Ghala la diwani wa CHADEMA lakutwa na tani 42 za dawa bandia, zilizobadilishwa muda; Mmiliki awatoroka Wanausalama


TFDA imekamata ghala bubu la dawa zisizofaa kwa binadamu zaidi ya tani 42 lililoko Mwanza, mali ya diwani wa kata ya Turwa mkani Mara kwa tiketi ya CHADEMA, Ndesi Mbusiro ambaye pia ni mmiliki wa duka la dawa baridi, Mbusiro Pharmacy.

Ukaguzi uliofanywa katika ghala hilo umegundua kuwa dawa hizo zilikuwa ama bandia au zilishakwisha muda wake wa matumizi kwa binadamu lakini zilibadilishwa tarehe na kuongezwa muda mpya.

Njia 3 muhimu katika ujenzi wa uchumi wa gesi Tanzania

UJENZI WA UCHUMI WA GESI TANZANIA: NJIA TATU MUHIMU


Na Dk. A. Massawe

YA KWANZA

Mojawapo ya njia zitakazofanikisha matumizi ya gesi yetu asilia hapa chini yawe yenye tija zaidi ni ile ya kuisambaza maeneo yote nchini kwa kuanzia na miji mikuu ya kanda au mikoa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani na kuzalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya pale pale unapozalishwa.

Kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam itakakotumika kuzalishia umeme, majumbani na viwandani ni sahihi tu kama umeme wote utakaozalishwa utatumika ndani ya ukanda wa Dar es Salaam.

Yaani, ni sehemu kidogo tu ya gesi asilia inayowasili Dar es Salaam ingebaki hapo hapo kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi ya majumbani na viwandani ndani ya ukanda wa Dar es Salaam na kitakachosalia kiendelee na safari yake hadi kanda nyingine za Tanzania kuzalisha umeme na kwa ajili ya matumizi mengine ya moja kwa moja majumbani na viwandani kuendana na mahitaji ya kila kanda.

Lengo ni kuondokana upotevu mkubwa wa umeme na gharama kubwa ya kuusafirisha umbali mkubwa kutoka kanda moja ya Tanzania hadi nyingine, pia ikizingatiwa kwamba, zaidi ya umeme, kila kanda hapa Tanzania pia inahitaji gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja majumbani na viwandani kama Dar es Salaam.

Na, ni kosa kuzalisha umeme wa megawati 3000 hapa Dar es Salaam kutokana na gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya matumizi ya ukanda wa Dar es Salaam na kanda nyingine zilizoko mbali na Dar es Salaam kwani njia sahihi ni kusambaza uzalishaji wa umeme utokanao na gesi asilia kote nchini kwa kusambaza gesi asilia kote nchini kwa njia ya mabomba na kufunga mitambo midogo midogo ya uzalishaji wa umeme wa gesi asilia kwenye kila kanda kuendana na mahitaji halisi ya kanda.

Hivyo, cha muhimu zaidi kwenye kufanikisha matumizi ya gesi asilia hapa nchini yawe yenye tija tosha ni kujenga miundo mbinu ya mabomba kwa ajili ya usambazaji gesi asilia kikanda kote nchini itakakozalisha umeme na kutumika moja kwa moja majumbani na viwandani kikanda kuendana na mahitaji halisi kikanda ili kukwepa upotevu mkubwa wa umeme na gharama kubwa za kuusafirisha umbali mkubwa kutoka kanda hadi kanda, huku ikizingatiwa kwamba, zaidi ya umeme, kanda zote pia zinahitaji gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja majumbani na viwandani kama Dar es Salaam.

Hicho ndicho kilichozingatiwa kwenye uamuzi sahihi wa kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam itakakotumika kuzalishia umeme, majumbani na viwandani badala kuzalisha umeme huo wa gesi asilia Mtwara kwa ajili ya kuusafirisha kwa nyaya hadi Dar es Salaam.

Ni hicho hicho cha kuzingatia kwenye kuchagua njia itakayofanikisha matumizi yenye tija tosha ya gesi asilia majumbani na viwandani, na kama kianzio cha nishati ya umeme kwenye kanda zote za nchi.

Ujenzi wa nyanya za kusafirisha umeme wa gesi asilia umbali mrefu kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam au kutoka kanda hadi kanda ni lazima uambatane na ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam au kutoka kanda hadi kanda itakakotumika majumbani na viwandani, yaani gharama ya ziada inayombatana na ujenzi wa njia ya umeme (nyaya), usafirishaji wa umeme na upotevu wa umeme njiani unaposafirishwa umbali mkubwa.

YA PILI

Njia ya pili itakayofanikisha matumizi yenye tija ya raslimali ya gesi asilia iliyogundulika hapa nchini ni kutumia hisa za Serikali kwenye raslimali hiyo iliyoko ardhini ikisubiria kuanza kuvunwa kama rehani kuchukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuzalishia umeme wa maji huko Stigler’s na wa makaa ya mawe huko Mchuchuma na kwingineko. Ni matumizi yanayowezesha kurudisha mikopo na kuleta faida hata kabla uchimbaji wa gesi asilia iliyotumiwa kama rehani haujaenda mbali sana, huku ikizingatiwa kwamba maelfu ya megwati za umeme wa maji ambazo hazijavunwa huko Stiglers na kwingineko hapa nchi huwa zikipotea kila saa miaka nenda rudi wakati gesi asilia na makaa ya mawe yanaweza kusubiri ardhini hadi uvunwaji wake kwa ajili ya uzalishaji wa umeme utakapoanza.

YA TATU

Njia ya tatu itakayofanikisha matumizi yenye tija tosha ya raslimali ya gesi asilia iliyogundulika hapa nchini ni kuwekeza mapato ya serikali yatokanayo na uvunwaji wa ralimali yake ya gesi asilia kwenye mfuko endelevu ‘’Sovereignity Fund’’wa kutolea mikopo yenye riba nafuu kwa sekta za umma (kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi na uendelezaji wa miundo mbinu ya kitaifa na kwenye makampuni ya kimataifa yaliyo mihimili mikuu ya maendeleo ya uchumi wa dunia kisayansi na kiteknolojia (kuiwezesha Tanzania kuwa sehemu ya wahimili wakuu wa uchumi wa dunia kisayansi na kitknolojia na kuwa mmojawapo ya wanaonufaika sana), na kwa sekta binafsi (kuwezesha ukuwaji wa ujasiriamali hapa nchini).

Ni kuzingatia kwamba raslimali ya gesi asilia hapa nchini ni urithi usio endelevu wa vizazi vyote vya Tanzania, na njia ya kuhakikisha matumizi yake ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa vizazi vyote vya Tanzania ni kutumia mapato ya serikali yatokanayo na uvunwaji wake kama kianzio endelevu cha mikopo yenye riba nafuu kwa sekta binafsi na za umma kote nchini.

Mwalimu Dar amweka kimada mwanafunzi wa STD VI


Mwalimu mmoja jijini Dar es Salaam anahojiwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumtorosha na kumgeuza kimada mwanafunzi wa darasa la sita kwa takribani mwaka mmoja, na kumkatiza masomo yake.
Vyuo Vikuu 9 vya Kiislam Afrika na Malaysia kukutana Zanzibar kuibua mbinu ya kuelimisha taathira za TEHAMA

Wataalamu 40 kutoka vyuo vikuu tisa vya Kiislamu vya Nchi za Afrika Mashariki na Malasyia watakutana Zanzibar kujadili maendeleo ya mitaala pamoja na kuangalia njia bora za kuwaepusha wanafunzi kutojihusiaha na matumizi mabaya ya mitandao ya jamii inayochangia kuwaingiza katika ugaidi na uhalifu.

Akizungumza mjini hapa, jana, Profesa Abdulrahaman Hikmany wa Chuo Kikuu cha Al Sumait cha Zanzibar, alisema mkutano huo wa kimataifa utaanza April 18 hadi 19, mwaka huu.

Profesa Hikmany alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua maendeleo ya mitaala ya elimu kwa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki na Kusini wa Afrika.

Alisema utandawazi kwa njia moja au nyingine una faida na hasara, na kutoa mfano kuwa binadamu hawezi kukatazwa asitumie kisu ila jambo la msingi kumpa njia kukitumia kwa tahadhari.

"Kusudio la mkutano huo ni kuibua mbinu mpya endelevu katika mitaala na kuelemisha vijana kuhusu madhara na taathira za utandawazi na mawasiliano, simu na mitandao katika matumizi ya kompyuta, tunachotaka wafahamu tija na kama zake hakuna chema kisicho na athari. Ndiyo maana kuna wanaotumia dawa za kulevya licha ya hatari ya jambo hilo," alisema.

Aidha alitaja teknolojia za mawasiliano kuwa zimerahisisha kazi za utafiti kufanyika muda mfupi na kwamba, eneo hilo limeathiri baadhi ya vijana kuitumia vibaya mitandao kinyume na mahitaji na kutumbukia katika matatizo ya uhalifu.

Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Fikra ya Kiislamu yenye makao yake nchini Malaysia. Vyuo vikuu vingine vitakavyoshiriki ni Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro, Chuo Kikuu cha Umma (Kenya), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Abdulrahaman Al Smait (Zanzibar), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Uganda, Chuo Kikuu cha Mussa Bin Bique (Msumbiji), Chuo Kikuu cha Kiislamu (Sudan Kusini), Chuo Kikuu cha Kiislamu (Malaysia) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) ambacho kitashiriki mkutano huo kama mtazamaji na mwalikwa.

 • Antar Sangali, Zanzibar via gazeti la UHURU 

Ufafanuzi kuhusu habari: 'Zitto amchongea Mengi kwa JK?'


Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari yenye kichwa cha maneno 'Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa Mwanahalisi online.

Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.

Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa mwanahalisi online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.

Habari hiyo ni ya kutunga yenye fitna zenye lengo la kuchonganisha watu. Naomba kufafanua ifuatavyo

 1. Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu ufisadi wa tshs 306 bilioni za Escrow hauhusiki na Bwana Reginald Mengi kwa namna yeyote ile. Mengi sio mbunge, sio mjumbe wa PAC na hakushawishi PAC kwa namna yeyote ile. Wezi wa Escrow wasitapetape kutafuta mchawi wakati mchawi ni wizi wao wenyewe. Porojo za kwamba Mengi alihonga wabunge ili kuishughulikia Serikali zinabaki porojo tu. Ila kama kuna mtu ana chembe ya ushahidi wa jambo hilo apeleke kwenye vyombo vya dola kwa hatua kuliko kurudia rudia porojo hizo kwenye vyombo vya habari. 

 2. Sihitaji kutumia watu ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwani ninaweza kukutana naye kwa taratibu za kawaida kabisa za kiserikali. Hadithi ya kwamba nimeomba watu wanikutanishe na Rais inaonyesha namna mwandishi alivyoshindwa kutunga uongo wake. Katika kukutana kwangu na Rais kikazi sijawahi hata mara moja kuzungumzia watu. Hivyo kusema nilikwenda Ikulu kumzungumzia Bwana Mengi ni kunidharau na kuidhalilisha Taasisi ya Urais. 

 3. Nimemwelekeza mwanasheria wangu achukue hatua za kisheria dhidi ya Gazeti la Taifa Imara na vilevile Gazeti la Mawio kwa mfululizo wa habari za kutunga uongo dhidi yangu kila kukicha. Nimeagiza tupeleke mashtaka kwenda Baraza la Habari Tanzania ili magazeti hayo yathibitishe habari zao. 

Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo

Kaaya atangaza kuwania ubunge Arumeru

JOTO la ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki limezidi kupanda baada ya kada wa CCM wilayani humo, Elirehema Kaaya, kutangaza kuwania kiti cha ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu.

Kaaya ambaye aliwahi kugombea nafasi hiyo mwaka 2005 na 2010, alisema juzi, kuwa hajakata tamaa kwa kuwa anaamini amejipanga kikamilifu.

Mtangaza nia huyo ambaye kwa sasa ni Ofisa Uhusiano wa Jiji la Mwanza, alisema kilichomsukuma kuwania ubunge ni pamoja na kusukumwa na dhamira ya kutatua kero mbalimbali za wakazi wa jimbo hilo, hususan migogoro ya ardhi.

Kaaya alisema jimbo hilo ni miongoni mwa majimbo yenye utajiri mkubwa ikiwa ni pamoja na vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA), lakini wananchi hawanufaiki na rasilimali hizo.

Alisema endapo chama kitampa ridhaa kupeperusha bendera, ana uhakika wa kunyakua ushindi kwa kuwa amejipanga kutangaza sera zitakazowavutia wananchi.

"Sitawapa pombe za viroba vijana, hususani wale wanaoendesha bodaboda. Nimejipanga kuwatangazia sera zitakazowavutia katika mikutano yangu," alisema Kaaya.

 • Tarifa ya Shaaban Mdoe, ARUMERU via gazeti la UHURU

CCM yavuna 24 kutoka CHADEMA Moshi


Wanachama wa CCM na viongozi wao mjini Moshi walifanya mkutano wa hadhara katika maeneo ya Pasua, Moshi mjini siku ya Jumamosi, Aprili 18, 2015.

Mkutano huo ulioudhuriwa na mamia ya watu ulivuta hisia za wengi na katika waliovutika ni pamoja na wanachama 24 wa CHADEMA ambao walirudisha kadi na kujiunga na CCM.

Jimbo la mjini Moshi limekuwa gumzo la kiasa kabla ya uchaguzi mkuu kutoaka na baadhi ya wananchi na vikundi mbalimbali vya kijamii kujitokeza kwa kumshawishi Daudi Babu Mrindoko achukue fomu za kugombea ubunge, kitendo ambacho kimekuwa kama cheche za moto kiasi cha baadhi ya vigogo kujitangaza kutogombae tena nafasi zao za udiwani na ubunge.

Baadhi ya wakazi wa Moshi wanadai kuwa wanataka mabadiliko 2015 wapate Mbunge kijana mwenye uwezo na wepesi wa kuwatumikia, na atakayekuwa kiungo wa jamii yote ya wakazi wa Moshi. 


Daudi Babu Mrindoko


Ujumbe wa harakati za Imetosha watembelea watoto Buhangija
Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.


Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga
Wajumbe wa Imetosha

Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.


Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo


Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha

Alisema, “Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa” alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10.Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.

Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284 wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.

Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho

Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands!Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga


Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho


Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali

Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.

 • Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira

Wahamiaji dini hii watuhumiwa kuwatupa wa dini ile baharini

Polisi ya Italia imewakamata wahamiaji kumi na tano kutoka Afrika ambao wanashukiwa kuwatupa baharini wahamiaji wenzao ambao ni Wakristo waliokua wakishirikiana safari.

Hata hivyo zaidi ya wahamiaji wengine arobani wamekufa maji baada ya meli yao kuzama wakati ilipokua ikijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean. Mamia ya wahamiaji walionusurika wamewasili siku za hivi karibuni katika mji wa Reggio Calabria, nchini Italia, wengi wao ni kutoka nchi za kusini mwa Sahara

Kulingana na ushahidi wa manusura tisa wa dini ya Kikristo, walionukuliwa na vyombo vya habari vya Italia, wahamiaji 105, wengi wao wakiwa ni kutoka Senegal na Côte d’Ivoire ambao ni Waislamu waliondoka pwani ya Libya Aprili 14 wakiwa wamejazana kwenye sehemu kulikokuwa kuliwekwa matairi. Wakati walipokua wakivuka bahari ya Mediterranean, rabsha ilitokea kati ya Waislamu na Wakristo.

Wahamiaji kutoka Nigeria, Ghana na Mali walitishiwa mara kadhaa kutupwa baharini kutokana na "dini yao ya Ukristo ” “Chanzo cha uhasama wao kinatokana na dini,” polisi imesema.

Inaarifiwa kuwa wakati wa usiku, Waislamu kumi na tano walichukuliwa hatua ya kutupa Wakristo kumi na mbili katika mawimbi, katika maji ya kimataifa. Wahamiaji wengine Wakristo hawakuweza kunusurika na baadae walikufa maji.

Meli, ambayo ilikuwa katika matatizo katika pwani ya Sicily, iliokolewa na manuari ya Italia na wakati abiria walipowasili katika mji wa Palerme, Wakristo walisikilizwa na Ofisi ya mashataka ya Palerme. Watuhumiwa kumi na tano waliohusika na kitendo cha kuwatupa wenzio baharini walikamatwa na kufungwa kwa tuhuma za mauaji yenye misingi ya kidini. Polisi ya Palerme imesema kuwa watuhumiwa hao ni raia kutoka Côte d’Ivoire, Mali na Senegal.

Taarifa kutoka RFI Kiswahili

Saudi Arabia supports WFP refugee operation in Tanzania

A ceremony held at WFP's Tanzania Country Office in Dar es Salaam was attended by Mr. Walid Bin Abdulrahman Alzinedi, a delegate from the Ministry of Finance of the Kingdom of Saudi Arabia and Mr. Wajih Bin Masoud Alotaibli, an attache of Economic and Culture Affairs with the Embassy of the Kingdom of Saudi Arabia to the Republic of Tanzania.

The consignment of 54 metric tons of dates arrived aboard MV City of Beijing in March and was immediately dispatched from Dar es Salaam to Nyaragusu refugee camp earlier this month. Distribution of the dates to the refugees is due to start in May.

"WFP is grateful to Saudi Arabia for this latest contribution of dates to our refugee operation," said WFP Tanzania Representative Richard Ragan. "The Kingdom of Saudi Arabia is a valued and consistent supporter of WFP, having contributed nearly US$4 million towards WFP's operations in Tanzania since 2006,"

The dates will supplement WFP's monthly food assistance to refugees which consists of maize meal, pulses, Super Cereal (nutritious porridge), salt and fortified vegetable oil. WFP also provides specialized nutritional support to mothers and young children in the camp.

Nyaragusu camp holds more than 65,000 refugees, mostly from DRC with a small number from Burundi. Tanzania has been hosting these refugees since the early 1990s.

Polisi yaviweka chini ya ulinzi vituo 3 vya kulelea na kufunza watoto dini na karateJESHI la Polisi Mkoani Dodoma limeviweka chini ya ulinzi vituo vitatu vya kulelea watoto vilivyopo eneo la Nkuhungu Mkoani hapa na kuendelea na uchunguzi wa watu wanaohusika kuendesha vituo ambavyo havijasajiliwa.

Kufuatia sakata hilo, watu 115 wakiwemo watoto walikutwa wakiishi katika vituo hivyo.

Kwa mujibu wa majirani wa vituo hivyo watoto hao walikuwa wakipatiwa mafundisho ya dini ya Kiislam na kareti na wametoka katika mikoa 14 nchini huku asilimia kubwa ya watoto hao wakitoka katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Juzi saa sita na nusu usiku polisi walifika katika eneo la kwanza na kukuta watoto 63 kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 ambapo wadogo kabisa wana umri chini ya miaka sita.

Kwenye kituo cha pili walikutwa watoto 40 ambapo kati yao walikuwa na umri chini ya miaka 18 ni 12 ambapo katika kituo cha tatu walikutwa watoto saba wenye umri chini ya miaka 18 walikuwa watano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alisema watoto idadi ya watoto waliokutwa katika vituo hivyo vitatu ni 63 na wenye umri wa miaka 18 -25 ni 52.

Alisema watoto hao wote ni wa kiume na wanatoka katika wilaya mbalimbali, ambapo Kondoa wanatoka watoto 50, Dodoma Mjini, Chamwino na Mpwapwa jumla yake watoto 26 na waliosalia wanatoka katika mikoa ya Kagera, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Zanzibar, Tanga, Tabora, Singida,
pwani Lindi, Mtwara Geita, Mwanza na Manyara.

Pia watoto hao walikutwa wakiwa wamechanganywa bila kujali umri katika mazingira ambayo kiuhalisia ni hatarishi.

“Uchunguzi unaendelea na yoyote atakayeguswa na ushahidi kuwa amekiuka sheria atafikishwa mahakamani ikiwemo wazazi waliowaruhusu watoto. watoto hao kuwa katika uangalizi ambao si wa kutosha kama sheria ya watoto inavyotaka” alisema.

Kamanda Misime alisema Polisi pia wanachunguza ili kufahamu vijana hao walikuwa wakifundishwa kitu gani na kama walikuwa wakihudhuria shule kulingana na umri wana na sheria za nchi zinavyoelekeza.


Baadhi ya majirani wakizungumza jana sharti la kutotajwa majina yao walisema wanashangazwa uwepo wa kituo hicho ambacho kina idadi kubwa ya watoto.

Wengine walionesha kushangazwa na kituo hicho ambacho muda mwingi watoto huonekana wapo peke yao bila uangalizi wowote.

Walisema walianza kuwaona watoto hao tangu mwaka jana.

“Mwanzoni tuliona kama kawaida lakini kadri siku zinavyokwenda tunashangaa mambo yanayoendelea, watoto hawa muda mwingi unawaona wapo peke yao,wale wakubwa ndio wanaopika chakula kikishakuwa tayari wanaitana kisha wanakaa katika makundi makundi kula chakula” alisema.

"Yaani hapa hawa watoto wanaishi peke yao..,hawana muangalizi yeyote..,walimu wao wakishamaliza kuwafundisha tu ..,wanaondoka."alisema mkazi mmoja wa jirani na nyumba hiyo kwa sharti la kutotajwa jina lake

Mkazi huyo alisema,kinachoshangaza zaidi ni wakati ambao watoto hao hucheza michezo ya kupigana huku wakionesha kama wanafanya mazoezi.

"Kuna wakati utaona wanacheza mchezo wa kupigana...,sijui wanaita kareti...,yaani wanavyokuwa wanacheza...,wanaonekana kama wanafanya mazoezi fulani hivi..,na hapo kwa mimi binafsi ndipo panaponitia hofu."

Mkazi mwingine anayoishi jirani na kituo hicho alisema,yeye hashangai kuwepo kwa watoto hao kwenye nyumba hiyo,isipokuwa alisema,hali ya mazingira katika nyumba hiyo siyo ya kuridhisha.

"Watoto kuwepo katika kituo hicho siyo shida,changamoto iliyopo katika kituo hicho ni mazingira...,kwa kweli mazingira ni mabaya na machafu hayafai kuwaweka watoto hao..,hii inaweza kuwasababishia mlipuko wa magonjwa yakiwemo ya kuhara."

Vile vile mkazi huyo alisema,pia kituo hicho hakijakidhi hatua ya kutunza watoto hao kwa kuwa hakuna msimamizi maalum wa kuwafundisha masuala ya nidhamu na kusababisha watoto hao kutokuwa na nidhamu kama Dini ya kiislamu inavyotaka.

Pia watoto hao wamekuwa wakilala chini kwenye mikeka na wengine hutandika nguo huku kukiwa na magodoro machache.

Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo,Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab alisema hakuna dhambi yoyote kwa watoto hao kulelewa katika kituo hicho na akisema hayo ni mafunzo katika madrasa ambayo harakati zake zilianza zamani ulimwenguni kote.

"Madrasa zilianza zamani... polisi haina Mamlaka ya kufunga madrasa labda kama watakuta kuna tatizo lolote la kuhatarisha amani."alisema sheikh Rajab.

Kuhusu suala la kusoma shule,sheikh huyo alisema kuwa suala hilo linamuhusu mzazi na mtoto wake.

"Suala la mtoto kwenda shule ama kutokwenda hilo linamhusu mzazi na mwanawe,maana yeye ndiye anayeamua ampeleke mwanae kwenye taaluma gani...,ya dini ama ya kidunia,”

Kuhusu mazingira ya eneo hilo kutoridhisha Sheikh Rajab alisema,hawezi kulizungumza suala hilo kwa kuwa kuna wanamazingira wanaopaswa kuliona na kulizungumzia.

"Mimi Siwezi kuzungumzia suala la Mazingira... wanamazingira wapo na wao ndio wanaopaswa kulizungumzia suala hilo..,kama hayaridhishi basi waambiwe na kupewa muda wa utekelezaji ...,wasipotekeleza ndipo hatua zichukuliwe." alisema Sheikh Rajab.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nkuhungu aliyefahamika kwa jina moja la Ponela alisema,alikuwa akiwaona watoto katika nyumba hiyo lakini hakuuliza chochote kwani aliamini ule ulikuwa ni uhuru wa Kuabudu.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Betty Mkwassa alisema amesikitishwa na hali ya mazingira waliyokuw wakiishi watoto hao.
“Lazima sheria ichukue mkondo wake” alisema.
Akihojiwa jana Katibu wa Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) Hassan Kuzungwa alisema baraza limesikitishwa sana na uwepo wa vituo hivyo.

Tangu walikuwa wakisali wakifanya mazoezi huku wakijitenga na majirani wanaowazunguka.
Baadhi ya watoto wanaolelewa na vituo hivyo
Taarifa via Lukwangule blog

[update] Maana yake nini hii?

Waliposema waliotutangulia ya kuwa, "usilolijua litakusumbua" hawakukosea kwani baada ya kutaka sana kufahamu kuhusu nilichochapisha hapo chini, hatimaye nimepata maelezo kutoka kwenye tovuti ya Appalachian History kama ifuatavyo:

Glass ‘bottle trees’ originated in ninth century Kongo during a period when superstitious Central African people believed that a genii or imp could be captured in a bottle. Legend had it that empty glass bottles placed outside, but near, the home could capture roving (usually evil) spirits at night, and the spirit would be destroyed the next day in the sunshine. One could then cork the bottles and throw them into the river to wash away the evil spirits.

Furthermore, the Kongo tree altar is a tradition of honoring deceased relatives with graveside memorials. The family will surround the grave with plates attached to sticks or trees. The plates are thought to resemble mushrooms, calling on a Kongo pun: matondo/tondo [the Kongo word formushroom is similar to their word to love].
And so, trees and bottles eventually came together.

This practice was taken to Europe and North America by African slaves. Thomas Atwood, in History of the Island of Domi (1791), made particular note of the bottle tree as a protection of the home through an invocation of the dead. Atwood writes of the confidence of the blacks “in the power of the dead, of the sun and the moon—nay, even of sticks, stones and earth from graves hung in bottles in their gardens.”

While Europeans adapted the bottle tree idea into hollow glass spheres known as “witch balls,” the practice of hanging bottles in trees became widespread in the plantation regions of Southern states and from there migrated north and inland into Appalachia.

Traditionally the bottles are placed on the branches of a crepe myrtle tree. The image of the myrtle tree recurs in the Old Testament, aligned with the Hebrews’ escape from slavery, their diaspora and the promise of the redemption of their homeland.

Bottle tree colors can range from blue, to clear, to brown, but cobalt blue are always preferred: in the Hoodoo folk-magic tradition, the elemental blues of water and sky place the bottle tree at a crossroads between heaven and earth, and therefore between the living and the dead. The bottle tree interacts with the unknown powers of both creative and destructive spirits.

The bottles are placed upside down with the neck facing the trunk. Trees need not be thickly populated with bottles. Malevolent spirits, on the prowl during the night, enter the bottles where they become trapped by an ‘encircling charm.’ It is said that when the wind blows past the tree, you can hear the moans of the ensnared spirits whistling on the breeze. Come morning they are burnt up by the rising sun.

Today, the bottle tree has entered the realm of folk art. Companies now market bottle tree armatures meant to serve, once clothed with milk, wine, or milk of magnesia bottles, as colorful garden ornaments. The poor man’s stained glass window, you might say.

Sources:
 1. www.cullmantimes.com/features/local_story_171000245.html
 2. www.lovelycitizen.com/story/1257420.html
 3. Tradition and Innovation in African-American Yards, by Grey Gundaker, African Arts, Vol. 26, No. 2 (Apr., 1993), pp. 58-96
 4. Alabama, One Big Front Porch, by Kathryn Tucker Windham, NewSouth Books, 2007


Rafiki yangu aliyepo katika safari ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, wakiwa njiani alfajiri ya leo wamestaajabishwa kwa kuona chupa nyingi zilizokuwa zikining'inia kwenye miti huko Nyakabango mkoani Kagera.

Binafsi nimejikuta nawaza kuwa huenda ni mbwembwe na mikogo ya kutunishiana msuli kuonyeshana nani zaidi katika ulimwengu wa mazingaombwe na imani za abracadabra. Huenda hayo yakawa ni mawazo yangu yasiyo sahihi, labda ipo maana njema zaidi yenye manufaa katika kufanya hivi.

Pengine urembo/mapambo?

Anayejua zaidi atatufahamisha bila shaka ili kutuondoa ujinga. Tafadhali tuelimishane ndiyo maana nimeuliza, "Maana yake nini hii?"
Scientists' recent best advice for staying sharp as you get older

The best advice for staying sharp as you get older: Be physically active. The sooner you start the better -- says Dr. Dan Blazer, an emeritus professor of psychiatry at Duke University, and adds:

 1. Control high blood pressure and diabetes, and don't smoke. Those are key risks for heart disease, and what's bad for your heart is bad for your brain.
 2. Some medications commonly taken by seniors - including certain anxiety or sleep drugs, antihistamines, bladder drugs and older antidepressants - can fog the brain, so ask about yours.
 3. Keep socially and intellectually active.
 4. Get enough sleep.
 5. Be careful of products that claim to improve cognitive functioning. There's no evidence that vitamins and dietary supplements like ginkgo biloba help. And the jury's still out on whether computer-based brain-training games do any good.

What's the difference between normal aging and cognitive decline?

Dr. Jason Karlawish of the University of Pennsylvania says: With Alzheimer's (disease), nerve cells in the brain die. With normal cognitive aging, neurons don't die - they just don't work as well.

Former IMF Head arrested for tax fraud

Former International Monetary Fund boss, Rodrigo Rato, who led the organisation from 2004 - 2007, was arrested in Spain on Thursday night over charges of tax evasion and money-laundering.

Tax and customs officials raided his Madrid home and took him away in a police car.

He was released overnight. A judge is preparing to charge him with money-laundering and tax fraud. He's accused of hiding part of his personal fortune overseas illegally and also of mismanaging funds at Bankia, the big Spanish bank he headed before it went bankrupt and needed a bailout.

Rato was the predecessor of Dominique Strauss-Khan. He's also a top figure from Spain's ruling conservative party. He served in the past as Spain's vice president and economy minister. He's now become a symbol of corruption revealed when Spain's economy collapsed.

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Aprili 18, 2015