Hotuba ya Rais Kikwete alipozungumza na viongozi wa dini Dar

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, WAKATI WA MAZUNGUMZO NA KAMATI YA HAKI NA AMANI YA VIONGOZI WA DINI MKOA WA DAR ES SALAAM, UKUMBI WA MIKUTANO WA JULIUS NYERERE, DAR ES SALAAM, TAREHE 28 MACHI, 2015


Sheikh Alhadi M. Salum, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam;
Mhasham Askofu Valentino Mokiwa, Kaimu Makamu Mwenyekiti,;
Fadha John Solomon, Katibu wa Kamati ya Haki na Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam;
Wajumbe wa Kamati ya Haki na Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam;
Viongozi wa Dini;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Shukrani
          Nianze kwa kuungana na walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetuwezesha kukutana siku hii ya leo tukiwa na afya njema.  Nawashukuru Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Haki na Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam kwa kunialika kushiriki nanyi katika mkutano huu maalum wa kutafakari afya ya jamii katika taifa letu.  Hili ni jambo muhimu hasa wakati huu taifa letu linapopitia kwenye hali isiyokuwa ya kawaida.
          Nawapongeza viongozi na wanakamati wote kwa juhudi kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha kwamba taifa letu linabakia kuwa kisiwa cha amani.  Hii si kazi ndogo hata kidogo.  Ni kazi kubwa yenye vikwazo vingi.  Inahitaji moyo wa ujasiri uvumilivu na wenye kuweka maslahi ya taifa mbele.  Unahitaji uongozi wenye kuona mbali na wenye kujali maslahi mapana ya taifa letu na watu wake.  Naamini ni kazi ambayo inampendeza Mwenyezi Mungu hivyo ina Baraka zake zote. 
Ndugu Viongozi wa Dini;
Kwenye mwaliko wenu mmenitaka nizungumzie mambo makubwa matatu; amani ya nchi, Katiba Inayopendekezwa na Mahakama ya Kadhi.  Suala la usalama na amani ya nchi yetu nimekuwa nalizungumza mara kadhaa na mara ya mwisho nililizungumzia kwa kirefu kwenye hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Februari, 2015.  Leo nitalizungumzia suala la amani kwa kulihusisha na wakati tulionao na hasa mwelekeo wa mambo yanayotokea hivi sasa nchini.  Huhitaji kuwa bingwa wa unajimu kuweza kujua kuwa hali ilivyo sasa hairidhishi na kama hatutachukua hatua thabiti kuubadili mwelekeo huu nchi yetu itaingia kwenye mfarakano mkubwa kati ya Wakristo na Waislamu.  Hatari ya kuvunjika kwa amani ni kubwa.
Kama sote tujuavyo mchakato wa kutunga Katiba Mpya unakaribia ukingoni baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa Rasimu ya Katiba na Bunge Maalumu la Katiba kutunga Katiba Inayopendekezwa.  Tunasubiri kupiga Kura ya Maoni ya kuamua juu ya hatma ya Katiba hiyo.  Upigaji kura huo utaendeshwa kwa kutumia Daftari la Wapiga Kura lililoboreshwa na siyo la zamani.  Kwa kuwa daftari linaboreshwa kwa kutumia teknolojia mpya kila mtu anapatiwa kitambulisho kipya cha mpiga kura.  Kinachoendelea sasa ni zoezi la uandikishaji wa wapiga kura na litakapokamilika ndipo Kura ya Maoni itakapofanyika. 
Kwa sasa wengi wetu tunasubiri zamu yetu ya kujiandikisha ili tupate vitambulisho vyetu vya Mpiga Kura, ili kuwa tayari kutimiza haki yetu ya Kisheria na Kikatiba ya kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa na baadae kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.  Bahati mbaya kasi ya uandikishaji haijaenda kama tulivyotangaziwa awali na Tume ya Uchaguzi.  Naamini wakati mwafaka Tume itatueleza na kutuelekeza kuhusu uandikishaji na mchakato mzima mpaka upigaji wa Kura ya Maoni. 
Waheshimiwa Viongozi wa Dini;
Katika kipindi cha kusubiri kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura, kumetokea matamko ya baadhi ya viongozi wa dini ya kuwataka waumini wajiandikishe kwa wingi ambalo ni jambo jema sana.  Lakini, pia wamewataka waipigie kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa.  Kauli hii imenisikitisha na kunihuzunisha kwa sababu sikutegemea viongozi wetu hawa tunaowaheshimu sana wangeweza kufanya hivyo na kwa namna ile waliyofanya.  Ninaposema hivyo sipendi nieleweke kuwa nahoji haki yao kama raia kutoa maoni ya kuunga mkono au kutokuunga mkono Katiba Inayopendekezwa.  Hiyo ni haki yao ya msingi kama ilivyo kwa raia ye yote.  Kinachonisumbua ni kutaka kulipa suala la Katiba Inayopendekezwa ambalo ni la raia wote, sura, mtazamo na msimamo wa kidini.  Kama ingekuwa Katiba Inayopendekezwa inakinzana na uhuru wa kuabudu hapo wangekuwa na haki ya kuikataa na mimi ningeungana nao kuipinga.
Ukweli ni kwamba Katiba Inayopendekezwa inatambua haki na uhuru wa watu kuabudu dini wanayoipenda.  Niruhusuni ninukuu Ibara ya 41 ya Katiba Inayopendekezwa ambayo ina vifungu saba lakini ninanukuu vichache (1, 2, 3, 5 na 6) inasema kwamba:     
(1)             Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.
(2)            Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi hakiuki sheria za nchi.
(3)            Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka za Serikali.
(5)   Ni marufuku kwa mtu, kikundi, au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.
(6)             Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote iakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.
Kwa kweli kulipa jambo la Katiba Inayopendekezwa sura, mtazamo na msimamo wa kidini linanipa taabu sana kuelewa.  Nasumbuliwa na ule ukweli kwamba haijakiuka misingi yoyote ya dini, labda dini ya shetani kama ipo.  Isitoshe mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya umekuwa na ushirikishwaji mkubwa na mpana wa watu katika hatua zote.  Viongozi wa dini na waumini wao walishiriki katika hatua zote za mchakato.  Haijapata kutokea mambo ya dini kupuuzwa au watu wa dini ye yote kubaguliwa.  Katiba Inayopendekezwa imezingatia, imeimarisha, kudumisha na kuendeleza misingi muhimu ya taifa letu.  Misingi hiyo ni pamoja na:
(i)                               Nchi yetu kutokuwa na ubaguzi wa aina yoyote, ubaguzi wa dini, rangi, kabila, jinsia au eneo mtu atokako.
(ii)                            Serikali yetu kutokuwa na dini ingawa wananchi wake wanaruhusiwa kuwa na dini.
(iii)                         Uhuru wa kuabudu.  Kila Mtanzania anao uhuru wa kufuata na kuabudu dini atakayo bila kubughudhiwa.  Uhuru huu umezingatiwa katika Katiba Inayopendekezwa.
(iv)                         Utoaji wa fursa sawa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wote bila upendeleo wala ubaguzi.
(v)                           Haki za msingi za makundi yote zimeainishwa.
 Ndugu Viongozi wa Dini;
Ndugu Wageni Waalikwa;
Kwa ajili hiyo sioni sababu kwa nini viongozi wa dini wawaelekeze waumini wao kuipigia Kura ya Hapana, Katiba Inayopendekezwa.  Kuna lipi la kidini au linalokwenda kinyume na haki na uhuru wa kuabudu?  Nimeisoma na kuirudia sijaliona linalokwenda kinyume na dini yo yote.  Kwa ajili hiyo nawasihi viongozi wa dini wawaache waumini wao kuamua wenyewe wanavyoona inafaa, bila ya kushinikizwa na mtu yeyote.  Katiba Inayopendekezwa ni ya taifa letu na ya Watanzania wote.  Tena walikuwa ni wawakilishi wazito, bora na makini kwa kila hali.  Lipi tena lililoharibika hadi tufikie hapa?
Nilifuatilia kwa undani nini kilichowafanya viongozi wetu wa dini kutoa matamko ya kuwataka waumini wao kuikataa Katiba Inayopendekezwa na kutokuipigia kura CCM.  Nimeona kuwa labda ni hasira kwa uamuzi wa Serikali kupeleka Bungeni Muswada unaohusu Mahakama ya Kadhi.  Pia wana hasira kuwa Katiba Inayopendekezwa imeyaacha baadhi ya mambo wanayoyaona kuwa ni muhimu.  Nitajaribu kuyazungumzia yote mawili, na namuomba Mwenyezi Mungu anijaalie kauli njema ili maelezo yangu yatosheleze kujibu hoja hizo.
Waheshimiwa Viongozi wa Dini;
Niruhusuni nianze na hili la pili la baadhi ya mambo waliyoyaona kuwa ya msingi kutokuwemo katika Katiba Inayopendekezwa.  Niseme kwa jumla tu kwamba si kila alichokitaka kila mtu kimejumuishwa au kingejumuishwa.  Isingekuwa rahisi kufanya hivyo.  Tungekuwa na Katiba ya ukubwa gani na ingeandikwaje na nani angeiandika!  Mchakato huu unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Kila taasisi au chombo kilichotakiwa kuundwa kwa mujibu wa Sheria hiyo kiliundwa na kutimiza ipasavyo wajibu wake.  Wapo waliohoji Mahakamani mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba kuhusu Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.  Walipata majibu stahiki kuwa Sheria ilizingatiwa na Bunge maalum lina mamlaka hayo.
Sioni ubaya wa mtu kuyasikitikia yale ambayo yamemkereketa sana, lakini kuyapa sura, mtazamo na msimamo wa kidini inanipa taabu.  Mambo ya dunia yanayotungwa na wanadamu hubadilika na nyakati, tofauti na maandiko matakatifu.  Linaloonekana linafaa leo kesho siyo na linaloonekana silo leo kesho litaonekana ndilo lenyewe.  Niliwahi kusema wakati mmoja kuwa kama jambo halipo sasa ipo siku litakuwepo. 
Mfano mzuri ni Orodha ya Mambo ya Muungano katika Katiba yetu ya sasa.  Yalipoingizwa yalionekana yanafaa na yanahitajika sana, leo baadhi yameonekana hayajitajiki na ni kikwazo.  Kwa mambo kama hayo kwa viongozi wa dini kuyawekea msimamo wa dini ni kwenda mbali mno.  Waachieni wanasiasa walumbane na waumini wenu waamue wanavyoona inafaa.  Mtawakwaza isivyostahiki.
Waheshimiwa Viongozi wa Dini;
Pengine niyasemee kidogo haya madai yahusuyo maadili.  Napenda kuwahakikishia kuwa maadili ya taifa pamoja na miiko ya uongozi vimezingatiwa. Katiba Inayopendekezwa imeyaainisha vizuri maadili ya viongozi tena kwa namna inayotekelezeka na kuunda mifumo na vyombo vya kusimamia. Miongoni mwa vyombo hivyo ni pamoja na Tume ya Maadili tofauti na ilivyo sasa ambapo ni Baraza la Maadili.  Katiba Inayopendekezwa inaitambua Sheria ya Maadili na TAKUKURU ambayo haikutajwa kabisa katika Rasimu ya Katiba ya Tume nayo imeingizwa.    
Kumekuwa na madai kwamba maadili ya viongozi na watendaji wa umma yameondolewa kwenye Katiba Inayopendekezwa.  Hiyo siyo kweli.  Ibara za 28 na 29 zinazungumzia maadili ya viongozi wa umma na Ibara ya 30 na 31 zinazungumzia maadili ya watendaji wa umma. Ibara ya228 inaunda Tume ya Maadili ya Umma na Ibara ya 249 inaunda Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU).  Kilichofanyika ni kuyaondoa maadili kutoka kwenye sehemu yaliyopendekezwa kuwekwa na kupelekewa sehemu nyingine ambako yanaweza kutekelezwa kwa mujibu wa sheria.  Tume iliandika maadili kama Tunu tu ambazo kimsingi hazipaswi kutekelezwa bali kuzingatiwa tu.  Bunge Maalumu la Katiba likaona liyajengee Mifumo ya Utekelezaji na vyombo vya kusimamia.
 Hivyo ndugu zangu, Katiba Inayopendekezwa ni bora kuliko Katiba ya sasa na Rasimu ya Katiba. Katiba Inayopendekezwa isipopita, tunarudi kwenye Katiba ya sasa na changamoto zake.  Ni vizuri sana ikaeleweka kuwa, chaguo ni kati ya Katiba Inayopendekezwa ambayo imeboreshwa na kukidhi mahitaji na maslahi ya makundi mbalimbali nchini au kubaki kwenye Katiba ya Sasa.   Pamoja na hayo, tutambue kwamba Katiba si Biblia au Msahafu vitabu ambavyo haviwezi kubadilishwa.  Zitakuwepo fursa mbalimbali za kuifanyia marekebisho kadri mahitaji ya wakati yatakavyojitokeza..  Tumekuwa tukifanya hivyo siku zote, sioni sababu ya watu kuhamanika na kuwa na mashaka safari hii.  Kile ambacho hakikupatikana leo kinaweza kupatikana kesho.
Mahakama ya Kadhi
Ndugu Viongozi wa Dini;
Ndugu Wageni Waalikwa;
Kuhusu Mahakama ya Kadhi, ni vizuri tukaelewa kwamba Serikali ilishafanya maamuzi kwamba Mahakama hiyo haitaanzishwa na Serikali bali na Waislamu wenyewe wakiona inafaa. Tulielewana pia kwamba Serikali haitaingia gharama za kuiendesha. Hayo yote yamezingatiwa na Mahakama hizo zimekwishaanzishwa na BAKWATA, Makadhi wamekwishateuliwa na zinaendeshwa na Waislamu wenyewe.   
Tunachotaka kufanya sasa Bungeni ni kuwezesha maamuzi yanayofanywa na Kadhi yatambuliwe kisheria.  Kwa mujibu wa Sheria zetu hilo siyo jambo geni na wala halikinzani na Katiba wala Sheria za nchi. Sheria zetu zinatambua Sheria tulizozirithi kutoka kwa Wakoloni, Sheria zilizotungwa na Bunge, Sheria za Kimila pamoja na Sheria za Kiislamu.  Hii ni kwa mujibu wa Sheria iitwayo Judicature and Application of Laws Act, 1961 (JALA) hususan kifungu cha 11(c)(ii) kinachoelekeza kwamba: Nothing in this Section shall prelude any Court from applying the rules of Islamic Law in matters of marriage, divorce, guardianship, inheritance, wakf and similar matters in relations to members of a Community which follows that law”.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Kabla ya Uhuru na mara tu baada ya uhuru, Sheria za Kiislamu zilisimamiwa na Mahakama zilizoundwa chini ya Sheria ya Mahakama za Wenyeji - Native Courts Ordinance  na baadaye Local Courts Ordiance.  Mahakama za Maliwali zilizoundwa katika maeneo ya wenyeji Waislamu zilisimamia Sheria za Kiislamu.
Kufuatia kuunganishwa kwa mifumo yetu ya Mahakama za wenyeji na Mahakama za wazungu na kuwa mfumo mmoja, mwaka 1963, kazi ya kusimamia sheria hizi ilikuwa chini ya Mahakama za Mwanzo.  
Mwaka 1964 ilitungwa Sheria iitwayo “The Islamic Law Restatement Act (Sura ya 378) ambayo ilimpa Waziri wa Sheria majukumu ya kutambua na kutangaza matamko mbalimbali ya sheria za kiislamu kwa mujibu wa madhehebu tofauti ya Kiislamu.  Sheria zote mbili (JALA) na Islamic Law Restatement Act, zilipiga marufuku matumizi ya Sheria za jinai za Kiislamu na Kimila. 
Mwaka 1971 kufuatia Tume ya Jaji Spry iliyoundwa mwaka 1968, ilitungwa Sheria mpya ya ndoa.  Sheria hii ya ndoa inatambua mifumo ya sheria na taratibu za kufunga ndoa zinazotumika na dini mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Wakristo na Waislamu.  Ndoa za Kikristo zinasajiliwa  na Wakristo wenyewe Makanisani na kwa Waislamu, Makadhi wanatakiwa kuhudhuria, kufungisha na kusajili ndoa za Kiislamu.  Hii ni kwa mujibu wa fungu la 43 la Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Sura ya 29 ya Sheria zetu ambayo inasema:
(2)  When a marriage is celebrated by a minister of religion according to the rites of a specified religion, it shall be his duty forthwith to register it.
(3)  When a marriage is contracted in Islamic form in the presence of a Kadhi, it shall be his duty forthwith to register it.
(4)  When a marriage is contracted in the presence of a registration officer in Islamic form (no kadhi being present) or according to customary law rites, it shall be the duty of the registration officer to take necessary steps to register the marriage with the district registrar or a kadhi.
Taratibu za kuvunja ndoa kwa mujibu wa fungu la 101 la Sheria hiyo, linawataka wahusika kwanza kupata suluhu ya Mabaraza ya Ndoa, ikiwa ni pamoja na yale ya Makanisa na ya Misikiti.  Kama mabaraza haya yakishindwa ndipo mtu anaweza kuomba talaka. Ingawa utaratibu huu umewekwa kwenye Sheria ya Ndoa, talaka ni utaratibu unaotumbulika na Waislamu, Wakristo hawana.  Kwao ndoa inayofungwa Kanisani haivunjiki.  Hivyo, usuluhishi wa Kiislamu ni tofauti sana na wa Kikristo.
Hivyo basi, kinachotafutwa kwenye muswada uliopo Bungeni siyo kitu kigeni, kipo kwenye Sheria ya JALA, Islamic Law Restatement Act na Sheria ya Ndoa.  Kwa kweli kinachotafutwa ni kidogo tu, kama Kadhi anafungisha ndoa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, kwa kutumia Sheria ya Kiislamu, inayotambulika kwa mujibu wa Sheria ya Islamic Law Restatement Act na JALA, basi mamlaka itambue maamuzi yake hayo na katika masuala ya mirathi na wakfu.  Ilivyo sasa, ni vigumu kwa Waislamu waliopitia kwenye Mahakama ya Kadhi, kupata haki zao kutoka kwenye Mamlaka mbalimbali za nchi kwa sababu maamuzi ya Mahakama hizo hayana nguvu ya kisheria.  Jamani ndugu zangu hili nalo lina ubaya gani mpaka tufike mahali pa kutaka kupata uhasama na kuhatarisha amani, usalama na utulivu wa nchi zetu? 
Sioni sababu ya kupandikiza chuki baina ya Wakristo na Serikali yao, au baina ya Wakristo na Chama cha Mapinduzi chenye hiyo Serikali.  Sioni sababu ya kuleta mfarakano baina ya Wakristo na Waislamu.  Haipo kabisa kwani sheria zetu zinatambua na kujali haki za msingi za dini zote.  Zipo Sheria zinazotambua mambo ya Wakristo kuhusu ndoa (Sheria ya Ndoa ya 1971 Sura 29), urithi Cap 345 ya 2002, Sheria ya Viapo na Matamko na kadhalika. 
Zipo sheria zinazowahusu Waislamu, sura 28 ya 2002 inayozungumzia mirathi ya muumini asiyekuwa mkristo au mwenye asili ya Kiasia (Non Christian – Non Asiatic Act, the Islamic Law (Restatement) Act.  Na Wahindu nao wanasheria yao kuhusu mirathi na kuendeleza mali za marehemu (Hindu Law Succession Act of 1870.
 Kila dini mambo yake yanatambuliwa kisheria tena kwa mujibu wa taratibu za dini hizo zinavyotaka iwe. Na, yote yanahusu ndoa, talaka, mirathi na wakfu.  Katu hairuhusu masuala ya jinai.  Na, Mahakama ya Kadhi inahusu mambo hayo.  Kama inavyofanywa kwa dini zote nyingine kama Waislamu wameamua Kadhi ndiyo wasimamie shughuli hizo iweje tuwakatalie?  Tutazua chuki isiyo kuwa na sababu.
Mwisho
Ndugu zangu, tunapoelekea kwenye uchaguzi kuna mambo mengi yatakayofanywa na mengi yanayosemwa.  Mengine kwa nia njema, na mengine kwa hila za kujitafutia ushindi katika chaguzi, na mengine kwa hila ya kuitakia nchi yetu mabaya. 
Tusikubali kuruhusu watu wenye nia mbaya na nchi yetu kutugawa kwa misingi ya dini zetu.  Daima tukumbuke kuwa yale yanayotuunganisha ni muhimu zaidi kuliko yale yanayotugawa.  Viongozi wa dini hamna budi kutambua kwamba nafasi na mamlaka yenu katika kujenga au kubomoa umoja na mshikamano wa kitaifa ni mkubwa.  Huko nyuma nilikwisha watahadharisha juu ya watu wenye dhamira ya kutaka kutufarakanisha kwa misingi ya dini.  Wako watu wanaojiuliza kwa nini Tanzania ni tulivu kwa nia ya kutafuta mbinu za kuwagawa na hata kuwasambaratisha kama ilivyo kwa baadhi ya nchi za Afrika. Kwa historia yetu si rahisi kutumia kabila, rangi na mengineyo. Wameamua kutumia imani zao za kidini.  Ninyi ndio viongozi wetu naomba muwe wepesi kutambua hila hizo na kuzizuia. Narudia kuwatahadharisha muwe macho na watu hao.  Hatutegemei viongozi wa dini wakatufikisha huko.
Kama viongozi wa kitaifa, tunao wajibu wa kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa.  Na si vinginevyo. 
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza!

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari atimuliwa

SAMUEL Sitta-Waziri wa Uchukuzi, amemng’oa rasmi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (PTA), Madeni Kipande, ambapo sasa anarejeshwa idara kuu ya utumishi ili kupangiwa majukumu mengine.

Kipande ambaye alisimamishwa kazi 16 Februari, 2015, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali dhidi yake, sasa nafasi yake itaendelea kukaimiwa na Awadhi Massawe.

Wakati akimsimamisha Kipande, Sitta alisema ni kutokana na kukiuka taratibu za manunuzi na zabuni na kuwa na mahusiano mabovu na wadau wa mamlaka hiyo na hivyo kuunda tume ya uchunguzi ambapo taarifa yake imetolewa leo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Sitta amesema tume ilikamilisha kazi yake 20 Machi, 2015 na kumkabidhi taarifa ya uchunguzi wao 24 Machi 2015 kwa hatua zaidi.

“Baada ya kuisoma taarifa ya tume na hatimaye kushauriana na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala haya, tumeridhika pasipo mashaka yoyote kwamba isingefaa Kipande kuendelea na kazi ya kuongoza PTA. 
“Hii ni kutokana na kudhihirika utawala mbovu aliouendesha uliosababisha manung’uniko mengi miongoni mwa wateja na wadau wa bandari na mgawanyiko mkubwa na wafanyakazi,”amesema Sitta.

Aidha, Sitta alitumia muda huo kutoa ufafanuzi wa uchunguzi kuhusu ununuzi wa mabehewa mabovu katika kampuni ya Reli Tanzania (TRL), akisema ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa TRL kuipitia taarifa hiyo ya tume na kutoa maelezo.

“Kwa ujumla imebainika kwamba; mabehewa mengi kati ya yaliyoagizwa yana kasoro, kulikuwa na uzembe katika uagizaji na ufuatiliaji kiwandani yalipokuwa yanatengenezwa na kulikuwa na uzembe katika kuendelea kuyapokea pamoja na ubovu wake kujulikana,”amesema.

Sitta ameongeza “siku ya Jumatatu tarehe 13 Aprili, 2015, wizara imeshtushwa kugundua kinyume na taarifa za awali na kinyume na masharti ya mkataba wa ununuzi wa mabehewa hayo mabovu yamefanyika kikamilifu.”

Amesema kuwa watengenezaji wamelipwa asilimia 100 ya fedha kinyume na masharti ya mkataba na kwamba wizara inaona kuwa utekelezaji wa mkataba huu yana dalili za hujuma kwa TRL na kwa nchi wala sio uzembe.

Kufuatia hali hiyo, Sitta ameagiza uchunguzi wa kubaini uwezekano wa hujuma ufanyike na kwamba madhumuni hayo amemwelekeza Katibu Mkuu wa wizara yake asimamie kuundwa kwa kamati ya uchunguzi.

Amesema kuwa kamati hiyo itaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akishirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Sitta ameipa kamati hiyo wiki tatu kuanzia 20 Aprili, 2015, kukamilisha uchunguzi huo, na katika kipindi hicho viongozi wakuu wa TRL wanawajibika na mkondo wa kashfa hiyo wote wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi.

Sitta amewataja viongozi hao kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu, mhandisi mkuu wa mitambo, Ngosomwile Ngosomiles, mhasibu mkuu, Mbaraka Mchopa, mkaguzi mkuu wa ndani, Jasper Kisiraga na meneja mkuu wa manunuzi, Ferdinand Soka.

  • Taarifa ya Sarafina Lidwino via MwanaHALIASI Online

Sitta awasimamisha kazi wakuu 5 wa TRL

Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akionyesha baadhi ya Ripoti za uchunguzi za mamlaka ya Bandari,TPA na Ripoti ya shirika la Reli jijini Dar es Salaam leo.

Wizara ya Uchukuzi nchini Tanzania imewasimamisha kazi viongozi wakuu watano wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL, kuhusiana na kuingizwa na kulipwa kwa manunuzi ya mabehewa mabovu, ili kupisha uchunguzi.

Akitangaza kuwasimamisha viongozi hao leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Samuel Sitta amesema Wizara itaunda kamati itakayoongozwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG, akishirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Sitta amesema Januari 5 mwaka huu Serikali ilifanya uchunguzi wa tuhuma zinazohusiana na mabehewa hayo mabovu chini ya aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe.

Vilevile alieleza Aprili 13 mwaka huu wizara ilishitushwa baada ya kugundua taarifa kinyume na za awali kuhusu masharti ya mkataba wa ununuzi wa mabehewa hayo kwamba malipo yangefanyika kwa awamu wakati mabehewa hayo mabovu yalilipwa kwa awamu moja, yaani watengenezaji walilipwa asilimia 100 ya fedha kinyume na masharti ya mkataba.

Alisema ametoa ametoa muda wa majuma matatu ya uchunguzi kuanzia Aprili 20 mwaka huu kwa zoezi hilo kuwa limekamilika.

Viongozi wakuu wa kampuni ya reli ambao watawajibika kwa kusimamishwa kwanza ili kupisha uchunguzi ni pamoja na:-

  1. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli, Kipalo Kisamfu; 
  2. Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles; 
  3. Mhasibu Mkuu wa Kampuni, Mbaraka Mchopa; 
  4. Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiraga 
  5. Meneja Mkuu wa Manunuzi, Fedinarnd Soka.

Alisisitiza kuwa wakati viongozi hao wakiwa wamesimamishwa ameiagiza bodi ya wakurugenzi ikae kikao cha dharura kesho kwa ajili ya uteuzi wa watumishi wenye sifa ili kukaimu nafasi hizo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.


  • Taarifa via EATv, Michuzi blog na GlobalPublishersWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ateta na Balozi wa Uingereza

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose wakati balozi huyo alipomtembelea Mheshimiwa Lukuvi ofisini kwake kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uendelezaji wa sekta ya ardhi nchini Tanzania.
-- Nanyaro, Clarence - Wizara ya Ardhi.

How strong US Dollar rattles world economies & markets
WASHINGTON (AP) -- The U.S. dollar hasn't been on a roll like this since Ronald Reagan sat in the White House and "Raiders of the Lost Ark" ruled the box office.

Since June 30, the greenback is up 28 percent against the euro, 18 percent against the Japanese yen and 40 percent against the Brazilian real. Not since 1981 has the dollar been so strong.

Some U.S. companies and investors wish it would take a breather. Delta Air Lines said Wednesday that the strong dollar is hurting ticket sales in some foreign markets and announced plans to pull back international service, primarily in Japan, Brazil, India, Africa and the Middle East. Johnson & Johnson on Tuesday blamed the dollar, in part, for dragging its first-quarter earnings down nearly 9 percent.

Meanwhile, the International Monetary Fund downgraded the outlook for U.S. economic growth this year and next, citing the strong dollar's damage to American exports.

The dollar is rising largely because the U.S. economy is outperforming most other developed economies and because U.S. interest rates are higher than those in Europe and Japan.

The run-up is having a big impact around the world. In the United States, it is pinching corporate profits, weighing on economic growth and delivering bargains for American tourists. In Europe and Japan, it's providing relief for economies that have been ailing for years. And in the emerging markets of Asia and Latin America, it is threatening financial stability.

Here's a look at the dollar's far-flung impact on:

CORPORATE PROFITS

The rising dollar hurts U.S. companies that do business abroad in two ways: It makes their products more expensive - and therefore less competitive - in foreign markets. And it means that the revenue U.S. companies collect in euros or yen is worth fewer dollars when they bring the money home.

J&J, for instance, said unfavorable exchange rates reduced the value of overseas sales by 13 percent in the first quarter.

Overall, the outlook for first-quarter corporate earnings has steadily deteriorated as the dollar climbed. At the end of last year, analysts were expecting Standard & Poor's 500 companies to register a 4 percent increase in earnings for the January-March period. By March 31, they were bracing for a 5 percent drop, according to FactSet and PNC Financial Services Group.

Earnings are expected to drop 12 percent for companies that get more than half their revenue outside the United States; the rest are expected to register flat earnings.

ECONOMIC GROWTH

Weighed down by a strong dollar, U.S. exports fell 3 percent last year and were down another 1 percent the first two months of this year compared to January-February 2014. A drop in exports reduces U.S. economic growth.

Citing the dollar's impact, the IMF on Tuesday downgraded the outlook for the U.S. economy. The IMF now expects economic growth of 3.1 percent both this year and next. That's solid - and an improvement on 2014's 2.4 percent expansion - but it's down from the IMF's January forecast of 3.6 percent growth in 2015 and 3.3 percent growth in 2016.

Meanwhile, Japan and Europe are poised to benefit from the dollar's might.

The IMF predicts the Japanese economy will grow 1 percent this year versus an earlier forecast of 0.6 percent. It also upgraded the forecast for the 19 countries that use the euro currency to 1.5 percent growth this year (up from a January forecast of 1.2 percent).

FINANCIAL STABILITY

In the emerging market countries of Asia and Latin America, the stronger dollar cuts two ways. Yes, it gives exporters a lift, but it also poses a threat to financial stability.

Enticed by low interest rates, emerging market countries borrowed heavily in U.S. dollars over the past decade. From 2005 to 2015, dollar-denominated debt - mostly corporate bonds and loans - shot up from $262 billion to $837 billion in the emerging markets of Asia and from $586 billion to $963 billion in Latin America, according to the Institute of International Finance.

As the dollar rises, it takes more local currency to generate enough dollars to meet loan payments. Emerging market corporate borrowers could get squeezed. The pain could spread if those companies suddenly withdrew deposits from local banks to meet their U.S. dollar payments, or if the investors who own the emerging market bonds get rattled and sell them in a panic.

In a report Wednesday, the IMF warned that "financial risks have increased in many emerging markets" and said a stronger dollar and weaker local currencies create "balance sheet strains for indebted emerging market firms" and for governments.

Things could get worse if the Fed this year decides to raise short-term U.S. rates, which have near zero since late 2008. That would draw more investors to the United States and drive the up the dollar even more. The IMF report warned that a Fed rate hike could cause "a bumpy ride" in financial markets.

TOURISM

The strong dollar makes European vacations cheaper for American tourists. Booking.com estimates that the average price for a four-star hotel room in Paris, Rome, Barcelona, Amsterdam and Berlin is down 21 percent from March 2014 because of the dollar's rise against the euro. The company calculates that an American could spend 14 days in Barcelona for the price of seven days in Palm Springs, California.

Lyssandros Tsilidis, president of the Hellenic Association of Travel and Tourist Agents, said Greece has seen a 15 percent to 20 percent increase in reservations from the U.S. - Europe's biggest long-haul market - compared to the same time last year. Spain saw a 12 percent increase in January and almost 19 percent in February.

---

AP Business Writers Stan Choe and Steve Rothwell in New York contributed to this report.

Follow Paul Wiseman on Twitter at https://twitter.com/PaulWisemanAP


IGP na Mashehe wa Dar es Salaam wazungumza

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiongozana na viongozi wa dini ya kiislamu (kulia) Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania katika Mafunzo hayo Sheikh Abubakar Zuber na kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwinyibaraka Sheikh Issa Othman wakati akilelekea kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini ya Kiislamu ili kuimarisha usalama nchini.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na viongozi wa dini ya kiislamu waliohudhuria katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa dini hiyo. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana..(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)

Semina ya Ukulima na Ufugaji


Farmchem Ltd kupitia vitengo vyake vya MOTISHA LIVE and AQUA – AGRI LIVESTOCK inaanda semina ya Kilimo na Ufugaji Bora siku ya APRIL 18, 2015 kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni, PICNIC VILLA, UBUNGO, ng’ambo ya kituo kipya cha Simu 2000. Kiingilio ni 25,000/= tu

Semina hii itatoa zana kwa wadau na wajisiriamali ili wajikomboe kiuchumi kwa kuwapatia elimu na ufahamu juu ya kilimo na ufugaji bora na wa kisasa.

Semina itaongozwa na wataalamu wa sekta za kilimo na ufugaji ambao watatambua, kutatua na kufungua mijadiliano kati yao na wadau wote kuhusu yafuatayo:

- Mfuko wa Pembejeo wa Taifa Maelekezo na jinsi ya kupata mikopo rahisi ya kilimo bora na cha kisasa

 - Dr. Kisui Ujasiriamali na jinsi ya kujikomboa kiuchumi

- Bw. Alex (Motisha Live) Kilimo bora cha umwagiliaji “Green house”

- Dr. Adam (Motisha Live) Haiba “Positive Thinking”

- Dr. Archie (Aqua-Agri Livestock) Ufugaji wa kisasa wa kibiashara – Sungura na Kware

 - Dr. Cristowelu (Aqua-Agri Livestock) Ufugaji bora wa samaki Uchimbaji wa mabwawa Kilimo cha kisasa cha Matikiti Maji
 
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Dr. Archi Lundo kupitia +255 71 6303 065 na Dr. Cristowelu Zephania kupitia +255 71 2368 550. Kwa ajili ya vipeperushi tafadhali nenda Whatsapp na Instagram MWISHO

Tanzia! Che Mundugwao

Che Mundugwao
Che Mundugwao

Che Mundugwao, msanii wa nyimbo za asili ambaye alikuwa anashikiliwa katika gereza la Segerea kwa kukosa dhamana ya kesi yake, ameaga dunia.

Kabla ya kufikwa na mauti, Che Mundugwao aliugua na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda mrefu. Alikamatwa na kufikishwa kizimbani mwaka jana kwa tuhuma za wizi wa pasipoti 26.

Taarifa zinasema kuwa amefariki leo asubuhi.

A terrorist with laptop may hack a plane via passenger Wi-Fi


WASHINGTON (AP) -- The same Internet access now available on most commercial flights makes it possible for hackers to bring down a plane, a government watchdog warned Tuesday.

The finding by the Government Accountability Office presents chilling new scenarios for passengers. The report doesn't suggest it would be easy to do, or very likely. But it points out that as airlines and the Federal Aviation Administration attempt to modernize planes and flight tracking with Internet-based technology, attackers have a new vulnerability they could exploit.

A worst-case scenario is that a terrorist with a laptop would sit among the passengers and take control of the airplane using its passenger Wi-Fi, said Rep. Peter DeFazio, an Oregon Democrat on the House Transportation and Infrastructure Committee who requested the investigation.

"That's a serious vulnerability, and FAA should work quickly" to fix the problem, DeFazio said.

The avionics in a cockpit operate as a self-contained unit and aren't connected to the same system used by passengers to watch movies or work on their laptops. But as airlines update their systems with Internet-based networks, it's not uncommon for Wi-Fi systems to share routers or internal wiring.

According to the report, FAA and cybersecurity experts told investigators that airlines are relying on "firewalls" to create barriers. But because firewalls are software, they could be hacked.

"According to cybersecurity experts we interviewed, Internet connectivity in the cabin should be considered a direct link between the aircraft and the outside world, which includes potential malicious actors," the report states.

The GAO released a separate report last March that determined the FAA's system for guiding planes and other aircraft also was at "increased and unnecessary risk" of being hacked.

One area of weakness is the ability to prevent and detect unauthorized access to the vast network of computer and communications systems the FAA uses to process and track flights around the world, the report said. The FAA relies on more than 100 of these air traffic systems to direct planes.

--

Online: Government Accountability Office report: http://www.gao.gov/products/GAO-15-370

Yericko Nyerere: Agalizo kwa wanaonuia uongozi wa kisiasa


Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima wa maisha ya jamii hiyo. Siasa sio ile ya "mchezo mchafu" kama umma ulivyo aminishwa.

Mwezi wa kumi mwaka huu tunaingia kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais,

Kwa sasa Tanzania ina wanasiasa wachache sana hawazidi wanne ama kumi, wengi wao ni wajasiliasiasa. Kwao siasa ni uwaniaji wa madaraka nakisha kuingia madarakani kuchuma/kuiba mali za umma tu.

Nitoe rai kuwa sasa ufike wakati wakutumia siasa za kisasa, siasa zinazokaa kwenye maandishi na sio za kuamini maalbino ndugu zetu.

Kwa mda uliosalia unatosha kuwa na mipango/mpango thabiti wa ushindi kisiasa ulioandaliwa na wataalumu kitaalamu, tunao wasomi wazuri waliobobea kwa kazi ya mipango mikakati ya kisiasa, hebu watumieni muone matunda yao, wamesoma kwaajili hiyo, nawengine serikali imewasomesha kwaajili hiyo lakini hawatumiki, wanasiasa mnakwenda kwa mazoea wakati wataalamu wapo??

Kuna faida nyingi kutumia wataalamu wa siasa,

1. Unapata kujitathimini nguvu yako kisiasa, kutambua aina ya ushindi utakaopata,

2. Kupunguza gharama za kampeni kwakupunguza masuala yasiyo na msingi, kujua gharama halisi za kampeni zako mpaka siku unaapishwa,

3. Kupunguza vifo vya maalbino (kama wapo watumiao).

4. Kujengwa kitaalamu namna ya kutoa hotuba thabiti za kampeni, kuwa na sera na agenda za kitaalam zihusuzo mahitaji ya umma wa eneo unalowania kugombea.

5. Kukabiliana na wapinzani wako ndani ya chama bila kuathiri taasisi (chama), kujua nguvu ya mpinzani wako rasmi (wa chama kingine) na udhaifu wake.

6. Kuiandaa mioyo yenu (nafsi) kushinda ama kushindwa. Hili linapunguza msongo wa mawazo na kifo baada ya uchaguzi hasa kama utashindwa.

Achaneni kuishi kwa mazoea, tumieni wataalamu waliopo kila pembe ya nchi.