KNCV is looking for a CHALLENGE TB FINANCIAL OFFICER for Tanzania


 (FULL TIME)
Duty station: Dar es Salaam, Tanzania
KNCV Tuberculosis Foundation
KNCV Tuberculosis Foundation is an international non-profit organization dedicated to the fight against tuberculosis (TB), still the second most deadly infectious disease in the world.
KNCV is an international center of expertise for TB control that promotes effective, efficient, innovative and sustainable tuberculosis control strategies in a national and international context.  We are an organization of passionate TB professionals, including doctors, researchers, training experts, nurses and epidemiologists. We aim to stop the spread of the worldwide epidemic of TB and to prevent the further spread of drug-resistant TB.
Over the past century we have built up a wealth of knowledge and expertise, initially by successfully controlling TB in the Netherlands. Since the 1970s, we have also shared our knowledge and expertise with the rest of the world. We operate from a central office in The Hague in the Netherlands, a regional office in Central Asia and country offices worldwide. KNCV raises funds from private, institutional, corporate, and government donors.
Challenge TB
KNCV is the lead partner in Challenge TB (CTB), the new USAID-funded 5-year global program to decrease TB mortality and morbidity in high burdened countries. We lead an international consortium with eight partner organizations: American Thoracic Society (ATS), Family Health International (FHI 360), Interactive Research & Development (IRD), Japanese Anti Tuberculosis Foundation (JATA), Management Sciences for Health (MSH), Program for Appropriate Technology in Health (PATH), The International Union Against Tuberculosis and Lung Disease (The Union), and the World Health Organization.
The overarching strategic objectives of Challenge TB are to improve access to quality patient centered care for TB, TB/HIV, and MDR-TB services; to prevent transmission and disease progression; and to strengthen TB platforms.
Purpose of the position
The position of Financial Officer is aimed at keeping timely, complete and correct financial transactions and reporting to the internal and external stakeholders and to support the KNCV Tuberculosis Foundation Country Representative in the administration and efficient financial management of the project. The Financial Officer ensures the accounting transactions are in accordance with Generally Accepted Accounting Principles, KNCV Policy, and any cost principles imposed by KNCV or donor agency; and agrees with supporting documents. S/he ensures monthly financial reporting to KNCV in The Hague and to donors, monitors availability of funds and is contact person for audits by external auditor. S/he supports the Country Representative in development of project and office budgets.
Who are we looking for?
  • Masters’ degree in Accounting, Finance or Business, or related field.
  • Professional qualification such as CPA or equivalent is an important advantage.
  • At least 3 years’ experience in a similar position in a foreign business or NGO.
  • Being familiar with USAID financial and administrative policies, rules and regulations is an advantage.
  • Proficiency in relevant software (Word, Excel, accounting system) and knowledgeable of United Republic of Tanzania tax law.
Country: 
Tanzania
Duty station: 
Dar es Salaam, Tanzania
Organisation: 
KNCV Tuberculosis Foundation

Application and information
Your application (with curriculum vitae, motivation letter, 3 professional references) should be sent before 20 March 2015 to:
KNCV Tuberculosis Foundation, PO Box 146, 2501 CC The Hague, the Netherlands for the attention of: Ms. Larissa Lutmers. E-mail: [email protected] under subject ’Tanzania Challenge TB Financial Officer’.
For more information please contact us: phone (070) 416 72 22. For further information on KNCV Tuberculosis Foundation, please see www.kncvtbc.org.
 KNCV Tuberculosis Foundation is an equal opportunity employer offering employment without regard to race, color, religion, sex, sexual orientation, age, national origin, citizenship, physical or mental handicap, or status as a disabled.
Apply before: 
Friday, March 20, 2015
Contact person(s): 
HRM department
Telephone: 
+31 70 416 7222
Email address: 

Sindano za saa... Kaazi kwei kwei!


NSSF's Dege Eco Village - Redefining Dar es SalaamDW mjadala na Shaba, Mnasi, Mjengwa na Wanafunzi kuhusu lugha ya kufundishia na kujifunza mashuleni

Katika meza ya Duara ya idhaa ya Kiswahili ya redio DW, Jumamosi hii Mohamed Abdulrahman aliendesha majadiliano kuhusu, je, ni lugha gani itumike kufundishia na kujifunza elimu nchini Tanzania?

Pamoja naye katika mjadala huo ni ndugu Richard Shaba (Naibu Mkuu wa Shirika la Ujerumani, la Konrad-Adenauer, Tanzania jijini Dar es Salaam), Haji Mnasi (Afisa Elimu kwa Shule za Msingi) na Mwandishi, Maggid Mjengwa pamoja na maoni ya wanafunzi kuhusu suala hili la kutumia lugha ya Kiingereza ama Kiswahili.

Je, sera iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kuanzia elimu ya awali hadi ya Chuo Kikuu ni suala la kimapinduzi au litadumaza elimu?

Tumekwama baina ya tulikotoka na tulikokuwa tukienda - Jenerali Ulimwengu

NIMEILETA simulizi kuhusu Balozi Steffler makusudi kabisa ili kubainisha mambo kadhaa yanayotuhusu. Mosi, ni kuhusu uhusiano wetu na hao tunaowaita wafadhili au wahisani. Tumekuwa tukijidhalilisha mno kiasi kwamba wanatuona kama watu tusiokuwa na thamani mbele yao.

Hili linaeleweka. Hatuwaheshimu ombaomba. Hata wale waungwana ambao kwao ni kawaida kutoa sadaka kila mara, huwa hawawaheshimu ombaomba. Ombaomba hawaheshimiki kwa sababu moja tu, kwamba wanaishi kwa kutegemea fadhila za watu wengine.

Hali inakuwa mbaya zaidi inapokuwa ombaomba anaonekana ni mtu anayeweza kufanya kazi na kujipatia kipato, lakini hafanyi kazi kwa sababu anaona kazi ni ngumu zaidi kuliko kuzurura akikinga bakuli.

Wafadhili wanaotupa misaada wanatushangaa kama sisi wenyewe tunavyowashangaa ombaomba wanaoonekana kuwa na viungo na akili timamu. Rasilimali tulizojaliwa kuwa nazo zinatosha kabisa kutuwezesha kujitegemea iwapo tungezitumia vizuri.

Badala yake tunaona ni rahisi zaidi kuwaachia wageni wachukue rasilimali zetu waende kuzifanyia kazi za kuwanufaisha wao, halafu sisi tuletewe makombo kama misaada. Hapa kuna kitu kimetusibu katika uwezo wetu wa kufikiri, kama vile tumeingiliwa na ‘virus’ katika bongo zetu, na ndiyo maana tunafanya mambo ambayo hayaingii akilini.

Nimewahi kutoa mfano wa tumbili tunaowaona kandokando ya njia katika mbuga ya Mikumi. Wanatoka msituni ambako kuna matunda mengi na yenye ubora wa upya (kwa maana ya ‘fresh’) kuja kushinda barabarani wakisubiri watalii wawarushie maganda mabovu ya ndizi zilizonyauka.
Ndivyo tulivyo, na kwa mtu kama Balozi Steffler ndivyo tulivyo. Hatuheshimu kwa sababu hatuheshimiki. Kila kitu tunataka tufanyiwe na wengine, hata pale ambapo ni dhahiri kwamba tunaweza kujifanyia sisi wenyewe.

Tuambizane ukweli. Ni kwamba wanatuona sisi ni sawa kabisa na nyani. Dharau waliyonayo kwetu inazidi pale tunapopewa ‘misaada’ kwa masharti fulani, na hayo masharti tunayakubali haraka haraka, lakini tukiisha kukabidhiwa ‘misaada’ hiyo tunayasahau yale masharti na kufanya tunavyotaka. Ndiyo kesi ya magari tuliyokuwa tumepewa kwa sharti kwamba yatafanya kazi jijini Dar es Salaam tu na si kwingineko.

Suala la kuheshimu makubaliano tuliyoyatilia saini ni muhimu mno. Ndipo tunapata tofauti kati ya muungwana na mhuni. Mhuni atatia saini waraka wowote, (bila hata kuusoma) alimradi kuna kitu anakitaka sasa hivi, lakini katika dhamira yake hana nia ya kuheshimu chochote kilicho ndani ya waraka huo. Akiisha kupata anachohitaji, anaweza wala asiuangalie huo mkataba tena.

Muungwana huheshimu makubaliano aliyoingia na wenzake, na katika kila hatua za utekelezaji ataurejea mkataba huo mara kwa mara kuhakikisha haendi kinyume cha makubaliano. Huo ndio uungwana. Ukiisha kuvunja makubaliano yako na ‘mfadhili’ kwa kulipeleka gari la ‘msaada’ kule ulikokatazwa, unakuwa umejiweka mahali pa kukemewa na mama ambaye alikwisha kutuona kama watu wa hovyo.

Kutokana na hayo niliyoyasema hapo juu, ndipo tunaweza kuelewa jeuri ya Balozi Steffler alipoingilia majadiliano baina yangu na mkurugenzi wa serikali ya Ujerumani. Ujumbe kutoka Ujerumani ulikuja kutafuta kupewa hadhi walioamini inastahili Asasi ya Goethe jijini Dar es Salaam.
Kama nilivyoeleza hii ni asasi iliyopewa jina la Mjerumani anayeheshimiwa labda kuliko Mjerumani yeyote nchini mwake. Kwetu sisi najua hili ni jambo geni, lakini nchini Ujerumani ni vigumu kumpata mtu anayepewa heshima kama mwandishi na mshairi huyu, ambaye pia alikuwa mwanafalsafa na mwanadiplomasia, Johann Wolfgang von Goethe (1749-1832).

Katika jamii zinazoheshimu utamaduni na ‘ustaarabu’ mtu kama huyu anapewa nafasi ya kipekee kwa sababu ni kielelezo cha ‘roho’ ya taifa. Kwa njia moja kuu, ile ya lugha na matumizi ya maneno na misemo, mashairi, ngano, simulizi, methali na nyimbo, Goether ni mkubwa kuliko akina Otto von Bismarck, makamanda wa vita na wanasiasa, marais na makansela wote wa Ujerumani. Hii ni kwa sababu Ujerumani inathamini utaifa wake uliojengwa kwa jitihada kubwa, na Goethe amesimama katikati ya jitihada hizo. Sisi hatuko hivyo.

Sisi ni tofauti kwa sababu hapa tulipo tumekwama kati ya dunia mbili. Dunia ya kwanza ni kule tulikokuwa kabla ya Wazungu kutuvamia nasi tukawaruhusu watukalie. Ile ilikuwa ndiyo dunia yetu, mataifa yetu ya asili: Wasukuma, Wanyakyusa, Wagogo….. Baada ya kuunganishwa katika utumwa na kupewa uhuru bandia, tukaamua kujenga taifa moja kutokana na mipaka ya utumwa wetu, lakini tumefika katikati ya safari tumesahau tulikuwa tunakwenda wapi, na tunachofanya sasa ni kukimbia katika mduara tukifuata mikia yetu: Tulikotoka hatuko tena, na tulikokusudia kwenda hatukumbuki ni wapi. Sasa tunagawana mbao za mashua yetu.

Kwa mtu kama Steffler, sisi na wao hatuwezi kuwa sawa. Hatuwezi kuwa sawa kwa sababu wao wana utamaduni na sisi hatuna utamaduni. Wao walijenga taifa, sisi tulianza kujenga taifa, lakini tukasahau. Steffler hakuweza kuelewa kwamba na sisi tulikuwa na jeuri ya kujitambulisha kama taifa na kudai hadhi sawa kati ya Shaaban Robert na Goethe.

Nakumbuka vyema jinsi mwanamama huyo alivyonibeza na kuniona sina akili sawa sawa, nami naamini alifanya hivyo kwa misingi alikuwa hakuzoea kubishiwa na Watanzania, tena wengine wakubwa zaidi, tena sana, kuliko mimi serikalini. Kwa kumjibu, nilimpa taarifa kwamba mimi mwenyewe nilikuwa nimehudhuria mafunzo ya Kijerumani katika Goethe Institute; nikamshauri kwamba itakapofunguliwa Shaaban Robert Institute mjini Bonn naye ataweza kujifunza Kiswahili na apate kuonja utamu wa lugha yetu. Hili lilizidi kumtibua Steffler, nami sikuweza kujizuia kutabasamu moyoni.

Sikuwa na shaka hata kidogo, na wala sina shaka leo hii, kwamba kwangu mimi, ninapolitafakari taifa tulilokuwa tukilijenga wakati huo, sina shaka hata kidogo kwamba Shaaban Robert ndiye Goethe wetu, ndiye Lev Tostoy wetu, ndiye Shakespeare wetu, ndiye Mark Twain wetu; ndiye Moliere wetu, ndiye Lu Xun wetu. Inawezekana Shaaban Robert hajapata kutambulika kama miamba hao, lakini hilo pia ni tatizo letu, sisi wenyewe tunaoweza kumsahau Shaaban na kuwaenzi wanasiasa uchwara ambao wamekwisha kusahaulika kabla hawajakufa.

Dharau za aina ya Steffler tunafanyiwa kila siku, lakini tunazikubali kwa sababu tumetekwa kiakili, na watu waliotekwa kiakili hawawezi kufurukuta katika jambo lolote. Kama hatuna lugha tunayoweza kuiita na kuifanya kuwa lugha ya taifa, hatuwezi kujiita taifa. Kuiita lugha ya taifa ni jambo rahisi; tulikwisha kufanya hivyo, na tumefanya hivyo kwa muda wa miongo mitano.

Lakini si kweli kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Ni kama vile ambavyo tumekuwa tukisema kwa miongo minne kwamba Dodoma ndio mji mkuu wa Tanzania wakati tukijua kwamba hilo nalo si kweli. Kila mtu anajua kwamba akitaka makao makuu ya serikali yafanye jambo fulani inabidi aende Dar es Salaam, na kama wahusika wako Dodoma kwa sababu ya kikao cha Bunge, atawasubiri warudi.

Ugumu wa kukubali ukweli katika hili, na hususan kwa watu wanaoiona lugha ya kigeni kama yenye hadhi ya utukufu kuliko lugha yao wenyewe umekuwapo kila mahali duniani. Lakini vile vile, inapotokea kwamba jamii inayojitambua kama taifa, hata kama ni taifa dogo, ikajihisi kwamba lugha yao inahujumiwa, jamii hiyo itachukua hatua za kupambana dhidi ya hujuma hizo, wakati mwingine kwa kumwaga damu.

Ikifikia hatua hiyo, jamii hiyo inakuwa na haki ya kujitambulisha kama taifa, na wakati mwingine utaifa huo unaweza ukawa hauna nchi, hauna ardhi ulipojisimika, lakini utaifa unadumu ndani ya nyoyo za watu wake, kokote kule waliko, hata kama wamesambaa na kutapakaa duniani kote.
Sisi hatuko hivyo.
Makala ya Jenerali Ulimwengu via Raia Mwema

Mradi wa adhabu ya 'vikobo arobaini toa kimoja' kupambana na ulevi Arumeru

Niko Kijiji cha Akeri kilichoko juu kidogo ya eneo ya Patandi katika Wilaya ya Arumeru umbaliwa wa kama kilometa mbili kutoka barabara kuu inayotoka Moshi kwenda Arusha. Nimekaa kwenye kiti katikati ya waombelezaji wengi waliokuja kwenye msiba. Nimesafiri kutoka Dar es Salaam pamoja na wenzangu kuja kuhudhuria  mazishi ya  mama wa mfanyakazi mwenzangu na mkuu wangu Idara. Watu ni wengi sana na kama ilivyo tamaduni ya kabila la Wameru, baada ya mazishi waombolezaji tumekusanyika kwenye boma la familia kwa ajili ya kumalizia ibada ya mazishi na kupata chakula cha pamoja. Watu mbalimbali wanasimama kutoa salamu za rambirambi na mwishoni anapewa nafasi kiongozi Mkuu wa Kimila wa Kabibu la Waremu ajulikanaye kama Mshili (enzi hizo aliitwa Mangi). Mshili huyu ambaye anatoka katika ukoo maarufu wa Sumari, anaongea mambo kadhaa lakini mojawapo anawasifu vijana kwa kazi kubwa waliyofanya katika msiba huu. Anataja michango kadhaa ya vijana ikiwa ni pamoja na fedha walizochanga na kujitolea kwa kazi za mikono na kuhudumia wageni. Mshili anasema hii ni jambo jema sana na jipya kwani kwa muda mrefu vijana wa kijiji hiki na vingine vya karibu hawakua kwenye nafasi ya kutoa mchango wa msingi kwenye jamii.
Katika kusifu mchango wa vijana, Mshili anatumia nafasi hii kuwasihi mamia ya vijana waliokuwepo msibani, kuachana na tabia mbaya  ya ulevi uliyopindukia na wajisughulishe katika mambo ya msingi ya kuwalete maendeleo. Katika maelezo yake, Mshili anasisitiza kwamba, kwa wale vijana wasiotaka kubadilika wajiandae vema kwani Mradi wa Viboko Arubaini To Kimoja utaendelea kutekelezwa kwa kasi na bila hofu. Nikajiuliza mradi huu ni kitu gani?
Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha ni moja ya maeneo ya Tanzania yenye hali nzuri sana ya hewa. Arumeru iko chini ya mteremoko wa Mlima Meru. Arumeru imegawanywa katika majimbo mawili ya ujachuzi moja likiwa ni lile la Arumeru Mashariki linalongozwa na Mheshimiwa Joshua Nassari na la pili likiwa ni lile la Arumeru Magharibi linaloongozwa na Mheshimiwa Goodluck Ole-Medeye.

C:\Users\User\Downloads\Arumeru\MountMeru1B.jpg C:\Users\User\Downloads\Arumeru\47-eh-eh-migomba-mori-by-f-macha.jpg
Mazingira na Uoto wa Arumeru Mashariki

Kihistoria wilaya hii imekua eneo muhim sana la uzalishaji hasa kutokana na ardhi yenye rutuba ambayo ina misuti mikubwa ya asili na kupandwa; vyanzo vingi vya maji na mito ya msimu; kilimo cha kahawa aina ya arabika; ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na kilimo cha ndizi na mazao mengine ya biashara kama mahindi. Wilaya hii ni kati ya maeneo ya nchi yetu yenye uwezo wa kuzalishaa chakula kingi na cha kutosha kwa mwaka mzima. Hali kadhalika, Arumeru iko katika eneo zuri sana kiutalii kwani iko karibu na mbuga kadhaa za wanyama lakini pia kuna mbuga ya wanyama ya Arusha ambayo iko ndani ya wilaya hii. Kuna wageni wengi toka nchi nyingi duniani walioweka makazi yao Arumeru na wenye miradi mikubwa ya maendeleo. Kutokana na rasilimali zilizoko, zaidi ya wenyeji ambao ni kabila la Wameru, Arumeru imekusanya watu wa makabila mengi sana ya Tanzania waliokuja kujitafutia kipato na kuweka makazi yao ya kudumu.

Pamoja na utajiri huu wa asili katika wilaya ya Arumeru, kwa muda mrefu kumekua hakuna maendeleo makubwa ya kijamii yanayoendana na hali iliyoko. Kwa mfano, pamoja na kwamba barabara kuu ya Arusha kwenda Moshi imepita katika ya Arumeru na kua karibu na jiji la Arusha na mji wa Usa River, bado maeneo mengi ya karibu kabisa hayana umeme. Pamoja na wingi wa vyanzo vya maji, bado wakazi wa arumeru wanahangaika kupata maji na wakati mwingine wanategemea vyanzo duni sana vya maji vinavyopatikana umbali mrefu. Bado barabara nyingi za ndani ya Arumeru ni mbaya sana na wakati mwingine ni ngumu kupitika kutokana na upovu wake.
C:\Users\User\Downloads\Arumeru\10518694_10152809413152938_7329313516532427734_n.jpg C:\Users\User\Downloads\Arumeru\10646688_10152715229152938_3575017344129347165_n.jpg
Mbunge Nassari akishiri miradi ya maji na barabara pamoja na wananchi wake

Ukiachilia mbali tatizo la kiundombinu, Arumeru ni kati ya maeneo ya nchi yetu ambayo wananchi wake wanakabiliwa na tatizo kubwa sana la ulevi. Tatizo la ulevi ambalo liko kila kona limekuwepo kwa muda mrefu sana na limesababisha watu kutofanya kazi; kutoweka msisitizo kwenye elimu; kuharibu uimara wa familia na umasikini wa kujitakia; na kushindwa kumudi miradi ya maendeleo katika ujumla wake. Wilaya hii ni kati ya maeneo ambayo yamejaa vilabu vya pombe za kienyeji hadi ndani kabisa kwenye makazi ya wananchi. Kila kona utakutana na makundi ya watu wanakunywa pombe aina ya gongo na mbege kuanzia mapema asubuhi. Vilabu hivi na biashara zingine kama maduka vimejaa pombe za aina nyingi kama banana, viroba na zingine zinazopatikana kwa bei nafuu na hivyo kurahisha unywaji ovyo na usio na tija.

Kati ya watu walioathirika sana na unywaji mbovu wa pombe ni vijana wa makundi yote. Unywaji wa pombe uliopindukia umeharibu sana maisha ya vijana wengi na umeingia hata katika mashule na kuharibu maisha ya vijana walioko masomoni. Vijana wengi walio wadogo wamezeeshwa na unywaji wa pombe. Ni kawaida kabisa asubuhi na mapema kukutana na vijana wamelewa hawajielewi wanazurura ovyo mitaaani. Pesa kidogo wanazozipata kwa kazi wanazojishughulisha nazo zinaishia kwenye unywaji wa pombe na wengine hawafanyi kazi zaidi ya kuvizia watu wa kuwaomba pesa waweze kunywa pombe. Kwa sehemu kubwa tatizo hili halijawahi kupata kiongozi au mtu wa kulipa uzito wake na kuwa na mikakati endelevu ya kuliondoa. Mbaya zaidi, mara nyingi hata wanasiasa wametumia mwanya huu wa ulevi katika kujipatia watu wa kuwaunga mkono kwani unapowapa vijana hawa pombe unakua umekidhi mahitaji yao ya muhimu sana. Pamoja na kwamba sina data za kitafiti maana huenda haujawahi kufanyika, ulevi umechangia sana maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, mimba kwa watoto wa shule, pamoja na makundi ya vijana wanaofanya uhalifu wa wizi, ubakaji na uporaji.
Katika Kijiji cha Akeri nilipokuja kuhudhuria mazishi, kulingana na maelezo ya wenyeji wachache ambao nimepata nafasi ya kuongea nao na kauli ya Mshili, kiwango cha unywaji pombe aina ya gongo kimefikia kiwango cha kutisha. Ni kawaida kabisa kukutana na vijana asubuhi na mapema wakiwa wamelala njiani na kwenye migomba wakiwa wamelewa hawajitambui. Hali imekua mbaya kama vile kuna laana imemwagwa ya kuharibu kizazi cha vijana.
Kwa kuliona hili, wazee wa ukoo pamoja na vijana wenyewe wamekutana na kuweka mkakati wa kukabiliana na hali hii. Wamekubaliana kwamba, kijana yoyote atakayekutwa amelewa muda wowote ule na haswa muda wa kazi, anapewa adhabu kali. Adhabu yenyewe ni KUCHAPWA VIBOKO AROBAINI TOA KIMOJA yaani VIBOKO THELATHINI NA TISA (39). Wazee wa mila wamepanga kwambwa adhabu hii itolewe na vijana wao wenyewe. Hivyo kila kijana ni askari wa mwenzake. Pale atakapokutana na kijana kalewa, basi taarifa inawafikia wengine mara moja na wanakusanyika kwa ajili ya kutoa adhabu hii. Kijana mlevi anachapa viboko bila huruma katika hali ya ulevi wake na hadi kinapofika cha 39 ulevi unakua umekwisha.
C:\Users\User\Downloads\Arumeru\azimia2.jpg
Adhabu ya Kiboko....19, 20, 21, ...29...33, 34.. Uache Ulevi

Kulingana na shuhuda kadhaa ninazopewa hapa na kauli ya Mshili wa kabila la Meru, mradi huu umesaidia sana kijiji cha Akeri na kingine cha jirani kwani umepelekea vijana wengi kuachana na ulevi kabisa. Wanasema kwa sasa sio rahisi kukutana na kijana mlevi muda na siku yoyote ile kwani kila mmoja anajua atakachokutana nacho iwapo atalewa. Badala yake vijana hawa wamejitosa katika shughuli za uzalishaji mali wenye faida kwao na familia zao. Wamejia kutunza familia zao na afya zao zimeleta matumaini. Mradi huu umebadilisha sura ya kijiji na kufanya kuwa na vijana wawajibikaji na Mshili anaelezea kwamba wanakwenda kuupanua kwenda kwenda vijiji vingine ili kurudisha hadhi na heshima ya jamii ya watu wa Meru.

Ninatafakari mradi huu kina. Mshili anasema wao kama wazee wa ukoo wana mamlaka juu ya makuzi ya vijana wao na hivyo hawahitaji ruhusa ya chombo kingine chochote kile katika kurekebisha maadili ya vijana wao. Ninaelewa kwamba baadhi ya watetezi wa haki za binadamu na wasimamia sheria wanaweza kupingana na wazee hawa na kuona kwamba unakiuka haki ya msingi ya raia na kujichukulia sheria mkononi. Wanaweza kusema huenda hatua inayochukuliwa kutatua tatizo sio sahihi maana ni ya mateso. Ninajaribu kuwaza ni hatua gani tofauti ambayo inaweza kushughulika na tatizo hili. Nimezaliwa na kukua Meru na ninaelewa ni kwa jinsi gani tatizo hili limekua mwiba kwenye jamii hii na kuharibu familia nyingi sana. Mara kadhaa kumetokea majaribio kadhaa ya kulitatua lakini bila mkazo na mkakati endelevu kuleta matokea ya kuridhisha na huenda ndio maana wazee wa jadi wameamua kulisimamia wenyewe kama utaratibu wa kurudisha maadili ya kijamii maana wenye mamlaka ya kiuongozi na kisheria hawana majibu wakati uharibifu unaendelea.
C:\Users\User\Downloads\Arumeru\092513103526destination.jpg
Mbuga ya Wanyama ya Arusha

Ninajifunza kwamba wananchi wana uwezo wa kutatau matatizo yao yanayowakabili. Wanajua kwa undani nini uzito wa matatizo yao na ni kwa uzito kiasi gani yanahitaji majibu mazito na hata ikibidi ya kubeba dhamana  kubwa. Wanajua msingi undani wa jamii zao na ni mambo gani wanaweza kuyapa uzito wa pamoja kama jamii. Kama wakipata viongozi wa kuwasikiliza na kuwasaidia pale wanapokwama wanaweza kusaidia kuleta mabadiliko makubwa katika jamii yetu na kuboresha hali ya maisha tuliyonayo.
Baada ya chakula ninapata nafasi ya kuongoea na watu kadhaa. Kabla ya kuja hapa nyumbani kumalizia ibada ya mazishi, nilipata wasaa wa kuongea na Mshili (Mangi) kwa muda mrefu zaidi na kunipa msingi wa historia ya Wameru kutoka enzi za mkoloni hadi walipofikia leo. Nimemwahidi Mshili kwamba nikipata muda, nitaandika makala kuhusu mazungumzo yetu maana kuna mengi nimejifunza.
Wakazi wa Kijiji cha Akeri wanatumia MRADI wa adhabu ya VIBOKO AROBAINI TOA KIMOJA kumaliza tatizo la ulevi uliopindukia katika kijiji chaa na mradi huu umebadili na kuokoa maisha ya vijana wengi walio nguvukazi ya taifa na jamii wanayoishi.

Mwalimu MM

Niandikie ([email protected])

Uzinduzi wa Ishi Kistaaa wa Vodacom ulivyonoga @ Escape One Dar


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa akiteta jambo na msaani wa bogofleva Linah Sanga wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Ishi Kistaa inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Green Telecom yenye malengo ya kuendeleza vipaji vya vijana chipukizi wa muziki na muvi kurekodi muziki au muvi na kuwapa frusa ya kuishi maisha ya kistaa ambayo wamekuwa wakiona wasanii wakiishi ili kushiriki katika promosheni hii unatakiwa kutuma neno STAA au STAR kwenda namba 15760 na utachagua staa unayempenda na utatumiwa maswali kuhusu huyo Staa na unaweza kuibuka mshindi,Kila wiki kuna mshindi mmoja anapatikana.Katikati ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.


Meneja wa Nje wa Vodacom Tanzania,Abigail Ambweni (kushoto),Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo Glory Mtui wakiwa katika pozi la picha na msanii wa muziki wa kizazi kipya Linah Sanga wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Ishi Kistaa inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa ushirikiana na Green Telecom yenye malengo ya kuendeleza vipaji vya vijana chipukizi wa muziki na muvi kurekodi muziki au muvi na kuwapa frusa ya kuishi maisha ya kistaa ambayo wamekuwa wakiona wasanii wakiishi ili kushiriki katika promosheni hii unatakiwa kutuma neno STAA au STAR kwenda namba 15760 na utachagua staa unayempenda na utatumiwa maswali kuhusu huyo Staa na unaweza kuibuka mshindi,Kila wiki kuna mshindi mmoja anapatikana.


MC wa uzinduzi wa promosheni ya Ishi Kistaa VJ Penny akiteta jambo na Ofisa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Glory Mtui wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Ishi Kistaa inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Green Telecom yenye malengo ya kuendeleza vipaji vya vijana chipukizi wa muziki na muvi kurekodi muziki au muvi na kuwapa frusa ya kuishi maisha ya kistaa ambayo wamekuwa wakiona wasanii wakiishi ili kushiriki katika promosheni hii unatakiwa kutuma neno STAA au STAR kwenda namba 15760 na utachagua staa unayempenda na utatumiwa maswali kuhusu huyo Staa na unaweza kuibuka mshindi,Kila wiki kuna mshindi mmoja anapatikana.


Msanii mahiri wa bongp feva Barnabas akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Shamsa Hamud(kushoto)na Glory Mtui wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya Ishi Kistaa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na Green Telecom yenye malengo ya kuendeleza vipaji vya vijana chipukizi wa muziki na muvi kurekodi muziki au muvi na kuwapa frusa ya kuishi maisha ya kistaa ambayo wamekuwa wakiona wasanii wakiishi ili kushiriki katika promosheni hii unatakiwa kutuma neno STAA au STAR kwenda namba 15760 na utachagua staa unayempenda na utatumiwa maswali kuhusu huyo Staa na unaweza kuibuka mshindi,Kila wiki kuna mshindi mmoja anapatikana.Ofisa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Glory Mtui akicheza muziki na msanii wa bongo fleva Barnabas wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Ishi Kistaa inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa ushirikiano wa Green Telecom yenye malengo ya kuendeleza vipaji vya vijana chipukizi wa muziki na muvi kurekodi muziki au muvi na kuwapa frusa ya kuishi maisha ya kistaa ambayo wamekuwa wakiona wasanii wakiishi ili kushiriki katika promosheni hii unatakiwa kutuma neno STAA au STAR kwenda namba 15760 na utachagua staa unayempenda na utatumiwa maswali kuhusu huyo Staa na unaweza kuibuka mshindi,Kila wiki kuna mshindi mmoja anapatikana.


Mwanamuziki wa kizazi kipya Izzo Business akisalimiana na Ofisa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Glory Mtui wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Ishi Kistaa inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Green Telecom yenye malengo ya kuendeleza vipaji vya vijana chipukizi wa muziki na muvi kurekodi muziki au muvi na kuwapa frusa ya kuishi maisha ya kistaa ambayo wamekuwa wakiona wasanii wakiishi ili kushiriki katika promosheni hii unatakiwa kutuma neno STAA au STAR kwenda namba 15760 na utachagua staa unayempenda na utatumiwa maswali kuhusu huyo Staa na unaweza kuibuka mshindi,Kila wiki kuna mshindi mmoja anapatikana.

Maoni ya LGFumbuka kuhusu "Waraka wa Jukwaa la Wakristo"

Nina maswali matatu:. La kwanza, nimesoma Katiba yote, hakuna inapotaja Mahakama ya Kadhi; and yet "JUKWAA" linasema sababu mojawapo ni Mahakama ya Kadhi. Wananchi ni watu wazima na akili zao timamu: kwa nini watishiwe nyau? Si wasubiri Sheria ya MK ikitungwa si hapo ndiyo wakatae?

Wanasema serkali "iliwahonga" Waislamu wakubali Katiba kwa ahadi ya MK. Strong words for a Bishop? Without proof?

Kulikuwa na Maaskofu kwenye Bunge la Katiba, wao je, hawana upako? Askofu Pengo, je, yeye hana upako? Alinukuliwa na Rais akisema matatizo ya serkali mbili dawa yake si serkali tatu, ni ya kuyatatua. Amenukuliwa akisema kuwa "JUKWAA" halina madaraka ya kutoa "Msimamo"‎ wa Wakatoliki, only the Bishops in Congregation have such authority: huyu je, yeye hana upako?

La pili: nimesoma Katiba yote, hakuna sehemu inasema mazeruzeru wauliwe. And yet "JUKWAA" linataka Wakristu wasiipigie CCM kwa kufuata "mapokeo". Katika Makanisa yote yaliyotajwa, ni Wakatoliki peke yao ambao tunatawaliwa na MAPOKEO - Papa, Bikira Maria, Jumapili, Mapadri kutooa, nk. - Makanisa mengine hawana mapokeo, yaliasi mapokeo ndiyo wakaacha Ukatoliki.

Je, UKAWA wamewarubuni Katoliki bila wao kujua?

Hilo liache, lakini tangu lini Mkristo akatoa hukumu hapa duniani? Adhabu kuuubwa kuliko zote ambayo Kanisa Katoliki linaweza kutoa ni Barua ya Kichungaji, na la mwisho watasema ni kuwataka waumini wake WASALI. Nashangaa leo adhabu imetoka kuwa wasiipigie kura CCM. Padri Slaa hapo alipo atakuwa analia, unless...

BTW magazeti ya leo yamemnukuu Mhe Mbatiya akisema ajali ya Iringa (walikufa watu 50) si mkono wa Mungu, ni njama ya serkali ya CCM. Kuna shimo barabarani karibu na ajali, anatakwa serkali iwajibishe wahusika kwa mauaji hayo. Mazeruzeru je? Mvua ya mawe Kahama? Nazo ni CCM?

La tatu: wamesema Bunge la Katiba lilikuwa na hila na ubabe na maafikiano. Hii ni lugha ya UKAWA. It goes on to say "Watanzania hawajaridhishwa na mfumo wa serkali na haki za binadamu na madaraka ya Rais...". Hii ni lugha ya UKAWA (serkali tatu, ukomo wa bunge, tunu za Warioba alizozitoa Chadema): haya si si ndiyo ya wananchi waachwe wasome Katiba waamue?

La mwisho ninaloliona mimi ni kwamba ("JUKWAA") limeshaamua, Waingereza husema "nailing your name on the mast". Kama Katiba itapita, sijui watapata wapi pa kujificha? Wata‎pata wapi moral authority ya kutoa tamko jingine?

Kwa uafafanuzi, kwa wasio Wakatoliki, ni kwamba this is no more than a love letter. Wakatoliki huwa wana Waraka wa Kichungaji: huandikwa baada ya tafakuri na kusali na kufunga kabla haujatolewa. Ni waraka kama huo unampa Papa infallibility: akitoa waraka wa kichungaji ex-cathedral maana yake ni kwamba kafunga jambo duniani na mbinguni litafuka (Matayo 16:16). Kwa vile CCT na Pentekoste ni Protestants - maana yake ni Waasi - haiweEkani Askofu Katoliki akakaa nao kutoa Barua ya Kichungaji.

Ila point ni kwamba UKAWA wape 100% marks for trying, no question about that.

Whatever they had in mind, huu Waraka hauna uzito wa Barua ya Kichungaji na wala hauna hadhi ya kusomwa Makanisani Jumapili.

Majority ‎ya Wakristu watapiga kura kuikubali Katiba.

I know, I am one of them.

LGFumbuka,
Dar es Salaam.

---
via Wanazuoni Yahoo! Groups.

Job opportunity at Jhpiego (in Tanzania)


[video] 10 min documentary ya Sekondari ya Ilboru

BBC Tanzanian Event - World War One: Tanzania and Colonial War


TANZANIA AND COLONIAL WAR


Thursday 19 March 2015

18.00 – 21.00

British Council

Corner Samora Machel Avenue and Ohio Street

Dar es Salaam

It’s remembered as a European conflict, but one hundred years ago the British and German Empires also fought the First World War in East Africa. The struggle over present-day Tanzania left an untold legacy that this debate will uncover. The BBC’s Audrey Brown will be joined by some of the world’s greatest experts in World War One: The South African historian Bill Nasson and the India historian Santanu Das are coming to Tanzania and will be joined by Oswald Masebo from Dar es Salaam University. He will present an essay on the Tanzanian Memory of The Great War.

Make history with the British Council and the BBC: come and join the debate and take part in the BBC recording. The event will be in English.

You must register in order to attend this event. Attendance is free of charge.

Should you have any further queries or are having difficulties in registering, please contact us by email [email protected] or telephone +255 (0) 22 2165 300