Waraka wa Jukwaa la Wakristo kuhusu Katiba, Mahakama ya Kadhi, usalama na amani


Petition ya Watanzania UK kupinga vikali utaratibu mpya wa ukaguzi magari

WATANZANIA NCHINI UINGEREZA/UK WANAPINGA VIKALI UTARATIBU MPYA WA UKAGUZI WA MAGARI KWA KUTUMIA KAMPUNI BINAFSI ISIYO NA UWEZO WALA VIWANGO KULINGANISHA NA UK STANDARD OF ROAD WORTHINESS (MOT).

  • Viwango vya kukidhi uhalali wa gari kuwa barabarani nchini Uingereza ni vya hali ya juu na havikwepeki kisheria.
  • Ni jambo la kujifunza nyumbani na kuliwekea uratibu wa kisheria kwa kila baada ya muda fulani gari lazima liwe linafanyiwa Road Worthiness Test na siyo kuiwekea kampuni binafsi hapa UK kwenye utaratibu unaofanya kazi.

Kituo cha kuthibitisha gari lako linakidhi ubora na usalama wa hali juu kuruhusiwa kutumika nchini Uingereza. MOT TEST CENTRE.

Mwanzo wa yote nataraji kuwa wote mko salama na mnaendelea vyema na uchapaji kazi kama kawaida.

Rejea kichwa cha habari hapo juu,tunaomba mtu peperushie hii habari ili wahusika wajue kitu wanachokifanya sio sawa na wasijaribu kutuburuza bila kutumia busara na kufuata sheria.

Ukitazama kwenye kiambatanisho cha habari hii utaona tangazo la TBS ambalo wanatangaza kuanzia tarehe 16/03/2015, Kuna kampuni binafsi inayomilikiwa na watanzania hapa nchini Uingereza (UK), ambao wanasemekana wameshinda zabuni ya kukagua magari yote yanayotarajiwa kuja Tanzania kwa gharama ya $200 kwa kila gari, hii ni uonevu na unyanyasaji kwa Watanzania wenzao, kwa sheria za hapa Uingereza (UK) kila gari linahitaji kukaguliwa na kutambulika kama linakidhi ubora wa kuendelea kuwa barabarani yaani (MOT) ambayo kwa sasa iko digital, kupitia link za DVLA au VOSA gonga hapa (https://www.gov.uk/check-mot-status). Hii MOT inafanywa na wataalamu walio bobea, wenye sifa na vifaa maalum, kwa magari madogo vituo viko kila mji na kwa maroli na mabasi kuna vituo maalumu, kwa magari madogo gharama yake ni £50 tu.

Ukaguzi wa gari hufanyika kwa umakini na vifaa vya kisasa yaani “electronic diagnosis” kupima uchakavu kama kutu, emissions, na ubora wa kila kifaa muhimu katika gari.

Ukaguzi wa gari hufanyika kwa umakini na vifaa vya kisasa yaani “electronic diagnosis” kupima uchakavu kama kutu, emissions, na ubora wa kila kifaa muhimu katika gari.

Tunasikitishwa kwa kitendo cha TBS kutangaza mzabuni huyu bila kufuata ushauri wa Watanzania na wa kisheria ili zoezi zima liweze kukubalika na bila kuwaumiza watanzania. Iweje leo tulipie $200 kwa kampuni binafsi wakati kuna MOT yenye kiwango cha hali ya juu na kinachakubalika kwa standard za uhakika hapa Uingereza na kwingineko kuliko hii ya mtu binafsi isiyotambulika hapa Uingereza na kwa pesa kubwa zaidi?


Kwa kigezo kuwa kuna fake MOT hili ni jambo la kushangaza na la kupotosha sana kwani vituo hivi vinaendeshwa kielectroniki kwa log in appointement ya gari husika lanalohitaji kufanyiwa MOT na moja ya requirement ni kituo kuwa na CCTV ambayo ni connected on the system , hiyo link juu ni sehemu ambayo kila mtu anaweza tizama uhalali wa MOT kwa kila gari iliyotoka UK.

Kifungu kipi cha sheria kinatumika kuweka kiwango hiki?, kulikuwa na kesi imefikia wapi hadi leo watujulishe kuwa kuna mzabuni na gharama hizi kubwa. Hii ni aina ya uongozi usio jali maslahi ya watanzania na wasio weza wapunguzia mzigo wenzao kisa matakwa yao binafsi ya kujitajirisha tu. Mfano mzuri ni kuwa mtu yuko North katika miji kama Leeds au Sheffield, New castle, Manchester nk , ambako kuna vituo vya MOT lakini kwa utaratibu huu anapaswa kuleta gari yake London, Tulibury port kwenye ofisi hizi binafsi kisha atume gari yake.Wakati kuna vituo vya MOT kila mahali na kuna bandari North sio lazima kuleta gari London. Huu si uhungwana hata kidogo Zaidi ya kutizama maslahi binafsi.

Watanzania wote walioko UK wanapinga utaratibu huu mpya wa kuhujumu watanzania na kuomba serikali na shirika lake la viwango TBS kusitisha zoezi hili mara moja na kutizama utaratibu mzuri wa kutumia MOT yenye kiwango kinachokubalika na serikali ya hapa nchini Uingereza.

Uchunguzi wa gari ukiendelea ili kuthibitisha gari linakidhi viwango vya MOT hapa UK.

MOT ni ya kiwango cha juu sana na ndiyo maana uingereza hakuna ajali kama nyumbani ni jambo la kujifunza na siyo kuweka kampuni ya viwango hewa na kuongeza ajali nchini.

Kwa pamoja Watanzania wa UK wameanza kuweka sahihi ya kuomba kusitishwa utaratibu huu gonga hapa kwenda kwenye petition.

Tunaomba kuwajulisha wahusika hali hii haitaweza kukubalika kwa sasa wala baadae kwa kuwa huu ni mradi wa kunufahisisha watu wachache tu.Tunatanguliza shukrani kwa wana habari wote wenye kusambaza habari hii na kuomba wananchi wajiandikishe kupinga hali hii ya uonevu na unyanyasaji.


Electronic and computerized diagnosis ya kila eneo la gari hadi matairi yana viwango vya kutumika.

Ni sisi Wana-diaspora UKTZ.

NB: Link ya petition, ikiwa hapo juu haipatikani: http://www.change.org/p/tanzania-goverment-foregn-affiars-tanzania-bureau-of-standard-tbs-to-stop-to-use-serengeti-freight-in-uk-for-vehicle-inspection-before-shipping-to-tanzania
Taarifa ya Rais ya kuiagiza JKT ijenge nyumba za walioathiriwa na mvua KahamaTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwajengea nyumba 403 mpya waathirika ambao walibomolewa nyumba zao kutokana na mvua kubwa, yenye mawe na upepo mkali iliyonyesha usiku wa Machi 3, 2015, katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kuwatunza na kuwapatia huduma zote za msingi watu walioathiriwa na maafa ya mvua hiyo hadi watakapokuwa na uwezo wa kujitegemea wenyewe.

Rais Kikwete pia amesema kuwa maafa ya mvua hiyo yasitumike kama kisingizio cha watu kulipiza kisasi kwa madai kuwa mvua hiyo ilinyesha kutokana na msukumo wa kishirikina.
Rais Kikwete ameyasema hayo, leo, Machi 12, 2015,wakati alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi katika Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambako anafanya ziara maalum ya siku mbili kutoa pole kwa wananchi wa vijiji vitatu vya kata hiyo walioathirika na mvua iliyonyesha usiku wa Machi 3, 2015.

Rais Kikwete amewaambia wananchi hao: “Nimekuja kuwapeni pole kutokana na maafa ya mvua. Napenda kuwahakikishieni kuwa Serikali iko nanyi. Msiba wenu ni msiba wetu, huzuni yenu ni huzuni yetu na machungu yenu ni machungu yetu.”
Rais Kikwete amewaambia wananchi kuwa Serikali itaendelea kuzikarabati nyumba ambazo ziko katika hali ya kukarabatiwa. “Zile za ukarabati tutaendelea kuzikarabati na zile zilizoharibika kabisa tutazijenga. Naambiwa zinahitaji kiasi cha Sh. Bilioni mbili, tutazitafuta na tutajenga kwa vyovyote vile. Naambiwa kuwa ni nyumba 403 mpya. Hakuna atayepewa fedha taslim, na wala mtu asije kuomba fedha, ili ajenge mwenyewe. Na wala zamu hii hakuna tenda kwa sababu tutatumia Jeshi letu la kujenga taifa – tayari nimewaambia waifanye hii kazi. Hii ni dharura na chombo chetu cha dharura ni Jeshi letu.”

Rais Kikwete pia amewashukuru wote ambao wamekuwa wanatoa misaada ya kusaidia wahanga wa mvua hiyo, ikiwa ni pamoja na wale ambao wametoa makazi ya dharura kwa waathirika na misaada mingine.

Rais Kikwete pia amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa misaada ya dharura kwa waathirika hadi watakapokuwa na uwezo wa kujitegemea wenyewe: “Tayari Serikali imetoa tani 20 za chakula, tumetoa mafuta na sukari. Tutaendelea kuwaunga mkono mpaka mvuke. Aidha, hakuna yoyote ambaye atapoteza maisha kwa sababu ya ukosefu wa chakula. Tayari kuna chakula cha kutosha mwezi mmoja mpaka mwezi ujao na kikiisha tutaleta kingine.”

Rais Kikwete ameongeza: “Tutakabiliana pia na magonjwa ya mlipuko. Tayari tuna kituo cha dharura cha afya na kinatoa huduma mzuri.”

Rais Kikwete ameamuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kuhakikisha kuwa yananunuliwa magodoro ya haraka ili watoto waweze kulala vizuri na kuepukana na magonjwa ya vichomi.

“Magodoro yatapatikana kesho, yapo hapa Kahama na kama hakuna yafuatwe hata Shinyanga. Lakini lazima yapatikane kesho (Ijumaa, Machi 13, 2015). Naambiwa mahitaji ya magodoro ni 649, tayari 558 yamepatikana na bado yapo mahitaji ya magodoro 149 na haya tutaleta kesho,”amesema Rais Kikwete.

Kuhusu imani za ushirikina ambazo zinaanza kuandamana na tukio la mvua hiyo, Rais Kikwete amesema:“Msijiingize katika mambo ya ushirikina na ramli. Mvua za mawe ni za kawaida duniani hata kama hazijapata kunyesha hapa. Msitoke hapa kwenda kutafuta waganga kuhusiana na mvua hii ili mpate sababu ya kuua watu.”

Ameongeza: “Mvua za namna hii ni matukio ya kawaida na maisha ya kawaida katika maeneo mengine. Hakuna mchawi hapa, bali ni rehema za Mwenyezi Mungu. Nimesikia sikia mambo haya. Hayana kichwa wala miguu. Hili ni tukio la kawaida.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali yenu ipo. Acheni kuamanika, acheni kubabaika. Asiwababaishe mtu yoyote. Leo nimekuja mwenyewe mkubwa wa Serikali. Watakuja wengi kuwadanyanga, hawana Serikali. Wakija waambieni hivi – mwenye Serikali tuliyemchangua kaja, keshatuahidi, chakula tunakula, huduma za awali tumezipata na hizo nyingine amesema atatutimizia. Ili kuja kuwapeni pole mwambieni awapeni pole tu, asiwababaishe.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Machi, 2015

Dk Slaa na makada 3 wa CHADEMA kupelekwa kortini na Polisi kwa tuhuma za kumpiga Kagenzi

Na KAROLI VINSENT

JESHI la Polsi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lipo katika hatua ya mwisho katika kukamilisha ushahidi ili kumfikikisha mahakamani Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dokta Wilbrod Slaa pamoja na makada wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda maalum Dar es Salaam Suleiman Kova ametaja sababu ya kumfikisha mahakani katibu huyo wa CHADEMA na makada wake inatokana na vitendo vinavyodaiwa ni vya kinyama alivyofanyiwa mlinzi wake vya kumteka, kumpiga na kumlazimisha kutaja watu wanaomtuma kumuua Katibu Mkuu wa CHADEMA. 

Hivyo hivyo Jeshi hilo la Polisi limesema kwa sasa linawashikilia makada watatu wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini ambao ni Boniface Jacob (miaka 32) mkazi wa Ubungo Kisiwani ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ubungo kupitia chama hicho, sambamba na Hemed Ally Sabula (miaka 48) mkazi wa Tandale kwa Tumbo ambaye anadaiwa ni Afisa Usalama wa chama hicho Taifa.

Mbali na hao pia Kamishna Kova amemtaja kada mwingine anayeshikiliwa kuwa ni Benson Mramba (miaka 30), mkazi Tabata Kisukulu ambaye ni Afisa Utawala wa CHADEMA.

Kamishna kova amebainisha kuwa ishahidi wao utakapokamilika mafaili yao yatafikishwa kwa Wakili wa Serikali ili hatua zichukuliwe. 

Aidha, akizungumzia sakata la mlinzi Kagenzi amesema kwa sasa wanamalizia kazi ya kukusanya ushahidi kutoka CHADEMA ambao wanamtuhumu bwana Kagenzi ambaye anafanya ushirikiano na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula na Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni kwa kuaandaa mpango wa kutaka kumuwekea sumu Dokta Slaa.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilifika Polisi tarehe 8 mwezi huu majira ya saa 11 jioni katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kupitia kwa wakili wa CHADEMA anayetambulika kwa jina la john Mallya akiambatana na mtuhumiwa Khalid Kagenzi ambaye ni mkazi wa Tandale kwa Tumbo ambapo Wakili huyo aliiambia polisi kwamba alimleta mtuhumiwa baada ya kuagizwa na Dokta Slaa ili kutoa malalamiko kwa niaba yake.

Katika maelezo yake anadai Wakili huyo kuwa uongozi wa CHADEMA ulikuwa ulichukuwa hatua mbalimbali dhidi ya Kagenzi ikiwemo kumbana na kujiridhisha kuwa anahusika na mipango ya kimauaji.

Kwa mujibu wa Kamishna Kova, katika mahojiano walibaini kuna vitendo vya kinyama ambavyo mlinzi huyo wa Dokta Slaa amefanyiwa na makada wa CHADEMA baada ya Jeshi hilo kumkuta akiwa na majeraha mbalimbali katika mwili wake.

Ibada ya kumbukumbu DMV ya shukrani ya maisha ya marehemu Wilbard W. Kente

Familia ya Deo na Mamertha Mosha pamoja na Henry Kente wanawakaribisha kwenye Ibada ya kumbukumbu na shukrani ya maisha ya marehemu Baba yao mpendwa Mr. Wilbard W. Kente, aliyefariki na kuzikwa tarehe 2/4/2015 huko Dar-es-Salaam, Tanzania.

Ibada itafanyika hapa Washington, DC Jumamosi, tarehe 21 Machi, 2015 kuanzia saa tisa mchana (3 pm). Anuani ya kanisa ni

Universal Holiness Church
2426 Elvans Rd. SE,
Washington, DC 20020

Kwa habari zaidi, unaweza kuwasiliana na

Deo Mosha: 240 441 8433
Henry Kente: 240 938 2452
Vitalis Gunda: 240 383 6950
Mrs. Tumaini K. Katule 301 433 3411

Tafadhali zingatia muda. Karibuni wote.

Mambo yapamba moto Texas kwa ajili ya Pazi Reunion, MarekaniWatatu toka kushoto ni Richard Kasesela alipokua akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa George Bush Intercontinental uliopo Houston, Texas nchini Marekani kwa ajili ya Pazi Reunion itakayofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 katika uwanja wa mpira wa kikapu wa Pilgrim uliopo katika kanisa la Lutheran lililopo Houston. Wengine katika picha ni wenyeji wake waliompokea, kutoka kushoto ni Willy Crrusa, Aika na Flora Mochiwa maarufu kama Madikodiko. Mchezaji mwingine anayekuja kwenye maadhimisho hayo ya Pazi toka nje ya Marekani ni Atiki Matata anayekuja siku ya Ijumaa Machi 13, 2015 akitokea Uingereza.Richard Kasesela akitest uwanja wa mpira wa kikapu mara tu alipowasili uwanjani hapo mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege kushoto ni Davis mchezaji mwingine wa mchezo huo, Flora Mochiwa na Willy Crrusa wakiangalia kama bado wamo. Richard Kasesela richa ya kuwa mchezaji wa Pazi pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania.Wachezaji wa mpira wa kikapu wakipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.Mdau toka Columbus, Ohio akiwa tayari kushuhudia Pazi Reunion itayaofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 ndani ya jiji la H-Town.Willy Crrusa katika picha ya pamoja na Andrew wakati wakiwa ndani ya madikodiko.Wageni wakipata chakula huku maongezi yakiendelea.Andrew akipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.

Kutana na Riziki Msola na muziki wake wa Kihehe katika vionjo vya kisasaRiziki Msola ni mwanamuziki chipukizi mzaliwa wa Iringa. Kwa sasa ni mjasiriamali na mwanamuziki mahiri na makini anayechipukia katika tasnia ya muziki wa asili ya Mtanzania.

Anapatikana katika eneo la Sinza-Meeda Club Jijini Dar es Salaam. Ameibuka hewani na nyimbo kadhaa za Kihehe katika vionjo vya kisasa akiwa na malengo ya kukamilisha video yake ya kwanza.

Tafadhali sana wapenzi na wafadhili wa utamaduni wa mtanzania tujitokeze kwa michango yetu ya hali mali ili ubunifu wa Rikizi usipotee na uhifadhiwe kwa manufaa ya kizazi chetu na vizazi vitakavyokuja.

Kumbuka: "Jasiri haachi na asili na muacha asili ni hasidi na hana akili"

Wasiliana naye na umpatie madokezo mema kwa namba hii: +255 759 523785

Watanzania wa Texas kurekodi kipindi kuhusu mauaji ya albino

Wadau kutoka New York katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa.

Wadau wa North Carolina wakiwa kwenye kipindi kilichopata kurekodiwa.

Timu ya Vijimambo ikishiriana na Kwanza Production inapenda kwanza kutoa pongezi kwa Watanzania Houston kwa jitihada zao za kupambana na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi Pia inaandaa kipindi cha video kuongelea hili swala kwa mapana zaidi na kuangalia jinsi gani ya kukomesha mauaji haya ambayo yanaleta fedheha na aibu ikiwemo ukiukaji wa haki za binadamu.

Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumampili saa 8 mchana (2pm) mahali ni Extended Stay America chumba namba 224 anuani ni 2424 West Sam Houston Prkway, Houston, TX 77042.

Kwa maelezo zaidi wasiana na 301 335 6383 asante

Ujumbe kutoka kwa ndugu zetu hapo chini.

Mkutano maalum wa wadau wa filamu za maadili


WASANII, WATAYARISHAJI, WASAMBAZI,WATAMAZAJI NA WAANDISHI WOTE MNAKARIBISHWA

Asalaam Alaaikum Warhmatullah Wabarakatuhu


Tunapenda kuwajulisha wadau wa maadili movies nchini kutakuwa na mkutano wa mkubwa utakaofanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 2.00 asubuhi ukumbi wa Jaffar Complex uliopo Mnazi mmoja jijini Dar es salaam

AGENDA ZA MKUTANO

Kuandaa daftar la orodha ya wasanii na kuchagua rasmi aina ya mfumo wa filamu zetu na mengineyo

Kuchagua uongozi wa wa muda uliona mpangilio rasmi na kuupa majukumu likiwepo la 

  1. Kuanzisha mtandao wenye hamasa na mwelekeo kwa wassii wote wa maadili Africa mashariki na Africa kwau ujumla
  2. Kushirikiana na kujenga na kuunga mkono kuimarisha soko la filamu

Tunapenda kuaalika waandishi wa habari watunzi waongozaji wasambazaji na hata watazamaji wa filamu za maadili wasanii wote nchini tunawaalika ila stara ya mavazi kwa wanawake izingatie muhimu kwa wanawake

"Maadili Movies Lengo ni kusimamia ulinzi wa maadili mema kupitia filamu za Kitanzania, kuazisha, kuendeleza na kuhamsisha uwepo na ukuwaji wa filamu zenye heshima, zinazozingatia maneno, matendo na mavazi yenye maadili."

Tuwe pamoja wana

  • BURUNDI
  • RWANDA 
  • KENYA 
  • UGANDA
  • CONGO
  • TANZANIA na AFRIKA KWA UJUMLA 

Kwa mawasiliano ya simu kwa wale watakaoshiriki kutoka nchi tofauti tofauti pamoja na nchini. Tafadhali tuwasiliane kwa simu kwa namba zifutazo:

00255 773 950 250
00255 715 305 528