[video] Rais Kikwete alipofungua jengo la ubalozi wa kudumu UM

Ngoma Africa Band - East Africa's golden voices, most wanted


The Ngoma Africa Band aka FFU also known as Anunnaki alien, is East Africa´s most wanted band in Europe. The German based band gained its popularity through their extraordinary stage performance on festivals and other events in and out of Europe, leaving fans always wanting for more.

Ngoma Africa Band with it´s more than two decades experience and encounter with diverse cultures and audiences which has marked it´s success in the music and entertainment industry.

The secret of Ngoma Africa Band can be explained as a result of a large research and fusion between traditional and modern music elements that creates a completely irrestitible dancing groove, difficult to resist by its fans. Nicknamed by fans as FFU (Field Force Unit), Anunnaki aliens or "watoto wa mbwa " expressions as a result of the irresitible nature of that transformation it´s audience into a dance fiesta

The Ngoma Africa Band has continously topped the East African music charts with its two released Albums and many singles, all songs composed and written by Founder and also band leader Ebrahim Makunja aka commander Ras Makunja.

With more than 50,000,000 media impressions, Ngoma Africa Band amongst others, recognitions from cultural institutions, international producers, music academies ,Festivals and agencies who will like to take East African music into their music repetoire, Ngoma Africa is a grassroot band and we like to stay focus on its vision, mission and objectives.

The youngest soloist Matondo Benda; drumer Jo Sausa aka surgent Major Jo Sousa, Gaiilo Prof, were onces fans and due to the chance accorded them by NGOMA AFRICA BAND, their dreams of playing on global stage with Ngoma Africa Band became a reality

Ngoma Africa Band´s talents and vocals are Flora William, Jessicha Ouyah, Glory , Aj Nbongo, Mo Benda, Bedi, including multi-talented Chris-B Bakotessa and bandleader Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja

What makes Ngoma Africa Band different from existing bands in this category, is their ability to communicate with fans at every level -emotions, feelings, happiness, tears, smiles, laughters and keeping their memories warm."Our music is a tool that creates new friendship and unites old relationships." Declares the band leader – Kamanda Ras Makunja

We enjoy travelling and visiting new places just to give our fans a great feeling and satisfaction that they deserved.

The 10 members of the band are focused on promoting the East African Music "Bongo Dansi" on the global stage, Germany, Europe and Africa, and the do this gesture most of the time from private spendings. "Most of the time band spend own money with no sponsors,just to transport East African Music to meet fans in their respective regions" declares members of the band!


The Ngoma Africa Band and fans shall keep the East african music alive on global stage forever! Thanks to our fans, bloggers, journalist and Djs for playing and spreading the news worldwide, together we promote and brand East Africa through our culture – music: We look forward to performing at your festival, events, private parties and other occassions of your choice. The Ngoma Africa Band is a community band made for community people worldwide.

Click at www.ngoma-africa.com to listen to the Ngoma Africa music. facebook.com/ngomaafricaband and www.reverbnation.com/ngomaafricaband

Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School watembelea ubalozi wa TanzaniaWanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe. Balozi Liberata Mulamula.Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Balozi Leberata Mulamula.Mhe. Bbalozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.


 • Picha tumeshirikishwa na Kwanza Production

Survey: World's 5 most and 5 least religious places

WIN/Gallup International, the world’s leading association in market research and polling, has today published its latest data exploring the religious beliefs of 63,898 people from 65 countries across the globe

Here is a map of the five-most religious countries and places.


In Africa and the Middle East more than 8 out of 10 people (86% and 82% respectively) portray themselves as religious while 7 out of 10 say so in Eastern Europe and America (71% and 66% respectively) and 6 out of 10 (62%) in Asia, say they are. 

The five least-religious places can be seen on this map.

This new research this Easter shows that worldwide six out of ten (63%) citizens say they are religious, while one in five (22%) say they are not and one in ten (11%) consider themselves convinced atheists.


Abou & Kichai Home Repairs: Huduma bora za ujenzi DMV

 

Kazi yetu ni kutoa huduma bora za ujenzi katika maeneo ya Washington DC, Maryland na Virginia, kwa huduma za ukarabati wa nyumba yako, kitaalamu na kwa ufanisi zaidi.

Tunaweza kushughulikia mahitaji yote ya matengenezo yanayohusu ujenzi ama ukarabati wa nyumba yako, ili kufanya urahisi wa kile ulichoharibikiwa, kwa uhakika na uwaminifu zaidi juu ya utendaji wa kazi zetu bora kwa ajili ya kusaidiana na mteja kwenye maswala ya ujenzi kwa wamiliki wa nyumba katika maeneo ya hapa DMV

Tunatoa huduma za vipimo vya nyumba yako bure yani (Free estimate) iwapo mteja ana tatizo lolote lilojiri kwa ukarabati wa nyumba yako .

Tupo DMV kwajili ya kumaliza tatizo la UKARABATI wa nyumba yako endapo utakuwa na tatizo la aina lolote lile.

Tafadhali wasiliana nasi kwa number za simu 202-361-0671 na 301-728-3977

Email: [email protected]

KICHAI HOME REPAIRS

Professional Handyman Services, wakishirikiana na Abou's Tile Contractors

Hii nchi ina mambo ya ajabu kweli: Aliyejeruhi mtoto afutiwa kesi 'kiaina'

Katika tukio lisilo la kawaida, Mahakama ya Mwanzo Ilemela jijini Mwanza, imedaiwa kufuta kesi ya kujeruhiwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka miwili na nusu, inayomkabili mlezi wa shule ya chekechea ya Nelca Day Care, Siwema Bujota, kinyume na sheria.

Wakati kesi hiyo ikifutwa, polisi mkoani Mwanza inamtafuta mtuhumiwa huyo anayedaiwa kumshambulia na kumdhuru mwili mwanafunzi, Sean Sinani.

Inadaiwa kuwa Machi 27, mwaka huu, katika mahakama hiyo, mtuhumiwa huyo alisimama mahakamani hapo akiwa na mtu mwingine na kujifanya ndiye mama mzazi wa mtoto na kusema ameamua kusamehe kesi wakati mhusika halali hakuwapo mahakamani.

Awali ilielezwa kuwa mlezi huyo alimjeruhi mwanafunzi kwa kumchapa kwa fimbo kwa madai ya kujisaidia shuleni.

NIPASHE Jumamosi ilizungumza na mama wa mtoto huyo, Sabrina Hamis, aliyesimulia kuwa mtoto wake alimkuta na majeraha maeneo ya mwili wake na kuamua kumfikisha kituo cha polisi cha Kirumba ambapo alipewa fomu ya polisi (PF3) na kumpeleka hospitalini.

Alisema alimpeleka hospitali ya Sekou Toure ambapo alitakiwa kufanywa kipimo cha X-ray lakini ilishindikana kwani kilikuwa hakifanyi kazi na kupewa rufaa hospitali ya Bugando.

Alisema majibu ya kipimo hicho yalitakiwa kupelekwa hospitali ya Sekou Toure ambapo mwanae aliendelea kupatiwa matibabu.

Alisema mwalimu huyo alikamatwa na polisi na siku iliyofuata Machi 27, alifikishwa mahakamani.

Hamis alisema akiwa mahakamani majira ya mchana, kesi yake ilikuwa haijaanza kusikilizwa na aliondoka kwenda hospitali kutokana na hali ya mtoto huyo kubadilika na kuamua kumrudisha hospitali.

Alisema alipotoka hospitalini hakuwahi mahakamani hali iliyomfanya ashindwe kuhudhuria kesi hiyo na kuamua kurudi nyumbani ambapo alipata taarifa kuwa kesi yake imefutwa.

Alisema taarifa hizo hakukubaliana nazo na kuamua kufika kituo cha polisi kufuatilia suala hilo ambapo alielezwa kuwa kesi hiyo imefutwa.

Alisema sababu za kufutwa kesi hiyo ni kutokana na upande wa mtuhumiwa mmoja wao alisimama mahakamani akijifanya ni mama wa mtoto na kusema ameamua kusamehe kesi hiyo na hakimu akaifuta.

Hamis alisema mazingira ya ufutwaji wa kesi hiyo yanaonekana kuzingirwa na rushwa kwani hakuhusishwa wakati yeye ndiye mlalamikaji.

Alisema mpelelezi wake anamlaumu kwa kuondoka mahakamani bila kusubiri kesi yake, bila kujali hali ya mtoto wake kwani ilibadilika na kumlazimu kuondoka akijua angewahi kutoka hospitali ili asikilize kesi hiyo.

Hata hivyo, alisema wiki hii aliamua kwenda mahakama kuulizia kesi hiyo na kujulishwa imefutwa na kutakiwa aende kituo cha polisi.

Alisema alirudi kituo cha polisi cha Kirumba lakini hawakumpa ushirikiano. "Cha kushangaza hawa askari wananiuliza huyo mtuhumiwa tutampata wapi maana hapatikani, hivi hilo swali linanihusu mimi inaonyesha kabisa kuna mchezo unaendelea ila haki ya mwanangu nitaipata," alisema.

"Hivi huyo hakimu aliiona sura yangu mahakamani hadi aifute kesi yangu nashangaa kesi inafutwa hata PF3 haijajazwa na mtoto wangu bado hajapona vizuri," alisema.

Kwa upande wake, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Japhet Lusingu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kesi hiyo ilifutwa Machi 27, mwaka huu.

Alisema kesi iliendeshwa na kufutwa siku hiyo hiyo na kwamba sababu za ufutwaji wa shauri hilo ni mlalamikaji kueleza watamalizana nje ya mahakama.

Lusingu alisema mlalamikaji alirudi kituo cha polisi na kulalamikia suala hilo, hivyo juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.

Aidha, alisema mlalamikaji huyo anatakiwa kurudisha PF3 na kwamba kuna uwezekano wa kesi hiyo kupelekwa wilayani.

 • via NIPASHE

Serikali yaagiza zifunguliwe mara moja shule zilizofungwa kwa kukosa chakula

Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam mpango wa Serikali kuajiri waalimu wa shule za msingi wenye elimu ngazi ya Stashahada badala ya Cheti kama ilivyo sasa. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
---Blogu ya Serikali ya Tanzania

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Jumanne Sagini ameagiza kufunguliwa mara moja kwa shule za Sekondari zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula na wanafunzi kurejea makwao.

Sagini amesema kuwa Serikali imeshapeleka asilimia 67% ya fedha katika Halmashauri zote nchini, kwa ajili ya chakula hivyo hakuna uhalali wa Wazabuni kushindwa kutoa huduma kwa sababu ya madeni.

Wiki iliyopita, wanafunzi katika shule 10 za Sekondari katika mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Dodoma na Tabora walilazimika kusitisha masomo na kurejea majumbani kutokana na ukosefu wa chakula.

Leo, gazeti la NIPASHE limeripoti taarifa ifuatayo:

Hali ni tete katika shule za kutwa za sekondari nchini, kutokana na kile kinachoelezwa ni kukosekana kwa chakula baada ya wazabuni kugoma kupeleka vyakula kutokana na kutolipwa fedha wanaozidai shule.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mikoa kadhaa nchini, kuwa baadhi ya shule zimelazimika kufungwa kutokana na kukosa chakula na kuwaacha wanafunzi wenye mitihani ya Taifa wa kidato cha pili, nne na sita.

Mkoani Kagera, shule saba za sekondari zimefungwa kutokana na ukosefu wa chakula na wanafunzi wa kidato cha kwanza, tatu na tano wakirudishwa nyumbani kwa muda usiojulikana.

Hali hiyo inatokana na wazabuni wanaotoa huduma ya chakula kwa shule hizo kutolipwa fedha wanazodai.

Ofisa Elimu wa mkoa wa Kagera, Florian Kimolo, alisema wanafunzi katika shule hizo wameongezewa muda wa kukaa nyumbani wakati huu ambao serikali inatafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Alizitaja baadhi ya shule hizo kuwa ni Rugambwa, Kahororo, Ihungo, Nyakato, Kimolo, Rukore, Kabanga na Muyenze za

Wilayani Ngara na kuwa tayari wamepeleka taarifa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwa ajili ya kupatiwa fedha za chakula ili wanafunzi warudi kuendelea na masomo.

“Kawaida binadamu yeyote anahitaji chakula na kinapokosekana siyo rahisi kuendelea kuishi na kuwa kumbakiza mwanafunzi shuleni bila kumpa chakula kuna athari kubwa kiafya,” alibainisha na kuongeza: “Kuwarudisha nyumbani kuna athari maana kunapunguza siku zao za masomo na wanaweza wasifundishwe baadhi ya mada.” “Sifahamu lini wanafunzi hao watarejeshwa shuleni, lakini sisi kama serikali tunafahamu madhara ya tatizo hilo, ndiyo maana tunafanya kila jitihada ili warejee mapema iwezekanavyo” alisema.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Chacha Mwita, alithibitisha kuwapo kwa tatizo hilo katika shule za sekondari za bweni na kuwa jitihada zinaendelea ili wanafunzi warejee shuleni mapema iwezekanavyo.

Chacha alisema kuna madeni na kudai kuwa wazabuni hawajagoma kutoa huduma na kuwa kuna kikao kimefanyika na mawasiliano yanaendelea kufanyika ili waendelee kutoa chakula shuleni.

Hata hivyo, hakubainisha kiasi cha chakula kinachohitajika kwa shule zote na kuahidi kutoa taarifa kamili siku zijazo.

Mkoani Dodoma, shule za sekondari za bweni zimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na ukosefu wa chakula kwa wanafunzi.

Taarifa zilizolifikia NIPASHE zinaeleza kuwa moja ya shule hizo ni Shule ya Sekondari Mpwapwa ambayo ilitakiwa kufunguliwa baada ya likizo fupi ya sikukuu ya Pasaka lakini mpaka sasa haijulikani itafunguliwa lini.

Mkuu wa shule hiyo, Nelson Mbilinyi, alisema wanafunzi walitakiwa kufungua shule siku tatu zilizopita, lakini hadi sasa wameshindwa kufungua shule kutokana na ukosefu wa chakula.

“Tulikuwa tufungue Aprili 8, mwaka huu, lakini hatujafungua hadi sasa chakula cha kuwalisha wanafunzi hakuna,” alisema.

Alisema bado hawajajua shule hiyo itafunguliwa lini, lakini kitu ambacho anakijua ni kwamba leo kuna kikao na Afisa Elimu wa Mkoa.

Katika shule ya sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo, Mkuu wa Shule hiyo, Mwasi Chibuni, alisema shule hiyo haijafungwa isipokuwa hali ya chakula si nzuri.

“Licha ya wanafunzi kuendelea na masomo, lakini hali ya chakula siyo nzuri na shule haijafungwa tunaendelea tuone tutaishia wapi,” alisema.

Alibainisha kuwa wataendelea kujisogeza hivyo hivyo na kama watashindwa, watalazimika kufunga shule.

Katika wilaya ya Kondoa, kuna taarifa kuwa hali ya chakula katika shule ya wasichana ya Kondoa ni mbaya na inaweza kufungwa.

Hata hivyo, Afisa Elimu sekondari wa wilaya hiyo, Lucy Gurtu, alikanusha kuwa hakuna shule iliyofungwa kutokana na uhaba wa chakula.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, alipoulizwa kuhusu tatizo hilo, alijibu kuwa hana taarifa kwa sasa analifuatilia.

Mkoani Kilimanjaro, Serikali imesema itamchukulia hatua kali za kisheria, ikiwa ni pamoja na kumsimamisha kazi, Mkuu yeyote wa shule ya sekondari atakayebainika kushindwa kufungua shule kuanzia leo kwa kisingizio kwamba shule yake haina chakula.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (RAS), Alfred Shayo, aliiambia NIPASHE jana kwa njia ya simu kwamba, tayari wamepokea fedha kutoka Hazina, kwa ajili ya kuzihudumia shule za serikali.

“Kama kuna mkuu wa shule ambaye hatafungua shule katika muda uliopangwa, atachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu Hazina

iliyopo chini ya Wizara ya Fedha, imekwishaleta hizo fedha za chakula, ila kama zimechelewa kuwafikia wakuu wa shule, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa haina taarifa hizo...Kwa maana hiyo shule zote zitafunguliwa leo kama kawaida.

Alisema ofisi hiyo haina taarifa yeyote ya shule za serikali mkoani hapa kubadili ratiba ya masomo baada ya kumalizika kwa mapumziko ya Pasaka kutokana na uhaba wa chakula.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alisema anachofahamu ni wazabuni wengi kutolipwa fedha zao na kwamba hana takwimu za kiasi wanachodai na shule zenye uhaba.

Shule nyingine zilizofungwani shule ya wavulana na wasichana Tabora za mkoani Tabora, shule ya wavulana Nsumba mkoani Mwanza, shule ya wasichana Masasi, Ndanda za mkoani Mtwara na shule ya sekondari ya wavulana ya Songea, mkoani Ruvuma.

Mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Ndanda ambaye hakutaja kutajwa jina lake, alisema wametakiwa kurudi nyumbani mwishoni mwa wiki kwa kuwa hakuna chakula.

Shule ya wasichana ya Tabora, mmoja wa wanafunzi alithibitisha kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi wasio na mitihani ya Taifa mwaka huu, tangu Machi 24, mwaka huu, kutokana na uhaba wa chakula.

MKURUGENZI TAMISEMI

Mkurugenzi wa Sekondari wa TAMISEMI, Paulina Nkwama, alipoulizwa na NIPASHE juu ya suala hilo, alisema amepata taarifahizo, lakini anachofahamu shule zinapelekewa fedha za kulipa madeni ya wazabuni.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi, alisema yeye si msemaji wa Wizara na kumtaka mwandishi kumtafuta Waziri husika.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (pichani) na Naibu wake, Kassimu Majaliwa, walipotafutwa na NIPASHE simu zao ziliita bila kupokelewa na hata walipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukujibiwa.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anna Kilango, alisema suala hilo lipo chini ya Tamisemi na kwamba waulizwe mawaziri husika.

Jitihada za kuwapata Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, na Naibu Mwigulu Nchemba, simu zao ziliita bila kupokelewa na hata walivyotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukujibiwa.

Imeandikwa na Lilian Lugakingira (Bukoba), Augusta Njoji, (Dodoma), Godfrey Mushi (Moshi) na Salome Kitomari (Dar).

Yericko Nyerere: Siri ya Malkia Elizabeth, Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

Siri ya Malkia Elizabeth wa Usikochi (UK), Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika


Je unajua Mwalimu Julius Nyerere hakupigania uhuru wa Tanganyika yeye kama yeye bali aliandaliwa angali mdogo akakabidhiwa na kanisa katoliki kwa ubia wa Malkia Elizabeth wa Uingereza?

Je unafahamu Mwaliu Julius Nyerere alinusurika mara 18 kwenye majaribio ya mauaji, na alinusurika mara sita kwenye majaribio ya mapinduzi?

Je unajua kuwa Mwalimu Nyerere ni sehemu ya familia ya Malkia Elizabeth na aliachiwa urithi kupitia Fabian Society?

Ufamilia wa Nyerere kwa Malkia Elizabeth ni wakuasili. Ni sawa na ufamilia wa Mkapa kwa Mwalimu Nyerere. Tofauti moja nikuwa ili uwe mwanafamilia wa Malkia Elizabeth ni lazima ujiunge na Fabian Society ambayo ipo duniani nzima na inamilikiwa na umalkia wa Kiingereza,

Zingatia sheria ya cyber-criminal haijasainiwa, Rais bado yupo USA anakagua kiwanda cha kutengenezea ndege za Boeing ingawa tz haina hata toy la ndege ya maonyesho kwa wanafunzi tu, wakati huo shirika la ndege linawafanyakazi 120 na wote wanalipwa vizuri kabisa.


Navumilia kuwa Mtanzania, sijivunii kuwa Mtanzania!

Kwanza naomba tumfahamu Mwalimu Nyerere kuzaliwa na mapito yake,

Aprili 13, mwaka 1922, safari ndefu ya maisha ya Mwalimu Kambarage Nyerere iliyochukua miaka 77 na miezi 6 ilianza Mwitongo kijijini Butiama, kilomita takribani 30 kutoka mji wa Musoma, mashariki mwa Ziwa Victorialililoko kaskazini mwa Tanzania. Siku hiyo mvua kubwa ilinyesha. Mama Mgaya Nyang’ombe, aliyekuwa mke wa tano kati ya 23 wa Chifu Nyerere Burito wa Zanaki,

Alijifungua mwanae wa pili. Kwa desturi za kabila la Wazanaki, mtoto wa kike ama wa kiume aliyezaliwa siku ya mvua alipewa jina la KAMBARAGE (mzimu wa mvua).Kambarage alikuwa mtoto wa maskini kama walivyokuwa watoto wengine kijijini. Ingawa baba yake alikuwa Chifu (Mtemi), cheo hicho alichopewa wakati wa utawala wa Kijerumani hakikuwa na maslahi yoyote ya maana. Kwa desturi za makabila mengi, watoto walilelewa na kutunzwa na mama zao. Kwa hiyo, Mama Mgaya alijitegemea mwenyewe katika kuwalea wanawe 6 alioishi nao kwenye kibanda cha udongo, na paa la nyasi. Kambarage alipofikia umri wa kuelewa mambo, alimuhurumia sana mama yake na kumsaidia kazi kwa kadri alivyoweza.Eneo la Mwitongo lilikuwa na mandhari ya kupendeza ya kilima kidogo kilichozungukwa na vichaka na mawe.

Mtoto Kambarage alicheza michezo ya kujificha kwenye vichaka na kukimbiza pimbi na tumbili kwenye mawe. Alichunga mbuzi za mamaye na alipofikia umri wa kutosha, alienda na vijana wenziwe kuwinda porini. Pamoja kumsaidia mamaye alipata muda wa kuwa karibu na babaye na kujifunza utamaduni wa kizanaki.Siku moja, akiwa na miaka 10 baba yake alimtuma afuatane na mama yake wa kambo kwenda kwenye kijiji kingine kuhudhuria msiba wa jamaa wa mama huyo. Wakati wa kurudi walipewa mbuzi. Kambarage alimfunga kamba mbuzi na kumwelekeza njia. Mbuzi akagoma. Wakati wanakukurushana naye mzee mmoja akamwambia atamrahisishia kazi. Mzee yule akang’oa nywele kidogo kutoka kichwa cha Kambarage na manyoya kidogo toka kichwa cha mbuzi akachanganya na mizizi fulani, akatafuna na kumpa mbuzi akala. Yule mbuzi akamfuata Kambarage mpaka wakafika nyumbani Mwitongo bila kumsumbua!Akiwa na umri wa miaka 11 baba yake akamtolea Kambarage mahari kwa binti mmoja kijijini. Kwa desturi za Kizanaki mzazi alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo ili kuwa na uhakika kwamba hata akifa wanawe wa kiume watakuwa na uwezo wa kuoa.Kambarage hakutegemea kwamba angeliweza kupata nafasi ya kwenda shule kwa sababu baba yake alikuwa hana uwezo wa kuwasomesha wanawe wote. Hata hivyo, alidhihirisha kuwa na akili nyingi zilizo muwezesha kujifunza mambo haraka. Alijifunza kucheza bao kutoka kwa baba aliyependa kucheza bao na mama yake aliyekuwa hodari wa mchezo huo. Kila alipopewa nafasi ya kucheza bao na marafiki wa baba yake Kambarage aliweza kuwafunga! Akili alizozidhihirisha katika mchezo huo ndizo zilizomuwezesha kupata bahati ya kwenda shule. Mmoja wa wazee hao alimshauri Chifu Nyerere amuingize mwanawe shule kwa kuwa alionekana kuwa na akili sana. Ilimuwia vigumu Chifu kuamua lakini mwanawe mkubwa Edward Wanzagi alimshawishi akakubali.

Hatimaye, siku moja ya mwezi Aprili mwaka 1934, Kambarage akiwa na umri wa miaka 12 aliamka mapema kwa furaha kwenda kuanza darasa la kwanza katika shule ya Mwisenge, Musoma mjini. Kambarage aliingia shule akiwa hajui Kiswahili sawasawa. Hata hivyo, haikupita muda akajua Kiswahili, akili alizoonyesha kwenye bao zilidhihirika darasani pia. Ingawa wakati alipoanza shule alikuwa amechelewa kwa miezi mitatu, aliweza kuelewa mambo kwa kasi kuwashinda wengine walioanza mapema. Alipoingia darasa la tatu walimu waliamua kumrusha hadi la nne, akasoma masomo ya miaka minne kwa miaka mitatu tu. Mwaka 1936 alifanya mtihani wa nchi nzima wa kuingia darasa la tano, akawa mtu wa kwanza Tanganyika nzima. Alichaguliwa kuingia shule ya bweni Tabora ambayo ilikuwa na darasa la tano hadi la kumi.

KIJANA KAMBARAGE

Mwaka 1937 Kambarage akiwa kijana wa miaka 15 alianza masomo ya darasa la tano akiwa na ari ya kusoma kwa bidii. Waalimu wake Tabora walimpenda kwa akili zake. Wanafunzi wenziwe nao walimpenda sana kwa sababu alikuwa mcheshi na mwema sana. Waliosoma naye waliwahi kueleza kwamba ingawa alikuwa akienda shule na fedha kidogo sana za matumizi, alikuwa radhi kutoa fedha zote alizokuwanazo kuwasaidia wanafunzi waliokuwa na shida. Pamoja na wema, alionyesha tabia ya kupenda kutetea HAKI. Hakukubali kuona uonevu uliokuwa ukifanywa na ma-kaka dhidi ya wanafunzi. Aliwahi kwenda kwa Mwalimu Mkuu kulalamika kuhusu adhabu ya kufungwa miguu na mikono aliyopewa mwanafunzi mmoja na kaka wa bweni. Kwenye kuamua shauri hilo Mwalimu Mkuu alimpendelea kaka na alimpa mwanafunzi huyo adhabu nyingine ya viboko. Kambarage aliamuriwa kumchapa, ilibidi amchape ingawa hakupenda kabisa kufanya hivyo! Hata hivyo, Kambarage hakuuacha msimamo wake wa kuwatetea waliokuwa wakionewa. Hatimaye, Waalimu waliamua kumpa naye cheo cha ‘Kaka’ lakini hiyo haikuwa dawa. Haikupita muda, alianzisha mgomo wa kupinga mtindo wa ma-kaka kupata upendeleo wa kujigawia chakula kingi kuliko wanafunzi wengine ingawa naye alikuwa kaka!Pamoja na kutetea haki za wanafunzi wenziwe, alidhihirisha uhodari wa kutetea kile alichoamini. Siku moja wakati wa kipindi cha majadiliano, mada ya “Tanganyika iendelee kuwa chini ya utawala wa Waingereza” ilikuwa ikijadiliwa. Katika kuchangia, bila woga wowote mbele ya Mwalimu Mkuu (Mwingereza) Kambarage alipinga kwa nguvu hoja ile na kuelezea waziwazi uovu mwingi uliokuwa ukifanywa na Serikali ya Uingereza katika kuitawala nchi kwa mabavu na kwa misingi ya ubaguzi wa rangi. Mwalimu Mkuu alimkatisha na kumwamuru akae chini asiendelee kuzungumza. Kambarage alihamaki na kuamua kutoka kwenda bwenini kubeba sanduku lake ili akapande gari moshi (treni) kurudi kwao Butiama! Ilibidi Mwalimu Mkuu atume watu kumshawishi arudi shuleni.

JULIUS KAMBARAGE

Akiwa shuleni Tabora Kambarage aliweza kubatizwa na kuwa Mkatoliki akajipa jina la ‘JULIUS’. Mwalimu aliwahi kusimulia kwamba ingawa alianza kuingia kwenye mafundisho ya dini akiwa shuleni Mwisenge, hakuweza kubatizwa kwa sababu mapadri walidhani kwamba angeweza kumrithi baba yake uchifu na hatimaye kuwa na wake wengi! Wamisionari walijaribu sana kumhubiria Chifu Nyerere Burito ajiunge na ukristo bila mafanikio. Mara nyingi mapadri walipomfuata kumhubiria aliishia yeye kuwahubiria wao! Kambarage aliweza kubatizwa baada ya baba yake kufariki mwaka 1942. Wasiwasi wa mapadri ulikuwa umeisha kwa sababu aliyerithi u-chifu alikuwa Edward Wanzagi.Baada ya masomo shuleni Tabora, Julius Kambarage alifanikiwa kwenda Chuo Kikuu cha Makerere. Akiwa huko kidogo kidogo alianza kujihusisha na mambo ya kisiasa. Alianzisha cha chake cha siasa kilichoitwa Tanganyika African Welfare Associate TAWA, na kisha kukifuta na kufungua tawi la chama cha TAA kilichokuwa kimeanzishwa Dar es Salaam kama chama cha kutetea maslahi ya Watumishi wa Serikali waliokuwa wakinyanyaswa na kudhulumiwa na Wakoloni.

MWALIMU JULIUS KAMBARAGE

Mwaka 1945 Julius Kambarage Nyerere alifaulu masomo yake na kupata Diploma ya ualimu. Akarudi kijijini Butiama na kumjengea mama yake nyumba kabla ya kwenda kuanza kazi Tabora. Uamuzi wake wa kutaka kuajiriwa kwenye shule ya misheni ya Mtakatifu Maria Tabora ni kielelezo kimoja cha msimamo wake kuhusu HAKI. Alikuwa amepokea barua mbili za ajira – moja kutoka Serikalini ikimpa nafasi ya kufundisha kwenye shule ya Sekondari ya Tabora na nyingine kutoka kwenye shule ya misheni ya Mtakatifu Maria (St. Mary's). Barua kutoka Serikalini ilimweleza juu ya mshahara atakaopata na marupurupu ya malipo ya pensheni na kwamba shule za misheni hazikuwa na marupurupu yoyote. Julius hakupendezwa na utaratibu wa marupurupu ya walimu wa serikali na misheni kutofautiana. Akaamua kwenda kufundisha shule ya Sekondari ya misheni isiyo na marupurupu yoyote.Tabia yake ya kupenda haki iliendelea kujidihirisha katika shughuli mbalimbali alizofanya akiwa Tabora. Aliendelea kujihusisha na chama cha TAA akawa katibu wa tawi la chama hicho mjini Tabora. Alishiriki kwenye midahalo ya shule za Sekondari na hoja alizotoa zilivutia sana. Katika mdahalo mmoja uliokuwa na mada “Mali ni bora kuliko Elimu” Julius alipinga vikali hoja. Akasema kwamba alichagua kazi ya ualimu ili iwawezeshe watu kuelewa mambo na kwamba wakielewa wanakuwa na furaha, si kwa sababu wana mali. Unaweza kuwa mtu mwenye mali lakini huna furaha!Mwalimu Julius alikuwa na hamu sana ya kwenda ng’ambo kwa masomo ya juu lakini kutokana na msimamo aliokuwanao dhidi ya Serikali, wakoloni hawakutaka kumpa nafasi hiyo. Hatimaye kwa kutetewa na rafiki yake aliyekuwa padri wa kizungu (Father Walsh mwenye nasaba ya Marlknol sisters) aliweza kupewa scholarship na Serikali kwenda Chuo Kikuu cha Edinburgh kuchukua masomo ya historia na uchumi. Akalipenda sana somo la filosofia. Mawazo ya kuingia kwenye siasa yalianza kujengeka wakati huo. Akiendelea na msimamo wake wa utetezi wa haki aliweza kuandika makala mbali mbali. Mbili alizopeleka kwenye mashindano alipata zawadi ya kwanza. Makala moja ilihusu ‘kuonewa wanawake’ akielezea kuhusu unyonge wa wanawake katika maisha ya makabila nchini. Ya pili ilikuwa na kichwa cha habari “Matatizo ya Ubaguzi wa Rangi katika Afrika Mashariki”. Katika makala hiyo alisema Wazungu alikuwa anatawala kudumisha umaarufu wao kwa njia ya unafiki.... Bepari Mhindi alikuwa anapata chakula chake kwa wizi mtupu au ujanja-ujanja na unafiki... Mwafrika naye alikuwa mnafiki alijipendekeza kwa Mzungu wakati moyoni anapasuka kwa wivu na chuki!Alimaliza vema masomo yake huko Edinburgh na kuwa Mwafrika wa kwanza nchini Tanzania kupata Stashahada ya Juu. Aliporudi nyumbani alipokelewa na mchumba wake Maria Magige aliyemchagua mwenyewe si yule aliyetolewa mahari na baba yake. Ikambidi afanye tena zoezi la kujenga nyumba kwa ajili yake na Maria watakapofunga ndoa. Wanakijiji walimshangaa walipomuona msomi kama yeye akichanganya simenti na mchanga kufyatua matofali kwa ajili ya kujengea. Wasomi hawakupaswa kufanya kazi kama hizo! Julius na Maria walifunga ndoa tarehe 24 Januari 1953 kwenye kanisa Katoliki Musoma. Katika maisha yao ya ndoa waliweza kuwapatia watoto 7, watatu wa kike na wanne wa kiume.

AWA KIONGOZI

Baada ya mapumziko yake Butiama Mwalimu Nyerere alienda kuanza kazi ya kufundisha katika shule aliyopangiwa ya Pugu Sekondari, Dar es Salaam. Mwaka huo wa 1953 akiwa Pugu alianza kujihusisha kikamilifu na shughuli za chama cha TAA. Aliitembea kwa miguu na wakati mwingine kwa baiskeli ya kua zima umbali wa maili 12 kwenda mjini Dar es Salaam kuhudhuria mikutano na shughuli za chama hicho. Haikupita muda akili na uwezo mkubwa aliokuwanao ulidhihirika akachaguliwa kukiongoza. Kutokana na uongozi wake mahiri chama cha TAA kikabadilishwa kuwa chama kamili cha siasa tarehe 7 Julai 1954, kikaitwa TANU.Chini ya uongozi wake baada ya kuanzishwa kwa chama cha TANU zilianza rasmi harakati za kupigania Uhuru. Pamoja na juhudi zote za Wakoloni kuchelewesha kupatikana kwa Uhuru hatimaye mwaka 1960 nchi ya Tanganyika ilifanikiwa kupata Serikali ya Madaraka. Desemba 9 1961 ikapata Uhuru kamili ,Mwalimu akawa Waziri Mkuu. 1962 nchi ya Tanganyika ikawa Jamhuri akawa Rais wa Kwanza wa Tanganyika Huru.Simulizi kuhusu uongozi uliotukuka miaka 24 wa Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Tanzania unahitaji makala nyingine nyingi. Hakuna maelezo mafupi yanayoweza kutosheleza historia ya uongozi wake. Itoshe kusema alikuwa kiongozi shupavu sana aliyepigania uhuru wa nchi yake na wa nchi zingine za Afrika. Alijishusha na kuwa pamoja na wananchi aliowaongoza – shida zao aliziona ni zake, zilimgusa na kumnyima usingizi! Akaondoa ubaguzi na kufuta matabaka ya walionacho na wasionacho. Akafuta ukabila na udini nchini. Watanzania wakaishi kidugu. Akafanikiwa kujenga AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO akiongozwa na dira ya MAENDELEO YANAYOLENGA WATU WOTE. Akafanya Tanzania ijulikane kuwa kisiwa cha AMANI duniani.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipendwa na kuheshimika sana ndani na nje ya nchi. Mwaka 1985 aliamua kwa hiari yake mwenyewe kuacha uongozi wa Taifa ili apumzike. Alizunguka nchi nzima kuwaaga Watanzania. Kwa mapenzi makubwa wakampa zawadi za kila aina. Wananchi walionyesha wazi huzuni waliyokuwanayo kwa uamuzi aliouchukua. Walimuaga wakilia machozi!Yote aliyoyaanza tangu utoto wake yalifikia kikomo tarehe 14 Oktoba 1999 alipoaga dunia kwenye kitanda cha hospitali ya Mtakatifu Thomas mjini London alikokwenda kwa matibabu. Kabla hajafariki dunia aliwakumbuka Watanzania wake akasema: “Najua nitakufa sitapona ugonjwa huu. Ninasikitika kuwaacha Watanzania wangu, najua watalia sana. Lakini nami nitawaombea kwa Mungu.” Naam, Watanzania wake walilia sana walipopata taarifa za kifo chake. Mwili wake ulipoletwa nchini waliomboleza kwa uchungu mno. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizikwa kijijini kwake Mwitongo Butiama kwa heshima zote na wananchi wa Tanzania, na wa mataifa mbalimbali wakiwemo viongozi mashuhuri waliokuja kwa ajili hiyo.Ni dhahiri msingi wa yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia utaendelea kudumu ndani ya mioyo ya kizazi chake, kizazi hiki na vizazi vijavyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa Muasisi na Baba wa Taifa katika kujenga taifa la Tanzania. Huyo ndiye mtoto aliyezaliwa siku ya mvua na kupewa jina la mzimu wa mvua KAMBARAGE; mwana wa Chifu Nyerere Burito na Mgaya wa Nyang’ombe. Ni dhahiri, tarehe aliyozaliwa – 13 Aprili mwaka 1922, Mgaya hakujua kwamba alikuwa amejifungua mtoto ambaye angekuja kuwa kiongozi maarufu sana nchini na duniani, aliyewapenda binadamu wote na kuwatumikia Watanzania kwa moyo wake wote, akili na nguvu zake zote!

Sasa tuje kwenye uwanda wa harakati za ukombozi na ukweli wa mambo, nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo. Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana,

Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa. Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya mchikichini Mzizima na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 34 tu, hiyo ni mwaka 1880 hadi 1953 Nje ya kuhudumu katika uislamu, alikuwa ni mvuvi aliyevua pamoja na Ally Ramadhan mwekahazina wa kwanza wa AA,

Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL) Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele za cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake! Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia. Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu, Woga.

Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere.

Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake. Mnamo tarehe 7/7/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia! Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 , Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa Kasisi Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni boss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 kila mwezi angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.

Imeandikwa na
Yericko Nyerere

Rais Kikwete azindua Kozi Maalum ya Maadili ya Uongozi; Amsimika Msekwa Uenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa shughuli tayari kuzindua Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Programu ya Uongozi na Maadili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Programu ya Uongozi na Maadili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsimika rasmi Mzee Pius Msekwa kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es Salaam leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mzee Pius Msekwa akitoa shukurani baada ya kusimikwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.

Rais Jakaya Mrisho Meza kuu akiwa imesimama na meza kuu kuimba wimbo wa Taifa baada ya uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.

Picha: IKULU

Waziri Membe aanza ziara ya kikazi Qatar, Kuwait na Oman

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (Mb.) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Quatar Mh. Dkt. Khalid Mohamed Al Attiyah, walipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Quatar pia kutangaza Fursa za uwekezaji nchini Tanzania. Waziri Membe yupo nchini Quatar kwa madhumuni ya kushiriki mkutano kuhusu Kuzuia Uhalifu na Haki za Wahalifu.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameanza ziara ya kikazi katika nchi za Qatar, Kuwait na Oman kuanzia tarehe 11 – 17 Aprili 2015.

Katika nchi ya Qatar, Mhe. Waziri atashiriki Mkutano wa 13 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Uhalifu na Haki za Wahalifu (Crimes Prevention and Criminal Justice). Aidha, Mhe. Waziri atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Al-Attiyah. Mazungumzo yao yatahusu masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar; fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini pamoja na fursa za ajira kwa Watanzania nchini Qatar.

Atakapokuwa nchini Kuwait, Mhe. Membe ataonana na Mwenyeji wake, Mhe. Sabah al Khalid al Sabah, Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait. Viongozi hao wawili wataongelea suala la Tanzania kufungua Ofisi ya Ubalozi nchini Kuwait. Aidha, Waziri Membe ataonana na viongozi wa Mfuko wa Kuwait kujadili suala la kufadhili miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Katika nchi ya Oman, Waziri Membe pia ataonana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mhe. Yusuf bin Allawi bin Abdullah. Viongozi hao pamoja na mambo mengine, watajadili ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji.

Waziri Membe atarejea nchini tarehe 17 Aprili 2015.

Imetolewa na Kitengo cha mawasiliano ya Serikali, 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Tarehe 13 April 2015

Rasilimali za Bank M Tanzania zafikia bilioni 728/=

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M Tanzania, Bi Jacguline Woiso, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kuongezeka kwa rasilimali za benki hiyo kutoka sh. Bilion 689 mwaka 2014 hadi sh. bilion 728.
Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Bw. Allan Msailiwa.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M Tanzania, Bi Jacguline Woiso akifafanua jambo alipoongea na waandishi wa habari, wakati akijibu maswali aliyoulizwa, Dar es Salaam leo.

Chama kipya cha siasa "Ujamaa na Uzalendo" chasajiliwa

 Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, (kulia) akimkabidhi hati ya Usajili wa Muda wa chama cha Kijamaa na Uzalendo (C.K.U.T), Mwenyikiti wa chama hicho Ramadhan Semtawa. Jijini Dar es Salaam. 

CHAMA cha siasa ili kiweze kuendeshwa vizuri kwa misingi ya utawala bora na baadae kifikie malengo yake ya kuchukua dola ni lazima kiwe na katiba yenye misingi ya kidemokrasia.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa, Sisty Nyahoza wakati wa kukabidhi cheti cha muda kwa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (C.K.U.T).

Alisema demokrasia ya kweli ni muhimu kuanza kujengwa ndani ya chama kwani itawasaidia viongozi kufikia malengo waliyojiwekea.

Nyahoza alisema viongozi pia wanawajibu wa kusoma sheria ya vyama vya sisasa ili kuepuka migongano na watendaji wa taasisi zingine za serikali.

“Leo tumetoa cheti cha usajili wa muda kwa chama cha C.K.U.T, tunawaomba sana viongozi wa chama hiki kukaa pamoja na wanachama wenu ili kupeana mawazo mazuri ya kujenga chama,asitokee mmoja wapo na kusema kuwa yeye ndiye mwenye chama, hivyo someni vizuri sheria ya vyama ili msiwe na mgogoro na taasisi zingine,” alisema.

Naye Msajili wa Vyama vya Siasa, Mstaafu Jaji Francis Mutungi alisema ofisi ya msajili ni taasisi hivyo itawahudumia watu wote wanaohitaji huduma.

Mwenyikiti wa Chama cha C.K.U.T, Ramadhan Semtawa. Jijini Dar es Salaam akifafanua jambo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Noel Antapa.

Mwenyekiti wa chama cha C.K.U.T Ramadhani Semtawa alisema wameanzisha chama kwa malengo maalumu ya kurejesha nchi kwenye misingi ya waasisi.

Alisema kumekuwepo kwa rushwa na masuala la kidini kumechangia nchi kuyumba na kutoka katika misingi ya kidemokrasia na utawala bora.

“Watu wanauwa kwa sababu za kidini na wengine upoteza maisha yao kwa imani za kishirikina, lakini pia wapo watu wamekuwa wakila fedha za serikali na awachukuliwi hatua yoyote, tunataka kuja kuibadilisha nchi hii maana aina muelekea kwa sasa,” alisema.

Semtawa alisema kinachofanyika sasa ni kutafuta wanachama ili waweze kupata usajili wa kudumu.

“Tunatakiwa tuwe na wanachama 2000 katika mikoa kumi na kila mkoa mmoja inatubidi tupate wanachama 200, tumejipanda vizuri na tunaamini kuwa tutapata usajili wa kudumu,”alisema.

Aidha Semtawa alisema awatahitaji kiongozi yoyote kutoka katika vyama vya upinzani kujiunga na chama hicho.

Mwenyekiti na Muasisi wa Chama cha kijamaa na uzalendo Tanzania,Ramadhani Semtawa akiwa ameshika katiba ya chama hicho na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Noel Antapa akiwa katika viwanja va ofisi ya msajili wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam.

 • via HabariMseto blog

Names of 10 Innovation Prize for Africa Awards nominees


A record 925 applications from 41 countries representing the continent received for IPA 2015 from Africa’s most talented innovators

ZURICH, Switzerland, April 13, 2015/ -- What do an environmentally-friendly minicab, a water distillation system and a fire alert detector have in common? They all represent outstanding innovation talent across Africa, applied for the celebrated Innovation Prize for Africa (IPA)  award this year, and are now being considered for the grand share prize of US$150 000! Since its inaugural launch in 2011, IPA has gathered great momentum, and is now recognized for leading the innovation frontier in Africa by rewarding innovators for their home-grown, market-led innovations that contribute to Africa’s growth, development and prosperity.

This year, AIF received a record 925 applications from 41 countries for its prestigious IPA awards, surpassing the previous year’s entry record of 903. The awards ceremony will be held on 12-13 May in, Skhirat, Morocco, a country fast trending as an innovation hub in Africa. The African Innovation Foundation (AIF) is partnering with the Ministry of Industry, Trade, Investment and the Digital Economy to host the 4th edition of IPA which has received eminent patronage from His Majesty King Mohammed VI of Morocco.

H.E.  Moulay Hafid Elalamy, Minister of Industry, Trade, Investment and the Digital Economy for Morocco expressed his enthusiasm to be co-hosting the IPA 4th edition in Morocco: “We have a strong commitment with AIF to unlock the innovation potential of the continent. The ambition is to make Africa a juncture of innovative and prosperous nations." By focusing on the unchallenged role of innovation in the development of economies, Mr. Elalamy added that "in Morocco, the commitment to promote research and innovation mobilizes both the government and private sector decision makers who join their efforts to make the national innovation system a force for development.“

This year’s finalists showcase a diverse range of innovations from agriculture, to education and e-health. The 10 nominees for IPA 2015 are:

 1. -Adnane Remmal, Morocco: A patented alternative to livestock antibiotics. This is a composition of natural phenolic molecules with anti-microbial (anti-bacterial, anti-parasitic, anti-fungal) properties. The natural, innovative formula reduces the health hazard to cattle and humans, and prevents the transmission of multi-resistant germs and possible carcinogens through meat, eggs and milk to humans at no extra cost to farmers.
 2. -Alex Mwaura Muriu, Kenya: Farm Capital Africa is a well developed risk sharing agri-business funding model that draws in investors for a share of farming profits. The initiative identifies, screens and shortlists full-time farmers with small holdings and helps them devise farming plans to attract potential investors who earn profits over time. This is a viable solution to address the inability of committed, small scale African “agripreneurs” -- who lack collateral and credit history to access traditional financing—from expanding their operations. An attractive farming initiative and investment option for those with extra capital, benefitting both small scale farmers and investors.
 3. -David Gluckman, South Africa: Lumkani fire detection. An off-the-shelf fire detection device and alert service that uses radio frequency (RF) transmission technology suitable for informal dwellings. In the event of a fire, the device triggers an alarm to alert the family. Within 20 seconds, the device transmits a signal that sets off heat detectors in a 60 meter radius to elicit a community-wide response to the fire. This device prevents fires from ravaging high population density communities and boosting community mobilization efforts.
 4. -Jean Bosco Kazirukanyo, Burundi: New type of cement "OSP" that protects waters against carcinogenic lubrication oil spills. A new formulation of cement that can be sprinkled on fresh or old lubricant and oil spills. The cement chemically reacts with the contaminants to form tiny lumps that can be easily removed and deposited in designated plastic bins before being transported to concrete plants where they can be used as concrete additives. This innovation effectively contains and recycles ecologically harmful oil spills that are currently being disposed of in an unsustainable manner across Africa, causing huge ecological damage.
 5. -Johann Pierre Kok, South Africa: Scientific engineering educational box: ‘Seebox’. A scientific engineering educational box that allows children to enjoy a practical and experimental way of learning the sciences and electronics, and measuring almost anything electronic or scientific. ‘Seebox’ also offers short videos explaining what is being measured. This tool addresses the shortage of electronic and scientific professionals, and affords children the opportunity to learn first-hand the principles of science and electronics by building, measuring and experimenting.
 6. -Kyai Mullei, Kenya: M-changa, also known as E-harambee. A mobile application that empowers individuals and organizations to initiate and manage fundraisers via sms or web devices in an efficient and cost effective way. Combining mass market mobile communication with money transfer technologies, m-changa allows users to solicit support for a cause, track contributions, and withdraw funds using their mobile phones without relying on internet connectivity. This innovation brings the benefits of mobile technology to all Africans, integrating unique aspects of African culture with technological innovation.
 7. -Lesley Erica Scott, South Africa: Smartspot TBcheck. Smartspot’s flagship product, TBcheck examines the accuracy of machines used to detect TB diagnosis. They are designed to assess whether these machines are functioning optimally. Unlike other products, TBcheck is easy and safe to use and can be delivered to laboratories safely and economically. This will make diagnosing TB far easier and might go a long way in curbing the TB epidemic in Africa. Today TB is second only to HIV and AIDS as a leading cause of death in the continent.
 8. -Marc Arthur Zang, Cameroon: The cardio-pad. An affordable tablet that records and processes the patient’s ECG (heart signal) before transferring it to a remote station using mobile phone networks. The device can be used in village hospital and clinic settings in the absence of a cardiologist. ECG results can be downloaded on a tablet by the cardiologist. The examination is then interpreted using cardio-pad’s computer-assisted diagnostic embedded application, then results and prescription transmitted to the nurse performing the procedure. This will ensure effective monitoring of heart patients living in rural areas with limited or no access to cardiologists.
 9. -Neil Du Preez, South Africa: Mellowcabs. This is a suite of technologies that includes recovering the kinetic energy that is typically lost in the braking process, converting it into electricity and storing it. Other associated innovations include hydrogen fueled Mellowcabs, adaptable, renewable body shells and an app to book cab rides that can be paid for with cash or credit. Its user-friendly services include tracking the cab’s location, wifi access and mobile charging during the ride. The minicab service fills the gap for commuters who need organized, safe and affordable micro transport within a three mile radius. This environmentally-friendly taxi service also eases traffic congestion in cities without causing pollution.
 10. -Samuel O. Otukol, Uganda: Water distillation system and process (dsp). This innovation proposes an alternative source of viable drinkable water in areas of water shortage or where only sea water is available. Salty water is evaporated at low temperatures (30 to 50 degrees Celsius) and then condensed into fresh water at lower costs than incurred using reverse osmosis. The proposed process can also use solar energy in remote areas. It helps water shortages in drought-stricken areas, or where existing desalination methods have proved ineffective. 

The panel of highly qualified IPA judges examined all entries through a rigorous process which included validation by technical experts. The calibre of entries this year was particularly impressive, says Chairman of the IPA 2015 selection panel, McLean Sibanda, noting that IPA has continued to gain importance and greater recognition each year, seen in the quality and depth of applications: “Shortlisting the top 10 was no easy task as each of the top 25 innovations are a response to a need or challenge within our communities. The IPA is indeed an important platform - not only for showcasing Africa’s ability to innovate to address its own challenges, but also for celebrating Africa’s ingenuity”.

Three winners will be chosen and announced in a glittering ceremony to be held in Skhirat, Morocco on 13 May 2015. The US$150 000 cash prize is shared between the winners, with the most outstanding innovation receiving US$100 000, and two prizes of US$25 000 for innovation with the highest social impact and best business potential respectively.

Reflecting on IPA achievements in catalysing the innovation spirit in Africa, Jean Claude Bastos de Morais, AIF and IPA Founder said: “The IPA has come a long way since its inception in 2011. The first major milestone was achieved in 2012 when the African Union (AU) and the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) passed a resolution to promote an innovation society for Africa’s socio-economic transformation. Today the IPA is playing a fundamental role in showcasing the continent’s immense potential to become thriving innovation economies. Year after year, the innovations that are presented for the IPA comprise high-value African solutions with positive socio-economic impact, and this year is no exception.”

Besides rewarding excellence in innovation on 13 May 2015, Skhirat will be showcasing yet more innovation through an innovation marketplace, an innovative Ideas Machine workshop targeting young visionaries and a press conference. With an impressive line-up of CNBC coverage, quality entertainment from Africa’s number 1 music extraordinaire, Youssour N’Dour, an innovator himself, and Lerato Mbele, presenter of Africa Business Report on BBC World News compering this ceremony, IPA 2015 promises to be the calendar event of Africa.

About Africa Innovation Foundation's Innovation Prize for Africa:

Africa Innovation Foundation (AIF) works to increase the prosperity of Africans by catalyzing the innovation spirit in Africa.

Innovation Prize for Africa (IPA) is a landmark initiative of the AIF and mobilizes African innovators to invest in African-led solutions to ensure a sustainable, prosperous Africa. Details on IPA 2015 events can be found on http://event.innovationprizeforafrica.org/

For more information on IPA 2015, contact:

For the African Innovation Foundation
Aulora Stally
Communications Manager
Strehlgasse 4
8001 Zurich, Switzerland

E-mail: [email protected]
Phone: +41 44 79 834 9163

For the Ministry of Industry

Trade, Investment and Digital Economy
Taoufiq Moucharraf
Communications Director
E-mail: [email protected]
Phone: +212 661 522 801.

Find us on:

The Internet: www.africaninnovation.org
Facebook: https://www.facebook.com/InnovationPrizeforAfrica
https://www.facebook.com/AfricanInnovationFoundation

Twitter: @AfrinnovFdn; @IPAPrize

Most doctors in Tanzania can’t correctly diagnose

Lest you think Tanzania’s challenges with basic services were limited to education, here’s an eye-opening statistic on health services, from the same World Bank study cited above. 

Researchers presented clinicians with hypothetical patients, suffering from a variety of symptoms that commonly afflict Tanzanians, and tested whether they could offer a correct diagnosis. Shockingly, only 27 percent of doctors could correctly diagnosis malaria with anemia, and 29 percent could correctly diagnose diarrhea with severe dehydration — two leading causes of death for Tanzanians.

Tanzania Fair Competition Commission on a study tour in Malawi

A six-­member delegation from the Tanzania Fair Competition Commission (FCC) is expected to jet in Malawi this weekend on a 7-day study tour, reported the MaraviPost in BLANTYRE, Malawi last Thursday, April 9, 2015.

That, according to Malawi’s Competition and Fair Trading Commission (CFTC), a government agency mandated to regulate, monitor, control and prevent acts or behavior that adversely affect competition and consumer welfare, the delegation will be in the country from 12 April to April 18 2015. 

Led by the Chairman of the Tanzanian Fair Competition Commission, Prof Samuel Wangwe, it is reported that the delegation is scheduled to meet a number of local stakeholders that deal with issues of fair competition and consumer protection. It will also meet stakeholders in the energy, telecommunications, standards setting, and financial sectors. 

Tanzania grants license to China Commercial Bank

THE Bank of Tanzania has licensed China Commercial Bank (CCB), to operate in the country bringing to over fifty, the number of financial institutions in the country.

According to the Central Bank, (BoT), the new bank has no banking affiliation with another bank in China or Tanzania.

The BoT Director of Banking Supervision, Mr Agapiti Kobelo, said CCB were on final stages of commencing operations with head quarter in Dar es Salaam.

Late last year BoT Governor, Prof Benno Ndulu, told Daily News that the CCB was a new bank formed by Chinese and Tanzanian businesspersons--with no additional link.

"It has no direct connection with any existing bank in China, except for some shareholders who are Chinese," Prof Ndulu said. Analysts suggest the bank could not have come at a better time.

Tanzania and China enjoy long standing friendship and cooperation thriving on the strong foundations built by the founding fathers of the nations, namely Mwalimu Julius Nyerere and Mao Zedong.

Bilateral trade between the two countries amounted to 3.7 bn US dollars in 2013 while Chinese investments in Tanzania reached 2.5bn US dollars with more than 500 Chinese companies doing business in the country.

The licensing of a new bank means one more player to the industry and it is believed that its entry will contribute in increasing the level of financial inclusion and also provide employment to Tanzanians.

A Global Microscope 2014 by The Economist Intelligence Unit shows that Tanzania is the first country in Sub-Saharan Africa and ninth globally for demonstrating sound financial inclusion.

Rapid growth in the number of Tanzanians with access to financial services shows it will reach 50 per cent target by 2016 as set by the National Financial Inclusion Framework.

In Sub-Saharan Africa, Tanzania scored 56 out of 100 points followed by Kenya and Rwanda which scored 55 each. Ghana, Nigeria and Uganda scored 51, 50 and 50 points respectively. The average score for Sub- Saharan Africa is 44.

Pata Vodacom ZTE kwa Sh 40,000


Vandalism forces Tanzania to recruit people to save historical monuments


Uhuru Monument Aug 2011.jpg
"Uhuru Monument Aug 2011" by Arthur Buliva (accessed online by wavuti.com 04.13.2015)


by Xinhua, Arusha -- Authorities in northern Tanzania have started working on measures towards preserving the country’s iconic historic features and tourist destinations which are being targeted by vandals and thieves, an official said on Saturday.

Reports have it that thieves are looking to illegally remove bronze, copper or other metals to sell on for scrap.

Arusha Declaration Monument, one of the iconic features of the northern Tanzania’s tourist hub of Arusha, is now under threat from vandalism.

This is raising fears on the security of other tourist attractions in the country’s tourist hub, after a plaque made of copper displayed below the monument with inscriptions of its significance to the history of the town and country has been plucked off by unknown people.

Arusha City Mayor Gaudence Lyimo said on Saturday that his office has started working on a programme to ensure all the monuments are protected for the current and future generations.
He attributed the situation to the failure by the Arusha City Council authority to recruit staff responsible for caring historical sites.

“So, we are going to recruit persons who will be responsible for taking care of the facility,” he said.
The monument was unveiled in 1977 to commemorate 10 years of Arusha Declaration, the Tanzania’s most prominent political statement of African socialism and self-reliance.

The northern zone manager of the Tanzania Tourist Board (TTB) Willy Lyimo expressed his worries on the theft and little care taken, saying this could impact on the number of visitors seeking information on important sites in Arusha.

“The visitors will not get important information on the monument,” he said, noting that the statute used to attract significant number of visitors, including tourists.

“This is a place where Arusha Declaration was born. Yet it is under threat of being further vandalized,” he said, adding that the changing management of the site between different government ministries and departments may have complicated matters.

One of the items plucked off the towering monument in the heart of the town is a plaque made of copper which was displayed below the monument amid claims of little care of the facility.

Lyimo said TTB has struggled to seek information contained in the plague carted away from the Antiquities Department of the Ministry of Natural Resources and Tourism but without any success.
He says the tourism promotion body was keen to restore the damaged part of the monument by having another plaque with vital information on Arusha Declaration but with little support from other stakeholders.

Arusha regional police chief Liberatus Sabas pledged to work on the threat by tracking down the culprits.

Arusha Declaration Monument is one of the iconic historical features of Arusha, the others being the Clock Tower and the Natural History Museum. Both of them attract thousands of visitors every year.
The Clock Tower is said to be midway between Cairo and Cape Town while the Natural History Museum has thousands of collections of hominid remains picked from Olduvai Gorge and other areas in northern Tanzania.

Maombi ya kazi kutoka Utumishi wa Umma sasa ni online


SEKRETARIETI ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inatarajia kuzindua mfumo mpya wa utumaji na upokeaji maombi ya kazi kwa njia ya mtandao utakaojulikana kama “Recruitment portal”.

Afisa habari wa Sekretarieti hiyo, Kassim Nyaki, amesema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kuboresha utendaji kazi wa taasisi katika kufikisha huduma kwa wateja.

Nyaki ametaja lengo lingine kuwa ni kukidhi mahitaji ya wadau, kuwafikia waombaji wengi wa nafasi za kazi na kudhibiti udanganyifu kwa kurahisisha ukaguzi na kuhakiki taarifa za waombaji.

Amesema, mfumo huo utawasaidia waombaji hao kuunganishwa na mifumo ya taasisi mbalimbali, pia kukidhi maelekezo ya sera mbalimbali za utumishi wa umma pamoja na Dira ya Taifa ya mwaka 2025.

Kwa mujibu wa Nyaki, walifanya majaribio ya kupokea maombi ya kazi kwa kutumia mfumo huo, kwa matangazo ya kazi matano ambayo yaliwahusu waajiri mbalimbali serikalini na mwitikio ulionekana kuwa mzuri wa kupokelewa na watu wengi.

Amesema, mfumo huo utapunguza changamoto baadhi ikiwemo ya barua kutofika kwa wakati, kupotea kwa kutumia njia ya posta, mrundikano wa barua na kuepuka gharama zisizo za msingi.

“Taratibu za uzinduzi rasmi wa mfumo huu, zitafanyika hivi karibuni, ambapo tunatarajia kupunguza muda wa uendeshaji wa mchakato wa ajira kwa asilimia 34. Tunatoa wito kwa waombaji kazi wote kutumia mfumo huu kwa kuingia katika mtandao wetu http://portal.ajira.go.tz ili kutuma wasifu binafsi (CV) pamoja na vyeti,”

Taarifa ya Sarafina Lidwino - MwanaHALISI OnlineCall for applications: SABMiller Royal Society Exchange Programme

The SABMiller Royal Society Exchange Programme will provide awards of three years' duration to enable African scientists in sub-Saharan Africa to partner with UK-based institutions.

Aims of the scheme

The Royal Society has received funding from SABMiller plc to support a 5 year programme to expand its capacity building activities in Africa. As a result, the Royal Society has launched a new scheme, the SABMiller Royal Society Exchange Programme, aimed at supporting collaborative research projects between researchers in the UK and researchers in sub-Saharan Africa. The programme will focus on, but not be restricted to Ghana and Tanzania.

The SABMiller Royal Society Exchange Programme will concentrate on threeresearch areas:

 • Water and Sanitation – including water engineering and irrigation, waste water management, and other related projects
 • Agriculture (except animal or veterinary science) and Crop Science (land, soil management and crop production)
 • Renewable Energy – including solar-/wind-/hydro-energies, energy capture and storage and other related projects

Eligibility requirements

The applicant must:

 • have a PhD or equivalent research experience
 • hold a permanent or fixed term contract in an eligible university or research institute which must span the duration of the project

Collaborations should be based on a single project between “the applicant” (UK based scientist) and “co-applicant” (African based scientist).

Applicants should ensure that they meet all the eligibility requirements, which are explained in the scheme notes.

Value and tenure

The award will cover the costs of:

 • travel and subsistence up to £5,000 per year for training purposes 
 • funds up to £2,000 per year for research costs

The award lasts for 3 years. The total value of the award over 3 years is £21,000.

Application process

All applications are reviewed and assessed by two members of the selection panel who have the most appropriate scientific expertise. It is expected that applicants will be notified of the outcome of their application by email about 4 months after the application deadline.

Applying for this scheme

This scheme is currently open to applications and will close on 28 May 2015.


Aliyekuwa Mbunge wa Kyerwa ahamia CHADEMA

Benedicto Mutarchoka Mutungilehi
Benedicto Mutarchoka Mutungilehi

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kyerwa mkoani Kagera kati ya mwaka 2000 hadi 2005, Benedicto Mutungirehi, amekihama Chama chake cha Tanzania Labour (TLP) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mutungirehi ambaye ni mwanasiasa msomi, amefikia uamuzi huo jana jimboni Kyerwa na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu.

Akiongozana na wanachama wenzake 26 wa TLP, Mutungirehi alikabidhiwa kadi ya CHADEMA na mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kyerwa, Deus Rutakyamirwa.

Katika uchaguzi mkuu wa 2000, Mutungirehi alishinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini akaenguliwa kwenye vikao vya uteuzi, jambo lililowafanya wananchi wa Kyerwa kumlazimisha ahamie upinzani.

Baada ya kutii sharti hilo, wananchi walimchagua kwa kura nyingi kuwa mbunge wao na hivyo kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Justuce Katagira.

Hata hivyo, katika uchaguzi mkuu uliofuata mwaka 2005, Mutungirehi aliangushwa na Katagira ambaye analishikilia jimbo hilo hadi sasa kutokana na TLP kupoteza mvuto baada ya mwenyekiti wake, Augustine Mrema kuporomoka kisiasa.

Zimekuwepo juhudi za muda mrefu sasa za wananchi wa Kyerwa kumshawishi Mutungirehi ahamie CHADEMA na kugombea ubunge kutokana na chama hicho kujijengea mtandao mkubwa ambao unampa uhakika wa kushinda.

Mutungirehi alirejea rasmi katika siasa za jimbo la Kyerwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo alikuwa mgeni rasmi kakika mkutano UKAWA uliofanyika Nkwenda Stand na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

MwanaHALISI "fact check": Zitto Kabwe mwongo

Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.

KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameendelea kuwadanganya wananchi kuwa kufukuzwa kwake katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumetokana na umakini wake wa kufuatilia “mambo yanayowakandamiza wanyonge.”

Akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Ruvuma, Zitto amesema baada ya kutambua baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawataki kuwatumia wanyonge kwa kuwapigia kura na kujipatia ruzuku, yeye wenzake wengine wameamua kuanzisha chama kitakacho watetea wanyonge wakiwemo wakulima ambao nguvu zao zikiisha wanakufa maskini.

Amedai kuwa yeye ndiye aliyeibua hoja ya mkataba wa madini wa Buzwagi ambako waziri wa nishati na madini, alifutwa kazi; hoja ya kumng’oa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa, Operesheni Tokomeza, wanaoficha fedha nje ya nchi na sakata la Escrow.

Amewataka wananchi wasiamini madai kuwa yeye ni msaliti bali wawapime wabunge wao kwa kazi walizozifanya.

Hata hivyo, katika yote aliyoeleza Zitto hakuna hata moja ambalo ni kweli.

Mathalani, hoja ya mkataba wa Buzwagwi, iliibuliwa na gazeti la kila wiki la MwanaHALISI; katkka sakata la Buzwagwi, kinyume na madai yake, hakuna waziri hata mmoja aliyefutwa kazi.

Aliyekuwa waziri wa nishati na madini, Nazir Karamagi ambaye alisaini mkataba huo nchini Uingereza, alifutwa kazi 18 Februari 2008, kutokana na kashifa ya maarufu ya Richmond.

Sakata la Richmond liliibuliwa bungeni na Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa chini ya aliyekuwa mbunge wa Bumbului (CCM), William Shelukindo.

Vilevile, kinachoitwa “Operesheni Tokomeza,” kiliibuliwa bungeni na Christopher ole Sendeka, mbunge wa Simanjiro (CCM).

Kamati Kuu (CC) ya Chadema, ilimfukuza uanachama Zitto na wenzake watatu – Prof. Kitila Mkumbo aliyekuwa mjumbe wa CC na Samson Mwigamba aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha – kwa madai ya usaliti, kusingizia viongozi wakuu wa chama na kushirikiana na maadui wa chama.

Akisoma maamuzi ya CC, tarehe 22 Novemba 2013, mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu alisema, Zitto na genge lake wametuhumiwa kwa makosa 11 ya usaliti, yaliyotokana na “Waraka wa Mabadiliko.”

Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Kitila, ulilenga kuteka chama na kukikabidhi kwa maadui wa chama wakiwamo watu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Zitto ndiye aliandaliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho; naye akakiri kutaka kufanya mapinduzi ya uongozi kinyume na katiba.

“…baada ya kumsikiliza Dk. Kitila, Kamati Kuu imebaini kuwa mkakati huo haukulenga kumfanya Zitto kuwa mwenyekiti pekee, bali ulikuwa na malengo makubwa ya kukibomoa chama hicho,” ameeleza Lissu.

Amesema, Zitto alikihujumu chama hicho na kushiriki kujitoa kwa wagombea wake wa ubunge katika majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini, Singida Mjini na kuwa mwaka 2006, alipewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM).

Tanzania tests drones to save elephants
Concerned about Tanzania’s dissipating elephant population, the creatively named Tanzanian Private Sector Foundation will try using drones to spy on poachers in the Selous Game Reserve in the south of the country. The French and American-produced drones will fly unmanned between April 27 and May 4 in hopes of aiding law enforcement agencies in tracking down poachers.

According to National Geographic, throughout Africa approximately 100,000 elephants were poached between 2010 and 2012. The World Wildlife Fund reports the two biggest threats against African Elephants are poaching and changes in land use. In 1989, the Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Fauna and Flora enacted a ban against the international trade of ivory, but the act continues illegally, especially in China, the largest importer of elephant tusks. In February, the country banned the import of ivory for one year because of its impact on African elephant populations.

If the drones are successful, the business federation will look to get government approval to permit drone deployment by private companies.

Afungwa maisha jela kwa kumbaka mwanaye wa miaka 9 na kumpa mimba akitimiza masharti mganga ya kumtibu mkewe

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Shinyanga imemhukumu kifungo cha maisha jela mkazi wa mtaa wa Kitangili katika manispaa ya Shinyanga baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mtoto wake wa kambo, mwanafunzi wa darasa la tatu.

Alimbaka mtoto huyo kutimiza masharti ya mganga ili kutoa tiba kwa mkewe.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi mwandamizi wa wilaya, Thomson Mtani alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Judith Tuka.

Mtuhumiwa Osward Charles (45) mkazi wa Kitangili alifikishwa mahakamani kwa tuhuma mbili. Kosa la kwanza likiwa ni kumbaka mtoto wake mwenye umri chini ya miaka kumi ambaye ni mwanafunzi kinyume na kifungu namba 130, kifungu kidogo cha kwanza na cha pili na kifungu namba 131 kifungu kidogo cha pili cha sura ya 16 cha kanuni ya adhabu.

Kosa la pili ni kumwingilia kimwili mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa shule na kumpa ujauzito kinyume na kanuni ya tano ya sheria ya elimu ya mwaka 2003 inayotoa adhabu kwa watu wanaowaoa na kuwapa mimba wanafunzi wa shule kama ilivyo katika kifungu cha 35 kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya elimu ya 353.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka mwanasheria wa serikali Judith Tuka kuwa, kati ya Novemba 12 mwaka 2012 na Septemba katika eneo la mtaa wa Kitangili manispaa ya Shinyanga mshitakiwa alimbaka mtoto wake wa kambo ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia ujauzito.

Awali mshitakiwa katika mwenendo wa kesi alikana kutenda makosa hayo lakini katika utetezi wake mbele ya mahakama kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo ili mahakama impunguzie adhabu alikiri kumbaka mtoto wake mbele ya mama yake mzazi kwenye kitanda kimoja baada ya kupewa maagizo ya mganga wa jadi kama sehemu ya tiba ya mke wake aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi.