Waliozaliwa, walioishi Kariakoo waanzisha Family FoundationMwenyekiti wa Kariakoo Family Foundation (KFF) Mohamed Bhinda akiongoza kikao cha Kamati ya Utendaji katika kuandaa rasimu ya katiba ya chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni kama taasisi isiyo ya kiserikali kwa nia ya kukutanisha upya wadau wote waliozaliwa, walioishi na wenye asili ya Kariakoo katika wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam. Mkutano huu umefanyika jioni ya Jumapili huko Kinondoni Studio. Kulia kwa Bhinda ni katibu wa chama hicho Senpai Wahid.Mtunza hazina wa KFF Yahaya Sameja akielezea namna chama hicho cha jamii ya wana Kariakoo kitavyoweza kujiendesha kwa njia za ada, michango na misaada ya wafadhili katika kuendeleza wanachama, ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika shida na raha. Kushoto ni Mwenyekiti wa KFF Mohamed Bhinda na kati ni Makamu Mwenyekiti Tatu LumeleziWana KFF wakipata mlo wa mchana wakati wa mapumzikoJopo la kamati ya utendaji ya KFF baada ya mkutano wao leo

Picha za mkutano Musoma wa Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA


Picha hizo za mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Kaimu Katibu Mkuu John Mnyika jioni ya Jumapili huko Musoma katika uwanja wa Mkendo baada ya asubuhi kuzindua mafunzo ya timu za kampeni, viongozi wa chama na viongozi wa serikali za mitaa kwa kanda ya Serengeti (Mara, Simiyu na Shinyanga), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushinda dola na kuongoza serikali, kama yalivyozinduliwa kitaifa na Mwenyekiti wa Taifa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
ISIL claims massacre of Ethiopian Christians in Libya

A new video from the Islamic State of Iraq and the Levant (ISIL) purportedly shows the group killing captured Ethiopian Christians in Libya.

The 29-minute video released online on Sunday shows two groups of dark-skinned captives. It says one group is held by an ISIL affiliate in eastern Libya and the other by an affiliate in the south.

A masked fighter delivers a long statement before the video switches between footage of the captives in the south being shot to death and the captives in the east being beheaded on a beach.

The footage released online shows one group of about 12 men being beheaded by armed men on a beach and another group of at least 16 being shot in the head in a desert area.

It was not immediately clear who the captives were.

Redwan Hussein, an Ethiopian government spokesman, told Reuters that he could not immediately confirm the nationalities of the victims.

In a separate interview with AFP news agency, Hussein condemned the killing "whether they are Ethiopians or not."

Ethiopia's embassy in Egypt was working to verify if those killed were indeed Ethiopians, he added.

The video bore the official logo of the ISIL media arm Al-Furqan and resembled previous videos released by the group.

A text on the screen identifies the men as "followers of the cross from the enemy Ethiopian Church".


IS yarusha video inayoonyesha mauaji ya Waethiopia


Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu limerusha hewani video ambamo linaeleza ushirikiano wake na Ukristo. Wakristo wa Raqqa, makao makuu ya kundi la kijihadi nchini Syria wameeleza kuwa wamekua wakitozwa kodi ili waendelee kuishi mjini humo wakiwa Wakristo.

Lakini video hiyo ya dakika 29 inamalizika kwa kuwaua zaidi ya raia thelathini wa Ethiopia nchini Libya.

Mwanzo wa filamu hii inaonekana kama tamthilia ya historia. Kundi hilo la wanajihadi wanaanza katika video hiyo kwa kuonyesha Makanisa mbalimbali ya Kikristo: Waumini wa kanisa Katoliki kutoka madhehebu ya Roman Catholic, Wakristo wa Mashariki na Waprotestanti.

Kisha kundi hilo la wanajihadi linaelezea tofauti za kiteolojia kati ya Ukristo na Uislamu. Kundi hili linaeleza utaratibu wa dhimmi, uliyosahihishwa na sheria ya kitamaduni ya Kiislamu kwa watu wasiokuwa Waislamu waishio katika nchi ya kiislamu.

Baada ya kulipa kodi na kukubali kuweka kando baadhi ya haki zao, jamii za watu wachache zinaweza kunufaika na uhuru mdogo wa ibada na ulinzi. Utaratibu ambao kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu linasema kuwa limepitisha kwa watu wasio Waislamu wanaoishi katika maeneo yake. Wakristo wa Raqqa, makao makuu ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kaskazini mwa Syria, wanaonekana mbele ya kamera na kusema kuwa wamechagua utaratibu huo.

Makundi mawili ya raia wa Ethiopia yalionyeshwa katika picha. Baadhi, wamevaa nguo za rangi ya machungwa ikimaanisha wafungwa wa Guantanamo,wakiwa karibu na bahari kaskazini mwa Libya. Wengine wamevaa suruali na shati vya bluu, huku wakiwa jangwani, katika mkoa wa Fezan nchini Libya, kwa mujibu wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Baadhi ya wanajihadi walikua tayari kuwakata vichwa mateka hao, huku wakifunika nyuso zao.

Kisa hiki cha tatu ni, tishio la moja kwa moja la kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu dhidi ya " waumini wa msalaba". Mtu aliyekua alijifunika uso wake aliweka bunduki yake kwenye kamera huku akiongea kwa lugha ya Kiingereza, akiwaeleza Wakristo wa ulimwengu mzima. " Hamtakua na usalama kama hamtakubali Uislamu, aidha kulipa Jizya (kodi) na kukubali kunyeyekea", amesema mtu huyo. Jizya ni kodi ambayo inapelekea watu wasio Waislamu waishio katika nchi ya kiislamu kuwa na uhuru fulani, kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.

Serikali ya Ethiopia imelaani mauaji ya raia wake zaidi ya thelathini huku ikiapa kupambana na Waislamu wenye itikadi kali za kidini.

CCM na. 7 Mzee Moyo afukuzwa chamani

Hassan Nassoro Moyo
Hassan Nassoro Moyo

MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwenye kadi namba saba Mzee Hassan Nassoro Moyo amefukuzwa katika chama hicho.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 81 ambaye amekuwa na msimamo tofauti na chama chake kuhusu Zanzibar ametimuliwa na mkoa wa kichama wa Magharibi Unguja.

Wamesema sababu ya kumtimua uanachama wa CCM, chama ambacho alishiriki kukiasisi, ni matendo yake kwenda kinyume na maadili na sera za chama hicho.

Kauli ya kutimuliwa imetolewa na katibu wa CCM mkoa wa Magharibi, Unguja Aziza Iddi Mapuri. Katibu huyo amesema matamshi mbalimbali aliyokuwa akiyatoa Mzee Moyo katika mikutano ya hadhara inayofanywa na chama cha wananchi, CUF inaonesha kwamba amekisaliti chama chake.

Taarifa hiyo imetoa mfano, tarehe 30-4-2014 katika mkutano wa CUF uliofanyika Kibanda Maiti, Katibu wa CUF, Seif Sharif Hamad alimsimamisha Mzee Moyo ambaye alisema serikali tatu ndiyo msimamo wa Wazanzibari wote.

Aidha, katika mkutano uliofanyika Tibirinzi huko Pemba tarehe 9-2-2014 Mzee Moyo alijitambulisha kwamba ni mwenyekiti wa maridhiano kutoka CCM wakati siyo kweli kwani Chama Cha Mapinduzi hakimtambui kiongozi huyo.

Taarifa hiyo imesema CCM baada ya kutafakari kwa kina imebaini kwamba kiongozi huyo amekuwa akiongoza upotoshaji wa hali ya juu na hafai kuendelea kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Iemtoa mfano kuwa, wakati akihutubia kongamano la CUF katika ukumbi wa taasisi ya Kiswahili na lugha za Kigeni, Moyo alibeza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kusema Mkataba wa Muungano wa tarehe 22-4-1964 haujulikani uliopo na wabunge wa Bunge Maalum la Katiba walikuwa hawajui wanachokifanya.

Hatua ya kumfukuza Mzee Moyo inaashiria kuwa Kamati ya Maridhiano iliyokuwa na wajumbe sita, 3 kutoka CCM na 3 kutoka Chama cha Wananchi, CUF, ni shubiri kwa CCM ambayo baadhi ya viongozi wake wakuu wanataka serikali ya umoja wa kitaifa ivunjwe.

Wawakilishi wa CCM katika Kamati ya Maridhiano waliokuwa pamoja na Mzee Moyo, tayari walishafukuzwa uanachama, hivyo tukio la hili linahitimisha kuwamaliza wanachama hao walioleta maridhiano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Waliokuwa na Mzee Moyo kwenye Kamati ya Maridhiano ni Mansour Yusuf Himid ambaye alifukuzwa Agosti 2013 na Mohammed (Eddy) Riyami aliyejiondoa.

Wote sasa wanafanya kazi na CUF kusaidia kampeni ya kupatikana Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Mansour ambaye ameteuliwa kuwa katibu wa kamati ya mkakati ya kuhakikisha ushindi wa Maalim Seif Sharrif Hamad, ameshatangaza kugombea uwakilishi jimbo la Kiembesamki.

Mzee Moyo aliliambia gazeti la MwanaHALISI Online kuwa taarifa hizo amezisikia juu juu tu, kwani hajapewa taarifa rasmi ya kufukuzwa uanachama wake.

“Mimi sipo Zanzibar, taarifa hizo nimezisikia juu juu tu, lakini muda muafaka ukifika nitatoa tamko rasmi,” anasema Mzee Moyo anayemiliki kadi namba saba.

Mzee Moyo anasema, hashangai kusikia kuwa amefukuzwa kwani mara kadhaa viongozi wa CCM wa mkoa wa Wilaya, walikuwa wanamtaka awarushie kadi yake ya uanachama, lakini aligoma na kuwaambia labda akiitaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Vuguvugu la kumvua uanachama Mzee Moyo ulianza tangu kamati yake ya Maridhiano ilipofanikisha kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa baada uchaguzi 2010 amekuwa akipigania kuwepo Muungano wa serikali anaosema ndio wa haki na utaipa Zanzibar serikali yenye mamlaka kamili kinyume na ilivyo uhai wote wa Muungano miaka zaidi ya hamsini.

Msimamo huu unapingana na sera ya CCM inayoshikilia Muungano wa Serikali mbili. Msimamo wake unachukuliwa kama ni msimamo unaoendana na CUF hivyo kuwekwa kundi la kusaliti CCM.

Taarifa ya CHADEMA kuhusu Watanzania wanaoishi Afrika Kusini

KURUGENZI YA MAMBO YA NJE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


SERIKALI YA TANZANIA ICHUKUE HATUA ZA HARAKA KUNUSURU WATANZANIA WAISHIO AFRIKA KUSINI DHIDI YA GHASIA NCHINI HUMO


Kumekuwepo na hali ya raia wa Afrika Kusini kushambulia , kujeruhi na kuua raia wa kigeni wa Kiafrika wanaoishi nchini Afrika Kusini. Hali hii inadaiwa kuchochewa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa wananchi wa Afrika Kusini wanaodai ajira hizo kuchukuliwa na Waafrika wa mataifa mengine na hivyo wao wenyeji kubakia kwenye dimbwi kuu la umasikini.

Ni mtazamo wa kuimarika kwa kiwango cha umasikini kwa wananchi wengi nchini humo dhidi ya kuimarika kwa kiwango cha utajiri kwa wachache kunakopelekea ghasia hizi. Zaidi, mali za Waafrika wageni nchini humo zimekuwa zikiharibiwa baada ya wamiliki kukoswa katika mashambulizi hayo. Aidha, kama nchi nyingine za Kiafrika, Tanzania ina idadi kubwa ya raia wake wanaoishi nakufanya kazi nchini Afrika Kusini. Na mpaka sasa inadaiwa kuwa watanzania wawili (2) wameuwawa katika ghasia hizo za wenyeji dhidi ya Waafrika wageni.
Kwa misingi hiyo:

1. CHADEMA inalaani vikali hali ya raia kudhuru na kutwaa uhai wa raia yoyote yule. CHADEMA kama muumini wa haki za binadamu inayojumuisha haki kuu ya kuishi inasikitishwa na hali hiyo ya machafuko inayoondoa usalama wa sio tu kwa raia wa kigeni wa Kiafrika walioko Afrika Kusini bali pia kwa raia wengine wa Afrika Kusini ambao hawawezi kufanya shughuli zao kwa ukosefu wa usalama nchini humo.

CHADEMA inawasihi raia wa Afrika Kusini kuwachukulia Waafrika wenzao kutoka mataifa mengine kama ndugu zao ambao kwapamoja walishrikiana kupambana na ubaguzi wa rangi na hatimaye kuleta uhuru kwa taifa hilo. Ni muhimu raia wa Afrika Kusini wakatatua matatizo yao ya ndani hasa ya kiuchumi kwa kushirikina na wenzao wa mataifa ya Afrika waishio nchini humo na si kuwaona kama maadui zao.

2. CHADEMA inaitaka serikali ya Tanzania ishirikiane na serikali ya Afrika Kusini kuchukua hatua za haraka kunusuru maisha ya watanzania waishio nchini Afrika Kusini dhidi ya ghasia hizi kwa kuwahakikishia usalama wao ama kuwawekea utaratibu wa kuondoka ama nchini humo na kurejea nyumbani ama kwenye miji yenye machafuko kama Durban na kuwapeleka kwenye miji ya usalama zaidi mpaka hali itakapotengamaa kwenye miji hiyo kama ilivyofanya kwa Watanzania waishio Yemen ambako nako machafuko yamekithiri. Ni muhimu Serikali ikawa makini kwa jambo hili kwani teyari mataifa mengine ya kiafrika ya Botswana, Malawi na Zimbabwe yaneshaanza kuwaondoa raia wake nchini humo kwa kuhofia usalama wao.

3. CHADEMA inazikumbusha nchi za Kiafrika ambazo zina utajiri mkubwa wa rasilimali kuhakikisha inatatua matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi hizo ikiwa ni pamoja na kupunguza tofauti ya kipato kati ya wengi wasio nacho na wachache wenye nacho.

Ni muhimu serikali hizi kujikita katika kupambana na umasikini kwa kutengeneza fursa za ajira kwa raia wake na hivyo kupunguza kiwango cha umasikini na hatimaye kuondoa mazingira ya machafuko yanayosababishwa na hasira za wananchi kutokana na hali yao ya umasikini. Kwa mantiki hiyo, ni muhimu Jumuiya za kikanda na Umoja wa Afrika wenyewe (AU) zikaweka msisitizo wa ukombozi wa kiuchumi unawaweza kukidhi haja na matakwa ya raia wa bara hili.

4. Kipekee, CHADEMA inaikumbusha serikali ya Tanzania kuichukilia hali ya Afrika Kusini kama taadhari kwake kwani hali ya umasikini na ukosefu wa ajira hapa nchini imekuwa kubwa kiasi cha kuibuka kwa vikundi vya kihalifu vya Komando Yoso na Panya Road vilivyofanya mashambulizi na uporaji kwa raia wengine. Tofauti ndogo iliyopo kati ya Afrika Kusini na Tanzania ni kwamba Afrika Kusini raia wazalendo wanashambulia waafrika wa mataifa mengine wakati hapa Tanzania ilikuwa ni kushambuliana baina ya Watanzania.

Imetolewa leo tarehe 18.04.2015 Jijini Dar es salaam na;
Deogratias Munishi
Mkuu wa Mambo ya Nje – CHADEMA
+255715887712

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Aprili 19, 2015Ujue undani wa maisha ya Linda kesho katika "HUYU NA YULE"


Kesho Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. 

Je mume wake, Mali walijuana wapi?... na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. 

Usikose mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na Kwanza Production Michigan, Alpha Igogo ambaye alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda.

Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta

Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho.

  • Tumeshirikishwa na Mubelwa Bandio/Kwanza Production

Nyalandu: Umoja wetu ndiyo utatufanya tusonge mbele

Waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na aliyewahi kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Joshua Kileo (Kulia) baada ya ibada katika kanisa la KKKT Mjini Kati siku ya Jumapili.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema pamoja na mitihani mikubwa ambayo taifa inakabiliana nayo, umoja wa Watanzania utaifanya nchi isonge mbele kama taifa linalozingatia sheria na demokrasia.

Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili ya Pili ya Pasaka iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mjini Kati jana, Nyalandu alisema nchi itafanikiwa kupita mitihani hiyo kama wananchi wataimarisha umoja kati yao.

“Nchi inapita huku kukiwa na mambo mengi makubwa kufanya…kila mmoja anahitaji amani na hiyo tunaweza kuipata au kufanikiwa kupita salama iwapo tutakuwa na umoja.

“Nchi yetu itasimama, itashinda mitihani ambayo tunayo kama ya uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu, upigaji wa kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” alisema.

Mapema katika mahubiri yake kanisani, Mteolojia Solomoni Dereva, aliwaomba Watanzania kuliombea taifa kwa Mungu ili liweze kupita kwa utulivu katika kipindi hiki chenye mambo makubwa.

“Tumuombe Mungu pia atuletee viongozi wazuri, wenye sifa ambao watatutoa hapa tulipo na kutufikisha mbele zaidi katika maendeleo,” alisema.

Alisema kiongozi mzuri ni sawa na mchungaji mwema ambaye huanza kuchunga nafsi yake dhidi ya matendo maovu kama rushwa na ubinafsi na pia huchunga familia yake na ofisi aliyokabidhiwa ili kuwatumikia wananchi.


  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Mroki Mroki

Balozi Mulamula ahudhuria Mkutano Mkuu wa Watanzania Wasabato MarekaniMchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.Nchungaji Hery Mhando akifanya mamombi maalum kabla ya kumkaribisha mchungaji Wilbert Nfubhusa kutoa mahubiri,Mshereheshaji Magoma akifafanua jamboMhahubiri yakiendelea

WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAOWatoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto


  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Mubelwa Bandio/Kwanza Production