Mapitio ya magazeti katika Tv mbalimbali, Machi 20, 2014Shukurani ya video @SimuTv 

Mashairi ya Amir Kulanteni, Mutabazi Mutabe na Albert Kissima kuhusu albinoKisa ni mbovu imani, Ndugu zetu mwawaua,
Mwamuabudu shetani, Mmezitupa sheria,
Twapita tu duniani, Kifo chaja kwenu pia,
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali?

Wenye dhima mwafanyani? Uhai kutulindia,
Wananchi mashakani, Nyie kiguu na njia,
Mara mpo marekani, Sisi huku tunalia,
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali?

Mwaiba mabilioni, Mwashindwa kututetea,
Ni kama watu usoni, Moyoni mwatumendea,
Ni kama tu hayawani, Imani zimepotea,
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali?

Vitendo vyangoja nini?, Matamko tu mwatoa,
Ndugu zetu kaburini, Hamuioni kadhia,
Matendo ya kishetani, Nyie mwayakaushia,
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali?

Twendeni makanisani, Tuombe huku twalia,
Twendeni misikitini, Tuzisome kali dua,
Mungu na awalaani, Motoni aje watia,
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali?

Amir Kulanteni
-------xxx-------
Amiri wa Kulanteni, Beti umezipatia, 
Ujumbe zimesheheni, Saluti nakupigia,
Ni qadar ya manani, Si hali walonunua,
Kilio cha Albino, Sioni kama twajali.

Tungeingia vitani, Madhubuti pigania,
Twaishia viririni, Badae twapuuzia,
Mungu tumjibu nini, Siku ikishawadia,
Kilio cha Albino, Sioni kama twajali.

Twakomaa vijiweni, Mpira kuongelea,
Twaingia huzunini, Mechi tukijikosea,
Albino mdomoni, Moyoni twajipetea,
Kilio cha Albino, Sioni kama twajali.

Siishie facebukuni, Makali kuoneshea,
Tuingie mitaani, Watu kuhamasishia,
Aridhia Rahmani, Haki tukipigania,
Kilio cha Albino, Sioni kama twajali. 

Mutabazi Muta Mutabe

-------xxx-------


Simanzi tele moyoni, Binadamu kuuana,
Tumekuwa hayawani, Rabuka tumemkana,
Utu u wapi jamani, Tunusuru maulana, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Ni ajabu duniani, Ugonjwa kuwa ni dili, 
Kisa hii melanini, Binadamu kawa mali, 
Potofu hii imani, Tupinge kwa kila hali, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Kwa panga wanawakata, Albino wakiwa hai, 
Mateso wanayopata, Nani ambaye halii?, 
Dhoruba itawakuta, Kamwe habaki adui, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Viungo vya binadamu, Kutolewa akiwa hai, 
Kwa mapanga sina hamu, Kuvumilia haifai,
Na kamwe hayatadumu, Wauaji mabedui, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Hali hii hadi lini, Tunaweza kukabili, 
Kwa pamoja tulaani, Sote na tuwe wakali,
Tuwaweke hadharani, Wauaji mafedhuli, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Baraka wa Cosimasi, Albino wa Sumbawanga, 
Mungu akupe wepesi, Na azidi kukuchunga, 
Upone kwa kasi, Akulinde na majanga, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Ulale pema Yohana, Alubino wa Geita, 
Hakupenda Maulana, Madhila yalokukuta, 
Tunamuomba rabana, Wengine kutowakuta, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? 

Dola chukua hatua, Madhila kuyamaliza, 
Raia tukiamua, Kukomesha tunaweza, 
Ndugu zetu wanalia, Ni sharti kuwatuliza, 
Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali?

Albert Kissima

Windows 10 is around the corner, you will get it for FREE, sign up!


Microsoft announced that Windows 10 is launching in 190 countries and 111 languages in a few months from now.

But here is a great news for those enthusiastic about it; Microsoft promised that they will offer a free upgrade to Windows 10 for qualified new or existing Windows 7, Windows 8.1 and Windows Phone 8.1 devices that upgrade in the first year! 

And even better: once a qualified Windows device is upgraded to Windows 10, they will continue to keep it up to date for the supported lifetime of the device, keeping it more secure, and introducing new features and functionality over time – for no additional charge.

 Microsoft Sign up for email on Windows 10 upgradeClick on the button to sign up for it.

Read more from their  blogs.windows.com

Mama Mitindo Asia Idarous kupamba Siku ya Mwanamke Duniani, ZanzibarBurudani kutolewa na Baby J, Coconut na Zanzibar One Modern taarab

Machi 22 mwaka huu Kisiwa cha Unguja, Zanzibar kinatarajiwa kuwa na tukio moja kubwa litakalowakutanisha Wanawake mbalimbali na kusheherekea siku ya Mwanamke Dunia, ndani ya ukumbi wa Bwawani Hoteli.

Katika tukio hilo, linatarajiwa kuwa pia na shamra shamra ikiwemo za mitindo ya mavazi kutoka kwa gwiji wa mitindo Nchini, Mama Asia Idarous Khamsin atakaye onesha mavazi mbalimbali siku hiyo akiwa sambamba na Mbunifu wa mavazi wa Zanzibar, Matilda Revelian wa Matty Designs.

Sherehe hizo zimeandaliwa na kikundi cha akina mama cha Zanzibalicious Women Group, chenye maendeleo makubwa kwa sasa hapa nchini.

Usiku huo utapambwa na burudani mbalimbali akiwemo mwanamuziki Baby J. Wengine ni bendi ya Coconut na Zanzibar One Modern taarab.

Aidha, Asia Idarous Khamisin amekisifia kikundi kilichoandaa halfa hiyo ya siku ya Mwanamke Duniani kwa Zanzibar, kwani ndio kwa mara ya kwanza Zanzibar wanawake na kusheherekea siku hiyo ya mwanamke duniani.

Usiku huo kiingilio kinatarajia kuwa sh. 35,000 kwa viti vya kawaida na sh 50,000 kwa upande wa V.I.P.

Aidha, kwa wadau wanaotaka tiketi wanaweza kutembelea katika maduka yaliyopo Mlandege Al Bashaer Tour, Magereza Ms Saloon, Michenzani Sas Saloon au kupitia mawasiliano ya simu ya namba: 0777418324, au 0777868766, 0715080399.

Taarifa ya Andrew Chale/MoDewji blog

Chereko chereko na mwenye mwana...! Ally Choki kutumbuiza Tokyo, Japan, Jumamosi


 WHITE PARTY 

KIONGOZI WA EXTRA BONGO BAND ALLY CHOKI KULITINGISHA JIJI LA TOKYO!

APEWA MAPOKEZI MAZURI NA KUPANDA JUKWAANI NA WAKONGWE
FRESH JUMBE NA ABBU OMARY

Ukumbi: Sonudai - Kanagawa Prefecture, Sagamihara City, Tokyo, Japan.

Mwanamuziki mahili wa muziki wa dansi Ally Choki ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya Extra Bongo aka "Wazee wa Kizigo" anatarajiwa kutingisha jukwaa siku ya Jumamosi 21 Machi 2015 ambapo wanamuziki wa Eagle's Vision watakuwepo kumsindikiza Ally Choki anayefuatana na Super Nyamwela.

Katika onesho hilo, wakongwe wawili wa muziki wa dansi watanzania wanaoishi Japan wanamuziki Fresh Jumbe Mkuu na Abou Omary watakuwepo jukwaani kuwapa baraka zote
wadogo zao Ally Choki na Super Nyamwela katika ukumbi wa sehemu inayoitwa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City pembeni kiduchu ya Jiji la Tokyo.

Madhumuni ya ziara ya Ally Choki na Super Nyamwela ni kuangalia ushirikiano na uwezekano wa soko la muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" ili muziki huo uweze kushika kasi kubwa na soko Japan na mashariki ya mbali kwa ujumla. Pia uwezekano wa bendi ya Extra Bongo kufanya ziara za kimataifa.

Wadau msikose kujitokeza kwa wingi katika onesho hili. Waswahili husema 'Chereko Chereko na mwenye mwana...!'

Madiwani Lindi wazuru Mapinga Satellite Project ya UTT-PID, Bagamoyo

Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo.

New Mapinga Satellite town located 30km from Mwenge along new Bagamoyo road with hundreds of serviced plots for residential, commercial and trade purpose ready for sale. The town is fully installed with electrical, water and roads facilities. For more info, visit: www.utt-pid.org

Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID) ilianza kazi zake Julai 1, 2013. Taasisi hii ilirithi kazi za miradi zilizokuwa zinafanywa na Taasisi mama yaani UTT.

Taarifa ya Andrew Chale wa Mo dewji blog aliyekuwa Bagamoyo

Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi Machi 17, wametembelea miradi mbali mbali ya UTT-PID iliyopo Dar es Salaam ikiwemo ule wa Bagamoyo wa New Mapinga Satellite.

Madiwani hao waliweza kujifunza mambo mbalimbali dhidi ya mradi huo ulivyoandaliwa na kufanya kazi na namna ulivyopangiliwa kwa ustadi mkubwa.

Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali alipongea juhudi za UTT-PID kwa kufanikisha ziara hiyo kwani wamejifunza mengi na pindi watakaporejea Lindi, watakuwa mfano wa kuigwa.

“Kule kwetu Lindi pia tuna mradi uliopo katika hatua mbaali mbali na UTT-PID tayari wamesha pima baadhi ya viwanja katika mfumo kama huu wa kisasa tunaojifunza hapa hivyo itatusaidia sana kwa sasa” alisema Meya Magali.

Kwa upande wake, Diwani wa Nachingwea, Omari Chitanda alieleza kuwa, wamepata kuielewa vyema UTT-PID na naamna ya ufanyaji wake wa kazi.

“tunaipongeza UTT-PID kwani imetufungulia mwangaza wa kimaendeleo. Tutakapo rejea Lindi tutaenda kufanya mambo ya kimaendeleo katika kuubadilisha mji wetu” alisema Diwani Chitanda.

Aidha kwa upande wake msimamizi wa mradi huo wa Mapinga kutoka UTT-PID, Godfrey Charles alisema kuwa hdi sasa mradi huo umefanikiwa kwa kiwango ambapo tayari vimebaki viwanja vichache kati ya zaidi ya 500 vilivyochukuliwa.

Pia madiwani hao, walipata elimu pamoja na ufanyaji wa kazi wa UTT-PID na wadau wanaoshirikiana nao huku hadi sasa ikiwa inasimamia miradi mbalimbali ikiwemo mikoa ya Pwani, Morogoro, Kagera, Dar es Salaam, Lindi na mikoa mingine hapa Nchini.

Aidha, kwa upande wa Madiwani hao walipongeza UTT-PID kwa hatua hiyo ya kuwapa elimu sambamba na kutembelea baadhi ya miradi inayoendeeshwa na taaisis hiyo.Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani).Madiwani na maofisa kutoka UTT-PID wakifuatilia kwa makini maelezo ya msimamizi wa mradi huo wa Mapinga uliochini ya UTT-PID (Hayupo pichani).

Madiwani wa Lindi wakijadili jambo.

Tanzania still ranks high in sickle cell births


  • Virtual clinic to help monitor medicine intake

Dar es Salaam, March 19, 2015: One hundred and fifty sickle cell patients are set to receive mobile handsets that will simplify monitoring of their health condition by sending videos of themselves taking their medication to the clinic from the comfort of their homes.

Sickle cell disease rate in Tanzania continues to rise as sickle cell births reach 11,000 a year. The Sickle Cell Foundation, a non-profit organization, is committed to contributing towards prevention, care and effective management of disease in Tanzania.

The Foundation is working with Muhimbili University on a project known as MDOTS that involves the use of mobile phone technology to improve adherence to medication. The mobile phones were donated by Vodacom Foundation today to the Sickle Cell Foundation of Tanzania.

As a pilot for the project 150 patients who receive long-term medication will be given mobile phones. These patients will not physically attend clinic but will monitor their health daily; record themselves ingesting the medication and send the video to the clinic through their phones.

Speaking during the handover ceremony today, MDOTS Program Coordinator, Dr. Robert Mongi said, “We prescribe medication for different strains of sickle cell. Patients with severe sickle cell disease are prescribed medication that must be taken daily however, not all patients observe these instructions. This project will help us determine whether monitoring intake of medication is effective in ensuring adherence to medication on a daily basis.”

Sickle Cell patients who are on long term medication tend to skip taking their medication based on lack of symptoms. This interferes with the medication’s work on the body and can result in their condition worsening.

“We understand the need to improve care and increase awareness of the sickle cell disease in Tanzania and that is why we have donated these 150 mobile handsets to enable this project. The handsets can be connected through any mobile network that patients choose,” said Head of the Vodacom Foundation, Reenu Verma.

“It is important for the private sector to join hands with the Government in efforts to build a healthier nation. We look to further support the Sickle Cell Foundation in future programs as we continue to align with Millenium Development Goal No. 6 which aims to both prevent and combat various diseases,” added Ms. Verma.

Sickle Cell disease is an inherited blood disorder. Tanzania ranks 4th in the world with the highest number of sickle cell disease births a year (up to 11,000) after Nigeria, India and DRC. Sickle cell disease is manageable through comprehensive care offered by the Sickle Cell Foundation through Muhimbili National Hospital here in Tanzania.

Raia wa Nigeria akamatwa JNIA na kete 100 za cocaine

RAIA wa Nigeria, Anthony Ifeanyichukwa Okafor (52), amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akidaiwa kumeza kete 100 za dawa za kulevya aina ya cocaine ambazo thamani yake bado haijafahamika.

Tukio hilo limetokea takribani siku 22 baada ya raia mwingine wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) kuvunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika uwanja huo.

Cole alikamatwa Jumatatu ya Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo. 
 
Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa amefika nchini kumfuata rafiki yake wa kike aliyekutana naye Hong Kong, China na baadaye Douala, Cameroon.

Nzowa alisema mtuhumiwa huyo alisema rafiki yake huyo wa Tanzania ni mpenzi wake na wako pamoja katika kazi hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema wauzaji wa dawa hizo siku hizi wamegundua mtindo mpya wa kuwatumia watu wazima ili wasigundulike kutokana na mwonekano wao.

  • Taarifa kwa mujibu wa blogu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanzania.

Baregu ambana Msuya aeleze ya nini alitamka, “kila mtu atabeba msalaba wake”; Mkapa alizindua Kavazi la Nyerere kimya

WAZIRI Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya amejikuta katika wakati mgumu wakati akitetea kauli yake ya “kila mtu atabeba msalaba wake.”

Msuya alijikuta akibanwa kuhusu kauli hiyo aliyoitoa miaka mingi iliyopita wakati akiwa Waziri wa Fedha katika mjadala wa maendeleo uliofanyika Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali.

Akitetea kauli yake, Msuya alisema alifanya hivyo kutokana na hali ngumu ya kiuchumi ambayo ilikuwa ikikabili taifa. Kauli hiyo ambayo iliudhi wananchi wengi aliitoa wakati akiwasilisha bajeti ambayo ilionekana haimjali mwananchi.

Baada ya malalamiko kuzidi Msuya alijibu kwa kusema kila mtu atabeba msalaba wake kauli iliyozua mjadala mkubwa kila kona ya nchi na kubaki kwenye vichwa vya Watanzania wengi hadi sasa.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, Msuya alisema alilazimika kusema hivyo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wabunge.

“Wakati ule nikiwa Waziri wa Fedha nilipeleka bajeti bungeni. Tukataka tutoze kodi kwenye kanga na vitenge sasa kukawa na debate (majadala) mkubwa pale bungeni, mbunge anasimama na kusema yeye ana wake wawili wengine watatu itakuwaje kuwe na hiyo kodi.

“Baada ya kuona mjadala hauishi na kila mtu anasema lake ndipo nikasema kila mtu atabeba msalaba wake kwani Mungu amesema tutaoa mke mmoja na si wengi… sasa kama kuna mtu anaoa wake wengi shauri yake, kwa maana kila mtu atabeba msalaba wake. Binadamu ni watu wa ajabu sana kila mtu anabehave kivyake. Waliopewa majukumu ya kuongoza na wananchi kwa ujumla wasiweke insensitive (hisia). Sasa kama ukioa wake wengi hiyo ni shauri yako,” alisisitiza Msuya.

Msuya alisema hayo baada ya kubanwa na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Prof. Mwesiga Baregu akimtaka aeleze ni kwa nini aliwahi kutoa kauli iliyokuwa imelenga kuwakomoa wananchi.

“Nashukuru hapa tunaye Waziri Mkuu mstaafu Msuya ambaye huko nyuma akiwa Waziri wa Fedha aliwahi kutoa kauli kwamba kila mtu atabeba msalaba wake jambo lililozua mjadala mkubwa, sasa atueleze ni kwa nini yeye kama kiongozi alitoa kauli ya namna hiyo.”

Prof. Baregu alisema viongozi wengi wamekuwa wakisababisha ubinafsi jambo linalosababisha vijana wengi kulalamika.

Kauli tata kama za Msuya zimeendelea kutolewa na viongozi, ambapo kauli “kutumia sh.10 milioni kununulia mboga” na ile maarufu ya “vijisenti” zimeelezewa kutikisa nchi katika siku za karibuni na kuibua hisia tofauti kutoka kwa wananchi.

Kauli ya Prof. Anna Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ndiyo iliyokuwa gumzo katika siku za karibuni baada ya mbunge huyo wa Muleba Kusini kusema alitumia sh. milioni 10 kununulia mboga wakati alipokuwa akihojiwa na Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhusu sh. bilioni 1.6 alizopewa na ambazo zinahusishwa na kashfa ya uchotwaji wa sh. bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Akilieleza baraza hilo namna alivyotumia baadhi ya fedha zilizoingizwa kwenye akaunti yake, Tibaijuka alisema: “Hivyo nilipolipwa (shilingi) milioni 117, nilitoa milioni mbili nikachangia Kanisa la Makongo na nikatoa 400,000 nikapeleka kanisani na milioni 10 niliitoa kwa ajili ya matumizi yangu ya kununulia mboga.”

Mkapa
Wakati huo huo, Rais wa mstafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alizindua Kavazi la Mwalimu Julius Nyerere kimya kimya bila kuzungumza neno lolote.

Uzinduzi huo ulifanyika ukiwa na lengo kukusanya na kuhifadhi nyaraka na taarifa mbalimbali za Mwalimu Nyerere.

Akizungumzia lengo la uzinduzi wa kavazi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda alisema ni kujadili na kuchambua fikra za Nyerere na kuzitazama kwenye mtazamo wa sasa na kufanyia tafiti.

Dk. Mshinda alisema uwepo wa kavazi hilo utainua hamasa ya kuinua vipaji, ubunifu na sekta ya sanaa kutokana na kuwa na nafasi kubwa katika jamii.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kwa hadhi ya maisha yaliyopo hayajengi ujamaa kwa tafsiri ya Mwalimu Nyerere.

Alisema Mwalimu Nyerere alikuwa akizungumza na kuhimiza usawa wa haki za binadamu, kisiasa na kiuchumi ambayo yalikuja kuonekana katika ujenzi wa taifa.

Aliongeza kuwa licha ya mambo aliyokuwa akihimiza, lakini viongozi wa sasa wanachakachua kwa manufaa ya kisiasa huku vitendo vyao vikiwa tofauti na Mwalimu Nyerere.

“Kwa sasa hatujengi Ujamaa kwa tafsiri ya Mwalimu Nyerere, hivyo ni vema tumuenzi kwa vitendo likiwemo suala la uadilifu kwani alikuwa akitilia mkazo,” alisema Prof. Lipumba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kavazi la Mwalimu, Profesa Issa Shivji alisema jina la Kavazi limetolewa kwa namna ya kipekee kwani makavazi yanayotunza nyaraka za mwalimu yana umuhimu na hadhi maalumu.

Alisema katika utafiti walikusanya taarifa za mwalimu kwa viongozi wa ndani na nje ya nchi ili kuzijadili na kuzichambua kwa ajili ya maendeleo.[audio] Kauli ya Maaskofu wa Kanda ya Ziwa kuhusu Katiba Inayopendekezwa


Pleya iliyopachikwa hapo juu ni ya audio ya Katibu wa Kamati ya Mabalozi wa Amani wa Kikristo Kanda ya Ziwa ambaye pia ni askofu wa kanisa Tanzania Field Evangelism (TFE) la mjini Shinyanga Edson Mwombeki akizungumza wakati wa kutoa Tamko la Kamati hiyo kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

Pleya iliyopachikwa hapo chini ina sauti ya Askofu Benjamin Madayi akisoma tamko la Kamati ya Mabalozi hao.Audio zimewekwa mtandaoni na Kadama Malunde (shukurani)

Mashehe wazungumzia kauli ya Maaskofu kuhusu Katiba Inayopendekezwa

TAASISI ya wa Mashekhe na Wanazuoni Kiislamu nchini, wameiomba Serikali kupuuza tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) badala yake iendelee na mchakato wa Mahakama ya Kadhi na Maaskofu wawe wavumilivu kwani Serikali ni ya Watanzania wote.

Aidha, imewasisitiza Watanzania kwa ujumla wao kupata elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kuisoma kwa makini na kuielewa vilivyo ili wawe na uwezo na uhuru wa kuchagua kile wanachokiona kina manufaa kwao bila kuwepo shinikizo la kiimani.

Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Shekhe Khamis Mataka aliyasema hayo leo jijii Dar es Salaam wakati akitoa tamko la taasisi hiyo kufuatia tamko la TCF kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Mahakama ya Kadhi na Hali ya Usalama na Amani ya Nchi.

“Taasisi imezipitia kwa kina nukta zote nne za Tamko hilo pamoja na hitimisho lake na kubaini kwamba maaskofu wamejisahau kwamba wao ni viongozi wa kiimani na kiroho ambao wanatakiwa wawe tayari kumpokea yeyote na kumpa neno la hekima lililojazwa faraja, bila hata ya kujali itikadi au chama chake cha siasa. Badala yake wameamua kutoa faraja kwa waumini wao kwa kuzingatia utashi wa kisiasa,” 
alisema.

Alisema Maaskofu wameamua kutumia msukumo wa kiimani pamoja na kuzitumia nyumba zao za ibada ili kuwazuilia Waislamu wasipate haki yao ya kuwa na Mahakama ya Kadhi na kutoa madai ya ‘Waislamu kupewa rushwa’ ili kufanikisha mchakato wa Katiba inayopendekezwa.

“Maaskofu wameamua kuanzisha utamaduni mpya wa kuyaendea mambo ya kisiasa kwa misingi ya kiimani na hivyo kutoa tishio la kuwagawa watanzania kwa misingi hiyo. Hivyo baada ya Taasisi yetu kujiridhisha na yaliyomo katika Tamko hilo la Maaskofu chini ya mwavuli wa TCF tunashauri hatua za kuchukua” Kwa kuwa serikali ina vyombo makini vyenye wataalamu wenye uwezo wa kufahamu na kuelewa uvunjifu wa katiba na Umoja wa Kitaifa, tunaomba ipuuze tamko hilo ambalo limeisikitisha taasisi yetu na kuwadhalilisha waislamu kwa kudai wamepewa Rushwa ya Mahakama ya Kadhi.”

Alisema madai hayo yanaonesha dharau, kiburi na kutowaheshimu waislamu jambo ambalo lina athari mbaya kwa mahusiano baina ya Waislamu na Wakristo nchini.

“Suala la Mahakama ya Kadhi ni haki ya Waislamu na haliwahusu wala halihitaji ridhaa ya wasiokuwa Waislamu kama ambavyo waislamu hawajapata kuombwa ridhaa yao katika yale ambayo Serikali imekuwa ikiwafanyia wakristo na makanisa yao” 

Shekhe Mataka alisema 
“Taasisi hii inapinga kwa nguvu zote madai ya Maaskofu kuwa Waislamu kuwa na mahakama ya Kadhi ni uvunjifu wa Katiba, kwani sheria za Kiislamu ni moja ya vyanzo vya sheria ya Tanzania… Mahakama za Tanzania zimekuwa zikitumia sheria hizo kuhukumu kesi za waislamu kuhusu ndoa, Talaka, Mirathi toka mwaka 1963 na kufuatiwa na sheria ya Tamko la Sheria ya Kiislamu ya mwaka 1964 na kuhitimishwa na sheria ya Ndoa ya mwaka 1971”.
 “Jambo la msingi hapa ni kuwa kesi hizo zinahukumiwa na mahakimu wasio na elimu wala ujuzi na sifa za kuwa Makadhi kwa mujibu wa Sheria za Kiislam na ndio msingi wa Waislamu kudai uwepo wa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara”.

Alisema Taasisi hiyo inawakumbusha Maaskofu kuzingatia kuwa madhara ya kuwagawa watanzania kwa misingi ya kiimani, dhambi yake haitoishia kwenye kadhia ya Mahakama ya Kadhi wala Katiba inayopendekezwa bali itaendelea kukita mizizi yake katika kila jambo linalowahusu watanzania.
“Tunawasihi watanzania wote kuendelea kudumisha undugu wao kama watanzania bila kujali rangi, dini, kabila na itikadi za kisiasa na tumkemee yeyote Yule anayetaka kutugawa kwa kutumia misingi ya kidini, kikabila, kisiasa na kiuchumi” 

Akizungumzia kuhusu hali ya usalama wa nchi, viashiria vya ugaidi na mauji ya Albino, Sheikh Mataka alisema Taasisi hiyo inawakumbusha watanzania kuwa suala la kulinda na kudumisha amani na utulivu nchini ni wajibu wa kila mtanzania na kuwaomba kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uilinzi na usalama katika kuzikabili changamoto hizo.

“Ifahamike kwamba mauaji ya albino, tishio la ugaidi na uhalifu mwingine, kamwe havitoweza kukomeshwa kama hatujengi utamaduni wa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini”
“Jukwaa linasisitiza viongozi wa dini wabaki kuwa walezi siyo kuwagawa watu. Mambo ya siasa tuwaachie wanasiasa sisi tubaki na heshima yetu ya kuwa viongozi wa dini kwa sababu hata waumini wetu wanaamini tunapoongea jambo kwamba ni tamko la Kimungu na wanatakiwa kulifuata. Kwa hili hata Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameona hili lina tatizo”.

Alisema.

via Lukwangule blog