Tanzania National Nutrition Survey 2014: Sharp drop in childhood stunting


DAR ES SALAAM, Tanzania, 10 April 2015 – The results of a National Nutrition Survey released in Tanzania show that between 2010 and 2014, chronic malnutrition – stunting, or low height for age – among children under five in the country fell from 42 per cent to 35 per cent.

"Undernutrition, and especially stunting, is one of the silent crises for children in Tanzania," said UNICEF Representative in Tanzania Dr Jama Gulaid. "Malnutrition has severe consequences. It blunts the intellect, saps the productivity of everyone it touches and perpetuates poverty. The success we are celebrating today is due to increased political commitment and improved coordination mechanisms for nutrition since 2011.”

In 2011, Tanzania became a key partner in the major global initiative called the Scaling Up Nutrition (SUN) movement, which is bringing much needed focus and investment for nutrition in a number of countries. President Jakaya M. Kikwete became a member of the high-level international SUN Lead Group and played a key role in the promotion of the nutrition agenda at the international level and in Tanzania.

“These results are very encouraging. The hidden crisis of chronic malnutrition is robbing thousands of our children of their full potential and hampering the social and economic progress of Tanzania”, said Mr. Obey Assery, SUN Focal Person for Tanzania.

The Government of Tanzania launched a five-year National Nutrition Strategy (2011-2016) with an Implementation Plan which guides actions by ministries, departments, agencies and local government authorities, as well as development partners.

The Government is also tracking investments in nutrition. In 2014, The Ministry of Finance conducted the first Public Expenditure Review of the nutrition sector and first Joint Multi-sectoral Review of Nutrition analysing the implementation of the first three years of the National Nutrition Strategy.

“Despite the achievements, child malnutrition remains an important challenge in Tanzania. All of us here in the country – government, communities, UNICEF and others – must redouble our efforts to combat this problem,” Dr Gulaid added.

According to estimates, Tanzania still has more than 2.7 million children under five who are stunted. More than 430,000 children suffer from acute malnutrition. Among these are some 100,000 diagnosed with severe acute malnutrition, which means they have a high risk of dying if they do not receive appropriate treatment.

Stunting can permanently impair a child’s physical and cognitive development, trapping them into a cycle of poverty and inequity. The damage often leads to poorer school performance, leading to future income reductions of up to 22 per cent on average. As adults, they are also at increased risk of illness and disease.

The National Nutrition Survey was conducted in 2014 by the Tanzania Food and Nutrition Centre of the Ministry of Health and Social Welfare and the Nutrition Unit of the Zanzibar Ministry of Health, with the technical and financial support of UNICEF, Irish AID and the United Kingdom’s Department for International Development (DFID).

###

About UNICEF
UNICEF promotes the rights and wellbeing of every child, in everything we do. Together with our partners, we work in 190 countries and territories to translate that commitment into practical action, focusing special effort on reaching the most vulnerable and excluded children, to the benefit of all children, everywhere. For more information about UNICEF and its work visit: www.unicef.org

Follow UNICEF Tanzania on Facebook

For more information, please contact: Sandra Bisin, UNICEF Dar es Salaam, Tel: +255 22 219 6634, Mobile: +255 787 600079, [email protected]

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Aprili 13, 2015

Gwajima "mimi si tajiri"

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa akiiingia ndani ya helikopta kuashiria kuizindua rasmi kwa safari mbali mbali za kihuduma ya kiroho, itakayotumiwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amesema yeye si tajiri kama inavyodhaniwa, bali alichonacho ikiwa ni pamoja na nyumba, magari na helikopta ni baraka tu za Mungu, lakini kama ni utajiri, anatarajia siku moja utamshukia.

Aliyasema hayo jana wakati akihubiri kanisani kwake Kawe, Dar es Salaam, ambako alisema anawashangaa watu wanaomfuatilia maisha yake huku wakisema yeye ni tajiri mkubwa.

“Wanaodai mimi ni tajiri wana wivu tu na wananionea, mimi si tajiri, bali ni masikini kama walivyo masikini wengine. Natarajia kutajirika hapo baadaye waumini wangu wakiwa matajiri, siwezi kutajirika kama waumini wangu bado ni masikini, nitatajirika pamoja nao,” 
alisema Gwajima.

Kuhusu mgogoro unaoendelea baina yake na Jeshi la Polisi, Askofu Gwajima alisema yeye anauona kama ni vita vya kiroho na hivyo ataendelea kumwomba Mungu ili amsaidie kupambana na kilichopo mbele yake na anaamini kuwa atashinda vita hiyo kwa uweza wa Mungu anayemtegemea.

“Mungu wangu na awasamehe wote wanaonituhumu kuwa mimi ni tajiri na kuamua kudhoofisha huduma, nasema huduma yangu haitakufa kamwe na wala hatutayumba katika mipango yetu ya kuhubiri injili. Tutapigana kwa uweza wa Mungu na tutashinda kama alivyosema kuwa tutapigana pamoja naye na tutashinda,” 
alisema Gwajima.

Akizungumzia afya yake, Askofu Gwajima alisema kwa sasa anaendelea vizuri na anaweza kusimama na kutembea, kuhubiri kama ilivyokuwa hapo awali na hatarajii kurejea tena kwenye kiti cha baiskeli ya magurudumu matatu bali atasimama imara daima.

Kuhusu kupeleka nyaraka kadhaa anazotakiwa aziwasilishe polisi siku ya mahojiano Aprili 16, mwaka huu, Askofu Gwajima alisema suala hilo bado wanasheria wake wanalishughulikia na wataendelea kufuata taratibu zote zinazotakiwa na jeshi hilo.

Gwajima anatakiwa kuwasilisha nyaraka muhimu za hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa, hati ya umiliki wa helikopta, hati ya nyumba anazomiliki, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake pamoja na hesabu za fedha za kanisani kwake zinazohusu mapato na matumizi.

Nyaraka zingine ni majina ya Bodi ya Udhamini wa kanisa, mpiga picha za video kanisani kwake siku ya ibada na shughuli zingine za kanisani hapo pamoja na waraka wa Maaskofu uliosomwa makanisani ambao Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alioupinga na kusababisha yeye kumkashifu kiongozi mwenzake huyo wa dini.

Akionekana kuwa makini sana na lugha anayotumia wakati wa kuhubiri, Gwajima aliwaomba waumini wake waendelee kufuatilia kila sehemu na kuchunguza mambo yote mabaya yanayosemwa juu yake na kanisa lake na kuyaripoti kwake au kwa uongozi wa kanisa ili wayafanyie kazi mara moja kabla hayajaleta madhara.

“Nawaombeni sana mfuatilie kila chanzo cha habari na kuchunguza mambo yote yanayosemwa juu yangu au kuhusu kanisa na kuyaleta mara moja hapa kanisani ili tuyafanyie kazi kabla hayajaleta madhara makubwa,” “tuendelee kuwa na umoja katika kipindi hiki ambapo shetani anataka kupigana nasi ili tuweze kushinda. Tukifarakana hatutaweza bali tukiwa kitu kimoja tutasonga mbele na kuwa huru”.

Wakati akikana kuwa tajiri, mwanzoni mwa mwaka jana alifanya mahojiano na gazeti hili (HabariLeo) na kukiri Mungu anambariki, ndiyo maana mambo yake yanamnyookea. Aliyasema hayo alipokuwa anazungumzia mpango wake wa kununua helikopta kwa ajili ya huduma za injili ndani na nje ya nchi.

Alikiri kutokana na utajiri anaosema unatokana na baraka za Mungu, anamiliki jumba la ghorofa nne eneo la Mbezi Beach katika Manispaa ya Kinondoni. Pia amewanunulia wachungaji wake 40 magari ya kutembelea kwa bei tofauti, yakiwemo ya chini ya Sh milioni 10 na mengine ya zaidi ya Sh milioni 20.

“Ni kweli nimewanunulia magari, unajua moja ya misingi yangu ya maisha ni kwamba, mimi siwezi kuishi maisha mazuri, wakati wachungaji wangu wanadhalilika, nimewanunulia magari karibia 40. Lakini nina wachungaji wa ngazi mbalimbali, hawa ni wale wa juu, wengine wachungaji wadogo wapo zaidi ya 670, hawa ni watenda kazi muhimu na wanatofautiana kwa ngazi zao, ndio maana kazi ya Mungu inasonga mbele hata nisipokuwepo,” 
alisema Gwajima.

Mbali na magari ya wachungaji, pia amenunua mabasi 20 ya kubeba waumini wake kutoka na kwenda kanisani, yakianzia maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Alithibitisha kuwa, kila moja limegharimu kati ya Sh milioni 80 na Sh milioni 100.

Pamoja na uwezo mkubwa wa kifedha alionao, Gwajima anayemiliki magari kadhaa likiwemo la kifahari aina ya Hummer lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200, anasema kamwe hatageukia biashara kwa kuwa hatafuti faida, bali kumtumikia Mungu ambaye naye anampa baraka za kipato alichonacho kwa sasa.

  • via gazeti la HABARI LEO

Mobile phones mean success for female students in Tanzania


by Aid for Africa

At a rural girls’ school in northern Tanzania, staff know that education is the first step to empowering their students. Ask them what the second step is, and they will say mobile phones.

When a woman has a mobile phone in rural Tanzania and other African countries, she has access to a number of tools and services that will help her succeed in life, according to Laura DeDominicis , executive director of Nurturing Minds — an Aid for Africa member. “A phone allows her to make secure banking transactions, monitor customer markets for her business, track changing weather patterns for her crops, and receive health care reminders and updates.”

At the SEGA School in Morogoro, Tanzania, each eleventh-grade graduate receives a mobile phone, thanks to Kidogo Kidogo, an organization that sells iPhone cases. Kidogo Kidogo is Swahili for “little by little.” When they sell two phone cases, Kidogo Kidogo donates a mobile phone, a phone number and 5,000 Tanzanian schillings of mobile credits to a woman in Tanzania.

Kidogo Kidogo has partnered with Nurturing Minds for two years to provide phones for all of their students graduating from the first level of secondary school, which is equivalent to eleventh grade in the U.S. system. Some of the graduates will continue their education in grades twelve and thirteen. Others will start businesses or attend vocational schools. In all cases, a phone is essential to success.

Nurturing Minds helps educate Tanzanian girls who are poor, marginalized and at-risk of becoming involved in exploitative forms of child labor. It supports the residential SEGA school for motivated Tanzanian girls who otherwise are unable to attend school due to extreme poverty.

SEGA graduate Rhoda was one of the students in Tanzania who passed the exams necessary to attend the last two years of “advanced level” secondary school. She is studying physics, chemistry and biology. Rhoda uses her phone to stay in touch with her family and friends and to receive money from home to pay for books and school fees. After graduation, Rhoda hopes to study business at a Tanzanian university and then to start a business of her own.

Other SEGA graduates are preparing for college and using their mobile phones to stay in contact with their support systems, including family, friends and SEGA teachers, which will ensure they achieve their goals.

Learn more about why educating girls is key to ending poverty here.

Aid for Africa is an alliance of 85 U.S.-based nonprofits and their African partners who help children, families, and communities throughout Sub-Saharan Africa. Aid for Africa’s grassroots programs focus on health, education, economic development, arts & culture, conservation, and wildlife protection in Africa.

Malawi orders police to shoot in a bid to protect albinos

LILONGWE (Thomson Reuters Foundation) - Malawi police are under orders to shoot anyone attacking albinos in the latest bid to crack down on a rising wave of violence against albinos in East Africa whose body parts are prized in black magic.

At least 15 people with albinism, mostly children, have been killed, wounded, abducted or kidnapped in East Africa in the past six months with a marked increase in Malawi, Tanzania and Burundi, according to the United Nations.

U.N officials said at least six attacks on albinos were reported in Malawi in the first 10 weeks of 2015 compared to four incidents over the previous two years and gangs were roaming the southern district of Machinga hunting for victims.

Tanzania has banned witchdoctors to try to stop the trade in body parts used in spells and charms claiming to bring luck, love and wealth, and Burundi is trying to safeguard albinos by accommodating them in housing with police protection.

The latest order came from Malawi's Inspector General of Police Lexen Kachama who instructed police to shoot any "dangerous criminals" caught abducting albinos, according to local media reports.

"Shoot every criminal who is violent when caught red-handed abducting people with albinism," said Kachama, adding that he was ordering police to use weapons in proportion to the crime.

"We cannot just watch while our friends with albinism are being killed like animals every day .. We do realise that these people are ruthless, have no mercy and therefore they need to be treated just like that."

A similar remark was made by Tanzania's Prime Minister Mizengo Pinda in 2009 when he urged citizens to kill anyone on the spot if they were found with the limbs or organs of albinos who lack pigment in their skin, hair and eyes.

Albino rights group have called for greater protection of albinos but said killing suspects was not going to deter criminals offered large sums of money for securing body parts as they were likely to still take the risk for the promised reward.

Witchdoctors will pay as much as $75,000 for a full set of albino body parts, according to a Red Cross report.

Vicky Ntetema, executive director of Under The Same Sun, a Canadian non-profit organisation defending albino rights, said campaigners wanted justice for those people kidnapped, mutilated and murdered.

"But we have to remember that all those goons caught red-handed ... are small fish - agents and executors of the big sharks out there," she said.

"Killing them on the spot is not going to help us catch the inducers, those with money to hire these gangs who continue to terrorize innocent people with albinism and their families."

Ntetema urged police in Tanzania, Malawi and Burundi to quiz suspects to get information about the witchdoctors who use albino body parts and their clients.

"We all need to unite and find the culprits who are hiding behind the killers ... Why would people kill albinos if they were not asked to get their organs by someone?" she said.

The plight of people with albinism has worsened in East Africa in recent years, according to U.N. and police figures, with concerns that an election in Tanzania this year will prompt more attacks as politicians seek luck at the ballot box.

The U.N. High Commissioner for Human Rights Said Zeid Ra’ad Al Hussein last month urged African governments to combat impunity for crimes against people with albinism.

Albinism is a congenital disorder which affects about one in 20,000 people worldwide, according to medical authorities. It is more common in sub-Saharan Africa and affects about one Tanzanian in 1,400.

Tanzania Comoros Trade Summit: Membe to lead Delegation


Minister of Foreign Affairs and International Cooperation Hon. Bernard K. Membe will lead the Tanzania Delegation to the Union of Comoros. This Summit will create Opportunities (fursa) for Tanzanian Businesses to trade with Comoros and vice versa.

About Summit | About Comoros | Delegates | Exhibition | FAQS

CONTACTS: Summit: +255767123055 | Delegate: +255785630007 | Exhibition: +255787747918

Rais Kikwete ahudhuria Sherehe za Uaskofu Shinyanga

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu wakati wa ibada ya kumweka wakfu iliyofanyika katika kanisa kuu la Parokia ya Mama mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga, Jumapili, Aprili 12, 2015.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Aprili 12, 2015 ameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Shinyanga, kuhudhuria Ibada rasmi ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu mpya wa Jimbo hilo, Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu.

Rais Kikwete amewasili kwenye Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga kiasi cha saa sita unusu mchana kwa ajili ya Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi 38, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Rais wa Mabaraza ya Kipapa na Katibu Mwambata wa Uenezaji Injili Ulimwenguni Askofu Mkuu Protase Rugambwa kutoka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Askofu Sangu ambaye amewekwa wakfu na kusimikwa kwenye Siku ya Huruma ya Mungu Duniani anakuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga na anachukua nafasi iliyoachwa wazi tokea Novemba 6, 2012, wakati aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo, Baba Askofu Aloysius Balina alipofariki dunia.

Kwa miaka karibu mitatu, jimbo hilo limekuwa chini ya Usimamizi wa Kitume wa Askofu Mkuu Yuda Tadei R’uaichii wa Jimbo Kuu la Mwanza.

Askofu Sangu mwenye umri wa miaka 52 baada ya kuwa amezaliwa Februari 19, mwaka 1963, katika Kijiji cha Mwazye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, alipata daraja la upadrisho Julai 3, mwaka 1994. Wakati anateuliwa na Baba Mtakatifu Francesco kuwa Askofu Februari 2, mwaka huu wa 2015, alikuwa na daraja la Mosinyori.

Akikabidhi Jimbo hilo kwa Askofu mpya, Askofu Mkuu R’uaichii amesema kuwa Jimbo la Shinyanga ni moja ya majimbo makubwa zaidi ya Kanisa Katoliki nchini, likiwa na kilomita za mraba karibu 30,000 na waumini Wakatoliki wanaokaridiwa kufikia 300,000 katika Mkoa ambao idadi kiasi ya wakazi wake bado wanaamini imani za jadi.

Amesema kuwa Jimbo hilo lina parokia 29, mapadre wa Jimbo 52, mapadre wa Kitawa 18 na hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa na jumla ya mapadre 70 na “jeshi kubwa” la watawa 70.

Kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na viongozi wengi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Lufunga, Askofu Sangu amepewa zawadi ya sh milioni 18, fimbo ya kiuchungaji na ng’ombe 10 wa maziwa na Wakatoliki wa Jimbo hilo.

Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam jioni ya leo baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo.

Rais Kikwete akitoa salamu zake za pongezi muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya kumweka wakfu askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu katika Kanisa Kuu Parokia ya Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga. 

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wa Katoliki muda mfupi Baada ya ibada ya kumweka wakfu askofu mpya wa jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu (wapili kulia pembeni ya Rais) huko Ngokolo mjini Shinyanga. 


Picha, Taarifa: Freddy Maro/IKULU

WM Pinda: Tanzania Diaspora hawataweza kupiga kura Oktoba

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania waishio ughaibuni hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa sababu kuna mambo kadhaa ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya zoezi hilo kufanyika.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Aprili 11, 2015) wakati akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Peter Kallaghe, yaliyoko Highgate, Kaskazini mwa Jiji la London.

Akizungumza na Watanzania hao ambao baadhi yao walitoka miji ya Leicester na Manchester, Waziri Mkuu alisema mambo makuu ambayo yanahitaji kuzingatiwa kabla hawajaweza kupiga kura ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 pamoja na uandikishwaji wa Watanzania wana-Diaspora kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

"Najua suala kubwa ambalo mnatamani kulisikia ni hili la Watanzania kuweza kupiga kura kutokea huku mliko. Hili inawezekana lisifanikiwe wakati huu kwa sababu kuna mambo muhimu ya kuzingatia kubwa likiwa ni marekebisho ya sheria na hili zoezi la uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Ili mwananchi aweze kupiga kura ni lazima awe ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura," alisema.

"Itabidi tuangalie kama mashine za BVR nazo zitapaswa kupelekwa kwenye kila ubalozi ili watu wetu waweze kujiandikisha au itafutwe njia nyingine ya kufanikisha hilo jambo.... lakini watu wa Tume wanaamini kwamba jambo hilo linaweza kufanikiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020," aliongeza.

Waziri Mkuu ambaye aliwapatia nakala zisizopungua 40 za Katiba Inayopendekezwa, alitumia fursa hiyo kuwasisitizia wasome kwa makini Katiba hiyo ili wawe na uelewa mpana na kisha wailinganishe na Katiba ya mwaka 1977 ambayo inatumika hivi sasa ili waweze kubaini kama kweli haina kitu kama ambavyo watu wengine wanadai.

"Moja ya changamoto zinazotukabili huko nyumbani ni mjadala kuhusu Katiba Inayopendekezwa,wako watu wanaosema kwamba hakuna kitu kipya kabisa kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini mimi nasema hayo ni mawazo yao binafsi," alisema.

Akifafanua kuhusu Katiba hiyo, Waziri Mkuu alisema: "Mimi nilikuwa sehemu ya Bunge Maalum la Katiba, ni kweli tulibadili baadhi ya vipengele lakini kwa nia ya kuiboresha. Ninawasihi kila mmoja wenu aisome na kuangalia kama kweli hamna kitu au kuna kitu kipya ikilinganishwa na Katiba inayotumika hivi sasa. Angalieni na pimeni, je kuna kitu kimeboreshwa au la?"

Aliwasihi waendelee kuiombea nchi ya Tanzania ili iendelee kuwa na amani na utulivu na hasa katika kipindi hiki ambacho inakabiliwa na uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais. "Ninawasihi muendelee kuiombea nchi yetu ili ipate viongozi wazuri ambao watajali maslahi ya wengi," aliongeza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, APRILI 12, 2015.

Tangazo kwa waajiriwa wa MUST

MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGYTANGAZO


MABADILIKO YA KURIPOTI KITUO CHA KAZI KWA WAAJIRIWA WAPYA


Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kinawatangazia waajiriwa wapya kuahirishwa kwa muda wa kuripoti kituo cha kazi kama mlivyotaarifiwa awali mpaka mtakavyotaarifiwa tena . Hii inatokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.

Chuo kinaomba radhi kwa usumbusu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na

Ofisi ya Uhusiano

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

Oman Academic Fellowship Program: Postgraduate (Masters, Doctorate) Scholarships

Oman Academic Fellowship (OAF) Program

POSTGRADUATE SCHOLARSHIPS

(MASTERS and DOCTORATE)

The Ministry of Education and Vocational Training, Zanzibar, in collaboration with the Ministry of Higher Education of Oman and Oman Academic Fellowship (OAF) Joint Committee is pleased to invite potential applicants of qualified Zanzibaris to apply for postgraduate scholarships under the Oman Academic Fellowship (OAF) Program.

ELIGIBILITY REQUIREMENTS

1. All applicants must be Zanzibaris.

2. Must not exceed 35 years of age for Masters and 45 years of age for PhD applicants.

3. Minimum GPA requirement for PhD and Masters Applicants shall be 3.7 out of 5 (equivalent to 3 out of 4). Preferences will be given to candidates with the highest GPAs.

4. Must have a score of at least 6.0 in (IELTS) or 550 in (paper based) TOEFL or equivalent in iBT TOEFL.

5. Must have specialized in a certain field of study with valid work experience. Noticeable accomplishments will be a plus.

6. Non-SUZA PhD and Masters Applicants should be residents of Tanzania at the time of application, and if employed by the government they should show proof of employment.

7. Non- SUZA candidates must sign a bond agreement stating that they will work for SUZA upon completion of their studies with minimum qualifications set by SUZA appointment guidelines, which include passing an oral interview. In case, the applicant does not qualify to work for SUZA. He/she should be assigned employment in other relevant units in the government.

8. All educational qualifications must be issued by accredited educational institutions and authenticated by credible educational bodies.

APPLICATION PROCEDURES

 All applicants must fill out the electronic application through the Higher

Education Admission Center via website: www.heac.gov.om

 Applicants must upload the following scanned documents:

i. Identification Documents (either Passport or Zanzibar ID Card)

ii. Master’s certificate and academic transcript (for PhD applicants only).

iii. Bachelor certificate and academic transcript.

iv. Form 4 and Form 6 certificates.

v. (IELTS) or TOEFL certificate.

vi. CV showing all work experience.

vii. Birth Certificate.

Program Areas: Masters or Doctorate

Masters (Internal Candidates)

 Mobile Computing

 Communication

 GIS & Remote Sensing

PhD (Internal Candidates)

 Educational Media and Technology

 Curriculum and Assessment

 Physics

 Mathematics

 Chemistry

 ICT for Education (E- learning)

Masters (External Candidates)

 Educational leadership and Management

 Early Childhood Education

 Physical Education

 Occupational health and safety

 Histology

 Embryology

 Family (community) medicine

 Medical parasitology

 Surgery

 Geophysics

 Petroleum Geology

 Chemical engineering

 Petroleum Engineering

 Geoscience Technology

 Tourism management

 Hospitality management

 Business Administration, specializing in Tourism

Electronic Applications should be submitted between 5th April 2015 and 4th May 2015.

For further information or assistance on how to upload electronic applications, please do not hesitate to contact The Consulate of Oman in Zanzibar on 0242 230066 or 0242 230700.

Please Note:

 Any application with incomplete documents as mentioned in the eligibility criteria will not be considered for the scholarship but may reapply in the future once their documents are complete.

 Note: Successful applicants shall be informed by formal letters, which shall include all scholarship benefits and specific amounts of allowances they will be under the scholarship.

Sponsorship in Anaesthesiology available for a Tanzanian


CCBRT (www.ccbrt.or.tz) is a locally registered non-governmental organisation that comprises among other activities a well-established Disability Hospital which includes ophthalmology, orthopaedics, reconstructive surgery and obstetric fistula. A new 200-bed Maternity and Newborn Hospital is under construction. Together the Disability Hospital and the Maternity and Newborn Hospital will form the Super Specialist Hospital for the Eastern Zone of Tanzania.

CCBRT is willing to sponsor for the academic year 2015 – 2016 two (2) Medical Doctors for a postgraduate degree in Anaesthesiology at MUHAS.

Candidate’s requirement:

  • Tanzanian citizenship,
  • Holder of a Doctor of Medicine degree (MMed) with a minimum GPA of 2.7 at undergraduate level,
  • The MMed has been achieved in the last four years (not before 2010),
  • Have applied and be eligible for MMed programme in Anaesthesiology at MUHAS for the academic year 2015 - 2016
  • Three names of referees, two of whom must be academicians/professionals.

Sponsorship extension for the following three academic years up to the graduation, depends on good academic results.

After post graduation degree the anaesthesiologists will be a potential hires for CCBRT.

APPLICATIONS SHOULD BE SUBMITTED TO:

Lorraine Dias
HR Manager
P.O. BOX 23310
DAR ES SALAAM, TANZANIA.

CLOSING DATE: 30th APRIL 2015

Katiba Inayopendekezwa ikipita 2015 Uchaguzi haufanyiki Oktoba

Mwanasiasa mashuhuri nchini, Mabere Marando,amesema iwapo Katiba Inayopendekezwa itapitishwa mwaka huu, basi Uchaguzi Mkuu wa Oktoba hautafanyika.

Kama hakutakuwepo uchaguzi mkuu,basi kuna uwezekano wa Raisi Jakaya Kikwete kuendelea kuwa madarakani, amesema Marando.

Kwa hiyo juhudi zozote za kutaka kura ya maoni sasa,wakati hakuna muda wa kutosha, amesema Marando, ni mbinu za kutaka Rais abaki madarakani zaidi ya muda aliopewa na katiba ya sasa.

Marando amesema kifungu cha 294 cha Katiba Inayopendekezwa kimeweka mashariti ya mpito ambayo lazima yatekelezwe kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Lakini amesema, masharti hayo hayawezi kutekelezwa katika kipindi kifupi kilichosalia, jambo ambalo litalazimisha uchaguzi huo kusogezwa mbele.

Miongoni mwa mashariti ambayo Marando anasema yatazui kufanyika uchaguzi mkuu, ikiwa kura ya maoni itafanyika na katiba kupitishwa, ni kutokuwapo kwa sheria mpya ya uchaguzi.

Amsema, kwa kuwa Bunge la Muungano litavunjwa Julai, hakutakuwa na Bunge la kutunga sheria zinazotamkwa katika Katiba Mpya na zinazohitajika kwa, "utekelezaji bora wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya mwaka 2014" ambayo inapaswa kuanza kutumika kwa mujibu wa sheria mara baada ya kupitishwa.

Naye Prof. Gamaeli Mgongo Fimbo, mmoja wa wasomi wa uandishi wa katiba, amesema kuwa kura ya maoni ikipigwa Oktoba, na wananchi wakapitisha katiba hiyo, naye Raisi akatangaza kutumika baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, taifa linaeweza kuingia katika matatizo.

Prof. Mgongo Fimbo amesema,"kwa hivi ilivyo, labda Rais atangaze Katiba Mpya kutumika baada ya uchaguzi. Vinginevyo, tutaingia katika mgogoro na pengine hata vurugu".

Msomi huyo amesema kuwa mgongano mkubwa uliopo katika mashariti ya Katiba Inayopendekezwa unatokana na Bunge Maalumu la Katiba kutupilia mbali Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba.

Amesema,"Kama wangefuata mapendekezo ya rasimu ya Jaji Warioba, kusingelikuwa na matatizo. Lakini kwa hivi walivyoweka, kulazimisha kura ya maoni, ni kutaka kutofanyika uchaguzi.

"Maana hapa itategemea raisi ameamkaje. Itategemea mstuko ulioko nyuma yake. Bali kwa kuwa inatoa muda wa kujiongezea nyadhifa, anaweza kuruhusu katiba itakayopatikana kuanza kutumika kesho, jambo ambalo litaathiri moja kwa moja uchaguzi mkuu,"amesisitiza.

Hata hivyo, Rais Kikwete tayari ameeleza mara kwa mara kuwa hana mpango wa kuendelea kubaki madarakani,kinyume na muda wake wa sasa uliotajwa na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya mwaka 1977.

Akiongelea hilo Marando anasema, "yawezekana Raisi Kikwete hataki kubaki Madarakani.Lakini kwa haya yaliyomo humu, hakuna namna ambavyo anaweza kujiepusha na kitu hicho.

Marando amesema mgongano mkubwa uliopo katika katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu,unaanzia kifungu cha 285 hadi 288,vinavyohusu utumishi wa umma katika Jamuhuri ya Muungano.

Kifungu cha 285 cha katiba kinasema, mtu ambae anashika madaraka ya uraisi kabla ya kuanza kutumika katiba hiyo,ataendelea kushika nafasi ya madaraka ya uraisi kwa mashariti ya katiba hii,hadi hapo raisi mwingine atakapochaguliwa badala yake katika uchaguzi mkuu kwa kufuata katiba mpya.

"Hii maana yake ni kwamba,ili uchaguzu mkuu ufanyike,lazima kuundwe vyombo vitakavyosimamia uchaguzi huo. Kwa mfano, lazima kuundwe Mahakama ya Juu ya Jamuhuri ya Muungano, ambayo itaruhusu matokeo ya uchaguzi kuhojiwa mahakamani," amefafanua.

Marando anasema,kizingiti kingine cha kutofanyika uchaguzi kiko katika mambo ya mpito kwa kwa Bunge Maalumu la Katiba, limewekewa kipindi cha mpito kuwa miaka minne;na kupendekeza kuwa katiba ya sasa itakufa mara baada ya katiba mpya kuanza kutumika.

"Anasema Jaji Warioba alikwenda mbali zaidi. Aliweka muda wa mwisho wa kipindi cha mpito kuwa 31 Desemba 2018.Kabla ya hapo,katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ingeendelea kutumika katika baadhi ya maeneo ambayo sheria zake hazijatungwa katika katiba mpya ya mwaka 2014.

"Lakini Katiba ya Sitta na Chenge, ilivifuta vifungu hivyo na kuelekeza kuwa Katiba ya 1977 itakoma mara baada ya katiba mpya kupitishwa na kuanza kutumika".

Akichambua kifungu kimoja baada ya kingine, Marando amesema,ikiwa Katiba inayopendekezwa itapita, itasababisha uchaguzi mkuu wa Oktoba kutofanyika.

Marando amesema kama raisi hataki kuendelea kubaki madarakani basi aachane na kura ya maoni kabla ya uchaguzi mkuu.

"Vinginevyo, hakuna namna ya kufanyika kura ya maoni;na wanaoileta wanataka kupata ushindi, na kisha katiba hiyo isiweze kutumika. Hakuna," amesisitiza.

  • Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Habari24

Job opportunities for Assistant Medical Officer and Nurses at Marie Stopes


CAREER OPPORTUNITIES

Marie Stopes Tanzania (MST) is a marketing-focused, results-oriented social enterprise, which uses modern management and marketing techniques to provide family planning, reproductive and sexual healthcare and allied services. MST is a member of the Marie Stopes International (MSI) Global Partnership, which operates in over 45 countries worldwide. MST’s goal is to improve quality of life in Tanzania by dramatically improving access to and use of family planning and other reproductive health services.

We are looking for dynamic individuals to join our highly motivated team in the following roles;

ASSISTANT MEDICAL OFFICER

Job purpose

The Assistant Medical Officer is responsible for provision of high quality integrated Reproductive Child Health Services and supervision of community demand creation in the outreach set up across Tanzania. The main focus of the post is to work independently in FP and VCT service delivery, ensuring the best clinical quality, and perform procedures in outreach set up in line with MSI Protocols. The Assistant Medical Officer reports directly to the Zonal Coordinator

Minimum requirements

 Diploma in Clinical medicine

 Registered with Medical Council of Tanganyika.

 4 years’ experience in clinical work internship inclusive

 Desirable: Experience of outreach service delivers

OUTREACH NURSES

Job purpose

The Outreach Nurse in collaboration with the Assistant Medical Officer is responsible for provision of high quality integrated Reproductive Child Health Services and community demand creation in the outreach set up across Tanzania. The main focus of the post is to work independently in FP and VCT service delivery, ensuring the best clinical quality, and perform procedures in outreach set up in line with MSI Protocols. The Outreach Nurse reports directly to the Zonal Coordinator

Key Responsibilities

 Work with the team to develop local plans with particular focus on maximizing access to family planning and Sexual and Reproductive Health and services and ensuring project target are met.

 Participate in evaluating, reporting and monitoring of the outreach performance.

 Work with outreach team to increase efficient client flow from information talk, through counselling, procedure and post procedure care;

 Practice good customer care by prioritizing the rights and the needs of clients;

 Comply diligently with MSI protocols for all procedures and for vocal local and infection prevention;

 Work with outreach teams to update knowledge of Family Planning methods for effective client counselling and drug dispensing practices;

 Provide clinical support to AMO/MO during medical procedures in the communities

Minimum requirements

 A Nursing Certificate.

 must be registered with relevant board and have a current nurses license

 At least 3 years working experience in a similar post

 Proven experience with outreach services in remote areas is desirable

 Knowledge of and appropriate application of the nursing process in family planning and sexual and reproductive health is required

 Working knowledge of computers and basic programs

 Desire to meet and exceed expectations is highly required

 Putting clients at the center of everything

 Building and maintaining effective long term working relationship with all stakeholders;

 Desire to become a true Marie Stopes Ambassador.

Mode of Application

If you feel that you are able to meet the requirements and you are motivated enough to be part of the team, please send your applications including a cover letter detailing your suitability and why you are interested in this post to the address below. Please indicate the work station of your interest.

Director of Human Resources and Administration
Marie Stopes Tanzania
P. O. Box 7072, Dar Es Salaam.

Telephone: +255 22 277 4991

E-mail: [email protected]

Only short listed candidates will be contacted.

Closing date: All applications should reach the addressee before Friday April 17, 2015

Binti kapata mchumba...


Dk Slaa aanza ziara ya kikazi Marekani

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini jana (Jumamosi Aprili 11, 2015) kuelekea nchini Marekani ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tisa.

Dk. Slaa katika safari hiyo ameambatana na mkewe Josephine Mushumbusi.

Ziara hii ya siku tisa ni mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana Mike Pence pamoja na taasisi mbalimbali za nchini humo ikiwemo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wa kisiasa na kijamii wa Katibu Mkuu huyo na chama chake katika maendeleo ya bara la Afrika na kipekee nchini Tanzania.

Ziara hiyo itamwezesha Dk. Slaa kushiriki mijadala mbalimbali inayohusu uwekezaji, elimu na uongozi iliyoandaliwa kwa ajili yake ambayo lengo lake kuu ni kuitangaza Tanzania kwa ukamilifu wake.

Kwa malengo hayo, Dk Slaa atafanya mihadhara (Public Lectures) kwenye vyuo vikuu vya Purdue, Indianapolis na Marion. Sanjari na mihadhara hiyo, Dk Slaa atakua na vikao vya mashauriano na baadhi ya Maprofesa waadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya kisiasa na maendeleo na kijamii na ushiriki wa Chadema katika siasa za Kimataifa.

Zaidi, ziara hii itamkutanisha pia Katibu Mkuu na viongozi na watendaji wakuu wa kiserikali na makampuni mbalimbali pamoja na taasisi kubwa za uwekezaji kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uchumi na uwekezeji Barani Afrika na kwa kipekee Tanzania.

........................
Deogratias Munishi
Head of Foreign Affars
CHADEMA Headquarters
P.O.BOX 31191, Dar es Salaam,
Cell: +255715887712

Utendaji kazi wa marehemu Edward Moringe Sokoine

Askari JKT afariki akipambana na majambazi

Watu wawili wamefariki mkoani Iringa akiwemo askari wa Jeshi la kujenga Taita (JKT) na mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa ni jambazi wakati wa kurushiana risasi na jeshi la polisi baada ya kufanya uporaji eneo la Mafinga wilaya ya Mufindi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Salma Semwiko mfanyabiashara na mkazi wa Mafinga akiwa anaelekea kazini alivamiwa na mtu aliyekuwa na silaha aina ya SMG kisha kumpora simu na fedha zaidi ya laki saba.

Ameongeza kuwa baada ya uporaji huo ilitokea pikipiki aina ya bodaboda na kumchukua jambazi huyo kisha kukimbilia eneo la Kinyanambo na ndipo yalipotokea majibizano ya silaha wakati polisi na wananchi wakifanya jitihada za kuwakamata majambazi hao.

Kamanda Mungi amesema Saidi Ng’umbi askari wa JKT amefariki papo hapo baada ya kupigwa kifuani upande wa kulia na majambazi hao.

Amesema jeshi la polisi wamefanikiwa kumkamata jambazi mmoja ambaye amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupigwa kwenye paja la mguu.

Aidha ameongeza kuwa jeshi la polisi mkoani Iringa linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumtafuta jambazi aliyekimbia katika tukio hilo.

Wakati huo huo Kamanda Mungi amesema Winifrida Frank umri wa miaka 25 mkazi wa eneo la Ipogolo Manispaa na Mkoa wa Iringa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya mauaji ya kumtupa mtoto mwenye umri siku tatu kwenye shimo la maji machafu.

  • Taarifa ya Yonna Mgaya via Malunde1 blog, Iringa

[update] Rais Mkapa atoa elimu ya uchumi kwa Mabalozi, Maofisa na WatumishiRais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akitoa mada katika semina ya masuala ya diplomasia ya uchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani). Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 9 Aprili 2015.


Mkaguzi Mkuu wa ndani Bw. Mathias Abisai (wakwanza kushoto), Mkurugenzi Idara ya Ununuzi Bw.Elias Suka (Katikati), wakiwa pamoja na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Paul Kabale wakati wa Semina hiyoSehemu ya Watumishi.Waziri Membe akitoa Ufafanuzi katika moja ya mambo yaliyo jadiliwaMkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (Kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Mindi KasigaSehemu nyingine ya walioudhuria Semina Hiyo.Balozi Mstaafu Mhe. Simon Mlay akiuliza swali meza kuuMkurugenzi wa Masomo wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Watengere Kitojo akiuliza swali.Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (mbele kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Irene Kasyanju wakifuatilia semina hiyo.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje Bi. Mindi KasigaMuhadhiri kutoka Chuo cha Diplomasia Dr. Lucy Shule akiuliza swaliRais Mstaafu Mkapa akiteta jambo na Mhe. Membe wakati wa semina hiyo ambapo alizungumzia changamoto za ushirikiano wa kiuchumi na diplomasia nchini Tanzania, na nje ya nchi na kwenye Jumuiya za Kimataifa. Andiko la mada hii litapatikana baada ya muda mfupi kwenye tovuti ya Wizara www.foreign.go.tz
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mjadala wa semina hiyo.Rais Mstaafu Benjamin W. Mkapa (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernard Membe na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajab Gamaha, kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Chuo cha Diplomasia.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimpokea Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Mwalimu Nyerere kwa ajili ya semina hiyo.

  • Picha: Reginald Philip/Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje blog

Mabalozi wa Tanzania na India wakutana kwa ajili ya ziara ya Rais Kikwete

Balozi wa India hapa Nchini Bw. Debnath Shaw, akisisitiza jambo kwa Balozi Mbelwa Kairuki katika mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na India. Kulia ni afisa mwandamizi Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Luangisa EFL akisikiliza kwa makini na kushoto ni katibu Muktasi wa balozi wa India hapa nchini Bi. Deepay.
--- Reuben Mchome

Maveterani wa Barcelona Ikulu Dar na Zanzibar na ziara mbuganiRais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji maveterani wa timu ya Barcelona walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam, Aprili 11. 2015Rais Kikwete akizungumza na wachezaji maveterani wa timu ya Barcelona wakati walimpomtembelea .


Mchezaji nyota wa Timu ya Barcelona Johann Cruyft akimkabidhi jezi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wachezaji Nyota wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakisalimiana na Waziri Mwinyihaji walipowasili Ikulu Zanzibar kwa kusalimiana na Rais wa Zanzibar katika mualiko wa chakula cha mchana aliowaandalia wageni wake.Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk akizungumza na mchezaji nyota wa timu ya Barcelona Kulvert wakati wa chakula cha mchana walioandaliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Johan Cruyff, wakati wa chakula cha mchana aliowaandalia wageni wake Ikulu Zanzibar, timu ya Barcelona ikiwa Zanzibar kwa mualiko wa Rais Shein.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na ujumbe wa timu ya wachezaji wa zamani nyota wa Barcelona wakati wa chakula cha mchana aliowaandalia Ikulu, kulia Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk na kushoto Kocha na Rais wa Heshima wa timu ya Barcelona Johan Cruyff.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wachezaji nyota wa timu ya Barcelona wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika Ikulu Zanzibar. Timu hiyo ikiwa Zanzibar kwa mwaliko wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.Wachezaji nyota wa Zamani wa timu ya Barcelona wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akizungumza na wachezaji hao walipofika Ikulu Zanzibar kuonana na mwenyeji wao Rais wa Zanzibar na kupata chakula cha mchana.Wachezaji nyota wa Zamani wa timu ya Barcelona wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akizungumza na wachezaji hao walipofika Ikulu Zanzibar kuonana na mwenyeji wao Rais wa Zanzibar na kupata chakula cha mchana.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa jezi ya Timu ya Barcelona yenye jina la Cruyff namba 14. Iliokuwa ikivaliwa na mchezaji huo, akimkabidhi jezi hiyo Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Johan Cruyff, wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika Ikulu Zanzibar.


  • Picha: Fredyy Maro/Ikulu na Othman Mapara/ZanziNews blog; Video: Shaffi Dauda. 

Mapitio ya magazet kwenye Tv, Aprili 12, 2014