Sababu 5 na Mbinu 4 za kuwezesha Wasomi kufikia uhuru wa kifedha


Ukiangalia katika jamii nyingi watu waliosoma sana wanaishia kuwa na maisha ya kawaida huku wakikosa na uhuru wa kifedha. Na katika jamii nyingi watu wengi ambao wana uhuru wa kifedha hawana elimu kubwa. Ni kitu ambacho kimekuwepo kwa muda mrefu na kinatokea dunia nzima. Je unajua nini kinasababisha hali hii? Leo tutajadili hapa ili uweze kuchukua hatua kama upo kwenye moja ya makundi haya mawili.

Kwanza kabisa tunaposema uhuru wa kifedha tunamaanisha hata mtu asipofanya kazi moja kwa moja bado ana kipato kinachomtosheleza kuendelea na maisha yake ya kila siku bila kuathiri kitu chochote.

Ukiangalia wasomi wengi wanaweza kuonekana wana fedha za kuwatosha, ila wanapoacha kazi au kustaafu ndio unaona wazi wazi kwamba hawakuwa na uhuru wa kifedha kwani maisha yanabadilika sana.

Sababu zinazowafanya wasomi kushindwa kufikia uhuru wa kifedha zipo wazi ila sio wengi ambao wanazijua na jinsi ya kuziepuka.

1. Wasomi wanatumia muda mwingi kwenye elimu.


Ukilinganisha wasomi na wale ambao sio wasomi sana, wasomi wanatumia muda mwingi sana kwenye elimu. Tuchukue mfano wa vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne mwaka mmoja, mmoja akaingia kwenye ulimwengu wa kazi au biashara na mwingine akaendelea na elimu. Aliyeendelea na elimu ana miaka 2 ya sekondari, miaka 3 ya shahada ya kwanza, miaka 2 ya shahada ya udhamili n.k. Kwa vyovyote vile huyu msomi atakua nyuma kiuzalishaji zaidi ya miaka 5 ukilinganisha na yule ambaye hakuendelea na shule.

2. Wasomi wanakosa elimu muhimu ya fedha.

Mfumo mzima wa elimu hakuna sehemu ambapo kunafundisha kitu chochote kinachohusiana na fedha binafsi. Kutokana na ukosefu wa alimu hii wasomi wanajikuta wana usimamizi mbovu wa fedha zao.

3. Wasomi wanatumia muda mwingi kwenye kazi zao.

Baadhi ya kazi za wasomi zinawahitaji kutumia muda mwingi sana na hivyo kukosa muda wa kufuatilia mambo yao ya fedha na hata uwekezaji. Kwa mfano daktari anajikuta ana kazi nyingi sana za kuokoa maisha ya watu na hivyo kusahau upande wake wa maisha ya kifedha. Injinia anaweza kuwa anasafiri sana kusimamia miradi mbalimbali na hivyo kushindwa kutuliza akili yake na kufanya uwekezaji mzuri.

4. Wasomi wana matumizi makubwa sana.

Pamoja na kwamba baadhi ya wasomi wanapata mishahara mikubwa na bado wana marupu rupu, matumizi yao ni makubwa sana. Hii inatokana na wao kutaka kuishi maisha ambayo jamii imeyajenga kwa wasomi. Kwa matumizi haya makubwa hata kama angekuwa na uwekezaji mdogo hauwezi kuhimili matumizi yake pale ambapo atakuwa hafanyi kazi.

5. Wasomi wanajiona wanajua kila kitu.

Wasomi wengi hata ambao ni maprofesa wana uelewa mdogo sana kuhusu mambo ya fedha na uwekezaji, lakini hutawaona wakijifunza kuhusu mambo hayo. Wakiona kuna semina zinaendesha kuhusiana na mambo hayo wanajisemea kwamba wanajua yote hayo, ukiwaambia wasome kitabu au kujifunza kwa njia nyingine watakuambia vitu hivyo wanavijua au hawana muda huo. Wanaweza kufikiria wanajua vitu hivyo ila ukwelini kwamba hawana uelewa mzuri kuhusu mambo ya fedha na uwekezaji.

Ufanye nini wewe msomi ili kuondoka kwenye mtego huo?

Kwanza kabisa kama utaendelea kukaa kwenye huo mtego, kazi ikiisha leo muda wa maisha yako unaweza ukahesabika. Kuna sababu kubwa sana kwa nini wastaafu wengi huwa wanakufa ndani miaka mitano baada ya kustaafu.

Ili kuepuka hali hiyo unaweza kuanzia hapa;

1. Amua kwamba unakwenda kufikia uhuru wa kifedha na weka malengo na mipango ya kufikia hatua hiyo.

2. Anza kubadili tabia ambazo zinakuzuia kufikia uhuru wa kifedha, anza na kupunguza matumizi yasiyo ya msingi.

3. Tenga saa moja kila siku kwa ajili ya kufuatilia maisha yako ya kifedha na uwekezaji pia. Hata kama upo bize kiasi gani usipuuze eneo hili la maisha yako. Unaweza kupata saa moja kwa kuamka mapema zaidi ya unavyoamka kila siku.

4. Kubali kwamba huna uelewa mkubwa kuhusu mambo ya fedha na uwekezaji na kubali kujifunza kupitia njia mbalimbali.

NMB yaunganisha Wafanyabiashara wakubwa mkoani Mbeya

Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB - Richard Makungwa (pili kulia) pamoja na Given Ngajilo wa kampuni ta Tunhimbaghe Traders Ltd (mteja).Wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB Executive Network jijini mbeya huku wakishuhudia ni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa NMB - Filbert Mponzi (kulia) na menejaa wa NMB Nyanda za juu - Lucrecia Mkarie

Katika mwendelezo wa kuwa karibu na wateja wake benki ya NMB imezindua mtandao utakaowaunganisha wateja wake wakubwa ‘Executive Network’ kwa jiji la mbeya ikiwa na lengo la kuwafanya kufurahia zaidi huduma za kibenki kutoka NMB.

Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya na kuwakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka vitongoji mbali mbali ikiwemo Kyela, Mbozi,Tunduma, Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe waliopata fursa ya kuwa kwenye mtandao wa wafanya bishara wa NMB.

Mtandao huu unaounganisha wateja wakubwa wa NMB vile vile umezinduliwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo; Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya ikiwa ya nne.

Maafisa wa NMB wakifurahi pamoja na mteja wao baada ya uzinduzi rasmi wa mtandao wa ‘NMB Executive Network’ 
Mmoja wa wateja wakubwa wa NMB akiomba ufafanuzi juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo wakati wa hafla iliyowakutanisha wateja wakubwa wa benki ya NMB

NesiWangu Show: Albinism


Karibu katika kipindi cha NesiWangu.

Katika kipindi hiki, Harriet Shangarai amezungumza na wanaharakati wa masuala ya albinism. Sehemu ya kwanza ni mazungumzo na Daisy Makwaia wa Albino Charity Organization na sehemu ya pili ni mazungumzo yao na mwanaharakati mwenye albinism, Babu Sikare wa Afrobino Ltd

Karibu

NACTE inakaribisha maombi ya kujiunga na Ualimu 2015/2016

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali kama zinavyopatikana kwenye tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbali mbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.Kulia ni Katibu msaidizi wa Baraza hilo Ramadhani Samainda.

ANWANI YA TOVUTI YA NACTE NI: www.nacte.go.tz

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali kama zinavyopatikana kwenye tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbali mbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.Kulia ni Katibu msaidizi wa Baraza hilo Ramadhani Samainda.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari pichani katika Makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali kama zinavyopatikana kwenye tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbalimbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari pichani katika Makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali kama zinavyopatikana kwenye tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbalimbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (hayupo pichani) alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika Makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam,Kuhusiana na kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne Oktoba 2014 na wengine wenye sifa mbalimbali kama zinavyopatikana kwenye tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji watakaoomba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga na mafunzo mnamo Aprili 15, 2015 kwenye vyuo mbalimbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.

Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) waliohudhuria katika mkutano wa waandishi wa habari na Katibu mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Primus Nkwela(hayupo pichani) alipokuwa akiongea na vyombo vya habari Makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam,Kuhusiana na kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali kama zinavyopatikana kwenye tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbalimbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.

Majina ya Wahamiaji haramu 63 na maiti mmoja waliokamatwa DodomaPOLISI mkoani hapa inashikilia raia 63 wa Ethiopia na maiti moja ambao walikuwa wakisafirishwa na dereva mtanzania kutoka Moshi kwenda Mbeya kwa kupitia njia za panya.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime amesema kwamba raia hao wa Ethioppia jumla yao ilikuwa ni 64 na kwamba mmoja alikuwa amekufa, wakati anawatia mbaroni kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kidoka.

Kwa mujibu wa Misime watu hao waliokamatwa katika tarafa ya Goma wilaya ya Chemba walikuwa wanasafirishwa na gari aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba ya usajili T 353 AYW lililokuwa likiendeshwa na Othman Mtekateka.

Aidha alisema aliyekutwa amekufa alitambuliwa kwa jina moja la Tajiru anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 – 30.

Imeelezwa kuwa juzi Jumamosi majira ya asubuhi katika kijiji cha Kidoka baada ya wananchi kuona watu wengi wasiofahamika wakiwa wamejificha katika vichaka na mashamba ya watu, huku wakionekana dhaifu, wengine wakila mahindi mabichi na na huku wakiomba kwa wanakijiji waliokuwa wakipita maeneo jirani msaada wa chakula na maji ya kunywa kwa ishara, wananchi waliamua kuitaarifu polisi.

Kamanda Misime alisema walipopewa taarifa walifika na kuanza msako wa kuwakamata na walipohojikwa walibainika kwamba ni raia wa Ethiopia na hawakuwa na vibali vya kuingia/kusafiria.

Aidha katika msako huo alikamatwa dereva wa gari hilo aitwaye Othman Mtekateka (45) mkazi wa Ilala Jangwani jijini Dar es Salaam ambaye alikiri kuwa yeye ndiye aliyekuwa anawasafirisha watu hao akiwa na wenzake wanne ambao walitoweka baada ya gari kuharibika.

Alidai kuwa aliwapakia watu hao Machi 12, mwaka huu huko Moshi – Kilimanjaro akitakiwa kuwapeleka Mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya.

Alisema baada ya gari kuharibika Jumamosi usiku katika kijiji cha Kidoka waliwashusha na kuwapeleka porini kuwaficha kisha kuendelea kutengeneza gari na iliposhindikana waliwatelekeza porini na gari kulitelekeza kijijini.

Orodha ya Wahamiaji haramu 63 waliokamatwa ni:-

1. FIWADO ERIBALO,

2. GANOLO ABABA, 15YRS

3. ABIRIHAM RILE 27YRS

4. DANIEL AVERA, 25YRS

5. ARABA LOBE, 18YRS

6. MEKSO GETACHA, 20YRS

7. MAMIRIS DANXE, 20YRS

8. GETACHAM HAFEBO, 25YRS

9. MIRATU ABINU, 21YRS

10. SABSIBE YOHANAS, 18YRS

11. ABIRIHAMU HADARO, 25YRS

12. ENDURE SASIE, 18YRS

13. KABABE WORIW, 22YRS

14. DANIEL S/O ABARE, 22YRS

15. ADISE TRAGO, 26YRS

16. GIRIMA S/O YOHANAS, 19YRS

17. XILAHUN S/O ABEBE, 18YRS

18. ESHETU S/O ABEBE, 18YRS

19. ABEYINE S/O ERTIRO, 26YRS

20. ENDIRAS S/O MAKANGO

21. ABABE S/O ACHISO, 30YRS

22. MISIGUNE S/O DALIKASO, 21YRS

23. AYANO S/O MALASE, 30YRS

24. DABADE MISHAMO 30YRS

25. ERIMIAS S/O ABEBO @ MASORE, 18YRS

26. ABIRIHAMU S/O ERISIMO, 20YRS

27. BIRANU S/O ABASE, 25YRS

28. EYASU S/O BEYENE, 26YRS

29. KAZALA S/O QADIVE, 2OYRS

30. ZAKADA S/O GIRIMA, 18YRS

31. TSAGAYE S/O DESTA, 25YRS

32. DAGINT S/O URIGO, 34YRS

33. DAGAZA S/O MOLA, 25YRS

34. MONAKU S/O ALUMU, 20YRS

35. ALAMAYU S/O KIZIE, 26YRS

36. BALAYME S/O WOLDE, 25YRS

37. ZALALAMU S/O ZAWIDE, 18YRS

38. FALAKA S/O ELKUCHE, 15YRS

39. ANA S/O ERSIDO, 27YRS

40. MALASA S/O TADASA, 22YRS

41. ASHANAZI S/O MULUNA, 20YRS

42. ASHANAZI S/O DESTA, 27YRS

43. SALAMU S/O AYALA, 25YRS

44. ARABA S/O LUBE, 28YRS

45. DANIEL S/O TADASA, 22YRS

46. MANI S/O SALAMU, 24YRS

47. FANTU S/O LAILA, 28YRS

48. MANAMU S/O NURYE, 23YRS

49. NASIRU S/O ANULO, 24YRS

50. DALALANG S/O ABRA, 20YRS

51. DELELAG S/O FEKADU, 23YRS

52. AHMAD S/O ELUSABO, 25YRS

53. FEKADU S/O ERBALO, 25YRS

54. GANURO S/O ABEBE, 25YRS

55. WORKAZAM S/O TIRZE, 28YRS

56. DANIEL S/O DETEBO, 22YRS

57. CHARNAT S/O ABEBA, 22YRS

58. TASHALA S/O BAYENE, 20YRS

59. ASAUZU S/O DAGAZA, 27YRS

60. SELAMU S/O WORKUNA, 2OYRS

61. MEGISO S/O GETACHAU, 2OYRS

62. TSAUGAYE S/O DETAMO, 15YRS

63. FANTU S/O TASO, 22YRS.


Rais Kikwete katika kikao cha Baraza la Mawaziri 15.03.2015

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri leo Jumapili Machi 15, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

Hotuba: Asanteni sana Kigoma Kaskazini - Zitto KabweHOTUBA YA MHE. ZITTO KABWE (MBUNGE KIGOMA KASKAZINI) ILIYOTOLEWA LEO TAREHE 15 MACHI 2015


Mwanamapinduzi na Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara alisema kuwa ili kuleta mabadiliko ya kimapinduzi ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu. Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na changamoto nyingi.

Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha ya wanakigoma, mwaka 2005 nilikuja kwenu kuwaomba ridhaa ya kuwatumikia kama mwakilishi wenu Dodoma. Nikiwa na umri wa miaka 29 tu. Labda ulikuwa ni msukumo wa matumaini yangu makubwa yanayoambatana na ujana yaliyowashawishi, kwani mliniamini na kunipa kazi hiyo ya heshima kubwa ya kuwawakilisha.

Mwaka 2010 mliniamini tena, naamini kutokana na utekelezaji wangu mzuri wa kazi na mafanikio tuliyoyaweza kuyapata katika jimbo letu. Hivyo kwa miaka kumi tumekuwa bega kwa bega katika safari hii ya pamoja ya kujenga na kuiendeleza jimbo letu, na leo nimekuja kuwashukuru kwa fursa mliyonipa kwani safari yetu inafikia mwisho. Fursa mliyonipa ni ya kipekee kwani ilikuwa fursa si tu ya kuwatumikia ninyi bali kulitumikia Taifa langu.

Katika miaka kumi hii kuna mambo makubwa tumeyafanya pamoja na kufanikiwa; na kuna mambo ambayo hatukuweza kuyafanya. Kwa yale ambayo hatukuweza kuyafanya naomba radhi. Kwa yale ambayo tumeweza kuyafanya naomba kuwapongeza sana kwa kufanikisha. Kwani kama Mwalimu Nyerere alivyotuambia kuhusu Uhuru na Maendeleo:

“Uongozi ni kuongea na kujadili na wananchi, kuwaelewesha na kuwashawishi. Uongozi ni kufanya kazi pamoja na wananchi na kuonyesha kwa vitendo mnachotaka kufikia. Uongozi ni kuwa mmoja wa wananchi na kutambua kuwa mko sawa…. Wananchi hawawezi kuendelezwa bali wanajiendeleza.” 

Na ndivyo tulivyofanya kwa miaka kumi, na kwa ushirikiano wenu tumeweza kufanikisha miradi mikubwa katika Jimbo letu.

Mwaka 2005 tulikuwa hatuna barabara ya lami hata moja. Leo hii, ninapoongea nanyi tuna barabara za lami zenye zaidi ya kilomita 100 kuunganisha Jimbo letu na majimbo mengine kwa pande zote za nchi kavu. Vilevile tuna mradi mkubwa wa kuunganisha vijiji vya ufukweni mwa Ziwa Tanganyika kwa barabara. Kiujumla kwa mkoa wa Kigoma tumefanikiwa kumaliza daraja la Malagarasi na hivyo kuunganisha mkoa wetu na mkoa wa Tabora kwa lami jambo ambalo lilikuwa kilio chetu cha muda mrefu sana tokea enzi na enzi. Muhimu zaidi ni kuwa barabara hizi zinatumika na wananchi, wafanyabiashara na wakulima ili kuwasiliana, kufanya biashara na kupanua masoko.

Tumefanikiwa kuongeza huduma ya Nishati ya Umeme kwa kuunganisha vijiji zaidi ya 16 hivi sasa. Changamoto kubwa iliyobakia mkoani kwetu ni uzalishaji mdogo wa umeme na wenye gharama kubwa sana. Suluhisho la kudumu ni kufanikisha mradi wa Malagarasi wenye uwezo wa kuzalisha 44MW ambao utakuwa nafuu na kuwezesha pia kusambaza umeme mikoa jirani ya Katavi na Tabora, na hata kuuza nchi jirani ya Burundi. Viongozi wa kisiasa wa mkoa wa Kigoma watakaoingia kwenye uongozi baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka 2015 hawana budi kuweka kipaumbele kikubwa kwa mradi huu. Bila ya umeme wa uhakika na nafuu hatuwezi kupiga hatua ya kuongeza thamani ya mazao yetu kwa kujenga viwanda vya usindikaji na kuongeza ajira ya vijana wetu.

Tumefanikiwa kuanza miradi ya Bandari na Soko kubwa kijiji cha Kagunga. Lengo likiwa ni kukuza biashara ya bidhaa kati yetu na nchi ya Burundi. Kigoma ni mji wa biashara kiasili na biashara ilichukua nafasi kubwa ya uchumi wa mkoa huu kwa miaka mingi sana. Kuimarishwa kwa miundombinu ya Biashara ni sehemu ya miradi ya kimkakati katika kuuweka mkoa kuchukua nafasi yake ya kiuchumi katika nchi yetu. Katika muktadha huo ndio maana tunaendelea na miradi ya Bandari Kibirizi na Bandari ya Nchi Kavu Katosho. Ndio maana tunaendelea na mradi wa Kituo cha Usafirishaji Mwandiga ( Mwandiga International Transportation Terminal ) na eneo maalumu la kiuchumi Ujiji. Haya yote tuliyaanzisha kwa pamoja nanyi ili kuhakikisha kuwa uchumi wetu unazalisha ajira kwa watu.

Tumefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa sekondari kwa kuwa na shule katika kata na baadhi ya kata tumejenga shule kila kijiji. Hata hivyo, tuna changamoto kubwa sana ya ubora wa elimu katika mkoa wetu. Katika jimbo la Kigoma Kaskazini zaidi ya 90% ya watahiniwa wa Kidato cha Nne wanapata madaraja ya mawili ya chini, wakati ule daraja la nne na daraja la sifuri. Tumeanzisha mradi wa majaribio ya kutoa motisha kwa Walimu ili kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha elimu inaboreshwa. Shirika la Twaweza linaendesha mradi mkubwa wa motisha kwa walimu na baada ya mwaka huu tutakuwa tumejifunza njia bora za kuongeza ubora wa elimu kwa watoto wetu. Bila Elimu bora miradi yote niliyoeleza hapo awali haina maana yeyote. Serikali imetoa Sera mpya ya Elimu, ni wajibu wetu kuona namna ya kuitekeleza katika ngazi yetu ili kupata mafanikio. Hata hivyo, uongozi wa kisiasa utakaoingia baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu hauna budi kujielekeza vya kutosha katika elimu ya ufundi ili kujenga stadi za kazi kwa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.

Tumefanikiwa kupanua huduma ya Afya kwa kuboresha Zahanati zetu chache zilizokuwepo na kujenga zahanati kadhaa mpya na miradi ya vituo vya afya vya Mahembe na Nyarubanda. Hata hivyo nasisitiza sana umuhimu wa kinga kuliko tiba kwani gharama za afya zimekuwa kubwa sana. Ndiyo maana tulipojadili hili suala, ilionekana kuwa suluhisho linatakiwa lipatikane kwa kufanya kile ambacho hatujawahi kufanya ili kuleta maendeleo ya kweli. Na mniruhusu hapa kunukuu wosia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alipotuasi kuwa “Maendeleo ni maendeleo ya watu. Barabara, Majengo, kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao na masuala mengi kama haya si maendeleo, bali ni vitendea kazi tu vya maendeleo” Ndiyo maana kulikuwa na umuhimu wa kutafuta njia mpya na mbadala kuboresha maisha ya mwananchi, hususan kwa upande wa afya. Uthibitisho wa ubunifu wetu ni kuwa katika kipindi hiki cha miaka 10 tumefanikiwa kuanzisha hifadhi ya jamii kwa wakulima.

Tulianza na Ushirika wa Wakulima wa Kahawa wa RUMAKU ambapo wananchi walijiunga na NSSF na hivyo kupata mikopo ya muda mfupi, huduma za afya bure na kujiwekea akiba kwa ajili ya mafao ya muda mrefu. Mafanikio makubwa yaliyopatikana yamewezesha wazo hili kusambaa nchi nzima na hivi sasa wakulima wa Korosho, Chai, Pamba, Tumbaku wanafuata nyayo za Wakulima wa Ushirika wa RUMAKU. Hapa Kigoma wazo hili sasa linatekelezwa kwa wavuvi wa mwambao mwa Ziwa Tanganyika. Ndoto yetu ni wananchi zaidi ya theluthi moja kwenye nguvu kazi wawe na Hifadhi ya Jamii. Natoa wito kwa wananchi wengine wenye uwezo wa kuchangia hifadhi ya jamii wajiunge na vikundi vya ushirika na kuchangia ili kufaidika na mafao ya muda mrefu kama pensheni lakini pia yale ya muda mfupi kama bima ya afya, mikopo kupitia SACCOS na mengine yatakayoanzishwa kama bima ya mazao.

Tumefanikiwa kujenga heshima ya watu wa Kigoma hapa nchini. Hivi sasa watu wa Kigoma tunatembea kifua mbele bila woga kuliko hapo awali. Kujiamini na kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano ni wajibu wetu kama raia. Changamoto za kujiona raia wa daraja la pili zimeondoka na zinaendelea kutokomezwa. Juhudi zetu ni silaha kubwa katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya Jamhuri yetu katika kila Nyanja za maisha yetu. Nafurahi kupata fursa ya kushiriki nanyi katika kujenga heshima hiyo ya Mkoa wetu. Nitaendelea kushiriki katika kudumisha heshima hiyo.

Nimejifunza mengi sana katika safari hii ya utumishi kwenu. Kama nilivyosema hapo awali, mliamua kufanya kile kisichozoeleka katika siasa ya nchi yetu kwa kunipa jukumu hili nikiwa kijana mdogo. Naamini kuwa ule ukichaa wangu mzuri wa kusimamia misingi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wangu na kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia nimezipigania. Na katika safari hii nimejenga marafiki wengi sana na pengine hata maadui ingawa hao ni wachache. Lakini haijalishi kwani mi binafsi sina uhasama na binadamu mwenzangu.

Katika utumishi wangu kwenu, bungeni nimejifunza namna nchi yetu inaendeshwa. Katika kujifunza huko kuna mambo kadhaa nimefanya ya kujivunia na mengine ni makosa. Mliniruhusu kufanya makosa na kuyarekebisha makosa hayo kwa hiyo kukomaa zaidi. Shukrani za dhati ziwaendee wazee wangu ambao mliniongoza mpaka hapa tulipofika na kunishauri hata kunionya pale palipohitajika. Kwa ujumla nimejifunza kuwa mzalendo zaidi kwa nchi yangu na kuwatumikia watu wa nchi hii. Ndio maana hamkunisikia tu kutetea watu wa Kigoma pekee, bali watu maeneo mengine ya nchi yetu na makundi mbalimbali ya kijamii kama Wakulima, Wafanyakazi, Wasanii, Wavuvi, Wana michezo na wana habari.

Katika safari hii ya miaka 10 kuna watu nimewafurahisha na kuna watu nimewaudhi. Kwa wale niliowaudhi ninaomba radhi. Kwa wale niliowafurahisha ninaomba wasiache kuniongoza na kunishauri kila wakati. Haikuwa safari rahisi na sikutegemea iwe rahisi. Kiuhalisia ilikuwa safari ngumu yenye mafunzo makubwa kwangu. Ilikuwa ni safari yangu kama kiongozi na pia safari yangu binafsi ya kupevuka kifikra na kupata mafunzo kuhusu maisha. Ukifika ulikokuwa unakwenda katika safari, unaweza kutathmini mengi kuhusu safari hiyo, lakini mwisho wa siku unatakiwa ujue kama safari hii ilikuwa njema ama la. Ninajivunia safari hii na ninasema kwa dhati kabisa ilikuwa ni safari njema.

Ni wakati sasa wa kutoa nafasi kwa nguvu mpya kuongoza Jimbo letu. Kushika kijiti pale ninapoishia. Kurekebisha pale nilipokosea. Kuimarisha pale nilipofikia.

Sitakuwa mbunge wenu baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini nitaendelea kutetea maslahi ya Mkoa wa Kigoma na Taifa letu kwa njia nyingine.

Sitaacha ule uendawazimu mzuri aliyoizungumzia Thomas Sankara unaoleta maendeleo ya kimapinduzi. Na misingi ni ileile na maadui ni walewale ambao mwasisi wetu Mwalimu Nyerere aliyokuwa anasema tupambane nao, yaani umaskini, ujinga, maradhi na sasa tumeongeza ufisadi. Kizazi chetu kina jukumu la kipekee kuendeleza mapambano haya na nitaendelea kuhakikisha tunafanya mapinduzi na kuwa na Taifa lenye misingi madhubuti ya uwajibikaji ili kuondoa kila aina ya ufisadi na kutumia rasilimali za nchi kuondoa umasikini, ujinga na maradhi.

Asanteni sana Kigoma Kaskazini!
#‎AsanteKigoma‬ kwa kunipa fursa ya kuhudumu kwa Taifa ‪#‎Humbled

Picha za harambee kuchangia ujenzi wa Chuo Kikuu Tumaini, Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani la Kanisa hilo, Askofu Alex Malasusa pamoja na wachungaji wengine wa KKKT wakati wa chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015. Katika uchangiaji huo, Rais Kikwete aliwezesha kupatikana kwa sh. bilioni 1.6 mbali na ahadi na fedha zitakazopatikana kutokana na bidhaa zilizouzwa kwa njia ya mnada.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine meza kuu wakati wa sala ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani la Kanisa hilo, Askofu Alex Malasusa pamoja na wachungaji wengine wa KKKT wakati wa chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015. Katika uchangiaji huo, Rais Kikwete aliwezesha kupatikana kwa sh. bilioni 1.6 mbali na ahadi na fedha zitakazopatikana kutokana na bidhaa zilizouzwa kwa njia ya mnada.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine meza kuu wakati wa  sala ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani la Kanisa hilo, Askofu Alex Malasusa pamoja na wachungaji wengine wa KKKT wakati wa chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015. Katika uchangiaji huo, Rais Kikwete aliwezesha kupatikana kwa sh. bilioni 1.6 mbali na ahadi na fedha zitakazopatikana kutokana na bidhaa zilizouzwa kwa njia ya mnada.

Picha kutoka Ikulu.

Wimbo murua wa Lokua Kanza na Fally Ipupa

IPTL na PAP zaichangia milioni 10/= kampeni ya Imetosha

Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. 

KAMPENI maalumu za kupinga mauaji ya watu wenye u-albino nchini inayojulikana kama 'Imetosha' iliyoanzishwa na balozi wa kujitolea, Henry Mdimu, chini ya Imetosha Foundation zimezidi kushika kasi baada ya makampuni ya IPTL na PAP kutoa shilingi milioni 10 kusaidia kampeni hizo.

Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege jana alimkabidhi balozi Mdimu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kama ishara ya kuunga mkono kampeni hizo za kutoa elimu kutokomeza imani potofu zilizojengeka kwa baadhi ya wanajamii juu ya watu wenye albino.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Makandege alisema matukio ya mauaji au kukatwa viungo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino yamefika hatua ya kutisha nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu kila mmoja bila ubaguzi kushiriki kusaidia mapambano hayo.

Alisema ulemavu wa ngozi waliyonao watu wenye albino ni mapungufu ya kibaiolojia ambayo ni mapenzi ya Mungu hivyo imani potofu zinazoendelea hazina budi kupigwa vita kwa nguvu zote.

"...Kuna minongono mitaaani kwamba watu wanatenda matukio hayo wana imani potofu kwamba ukitumia kiungo cha mtu mwenye albinism, ndipo utafanikiwa. Kama kweli viungo vyao vingekuwa vinaleta utajiri, basi watu wenye albinism wangekuwa matajiri namba moja duniani," alisema Makandege akizungumza.

"...Sisi IPTL na PAP tumeguswa sana na jambo hili. Kwa wote wanaofanya matendo haya, mnapaswa kuwa na hofu ya Mungu mkijua kuwa siku ya kihama, kila mtu atajibu na kuhukumiwa kwa matendo yake. Tunakubaliana kabisa na wenzetu IMETOSHA Foundation kwamba, imefika wakati kila Mtanzania, na hata wageni waishio Tanzania, kusema IMETOSHA na kusimama kidete kuwalinda hawa ndugu zetu," alisisitiza kiongozi huyo wa IPTL.

Aidha kampuni za IPTL na PAP zimeyataka makampuni mengine nchini na watu binafsi kuungana kwa kuchangia harakati hizi za imetosha ili kusaidia kampeni ya imetosha kupita mikoa ya kanda ya ziwa kupaza sauti na kuielimisha jamii juu ya uwepo wa imani potofu zinazoendeleza mauaji ya watu wenye u-albino.

Kwa upande wake Balozi wa Imetosha, Mdimu aliishukuru kampuni za IPTL na PAP kwa moyo wauliouonesha wa kusaidia harakati hizo na kumtaka kila Mtanzania kwa nafasi yake kusaidia kupaza sauti kwamba imetosha mauaji na unyanyasaji wanaoupata watu wenye ualbino. Alisema mauaji haya yanamgusa kila Mtanzania na kuendelea kuichafua nchi yetu hivyo kumtaka kila mmoja kupaza sauti yake kupinga vitendo hivyo.

Machi 28, 2015 Imetosha Foundation inatarajia kufanya matembezi ya hisani kuchangisha fedha zaidi ili kusaidia kampeni za kukomesha mauaji ya watu wenye u-albino kabla ya kuanza rasmi safari za kuzunguka katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na wasanii waliojitolea kueneza elimu hiyo kwa jamii moja kwa moja.

Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.

Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.
Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.

Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.

Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.
Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.


  • Tumeshirikishwa taarifa hii na TheHabari.com