Ijue timu ya watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili DW

Timu ya Idhaa ya Kiswahili ya DW inakutakia siku njema, afya na furaha.

Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Mohamed Abdulrahman, Josephat Charo na Sekione Kitojo. Waliosimama kutoka kushoto ni Andrea Schmidt, Mohammed Khelef, Saumu Mwasimba, Sudi Mnette, Bruce Amani, Iddi Ssessanga, Caro Robi, Oummilkheir, Nina Markgraf na Daniel Gakuba.

picha via DW WhatsApp (nawe unaweza kujiunga kupokea habari zao kwenye simu kwa kubofya hapa)


Wananchi wacharuka na kuzuia uhamisho wa Mwl. Mkuu anayetuhumiwa ubadhirifu

Mapitio ya magazeti katika Tv mbalimbali Machi 27, 2015

Ulikuwa unavusha nini?

Jamaa na pikipiki yake kafika mpakani anataka kuvuka kwenda nchi jirani, huku akiwa amepakia viroba viwili kwenye pikipiki.

Afisa Forodha: Umebeba nini?

Jamaa: Mchanga.

Akaambiwa ashushe uchekiwe, wakamlaza ndani wakacheki mzigo na kukuta kweli ni mchanga, wakamuomba msamaha akaruhusiwa kupita. Kesho yake akarudi tena na mzigo kama jana yake, akakamatwa na tena ikaonekana kabeba mchanga. Mchezo huo ukaendelea mwaka mzima. Siku moja akakakutana kwenye baa na Ofisa wa Forodha.

Afisa Forodha: Najua wewe kuna kitu ulikuwa unavusha lakini mwaka mzima hatukugundua, ulikuwa unavusha nini?

Jamaa: Nilikuwa navusha pikipiki.

via blogu ya Kitime

Kero ya udhalilishaji wa kijinsia unaofanywa na wauza mitumba

Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mambo ya aibu katika jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ule wa maungoni hasa kwa wanawake.

Kwa muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya kwa jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo jiji la Dar es Salaam.

Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Mtandao huu umekuwa ukishuhudia vitendo hivyo vibaya kwa jamii ambapo wengi wa vijana wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuwadhalilisha wanawake hasa wasichana wadogo kwa kuwashika maungoni (makalio, kifua/maziwa) huku wakiwalazimisha kununua bidhaa zao.

Vitendo hivi vimekuwa ni kama mchezo wa kawaida kwani vijana hao wamekuwa wakiendeleza hali hiyo kwa muda mrefu sasa huku wasichana/wakike hao wanaofanyiwa vitendo hivyo wakiwa hawana wa la kufanya, Mtandao huu tunasema huo ni udhalilishaji na unatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka kukomeshwa kwani unakiuka maadili na utu wa mwanamke.

Modewji blog tunatambua ipo mamlaka husika zinazoweza kulichukulia hatua suala hili basi kama zipo zianze sasa kwani udhalilishaji huu huko mbele unaweza kuleta madhara makubwa kwa mtendewa na hata anayetenda kwani akiachwa sasa baadae anaweza kufanya tukio kubwa na likafumbiwa macho ikiwemo kubaka.

Nachelea kuamini kama vijana hawa wanafanya hivi kwa kujiamini ama kuna nguvu ya msukumo nyuma yake? Kipindi cha nyuma sote tumekuwa tukishuhudia vijana hao wakiwachania nguo wanawake waliokuwa wakivaa vimini waliokuwa wakipita katikati ya mitaa ya Kariakoo wakati huo huo wamesahau kuwa nguo hizo wamewauzia wao, tukiacha hilo pia wapo hawa Makondakta wa daladala nao ni miongoni mwa watu wanaoongoza kufanya vitendo vya kidhalilishaji wanawake.

Mtandao huu umeweza kuliona hilo kwa upande wa Makondakta wa Daladala nyingi hasa nyakati za abiria wa kike anapopanda hatua ya kwanza wao wanapeleka mkono kwenye ‘Makalio’ ya Mwanamke na kumvutia ndani ya daladala, yaani kama sapoti ya kumuingiza ndani.

Kondakta anafanya hivyo wakati huo amekaa mlangoni mwa daladala yake, lakini anapopanda mwanaume usogea ndani ama hushuka chini bila hata ya kumshika, lakini akipanda Mwanamke tu utakuta Konda anamshika makalio kuona kwamba ni jambo la kawaida, Hivyo ni wakati sasa wa kubadilika jamani vitu vingine hivi ni kushusha utu wa mwanamke hivyo tubadilike na tuchukue hatua, Asante.

Tuma maoni yakoo hapa kwenye blog hii ama kupitia simu 0719076376

Taarifa ya Ikulu: Rais Kikwete ateua Wabunge 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:

- Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
- Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
- Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
- Mhe. Janet Zebedayo Mbene
- Mhe. Saada Salum Mkuya
- Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
- Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
- Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
26 Machi, 2015

Jembe FM Mwanza yapata leseni kutoka TCRA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni kwa redio ya Jembe FM ya jijini Mwanza kwenye ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa kurusha vipindi vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akikabidhi leseni kwa radio Jembe FM.

Alisema matumizi yasiyo sahihi yatasababisha mamlaka hiyo kunyang’anya leseni walioitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Alisema pamoja na haja ya kushiriki katika ushindani, kituo hicho kipya kinatakiwa kufuata masharti ya utangazaji ambayo yamo katika leseni waliyoiomba.

Alisema radio hiyo ya Mwanza inaongeza ushindani katika eneo hilo katika jumla ya radio FM 12 zinazosikika mjini humo, radio za kitaifa saba, za kikanda 11 na radio ya jamii 1.

Aliwataka kuwa waangalifu na kufuata kanuni za kitaalamua kufanyakazi wanasotahili za kuelimisha na kuburudisha.

Alisema si radio tu ambayo ina nguvu ndiyo inayoweza kuhimili ushindani lakini pia ufuataji wa kanuni na maadili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk. Sebastian Ndege amesema kwamba wameanzisha radio hiyo kwa lengo la zaidi ya kuburudisha na kuelimisha bali kusaidia vijana kushika hatamu na kujitengenezea uwezo wa ajira.

Alisema kwamba ili kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kitaaluma wameajiri watu ambao wamesomea kazi husika ili kuhakikisha kwamba hawaendi kinyume na leseni yao.

Alisema kwamba wanaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kujaza mapengo ambayo yapo katika urushaji wa matangazo kwa sasa ili kuhudumia mji wa Mwanza ambao unakua kwa kasi kwa sasa.

Alisema vipindi vyao vimezingatia haja ya jamii katika uchumi, elimu na afya.

Aidha amesema kwamba wanategemea kuwa na vipindi vizuri zaidi hasa kutokana na na uzoefu waliokuwa nao hasa wa uandaaji wa njia ya panda.

Jembe FM inamilikiwa na Jembe Media Limited.

Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi (kushoto) akisisitiza jambo kwa uongozi wa JEMBE FM wakati wa hafla ya kukabidhi leseni kwa uongozi huo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam makao makuu ya ofisi za TCRA.Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk Sebastian Ndege (wa kwanza kushoto) na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited wakimsikiliza kwa makini kabisa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa leseni rasmi ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza.Baadhi ya wawakilishi wa kampuni ya Ndege Insurance inayomilikiwa na Dk. Sebastian Ndege waliojumuika kwenye hafla hiyo fupi.Maofisa mbalimbali kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (kulia) akimkabidhi rasmi leseni ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege (katikati) katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya ofisi za TCRA jijini Dar. Kushoto ni Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi.Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege akitoa neno la shukrani ambapo pia maeahidi kuwa atafuata masharti na kanuni zote zilizowekwa na mamlaka hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Jembe Media Ltd, Renata Ndege.Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege na Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege wakionyesha leseni hiyo iliyoambatanishwa na miongozi ya Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria hafla hiyo.


 • Taarifa hii tumeshirikishwa na Zainul Mzige/modewjiblog

Taarifa ya Kova ya kumhoji Gwajima kwa aliyosema dhidi ya Pengo

JAMHURI YAA MUUNGANO WA TANZANIÀ 

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 

JESHI LA POLISI TANZANIA 

PRESS RELEASE 26/03/2015 

ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na:
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


----

wavuti.com imepata nakala ya sauti hiyo via WhatsApp, imo kwenye pleya iliyopachikwa hapo chini.
Rais Kagame ahudhuria mkutano Dar na kuzindua treni ya mizigoRais Jakaya Mrisho Kikwete akimraribisha Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika picha ya pamoja na mawaziri wa Tanzania, kenya, DRC na Uganda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakisiliza maelezo toka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade walipotembelea kituo cha kulipia ushuru wa aina zote chini ya paa moja katika bandari ya Dar es salaam leo Machi 26, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakisiliza maelezo toka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade walipotembelea kituo cha kulipia ushuru wa aina zote chini ya paa moja katika bandari ya Dar es salaam leo Machi 26, 2015.Rais Paul Kagame akisalimiana na viongozi wakuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wakati alipofika katika Stesheni ya Dar es Salaam kuindua Treni ya Mizigo ya kwenda Rwanda. (Picha na Francis Dande)


Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Paul Kagame wakati wa uzinduzi wa Treni ya Mizigo ya kwenda Rwanda. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick. (Picha na Francis Dande)


Rais Kagame akielekea katika uzinduzi wa Treni ya Mizigo ya Rwanda jijini Dar es Salaam. 


Rais Kagame akiwa amenyanyua bendera kuashiria uzinduzi wa Treni ya Mizigo ya Rwanda jijini Dar es Salaam.


Jakaya Kikwete akiteta jambo na Rais Paul Kagame wa Rwanda.


Rais Paul Kagame akiwa na Rais Jakaya Kikwete wakiwasili katika Stesheni ya Dar es Salaam leo.


Rais Kagame akiwa akizindua rasmi Treni ya mizigo ya kutoka Dar hadi Kigari Rwanda.


Rais Paul Kagame wa Rwanda akipeperusha bendera kuashiria kuzinduliwa kwa safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya reli ya Dar es salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho kikwete leo Machi 26, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo walipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Machi 26, 2015.

 • Picha kutoka kwa Francis Dande na IKULU

Taarifa ya ACT Tanzania kwa ummaChama cha Wazalendo (ACT - Tanzania )

Kama mnavyofahamu, Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kitafanya mkutano wake mkuu na uzinduzi wa chama mnamo tarehe 28 na 29 Machi 2015. Katika mkutano Mkuu chama kitapitisha katiba mpya ya chama na kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Chama, Makamu wenyeviti, Katibu Mkuu na Manaibu makatibu wakuu. Pia chama kitachagua wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.

Katika uzinduzi wa chama tarehe 29 Machi 2015 kuanzia saa tisa alasiri, viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamealikwa. ACT – Tanzania imemwalika Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kuzungumza kwa niaba ya vyama vya upinzani nchini kuhusu ‘ kwa nini Tanzania bado ni nchi masikini na nini cha kufanya kuondoa umasikini’. Pia viongozi wote wa vyama vya siasa nchini, mabalozi wa nchi mbalimbali na wakuu wa asasi zisizo za kiserikali wamealikwa. Uzinduzi utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na radio kadhaa hapa nchini.

Mheshimiwa Samia Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa kwanza wa Ghana Osagyefo Kwame Nkrumah amealikwa pamoja na Mheshimiwa Ababu Namwamba, Katibu Mkuu wa chama cha ODM cha Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya. Vile vile ACT – Tanzania inatarajiwa kupata wageni kutoka vyama rafiki vya Ujerumani Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto Progressive Alliance.

Baada ya Uzinduzi ACT Tanzania itafanya mikutano ya hadhara nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Mbeya. Jijini Arusha ACT – Tanzania itahuisha Azimio la Arusha na kuelezea mwelekeo wa kisera wa chama katika kujenga Tanzania mpya yenye kufuata misingi Usawa, Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Demokrasia na Uadilifu.

Abdallah Khamis

Look elegant & smart in suit by matching width of a tie; Here is howInstead of thinking about tie width by itself, its something you should consider in conjunction with your lapel width.

It’s about proportions. Choosing your tie width, much like choosing the other aspects of your suit, should factor in its surroundings–your chest and shoulder size, the fit of your suit, shirt collar width, lapel width and your face shape.

Here’s a simple rule that’s easy to remember: Match the widest point of your tie to the widest point of your suit lapel.

It’s not an exact science and you can go up or down (mismatch the width) by about 0.25″ either direction, but this rule of thumb will help you achieve a more balanced look. Just don’t start looking for suits with 1.00″ lapels to match your uber-skinny tie.

Mwaliko wa semina ya ujasiriamali bila malipo Jumamosi

Kampuni ya CPM Business Consultants, inayojishughulisha na kutoa mafunzo ya ujasiriamali na ushauri wa biashara, itatoa semina ya ujasiriamali kwa watu wote bila malipo yoyote siku ya Jumamosi tarehe 28/3/2015 saa 5.00 asubuhi katika ukumbi wa Hawaii Kimara Baruti.

Katika semina hiyo tutatoa fursa kwa washiriki kununua vitabu vya ujasiriamali ambavyo gharama yake ni sh. 6,000/= kwa wale watakaohitaji.

Mada zitakazotolewa ni: 

– Namna ya kuanzisha biashara
– Namna ya kufanya utafiti wa soko na kutangaza biashara yako.
– Jinsi ya kutunza kumbukumbu za hesabu za biashara yako.
– Fursa za biashara kulingana na mazingira yako.
– Maswali na majibu. 

Kwa maelezo zaidi au kuthibitisha ushiriki kwenye semina, piga simu namba 0784394701. Tafadhali mwambie na mwenzako, sambaza ujumbe huu kadiri inavyowezekana.

Zanzibar featured on NPR: Vanilla, nutmeg spice and everything nice

A spice farmer on the island of Zanzibar off the coast of Tanzania shaves off bark of the cinnamon tree.Gregory Warner/NPR

This is nutmeg, used in cake and coffee and also locally in nutmeg porridge, an alleged aphrodisiac. "If your husband is not around, don't eat nutmeg porridge," says Fadhili.

Click here to listen to the audio at the NPR and read more.

Call for Tanzanians to apply for Fulbright Junior Staff Development (JSD) Program

*** Application cycle 2016 - 2017 ***

The Public Affairs Section of the United States Embassy in Dar es Salaam is seeking qualified candidates for the Fulbright Junior Staff Development (JSD) Program. Online applications are now available starting February 5, 2015. Deadline for submitting applications will be no later than May 1, 2015. Only successful candidates will be called for interviews scheduled for mid-May, 2015.


The Fulbright Junior Staff Development (JSD) Program is the largest Fulbright program with Africa and provides financial assistance for a maximum of two years of study toward a graduate degree in a U.S. university or for participation in a non-degree research or nonacademic professional program. It is designed primarily to strengthen African universities through higher degree training for faculty members. Applications are also accepted from prospective candidates in public and private educational and cultural institutions, independent research institutes, and professional institutions.

The JSD program is open to any qualified candidate but strongly encourages the inclusion of female candidates and prefers candidates who have not had extensive recent experience in the United States. Recent (within three years) recipients of Fulbright grants are not eligible to apply, and it should be emphasized that funding is for a maximum period of two years only. It is important to note that doctoral degree candidates will typically need to secure additional funding to complete their course of study and we now prioritize the selection of Fulbright Master’s candidates over Ph.D. candidates.

Eligibility Requirements

 1. Applicants must be citizens of Tanzania or permanent residents qualified to hold a valid passport issued by Tanzania.
 2. Applicants must have a record of outstanding academic achievement and preparation in their chosen field of study. They must show high motivation and serious commitment to completing the program and to returning home.
 3. Applicants should either be candidates for an advanced degree in their current field or for a specialized non-degree program in a field for which they are well prepared. Applicants who wish to pursue study in a field other than their current field of study must demonstrate adequate background in that field.
 4. Applicants must be affiliated with or committed to working at an academic institution or public or private institutions in Tanzania upon return, and should have the endorsement of their home institution.
 5. Applicants should have a high motivation and a serious commitment to completing the program as scheduled and to returning home.
 6. Applicants with no extensive or recent U.S. experience will be given preference.
 7. Applicants must have a sufficiently high level of English proficiency to enable them to complete a full-time program of graduate study in the United States.

In Tanzania, the Fulbright Junior Staff Development Program is administered by the U.S. Embassy's Public Affairs Section, which nominates candidates to the Fulbright Scholarship Board in Washington, DC. The Fulbright Scholarship Board makes the final selection of candidates. In order for the Embassy to complete the nomination process before the deadline date for submission, we urge aspiring candidates to submit their applications to the Embassy by May 1, 2015; applications received after this date will not be considered.

All application forms must be prepared electronically, on-line application is preferred: hand-written applications will not be accepted. Candidates must submit completed application forms, academic transcripts, and three confidential letters of reference online. Please note that only those short-listed for final consideration will be called for a panel interview. Only finalists will be required to submit their medical history, supplemental forms and complete standardized English and Graduate Record Exam tests.

The online application utility can be found on the internet at https://apply.embark.com/student/fulbright/international/20/

Applications should be submitted to:

Fulbright Program Officer
Fulbright JSD Program
Office of Public Affairs, American Embassy,
686 Old Bagamoyo Road, Msasani,
P.O. Box 9123, Dar es Salaam, Tanzania,
or by e-mail to [email protected]


Tel: 022 2294000 Ext: 4192/4813 or via the online application process.

Tafadhali usitumie mfano wa mchicha...


Kumbe ndiyo maana wanaume wanachepuka sana...

...siyo kosa lao maana ilikwisha andikwa Mungu aliwaumba ADAMU na HAWA, hakuumba ADAMU na HUYU.

via blogu ya Kitime.

SUA: New University Fees with Effect from Academic Year 2015/2016


The office of the Deputy Vice Chancellor (Academics) Wishes to inform the general public, the continuing; and prospective students that, the Management has reviewed the University fees for Postgraduate, Undergraduate; and Non-degree programs.

Please click the following link to download a document with details: suanet.ac.tz/...university_fees_2015_2016.pdf

Call for Tanzanians to apply for Fulbright Foreign Language Teaching Assistant

*** Application cycle 2016 - 2017 is now open ***

The Public Affairs Section of the United States Embassy in Dar es Salaam is seeking qualified candidates for the Fulbright Foreign Language Teaching Assistant (FLTA) program. Online applications are now available starting March 25, 2015. Deadline for submitting applications will be no later than May 1, 2015. Only successful candidates will be called for interviews scheduled for mid-May, 2015.

The Foreign Language Teaching Assistant (FLTA) Program is funded by the U.S. Department of State. Teaching Assistants are vetted through the J. William Fulbright Foreign Scholarship Board. The program aims to strengthen U.S. foreign language instruction and promote mutual understanding by establishing a foreign language native speaker expertise on U.S. campuses. The program enables the teaching assistants to complete their home country pre-service training by engaging in non-degree studies at accredited post-secondary U.S. educational institutions while teaching one or two language courses. Additionally they serve as resource persons in conversation groups, cultural representatives, attendants in language laboratories, coordinators of extracurricular activities or supervisors of clubs and language houses. Selected teaching assistants will enjoy Fulbright status in the United Status. They are expected to teach their language/culture for up to 20 hours per week while taking two courses per semester. All FLTA's receive room and board, a monthly stipend, and tuition waiver for the required coursework, in addition to Fulbright immigration services. The Fulbright grant is for one academic year and is non-renewable.

The Institute of International Education (IIE) on behalf of Department of State, USA, would like to place several language teaching assistants at universities and colleges in the US as part of a strategic language initiative.

Kiswahili is one of the targeted languages.

These teaching assistants would be Fulbright Scholars and are expected to teach their language/culture for up to 20 hours per week while taking two courses per semester. The grant is for one academic year and is non-renewable. The program is designed to have native language and cultural informants who are close in age to undergraduate students in the USA. Normally, FLTAs would teach:
 • beginning level or conversation courses
 • work in a language lab
 • animate a language table
 • organize cultural activities or have similar duties

Each institution assigns duties that will best meet the needs of their school's unique circumstances.

Fulbright will pay for travel, health insurance and monthly maintenance of the selected candidates. Institutions where the FLTAs are placed provide tuition scholarships for the required coursework. The selection process for Tanzania is facilitated through the American Embassy in Dar es Salaam.

Applicants must be teachers of English or in training to become teachers of English, and at minimum must possess the equivalent of a U.S. Bachelor's degree by June 1, 2016 to allow time to submit an official transcript prior to the start of the Fulbright FLTA Program and who are willing to travel without their dependants for one academic year.

This is an excellent opportunity for young teachers in Tanzania. To apply, please refer to the requirements listed here, and if you qualify, apply through online application process. Three reference letters should be filled out by teachers or other professionals you have worked with, and submitted directly to the address below. Signature page should be submitted together with relevant certificates and transcripts to:

Fulbright Program Coordinator,
Fulbright FLTA program,
Office of Public Affairs,
American Embassy,
686 Old Bagamoyo Rd. - Msasani,
Box 9123, Dar es Salaam.
Voice: 255 22 229 4813
Fax: 255 22 229 4722
Email [email protected]

Please note that only short-listed applicants will be contacted for an interview. Also, only nominated candidates will be required to sit for the TOEFL exam and submit a medical report.