Kamera ilivyonasa picha za Wabunge wetu hapa na pale Bungeni


Edward Lowassa, Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu akiwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani mwenye mafanikio makubwa.Mbunge ambaye tayari ameshatangaza nia yake ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Mbunge wa Nzenga, Dk Hamisi Kingwangala akiwa Bungeni mjini Dodoma hii leo. Akiuliza Swali hii leo kwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira kuwa atamsaidiaje kunyanyua bei ya zao la pamba.


Manaibu Waziri wakijadiliana jambo na Mbunge.


Mbunge wa Arumeru Mashariki Goodluck Ole Medeye akiperuzi gazeti tando (blog) kupitia tablet yake akiwa Bungeni Mjini Dodoma. Upatikanaji wa habari na taarifa siku hizi umekuwa rahisi.


Martha Mlata Mbunge wa Viti Maalum akiwa Bungeni


Wabunge wakiendelea na shughuli zao Bungeni


Prof. Tibaijuka asafiri kwa bodaboda km 13 na kuwa Mbunge wa kwanza baada ya uhuru kuzuru KaaziMbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka alitembelea Kata ya Kimwani. kijiji cha Kaguramo kitongoji cha Kaazi Nyakishabo na kulakiwa na mamia ya wananchi waliopanda mlimani wakiwa na matawi ya miti huku wakiimba.

Kaazi pana kambi kubwa ya wavuvi. Mwenyekiti wa kitongoji cha Kaazi, Nyakishabo Ndugu Ojax Dorolyma Lyapa alionyesha furaha yake kwa kusoma risala ya kijiji kwa lugha ya kimombo huku akishangiliwa alipokuwa anaitafsiri. Mwenyekiti huyo alisema Prof. Tibaijuka ametengeneza historia kuwa Mbunge wa kwanza tangu uhuru kufika kwenye kijiji hicho kilicho mwambao wa ziwa.

Prof. Tibaijuka aliwasili Kyota majira ya saa 11 jioni akiwa amechelewa akitokea Bukoba ambapo alilazimika kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa ya Chama Cha Mapinduzi ambamo yeye ni mjumbe.

Kwa ubovu wa barabara Prof. aliacha gari yake Kyota na kupanda pikipiki kilometa 13 hadi Kaguramo Mwisho ambapo alishuka na kutembea kilometa 2 kuteremka mlima mkali hadi Kaazi Nyakishabo.Alishuhudia mamia ya watoto wa shule ya msingi wanaolazimika kutembea kilometa 7 kila siku kwenda shule ya msingi kaguramo.

Mwenyekiti wa kijiji aliomba Prof. Tibaijuka akubali kufadhili ujenzi wa shule ya msingi itakayojulikana kwa jina lake kijijini hapo. Bila kumungunya maneno mwenyekiti huyo wa CCM alimtaka Prof. kuendelea na Ubunge wa jimbo hilo kuleta maendeleo.
Prof. alianza hotuba yake kwa kuwataka watoto wasiokwenda shule kijitokeza. Mtoto Abdu alitoka mbele na kusema ameacha shule akiwa darasa la 3 kwa kukosa sare ya shule. Papo hapo Prof. Tibaijuka alitoa fedha za kumshonea sare. Prof. pia alichangia shilingi laki mbili na nusu kwenye mfuko wa kuwasaidia watoto wahitaji ili waendelee na masomo. Prof akaafiki kushirikiana na wanakijiji kujenga shule ya msingi baada ya kuambiwa kijiji cha Nyakishabo kina kaya 400. Prof alisema atawasiliana na Halmashauri kuhusu suala hilo.

Mwenyekiti wa kijiji aliorodhesha kero ya umeme, barabara na Prof akaafiki na kuahidi kuzifanyia kazi. Prof. alitoa michango mbalimbali kwa vikundi vya wanawake na vijana waliosoma risala zao, jumla ya milioni mbili na nusu.Mkutano wa Kyota uliahirishwa baada ya kiza cha usiku kuingia, hata hivyo Prof. aliwasalimia wananchi waliomdubiri hadi usiku na kuahidi kurejea siku nyingine.

  • Taarifa via JamiiForums

Faini zilizopigwa na TFF kwa timu, wachezaji

Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kilichoketi jumanne ya tarehe 24, Machi 2015 jijini Dar es salaam, kimepitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu kwa wachezaji na vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom.

Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi Anold Bugado.

Mechi namba 108 iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, (Stand United dhidi Simba SC), wenyeji timu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika ishirini.

Mchezo namba 117 uliozikutanisha Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu ya Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kukataa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Nayo klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(11) baada ya timu yake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano kwenye mchezo dhidi ya Simba SC, huku mshambualiji wake Dany Mrwanda akipigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(12) kwa kutopeana mikono na wachezaji wa timu hiyo.

Mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga amepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 37(f) kwa kupiga teke meza ya mwamuzi wa akiba baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Suala la mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe kumshika korodani beki wa Simba SC Murshid Juuko limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu.

Kipa wa timu ya Simba SC, Ivo Mapunda amepewa onyo kwa kufunika tangazo la mdhamini wa Ligi Kuu (Vodacom) kwa kutumia taulo lake wakati wa mechi dhidi ya Yanga, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake iwapo atarudia kufanya tukio la aina hiyo.

Nao wachezaji Salum Abubakar wa Azam FC na Richard Maranya wa JKT Ruvu wamepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kila mmoja na kusimamishwa mechi tatu kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) kwa kupigana uwanjani kwenye mechi namba 123 ambapo walitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Klabu ya Kagera Sugar imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) baada ya timu yake kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo namba 130 dhidi ya Young Africans uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi namba 132 iliyozikutanisha Azam na Ndanda SC kwenye uwanja wa Chamazi, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) baada ya washabiki wake kuwamwagia maji na kuwarushia chupa za maji washabiki wa Azam.

Aidha klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi namba 134 dhidi ya timu ya Mbeya City, pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo huo.

Kiongozi wa Stand United, Muhibu Kanu amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu baada ya kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City kutokana na kutumia lugha ya kuhamasisha vurugu kwa timu yake na kupinga uamuzi wa refarii.

Katika mchezo namba 135 uliochezwa jijini Tanga na kuwakutanisha wenyeji Mgambo Shooting dhidi ya Yanga SC, Yanga SC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) kutokana na washabiki wake kuvamia uwanja baada ya mechi namba 135 dhidi ya Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Hawa punda wa mwaka huu, tutafika?


TRA yazungumza na Wafanyabiashara Kigoma kuhusu mgomo wa EFDs

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Mkoa wa Kigoma, Thadeo Joseph Kaliza, akiongea na Wafanyabiashara kwenye Ukumbi wa Kibo Peak, Mjini Kigoma, wakati wa kikao baina ya pande hizo mbili chenye lengo la kujadili changamoto za Wafanyabiashara na mustakabali wa Mashine za kutolea risiti EFDs.

WAFANYABIASHARA Mkoani Kigoma wameendelea kuililia Serikali kuhusu suala la Mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD’s), ambapo wameitaka serikali kubadili mfumo wa mashine hizo ili kutoa nafuu kwa mfanyabiashara kufanya biashara katika mazingira mazuri.

Akiongea katika kikao cha Wafanyabiashara na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Kigoma, Mwenyekiti wa muda wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Kigoma, Juma Rashid Chaurembo, amesema kuwa mfumo wa EFD’s bado sio rafiki kwa mfanyabiashara kutokana na utaratibu uliowekwa na serikali.

“Tumewahi kuzungumza kuhusiana na tatizo la mashine hizi za ki-electronic ni jinsi gani wafanyabiashara mpaka sasa tunahitaji mfumo huu ubadilike ili uweze kuwa rafiki kwa mfanyabiashara,”alisema Chaurembo.

Mbali na suala la mashine za EFD’s, wafanyabiashara hao pia wamelalamikia kupandishiwa kodi kwa asilimia 100% kwa mwaka mmoja na kuhoji taratibu za kuwapandishia kodi wafanyabiashara zinazingatia nini, huku wakimtuma Meneja wa TRA mkoa wa Kigoma kuiomba serikali ili walipe kodi ya awali wakati majadiliano juu ya ongezeko la kodi yakiendelea.

Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya Wafanyabiashara hao, Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma, Thadeo Joseph Kaliza, amesema kuwa hilo sio suala la TRA, bali ni suala la bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linatunga sheria.

“Zipo njia nyingi za kuhakikisha kwamba suala hilo linapatiwa ufumbuzi kwa njia za amani na serikali pia inajaribu kutafuta njia ya kuyapatia ufumbuzi masuala yanayohusu wafanyabiashara,”alisema Kaliza.

Aidha Kaliza, alisema kuwa kumekuwepo na hali ya kuchanganya taarifa ya kwamba mama ntilie nao wanatakiwa kununua mashine za EFD’s, na kusisitiza kuwa TRA wameweka majina kwenye mbao za matangazo, ya wafanyabiashara wanaopaswa kutumia mashine hizo.

“Kama tunajadili haya mambo, tujadili kwa maslahi mapana ya taifa. Hiyo kodi mnayolipa ambayo hata mimi mwenyewe nailipa, ndio inatuwezesha hata sisi watumishi wa serikali kuwepo hapa tulipo.”

Aliongeza kuwa msingi mkubwa ni kwamba mtu aliyepata mapato yanayostahili kulipa kodi alipe na kama kuna matatizo mengine yanayojitokeza yajadiliwe kwa njia ya amani.

Baadhi ya Wafanyabiashara wakimsikiliza Meneja wa TRA, Mkoa wa Kigoma, (hayupo pichani), wakati wa kikao na wafanyabiashara hao.

Katibu Mkuu Utumishi, George Yambesi astaaafu

Yambesi (kushoto) akikabidhi ofisi kwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Mkwizu

George D. Yambesi aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amestaafu. 

“Nimefurahi kufanya kazi na kila mmoja wenu katika kipindi chote hata pale rasilimali zilipokua chache kila mmoja wenu alijitahidi kufikia lengo la kuwahudumia wadau wetu” alisema Yambesi   ambaye amekua Mtumishi wa Umma kwa muda wa miaka 38.

Kesi ya Mtikila vs Mahakama ya Kadhi kusikilizwa Machi 30 yapangiwa Jaji


Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Machi 30, mwaka huu kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila, akipinga kitendo cha Serikali kupeleka Muswada bungeni wa kutunga sheria ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, kwamba uko kinyume na Katiba ya nchi.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Richard Mziray.

Katika kesi hiyo kupitia hati yake ya madai iliyopewa usajili namba 14 ya mwaka huu, Mtikila:

  1. Ameiomba mahakama itoe amri kwamba wale walio kwenye mamlaka ya Serikali akiwaemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Mary Nagu; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira na wenzao watoe sababu kwa nini wasifungwe kifungo kisichopungua miaka mitano endapo watashindwa kujieleza.
  2. Itoe amri ya vigogo hao kufungwa kifungo hicho kutokana na kuchezea Katiba ambayo ni sheria mama ya nchi. 
  3. Ameiomba mahakama itoe amri kwamba Mahakama ya Kadhi na Jumuia ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC) itangaze ni haramu kwenye ardhi ya Tanzania.
  4. Anadai kuwa suala la serikali kuandaa muswada wa Kiislamu na kuuwasilisha bungeni na kitendo cha Bunge kukubali ni sawa na uhaini. Anadai kuwa kitendo hicho ni sawa na uvunjifu mkubwa wa viapo walivyoapa viongozi hao wakati wa kushika madaraka ya umma na ni kinyume cha ibara ya 19 ya katiba ya nchi inayoeleza kwamba masuala ya dini na kuabudu yatakuwa ni ya mtu binafsi na kwamba uendeshaji wa mambo au taasisi za kidini hazitakuwa sehemu ya mamlaka ya nchi.
via NIPASHE

IPTL yajiondoa kwenye kesi ya kuzuia maazimio ya Bunge

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imejiondoa katika kesi ya kikatiba iliyoifungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupinga utekelezaji wa maazimio nane yaliyopitishwa na Bunge baada ya kushindwa kupinga mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa serikali.

Mbali na IPTL kampuni nyingine zilizohusika kupinga maazimio hayo ni Pan Africa Power Solution Ltd (PAP) mmiliki wa IPTL, Habinder Sethi, na mmiliki wa kamapuni VIP Engineering and Marketing Ltd, James Rugemalira.

Mbele ya Jaji Stella Mugasha, wakili wa upande wa utetezi, Gabriel Munyele, akisaidiana na wakili Joseph Sungwa, aliiambia mahakama kuwa hakuna haja ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo kwani zuio la muda waliloomba lilikuwa limeshaanza kutekelezwa na Bunge.

Upande wa serikali ukiongozwa na naibu Mwanasheria Mkuu, Gabriel Malata, ulidai kuwa ulipwe gharama za kesi kutokana na usumbufu uliofanywa na IPTL kung’ang’ania kupinga maazimio ambayo yalikuwa yalishaanza kutekelezwa.

Malata alidai kuwa IPTL inatakiwa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi zikiwamo uchapishaji wa majalada na muda waliotumia kuja mahakamani.

Aidha aliiomba Mahakama itumie vifungu vya sheria vinavyoelezea na masuala ya gharama za kesi kuiamuru IPTL kulipa gharama hizo.

Malata aliiomba mahakama itende haki ili kukomesha usumbufu unaofanywa na kampuni au watu wanaofungua kesi wakati wakijua hawawezi kushinda.

Jaji Mugasha aliitaka kampuni ya IPTL iwajibike kwa kulipa gharama za kesi kwa kushindwa kujiondoa mapema kupinga maazimio hayo, huku wakijua fika yalishaanza kutekelezwa.

Wakili Malata alisisitiza kuwa upande wa serikali utafuatilia ili kuhakikisha IPTL inalipa gharama za kesi kwa wakati mwafaka.

via NIPASHE

Govt Order! All bank computer servers be housed in country


All banks, both local and foreign, are to have their computer servers physically present in the country the government has ordered.

The development comes as part of ongoing government efforts to check movement of financial transactions and control cybercrime.

Giving the order yesterday in the House when winding up the proposed National Payment Systems Bill 2015 that was tabled on Monday, Deputy Minister for finance Adam Malima, said the decision is meant to allow the government access to the banks financial transactions.

Malima explained that, some banks have their serves located abroad which makes it difficult to access their database.

He also reassured the House that so far, all banks have responded positively to the directive with only two requesting for a time extension to comply.

He pointed out that the Bank of Tanzania (BoT), Financial Intelligence Unit (FIU) and Ministry of Finance are responsible to oversee the compliance and subsequent review and monitoring of the transactions.

Read more: IPP Media's The Guardian newspaper.

Gwajima ajisalimisha Polisi na kusema aliyoyatoa ni maneno ya mungu


Kwa mujibu wa taarifa ya ITV, kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima askofu Joseph Gwajima amefika katika kituo kikuu cha polisi cha jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na jeshi hilo kwa madai ya kutoa kauli, matusi na maneno makali kwa kiongozi wa kanisa katoliki nchini Muadhama Polycarp Kardinal Pengo.

Kundi la waanmdishi wa habari liliweka kambi katika kituo kikuu cha polisi cha jijini Dar es Salaam kutokana na wito wa jeshi la polisi kupitia vyombo vya habari kumtaka kiongozi huyo wa kanisa la ufufuo na uzima kufika kituoni hapo kwa mahojiano kwa madai ya maneno ya kashfa na matusi kwa kiongozi wa kanisa katoliki nchini.

Kutokana na adha ya foleni kubwa ya magari katika jiji la Dar es Salaam ilibidi kushuka katika gari lake na kutembea kwa miguu akiwa na walinzi wake kutoka katikati ya jiji hadi kituo kikuu cha polisi.

Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho alipokelewa kwa mahojiano ya awali kutoka kwa vyombo vya habari ambapo askofu Gwajima amesema maneno aliyoyatoa ni ya kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho kwa madai ya kukiuka msimamo wa viongozi wengine wa dini wa kuikataa mahakama ya kadhi.

Akijibu swali kuhusu sababu za kufanya hivyo badala ya kutumia maneno ya kistaarabu askofu Gwajima amedai kuwa maneno aliyoyatoa ni maneno ya mungu huku akishangazwa na wito wa polisi kwa kuwa maneno hayo hakuyatoa kwa jeshi la polisi bali kwa kiongozi mwenzie wa kiroho.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezagaa picha za video zikiambatana na maneno ya kashfa kwenda kwa kiongozi wa kanisa katoliki nchini Muadhama Polycarp Kardinal Pengo jambo lililofanya jeshi la polisi kumtaka kufika kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano zaidi.

JAMHURI YAA MUUNGANO WA TANZANIÀ

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE 27/03/201

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanza kumhoji Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kujisalimisha kama alivyotakiwa kufanya hivyo na Kamishana wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Askofu Gwajima alifika kituo kikuu cha Polisi saa nane na dakika kumi na tano mchana wa tarehe 27/03/2015. Mara baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Constantine Masawe ambaye alikuwa akisubiri kufika kwake.

Tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima ni pamoja na kumkashfu na kumtukana hadharani Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Taratibu za mahojiano zimekwishaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki yake anayemwamini au wakili wake.

Kama ilivyo kawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea na athari zake.

Baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili, ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hili ambalo sasa limepata mvuto mkubwa katika jamii.

Imetolewa na:
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Madereva 21 wa Majinjah wapewa mafunzo na vyeti NIT

Wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao na viongozi wa NIT.
Wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao na viongozi wa NIT.
Madereva 21 wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wamepatiwa mafunzo ya siku tatu katika Chuo cha Taifa cha Usafirishji (NIT).

Mafunzo hayo yalihusu Alama na Michoro ya barabarani,Sheria,Udereva wa Kujihami,Vyanzo vya Ajali jinsi ya kuzizuia,Huduma kwa Wateja na mawasiliano ya Barabarani.

Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu, Dk. Ethel Kasembe, aliwaambia madereva kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuepusha ajali za barabarani wakati wakiendesha mabasi yanayobeba abiria na kuwataka waendelee kupata elimu ya kutosha.

Alisema kuwa imani yake takwimu za ajali zitapungua na hata kwisha kabisa kama watazingatia waliyofundishwa na kuwasisitiza kwenda Chuoni hapo mara kwa mara kuendelea kupata elimu.

Pia alisisitiza kuwa watabadilika baada ya kumaliza mafunzo ya hapo na kuwa vyanzo vya ajali watavizuia kwa kutumia udereva wa kujihami wakiwa barabarani wakati wote.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka kushoto mstari wa mbele (wa pili) Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete, Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT), Dk. Ethel Kasembe, Mhandisi, Charles Kisunga na Dereva wa kike wa Majinjah,Grace Andrew.

Mwalimu wa Madereva, Daniel Kasisi, akifuatilia utoaji wa Vyeti kwa Wahitimu 21 wa Maginjah Logistics Ltd.

  • Taarifa kutoka kwa Mroki Mroki/Father Kidevu blog

Zuwena receives her 10m/= JayMillions promotion


Dar es Salaam, March 27, 2015: Zuwena Rajabu (22), a hairdresser from Tabata Segerea received her Tshs. 10m/- that she won through Vodacom Tanzania’s JayMillions promotion.

Zuwena was handed over her millions by fellow millionaire Ibrahim M. Ibrahim, a student at St. Joseph University who also won Tshs. 10m/- last week. The handover which took place in Tagata Segerea at the salon where Zuwena is employed was witnessed by her colleagues and the media.

Shortly after receiving her millions, Zuwena expressed her gratitude to God for answering her prayer. She had long been praying for the capital to start her own modern hair salon and cosmetics business.

“I especially thank Vodacom Tanzania for making my dream of becoming a successful entrepreneur come true. I am living proof that the JayMillions promotion is here to transform the impoverished from rags to riches,” said an ecstatic Zuwena

The JayMillions promotion was launched in January this year for 100 days and continues to transform the lives of ordinary, low-income Tanzanians. Todate, the promotion has produced one Tshs. 100m/- winner, four Tshs. 10m/- winners and 38 Tshs.1m/- winners.

Uwezo Madengede from Kilolo, Iringa landed the Tshs. 100m/- jackpot Mshindi wa milioni 100/- and apart from Zuwena Hyness Petro Kanumba from Rukwa, James Mangu from Mwanza and Deborah Stanley from Kimara Dar es Salaam also won Tshs. 10m/- of the 30bn/- Jay millions.

Speaking during the handover ceremony, Vodacom Tanzania’s Public Relations Manager Matina Nkurlu congratulated Zuwena saying the money has found the right winner who has smart goals for her winnings.

He urged all subscribers to grab the opportunity that JayMillions presents especially as the promotion draws to a close so they too can win by sending JAY to 15544. Subscribers can also send AUTO to 15544 for automated checking even if the customer does not have airtime and will be deducted Tshs 300/- only once they recharge.

Wabunge Dk Puja na Sebba walioteuliwa na Rais Kikwete wala kiapo

Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Dkt Grace Puja akila kiapo ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma,tarehe 27/03/2015.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Innocent Sebba akila kiapo ndani ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, tarehe 27/03/2015.

(picha: Anitha Jonas - Dodoma).

Mheshimiwa Sebba akizungumzia uteuzi wake alisema, "namshukuru sana Mheshimwa Rais Jakaya Kikwete kwa kuniteua na kwa sasa nina ahidi kuitumikia nafasi hii kwa uadilifu mkubwa."

Alisema yeye ni Muumini wa Kanisa la TAG na kabla ya kuteuliwa alikuwa akifanya kazi ya kusambaza neno la Mungu kwenye mikoa mbalimbali nchini pamoja na kujishughulisha na masuala ya uchapishaji akiwa na wenzake.

Tanzania yaikabidhi msaada kwa wahanga wa mafuriko Malawi

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick Luciano Tsere (kulia) akikabidhi Dawa za Binadamu na Mahindi kwa Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna anayeshughulikia masuala ya Maafa aktika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi ikiwa ni sehemu ya msaada wa Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa nchi hiyo kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo mwezi Januari 2015.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA YAIKABIDHI MALAWI MSAADA KWA AJILI YA WAHANGA WA MAFURIKO


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu kwa Serikali ya Malawi ikiwa ni msaada wake kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea nchini humo mwezi Januari mwaka huu na kusababisha maafa makubwa.

Msaada huo umekabidhiwa hivi karibuni na Mhe. Patrick Luciano Tsere, Balozi wa Tanzania nchini Malawi kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kupokelewa na Katibu Mkuu na Kamishna wa Idara ya Maafa, Bw. Paul Chiunguzeni kwa niaba ya Serikali ya Malawi. Aidha, msafara uliopeleka msaada huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), uliongozwa na Luteni Kanali B.B. Kisinda.

Katika hotuba yake fupi wakati wa makabidhiano, Balozi Tsere alisema kwamba msaada huo umetolewa na Tanzania ikiwa ni agizo kutoka kwa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kuguswa kwake na maafa hayo makubwa na pia kuitikia wito uliotolewa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Prof. Arthur Bingu Mutharika kwa Jumuiya ya Kimataifa na watu mbalimbali wenye uwezo kutoa msaada kwa wahanga hao wa mafuriko.

Aidha, Balozi Tsere alieleza kwamba, Malawi na Tanzania ni nchi jirani, marafiki na zinazoshirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo majukwaa ya kimataifa kama vile Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa.

“Hivyo, kwa kutambua mahusiano hayo ya ujirani mwema na udugu baina ya nchi hizi na watu wake, Tanzania imeona ni jambo jema kushirikiana na jirani yake katika kupunguza athari za maafa hayo kwa wahanga hao kwani siyo vyema kuona jirani yako amepatwa na matatizo na kisha unakaa kimya” alisema Balozi Tsere.

Mhe. Tsere aliongeza kwamba ingawa msaada huo hautoshelezi kutatua tatizo hilo kabisa bado utaweza kusaidia wahanga hao na kupunguza tatizo lililopo kwa kiasi Fulani.

Malawi ilikumbwa na mafuriko mwezi Januari mwaka huu. Mafuriko hayo yalisababisha maafa makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha, nyumba kuharibiwa na mazao mashambani kusombwa na maji. Kwa hivi sasa familia katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo hazina mahali pa kuishi na zinahitaji msaada wa chakula na kumekuwa na magonjwa ya mlipuko katika maeneo hayo kama vile kipindupindu.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

27 MACHI, 2015

Mhe. Balozi Tsere akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Chiunguzeni. Wengine katika picha ni Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Malawi nchini Tanzania, Ufulu Kalino (kushoto) akifuatiwa na Kanali Rugeumbiza kutoka JWTZ ambaye alikuwa msimamizi wa zoezi la usafirishaji wa msaada huo kutoka Tanzania na Luteni Kanali B.B. Kisinda (wa tatu kulia) kutoka JWTZ ambaye alikuwa Kiongozi wa Msafara pamoja na Makamanda wa JWTZ.


Machel Tarimo - Wasafirishaji mboga za Tanzania kwenda Ulaya


Video fupi iliyopachikwa hapo chini inamwonesha kijana Machel Tarimo, Mkurugenzi na mmoja kati ya watatu waanzilishi wa HomeVeg Tanzania Ltd. aliyekuwa katika studio ya ITV mwishoni mwa mwaka jana kwenye kipindi cha Vijana na Kilimo Biashara akielezea alivyofanikiwa kwenye kusafirisha mbogamboga kwenye masoko ya Ulaya. Kwa mawasiliano zaidi na Machel piga namba 0786683212.[video] Gaddafi Awadhi - Mfugaji wa samaki aelezea mradi wake

Finally, Doctors solve Medical mystery of how Malaria in brain kills

The effects of malaria in the brain are clear: A healthy brain, right, has many grooves and crevices. But when the brain swells up, left, these crevices smooth out. Courtesy of Michigan State University

The image showed massive swelling in the brain. At the time, researchers knew cerebral malaria could do this. They had seen it in autopsies.

But what they didn't know was how that swelling caused death. The answer was clear on the MRI image: The brain was so swollen that it got pushed out of the base of the skull and pressed against the brain stem.

"Unfortunately when that happens it presses on the respiratory center in the brain stem," Taylor says. "It's like flipping a light switch: Boom! They just stop breathing. And the child dies in 15 or 20 minutes without ventilation."

Taylor and her team imaged the brains of about 170 children. The ones who died were much more likely to have massive brain swelling that brought pressure on the brain stem. She and her team published the study Wednesday in the New England Journal of Medicine.

via The NPR.org