Mansour atangaza nia ya kuwania uwakilishi Kiembesamaki


Aliyewahi kuwa Waziri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mansour Himid Yussuf, ametangaza kujitosa katika kinyang’anyiro cha Uwakilishi katika jimbo la Kiembesamaki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Atachukua fomu ya kuwania jimbo hilo kupitia CUF.

Mansour ambaye alifukuzwa uanachama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Agosti 26 mwaka huu, baadaye alitangaza kujiunga na CUF.

Akituhubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Bustanini, Kiembesamaki, alisema tayari amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo na ameirejesha.

Mwanasiasa huyo alitumia mkutano huo kuwaomba radhi kwa matendo aliyokuwa akiyaona wakitendewa Wazanzibari, yakiwamo kupigwa na kudhalilishwa na Serikali wakati wote akiwa ndani ya Serikali.

Akizungumzia safari yake ya kujiunga na CUF, Mansour alisema haikuwa rahisi kwake kwani wazee wa Kiembesamaki na wananchi waliamini amekwisha katika siasa.

“Mlilia sana, niliwaambia tulieni wakati bado…milinifariji katika safari yangu ya kujiunga CUF, pamoja na ugumu uliopo lazima niseme ukweli, mlikuwa na wasiwasi kwamba baada ya mimi kwenda jela labda sitogombea.

“Mliona nilikuwa taabani na nawapa pole wale wote waliopata misukosuko kama yangu, wazee walikuwa na wasiwasi labda sitogombea lakini sasa nasema wazi sitorudi nyuma,” alisema Mnsour.

Mansour alisema katika harakati zake za kuwania uwakilishi katika jimbo hilo ataomba kura hata katika matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani ni yeye ndiye aliyejenga matawi hayo.

“Sitoogopa kuingia katika tawi lolote la CCM kuomba kura, yote nimejenga mwenyewe, nitakwenda humo humo, hizi ndiyo siasa za CUF za leo, CCM na CUF wote wangu,” alisema Mansour.

Mansour alisema hajuti kufukuzwa kwake CCM wala hawezi kumnunia mtu yeyote lakini akasisitiza ataendelea kuwaheshimu kwa vile ni chama chao.

Alisema mwaka 2010 yalipokuwapo mazungumzo ya maridhiano aliwaambia wananchi wa Kiembesamaki umuhimu wa maridhiano hayo katika kujenga jamii iliyotulia Zanzibar.

Alisema ingawa wawakilishi wengi walipinga ndani ya Baraza la Wawakilishi lakini hakutetereka kwa kuwa aliamini lengo la maridhiano haikuwa ni kumtengenezea Seif nafasi ya uongozi au mawaziri saba kutoka CUF.

“Maalim hana njaa, mawaziri hawana njaa, lengo ni kuleta utulivu, Maalim anaumwa na siasa hizi za ufisadi, lengo ni kuondoa chuki na kujenga historia mpya na kujenga vyombo vya Serikali vinavyowajibika kwa dola,” alisema Mansour.

Katika mkutano huo, Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Seif Sharif Hamad aliwataka viongozi wa Jeshi la Polisi Zanzibar kusoma sheria ya vyama vya siasa na kuacha kuiburuza CUF.

Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, alilazimika kutoa ushauri huo baada ya kile kinachodaiwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mjini kuuzuia mkutano kwa sababu zisizoeleweka.

Alisema CUF haitaweza kuendelea kuvumilia uonevu unaofanywa na jeshi hilo kwa kuzuia mikutano yao kwa sababu chama hicho kina haki sawa katika serikali ya umoja wa taifa kama ilivyo CCM.

Akizungumzia hatua ya Mansour, Seif alisema Mansour ndiye mgombea sahihi wa Kiembesamaki kwa Chama cha Wananchi (CUF).

  • SARAH MOSSI na IS-HAKA HASSAN, ZANZIBAR via gazeti la Mtanzania

Polisi yapiga marufuku wimbo wa CHADEMA

Call for proposals - Saving Lives at Birth: A Grand Challenge for Development

USAID, the Government of Norway, the Bill & Melinda Gates Foundation, Grand Challenges Canada and DFID
Saving Lives at Birth: A Grand Challenge for development

USAID, the Government of Norway, the Bill & Melinda Gates Foundation, Grand Challenges Canada, and DFID have joined together to launch Saving Lives at Birth: A Grand Challenge for Development, to find the tools and approaches to help the mothers and newborns during their most vulnerable hours.

Types of Awards: We will invest in a portfolio of projects. Through this portfolio, we will seek ground breaking innovations by providing:
  • Seed Funds to support the development and validation of ideas capable of impacting health outcomes for pregnant women and their babies in low-resource settings,
  • Validation Funds to introduce and validate the effectiveness of innovations to reach proof-of-concept, and
  • Transition to Scale Funds to develop, refine, and rigorously test the impact of integrated solutions that have previously measured promising health outcomes in a controlled or limited setting and have the potential to credibly scale to improve the lives of millions of pregnant women and newborns in multiple countries. Transition funding is limited to integrated solutions that unite technology, service delivery, and demand.

Further information available at: www.savinglivesatbirth.net/apply

WHO Special Programme for Research and Training in Tropical Diseases

2015 Short-term training grants for research capacity strengthening and knowledge management

This short-term training grant scheme is designed to help health researchers or research teams contribute more effectively to disease control through implementation research, in line with TDR’s strategy. This is the third round of the TDR grant scheme conducted in 2013 and 2014 as the impact grant scheme. The focus of this round is on support for research training. Application from previous TDR grantees and from women are encouraged.

Applicants must:
  • Be citizens from a low-and-middle-income country (LMIC) and resident there
  • Have been employed by a governmental or non-governmental organization for at least 12 months by the submission deadline
  • Be able to complete the training within 12months of the start of the grant
  • Provide a clear training plan
  • Be endorsed by the head of the home institution

Cost: Each grant will be up to a maximum of US$ 50 000.

Application deadline: April 12, 2015

Further information and examples of eligible activities can be found at: www.who.int/tdr/grants/en

Mavazi 'yaliyotokelezea' katika zulia jekundu Siku ya Wanawake, ZanzibarZifuatazo ni picha za matukio mbalimbali kwenye red carpet wakati wa sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani iliyowakutanisha wanawake kutoka kila kona ya visiwani Zanzibar ambayo iliandaliwa na Kikundi cha Wanawake cha Zanzibalicious na kufanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Bwawani.

Picha na taarifa hii tumeshirikishwa na Zainul Mzige
Wanaume nao hawakubaki nyuma kutoa sapoti kwa wanawake.


Mbunifu wa mavazi kutoka bara Mama wa mitindo Asia Idarous (kushoto) akipozi na mbunifu wa mavazi kutoka visiwani Zanzibar Matilda Ishungisa wa Malty design.Makamu mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious, Zaning'ha Otembo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson.
Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Thuwaiba Kisasi.


Mama wa mitindo Asia Idarous aking'ara kwenye red carpet.Kutoka kushoto ni Make up artist Sada, Mama wa mitindo Asia Idarous na MC wa sherehe ya siku ya wanawake duniani visiwani Zanzibar, Mishi Bomba ambaye pia ni mtangazaji wa Magic FM.
Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo (kulia) akiwa na Mama wa mitindo Asia Idarous. 

Pres. Kikwete meets Ms. Baroness Lindsay Northover

President Jakaya Mrisho Kikwete escorts Ms. Baroness Lindsay Northover, UK's Parliamentary Under-Secretary of State for International Development after holding talks with her at the State House . Behing them is the British High Commissioner to Tanzania Ambassador Diana Melrose

President Jakaya Mrisho Kikwete and Ms. Baroness Lindsay Northover, UK's Parliamentary Under-Secretary of State for International Development pose for a souvenir photo taken by the British High Commissioner to Tanzania Ambassador Diana Melrose and another official after holding talks with at the State House

President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Ms. Baroness Lindsay Northover, UK's Parliamentary Under-Secretary of State for International Development after holding talks with her at the State House Monday March 23, 2015. Behing them is the British High Commissioner to Tanzania Ambassador Diana Melrose.

PHOTO BY STATE HOUSE

Baada ya Zitto kuondoka, Mwidau ashika usukani PAC

Amina Mwidau
Amina Mwidau

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Amina Mwidau amerithi mikoba ya aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Kabla ya kujiuzulu ubunge Ijumaa iliyopita, Zitto alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana, uchaguzi huo ulifanyika jana mchana katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha habari, kimesema nafasi hiyo iligombewa na mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Lucy Owenya ambaye aliambulia kura mbili kati ya 17 zilizopigwa katika uchaguzi huo.

Amina aliibuka mshindi baada ya kuzoa kura 15 katika uchaguzi huo.

Wajumbe ambao hawakuwapo kwenye uchaguzi huo ni wabunge wa Viti maalumu, Easter Matiku (CHADEMA) na Catherine Magige (CCM) na Mbunge wa Magogoni, Kombo Khamis Kombo.

Alipoulizwa kuhusu uchaguzi huo, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema hana taarifa za kufanyika kwa uchaguzi huo.

“Hata sijui kama kuna uchaguzi umefanyika leo wa kamati yoyote,”
alisema Joel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge.

Akizungumza na gazeti hili jana jioni, Amina alisema ataendeleza pale alipoishia Zitto na Watanzania wategemee uwazi zaidi katika utekelezaji wa kazi za kamati hiyo.

“Kamati hii ina action plan (mpango kazi) ambao imepanga kuufanyia kazi, kwa hiyo nitaangalia pale alipoishia Zitto na mimi nitaendeleza,”
alisema Amina.

Alipoulizwa kuhusu changamoto, alisema kazi itakuwa rahisi kutokana na ushirikiano na umoja walionao wajumbe wa kamati hiyo.

“Sisi katika kamati tulikuwa wapinzani watano tu wengine wote ni kutoka CCM, lakini kwa ushirikiano na umoja tulioujenga ndani ya kamati, wakati mwingine huwa tunasahau kabisa kama tunatoka kama vyama tofauti, naahidi kuendeleza na kuusimamia umoja huo,” 
alisema Amina.

via gazeti la MWANANCHI

Ruhusuni wanaume kuingia wodi za uzazi - Naibu WaziriNAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.

Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.

Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki.

Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha maelezo kazi zinazofanywa na taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.
(picha:  Zainul Mzige/modewjiblog)

Aidha ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.

Alisema pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi wa watoto njiti.

Alisema kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.

Awali wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto njiti waweze kuendelea kuishi.

Wakati huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema kwamba yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 alisema zaidi ya watoto 200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.

Alisema wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka hospitalini.

Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa.

Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.Muuguzi wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akielezea makuzi yake baada ya kuzaliwa njiti wa uzito wa kilio 1.2 na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.

Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimpongeza Balozi Mwanaidi Sinare kwa risala nzuri aliyoitoa wakati wa sherehe za uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mwishoni mwa wiki jijini Dar. Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza na kumpongeza Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.Meza kuu wakijianda kuelekea sehemu maalum ya kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel na mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba kwa pamoja wakikata utepe kuzindua taasisi yao huku Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Balozi Mwanaidi Sinare wakishuhudia tukio hilo.Sasa imezinduliwa rasmi.

Balozi Mwanaidi Sinare (kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel kwenye uzinduzi huo.Sehemu ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.Meza kuu kwa pamoja wakikata cake maalum wakati wa uzinduzi huo.Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi.Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Balozi Mwanaidi Sinare.Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Muuguzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda (kushoto).Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba.

Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mama yake mzazi Celina Mollel.Rachel Temu, William Malecela pamoja na mdau wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo (kulia) Mdau wa Doris Mollel Foundation, Suleiman Saleh pamoja mgeni mwalikwa.Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi (kulia).Mtangazaji wa kituo cha Channel Ten na Magic FM, Salma Msangi na rafiki yake wakati wa uzinduzi huo.Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo Leo, Juma Pinto (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Benny Kisaka (wa pili kulia) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo.Mama mzazi wa Doris Mollel , Bi. Celina Mollel (kushoto) katika picha ya pamoja na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Ramesh Patel.Mjasiriamali Maznat Yusuph Sinare (aliyesimama katikati) akiteta jambo na Balozi Mwanaidi Sinare (kulia) kwenye sherehe fupi za uzinduzi wa Doris Mollel Foundation.Balozi Mwanaidi Sinare akisalimiana na Mh. Iddi Simba (aliyeipa mgongo kamera yetu) Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kushoto) Balozi Mwanaidi Sinare pamoja na mshirika mwenza wa taasisi ya Doris Mollel, Heena Mujtaba.Pichani juu na chini ni Doris Mollel na familia yake akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi wa taasisi yake.Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Rafiki wa Doris Mollel ambaye ni Mlemavu Sophia.Kutoka kushoto ni Msanii wa filamu nchini, Sinta, Hoyce Temu pamoja na Rachel Temu wakipiga picha kumbukumbu mara baada ya uzinduzi huo kufikia tamati.Doris Mollel na Sintah.Mdau Chiku Lweno (kulia) akipozi na Doris Mollel pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.