Mapitio ya magazeti katika Tv, Jumamosi Machi 21, 2015

Prof. Muhongo: Tanzania Ijayo - Ufugaji wa Kisasa

TANZANIA IJAYO: UFUGAJI WA KISASA NA BIASHARA KUBWA YA MAZAO YA MIFUGO YETU


BIASHARA YA MAZAO YA NG’OMBE DUNIANI

Mazao makuu ya ng’ombe (cattle) ni: (i) NYAMA: beef (adult cattle) na veal (calves) na  sehemu nyingine za ng’ombe zinatumika kwa chakula; (ii) MAZIWA (maziwa ya ng’ombe-diary milk na mazao makuu mengine ni: butter-siagi, yogurt-mtindi and cheese-jibini); na (iii) NGOZI (hides and skins - leather, viatu, mabegi, nguo, mikanda, viti na sofa) ndiyo mazao muhimu ya biashara kwa soko la ndani na kwa masoko ya kimataifa.

Tanzania inalazimika kufanya ufugaji wa kisasa, unaotumia sayansi, teknolojia na ubunifu (science, technology and innovation) kwa sababu watu bilioni 7.3 (2015), bilioni 8.1 (2025), bilioni 9.6 (2050) na bilioni 10.9 (2100) wengi wao watahitaji maziwa ya ng’ombe, nyama na mazao mengine ya mifugo ya aina mbalimbali. Takwimu zinaonyesha kwamba kwa zaidi ya miaka 50, uzalishaji wa nyama Duniani UMEONGEZEKA MARA NNE, kutoka tani milioni 78 kwa mwaka hadi kufikia tani milioni 308 kwa mwaka kati ya Mwaka 1963 na 2014; na wastani wa utumiaji wa nyama kwa mtu mmoja Duniani (consumption per capita) kwa sasa unakadiriwa kuwa kilo 42.9 kwa mwaka.

IDADI YA MIFUGO TANZANIA

Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe (cattle) milioni 23 na asilimia 97 (97%) ya ng’ombe hao wanafugwa kiasilia (indigenous). Sensa ya Mwaka 2012, inaonyesha kwamba kwa Mwaka 2007/08, nchi yetu ilikuwa na idadi ya mashamba makubwa ya ufugaji kama ifuatavyo: kuku-mashamba 494,866; ng’ombe 120,014; mbuzi 24,193; na kondoo 14, 609. 

Idadi ya mashamba makubwa ya mifugo, kwa wakati huo, hayakuzidi 700, 000.

IDADI YA MIFUGO NA ENEO LA MALISHO DUNIANI

Mwaka 2013, idadi ya ng’ombe Duniani ilikadiriwa kufikia bilioni 1.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54 (54%) ya idadi iliyokuwepo Mwaka 1963. Kati ya Mwaka 2008 na 2013, idadi ya kondoo Duniani ilikardiriwa kuwa bilioni 1.1 na mbuzi milioni 881.6. Nchi zenye ng’ombe wengi Duniani ni: (1) India– milioni 329.6; (2) Brazil- milioni 209.8; (3) China- milioni 104.2; (4) USA- milioni 89; na (5) Umoja wa Ulaya- milioni 84.8.

Idadi ya kuku Duniani wanaofugwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu wameongezeka kutoka bilioni 4.1 hadi bilioni 21.7 kati ya Mwaka 1963 na 2013.

Mifugo ndiyo inakisiwa kutumia eneo kubwa la ardhi Duniani (pasture and land dedicated to the production of feed), ikitumia takribani asilimia 80 (80%) ya ardhi yote itumiwayo kwa kilimo: Hekta bilioni 3.4 zinatumika kwa ufugaji (grazing) and theluthi moja ya ardhi inayofaa kwa kilimo Duniani inatumika kuzalisha chakula cha mifugo (The sector uses 3.4 billion hectares for grazing and one-third of global arable land to grow feed crops).

Livestock is the world’s largest user of land resources, with pasture and land dedicated to the production of feed representing almost 80% of the total agricultural land.

UZALISHAJI WA NYAMA DUNIANI

Mwaka 2012, nyama ya takribani tani milioni 304 ilizalishwa Duniani (produced worldwide); na makadirio ya wastani wa matumizi ya nyama yalikuwa kilo 42.8 kwa kila mmoja wetu kwa mwaka (consumption per capita) kwa wakati huo – kwa nchi zinazoendelea ikiwa ni kilo 33.4 kwa mtu mmoja kwa mwaka, na kwa nchi zilizoendelea ikiwa ni wastani wa kilo 76.2 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Kwa Mwaka 2014, FAO ilikadiria ongezeko la uzalishaji wa nyama Duniani kufikia jumla ya takribani tani milioni 311.6. FAO inakadiria kwamba ifikapo Mwaka 2050 (Idadi ya watu Duniani inakadiriwa kuwa bilioni 9.6), uzalishaji wa nyama Duniani utafikia tani milioni 455.

WAUZAJI WAKUBWA WA NYAMA DUNIANI


Brazil na India kwa pamoja ziliuza nyama kwa kiasi cha asilimia 40 (40%) ya nyama yote iliyouzwa Duniani kote (2013). Uuzaji mkubwa Duniani kwa Mwaka 2013 ilikuwa kama ifuatavyo: (1) Brazil iliuza takribani tani milioni 1.85 (20.17% ya mauzo ya Dunia nzima), (2) India tani milioni 1.77 (19.26% ya mauzo ya Dunia nzima), (3) Australia tani milioni 1.59 (17.38%), (4) USA tani milioni 1.17 (12.79%) na (5) New Zealand, tani 528,000 (5.77% ya mauzo Dunia nzima). Kwa upande wa Afrika, muuzaji mkubwa Duniani alikuwa ni Afrika Kusini (namba 22 Duniani) - iliuza tani 13,000 (0.14% ya mauzo ya Dunia nzima).

UZALISHAJI WA MAZIWA YA NG’OMBE DUNIANI

Uzalishaji wa maziwa Duniani unakisiwa KUONGEZEKA ZAIDI YA ASILIMIA 50 (50%) kutoka tani milioni 482 Mwaka 1982 hadi kufikia tani milioni 754 Mwaka 2012. India ndiyo inaongoza kwa kuzalisha maziwa mengi kuliko nchi zote Duniani, inazalisha karibu asilimia 16 (16%) ya maziwa yote ya Dunia, ambayo ni takribani tani milioni 122 kwa mwaka. India inafuatiwa na USA, China, Pakistani na Brazil. OECD na FAO wanakisia kwamba kati ya Mwaka 2010 na 2020 uzalishaji wa maziwa utaongezeka kwa kiasi cha tani milioni 153.

UTUMIAJI WA MAZIWA DUNIANI

Inakadiriwa kwamba kila mmoja wetu (Jumla ya watu bilioni 7.3 Duniani) anatumia wastani wa takribani kilo 108 za maziwa kwa mwaka. Takwimu zinaonyesha utumiaji wa maziwa Duniani kwa kikanda ni kama hivi: (1) Asia: 39% ya utumiaji wa maziwa Duniani, (2) Ulaya (Europe) 29%, (3) Amerika Kaskazini 13%, (4) Amerika Kusini 9%, (5) Afrika 6%, (6) Amerika ya Kati (ikiwemo Mexico) 3%, na (7) Oceania (Australia, New Zealand , n.k.) 1%

BIASHARA YA NGOZI (HIDES & SKINS)

Ngozi za aina mbalimbali zinatokana na wanyama wanaochinjwa au kuuawa. Kati ya Mwaka 2008 na 2013, FAO inakadiria uchinjaji kwa mwaka ulikuwa hivi: kondoo 542.5 milioni na mbuzi milioni 426.6.

Afrika inakadiriwa kuwa na asilimia 15 (15%) ya jumla ya ng’ombe na takribani asilimia 25 (25%) ya kondoo na mbuzi wote Duniani. Hata hivyo, mbali ya wingi huo wa mifugo, Afrika inazalisha asilimia 8 (8%) tu ya ngozi za ng’ombe na takribani asilimia 14 (14%) tu ya ngozi za kondoo na mbuzi Duniani - Idadi ya ngozi zinazozalishwa Duniani inakadiriwa kuwa takribani milioni 240 kwa mwaka.

MTAJI MKUBWA WA UFUGAJI WA KISASA KUTOKA KWENYE UCHUMI WA GESI
ASILIA: Kama ilivyo kwenye KILIMO na UVUVI wa kisasa, UFUGAJI wa kisasa wenye lengo la kuuza mazao ya mifugo yetu kwenye soko la ndani na masoko makubwa ya nje, tunahitaji vitu vitano muhimu sana: (i) ardhi ya malisho kwa wafugaji, (ii) matumizi makubwa ya sayansi, teknolojia na ubunifu - wataalamu na taasisi zao za mafunzo na utafiti wa kaliba ya juu, (iii) rasilimali fedha, (iv) viwanda vya kuthaminisha (value addition) na kukamilisha utengenezaji wa mazao ya mifugo yetu, na (v) sera na sheria za kustawisha ufugaji na wafugaji.

Nchi 10 bora kwa uzalishaji mwingi wa Gesi Asilia Duniani ni: (1) USA, (2) Russia, (3) Iran, (4) Canada, (5) Qatar (GDP per capita: US$ 98,986), (6) Norway (GDP per capita: US$ 100, 579), (7) China (GDP per capita: US$ 6,959), (8) Saudi Arabia (GDP per capita: US$ 24, 953), (9) Algeria (GDP per capita: US$ 5,606) na (10) Netherlands (Uholanzi). Kwa hiyo Uchumi wa Gesi Asilia ni muhimu sana kwa upatikanaji wa mitaji ya uhakika ya kuboresha na kukuza Uchumi wa Mifugo nchini mwetu (Tanzania - GDP per capita: US$ 719).

Ushirikiano na mpangilio unaotekelezeka vizuri kati ya Uchumi wa Mifugo na Kilimo; na Uchumi wa Gesi Asilia, Viwanda na Huduma (services) ndio utakaokuza uchumi wetu kwa zaidi ya 10% kwa mwaka, boresha na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja, na hatimae kutokomeza umaskini wetu na kutufanya tuwe nchi ya kipato cha kati ifikapo Mwaka 2025 (Dira yetu ya Maendeleo).

Document No. 7
Tarehe: 18 March 2015

Prof Dr Sospeter M. Muhongo (Officier, Ordre des Palmes Académiques)
FGSAf, FAAS, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FASI, FTWAS, HonFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol.

Taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini ya ufadhili wa masomo nchini China

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

UFADHILI WA MASOMO NCHINI CHINA.


Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwataarifu watanzania wenye vigezo vya kuomba nafasi za masomo ya shahada ya juu ya Uzamili (Postgratuate) katika fani ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi cha China kijulikanacho kama China University of Geosciences (Wuhan), Chini ya ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, kuwa muda wa kutuma maombi hayo umeongezwa hadi kufikia tarehe 30/03/2015.

Wizara ya Nishati na Madini inaendelea kuwasisitiza watanzania wenye vigezo kutumia fursa hii kwa kujaza fomu zinazopatikana katika tovuti za http://www.csc.edu.cn/laihua au www.campuschina.org na www.mem.go.tz. Pia wanaweza kufika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, ghorofa ya Tatu ili kupata taarifa husika.

IMETOLEWA NA;

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

20 Machi, 2015

Hotuba ya Godbless Lema, Waziri Kivuli Wizara ya Mambo ya Ndani

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. GODBLESS LEMA (MB)UTANGULIZI 

Mheshimiwa Spika, Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu, familia yangu na viongozi wangu wa chama na wananchi wa Jimbo langu. Nawashukuru pia maadui zangu kwa dhati kwani uadui wao, hila zao, na mbinu zao chafu dhidi yangu zimeendelea kuiimarisha imani yangu na tumaini langu siku hadi siku, katika vita hii muhimu tunayopigana ya kulikomboa taifa hili.

Mheshimiwa Spika,Muswada huu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi unaletwa katika Bunge lako tukufu wakati ambapo nchi hii iko katika mtanziko mkubwa ambapo matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yamekithiri; mauaji ya raia kwa kutumia silaha za moto yameongezeka; matukio yenye sura ya ugaidi ya utekaji na utesaji yameshuhudiwa hapa nchini, matukio ya uvamizi na uporaji wa silaha katika vituo vya polisi yanashamiri na uhamiaji haramu umekuwa ukiongezeka pia kwa kasi hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Ni ukweli usiopingika kwamba matukio yote haya yametokea huku kukiwa na sheria ya Usimamizi wa Silaha na Risasi ambayo itafutwa na muswada huu kama utapitishwa na Bunge. Hii ni dhahiri kwamba tatizo kubwa la nchi hii sio sheria na matumizi yake, bali ni uongozi uliokosa fikra chanya na utu katika kutawala.

Ndio maana leo, Serikali inafikiri kupambana na janga la Mauaji ya Albino ni kuwatenga Albino na jamii kutoka kwenye makazi yao ya kawaida wakati tatizo la msingi ni imani potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba; huwezi kuipinga imani kwa kutumia silaha isipokuwa kwa habari njema (imani inayojali utu) kuwafikia watu wote.

Mheshimiwa Spika,Pamoja na nia njema ya Serikali ya kuleta Muswada huu, Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kwamba, kama Serikali itajali utu, usawa, haki na demokrasia ya kweli pengine hakungekuwa na hofu ya matumizi mabaya ya silaha miongoni mwa wananchi na hivyo kusingekuwa na na haja ya kuleta sheria za kudhibiti silaha na kuweka masharti magumu kwa wananchi kumiliki silaha, hasa kipindi hiki ambacho kumekuwa na matukio mengi ya kigaidi, ya uvamizi, utekaji na utesaji ambapo kimsingi wananchi wanahitaji ulinzi wa Serikali na ulinzi binafsi zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Mheshimiwa Spika,Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ifikapo Oktoba mwaka huu wa 2015. Matumizi bora ya sheria za kulinda amani nchini ni muhimu sana wakati huu. Lakini mambo muhimu na ya msingi yakipuuzwa amani inaweza kutoweka licha ya sheria ngumu za udhibiti ikiwemo ya udhibiti wa silaha kuwepo: Masuala hayo ni kama yafuatayo:

i. Kuchezea haki ya mwananchi kujiandikisha kuwa mpiga kura:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kwamba, mzaha katika jambo hili hautavumilika. Aidha, ijulikane kwamba wananchi watakapotambua kuwa hawawezi kuwapata viongozi wao wanaowataka kupitia sanduku la kura, basi wanaweza kutafuta haki yao kwa njia nyingine hali ambayo inaweza kuliingiza taifa katika machafuko kwani haki haiombwi ila inadaiwa.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili waweze kuamua nani atakuwa kiongozi wao kwenye uchaguzi Mkuu unaokuja. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamkumbusha kila mwananchi atambue kwamba “Kura yako ni Maisha yako, Nenda Kajiandikishe Sasa”

ii. Kufanya Mzaha na uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaionya Serikali kutofanya Mzaha na jambo hili kwani linaweza kuiingiza nchi katika machafuko makubwa. Mheshimiwa Spika, Viongozi wa nchi hii wamekuwa wakifanya mizaha kuhusu maisha ya wananchi kwa mambo mengi, yakiwemo ufisadi uliokithiri. Kwa mfano wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, uliwahi kumwomba Mheshimiwa Andrew Chenge kutoa mwongozo wa kutengeneza maazimio ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa wizi wa fedha za Escrow wakati yeye mwenyewe alikuwa ni mtuhumiwa.

Huu ni mzaha mkubwa ambao kwa tafsiri inaonyesha kwamba watawala wanawaona watanzania kuwa ni wajinga. Kambi Rasmi ya Upinzani inaonya kuwa mizaha kama hii ikiletwa kwenye suala la uwepo wa tume huru ya uchaguzi, taifa hili linaweza likasambaratika. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinataka Tume Huru ya Uchaguzi, si kwa sababu inataka kushinda uchaguzi bali ni kwa sababu inataka kujenga na kulinda Imani ya Mpiga Kura ili kulinda amani ya nchi yetu”.

iii. Matumizi ya Kisiasa ya Jeshi la Polisi:

Mheshimiwa Spika, kwa vile imethibitika pasipo shaka yoyote kwamba Polisi mkatili na mkorofi dhidi ya Upinzani anapandishwa cheo, ni dhahiri kwamba kitendo hiki kimejenga msingi (precedence) wa polisi kuwaonea, kuwadhalilisha na kuwafedhehesha viongozi wa Upinzani kwa matarajio kwamba watapongezwa na kupandishwa vyeo na Serikali.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani imepigia kelele sana suala hili la matumizi mabaya ya Jeshi la Polisi ya kulinda maslahi ya kisiasa ya watawala kwa miaka yote. Viongozi, wanaharakati na wananchi wanaounga mkono mageuzi wamepita kwenye bonde la uvuli wa mauti kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, Hatukuonewa kwa sababu sisi ni wanyonge, ila ni kwa sababu tumeendelea kuwa wavumilivu. Nina mashaka kama uvumilivu huo utandelea kuwepo kama uonevu na ukandamizaji utaendelea.

Mheshimiwa Spika, Mwenyezi Mungu, pamoja na upole wake, ukarimu wake, upendo wake, rehema zake kwa watu wote lakini bado ametenga Jehanamu kwa watenda dhambi ambao amewaumba yeye mwenyewe. Tusisubiri wananchi wachoke kuvumilia, bali hekima ya Mungu ituongoze ili kuliepusha taifa letu na majanga ya uvunjifu wa amani pindi watu watakapokosa uvumilivu wa mateso.

iv. Ulinzi wa Raia na Mali zao:Mheshimiwa Spika,

Kukosekana kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao kunaweza kuliingiza taifa katika machafuko. Matukio ya kuuwawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, mauaji ya vikongwe na wanawake kutokana na imani za kishirikina yamekithiri sana katika nchi yetu licha ya kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Hali hii imefanya wananchi kukosa imani na Serikali kwa kuwa bado yanaendelea licha ya kampeni nyingi kutoka kwawanaharakati mbalimbali kupinga mauaji ya Albino. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitahadharisaha Serikali kutodharau kundi la Albino kuwa ni dogo na kutolipatia ulinzi wa kutosha.

Mheshimiwa Spika,Baada ya utangulizi huo, sasa naomba nijielekeze kwenye muswada wa Sheria uliopo mbele yetu unaohusu Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi.

Mheshimiwa Spika,Matukio yote niliyoyataja hivi punde, ni matukio ambayo kwa kiasi kikubwa yamedhoofisha hali ya usalama hapa nchini. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba muswada huu umekuja wakati muafaka kwa kuwa matukio niliyoyataja hapo juu ambayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini, ni matukio ambayo utekelezaji wake unahitaji silaha. Na kwa kuwa matukio hayo ni ya kihalifu, ni dhahiri kwamba hata silaha zinazotumika, hazina uhalali.

Hivyo sheria bora itakayoweka udhibiti na usimamizi wa matumizi ya silaha hapa nchini inaweza kufanikiwa kupunguza matukio ya kihalifu ikiwa itatungwa kwa nia njema ya kulinda usalama wa raia wote na sio kwa lengo la kukandamiza kundi fulani la watu ili kukidhi matakwa ya kisisasa ya kundi la watu wachache.

MAONI NA MAPENDEKEZO YA JUMLA
Mheshimiwa Spika,Kabla sijaanza kuchambua vifungu vya muswada huu, naomba nitoe maoni ya jumla ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu utekelezaji bora wa muswada huu pindi utakapokuwa sheria kama ifuatavyo:

i. Serikali iimarishe ulinzi wa raia na viongozi sambamba na matumizi ya Sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi. Itakuwa haina maana sana kuweka sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi kama wananchi na viongozi watakuwa hawana ulinzi dhidi ya watu wanaotumia silaha kwa malengo ya kihalifu.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa ninapowasilisha maoni haya ya Kambi ya Upinzani kuhusu muswada huu, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana ulinzi wa Serikali. Ni ajabu kwamba Mbunge ambaye kimsingi kazi zake zinamfanya awe na maadaui ambao ni wahalifu na mafisadi anakuwa hana ulinzi wowote wa serikali.

Kwa mfano maisha ya Mhe. David Kafulila aliyeibua sakata la wizi wa Escrow na kusababisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mawaziri kufukuzwa kazi yako hatarini kwa kuwa hana ulinzi wowote. Lakini wakuu wa Wilaya ambao kazi zao ni kupokea mwenge, kusoma taarifa za UKIMWI na njaa wilayani na kupokea wageni wa kitaifa wana ulinzi majumbani mwao.

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka tukio la kuvamiwa na kuchomewa nyumba kwa wabunge wenzetu. Wabunge hawa wangekuwa wamepatiwa ulinzi wa polisi wenye silaha yamkini uvamizi ule ungeweza kuepukika.

Kwa mantiki hii Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuanzia sasa kutoa ulinzi kwenye nyumba za wabunge na viongozi wengine wanaostahili huduma hiyo kama ambavyo Serikali ya Kenya imefanya kwa wabunge na viongozi wake. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutofanya ubaguzi wa ki-ulinzi kwa viongozi katika mihimili mitatu ya Dola (yani Serikali, Bunge na Mahakama).

ii. Wabunge wote na viongozi wote wenye hadhi ya kidiplomasia (Diplomats) wawe na sifa za moja kwa moja (direct entitlement) za kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda mara tu wanapopata hadhi hiyo ya kidiplomasia.

Utaratibu wa kuwatambulisha kwa msajili wa Silaha ili kupatiwa leseni ya umiliki wa silaha ufanywe na taasisi wanazozitumikia. Lengo hapa ni kuepusha mlolongo mrefu wa kuwajadili viongozi walioaminiwa na wananchi walio wengi (kama Rais na wabubunge) au viongozi walioaminiwa kwa kiwango cha juu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliwa na ngazi za chini za uongozi katika vitongoji na mitaa kama ambavyo sheria ya sasa inavyoelekeza.

Kitendo cha kuruhusu viongozi wakuu walioaminika kujadiliwa na ngazi za chini kama wana sifa au hawana sifa za kumiliki silaha ni udhalilishaji wa itifaki (humiliation of protocol)

iii. Ulinzi na Usalama ni pamoja na kutambua hadhi na Itifaki.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutambua hadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya siasa ambao si wabunge lakini vyama vyao vina uwakilishi Bungeni na kuwapa hadhi ya kidiplomasia. Mheshimiwa Spika haiingii akilini kuona kiongozi wa Kitaifa kama Profesa Ibrahim Lipumba ambaye chama chake kina wabunge wengi bungeni na kinaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar anakuwa hana hadhi ya ki-diplomasia.

Kwa upande mwingine inashangaza kuona kiongozi wa kitaifa kama Dkt. Wilbroad Slaa ambaye chama anachokiongoza kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia anakuwa hana hadhi ya kidipolmasia wakati wabunge walioko chini yake wana hadhi hiyo.Mheshimiwa Spika, viongozi wakuu wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi mkubwa bungeni ni viongozi wa Serikali watarajiwa.

Hivyo kupuuza itifaki na ulinzi wao ni kuiweka nchi katika mtanziko na mashaka. Hili si jambo ambalo mnaweza kuliunga mkono kwa sasa lakini ni jambo muhimu kwenu kuelewa.

MAONI NA MAPENDEKEZO YA VIFUNGU MAHSUSI
Mamlaka ya Msajili wa Silaha

Mheshimiwa Spika,Mamlaka na majukumu ya Msajili wa Silaha yametolewa chini ya kifungu cha 8(2) cha muswada huu wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha. Lakini kifungu hicho, hakijatoa mwongozo au mipaka ya utekelezaji wa majukumu ya Msajili wa Silaha. Matokeo yake ni kwamba katika maeneo mbalimbali ya sheria hii, Msajili amepewa mwanya mkubwa wa kuamua anavyotaka (discretion).

Kwa mfano kifungu cha 17 (1) na (2) kinampa Msajili wa Silaha mamlaka ya kutoa kibali cha kumiliki silaha kwa mtu yeyote kwa kipindi ambacho ataamua yeye mwenyewe na kuweka masharti ya kibali hicho yeye mwenyewe. Aidha, Msajili anaweza katika muda wowote kufuta kibali cha umiliki wa silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtazamo kwamba, ni bora zaidi masharti ya utoaji kibali cha muda, masharti ya muda au kipindi ambacho kibali hicho kitakoma na masharti ya kufuta kibali yakawekwa na sheria na sio kutegemea utashi wa Msajili wa Silaha. Kwa kufanya hivyo, mianya ya rushwa au upendeleo au uonevu wa aina yoyote katika utekelezaji wa majukumu ya Msajili wa silaha inaweza kuzibwa na kuepukwa.

Watu wasio na Sifa ya Kumiliki Silaha

Mheshimiwa Spika,Katika kifungu cha 26(1) cha muswada huu ipo orodha ya mambo au tabia zinazoweza kumkosesha mtu sifa ya kumiliki silaha. Miongoni mwa tabia hizo ni pamoja na Ukorofi.Kwa kuwa tafsiri ya neno ukorofi ni subjective , na kwa kuwa kila mtu anaweza kutafsiri ukorofi kwa namna yake, hivyo msajili wa Silaha anaweza kuwa na tafsiri yake ya ukorofi kutokana na hisia zake na kumnyima mtu leseni ya kumiliki silaha kwa kisingizio kwamba mtu huyo ni mkorofi.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kwamba neno ukorofi litafsiriwe na sheria hii ili kuondoa mkanganyiko wa tafsiri pindi sheria hii itakapoanza kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, Kifungu 26(2) cha muswada huu kinaeleza kwamba endapo msajili wa silaha ataridhika kwamba kuna sababu za msingi za kuamini kwamba mtu hana sifa ya kumiliki silaha, atatoa notisi ya maandishi akimtaka mtu huyo kufika mbele yake katika muda na sehemu iliyotajwa katika notisi hiyo ili kuonyesha ni kwa sababu gani asitangazwe kuwa hana sifa ya kumiliki silaha. Aidha, ikiwa mtu aliyepewa notisi hiyo atashindwa kuhudhuria katika muda na sehemu iliyotajwa katika notisi, Msajili wa silaha atamtangaza mtu huyo kuwa hana sifa ya kumiliki silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba kifungi hiki kina mapungufu. Mapungufu hayo ni pamoja na muda wa kufika mbele ya msajili kutowekwa na sheria na badala yake kuachwa katika utashi (discretion) ya msajili wa silaha; na sharti la kufika mbele ya msajili wa silaha mwenyewe kujieleza kama mtu ana sifa ya kumiliki silaha iwapo kuna mashaka juu yake.

Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kwamba muda wa kufika mbele ya msajili uwekwe na sheria ili kuziba mwanya wa uonevu unaoweza kutumika kwa kuweka muda mfupi ili mtuhumiwa ashindwe kufika katika muda huo na kutangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha. Aidha, sharti la kufika mbele ya Msajili mwenyewe liondolewe na badala yake sheria iweke wasajili wasaidizi katika mikoa ili kupunguza adha na ghrama za kusafiri kumfuata msajili wa Silaha mmoja ambaye kwa vyovyote vile ofisi yake itakuwa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26(3) kinasema kwamba cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na kibali kilichotolewa kwa mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha vitapoteza uhalali wake kuanzia tarehe ya kutangazwa huko. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji, ni kwa nini Serikali itoe cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na kibali kwa mtu ambaye hana sifa?

Nasema hivi kwa sababu ikiwa Serikali itakuwa makini tangu mwanzo mtu anapoomba leseni au kibali cha kumiliki silaha basi uwezekano mtu huyo aliyekidhi vigezo tangu mwanzo vya kumiliki silaha kupoteza sifa na kutangazwa kuwa hana sifa utakuwa ni mdogo sana vinginevyo awe amekuwa kichaa ghafla.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26(4) kinasema kwa pia kwamba mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha, basi atasalimisha katika kituo cha Polisi haraka iwezekanavyo cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na vibali vilivyotolewa kwake na silaha pamoja na risasi zilizo katika umiliki wake.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kwamba huu unaweza kuwa ni uporaji wa hila wa silaha za wananchi kwa kutumia sheria, kwa kuwa muswada huu haujatamka ni hatua gani zitafuata baada ya mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa za kumiliki silaha atakaposalimisha silaha yake na nyaraka za umiliki katika kituo cha polisi. Sheria hii ikiachwa kama ilivyo inaweza kutumika kwa kulipiza visasi au kutekeleza maelekezo yenye nia mbaya.

Utoaji wa silaha na risasi kutoka katika ghala la umma au kituo cha Polisi

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 29(1) cha muswada huu kinaeleza kwamba silaha au risasi zilizohifadhiwa katika ghala la umma, kituo cha polisi au sehemu nyingine yoyote iliyoelezewa na Msajili hazitatolewa humo isipokuwa kwa kibali kilichosainiwa na msajili. Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kuwe na ugatuzi wa madaraka ili kibali cha kuondoa silaha katika ghala la umma au sehemu nyingine yoyote kiweze kusainiwa na Wakuu wa Polisi wa Mikoa hasa pale kunapotokea dharura mfano ujambazi, uasi, wanyama hatari nk.

Masharti kwa Wauzaji wa Silaha

Mheshimiwa Spika,Kifungu cha 33 cha muswada huu kinampa Waziri mamlaka makubwa ya kutunga kanuni zitakazoweka masharti ya utoaji wa kibali cha muuzaji wa silaha, masharti kuhusiana na eneo la biashara la muuzaji, masharti ya kutolewa upya kwa kibali cha muuzaji na masharti ya kusitishwa, kufutwa kwa muda kwa kibali cha muuzaji wa silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza masharti hayo yatajwe na sheria ili kuziba mwanya wa Waziri kutumia madaraka yake vibaya kwa kuweka masharti kandamizi au ya upendeleo kwa baadhi ya makundi ya wauzaji wa silaha.

Upekuzi na Ukamataji wa Silaha

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 54 cha muswada huu kinasema kwamba “Hakuna mashtaka au hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya Msajili au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa anayetekeleza majukumu yoyote chini ya sheria hii kwa lolote atakalolitenda wa nia njema”

Mheshimiwa Spika, Hakuna utendaji bora usiokuwa na mipaka. Kifungu hiki kinaweza kutumika vibaya kwa kuwa kinatoa mwanya mkubwa kwa Msajili au afisa yeyote aliyeidhinishwa kupekua au kukamata silaha kufanya jambo lolote hata kama ni ovu kwa kisingizio cha “nia njema. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba sheria hii imtake msajili au afisa aliyeidhinishwa kuzingatia kanuni na taratibu za upekuzi na ukamataji, kwani kumiliki silaha kihalali sio kosa la jinai hivyo upekuzi na ukamataji uzingatie taratibu za kisheria hasa kwa wale wanaomiliki silaha kihalali.

Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya marekebisho ya baadhi ya vifungu yataletwa katika jedwali la marekebisho wakati wa Kamati ya Bunge zima.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Imekuwa ni desturi kwa Serikali zilizoko madarakani kuleta miswada ya sheria kwa ajili ya kulinda maslahi yake yenyewe bila kujali maslahi mapana ya wananchi na taifa kwa jumla. Aidha, imekuwa ni desturi sheria nyingi kupitishwa haraka hara bila kupata maoni ya wadau wengi jambo ambalo husababisha sheria nyingi kupingwa kabla hata hazijaanza kutumika. Mfano halisi ni Muswada huu kutoshirikisha wadau ipasavyo. Wadau wengi walilalamika mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kwamba hawakushirikishwa kabisa katika mchakato wa kuandaa muswada huu.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaihoji Serikali ni kwa nini inapuuza wadau katika sheria muhimu kama hii? Je, Serikali haioni kuna athari kubwa kiulinzi na kiusalama kwa kutowashirikisha wadau wakubwa wa silaha na risasi kama vile makampuni ya ulinzi binafsi, na wafanyabiashara wakubwa wa silaha hapa nchini?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza tena kwamba Amani na utulivu wa nchi hii hautategeme tu uwepo wa sheria ya udhibiti na usimamizi wa silaha na risasi bali uongozi unaozingatia misingi ya utawala bora, haki, usawa, ukweli na usitawi wa jamii nzima kwa jumla. Aidha, ugumu wa maisha unaosababishwa na umasikini uliokithiri kutokana na mfumuko wa bei, elimu duni, maradhi, ukosefu wa ajira, ukosefu wa maji safi na salama nk. ni viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani kuliko silaha na risasi ambazo Serikali inafanya bidii kubwa kutungia sheria.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni bado inaitaka Serikali kukumbuka na kuzingatia barabara masuwala manne muhimu iliyotahadharisha yasichezewe au kufanyiwa mzaha kwani yanaweza kuliingiza taifa katika machafuko.

Masuala hayo ni kuchezea haki ya mwananchi kujiandikisha kuwa mpiga kura, Kufanya Mzaha na uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, Matumizi ya Kisiasa ya Jeshi la Polisi na Ulinzi wa Raia na Mali zao hususan ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Mheshimiwa Spika,Baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, naomba kuwasilisha.

Godbless Jonathan Lema (Mb)
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
NA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
19 Machi, 2015

Barua na hotuba ya Zitto ya kuaga CHADEMA na Bunge

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBEIR KABWE, MB KUHUSU UANACHAMA WAKE KATIKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA HATMA YAKE KAMA MBUNGE KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

DODOMA, ALHAMISI 19 MACHI 2015.
____________________________________

1)      Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa fursa uliyonipa kutoa maelezo yangu binafsi katika Bunge lako Tukufu leo. Ninatoa maelezo haya kwa mujibu wa Kifungu cha 50 (1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 kinachosema kwamba,

“Mbunge yeyote anaweza, kwa idhini ya Spika, kutoa maelezo binafsi Bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii”

2)      Mheshimiwa Spika, Nilijiunga na Bunge lako Tukufu kwa mara ya kwanza Mwaka 2015 nikiwa na lengo kuu la kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na kutetea maslahi ya Watanzania hususani Wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma, na Watanzania kwa ujumla. Nilichaguliwa na wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Wananchi wa Kigoma Kaskazini walinichagua tena Mwaka 2010 kupitia tiketi ya CHADEMA.

3)      Mheshimiwa Spika, kupitia fursa ya ubunge niliyopewa na wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa udhamini wa CHADEMA, nimejifunza mengi hapa Bungeni na nje ya Bunge hili. Nimeijua nchi yangu, nimejua siasa na nimejulikana ndani na nje ya Tanzania. Muhimu zaidi ni kwamba nimepata fursa adhimu ya kutoa mchango wangu katika kutunga sheria na sera mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Aidha, nilipata fursa ya kipekee kama Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati zako mbili ya kuisimamia, kuishauri na kuiajibisha serikali.

4)      Mheshimiwa Spika, Ninawashukuru sana wanachama wa CHADEMA kwa dhamana mbalimbali walizonipa ndani ya CHADEMA. Ninawashukuru viongozi wangu na hasa Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa kunilea na kuniamini kufanya naye kazi kwa kipindi chote tangu nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, katika chama na hapa Bungeni. Kama ambavyo nimesema mara nyingi, CHADEMA imenilea na kunikuza tangu nikiwa na umri wa miaka 16 na tangu kipindi hicho nimejifunza mengi.

5)      Mheshimiwa Spika, Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa mapenzi yao na imani waliyonipa na kuniwezesha kukalia KITI hiki ninachokalia ndani ya Bunge lako Tukufu. Nashukuru kwamba juzi nilipata fursa ya kipekee ya kuwashukuru kwa imani waliyonipa kuwatumikia kwa vipindi viwili mfululizo. Mola atawalipa wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa imani kubwa walioionyesha kwangu na kuniwezesha kulitumikia Taifa langu kwa namna nilivyolitumikia.

6)      Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa pamekuwa na msuguano wa kiuongozi kati yangu na viongozi wangu ndani ya CHADEMA uliosababishwa na tofauti za kimtazamo juu ya tafsiri pana ya demokrasia ndani ya chama chetu. Hatimaye tofauti hizi zilipelekea mwezi Novemba 2013 Kamati Kuu ya CHADEMA kunivua nafasi zangu zote za uongozi nilizokuwa nazo. Sikuridhika na maamuzi hayo na hivyo nikaonyesha kusudio la kukata rufaa katika Baraza Kuu la chama chetu kama taratibu za kikatiba za chama chetu zinavyotaka. Bahati mbaya ofisi ya Katibu Mkuu haikunipa fursa hiyo, na huo ndio ukawa msingi wa mimi kufungua kesi mahakamani kuweka pingamizi la Kikao cha Kamati Kuu kujadili hatima ya uanachama wangu hadi pale ofisi ya Katibu Mkuu itakaponipa fursa ya kukata rufaa katika vikao vya chama. Yaliyotokea baada ya hapo ni historia, lakini hatimaye Mahakama Kuu imetoa hukumu yake tarehe 10 Machi 2015. Katika hukumu hii, nimeshindwa kwa sababu za kiufundi kwa maelezo kwamba pingamizi letu liliwasilishwa kimakosa.

Pamoja na kwamba hatukuridhika na mwenendo wa jinsi kesi hii ilivyoamuliwa pamoja na maudhui ya hukumu yenyewe, ninaheshimu maamuzi ya mahakama na sina mpango wa kukata rufaa.

7)      Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, ilitarajiwa kwamba baada ya maamuzi ya Mahakama Kuu, Kamati Kuu ingekaa na kunipa rasmi mashtaka yangu yanayohusu uanachama wangu, mimi kuitwa kujieleza na hatimaye Kamati Kuu kutoa uamuzi wake. Hata hivyo, mara baada ya hukumu ya Mahakama Kuu dunia nzima ilitangaziwa na Mwanasheria wetu Mkuu, kwa niaba ya chama, kwamba mimi nimeshafukuzwa na sio mwanachama tena wa CHADEMA. Baada ya hapo viongozi wangu wametoa matamko mbalimbali yote yakionyesha kwamba sitakiwi tena katika chama hiki, pamoja na kwamba hadi ninapoongea hapa leo sijawahi kukabidhiwa barua yeyote inayonitaarifu kufukuzwa kwangu katika chama.

8)      Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ni wazi kwamba uanachama wangu wa kisiasa ndani ya CHADEMA umeshaondolewa. Ninaweza kuendelea kupigania uanachama wangu kisheria na kwa kweli nina sababu na misingi yote kubaki na uanachama wangu kisheria. Lakini mimi ni mwanasiasa. Sikuja hapa bungeni kwa sababu ya kushinda kesi mahakamani. Nilichaguliwa na wananchi wa Kigoma Kaskazini na ninatambua kwamba huwezi kuwa mbunge bila udhamini wa chama cha siasa. Huu ndio utaratibu wa kisheria tuliojiwekea. Kwa mujibu wa viongozi wangu katika chama ni kwamba udhamini wa chama changu umekwishaondolewa.

9)      Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ninaomba kukutaarifu wewe na Bunge lako tukufu kwamba sina mpango wa kuendelea kupigania uanachama wangu wa CHADEMA katika viunga vya mahakama. Kwa hiyo ninatangaza rasmi leo kwamba taratibu za kikatiba zitakapokamilika tu nitaachia uanachama wa CHADEMA, chama nilichokipenda sana kwa sababu ya kuendelea kukua kwa tofauti za kiitikadi, kimtazamo na hata kibinafsi kati yangu na viongozi katika chama changu. Nimeona kuwa kuendelea kupigania uanachama kisheria ni kutatiza na kukwaza harakati za mabadiliko hapa nchini katika wakati ambapo mfumo wa kisiasa unatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa. Kwa kuwa taratibu hizo sijui zitakamilika lini,  natumia fursa hii kuwaaga wabunge wenzangu.

10)  Mheshimiwa Spika, vyama vya siasa ni jukwaa muhimu katika ujenzi wa demokrasia lakini havipaswi kamwe kuwa juu ya wananchi. Kwa hiyo ni maoni yangu kwamba wakati sasa umefika wa kukomesha udola na ufalme wa vyama vya siasa hapa nchini. Mfumo wa siasa ambao unavipa vyama vya siasa mamlaka ya kisheria ya kukanyaga mamlaka ya wananchi haupaswi kuendelea katika Karne ya 21 na katika nchi ambayo inaendeshwa kwa misingi ya demokrasia ya kuheshimu wananchi. Mimi ninaondoka bungeni sio kwa sababu wananchi wangu wa Kigoma Kaskazini walionichagua wametaka niondoke. Siondoki kwa sababu nimeshindwa kufanya kazi zangu za ubunge. Na kwa kweli siondoki kwa sababu wanachama wenzangu katika CHADEMA wametaka niondoke. Ninaondoka kwa sababu mfumo wetu wa kisheria unavipa vyama vya siasa mamlaka juu ya wananchi na wapiga kura. Ni matumaini yangu kwamba Bunge lako tukufu halitaruhusu mfumo huu unaoruhusu vyama vya siasa kupora mamlaka ya wananchi uendelee. Ni Bunge lako pekee lenye uwezo wa kukomesha mfumo ambao unatukuza Parties’ Power, badala ya People’s Power.

11)  Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali kwamba vyama vya siasa ni jukwaa. Bahati nzuri nchi yetu inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa na sasa tuna vyama 22. Kwa hivyo, wananchi wanaoniunga mkono wasisikitike kwa maamuzi yangu ya leo. Bado ninayo fursa ya kuwatumikia kupitia jukwaa lingine ambalo nitaamua katika siku chache zijazo, na inshala Mungu akitujalia nitarudi tena hapa Bungeni katika Bunge la 11 kwa nguvu za wananchi.

12)  Mheshimiwa Spika, kwa miaka kumi niliyotumikia hapa Bungeni, si yote niliyoyafanya yalikuwa sahihi, yapo ambayo niliyakosea kama mwanadamu katika kufanya kazi zangu, kwa namna yeyote ile naomba radhi Watanzania wote kwa yote ambayo sikuyafanya kwa usahihi. Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu, sijakamilika. Ni Mola peke yake aliyekamilika.

13)  Mheshimiwa Spika, siwezi kuanza maisha yangu mapya kisiasa bila ya kulishukuru Bunge lako Tukufu. Kwanza, Bunge la Tisa chini ya Mzee Samwel Sitta, mzee wa kasi na viwango! Bado ninakumbuka vizuri jinsi hoja ya Buzwagi ilivyotikisa Bunge lake na hatimaye kupelekea nchi yetu kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa sekta ya madini (Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ) na hivyo kukuza mapato ya sekta ya madini kutoka Tshs. 32 bilioni kwa mwaka mpaka Tshs. 450 bilioni kwa mwaka.

14)  Mheshimiwa Spika, ninajivunia kuwa sehemu ya Bunge la Kumi chini yako, Mama shupavu Anna Semamba Makinda. Katika Bunge hili nimekuzwa, nimejifunza, nimepambana, nimefurahi na nimelia ndani ya Bunge hili. Kwa pamoja tumepigania maslahi ya wananchi wetu kwa juhudi na maarifa na hivyo kuleta mabadiliko kadhaa. Ni katika kipindi hiki ambapo wabunge tumekuwa na sauti. Bunge la Tisa lilijijenga likawa ‘Bunge lenye Meno’ katika kupambana na ufisadi. Bunge la Kumi limejenga ‘Bunge lenye Nguvu’ katika mfumo wa Bajeti ya nchi yetu. Kupitia Bunge hili tumeweka misingi ya kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji katika nchi yetu. Na katika siku za hivi karibuni Bunge la Kumi litakumbukwa kwa Hoja Maalumu ya Tegeta Escrow iliyopelekea mfumo wetu wa maadili ya Viongozi kupitia Baraza la Maadili kuanza kufanya kazi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miaka iliyopita.

15)  Mheshimiwa Spika, wajumbe wa PAC ( ambao nimeishi nao kama familia ) tumekuwa nguzo kubwa ya kujenga uwajibikaji wa Serikali kwa Bunge na wananchi. Napenda kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa kuniunga mkono na kwa kunipa ushirikiano kama Mwenyekiti wao. Changamoto na malezi mliyonipa kwa miaka yote hii yamejenga Mtanzania mmoja mwenye nia ya dhati ya kuitumikia nchi yake, muda wowote, wakati wowote na kwa namna yeyote ile bila woga wala upendeleo. Nawashukuru kwa kujitoa kwenu kwa nchi yetu na dhamira isiyo na mawaa ya kujenga Taifa imara zaidi. Pamoja na kwamba ninaondoka Bungeni leo, ninaahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Kigoma Kaskazini na Taifa langu katika kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote.

16)  Mheshimiwa Spika, Kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Baraza hili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini. Inawezekana tusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika dhamira kubwa ya kuijenga nchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, yaani Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni matumaini yangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakati hizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi! Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuweka tofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu.

17)  Mheshimiwa Spika, Ninawashukuru tena na tena wana Kigoma na wananchi wote wa Tanzania ambao kwa ridhaa yao nimekaa katika viti hivi kwa miaka takribani kumi. Ninawahakikishia kuwa changamoto nilizokumbana nazo na ambazo zimenilazimisha leo niondoke bungeni zimechochea zaidi dhamira, nia na sababu yangu ya kuwatumikia kwa nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Huu ni mwanzo mpya.

Mheshimiwa Spika,

Asanteni sana na Kwa herini!

Lecture: How Could Non-Communicable Diseases (NCDs) be Reduced and Prevented?

ZIRPP Monthly Lecture

Chairperson: Ms. Mariam M. Hamdani

Speaker: Dr. Faiza Kassim Suleiman

Subject: "How Could Non-Communicable Diseases (NCDs) be Reduced and Prevented?"

Date & Time: Saturday 28 March 2015; at 4:00 pm.

Venue: ZIRPP Office; Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK)

Abstract: Non Communicable Diseases (NCD) represent a knew frontier in the fight to improve global health. Worldwide, the increase in such diseases means that they are now responsible for more deaths than all other causes combined. Commonly known as chronic or lifestyle related diseases , the main NCDs are Cardiovascular diseases, diabetes, cancers and chronic respiratory diseases. While the international community has focused more on communicable diseases, such as HIV/AIDS, Malaria and Tuberculosis, the four main NCDs have emerged relatively un-noticed in the developing world and are now becoming a global epidemic. However, such diseases could be significantly reduced and prevented, with millions of lives saved and untold suffering avoided, through proven and affordable measures. It is time to act to save future generations from the health and social economic harm of such diseases.

Dr. Faiza Kassim Suleiman, Diabetologist and Head of Diabetes Services at Mnazi Mmoja Hospital, ZANZIBAR, will tell us how to achieve just that.

The lecture will be followed by the ceremony of formal presentation of the Certificates of Completion of Internship to our two interns from the United States of America for their exemplary work at ZIRPP; as well as the presentation of Certificates of Appreciation to our four distinguished Members for their invaluable contribution to the work and ideals of the Institute.

Tea, Coffee and Snacks will be served freely.

Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: [email protected]

Please confirm your participation.

All are welcome.

Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475;
Cellular: 0777 707820;
Email: [email protected];
Weblog: www.zirpo.wordpress.com
Website: www.zirpp.info

Tanzania Institute of Bankers - Continuing Banking Education Programme 2015


Amwacha 'sugar mammy' wake baada ya 'kumtumia kupata makaratasi'

Mwanamke mmoja nchini Uingereza mwenye miaka 64 ametelekezwa na kuachwa na kijana wake wa Kiafrika mwenye miaka 26 baada ya kumkamilishia taratibu za visa.

Mwanamke huyo mlemavu, Patricia ambaye alimpenda mvulana wa asili ya Tunisia kupitia mitandao ya kijamii, alimkamilishia taratibu zote za kufika na kuishi Uingereza.

Patricia alijuana na Mtunisia huyo, Mondhler katika tovuti ya mahusiano na kumpenda hatimaye kufanya taratibu za ndoa.

Patricia ambaye anaishi Midlands, alielezea namna alivyokua akitafuta mpenzi wa kuishi naye milele katika redio Channel 5 nchini Uingereza.

"Mwanzoni alionesha kuwa ana mapenzi ya dhati na kunishawishi kuwa miaka haimaanishi kitu zaidi ya tarakimu tu", alieleza Patricia.

Lakini Mondhler alipofika tu Uingereza alimtelekeza na kumuacha mwanamke huyo solemba.

via TRT Swahili

Walimu wajiondoa CWT na kuunda CHAKAMWATA

CHAMA kipya cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kimesajiliwa rasmi na kupata cheti cha usajili wa kudumu kutoka Wizara ya Kazi na Ajira.

Akizungumza na FikraPevu, Katibu Mkuu wa Chakamwata, Mwalimu Meshack Kapange, anasema chama hicho kipya kinaundwa na walimu nchini waliojiondoa kutoka mikononi mwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Kapange amesema mchakato wake wa kukisajili chama hicho ulianza miaka minne iliyopita, hadi hivi juzi kilipopewa usajili wa kuendelea na shuhuli zake kisheria.

“Ni furaha iliyoje kupata usajili huu wa chama chetu cha kutetea haki na maslahi ya walimu? Huu ni ukombozi kwa walimu wanaokatwa asilimia mbili za mishahara yao bila kurejeshewa wanapostaafu,” anasema Katibu Mkuu huyo.

Kuundwa kwa chama kipya hicho kumetajwa na wachambuzi wa mambo kwamba kunaweza kuipasua CWT na pia kutahitimisha ukiritimba wa muda mrefu mrefu wa chama hicho. Aidha, chama hicho kitatoa fursa sasa kwa walimu nchini kuwa na hiyari ya kujiunga na chama ambacho wataona kina maslahi kwao badala ya ilivyo sasa ambapo walimu walikuwa hawana chaguo zaidi ya kujiunga na CWT.

Kwa mujibu wa Mwalimu Kapange, Makao Makuu ya sasa ya chama hicho yatakuwa Jijini Mbeya. Anasema walimu watakaohitaji kujiunga na chama hicho kipya, watafanya hivyo kwa hiari yao kama sheria za kazi zinavyoelekeza tofauti na CWT ambayo kila mwalimu anayepata ajira serikalini alikuwa analazimishwa kujiunga na kuanza kukatwa fedha zake kutoka kwenye mshahara wake bila ridhaa yake na kinyume cha sheria za ajira.

“Kila mwanachama atachangia asilimia moja tu ya mshahara wake kwa kila mwezi badala ya asilimia mbili kama ilivyo kwa CWT. Wakati mwanachama anapostaafu, atapewa ‘bonus’ kama asante kwa kuchangia Chama,” anasema Mwalimu Kapange.

Mbali na hilo, Kapange anasema Chakamwata kitafanya jitihada za kuwajengea wanachama wake uwezo wa kutambua wajibu wao, haki zao na jinsi ya kuzidai, badala ya kutambua wajibu pekee kama ilivyo ndani ya CWT, kwa maelezo kwamba hakuna wajibu kwa mtumishi yeyote wa umma usiokwenda sambamba na haki yake.

“Tulipokuwa tukiomba usajili kwa mara ya kwanza Mei, 2012, tulikuwa wanachama 400 ingawa masharti ya kisheria ya kuanzisha vyama kama hivi yanataka wanachama 20 tu. Nashukuru kwamba hadi tunapata usajili huu, wanachama wetu wanafikia 9,743, wengi wao wakitokea mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Arusha, Mara, Morogoro, Singida na Kagera,” amesema.

Chama kipya hicho, kabla hakijasajiliwa, kilikuwa kikijulikana kwa jina la Umoja wa Maofisa Elimu Tanzania (UMET). Hata hivyo, uongozi wa muda wa chama hicho ulikaa tena na kukipa chama hicho jina la Chakamwata. Chama hicho kimepewa usajili kwa namba 031, huku cheti chake kikiwa kimesainiwa na Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri nchini, Doroth Uiso.

FikraPevu inaendelea kumtafuta Rais wa CWT, Gratian Mukoba, pamoja na maoni ya walimu mbalimbali nchini, ili pamoja na mambo mengine, waweze kuelezea ujio wa chama kipya hicho cha walimu nchini na athari zake katika mstakabali wa mshikamano na utengamano wa walimu nchini katika siku za usoni.

  • via FikraPevu

[video] Kauli za kada wa CHADEMA baada ya kuachiwa kwa dhamana


Wanachana wa CHADEMA waliokuwa wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumtesa Khalid Kangezi aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willibrod Slaa wameungumza baada ya kutolewa nje kwa dhamana.

How much should you pay Engineers? Infographic of what pays mostPlease visit startupcompass.co for more about this infographic (and also if not visible above).