Mapitio ya magazeti katika Tv, Aprili 7, 2015
High Court throws suit over land in Kigamboni

THE High Court's Commercial Division has rejected the suit lodged by a resident of Kigamboni in Dar es Salaam, Elifaraja Tummino, opposing the sale of his plot to satisfy a decree of about 3bn/- in favour of Citibank Tanzania Limited.

Mr Tummino, who filed the commercial dispute through the power of attorney of one Leonardo Tummino, had claimed that he was the legal owner of the Plot Number 60 Block A at Kimbiji area.

He claimed that the sale would interfere with his lawful possession and render his family homeless. But in his ruling, Judge Haruna Songoro granted grounds of objection presented by defendants that Mr Tummino had no locus standi to file the case under power of attorney and all action taken by him to verify, sign and institute the suit were done with no filing any appointing instrument or its certified copy.

"It is my view that there is uncertainty on part of the defendants and even if the appointment of an agent was done because there is no any instrument or its certified copy filed in the registry which the court may act and rely on it," he said.

Other respondents in the matter apart from the Bank are MPS Oil Tanzania Limited, the company and officials Amran Talib and Asile Mousud and law firm, Apex Attorneys Advocates. Advocate Paschal Kamala from Kesaria and Company Advocates, represented the bank in the matter.

According to him, non filling of appointing instrument or its certified copy in court as required by law prejudice the rights of the defendants and even the court of knowing of Mr Tummino indeed was appointed by power of attorney.

The judge said that since the court actions of filing a plaint and subsequent steps were done by Leonardo Tummino without filing his instrument of appointment then his actions were legally wrong because the appointed instrument was never filed in court as statutorily required.

"Consequently, I hereby strike out the plaintiff's plaint for reason that it was instituted and pursued by so-called agent for about 10 months without filing in court original power of attorney or its certified copy and that was legally wrong," he ruled.

In the main suit, the plaintiff had accused the defendants of colluding to dispose his plot before he was paid a sum of 4.1bn/- being balance of purchase price agreed in a sale transaction negotiated in 2012.

He claimed that the defendants wrongly colluded to mortgage his plot to the bank while knowing that the agreed consideration has not been fully paid.

Therefore, he sought for declaration that the mortgage created by the defendants on the plot is null and void. The plaintiff had further requested the court to declare that the defendants were in breach of contract of purchase of the plot in question which is situated in Temeke Municipality and registered under Certificate Title number 59143.

Aliyenusurika Garissa asimulia alivyoishi saa 53 bila kujigusa

Cynthia
CynthiaCynthia Cherotich ni mmoja wa waliobahatika kuwa hai na kukwepa mauaji yaliyofanyika katika chuo Kikuu cha Garissa wiki iliypita. Mtangazaji wa runinga ya NTV, Victoria Rubadiri ameripoti taarifa ifuatayo ambapo Cynthia anaeleza kilichomtokea...

Kubenea: "Kesi ya Askofu Gwajima... hakuna usawa" na Makonda hana usafi wa kumhoji

Hakuna asiyemfahamu Makonda – mkuu mpya wa wilaya ya Kinondoni. Hakuna! Vitendo vyake; kauli zake na minendo yake, vinafahamika. Hana mamlaka ya kimaadili wala kisheria wa kusimamia anachokieleza.

Rekodi zake zipo na zinajulikana na wengi.

Kwanza, angalau Askofu Gwajima amesema, hatapoteza muda kwenda kumuona Makonda. Barua aliyoipata kutoka katika ofisi yake, hataijibu. Ni barua iliyomfedhehesha; itajibiwa na maombi ya mnyororo yanayoendelea.

Makonda hana mamlaka ya kisheria wala kimaadili ya kumuita Askofu Gwajima. Kama kuna kesi ya jinai, wanaopaswa kuchunguza na kushitaki, ni polisi. Siyo Makonda.

Lakini jambo ambalo liko wazi, ni kuwa ukipitia kauli za Askofu Gwajima dhidi ya Kardinali Pengo, unagundua kuwa alichokitenda ni madai. Siyo jinai; anayepaswa kushitaki au kulalamika katika kaei ya madai, ni Kardinali Pengo. Siyo Makonda, wala Sulemain Kova.

Pili, ni Makonda huyuhuyu, aliyeasisi vurugu, kulipa vijana, kuwaongoza na kisha kushambulia; naye kukiri kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Makonda alifanya vurugu hizo katika mdahalo ulioitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), tarehe 2 Novemba 2014. Ulifanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa katikati ya mjadala, ambako Jaji Warioba, kwa ustadi mkubwa alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine, juu ya maudhui na kilichomo katika Rasimu ya Pili ya Katiba, ambayo ilikuwa imesheheni maoni ya wananchi.

Mbali na vurugu za Makonda kuvunja mdahalo, lakini pia Jaji Warioba – waziri mkuu na makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri – alipigwa na Makonda na wafuasi wake. Karibu wote waliompiga na kumfanyia vurugu Jaji Warioba, ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wakati Makonda anapanga kumshambulia Jaji Warioba, alikuwa anajua kuwa alikuwa anavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inayoruhusu uhuru wa kutoa maoni na kukusanyika.

Aidha, katiba hiyohiyo inatoa uhuru wa Kardinali Pengo kutoa maoni yake kuhusu msimamo wa makanisa; sawa na Gwajima alivyotoa maoni yake kuhusu Kardinali Pengo.

Lakini hata kama Gwajima angekuwa na makosa, Makonda hana mamlaka ya kimaadili wala kisheria ya kusikiliza kesi dhidi ya kiongozi huyo wa kiroho.

Si hivyo tu: Ni Makonda aliyekuwa akiporomosha mvua ya matusi dhidi ya Edward Lowassa na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya kidini. Amekuwa akimgombanisha Lowassa na Rais Jakaya Kikwete; Lowassa na chama chake na Lowassa na vyombo vya habari.

Hakuwahi kuhojiwa na jeshi la polisi wala kinachoitwa, “Kamati ya ulinzi na usalama.” Bila shaka alikuwa kazini. Alikuwa anawatumikia waliomtuma.

Hata hivyo, kesi ya Askofu Gwajima, imerejea yaleyale ambayo yamekuwa yakielezwa kwa zaidi ya miaka 15 sasa; hakuna usawa katika taifa. Kumesheheni ukaburu.

Kuna orodha ndefu ya watu wakikashifu mtu mwingine, wanapongezwa kwa kupewa vyeo. Lakini wengine wanatafutwa kwa marungu, kuzuiliwa na kufunguliwa mashitaka.

[video] Garissa attack: Cynthia, who lived to tell her tale
Cynthia Cherotich was certainly one of the lucky ones, who managed to walk off the Garissa University College campus after Al Shabaab militants massacred over 140 of her colleagues. Victoria Rubadiri (NTV) with her story, in the video above, of unbelievable resilience and hope to live another day.

Unlikely terrorist: An A- student; Lawyer; Son of a gov. official

Abdirahim Mohammed Abdullahi
Abdirahim Mohammed Abdullahi

The son of a Kenyan government official has been identified as one of the gunmen who attacked a Kenyan college where 148 people were killed, authorities said Sunday.

Abdirahim Mohammed Abdullahi, one of the Islamic extremists who attacked Garissa University College, was the son of a government chief in Mandera County, Interior Ministry spokesman Mwenda Njoka told The Associated Press.

The chief had reported his son missing last year and said he feared that he had gone to Somalia, said Njoka.

All four attackers were killed by Kenyan security forces on Thursday.

Somalia's al-Shabab Islamic militants claimed responsibility for the attack on Garissa college Thursday saying it is retribution for Kenya deploying troops to Somalia to fight the extremist rebels.
Fundi abwaga gari la mteja mtoni

Gari likiwa ndani ya mto kwenye daraja la Buluba lisilokuwa na kingo hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kwani mto ni mkubwa hivyo kuhatarisha maisha ya watumiaji wa daraja hilo hasa kipindi cha mvua na nyakati za usiku. Watu wengi wamekuwa wakitumbukia katika mto huo kwenye daraja hilo na jingine lililopo jirani na Moleka Hotel ambako mto huo pia unapita.

Kumetokea ajali ya aina yake jioni ya Jumatatu, Aprili 6, 2015 majira ya saa 12 mjini Shinyanga ambapo gari dogo aina ya Suzuki Escudo lenye namba za usajili T128 ASZ (pichani) ikiendeshwa na mtu mmoja aliyejukana kwa jina la Ezekiel, fundi magari, limetumbukia katika daraja lisilo kuwa na kingo la Buluba katika barabara ya Magadula, linayotenganisha kata ya Ngokolo na Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema dereva wa gari hiyo ambaye ni fundi magari alikuwa katika mwendo kasi hali ambayo ilimshinda gari na kutumbukia kwenye mto unaopita katika daraja hilo.

  • Picha na taarifa via Malunde1 blog

Rai ya Waziri Membe kwa Watanzania alipotembelea yatima na wazee katika nyumba ya Furaha na Amani

Waziri Membe akiwalisha watoto keki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wasiojiweza waliopo kwenye jamii wakiwemo watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

Waziri Membe ametoa wito huo hivi karibuni alipotembelea Kituo cha Kulelea watoto yatima na wazee cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Membe alisema kuwa katika jamii za watu kumekuwa na makundi ambayo yanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamejaaliwa kipato kidogo na afya. Alisema kuwa ni wajibu wa watu wa aina hiyo kuwasaidia wale wanaohitaji kama vile watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

Waziri Membe ambaye alikuwa amefuatana na Mke wake, Mama Dorcas Membe aliguswa sana na historia ya baadhi ya watoto yatima aliowatembelea kituoni wakiwemo wale waliotupwa jalalani na kuokotwa wakiwa kwenye hali mbaya.

“Lipo kundi linalopata mateso na matatizo katika jamii zetu tunazoishi. Ni vizuri Watanzania tukajenga utamaduni wa kutembelea sehemu kama hizi ili kujionea wenyewe hali halisi.

Kwa kweli ni hali ya kusikitisha kuona baadhi ya watoto walitupwa na kuokotwa jalalani na wengine tayari wakiwa wamepata majeraha ya kung’atwa na mbwa. Hivyo ni wajibu wetu sote kuwasaidia kwa chochote kidogo tunachojaaliwa kupata”, alisema Waziri Membe.

Aidha, Mhe. Membe aliwapongeza na kuwasifu Masista wa Shirika la Mama Theresa ambao ndio wasimamizi wa kituo hicho kwa kuwalea watoto, vijana na wazee wenye matatizo mbalimbali na kuwaomba waendelee kujipa moyo katika kazi hiyo kwani ni njia moja wapo ya kumtumikia Mungu.

Awali akimkaribisha Waziri Membe kituoni hapo, Sista Mkuu wa Kituo hicho, Sista Mary Bakhita, alisema kuwa wamefurahia sana ziara hiyo ya Mhe. Membe hususan katika Siku Kuu ya Pasaka kwani ni faraja kubwa kwao kwa Watoto na Wazee wanaolelewa kituoni hapo.

“Tumefarijika sana kula pasaka pamoja nawe Mhe. Waziri. Watoto na Wazee hawa wanajisikia vizuri pale wanapotembelewa na tunaomba uendelee na moyo huo huo,” alisema Sista Bakhita.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Membe na familia yake walitoa zawadi mbalimbali kwa kituo hicho ikiwemo vyakula, sabuni na fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali kituoni hapo.Mama Dorcas Membe akiwalisha watoto keki.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akimtazama kwa furaha mmoja wa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Kigogo Mburahati, Jijini Dar es Salaam. Waziri Membe alikitembelea kituo hicho wakati wa Siku Kuu ya Pasaka.


Mhe. Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe wakipata maelezo juu ya watoto waishio katika kituo hich kutoka kwa Sista Mary Bakhita.

  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Cuthbert Kajuna/KajunaSon blog.

Picha za Ali Kiba alivyochekecha na kucheketua Dar Live

Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live iliyokuwa ikipigwa kwa 'Live Band'.

MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake waliojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live kwenye Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Ali Kiba akiwa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba waliangusha bonge la burudani huku wakiimba nyimbo zao zote kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’.

Shoo hiyo ilisindikizwa na Isha Mashauzi akiwa na Mashauzi Classic, Msaga Sumu na Pamela Daffa 'Pam D' ambao walitoa burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo.Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakichekecha na kucheketua.Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live Sikukuu ya Pasaka.Mashabiki wa Ali Kiba wakicheza staili mpya ya Chekecha Cheketua.Shabiki wa Ali Kiba akiwa na tisheti kuonyesha kuwa yeye ni 'Team Kiba'.Ali Kiba akizidi kulitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.Wapiga vyombo wa Ali Kiba wakiwa kazini.Mwanamuziki Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live Sikukuu ya Pasaka.Nyomi ikimpa shangwe Msaga Sumu.
Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic wakilishambulia jukwaa la Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live.Isha Mashauzi akifanya yake stejini.Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Pamela Daffa 'Pam D' akiwarusha mashabiki wa Dar Live kwa songi lake kali la Nimempata.Vijana wa Pam D wakifanya yao stejini.Pam D akizidi kuwadatisha mashabiki.
  • Taarifa hii tumeshirkishwa na Global Publishers

Filikunjombe asherehekea Pasaka na wagonjwa Ludewa

Paroko wa kanisa la anglikana ludewa Andrew Hiluka kushoto akilishwa chakula na mbnge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kulia huku mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akimsaidia kushika sahani ya chakula jana baada ya mbunge huyo na mkuu wa mkoa kuwaandalia chakula wagonjwa wote wa hospitali ya wilaya ya Ludewa

MKUU wa mkoa wa Njombe Dk Rehema Nchimbi amempongeza mbunge Ludewa mkoani Njombe Bw Deo Filikunjombe kwa kutumia sikukuu ya pasaka kuwaandalia chakula watu wenye matatizo wakiwemo wafungwa wa gereza la Ludewa na wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa huku akiagiza Halmashauri ya Ludewa kuanzisha huduma ya chakula kwa wagonjwa .

Dk Nchimbi alitoa pongezi hizo jana wakati alipoungana na mbunge huyo na viongozi mbali mbali wa mkoa na wilaya ya Ludewa kushiriki hadla hiyo ya mbunge kula chakula pamoja na wagonjwa na  kuwapa misaada mbali mbali kama ulivyoutaratibu wake kwa kila sikukuu kula na wagonjwa na wafungwa.

Alisema utaratibu unaotumiwa na Mbunge huyo ni utaratibu mzuri ambao unapaswa kuigwa na wabunge wengine nchini kwa kuyatembelea makundi mbali mbali ya kijamii wakati wa sikukuu ama siku nyingine badala ya kusherekea sikukuu kwa kufanya anasa.

'Kweli ni jambo la kumpongeza sana mbunge Filikunjombe kwa huu utaratibu ambao amekuwa akiufanya binafasi niliposikia mbunge anakuja kufanya jambo hili kubwa la kula na wagonjwa pasaka niliamua kufunga safari na mimi kuja kushiriki zoezi hili na kumtia moyo zaidi mbunge kwa hili si wabunge wote ambao wanakawaida ya kutembelea na kuwafariji wagonjwa na wafungwa kama hivi 'alisema mkuu huyo.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa katika kumuunga mkono mbunge Filikunjombe kwa wazo hilo zuri kwa upande wake anachangia ngunia 5 za mahindi ili kuwaanzishia wagonjwa wanaofika kujifungua huduma ya chakula kwa kipindi chote wawapo hospitalini hapo kama njia ya kuepusha wagonjwa kuwa na mawazo ya wapi watapata chakula.

Kwani alisema si wagonjwa wote wanaofika kusubiri muda wa kujifungua hospitalini hapo wanauwezo wa kiuchumi hivyo kuiagiza halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuangalia uwezekano wa kuchangisha chakula kwa wananchi ili kusaidia huduma ya chakula kwa wagonjwa.

Alisema wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla hauna shida ya chakula kama ilivyomikoa mingine hivyo uwezekano wa kuanzisha utaratibu wa kutoa chakula kwa wagonjwa unawezekana.

Akishukuru kwa msaada huo wa chakula kwa niaba ya wagonjwa wengne waliolazwa hospitalini hapo paroko wa kanisa la anglikana ludewa Andrew Hiluka alisema kuwa alichokifanya mbunge huyo ni moja kati ya baraka kubwa kwake na kuwa baadhi ya wanasiasa wanapoteza nafasi zao kutokana na kuwa na roho mbaya na uchoyo kwa wale waliowachagua.

Kwani alisema Ludewa imepata kuwa na wabunge zaidi ya watano ila wakati wa sikukuu kama hizo wabunge hao walikuwa wakitoka nje ya Ludewa ama kujifungia na familia zao kula sikukuu tofauti na Filikunjombe ambae amekuwa ni mbunge wa aina yake kwa siku ya sikukuu kuandaa chakula cha pamoja na wagonjwa kwa kula nao chakula wodini.

Paroko Hiluka alitoa wito kwa wananchi wa jimbo la Ludewa kuendelea kumchangua kwa miaka mingine zaidi mbunge Filikunjombe kwani ametambua mahitaji sahihi ya wana Ludewa kwa kusaidia maendeleo ya jimbo hilo pia kuwagusa wote wenye matatizo mbali mbali ambao ni nje ya ahadi zake za ubunge.

Alisema ni kipindi cha Filikunjombe kasi kubwa ya maendeleo imeonekana kwa kila mwananchi wa wilaya hiyo na nje ya wilaya lakini pia ni mbunge pekee kusomesha sekondari watoto yatima zaidi ya 700 katika wilaya hiyo kwa kila mwaka huku wabunge waliopita labda aliyejitiahidi kusomesha basi haikuzidi watoto 2 kwa miaka yote mitano.

Nae mbunge Filikunjombe alisema kuwa utaratibu huo wa kula chakula na wagonjwa amekuwa akiufanya kila mwaka toka alipoingia madarakani mwaka 2010 na kuwa iwapo wananchi wa jimbo hili watamchagua ataendelea kuwaletea maendeleo lakini pia kuwasaidia watu wenye matatizo kwani anachoamini na kuendelea kuamini kuwa wazima na wagonjwa wote ni wapiga kura wake na kuwa furaha yake ni kuona wagonjwa wanapona ili waweze kumchagua tena.Mbunge wa Ludewa Filikunjombe akiongoza msafara wa viongozi mbali mbali akiwemo mkuu wa mkoa wa Njombe Dk Nchimbi kutembelea wagonjwa hospitali ya wilaya ya LudewaFilikunjombe na Rc njombe wakitoa msaada wa vitu mbali mbali kama sabuni , mafuta na taulo kwa wagonjwa waliyelazwa hospitali ya wilaya ya Ludewa jana

Watoto wa Filikunjombe wakishirikiana na Rc njombe kutoa msaada kwa wagonjwa


Dk Nchimbi na filikunjombe wakitoa maada wa chakula na vitu mbali mbali kwa mgonjwa


Mtoto wa Filikunjmbe akitoa maada wa chakula kwa mgonjwaRC wa jombe (kulia) akimlisha chakula mgonjwa huku Flikunjombe akimsaidia kushika bakuliFilikunjombe akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Nchimbi wakati akizungumza na wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya LudewaKatibu mwenezi Mkoa wa Njombe, Honoratus Mgaya na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Nchimbi wakitoa chakula kwa wagonjwaMkuu wa Wilaya ya Ludewa, Bw Anatory Chowa akitoa maada wa vitu mbali mbali kwa mgonjwa hospitali ya LudewaFilikunjombe akiwa amempakata mtoto katika hospitali ya wilaya ya Ludewa


Filikunjombe akitoa msaada wa chakulaMkuu wa mkoa njombe akila chakula na mgonjwaFilikunjombe akila chakula na mgonjwa

DC Ludewa akila chakula na mgonjwaMwanahabari wa TBC, Irene Mwakalinga akila pasaka na wagonjwa hospitali ya wilaya ya LudewaMbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe wa pili kulia akishiriki kula chakula na wauguzi pamoja na mmoja kati ya wanawake waliolazwa katika wodi la wanawake waliojifungua kwenye hospitali ya wilaya ya Ludewa wakati wa sikukuu ya pasakaMwalimu DOMINIC HAULE akila chakula na wagonjwa


FILIKUNJNOMBE KATIKATI AKILA CHAKULA NA MUUNGUZI NA MGONJWAZIARA YA MBUNGE FILIKUNJOMBE NA RC NJOMBE KWENDA KULA CHAKULA NA WAGONJWAFILIKUNJOMBE AKIFURAHI WAKATI WAUGUZI WA WAGONJWA WAKIMSHANGILIA

FILIKUNJOMBE AKILA CHAKULA NA MGONJWA  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Francis Godwin/MatukioDaima blog