya jaribio hilo, “Urusi ikiwemo.” Urusi, hata hivyo, imekuwa ikikana.

Yushchenko alilishwa sumu muda mfupi kabla ya kuchukua urais mwaka 2007, akimwondoa madarakani waziri mkuu Viktor Yanukovych aliyekuwa akidaiwa “kushinda uchaguzi kwa wizi.”

Turudi nyumbani. Madai ya kuua, kujeruhi, kupoteza na kudhuru kwa njia mbalimbali, hayawezi kupuuzwa. Hii ni kwa sababu nchi hii siyo kisiwa; na hata visiwa vinafikika na kuzama katika matendo ya kiharamia.

Ni Chadema waliokosesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) usingizi mwaka 2010; kwani waliporomosha umaarufu wa Rais Jakaya Kikwete (wa 2005), kutoka asilimia 80.28 za kura hadi asilimia 62.83 katika uchaguzi uliopita.

Ni Chadema waliozoa, katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana, vijiji, vitongoji na mitaa mingi kuliko wakati wowote tangu uchaguzi katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Ni Chadema na UKAWA sasa ambao wameshikia bango kashfa hii na ile ambazo zimeikumba serikali ya Rais Kikwete na kujipa jukumu la kueleza wananchi na dunia nzima kuwa “watawala wamechafuka; wamechoka, wakae pembeni.”

Ni vyama vya upinzani ambavyo kila kukicha vinazuiwa kufanya mikutano na kufanya maandamano. Vinafyatuliwa risasi na mabomu ya pilipili.

Ni vyama hivi ambavyo viongozi wake maeneo ya shamba – vijijini, wanatishwa, wanawekwa rumade bila sababu za msingi; na mwaka jana wengi waliporwa fursa na haki ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika mazingira haya, huwezi kupuuzia kauli au tuhuma au madai tu kuwa kiongozi huyu au yule ameundiwa njama za kumjeruhi, kumuua au kumpoteza. Ni mazingira tete. Ni mazingira hatarishi. Ni wakati wa kujenga shaka kwa kila kitu na kila kauli.

Mazingira haya katili yanaimarishwa na kauli, kwa mfano kutoka Sauti ya Kisonge (Mwembe Kisonge) Zanzibar, kuwa wao (CCM) hawatoi “nchi kwa yoyote.”

Ni kauli zinazoimarisha utukutu katika siasa; hadi viwango vya wanasiasa wa CCM kuviambia vyama vingine vya siasa na kuvitolea kauli kama, “ikulu mtaisikia redioni!”

Hizi ni kauli za ujambazi kisiasa. Haziashirii mwafaka wa aina yoyote. Ni kufa tu. Hakuna kupona. Katika mazingira haya, tena karibu na uchaguzi mkuu, madai na tuhuma za aina yoyote ile zaweza kuwa kweli.

Nchi hizi – Tanganyika na Zanzibar, ni zetu sote. Kupata mwafaka – kwa njia ya mashindano huru na haki – kwenye sanduku la kura, ndiko kila mmoja mwenye nia safi anatafuta na angetarajiwa kutafuta.

Kuua kwa sumu au silaha, visiwe sehemu ya msamiati, vitendo, wala imani za Watanzania. Dk. Slaa awepo kama wengine. Ulingo wa siasa uwe wazi na anayetaka kushindana naye apande jukwaani tumuone: Pale!

0713 614872
[email protected]
Makala hii imechapishwa katika gazeti la MAWIO, 12 Machi 2015

Video iliyorekodiwa kwa simu wakati majambazi yakiiba Mikocheni kwa Nyerere duka la MohansVideo iliyopachikwa hapo juu (imepatikana via WhatsApp) inaonesha tukio la leo Alhamisi, Machi 12, 2015 la majambazi wakivamia na kisha kupora fedha kutoka kwenye maduka katika eneo la Mikochieni mitaa ya kwa Mwalimu Nyerere kutoka kwenye ATM ya CRDB na duka la vinywaji la Mohans na maduka mengine ya jirani, ambapo inasadikiwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 100/= kilichukuliwa.

Taarifa ya kuokotwa pasipoti na nyaraka nyingine a Gladness MartinBi Gladness Martin Brush, pasipoti yako na vitu vyako vingine ambavyo ulipoteza ama kwa kudondosha au kuporwa pochi yako, basi hati yako hiyo na vitu vingine mbalimbali vimeokotwa na vipo katika mikono salama.

Yeyote anayemfahamu mhusika ampe taarifa afike Ofisi ya Mtendaji, Kata ya Tabata Mzimbazi Sokoni, naye atakabidhiwa.

Kwa maelezo zaidi, piga 0713624583