[video] Rais Kikwete alipokanyaga mitaa ya Buguruni Kwa Mnyamani kukagua walioathiriwa na mvuaZiara hii ilifanyika huko Buguruni Kwa Mnyamani, wilayani Ilala, Dar es salaam siku ya Jumanne, Machi 24, 2015

Mapitio ya magazeti kwenye Tv mbalimbali Machi 25, 2015


Tahadhari ya Wizara kuhusu utapeli wa Ajira ya Walimu wapya 2015/16

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2015/16JIHADHARI NA MATAPELI


Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.

Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.

Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
24 Machi, 2015

[video] Wabunge wapendekeza kifo ili kudhibiti dawa za kulevyaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama amesoma Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya wa mwaka 2014 kwa mara pili Bungeni Mjini Dodoma tarehe 24.03.2015.

Mhe.Mhagama alisema kupitia Muswada huu Serikali itaunda chombo kitakachosimamia na kudhibiti biashara ya Madawa ya Kulevya pamoja na kuanzisha vituo vitakavyo toa tiba kwa waathirika wa madawa ya kulevya.

“Sehemu ya sita ya Muswada huu unahusu uanzishwaji wa Mfuko wa Udhibiti wa Kupambana na madawa ya kulevya na na pia sehemu tano inahusu kufilisi mali wafanyabiashara za madawa ya kulevya pale wanapitiwa hatiani,hivyo basi sheria hii itaipa meno Mamlaka itakayoundwa kwa ajili ya kupambana nawafanya biashara wa Madawa ya Kulevya pamoja na wahusika wote wanajihusisha na madawa ya kulevya,ikiwa ni pamoja na ujazaji wa fomu kwa watuhumiwa watakao kamatwa katika biashara hizo,”
alisema Mhe.Mhagama.

Kwa upande wa maoni ya kambi ya Upinzani inayoshughulikia masuala ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) yaliyosomwa na Mhe. Rajab Mbarouk alisema kambi ya Upinzani inaishauri Serikali kwa ujumla katika vifungu vyake mbalimbali vinavotoa adhabu ya faini viondolewa na badala yake iwe ni kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa.

Kwa upande wa uchangia wa maoni kutoka kwa wabunge juu ya muswada huo Mhe. Kangi Lugola (Mb, CCM) aliishauri Serikali kutoa hukumu kwa watakaokamatwa na madawa papo kwa papo kwa mfano mtu alinayekamatwa na madawa ya kulevya akiwa ameyameza au kuyabeba. Pia alisisitiza kwa kuiomba Serikali iondoe suala la faini na badala yake iwe ni kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa.

Aidha, Mhe. David Silinde (Mb) alitoa maoni kwa Serikali kwa kuiomba Sheria hii ionyeshe ni namna gani itadhibiti suala la usafirisha wa madawa ya kulevya katika mipaka yote ya nchi, vilevile Serikali ifikirie juu kuanzisha mahakama maalum zitakazo shughulikia kesi za madawa ya kulevya. Pia alipendeza bunge kuwa msimamizi wa utekelezwaji wa hukumu kwa kesi za madawa ya kulevya na adhabu iwe imetekelezwa angalau ndani ya wiki mbili.

Katika maoni kutoka kwa wabunge mbalimbali walisema wanaiomba Serikali kuwa Muswada huu uangalie ni namna gani utalinda haki ya mtu kutoa siri ya mtu atakayetoa taarifa za wafanyabiashara wa Madawa ya Kulevya nchini.
  • Taarifa ya Anitha Jonas - Dodoma via Blogu ya Serikali

2-day finance workshop for non-finance Managers in DarJoin our 2-day workshop to acquire greater confidence and working knowledge of important finance concepts.

When: 29th & 30th April, 2015, Where: The Colosseum, DSM For further details and registration, visit www.peoplepower.co.tz (click on 'Finance for Non Finance Managers') or call us on +255-752-124-124

MO Dewji Foundation yampa baikeli kijana aliyepooza

Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald Mgesi David akimkabidhi rasmi kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila siku

Andrew Chale/Modewji blog

Taasisi ya MO DEWJI FOUNDATION inayojishughulisha na miradi ya kusaidia jamii Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo Afya, elimu na maji mwishoni mwa wiki imeweza kumpatia kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila siku.

Tukio hilo la makabidhiano limefanyika katika ofisi za Mo Dewji Foundation jijini Dar es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald Mgesi David alikabidhi msaada huo kwa kijana Paulo Ezekieli

Akizungumza na Modewjiblog, Mtendaji mkuu wa Mo Dewji Foundation amesema, waliguswa na usumbufu aliokuwa anaupata kijana na hivyo kuona ni vyema kumsaidia ili aweze kumudu kuendesha shughuli zake za kila siku.

Mo Dewji Foundation imejikita katika kutekeleza miradi ya kijamii ambayo inalenga kusaidia jamii ya kitanzania katika kujikwamua katika hali ya umaskini na kuinua kipato.

Kwa upande wake, kijana Paulo Ezekiel ambaye muda mfupi baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo, alifanya mahojiano maalum na mtandao huu ambapo alieza kuwa, tatizohilo la kulemaa mguu, lilimtokea ghafla wakati yupo mitaa ya Kariakoo kwenye shughuli zake binafsi.

“Nakumbuka nilikuwa kwenye matembezi maeneo ya Kariakoo, ghafla nilipata kuhisi hali ya kupooza mguu mmoja wa kulia na kupoteza nguvu wasamaria wema waliniokota na kunipeleka Muhimbili” anaeleza Paulo Ezekiel.

Alieleza kuwa, alikaa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa muda wa miezi sita huku akipatiwa matibabu na baadae aliruhusiwa.

“Niliporuhusiwa hali ilikuwa ngumu sana. Kwani nilianza kuomba omba kwa watu msaada ikiwemo kifaa cha kuniwezesha kunisaidia kutembelea. Kule Muhimbili nilikuwa natumia baiskeli kutembelea hivyo nilivyoruhusiwa iliniwia vigumu sana kutumia vifaa vya ulemavu ikiwemo haya magongo.
Kuna siku katika kuomba omba. Nilikutana na mtu mmoja ambaye alinielekeza kwa Mh. Dewji. Nilipofika kwake msaidizi wake alinitaka nifuatilia kuona kama watafanikisha kwani tayari bajeti ilikuwa imeshafungwa hadi kipindi kingine” alieleza Paulo Ezekiel.


Mwandishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale (kushoto) akifanya mahojiano na Paulo Ezekiel mara baada ya kukabidhi msaada wa baiskeli ya magudumu matatu.
Hata hivyo Paulo Ezekiel alibainisha kuwa, wakati yupo nyumbani kwao, alipigiwa simu juu ya kuitwa kukabidhiwa baiskeli hiyo.

“Sikuamini kama ningeweza kupata msaada huu. Hadi nilipofika hapa kukabidhiwa namshukuru Mungu pia namuombea kwa Mungu Mh. Mohammed Dewji kwa msaada wake, kwani simjui na wala hanijui..Ilikuwa ni kama bahati kufika katika ofisi yake na kuomba msaada huu asante sana na namuombea maisha marefu Dewji na familia yake, wafanyakazi wake wote popote pale kwani kuniwezesha mimi ni ubinadamu mkubwa sana” alimalizia kijana Paulo Ezekiel.

Paulo Ezekiel anabainisha kuwa, ilikua vigumu sana kwa yeye kutembelea magongo siku za mwanzoni ambapo anasema hakuwahi kutegemea kama siku moja atakuja kuwa mlemavu.

“Hujafa, hujaumbika naamini hilo, kwani awali nilikuwa najitafutia riziki zangu za kujikimu kimaisha lakini nilipopata tatizo hili la kupooza mguu na kulemaa ndoto zangu zote zimeyeyuka ila sijakata tama” Hivi ndivyo anavyomalizia Paulo Ezekiel ambaye anaishi Mbagala, Temeke Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kijana huyu awali alikua akifanya shughuli za kutafsiri Lugha kwa wageni wanaokuja kununua bidhaa kwenye maduka ya Kariakoo na Bandari ya Dar es Salaam hasa wafanyabiashara wanaotoka Congo, Rwanda, Zambia, Malawi, Burundi na maeneo mbalimbali.

Paulo Ezekiel ni mtoto wa pili kati ya watoto nne, anatokea Mkoa wa Kilimanjaro na kabila lake ni Mchaga.
Mohammed Dewji maarufu ‘MO’

MO DEWJI FOUNDATION: Ni taasisi iliyoanzishwa na Mbunge wa Singida Mjini (CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu ‘MO’ ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya kiongozi bora aliyejitolea kwa kiasi kikubwa katika jamii na kuleta mabadiliko Afrika kwa mwaka 2014.

Tuzo hiyo aliyotunukiwa MO iitwayo African Philanthropist of the year Award 2014, Ilitolewa na jarida la uongozi la Uingereza, jijini Dubai wakati wa Jukwaa la Viongozi wa Afrika.

Kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo, sifa kuu aliyokuwa nayo MO kama alivyofafanua wakati wa kukabidhiwa tuzo hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa jarida hilo, Dk Ken Giami alisema wataalamu waelekezi walimchagua Dewji kuwa mshindi kutokana na: Uongozi bora katika Kampuni yake ya Mohammed Enterprises (MeTL GROUP) Pia kigezo kingine kilichompa ushindi ni namna anavyojihusisha na kazi mbalimbali za kijamii.

Pia Mchango wa MO katika elimu ni sehemu kubwa ya mafanikio yake hususan kwa kuendeleza ujenzi wa shule mbili hadi 12, pamoja na kujitolea kiasi cha zaidi ya Sh520 milioni katika kuendeleza sekta hiyo ya elimu ndani ya jimbo lake hilo la Ubunge la Singida Mjini.

MO pia amekuwa akisaidia sekta ya afya kwa ushirikiano na Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania kwa kuwaleta madaktari waliowafanyia upasuaji wagonjwa wa macho na 179 kupata miwani, kusambaza maji safi na salama kwa kuchimba visima vingi vya maji ndani ya jimbo na n.k.

Kwa sasa MO ndie Bilionea kijana Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes. Unaweza kusoma zaidi kupitia forbes.com/profile/mohammed-dewji

Kwa hali hiyo pia Dewji ameingia katika orodha ya Philanthropist duniani pia waweza kuona watu wengine waliotunukiwa tuzo kama hiyo kupitia wikipedia.org/wiki/List_of_philanthropists

Msomaji wetu unaendelea kuperuzi mtandao wako wa Modewji blog, tutakuletea makala maalum juu ya tatizo hili la kupooza ghafla kwa viungo hadi kusababishia kilema. Endelea kuwa nasi. Asante pia waweza kutuma maoni yako kupitia hapo chini ndani ya mtandao huu ama kupitia simu 0719076376 au 0689858799 au email [email protected]

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Zainul Mzige

Kagera: Wakamatwa kwa kufukua maiti ya albino na kuinyofoa viungoVideo iliyopachikwa hapo juu inawaonesha watu wawili huko mkoani Kagera wakikiri kuhusika na kufukua maiti ya albino aliyezikwa mwaka 2006 na kuchukua baadhi ya viungo kadiri walivyoagizwa na mganga.

Egypt, Ethiopia and Sudan sign deal on Nile river water sharing

River-nile

Egypt, Ethiopia and Sudan signed an initial agreement Monday on sharing water from the Nile, which runs through all three, as Ethiopia presses ahead with its construction of a massive new dam it hopes will help alleviate the country’s power shortages.

The dam had been an issue of contention among the countries, with Egypt concerned it would reduce its share of the Nile established under a colonial-era agreement. But on Monday, leaders of the three nations welcomed the agreement in speeches in Khartoum. It outlines principles by which they are to cooperate to use the water fairly and resolve any potential disputes peacefully, leaving details on specific procedures to be determined later after the release of joint, expert studies.

A version of this brief appears in print on March 24, 2015, on page A9 of the New York edition with the headline: Africa; Sudan: Three Nations Sign Deal on Water Sharing.

via The NY Times

Woolworths yashusha gharama kwa 50% ya bei Pasaka

Baadhi ya wateja wa wakinunua bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika duka la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa punguzo la bei litakaloduma kwa wiki nne kwa maduka yote nchini kwa asilimia 50% kwa bidhaa zote zinazouzwa katika maduka yote ya Woolworths yaliyopo jijini Arusha na Dar es Salaam.

Katika pindi hiki cha sikuu ya Pasaka Watanzania wanaweza kununua nguo zenye ubora kwa nusu bei kufuatia punguzo la silimi 50 lililotangazwa jana na duka maarufu la nguo la Woolworths jijnini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa punguzo hilo, mkurugenzi wa duka hilo Joehans Bushiri aliawambia wateja waliofika dukani hapo kuwa punguzo hilo titadumu kwa muda wa wiki nne.
Alisema lengo kubwa la Woolworths ni kuwawezesha watanzania wenye vipato vya aina mbali mbali kufurahia sikukuu ya Pasaka kwa kupata nguo za kisasa zenye ubora kwa gharama nafuu.

Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kuachana na nguo za mtumba,  “Tunawasihi watanzania kuepukana na matumizi ya nguo za mtumba kwani si salama kwa afya zao. Katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka duka la Woolworths linatoa punguzo kubwa ili kuwawezesha watanzania kupata nguo mpya na zenye ubora.,” alisema.

Bushiri alisema duka hilo ambalo ni moja kati ya maduka makubwa ya nguo hapa nchini, litaendelea kuwahudumia wateja wake kwa kuwaletea nguo nzuri na zenye ubora kwa gharama nafuu na hivyo kuwasaidia kuepukana na nguo za mtumba.

“Mteja anayekuja kununua nguo dukani kwetu anakuwa amefanya uamuzi sahini kwani atapa nguo zenye ubora kwa gharama nafuu na atakuwa amepata kitu ambacho kinaendana na thamani ya pesa yake,” alieleza.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, duka hilo pia linatoa nafasi kwa wateja kununua nguo kwa kulipia kidogo hadi kwa muda wa miezi mitatu ili kuwawezesha wale wasio na fedha za kutusha kulipa mara moja kuweza kufurahia nguo zenye ubora.

Kuhakikisha wateja wetu wanapata vitu bora kabisa, vinavyoendana na wakati na kwa mda muafaka, Woolworths imeweza kubadilisha mfumo wa uletaji wa bidhaa nchini badala ya kutumia meli kama zamani sasa inatumia usafiri wa ndege. Kabla ya hapo tulikuwa tun kunatumia muda wa mwezi mmoja hadi miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa tunatumia mda wa wiki mbili hadi tatu.

Bwana Bushiri pia akasisitiza kwamba anapenda kuwahakikishia wateja wao kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote kama zinazopatikana South Africa na kwa bei zinazofaa kabisa. 

Kwa upande wake Manfred Ngatunga ambaye ni mmoja kati ya wateja wazuri wa duka hilo alitoa shukrani zake kwa uongozi wa duka hilo kwa kutoa punguzo kubwa haswa katika mismu huu wa sikuu ya Pasaka.

Uamuzi wa punguzo la bei umekuja kipindi kizuri sana. Kipindi hiki na kipindi ambacho familia zinafanya manunuzi kwa ajili ya sikuu ya Pasaka. Tunashukuru kwa kuwa tutapata nguo zenye ubora kwa nusu bei, kila mtu sasa anaweza kupendeza,” alieleza.


Meneja Masoko wa maduka ya Woolworths Tanzania,Edwina Barongo akisisitiza jambo kwa wateja waliofika katika Uzinduzi wa punguzo la bei ya bidhaa zote zinazouzwa katika Maduka yote ya Woolworths yaliyopo Arusha na Dar es Salaam, Punguzo hilo litadumu kwa muda wa wiki Nne ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.


Meneja Mkuu wa kampuni ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushiri akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa punguzo la bei kwa bidhaa zinazouzwa katika maduka yote ya Woolworth, kwa kipindi cha wiki Nne ikiwa ni sehemu ya ponguzo la kununua bidhaa bora kwa kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam.


Mgeni rasmi (Loyal Customer) Manfred Ngantunga (kulia) akizindua duka la Woolworths lililopo mtaa wa Ohio jengo la PPF Tower ikiwa ni sehemu ya kuzindua punguzo la bei nafuu kwa bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo katika maduka yaliyopo Arusha na Dar es Salaa.Katikati ni Meneja Mkuu wa Woolworths Tanzania Joehans Bushiri na Mkurugenzi wa fedha Samson Katemi (kushoto).Uzinduzi huo wa Punguzo la bei kwa asilimia 50 utadumu kwa muda wa wiki Nne ulifanyika jijini Dar es Salaam.


Mteja wa muda mrefu wa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths (Loyal Customer) Manfred Ngantunga (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi na Meneja Mkuu wa Woolworths Tanzania Joehans Bushiri wakiingia ndani ya duka hilo mara baada ya uzinduzi wa punguzo la bei la bidhaa zinazouzwa katika maduka hayo.Kushoto ni Mkurugenzi wa fedha Samson Katemi hafla hiyo ya Punguzo la bei kwa asilimia 50 ilifanyika jijini Dar es Salaam itadumu utadumu kwa muda wa wiki nne.


Mteja wa muda mrefu wa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati) akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths jijini Dar es Salaam.


Kwenda kwa Lowasa: Bulembo ageukwa

Mjumbe wa Baraza la Wazazi, Taifa na Mbunge wa Korogwe, Steven Ngonyani 'Prof .Maji Marefu' akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hii leo juu ya tuhuma za yeye kutajwa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo kuwa aliratibu na kulazimisha baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kwenda kumuona Mbunge wa Munduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
VIONGOZI waliotajwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCMTaifa, Abdallah Bulembo, kuratibu safari ya baadhji ya wajumbe wa jumuia hiyo na baraza la Wazazi Taifa kwenda kumsalimia Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa leo wamekanusha vikali kuhusika na uratibu wa baraza hilo.

Jana Bulembo aliwashukia wajumbe waliokwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward lowassa, na kumchakingaia fedha na kumshawishi agombee Urais na kuwataka waombe radhi kutumia jina la baraza hilo na kasha kusubiri kamati ya maadili.

Wakizungumza hii leo baadhi ya wajumbe hao wamewataja waratibu walioongoza msafara wao kuwa ni pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Vioroka Kajoro na Mjumbe wa baraza hilo kutoka mkoani Ruvuma, Jackline Ngonyani na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa.

Mjumbe wa jumuiya hiyo kutoka Mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza, alisema aliyekuwa akiandika majina ya wajumbe waliokwenda katika ziara hiyo ni Jackline Ngonyani.

“Niliwasikia wakisema kwa Mzee ni saa tatu, nikawauliza mnataka kwenda wapi, wakaniambia kuwa wanataka kwenda kumsalimia Lowassa, name nikaandikisha jina kwa ajili ya kwenda huko,”alisema Lupenza.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye alibainisha kuwa hakuna mtu aliyeshinikizwa katika safari hiyo na ilikuwa ni huru kuamua kwenda au kubaki.

“Hakuna mtu aliyeshinikizwa kwenda kwa Lowassa kila mtu alikwenda kwa mapenzi yake. Na hakuna mtu aliyetumia jina la Jumuiya wakati tulipokwenda bali watu walijitambulisha mmoja mmoja,”alisema na kuungwa mkono na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.

Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko.

“Nimekuwa katika jumuiya hii kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko tayari uomba radhi kwasababu sina kosa nililotenda,”alisema Ngonyani.

Alisema hajawahi kumshawishi mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye.

Dk Mukassa alisema yeye aliratibu ziara hiyo kama mwenyeji wa mkoa wa Dodoma ambaye anakufahamu nyumbani kwa Lowassa.

Alisema fedha walizotoa kwa ajili ya kumchangia kuchukua fomu za Sh 600,000 zimetokana na mchango wao wenyewe kama wanachama wa kikundi cha kusaidia cha wajumbe wa jumuiya hiyo.

“Fedha zile hazikutoka kwenye jumuiya ya chama wala hakuna aliyekwenda pale kuwakilisha jumuiya na niliwaeleza pale mliponiuliza na kila mtu alijitambulisha kama yeye,”alisema.Jackline Ngonyani aliyejitambulisha kwa Lowassa kama 'Maji mafupi' na kutoa salam za shukrai kwa wana Ruvuma kwa jinsi Lowassa alivyo shiriki katika mazishi ya Capt.John Komba lakini jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa alilazimishwa kushiriki katika msafara huo. Lakini wenzake wanasema yeye alikuwa mmoja wa waratibu.Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza, akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yao kwenda kwa Lowassa. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa, akiwaonesha waandishi wa habari picha ambayo mjumbe mwenzao alisema wamelazimishwa kwewnda kwa Lowassa jinsi alivyo kula pozi na Lowassa.


  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Mroki Mroki/Father Kidevu blog

Taarifa ya kisomo cha Baba yake Ally Mikidadi

Ally Mussa Mikidadi anawataarifu kisomo cha marehemu mpendwa baba yake kitakachofanyika siku ya Jumamosi March 28, 2015 saa 11 jioni (5pm) anuani ya mahali kitakapofanyika kisomo ni

Pinecrest Local Park
301 St. Laurance Dr
Silver Spring, MD

Kama ilivyo kawaida yetu kusaidiana na kushikamana hasa katika kipindi hiki kigumu cha Ally Mussa Mikidadi kuondokewa na mpendwa baba yake, tunaomba msaada kwa wakina baba walete vinywaji na akina mama tusaidiane vyakula ili tuweze kufanikisha shughuli hii ya kisomo cha baba mzazi wa mwenzetu, ndugu yetu, Mtanzania mwenzetu na kaka yetu. Tunatanguliza shukurani.

Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na


Ukipata taarifa hii mjulishe na mwenzio na tafadhali tuzingatie muda.

MMtoi: Maandamano kila kona, wanataka nigombee

Mohamedi Mtoi

TAFAKURI CHOKONOZI: MAANDAMANO KILA KONA WANATAKA NIGOMBEE


Nawafikiria masheikh na wachungaji, nasikia kuna na vijana wa bodaboda na wanafunzi wa vyuo vikuu wanaandama kuja nyumbani. Sina miadi nao lakini nimeshatega turubai. Nimesha mpitia dada kamanda Latifah Makau aandae box za juice ya Azam yuko tayari kutoa fuso nzima ya vijoti

Nitambembeleza na mjomba angu Shaban Mbwana kwa kuwa ni mtaalamu wa maswala ya fedha awe ndio mpanga bajeti, nimeshakamilisha mipango yote ya gari la kampeni Cide Shekonga kakubali kutoa Land Cruiser yake kwa ajili ya kampeni. Niliwaza sana kuhusu PA system lakini sina wasiwasi tena ndugu zangu wa Five brothers wamekubali ku-sponsor, meneja Jafari Mdoe amekubali gari itatangulia field kabla hata sijafanya maamuzi.

Nimesha check na mafundi wa kombati za miezi mitatu nikiwa field kamand aJohn Heche anasema bajeti iko tayari, kabla sijawaza kuhusu kuandaa timu ya kampeni malkia Hafsa Zahoro ananipigia simu anasema umoja wa kina mama wafanya biashara nao wako na mabongo wanasema wamewatangulia kina mama ntile wanasema "dear lazima ugombee ".

Namwambia atulie niko busy nasoma email ya mwalimu wa mwanangu Fariss naye anasema watoto wote wa chekechea na standard one wamegoma kuingia darasani! Nauliza kisa nini?! Wanasema lazima baba Fariss agombee tena jukwaani awe anapanda na Firdaus. Daah hii nayo kali mpaka chekechea

Siwazi kuhusu atakaye simamia usafiri. Mdogo wangu Ally Manguo atafanya hiyo kazi naye anasubiria tu niseme, japo anasema madereva wa malori nao wanaandama kuelekea kwenye ofisi yao, wanataka kuchangishana fedha za kampeni.

Washkaji zangu mawakili nao wako busy namuona Peter Kibatala na Jonathan W. Mndeme wanaandaa makarabrasha wanadai lazima nitawekewa pingamizi. Namuoan Ally Bananga naye mbio! Osie n'zeze?! Niiva wagombea...

Maandamano yamezidi nasikia walioko magereza nao wamegoma kula kisa wanataka nigombee, kamanda Jestina Hakizimana naye anasema magari yote DSM syio kuwa ni foleni bali ni maandamano na mgomo baridi nao wanasema lazima nigombee. Hekima Mwasipu ananitonya eti hata mvua inayosemekana imejiunga kifurushi cha wiki nayo haitaacha kuonyesha mpaka nigombee.

Nadhani nitakubali, hata washkaji zangu wa ughaibuni kina Anasia MalekoSubi NuktaAmiri HazaliBakari HazaliKaseeb J Kupaza, Alex PaurineSalim Amar hawatakuwa kimya, maana wanapanga kuandamana na mabango kuelekea ubalozini.

Najaribu tu kuwaza kwa sauti, anachokifanya Lowasa.

Niko gereji magari nayo yameandamana

Mohamedi Mtoi

Idadi ya wasiojua kusoma na kuandika - NW Elimu, Anne Kilango atoa jibu

Ukweli wa uhalisia wa maisha kila Mwanachuo anapaswa aujue kabla hajahitimu“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” (Hosea 4:6) ni moja ya mistari maarufu sana katika kitabu kitakatifu Biblia. Ni moja ya sentensi zinazoigusa jamii yetu kwa sasa, hapa Tanzania, Afika na dunia kwa ujumla. Kitabu hiki cha ‘Graduate with PlanB in Mind’ kimekuja wakati muafaka kabisa kwa Taifa letu na dunia kwa ujumla. Hii ni kwa sababu kimetokea wakati ambao vijana wengi wa kike na wa kiume waliopo katika ngazi mbalimbali za kielimu wamekuwa wakiyumba yumba sana na wasijue cha kufanya wanapokuwa wamehitimu masomo yao. Wengi wao wamekuwa ni wahitimu walalamishi badala ya kuwa wahitimu wafumbuzi wa matatizo ya kijamii inayowazunguka.

Nilipokisoma kitabu hiki kilipokuwa katika hatua za awali, mawazo yangu ya kina yalilipuka upya. Nilitamani kama ningekisoma kitabu hiki mwanzo kabisa nikiwa shule ya sekondari ya kawaida. Nilishasoma vitabu vingi sana vilivyoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili, na kingereza vikiongelea namna ya kufanikiwa katika maisha, namna ya kushinda kwenye usaili, na vingine vingi vya aina hiyo. Lakini sikuwahi kusoma kitabu ambacho kingenipatia mbadala wa maisha. (Plan B). Wengi wetu tunapotoka vyuo vikuu tunakuwa tumebeba wazo moja kuu la ‘ajira’, kana kwamba ajira ni moja ya amri kumi takatifu za nabii Musa ambazo ukiikosea moja tu unapigwa mawe. Tunapofika mitaani kwetu tunakuta kitu kingine. Tunapokuwa chuo kikuu ama katika ngazi za chini za elimu tunajisahau sana. Tunakuwa kwenye ulimwengu wa chuo kikuu kana kwamba hatutaondoka kwenye majengo ya vyuo na kutufanya tusahau ulimwengu wa halisi wa mtaani kwetu.

Kama wewe ni mwanafunzi wa ngazi yoyote ile unayoifahamu, hakikisha unakisoma kitabu hiki, kwanini uendelee kuangamizwa kwa kukosa maarifa na kuendelea kuamini mawazo ya walioshindwa ama kubebwa na matukio ya mitaani ama kwenye mitandao ya kijamii? Ama mawazo ya wanafunzi wenzako na mawazo ya walimu na wazazi waoishi maisha ya uoga? Wanaoamini kwamba maisha ni ajira pekee? Tumekuwa watu wenye kubebwa na wazo moja tu la ajira kana kwamba bila ajira maisha hayaendi. Tumechelewa sana kuangalia na kujifunza kwa wenzetu wa nchi za dunia ya kwanza ambako maisha ni zaidi ya ajira. Tupo kwenye dunia ambayo wasomi na wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu wabuni ajira,maana kila anaehitimu akiwaza kuajiliwa basi kuna hatari ya kuwa wategemezi kwenye vipengele mbalimbali vya maisha. Bahati nzuri Tanzania ni moja ya nchi pekee duniani iliyosheheni fursa za kila aina fursa unazoweza kuzifanya hata kabla ya kutoka shule ama chuo. Uamuzi unabakia mkononi mwako, kujifunza maarifa na kuzitumia fursa ama kutojifunza ili ukihitimu masomo yako ubakie kuwa mlalamikaji.

Mawazo yaliyo andikwa na Mwandishi wa kitabu hiki ni mawazo yaliyofanyiwa utafiti wa kina na lengo lake ni kuzalisha mitazamo mipya miongoni wa wasomi waliopo vyuoni, wazazi, walimu, viongozi mbalimbali wa kisiasa, kidini na kijamii kwa ujumla. Ninatoa rai yangu kwa wazazi, walimu na wakuu wa vyuo na shule kukinunua kitabu hiki na kukiweka kwenye maktaba zao ili kiwe msaada kwa wanafunzi na watoto wao. Dunia ya sasa ni dunia ya wanadamu wanaojua ni kitu gani wanaweza. Siyo dunia ya kufuata mkumbo wala bendera kufuata upepo na matukio ya kijamii kama ilivyokuwa katika karne ya zama za kati za mawe, enzi ambazo wanajamii walikuwa wakifanya mambo kwa kubanwa na mazingira ya wakati huo. Kauli za ‘Kupata ni majaliwa’ Ng’ombe wa maskini hazai’ serkali haituthamini’, ‘sijasoma’, mimi ni mlalahoi ama mlalatabani, 'mkoa wangu ni wa pembezoni,’ ‘kabila letu limesahaulika’, nk, ni kauli za kimaskini, ni kauli za kutafuta visingizio. Kwakukisoma kitabu hiki utatambua nguvu ya mawazo yako ya kina na utatambua kusudi la wewe kuwepo duniani. Pigania kile ukitakacho usivunjwe moyo na waliochoka kiakili, waliochoka kufikiri, na wasiokuwa na malengo. Na wanaosema ponda mali kufa kwajwa. Go Big or Go Home.

Meshack C. Maganga.

Dar es Salaam

Wabunge wataka haki ya kushitaki benki kwa wizi kwenye ATM na bahati nasibu, salio/virufurshi vya simu

Wellcome Trust: Public health and tropical medicine fellowships

These fellowships are a series of career awards aimed at building sustainable capacity in areas of research that have the potential for increasing health benefits for people and their livestock in low-middle-income countries. Support is provided for researchers in low- and middle-income countries in public health and tropical medicine at all stages of their careers;

  • Intermediate Fellowships: This scheme enables high-calibre, mid-career researchers from low- and middle-income countries to establish independent research programme. Eligible candidates must be a national or legal resident of a low- and middle-income country and should be either: a graduate in a subject relevant to public health or tropical medicine with a PhD and three to six years' postdoctoral experience, or a medical graduate with a higher qualification equivalent to membership of the UK Royal Colleges of Physicians (i.e. qualified to enter higher specialist training) or recognized as a specialist within a relevant research area, with three to six years' research experience.
  • Training Fellowships in Public Health and Tropical Medicine Provide support for researchers from low- and middle-income countries who are at an early stage in their research careers, to gain research

Preliminary application deadlines: April 29, 2015

For more information visit www.wellcome.ac.uk/Funding/Biomedical-science/Funding-schemes/Fellowships/Public-health-and-tropical-medicine/index.htm

Vyuo Vikuu Mbeya wamtaka Prof. Mwandosya awanie Urais

Idd Mambo (katibu Itidadi na Uendezi, Chuo Kikuu TEKU) akimkaribisha mtoaji tamko hilo

Shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Mbeya limefaya kongomano lililohusu uchaguzi mkuu lililofanyika katika ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini hapa na kuchukua nafasi hiyo ya kumshawishi Prof. Mark Mwandosya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu huu.

Akisoma tamko loa wanazuoni hao mbele ya waandishi wa habari, Katibu wa shirikisho hilo Oscar Mwaihabi kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona ndani ya chama hicho hakuna kiongozi mwenye sifa ya kufanana na Prof. Mwandosya na hivyo wameona Tanzania ijayo iongozwe na kiongozi huyo.

“Sisi wanazuoni tumeona kuwa wewe Prof. Mark J. Mwandosya unafaa kabisa kupokea kijiti cha Urais kutoka kwa Jakaya Kikwete kwa kuwa unafaa na ni tofauti na wengine wote waliojitokeza kutangaza nia katika Chama Cha mapinduzi kutokana na uongozi uliowahi kushiriki. Hujawahi kupata tuhuma yoyote mpaka leo hii, pia Taifa linahitaji kiongozi mwenye hekima na maamuzi magumu hata utafiti unaonesha uwezo ulionao wa kiuongozi,” 
amesema Mwaihabi.

Hadi sasa, wanachama waliojitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, January Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia), Hamisi Kigwangala, na Lazaro Nyalandu ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.

Pia wako wanaotajwa kuwania urais lakini hawajatangaza ambao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sita; William Ngeleja, Emmanuel Nchimbi, Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira, Bernard Membe na Edward Lowasa.

Baadhi ya wanachama wa CCM na wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliokuwepo wakati wa kutoa tamko hilo
Oscar Mwaihabi akitoa tamko kwa wanahabari, kwa niaba ya Wanazuoni mkoani Mbeya

TEG PG Training fellowship in Medical Stats for African Scientists at LSHTM

London School of Hygiene and Tropical Medicine, UK

TEG Postgraduate Training fellowship in Medical statistics for African Scientists


This fellowship, which is funded by the UK Medical Research Council (MRC), provides support for two years training in medical statistics. For the first year the successful applicant will study for the MSc degree in Medical Statistics at the London School of Tropical Medicine and Hygiene (LSHTM). This will be followed by a one-year professional attachment at one of the African centres associated with the research programme of the Tropical Epidemiology Group (TEG) at LSHTM. During the professional attachment, training Fellows will develop their statistical and research skills by working on studies with guidance from TEG staff.

This support is intended to foster excellence in the field of medical statistics and epidemiology in sub-Saharan Africa. The fellowship will provide costs for fees, stipend (£15,000 per annum) and return air travel.

Eligibility: To be eligible, candidates must: (i) be resident in and a national of a country in sub-Saharan Africa

(ii) be in possession of an excellent first degree with a background in mathematics, statistics or a related subject

(iii) have at least 1 year of work experience in medical statistics or epidemiology

Application: Candidates should complete a TEG Fellowship Application Form and provide a curriculum vitae, two Reference Forms, and an academic transcript. The closing date for applications is 30th April 2015.

More info at: lshtm.ac.uk/study/funding/teg_fellowship_in_medical_statistics_for_african_scientists.html