[video] Kero ya mvua Dar ni ile ile nenda rudi msimu uliopita, huu, ujao

Kibonzo via WhatsApp
Mapitio ya magazeti katika Tv Jumapili, Machi 22, 2015


[video] Wachoma nyumba baada ya mwenzao kuuawa 'alipofumaniwa' akiwa na binti wa kazi


Mswada binafsi wa Baraza la Vijana la Taifa kujadiliwa Bungeni

MUSWADA BINAFSI WA BARAZA LA VIJANA LA TAIFA KUJADILIWA BUNGENI TAREHE 31 MACHI 2015


Nashukuru wote ambao mmekuwa mkifuatilia hatma ya muswada binafsi wa Baraza la Vijana la Taifa niliouwasilisha tarehe 31 Oktoba 2013.

Vijana na wadau wa maendeleo ya vijana mzingatie kwamba muswada huo hatimaye umepangwa kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni Jumanne tarehe 31 Machi 2015 katika Mkutano wa 19 wa Bunge.

Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa 14 wa Bunge tarehe 21 Disemba 2013. Maoni kutoka kwa wadau yalikusanywa Oktoba 2014 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

Baraza la Vijana la Taifa pamoja na malengo mengine litawezesha vijana kuanzia kwenye vijiji/mitaa mpaka taifa kuweza kuwa na vyombo vya kuwaunganisha vijana kwa kike na wa kiume kwa ajili ya maendeleo yao na ya taifa.

Aidha, Baraza hilo litafuatilia pia kwa karibu utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya vijana ikiwemo kuhusu ajira, elimu na sekta zingine katika Halmashauri, Serikali kuu, katika vyombo mbalimbali vya maendeleo na wadau wa maendeleo.

Pia, Muswada huo utawezeshwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kulipa jukumu Baraza la Vijana kufuatilia kwa karibu utendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; kuhakikisha kwamba fedha zinatengwa za kutosha na kufika kwa walengwa kuwawezesha vijana kujiajiri, kukuza vipaji vyao na kushughulikia maendeleo yao kwa ujumla.

Kujadiliwa kwa muswada huo ni hatua ya pekee katika historia ya harakati za vijana nchini kwa kuzingatia kuwa Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 ilitamka kwamba kutaanzishwa Baraza la Vijana na suala hilo kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007.

Hata hivyo Serikali imekuwa ikikwepa kuhakikisha kwamba matakwa hayo ya sera tajwa yanatekelezwa kwa wakati pamoja na kuwa suala hilo linahusu mustakabali wa maendeleo ya vijana nchini.

Natambua mchango wa vijana na taasisi zote za vijana mlioshiriki katika maandalizi ya muswada huu, unaitwa binafsi kwa sababu tu ndio neno linalopaswa kutumika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge lakini ukweli ni kwamba huu ni muswada wenu; mimi ni mwakilishi.

John Mnyika (Mb)
Machi 2015

Watanzania tuliopo Japan tunapinga ukaguzi wa magari na baiskeliSisi watanzania tuishio Japani kupitia umoja wetu wa WANATIJA tunaungana na wenzetu Waishio England Kupinga kwa moyo mmoja ukaguzi wa magari na Baskeli ziingiazo Tanzania japo serekali imekuwa kipofu na kiziwi kutokujua mchango wetu wanachi wa tanzania tunao ishi nnje ya nchi.
Lakini sisi tunaamini kuwa tumekuwa sehemu kubwa ya kuleta maendeleo yaliyopo sasa nchini mwetu.

Ni mara nyingi tumelalamika juu ya swala hili lakini limekuwa likipuuzwa kwa kuwa lina mikono ya rushwa ndani yake.

Ukweli ni kwamba kuweka ukaguzi wa magari yaingiyao Tanzania ni mradi wa watu wachache wanaoendeleza unyonyaji ulio wazi.

Tukichukulia ukweli wa nchi tunazoishi ni kwamba gari hukaguliwa pale linapopewa usajili na namba kwa ajili ya kuanza kutumika katika kipindi chote cha matumizi, hata kama litatumika katika miaka 10 hadi miaka 100 huu utaraibu unasaidia sana nchi kuwa na magari yaliyo katika hali nzuri sana.

Mfano hapa Japan na England: Gari jipya hukaguliwa kila baada ya mwaka 1 miaka 2 mpaka miaka 3 hii hulingana na aina ya magari na matumizi ya gari. Hi husaidia kujua ubora wa gari kwa kipindi chote lilotumika kutoka kusajilia katika matumizi ya mwanzo.

Tofauti na kwetu Tanzania, hao wataalamu wanao lipiwa first class ticket kwenda nje ya nchi kujifunza wenzetu wanachofanya huja na idea tofauti kabisa na kuanda mazingira ya rushwa kwa kuwakandamiza Watanzania kwa kuwanufaisha walio wachache na muathirika mkubwa akiwa ni Mtanzania atakayenunua gari kwa matumizi yake, kwa kuwajibika kulipa ghara kubwa sana.

Type of VehicleValid Term
First inspectionFrom the 2nd inspection
Trucksover 8 tons1 year1 year
under 8 tons2 years1 year
Buses/Taxis1 year1 year
Rental Cars (Passenger cars only)2 years1 year
Mini-sized Trucks
Small-sized Motorcycles
Large-sized Special Motor Vehicles
2 years2 years
Private Passenger Motor Vehicles
Mini-sized Passenger Motor Vehicles
3 years2 years

Kuna maswali mengi ya msingi ya kujiuliza kwa watu wenye akili timamu

(1) Unapokagua gari nchini Japan au England lilopasi ukaguzi katika viwango vya juu na si vya kitapeli kama hivi tunavyo peana kwa kujuana kwa tender za kinafiki na kuja kutumika nchini bila kukaguliwa tena ipi bora kwa nchi yetu?

(2) Unaposema kuwa utakagua radiation ya nuclear nchini Tanzania wakati gari hizi hukaguliwa hapa Japan kabla ya kuuzwa auctions na pia hupitia tena free inspection bandarini kwa gari zote zinazotoka nje ya japan bila kujali nchi zinakokwenda na inayo kuwa na radiation huwa haziruhusiwi kutoka nje ya Japan, ninyi Tanzania mnakagua nini? au ndiyo mazingira ya kuwaibia wananchi?

Inabidi kufika wakati tupunguze mzigo kwa wananchi wa Tanzania kwa kuwa wao ndio wanunuzi wa mwisho.

Ni ukweli kuwa wafanyabiashara huwa wanapiga gharama zote hizi mnazochomekewa na kumtwishwa Mtanzania masikini.

Kwa nini baadhi ya watu wenye uchu wa fedha wametumia mgongo wa serekali kwa kushirikiana na TBS kufanya wizi ulio wazi na serekali imebaki kimya ikingalia tu?

Watanzania tumekuwa wavumilivu kupita kiasi ila sasa tuungane na kusema YATOSHA tumekuwa tukulipishwa kodi ya vehicle inspection mara mbili. Gari inapoingia Tanzania hata kama imekaguliwa huko itokako bado unalipa vehicle inspection, hii ni ya nini? 

Ushuru wa magari imepanda mpaka kufika 180 percent.

Iko wazi dunia nzima kupitia mitandao ya kuuza magari kuna gari mpaka ya dollar $100-200
lakini cha kushangaza ni mipango ya ushuru mkubwa unaotozwa na TRA bila hata kufikiria kuwa tunazidi kuweka matabaka ya walio nacho na wasiyo nacho.

Watu wengi akili zao zipo katika matumbo yao na familia zao tu bila kujua vita zote zinazotokea Duniani zinatokana na matabaka yaliyopo katika jamii.

Ushuru ulipo sasa wa magari unatisha na unatia aibu kwa watu wenye akili timamu. Kwa mfano Fusso Truck inayofika tanzania kwa CIF dollar $14,000 kwa exchange rate 1,800Tsh sawa 25,200,000 Tanzania sh, ushuru wake milioni 22,000,000 Tsh mpaka 24,000,000 Tsh
sasa jiulize ushuru huu unatoka wapi? Gari inayofika milioni 49Tsh mwanchi mkulima atainunu kwa kiasi gani?

Gari ndogo za dollar $2,000$ Cif =1,800 = 3,600,000Tsh ushuru wake ni milion 4,800,000Tsh. Kweli bila kuwa wakweli tutazidi kuteswa na serikali yetu wenyewe.

Tunakwenda wapi? Hii ndiyo Tanzania tuliyoachiwa na Mwalimu ya kunufaisha mabwenyenye na kuwatesa wananchi?

BASKELI

Tukirejea katika swala la baskeli hakuna asiye jua baskeli ni chombo kinachotumika na wanafunzi kwendea shule na wakulima kwendea mashamabani na baadhi ya Watanzania masikini kubebae bidhaa zao ndogondogo.

Ni chombo kisichotumia mafuta kusema inachafua mazingira (is a human-powered) hutumia jasho na damu ya mwendeshaji.

Ni ukweli usiofichika katika dunia nzima uchunguzi tuliofanya inaonyesha kuwa Tanzania ndiyo inchi pekee yenye ukaguzi wa baskeli tena kwa gharama kubwa inayofikia 800,000Tsh -1,000,000Tsh kwa kushirikiana na kampuni moja iliyopo Osaka, Japan Bureau Veritas ambayo imeanzishwa 1828 ambayo makao makuu yake ni huko Neuilly-sur-seine Paris, France.

Serikali iwe na huruma na wananchi wake kwa kuwapunguzia gharama kwa kuwa ukaguzi wa baskeli hauna tija yoyote zaidi ya kuwanyonya na kuwabana raia tu.

Huwezi kukagua baskeli ambazo huingizwa katika container pisi 400 mpaka 500 kwa kulalishwa. Inabidi wakati mwingine tukubali ukweli ili kusaidi wanachi masikini wa Tanzania na tuache sera za UMIMI na tutangaze sera za UMOJA.

Bakeli unayonunua kwa dollar $2-3 sawa na shiling 3,600Tsh hapo mwanzo tulikuwa tukilipa ushuru wa container 3,600,000Tsh, lakini sasa ushuru umefika milioni 9Tsh. Baskeli kutoka shilingi 40,000Tsh sasa mwanachi inambidi anunue kwa Sh 80,000Tsh kutokana na serikali kuweka ukaguzi na kuongeza ushuru maradufu.

Wananchi wa Tanzania wanabeba mzigo mzito kutoka katika serikali yao wenyewe. Tunaomba sana hatua za haraka zichukuliwe kuokoa Tanzania inayoangamia kwa tamaa ya viongozi wachache.

---

Tanzania Children's Project yafanya harambee Maryland, MarekaniBalozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akihudhuria harambee ya Tanzania Children's Project inayoshughulisha na miradi ya afya na elimu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland. Kulia ni Timothy Lynch ambaye ni Rais wa NGO hiyo, Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliongozana na Afisa wa Ubalozi Switebert Mkama(pichani kushoto)Rais wa Tanzania Children's Project Bwn. Timothy Lynch katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.Wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya Tanzania Children's Project iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland nchini Marekani.picha ya pamojaPicha ya pamojaKikundi cha muziki kikitoa burudani.

How to automatically post to Twitter, Facebook from BloggerIf-This-Then-That (IFTTT) service is the easiest way to integrate Blogger and Twitter, Facebook or any other social media.

  1. Click here to go to IFTTT
  2. Login or Create an account
  3. Click on the icon which says, "Create a Recipe" then follow the few steps to verify your blog and social networks that you want to share posts with your audience.

Note: 

You have 3 options on how you want to share your posts on Facebook that is at a Personal profile, Facebook Groups and Facebook Pages (see the image below), make a right selection. If you want to post on all three, you will have to create a recipe for each.


Taarifa ya CHADEMA kuhusu UKAWA kugawana majimbo

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UKAWA KUGAWANA MAJIMBO


Tangu jana kumekuwa na taarifa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari kuhusu msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya ubunge kwenye majimbo ya uchaguzi nchini.

Habari hizo ambazo zingine zimeripotiwa kwenye vyombo vya habari hususan magazeti ya jana (Alhamis) na leo (Ijumaa), zimesema kuwa UKAWA ‘wameshagawana’ majimbo kadha wa kadha na kwamba bado kuna ubishano katika baadhi ya majimbo kutafuta mwafaka wa kufikia lengo la kuwa na mgombea mmoja badala ya kila chama kuweka mgombea wake.

Tunapenda kutoa ufafanuzi juu ya habari hizo ambazo kwa namna moja ama nyingine zimesababisha usumbufu usio wa lazima kwa wafuasi, wapenzi, wanachama na viongozi wa CHADEMA na wanachama wa vyama vingine vinavyounda UKAWA.

CHADEMA kama walivyo washirika wenza wa UKAWA, kiko kwenye mazungumzo vyama vingine katika umoja huo ili kuhakikisha lengo la kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaohusisha nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge na urais, linafikiwa.

Mazungumzo bado yanaendelea vizuri. Hayajafikia tamati. Hivyo taarifa hizo ambazo zimeendelea kusambaa kwamba UKAWA ‘wameachiana au kugawana majimbo’ na kwamba kuna maeneo tayari yamepewa chama fulani na maeneo mengine mwafaka haujafikiwa, si rasmi wala si sahihi.

Kwa uzito wa hatua hiyo, mazungumzo yakikamilika na makubaliano kufikiwa, viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA, kikiwemo CHADEMA, watatoa taarifa rasmi na sahihi kwa umma wa Watanzania ili Watanzania waelewe kwa ukamilifu uamuzi huo.

Wafuasi, wapenzi, wanachama na viongozi wa CHADEMA wanaendelea kufanya kazi za ujenzi na uimarishaji wa chama katika kila eneo kadri ya maagizo ya vikao vya chama, hususan kupitia program endelevu ya CHADEMA ni Msingi, operesheni mbalimbali mf; kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, n.k.

Katika shughuli za uenezi na uimarishaji wa CHADEMA, kwa kadri ya maagizo ya chama, viongozi waendelee kusimamia misingi ya ushirikiano wa UKAWA kwa ajili ya matumaini na haki za Watanzania ambao wanajiandaa kutimiza kiu yao ya kufanya mabadiliko kwa kuiondoa CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Imetolewa leo Ijumaa, Machi 20, 2014 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

[update] Zitto aonekana ACT

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe akinzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania, katika mkutano uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.

Maelezo ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kufuatia Kung’atuka Ubunge na Kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo


Jumapili, 22 Machi 2015, Serena Hoteli, Dar es Salaam

Ndugu Waandishi wa habari, wanachama na wapenzi wa ACT-Wazalendo na wote mliohudhuria mkutano huu,

Kama mnavyojua siku ya Ijumaa tarehe 19 Machi 2015 ilikuwa siku yangu ya mwisho kuhudhuria bunge la kumi linaloendelea Mjini Dodoma. Baada ya kung’atuka ubunge kufuatia kukoma uanachama wangu wa chama nilichotumia kuingia Bungeni, wengi mliniuliza ‘what is next?’

Sasa ninapenda kuwataarifu, kama ambavyo baadhi yenu tayari mnajua, kwamba jana siku ya Jumamosi tarehe 20 Machi 2015 nilijiunga rasmi na Chama cha ACT - Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Mwenyekti wa Tawi la Tegeta. Hii ilikuwa ni moja kati ya siku muhimu kabisa katika maisha yangu ya kisiasa. Na kwa leo kwa kweli nisingependa nizungumzie mgogoro uliokuwepo kati yangu na viongozi wangu wa chama cha zamani wala kile kilichotokea Bungeni. Hayo yote mnayajua, yameandikwa sana na yameshapita. Sasa ni wakati wa kusonga mbele. Rais Kwame Nkrumah alipata kusema "forward ever, backward never". Na kama nilivyosema Bungeni, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Kwa hiyo leo nitazungumzia uanachama wangu katika chama changu kipya cha ACT - Wazalendo.

Tuna vyama 22 kwa sasa. Na kwa kweli wengi watakuwa wanajiuliza kwa nini nijiunge na chama kipya ambacho kimeanzishwa juzi tu na ambacho pengine wanachama wake bado wanajaa katika kiganja cha mkono?

Nimejiunga na ACT kwa sababu ninaona kwamba huku ndiko kunakoendana na kile ambacho mimi nimekipigania kwa miaka yote tangu nianze siasa, ambacho ni kuweka mbele maslahi ya Taifa dhidi ya kitu kingine chochote. Kwa kifupi nimepigania uzalendo kwa nchi yangu na huu ndiyo msingi mama wa Chama cha ACT - Wazalendo.

Kama mnavyojua mimi ni mjamaa na ninaamini katika misingi ambayo Mwalimu Nyerere aliisimamia. ACT-Wazalendo ni chama pekee nchini kinachokubaliana na Itikadi ya ujamaa na kinaamini katika Falsafa ya Unyerere ikiwa na lengo la kuirudisha nchi katika misingi iliyoasisi taifa. Ninajiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ni chama kinachoamini katika msingi wa uadilifu na kimeweka miiko na maadili ya viongozi katika kuhakikisha kwamba viongozi wote wa ACT-Wazalendo wanakubaliana nayo kwa kusaini. Naamini kuwa na miiko na maadili kwa viongozi ni mwanzo wa kuhakikisha kwamba jamii yetu inaishi katika uadilifu na kwamba viongozi wanakuwa mfano wa uadilifu katika jamii. Uadilifu ni nguzo muhimu katika kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji nchini kwetu.

Mtakumbuka kwamba katika miaka yangu yote ya ubunge nimepigania uwajibikaji na uwazi. Hii ni misingi ambayo ninaamini kwamba ni moyo wa utumishi wa umma. Nimefurahi kwamba kati ya misingi kumi ya ACT-Wazalendo, uwajibikaji na uwazi ni sehemu muhimu kabisa ya misingi hiyo. Uwazi ni sehemu ya jina la chama hiki. Yote haya yamenifanya nione kwamba sitojiona mgeni katika chama hiki. Huku ndiko nyumbani kwangu kisiasa na katika utumishi wa umma.

Nimejiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ninakubaliana na imani yao kwamba Kujitegemea, bidii, umakini na weledi katika kazi ndiyo msingi wa maendeleo. Hakuna namna nchi yetu na wananchi watapiga hatua ya kimaendeleo bila sisi sote kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia umakini na weledi. Ninakubaliana na ACT-Wazalendo kwamba raslimali za Taifa lazima zitumike kuondosha umaskini wa watu wetu. Ninajiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ninakubaliana na imani yao kwamba Umoja ni ngao muhimu katika ujenzi wa taifa letu na Afrika kwa ujumla. Lazima tuirudishe nchi yetu katika misingi iliyoasisi taifa hili. Lazima tuirudishe nchi yetu katika heshima na uongozi wa bara hili la Afrika.

Ninaahidi kufanya kazi na vijana, wanawake, wanaume na watu wote wanaoamini katika siasa safi na siasa za hoja. Tunataka tufungue ukurasa mpya wa siasa hapa nchini. Siasa za masuala ya nchi yetu. Siasa za masuala ya vijana, wanawake, wazee, wakulima, wafanyakazi, wajasirialimali, wafanyabiashara na wote wanahangaika kuijenga nchi yetu na katika kuondoa umaskini. Tunataka tuzungumze namna bora ya kuendesha elimu, afya, hifadhi ya jamii, na ajira. Tunataka tujenga hoja mbadala kuhusu namna endelevu ya kujenga uchumi shirikishi ambapo kila mwananchi anajisikia sehemu yake.

Mwezi Oktoba mwaka 1966 Mwalimu Nyerere alipokea maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ikulu. Maandamano yale yalichochewa na kasi kubwa ya rushwa na maisha ya kifahari ya viongozi (wabenzi). Mwalimu alifoka kwa kuuliza “ Tunajenga nchi ya namna gani”? Hatimaye Azimio la Arusha likatangazwa.

Chama hiki kipya kimeanzishwa katika mazingira yale yale ya mwaka 1966. Ni wakati wa kujiuliza na kupata majawabu ya aina ya nchi tunayojenga. Sisi ACT – Wazalendo tumeona jawabu ni kurudi kwenye misingi. Waingereza wanasema ‘back to the future’ Let the new beginning begin.

Ahsante sana kwa kunisikiliza.

Zitto Zubeir Kabwe
Dar es Salaam, 22 Machi 2015.Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiongea na wanahabari hivi sasa katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo. Wengine ni viongozi wa juu wa chama cha ACT alikohamia rasmi jana.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya yenye namba 007184 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam leo.

BAADA ya minong’ono ya muda mrefu hatimaye, Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.

Zitto aling’atuka Ubunge, Alhamisi iliyopita na jana kujiunga na ACT kupitia tawi la Tegeta Dar es salaam na kukabidhiwa kadi namba 007194.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Zitto aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema ameamua kujiunga na chama hicho ili kuendeleza mapambano ya demokrasia nchini kwa kuwa chama hicho ni wazalendo wa kweli.

Zitto alisema: “Nimejiunga na ACT kwa sababu ninaona huku ndiko kunakoendana na kile ambacho nimekipigania kwa miaka yote tangu nianze siasa, kuweka mbele maslahi ya Taifa dhidi ya kitu kingine chochote. Kwa kifupi nimepigania uzalendo kwa nchi yangu na huu ndiyo msingi mama wa Chama cha ACT – Wazalendo.

“Kama mnavyojua mimi ni mjamaa na ninaamini katika misingi ambayo Mwalimu Nyerere aliisimamia. ACT-Wazalendo ni chama pekee nchini kinachokubaliana na Itikadi ya ujamaa na kinaamini katika Falsafa ya Unyerere ikiwa na lengo la kuirudisha nchi katika misingi iliyoasisi taifa.

“Ninajiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ni chama kinachoamini katika msingi wa uadilifu na kimeweka miiko na maadili ya viongozi katika kuhakikisha kwamba viongozi wote wa ACT-Wazalendo wanakubaliana nayo kwa kusaini.

“Naamini kuwa na miiko na maadili kwa viongozi ni mwanzo wa kuhakikisha kwamba jamii yetu inaishi katika uadilifu na kwamba viongozi wanakuwa mfano wa uadilifu katika jamii. Uadilifu ni nguzo muhimu katika kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji nchini kwetu.

“Nimejiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ninakubaliana na imani yao kwamba Kujitegemea, bidii, umakini na weledi katika kazi ndiyo msingi wa maendeleo.

“Hakuna namna nchi yetu na wananchi watapiga hatua ya kimaendeleo bila sisi sote kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia umakini na weledi. Ninakubaliana na ACT-Wazalendo kwamba raslimali za Taifa lazima zitumike kuondosha umaskini wa watu wetu.

“Ninajiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ninakubaliana na imani yao kwamba Umoja ni ngao muhimu katika ujenzi wa taifa letu na Afrika kwa ujumla. Lazima tuirudishe nchi yetu katika misingi iliyoasisi taifa hili. Lazima tuirudishe nchi yetu katika heshima na uongozi wa bara hili la Afrika.

“Ninaahidi kufanya kazi na vijana, wanawake, wanaume na watu wote wanaoamini katika siasa safi na siasa za hoja. Tunataka tufungue ukurasa mpya wa siasa hapa nchini.

“Siasa za masuala ya nchi yetu. Siasa za masuala ya vijana, wanawake, wazee, wakulima, wafanyakazi, wajasirialimali, wafanyabiashara na wote wanahangaika kuijenga nchi yetu na katika kuondoa umaskini.

“Tunataka tuzungumze namna bora ya kuendesha elimu, afya, hifadhi ya jamii, na ajira. Tunataka tujenga hoja mbadala kuhusu namna endelevu ya kujenga uchumi shirikishi ambapo kila mwananchi anajisikia sehemu yake.”

Katika mkutano huo, naye msanii wa bongo fleva, Seleman Msindi aka ‘Afande Sele’ ametangaza kukihama Chadema na ACT Wazalendo.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Selemani Msindi "Afande Selle" akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kuungana na Mh. Zitto Kabwe kujiunga na chama ACT-Tanzania kutokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba na kushoto ni rafiki wa Afande Selle ambaye nae amejiunga na Chama hicho, Adam Shanzy.


Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba akimkabishi kadi ya uwanachama, Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Selemani Msindi "Afande Selle" ambaye amejiunga na chama hicho akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Sehemu ya Wanachama wa Chama ACT-Tanzania wakionyesha mabango ya kumkaribisha Mwanachama mwenzao ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe na Afande Sele na wanachama wengine wapya wakionesha kadi zao mpya ya ACT
Mhe. Zitto Kobwe akiwasili katika viwanja wa ofisi ya chama cha ACT tawi la Tegeta kwa ajili ya kujiunga rasmi na chama hicho. 

Kabwe akijaza fomu yake ya kujiunga na chama cha ACT alipowasili katika tawi la ACT Tegeta jana. ili kujiunga rasmin na chama hicho. 
Mhe Kabwe akilipa ada ya uanachama wakati alipofika katika ofisi za ACT Tawi la Tegeta kujiunga rasmi na chama hicho.
Mhe Kabwe akionesha kadi yake baada ya kukabidhiwa na Menyekiti wa tawi la chama cha ACT Tegeta. 


Mhe Kabwe akisaini fomu baada ya kukabidhiwa Kadi yake ya uanachama wa ACT tawi la Tegeta.

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe akisaini kitabu baada ya kupewa kadi ya C
ama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania, siku ya
Jumamosi ya Machi 21, 2015 nakupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yenye namba 007194.

Hili limetokea siku moja tu baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.Mhe Kabwe akitoka katika Ofisi za Chama cha ACT Tawi la Tegeta Mjini Dar-es-Salaama baada ya kufika kastika Tawi hilo kujiunga rasmin na ACT baada ya kungatuka CHADEMA hivi karibu na kujiuzulu Ubunge wa Kigoma


Mhe Kabwe akisalimiana na Wanachama wa cha cha ACT, baada ya kumaliza taratibu za kujiunga na chama hicho katika tawi la Tegeta na kukabidhiwa Kadi yake na Mwenyekiti wa tawi hilo

[audio] Aikande Kwayu's presentation at School of Oriental and African Studies regarding Tanzania Proposed Constitution

Below is a 14 minutes audio record of Dr Aikande Kwayu's presentation at the  School of Oriental and African Studies (SOAS) on February 28th, 2015.

The talk was about The New Constitution in Tanzania. 
The panel was chaired by Prof. Andrew Coulson (author of the book: Tanzania: Political Economy).

Maradhi yatokanayo na utajiri wa ghafla

Siku hizi mazungumzo yanayohusu pesa, mali na utajiri kwa ujumla, yamekuwa ni jambo la msingi linalopewa kipaumbele na kila mtu katika jamii yetu. Ingawa, tamaa ya kutaka kujitajirisha kwa vyovyote vile, imejengeka na kujizatiti ndani ya mioyo ya watu kiasi cha kutufanya kuwa kama watumwa vile. Mwelekeo huu wa kupenda na kutamani sana utajiri, umewafanya baadhi ya watu wavuke mipaka ya maadili mema na kuutafuta utajiri huo kwa njia za mkato, zisizo halali.

Nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja kipindi cha nyuma kidogo, baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza ya biashara katika chuo kimojawapo hapa nchini, aliweza kubahatika kuajiriwa na serikali katika idara moja iliyokuwa ikijihusisha na maduhuri ya serikali kutoka kwa wafanyabishara wadogo na hata kwa wale wakubwa. Katika muda wa miaka tu tokea aajiriwe, jamaa huyu aliweza kujitajirisha kwa kiwango kikubwa na cha kutisha sana.

Njia alizotumia katika kujitajirisha kwake bado inabaki kuwa siri yake. Lakini kwawatu wenye kujua kiwango chake cha mshahara na muda aliofanya kazi, hawakusita kusema kwamba, utajiri huo ulipatikana kwa njia za mkato mkato, ikiwa ni pamoja na kuibia serikali. Mara baada ya kuona kwamba ametajirika kiasi cha kuogofya, akawa sasa hata mwenyewe anaonekana kutokuamini, kutokana na wingi wa pesa alizokuwa nazo. Hivyo kutokana na hali hiyo, alianza kushitakiwa na dhamira yake.

Matokeo yake ni kwamba , alianza kuingiwa na hofu ya kuja kukamatwa na mwajiri wake. Hali hiyo iliendelea kumsumbua kwa muda mrefu. Katika hali kama hii aliendelea kusumbuliwa na maumivu makubwa ya kiakili na kihisia. Hivyo, ikawa kwamba, katika harakati za jamaa huyu kuondokana na maumivu hayo, aliamua kutafuta mwavuli wa kumpa nafuu. Ilibidi aanze ufujaji wa pesa hizo kwa kulewa kupita kiasi na ngono za hovyo.

Ilifika hatua ambapo jamaa huyu akawa anashindana na mkewe katika kuzichota fedha hizo kutoka sehemu walikokuwa wakizihifadhi ndani ya nyumba yao. Migogoro ya ugomvi kwenye ndoa yake likawa ni jambo la kawaida. Vilevile jamaa huyu akawa anawaalika jamaa zake aliomaliza nao masomo ya chuo kikuu, wakanywa na kufurahia maisha.

Alifanya hivyo, bila yeye mwenyewe kujua kwamba, ilikuwa ni jitihada yake ya kutibu majeraha ya hisia zake, kutokana na kushtakiwa na dhamira zake, kwa vitendo vyake vya ubadhirifu, rushwa na wizi wa fedhaza ofisi yake. Hata hivyo, tiba hiyo haikufua dafu kwani hatimaye jamaa huyu aliamua kuacha kazi yeye mwenyewe kwa hofu ya kudakwa na mwajiri wake.

Wataalamu wengi wa afya ya akili wanadai kwamba mtu anapopata utajiri wa ghafla huwa ni ngumu sana kwake kuweza kukabiliana nao huo utajiri wa ghafla. Wataalamu huweza kuongeza kuwa utajiri huo huweza kusababisha familia kuvunjika na kuharibu kabisa maisha yao. Na kwamba fedha hizo, zinakuwa haziwaletei tena amani, uraha na hata kuridhika kama walivyokuwa wakifikiri mwanzo.

Vilevile kulingana na maoni ya wataalamu mbalimbali wa masuala yahusuyo afya ya akili, wanaendelea kudai kuwa watu wengi ambao hupata utajiri huu wa ghafla na wa kupindukia mara nyingi huwa ni watu wa kuugua maradhi ambayo yamepewa jina la maradhi ya utajiri wa ghafla, ambayo huwa yana dalili kama vile: Kushtuka moyo sana, hofu za ghafla na ya mara kwa mara, kukosa usingizi, kukosa amani na kuhisi kuwa na hatia kwa sababu ya kuwa na pesa nyingi kupindukia ambazo tena ukiangalia sio za halali. Pia, kuhisi kwamba hawastahili kuwa na pesa au utajiri mkubwa wa kiasi hicho. Watu wengi wenye utajiri mkubwa na wa ghafla ndivyo walivyo na wanaishi na maradhi ya utajiri wa ghafla, ingawa sio rahisi sana kubaini na hawawezi pia kukwambia.

Hivyo, ni vizuri tukawa na mtazamo chanya na unaofaa kuelekea kwenye utajiri tunaoutaka na kuumiliki baada ya kufanya kazi halali tena pengine muda mrefu, ni sehemu tu ya jitihada za kujipatia mafanikio ya kweli. Kwani mafanikio haya yanatutaka tuutumie utajiri huo vizuri. Kutumia utajiri huo vizuri ni pamoja na kuutumia katika kuwatendea mema watu wengine, kuutumia katika kazi na miradi mbalimbali ya kijamii.

Kwa kufanya hivyo, ni wazi kabisa tutakuwa tumeigundua na kuipata siri au tiba itakayoweza kutusaidia katika kuepukana na mashtaka hata hukumu itokanayo na utajiri wa haraka haraka.

IMANI NGWANGWALU

[audio] Lowasa asema, "Mashehe wa Bagamoyo mmenishawishi kugombea Urais 2015"MASHEKHE wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania Urais 2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia kwenye picha juu) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.

Msikilize kwenye audio iliyopachikwa hapa...Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.

Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.

"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu," alisema.

Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.

Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Mashekhe kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Shekhe Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya.MASHEKHE hao wakiwasili nyumbani hapo kwaajili ya mazungumzo na Lowassa.Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasikiliza viongozi wa msafara huo.Edward Lowassa akizungumza na Mashekhe hao mjini Dodoma.

Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlingotini, Kaole, Chalinze, Lugoba, Msata na kwingineko.

Duaa ilisomwa na viongozi hao wa dini.Edward Lowassa akiwasindikiza viongozi hao.Lowassa akiagana na Sheikh Alli Mtumwa mmoja wa viongozi wa msafara huo.Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiagana na viongozi hao.Lowassa akimsikiliza mmoja wa Mashekhe hao.


  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Mroki Mroki/Father Kidevu blog.

Huko China, wapenzi wa Wu Hsia wamejitupa mtoni, afanyeje?


Mwanaume mmoja alijikuta katika wakati mgumu baada ya mpenzi wake wa sasa na aliyeachana naye kujitosa mtoni.

Wu Hsia, 20 aliachana na msichana wake wa awali, Jun Tang, 20 baada ya kumpata mpenzi wake mpya, Rong Tsao mwenye umri wa miaka 22.

Baada ya kupita miezi mitatu, Jun akaanza kufanya jitihada za kumpata tena mvulana wake. Wu akasema "nimechoka kuchanganywa na wasichana," akaamua kupanga wakutane wote watatu ili waamue abaki na nani. Lakini hali ilikua tete walipokutana mjii Ningbo, Mashariki mwa jimbo la Zhejiang ili kujadili suala hilo.

Msemaji wa polisi alieleza kuwa wasichana hao walianza kubishana na Jun akahisi kutukanwa na Rong hivyo akachukua uamuzi wa kujitosa mtoni na kuanza kumpigia kelele Wu amuokoe.

Rong alipoona hivyo, na yeye akajitosa mtoni kisha wote wakaanza kupiga kelele wakitaka msaada wa kuokolewa na Wu huku wakitaka kuona nani ataanza kuokolewa.