Imani abainisha kanuni rahisi ya kupata mafanikio makubwa

Ni hivi. Ili uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa unayotaka iwe katika masomo, kupata kazi, kuvuna sana mazao shambani, kupata faida katika biashara au kuwa na uhusiano mzuri na ndoa nzuri, ni lazima kwanza ujue kwamba hayo yote yanawezekana na yanakuhusu wewe moja kwa moja kwa asilimia zote na siyo bah

Unapotaka mafanikio ambayo huamini kwamba unastahili kuyapata, huwezi kamwe kuyapata hata kama ungefanya nini. Unapotaka kupata ajira, lakini ukajiambia kwamba kuna watu wengi wenye sifa kuliko wewe, ambao watapata kazi hiyo na siyo wewe, ni wazi pia hutapata kazi hiyo unayoitafuta.

Unapoamini kwamba utapata kazi hiyo kwa juu juu, lakini ndani kabisa mawazoni mwako unajua ni jambo gumu litakuwa gumu kweli. Unapoingia kwenye biashara kwa kuamini kwamba hutaweza kufanikiwa kwa sababu haijawahi kutokea ukafanikiwa au kwa sababu wewe una mtaji mdogo, hufahamiki na pengine hukusoma sana kama wengine, ni wazi hutafanikiwa.

Unaposema na kuamini kwamba una mkosi, utaendelea kuwa na mkosi hadi unaingia kaburini. Sisi binadamu ni kile tunachoamini. Kwa nini inakuwa hivyo, kwamba tunapoamini kuwa hatuwezi au tuna mkosi, mambo yanakuwa kama tunavyoamini?

Siyo kuamini tu kwamba mambo yatakwenda vibaya au tuna mkosi, lakini hata tunapoamini kwamba tunaweza, tutamudu, tutashinda, tutafurahi na tutatekeleza, basi ni wazi itakuwa hivyo. Hii ni kanuni ya kimaumbile, na ndiyo kanuni pekee ambayo ukiitumia ni lazima ikupe mafanikio unayoyataka. Kwa mujibu wa kanuni hii kwa vyovyote vile, tunavyofikiri na kuamini ndicho kinachokuwa chetu, iwe ni katika mafanikio au maanguko.

Kwa hiyo, ili kuweza kupata kile unachokihitaji katika maisha na kuenda sawa na kanuni hii ambayo ni rahisi kwako kuitumia na kukupa mafanikio, ni lazima kuweza kutambua umuhimu wa kufikiri vizuri. Kwa kufikiri kwetu vizuri itatusaidia kuweza kumudu na kutenda kwa mkabala wa kimafanikio na kuweza kuvuta mafanikio makubwa kwa upande wetu zaidi.

Kwa kufikiri kwamba hatuwezi au hatustahili, bila wenyewe kujua, tutafanya kwa mkabala wa kutoweza na kutostahili. Kumbuka kuwa upo uhusiano mkubwa sana kati ya fikra zetu, hisia zetu na tabia au matendo yetu. Tunapofikiri kwamba hatuwezi, bila kujua, tutakuwa na tabia zitakazotupeleka mahali ambapo hatutaweza kweli.

Mwandishi na mwanafalsafa maarufu duniani Shakespeare aliwahi kusema: ‘Hakuna jambo baya au zuri, bali kufikiri kwetu ndiko kunakolifanya jambo kuwa hivyo’. Huu ndiyo ukweli , kwamba, kufikiri vibaya hutudhuru sana , tuwe tunajua au hatujui. Ubaya au uzuri wa mawazo yetu, hasa yale ya kina ni kwamba, kile tunachokifikiri na kukiamini ndicho kinachotokea au kufanyiwa kazi, hayachagui au kutuhurumia ati kwa sababu hatujui juu ya ukweli huo.

Kwa hiyo, hatua ya awali kabisa ya mafanikio ya binadamu yako kichwani au mawazoni mwake. Kuna familia, koo, hata makabila ambayo yamekuwa na fikra kwamba hayawezi au hayastahili. Mtu kutoka familia, koo au makabila hayo anaweza kuwa na uwezo mkubwa sana katika kutenda, kipaji na ufahamu mkubwa ajabu, lakini akabaki kuwa mbumbumbu ambaye familia , ukoo au kabila lake limefanywa kuaminika kwamba ndilo linalostahili kuweza au kuwa nacho.

Bila kuanza kukagua namna tunavyofikiri, inaweza kuwa kazi bure kujaribu kutafuta au kuzungumzia mafanikio kwa ngazi yoyote, iwe mtu binafsi au taifa. Ni lazima tuanze kwa kujiuliza kile tunachoamini kuhusu mafanikio, yaani kupata kile tukitakacho maishani. Inawezekana kabisa, bila sisi wenyewe kujua tulishawekewa mipaka ya mafanikio tangu wakati tukiwa wadogo. Mipaka kama hii huwekwa vipi?

Inawezekana kabisa wazazi au jamii yote tulimokulia ilikuwa ikisema na kutenda kwa njia ambayo ilituonyesha kwamba tunachoweza sanasana ni kuhangaika na kupata ajira mahali, basi. Pengine ilisema na kutenda kwa njia ambayo ilituonyesha kwamba, ni vigumu kwetu kumiliki gari. Inawezekana kwamba ilisema na kutenda kwa njia ambayo ilituonyesha kwamba hatupaswi kuinuka sana kimaisha kwani sisi kwa ukoo au kabila fulani hatustahili.

Pia kuna wakati tunajikuta tukitamani kusonga mbele katika kutafuta kile tunachokitaka, lakini tunazuiwa na uvivu wa aina fulani tu tusioujua sababu yake, tunazuiwa na kuahirisha kufanya hivyo, bila kujua ni kwa nini. Inawezekana kabisa kwamba hiyo inatokana na malezi, mazingira tulimokulia au uzoefu wetu maishani.

Kumbuka kuwa kuna vizuizi vingi vilivyowekwa kwenye mawazo yetu katika hatua hizo tulizopitia maishani. Lakini ili uweze kumudu kuondokana na vizuizi hivyo ni muhimu kwako kujua mambo mawili tu, ambayo ni kuweza kutumia kanuni tuliyoongelea ya kuamini kuwa katika maisha yetu tutaweza, tutamudu, tutashinda na tutatekeleza na jambo la pili ni kubadili mtindo wako mzima wa kufikiri.

Unapoamua kubadili mtindo wako wa kufikiri sio kwamba tu unakuwa unajiondoa kwenye vizuizi vya kutofanikiwa, bali pia unakuwa unajiweka katika nafasi nzuri ya kupata kile unachokihitaji. Je, unawezaje kubadili mfumo wako mzima wa kufikiri na kukuwezesha kukupatia kile unachohitaji ama kufanikiwa kwa ujumla? Kujua hilo hakikisha unafuatilia makala ijayo katika DIRA YA MAFANIKIO bila kukosa, ili kujua mawazo yako jinsi yanavyoweza kufanya kazi na kukupa utajiri.

Ansante sana kwa kuwa msomaji mzuri wa DIRA YA MAFANIKIO, endelea kuwashirikisha wengine kujifunza zaidi kupitia mtandao huu. Kwa pamoja tukishirikiana tunaweza kabisa kufika mbali kimafanikio na kuufuta umaskini.

DAIMA TUKO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.

IMANI NGWANGWALU,
0713048035,
[email protected]

Call - CODESRIA Governance Research Program


Governance Research Program

International Conference
on
Public health governance in Africa

Date: November 12-13, 2015; Venue: Windhoek, Namibia

Application deadline: May 31, 2015

CODESRIA is a Pan-African membership research organization established in 1973 with the broad goal of promoting the work of African and Diaspora social scientists. The intersecting fields of governance and healthcare have for years been at the core of the work of CODESRIA with multiple research networks focusing on various aspects of these themes resulting in a series of cutting edge publications on these issues. The council has since 1992 also had an annual Democratic Governance Institute, which has over the years, focused on a wide range of themes. Similarly, it has had an Institute on Health, Politics and Society that broached many important themes including private healthcare systems, the global pharmaceutical industry, HIV/AIDS and the governance of African health systems.

The ongoing Ebola Virus Disease (EVD) outbreak in the Mano River Basin of West Africa has surpassed preceeding outbreaks in rates of infection, numbers of casualties and in the geographical spread of the disease. Its centering on three countries, which suffered greatly from the recent wars in Sierra Leone and Liberia has significantly set back post-conflict reconstruction processes that were underway in these countries. Importantly, while the disease has caused significant casualties, its impact on health systems, educational and security systems and economies, to name a few, may even be more damaging.

Unsurprisingly, the outbreak has brought to the fore many themes that often rise to the surface in debates on public health in Africa. Many of these issues, which had come up at the height of the HIV/AIDS pandemic are being reharshed with new undertones and inflections. They include questions of global inequalities and their impact on public health in developing countries, the challenges of public healthcare provision and problems of social welfare and social security systems in developing countries and the intricacies of intra and inter-state relations in the face of healthcare challenges. Salutory efforts have been made by social scientists to encourage an approach to dealing with EVD that goes beyond a purely medical approach to raise questions of culture, economics and politics. These have led to interesting questions about the impact of histories of governmentality on epidemic control, the economics and politics of care and the social meanings of illhealth and wellness among others.

Through its conference on the theme ‘Public health governance in Africa’CODESRIA wishes to seize on opportunities for debate presented by the ongoing EVD epidemic to rekindle wider conversations about public health governance in Africa. While acknowledging the biological dimension of diseases and the systems that are (supposed to be) put in place to deal with them at a societal level, this conference will deliberately seek to insert conversations about these in broader discussions concerning economics, politics, culture and spirituality.

CODESRIA invites abstracts on the following themes from scholars and practitioners that are interested in participating in this conference:

· Global inequalities and public health delivery in African countries

· Histories of governance and public health systems in Africa

· African state evolution, structural adjustment programs and public health provision in Africa

· Public health governance and broader social policy regimes in Africa

· The social and cultural meaning of illness and good health

· The performance and representation of illness, good health, care and empathy

· The ethics, politics and economics of caregiving and biomedical research

· Epidemic control, popular culture and the arts

· Patents (property rights) and human rights in regimes of care

· Identity politics, integration efforts and processes of othering in the face of public health challenges

· The gendered dimensions of epidemics, epidemic control and public health governance in Africa

Those interested in participating in the conference, which will be held in Windhoek, Namibia onNovember 19-20, 2015 are invited to send their abstracts and CVs with full contact details including email addresses and phone numbers to CODESRIA not later than May 31, 2015. Authors of abstracts selected should be ready to submit full papers by 31st August 2015. All documents should be sent by email to [email protected] Please use the subject line ‘Governance Research Program’ when sending your email.

Governance Research Program
CODESRIA
BP 3304, CP 18524
Dakar, Senegal

Tel: +221 - 33 825 9822/23
Fax: +221- 33 824 1289
E-mail: [email protected]
Website: http://www.codesria.org

Hotuba ya Rais Mwinyi katika mkutano wa CHAUKIDU, MarekaniIfuatayo ni hotuba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipohutubia Mkutano wa 4 wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) uliofanyika tarehe 23 Aprili 2015 katika Chuo Kikuu cha Howard jijini Washington DC, nchini Marekani.

KARIBU


Wadau wa Kiswahili kwenye siku ya CHAUKIDU katika Chuo Kikuu cha HowardAsha Nyang.anyi akiwa kwenye meza akikagua majina ya wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya Chama Cha Ukuzaji Wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) inayoendelea sasa hizi chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC na Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi atakua mgeni rasmi.Wadau wa Kiswahili wakiendelea kuingia ukumbini.Wadau kutoka Zanzibar wakipata pichaWalimu wa kiswahili wa vyuo mbalimbali wakipata picha ya pamoja.wadau wa Kiswahili wakihudhuria sherehe ya CHAUKIDUWalimu na maporofesa wa vyuo wakiwa ndani ukumbi wa Blackburn Center siku ya Alhamisi April 23, 2015 chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.Wadau wa Kiswahili wakibadilishana mawili matatu.

Rais wa CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo kikuu cha Howard Washington, DC katika sherehe ya chama cha ukuzaji wa Kiswahili Duniani siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof Venessa White JacksonRais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtambulisha mkewe mama Sitti Mwinyi kwa mwenyeji wao Prof Lioba Moshi pia na yeye akimtambulisha mama Sitti Mwinyi kwa Prof Venessa White Jackson kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula. Prof Lioba Moshi Rais CHAUKIDU akielezea historia fupi ya CHAUKIDU na baadae kumkaribisha Rais mstaafu kuongea na wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya chama hicho iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015 katika chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.Ms Mamburi Lyambaya (kushoto) akimtambulisha Prof Venessa White Jackon na yeye kuwasalimia wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya CHAUKIDU iliyofanyika katika chuo kikuu cha Howard Washington, DC.Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa meza kuu kulia ni prof Venessa White Jackson 'Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba kwa kuwashukuru CHAUKIDU kwa kummpa mwaliko na kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa lugha ya Kiswahili hakusita kukubali kuja kujumuika nao pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliwapongeza kwa kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Afrika Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na mama Sitti Mwinyi wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.Wanafunzi wa chuo kikuu cha Howard wakiimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi mkubwa kuliko wastajabisha Watanzania na wadau wengine wa Kiswahili.Wadau wa Kiswahili wakifuatilia sherehe ya CHAUKIDU

How to spot a counterfeit US $ bill

Umati wafurika Itilima kumsikiliza Mbowe kuhusu "Ulinzi wa Kura"


Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kijijini Lagangabili jimbo la Itilima mkoani Simiyu jioni ya jana (Aprili 23, 2015) wakati wa uzinduzi wa FTP 200 ambao ni mpango wa ulinzi wa kura.
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Itilima katika Mkutano wa hadhara ulifanyika katika viwanja vya Lagangabili katika Makao Makuu ya ya Wilaya • via Malunde1 blog

Kanali Simbakalia ateuliwa Mwenyekiti COSTECH

Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia.
Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BARAZA LA TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikiwete, amemteua Mhandisi, Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Aprili 2015.

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Kifungu Na. 4 cha Sheria Na. 7 ya Mwaka 1986 iliyounda Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia. Mhandisi Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA).

Imetolewa na:

John Mngodo
KAIMU KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Various job opportunities at SUA

SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE 

MOROGOROJOB OPPORTUNITIES

ADVERTISEMENT

The Management of Sokoine University of Agriculture (SUA) invites suitable qualified Tanzanians to apply for positions of Tutorial Assistants (TA’s) (<35 yrs of age) and Assistant Lecturers (<45 years). Applicants are advised to note that the minimum GPA of 3.8 or an average of B for unclassified degrees such as that of Veterinary and Medical graduates at undergraduate level applies for TA’s and 3.5 at BSc/BA level or equivalent (i.e. an average of B for Veterinary and Medical graduates) and a good Master degree is applicable for those with postgraduate qualifications. Only registered Veterinarians will be considered for interviews.

Applicants are advised to note that salary packages and fringe benefits shall be as per Treasury Registrar’s Circular No. 2 of 2014, which is applicable at the moment.

The deadline for submission of application letters indicating names and addresses of three referees, together with certified copies of certificates and transcripts, curriculum vitae and testimonials shall be two weeks after the date of the first advertisement. Only short listed applicants will be contacted for interview. Those who had applied for similar posts in the past are encouraged to re - apply. Application letters should be sent to the undersigned.

A. TUTORIAL ASSISTANT (6 POSITIONS)

1. DEPARTMENT OF SOIL SCIENCE


Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Soil Survey/ Pedology/ Land Evaluation for applicants in possession of a BSc in Soil Science/Agronomy/Agriculture General/Horticulture. Applicants should have a very good pass of grades “A” or “B+” in either Soil Classification and Land Resource Inventory or Agricultural Land Use Planning. Qualifications in Remote Sensing & Geographic Information System (GIS) and Principles of Land Use Planning (including Land Evaluation) will be an added advantage.

2. DEPARTMENT OF ANIMAL SCIENCE AND PRODUCTION

Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Dairy Science for applicants in possession of a BSc. in Animal Science with a score of at least B+ in Dairy Cattle Management and Milk Processing courses.

3. DEPARTMENT OF CROP SCIENCE AND PRODUCTION

Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Botany for applicants in possession of a BSc. in Botany/ Agriculture General/ Horticulture/ Agronomy/ Forestry.

4. DEPARTMENT OF INFORMATICS

Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Artificial Intelligence for candidates in possession of a BSc. in Informatics/Information Systems/ Information Technology/Computer Science / Computer Engineering and Information Technology and related fields. The candidate must demonstrate adequate coverage of the relevant courses for each specialty.

Competence in computer programming in low-level and high-level programming languages is a compulsory requirement. A post graduate research experience in the same field and/or good working experience in academic and/or research institution will be an added advantage.

5. DEPARTMENT OF VETERINARY SURGERY AND THERIOGENOLOGY

Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Veterinary Theriogenology for applicants in possession of a BVM/BVSc from a recognised Institution with an overall minimum average of “B” grade or higher at Bachelor level.

6. DEPARTMENT OF VETERINARY PATHOLOGY

Tutorial Assistant (1 Post) for applicants in possession of a BVM/BVSc degree from a recognised Institution. The applicant must have an overall minimum score of “B” or above for all subjects. In addition must have an average of “B” or above in Veterinary Pathology courses.

B. ASSISTANT LECTURERS/ LIBRARIAN (12 POSITIONS)

1. DEPARTMENT OF AGRICULTURAL ENGINEERING AND LAND PLANNING

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Farm Machinery and Mechanization for applicants in possession of a BSc in Electro – Mechanical Engineering/ Mechanical Engineering/Agricultural Engineering or related field and a MSc in the areas related to Farm Machinery and Mechanization/ Agricultural Engineering/ Mechanical Engineering. Those working in the industry are encouraged to apply.

2. DEPARTMENT OF AGRICULTURAL ECONOMICS AND AGRIBUSINESS

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Business Management for applicants in possession of a Bachelors degree in business related disciplines including Agribusiness/ Marketing/ Finance/ Accounting/ Human Resource Management/ Business Management; and a Masters degree in Business and Management related disciplines majoring in Human Resource Management/International Business Management/ Banking and Finance/ Accounting and Finance/ Entrepreneurship.

3. DEPARTMENT OF FOREST MENSURATION AND MANAGEMENT

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Forest Resource Assessment in the fields of Forest Mensuration, GIS and Remote Sensing for applicants in possession of a BSc Forestry and MSc. in Forestry Mensuration and Management/ Forestry Resource Assessment and Management and/or related field.

4. DEPARTMENT OF BIOMETRY AND MATHEMATICS

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Complex and/or Functional Analysis for applicants in possession of a BSc and MSc. degree in Mathematics or related fields with a score of at least B+ in the discipline of Complex and/or Functional Analysis.

5. DEPARTMENT OF WILDLIFE MANAGEMENT

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Foreign Languages (English, French and Spanish) for applicants in possession of a BA and a MA specializing in either of the two languages English, French or Spanish languages.

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Food and Beverages Management for applicants in possession of Bachelor and Master degree in Hotel Management or related fields.

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Law for applicants in possession of a LLB and LLM majoring in Tourism, Business or other related disciplines.

Assistant Lecturer (1Post) in the discipline of Information and Communication Technology for applicants in possession of a Bachelor and Master degree in Computer Engineering/ Information Technology / Computer Science/ Information Systems/ Informatics or related fields.

6. DEPARTMENT OF VETERINARY MICROBIOLOGY AND PARASITOLOGY

Assistant Lecturer (1 Posts) in the discipline of Veterinary Microbiology for applicants in possession of a BVM/BVSc degree and MSc in Veterinary Microbiology from a recognised Institution and who has an overall of “B” grade or above for BVM and should in addition have scored “B” grade or above in Veterinary Microbiology at Undergraduate.

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Veterinary Immunology for applicants in possession of a BVM degree and MVM/MVSc/MSc in Veterinary Immunology from a recognised Institution and who have an overall “B” grade or higher at Bachelor degree and should in addition have scored “B” grade or above in Immunology.

Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Veterinary Parasitology for applicants in possession of a BVM degree and MVM/MVSc/MSc in Veterinary Parasitology from a recognised Institution and who have an overall “B” grade or higher at Bachelor degree and should in addition have scored “B” grade or above in Parasitology. Working experience of at least three years in the same or related field will be an added advantage.

7. SOKOINE NATIONAL AGRICULTURAL LIBRARY
Assistant Librarian (1 Post) for applicants in possession of a Bachelor degree in any field and a Master degree in Librarianship/ Information Studies/ Information Science/ Information and Communication Technology/ Information Technology. The knowledge of cataloguing and classification will be an added advantage.

Please Note:-

 • Only shortlisted candidates will be contact through their addresses/ e-mail and/or telephone.
 • Those who applied previously are encouraged to apply.
 • Those working in the Public Service are advised to route their applications through their current employers.
 • During application the applicant should state the Department, Position and Discipline one is vying for.

Issued by

Office of the Deputy Vice-Chancellor (A & F)
Sokoine University of Agriculture
P. Box 3000, Chuo Kikuu,
MOROGORO - TANZANIA

Yericko Nyerere: Watu wakweli wana nafasi gani Tanzania?

Historia ndiyo Darubini kali iliyomwibua mmoja wa Wanafalsafa wakubwa Ugiriki, ambaye anaweza kutwambia nini maana ya Ukweli na watu wakweli wa wananafasi gani Tanzania na Duniani?

Aristotle wa Athens aliyeishi kati ya mwaka 384 hadi 322 BC. Alipata kusema: “Truth is agreement with FACTS and REALITY” , tafsiri yangu ni kwamba, ukweli ni mwafaka baina ya habari ya kilichotukia na usahihi ama uhalisia wa mambo.

Kulingana na Aristotle, ukweli huweza kuongopa ikiwa UKWELI nusu-nusu unapowaongoza watu kwenye UONGO. Aristotle alisema hivi:

“To say what is that is not or of what is not that is-is FALSE, while to say what of what is that it is, and what is not that is not-is TRUE!!

Tafsiri yangu isiyo rasmi ni kwamba Aristotle alisema kusema jambo kwa namna isivyokuwa namna kitu kilivyokuwa hakika,ni UONGO;wakati kusema kitu kilivyo hakika na ukasema kwamba hakiko hivyo wakati hakiko hivyo huo ni Ukweli.

Aristotle, hutwambia kuhusu UONGO WA UKWELI(The lie of Truth) ambao mfano wake ni kama kudondosha tone la ukweli katika pipa la Uongo.Ukweli hauchanganywi na uongo ukabaki ukweli.Sumu kidogo ya panya haichanganywi na unga au mkate,kikabaki kuwa chakula bali sumu! Chakula jumlisha sumu ni sumu,basi.

Naam, ‘a little truth drop in the bucket’ matokeo yake ni jamii kuamini uongo na kuufanyia kazi, ndivyo ilivyo hata hapa Tanzania.Jamii hufanyia kazi umbeya,uongo na upumbavu tu! Watu wengi hata hapa Tanzania hudanganywa kwa ukweli kidogo ndani ya uongo mwingi,na tayari wameathiriwa na sumu ya uongo na umbeya,mishipa yao ya fahamu imedhoofishwa na majungu na uvumi.

Huwa naamini kwamba, Daktari akisema ‘Unaumwa Ukimwi’ ni FACTS-ni ukweli dhahiri. Lakini mpigadebe akisema kwakuwa una kikohozi na kichomi na umekonda-ni ‘Opinion’ ni maoni tu-maoni siyo ukweli halisi,ni kukisia na umbeya tu.Angalia sasa nchi hii walivyo hawatofautishi Opinion na Facts!Ukweli haufahamiki kwa kusemwa na watu wengi ama kwa njia ya sanduku la kura!

Mwandishi, Derek J.Morris aliandika katika Jarida la MINISTRY la Juni mwaka huu 2013, kama ifuatavyo:

“TRUTH is not determined by opinion poll or popular vote!”

Ukweli hauamuliwi kwa wingi wa kura za maoni za watu wengi vijiweni! UKWELI huweza kusemwa na mtu mmoja mwenye taaluma kama daktari kusema ‘una ukimwi’ ndugu zako na jamaa wote wakashikilia umerogwa!

Ukweli hauamuliwi kwa sauti kubwa na maandamano ya vibaka na wanasiasa wakasema ndiyo NGUVU YA UMMA!

Aristotle amesema watu wengi huchelea kusema ukweli wasije wakachukiwa na umma mkubwa, ‘PEOPLES POWER’.

Watu wengi siyo wa kuamini,na mawazo yao siyo ya kufanyia kazi mara zote,wapo wafuata mkumbo tu, mashabiki na mabingwa wa kuigiza kila jambo na kuangamiza jambii kama tunavyoona leo madawa ya kulevya, bangi na ndoa za jinsia moja!

Bendera kufuata upepo tu! Kizazi hiki kimepotoka mno,kwa kuiga ya Magharibi ya watu wengi, sasa wachache hawana cha kusema,wataalam kama madaktari, wahandisi,maprofesa n.k ushauri wao ulishakataliwa na public opinion.

Siku hizi ‘wengi wape’ japo wapumbavu sana!

Watu wengi, aghalabu mbumbumbu mzungu wa reli fuata mkumbo, propaganda za siasa huishia kuipotosha jamii na kizazi hiki kwamba ndiyo haki za Binadamu.Haki za Mashoga,haki za wasagaji,haki za watoto kutochapwa viboko n.k

Watu wachache wenye haki aghalabu hawana ubavu wa kutetea ukweli usiochanganywa na uongo,umbeya,hisia tu na majungu.


Wakristo wameonywa sana kuwa waangalifu katika kuamua kati ya UKWELI (right) na uongo (wrong) kwa kufuata kura za maoni za wajinga wengi (opinion poll) ama kura za watu wengi wanaopenda uhalifu na uovu(popular vote).

Kuna watu hawataki hata sheria ziwepo ili waingie mitaani na kupora mali za wenzao kwa kisingizio, Maisha ni Magumu!

Wachache wenye hekima wanajua matokeo ya kukosekana kwa sheria,lakini wapumbavu wengi watalaani kuwepo sheria, mahakama, polisi, mgambo, mahakimu n.k hawa wote ni vibaka akilini.

Ukweli na uongo,sharti kuamuliwa kwa muktadha wa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu(Biblia n.k)Kwa mfano Zaburi 119:105 HUSEMA Neno la Mungu ni Taa iongozayo miguu ya wenye haki.

Watu wanasema Mungu alishakufa, hayupo na neno lake ni batili, sasa hawa wanakwenda njia gani halafu uwafuate gizani?

Watu wanapotaka kwenda upande wa kweli wa Historia,wanapaswa kugeukia hekima ya Mungu tu basi. Hekima ya Mungu ni ukweli, haki, amani, upendo n.k

Biblia, kwa mfano husema njia ni nyembamba sana iendayo kwenye ukweli nao wanaoona ukweli ni wachache tu.Wengi huenda kwenye uongo,maana njia ya uongo ni pana hata mbumbumbu huiona.

Njia ya haki huonwa na wenye hekima,ni nyembamba hutazamwa kwa hadubini kali.

Ni kwa sababu hii,watu shupavu wanaotetea ukweli (rejea tafsiri ya ukweli) hawapendwi na wengi;huishia kutengwa, kusulubiwa.

Kusema kwamba kitu hiki hakiko hivyo wakati kweli hakiko hivyo ni hatari,unafanywa kama Nabii Yeremia,Martin Luther King Jr, Martin Luther wa Ujerumani, Socrates, Yohana Mbatizaji, orodha ndefu.

Katika kitabu cha Luka Mtakatifu 3:11-14 Yohana Mbatizaji anapokemea rushwa,ufisadi miongoni mwa maofisa wa serikali fisadi, anapokataza masikini kuporwa wake na mali zao, anaishiwa kunyongwa kijinga.

Nani atatetea kichwa ili akatwe kichwa?

Marko Mtakatifu 6: 17 na 18 hutwambia kwamba ni mtu labda mmoja tu anayekubali ukweli usemwe potelea mbali apoteze maisha yake,kuliko kuacha wajinga wengi waseme uongo na kuufurahia.

Public Opinion, mara nyingi hukinzana na ukweli na uhalisia wa mambo-husema minyoo huletwa na wachawi,na wala siyo uchafu na kula bila kunawa ama kunywa maji yasiyo chemshwa!

Ukisema ukweli utaitwa msaliti! Kuna mifano tele katika Biblia,niiache wengine wananiambia hataki kusoma biblia. Biblia ni kitabu, hawapendi kusoma ila kucheza na kucheka-cheka tu.

Nimesema kwamba ukweli huonwa na wachache tu na husimamiwa na watu shupavu wawili ama watatu tu-wengine bendera kufuata upepo unakoelekea, watu wengi wanafiki tu.

Wanaosema ukweli huitwa waongo na waongo huitwa wakweli.Mara nyingi waongo huenda kinyume cha Historia-The wrong side of history.

Historia inamsema Socrates (469-400 BC) ALIVYOULIWA na utawala wa Athens kwa kukataa umbeya kwamba kuna miungu 391 inatawala juu ya Mlima Olympus!

Walimpa sumu ainywe kwa kutetea kwamba kuna Mungu mmoja na huishi mbinguni tu. Yesu aligoma kufuata dini ya ukandamizi ya Kiyahudi, Martin Luther aligomea mafundisho ya Kipapa, Martin Luther King Jr. ambaye juzi Ndoto yake( (I Have A Dream) ilisherehekewa miaka 50 na akina Obama, aliuliwa Aprili 1968 kwa kusisitiza ukweli kuhusu ubaguzi wa rangi Marekani, aliuliwa na Pentagon kwa kutetea ukweli.

Wapo akina Mandela wamesota rumande miaka 27, wapo wengine walifukuzwa kazi n.k

Katika mfululizo wa tafakuri zangu nikiwa shambani kwangu Mbutu, nitatilia shaka kila kinachoitwa UKWELI ili kunifanya kuchunguza mambo kwa akili tunduizi(critical mind) kuacha mikumbo na umbeya wa siasa za kipumbavu zinazoleta ugomvi katika jamii hii na ukiwa na ukame wa fikra mpya.

Nitaangaza ‘fuata mkumbo’ iliyoleta shida hapa Tanzania, katika Nyanja tofauti siyo siasa tu hata dini zilizoletwa kwa majahazi zinazoshadidiwa na watu na kuacha dini zao za asili za kiafrika.

Nimetumia nukuu za wanafalsafa,wasomi,wataalam lengo ni kukiokoa kizazi hiki na kuiga na kufuata mkumbo wa kila kinachosemwa ili tuepuke propaganda,matangazo ya uongo redioni kwenye tv na maamuzi ya wengi katika kura za maoni (opinion polls)

Ninatilia shaka hata hoja itakayoamuliwa na wengi katika katika marafiki zangu JF, Twitter, FB na kwenye makundi haya ya WhatsApp, lakini vipofu wakaacha hoja ya wachache ama mmoja mwenye hekima, mtu wa haki mnyoofu.

 • Yericko Nyerere

OnePlus One is celebrating a year today with some discounts

OnePlus in celebrating one year since the One was announced, it is:-

 1. Cutting its price by $1.00 (or one unit in your local currency), as a symbolic gesture
 2. Knocking 50% off all t-shirts and select accessories on oneplus.net
 3. Inviting fans to join the #NeverSettle Party for a chance to win free t-shirts
 4. Giving their biggest prize to date: four lucky winners will each receive a special bundle of the One in Sandstone Black or Silk White and a matching Power Bank. Why four, exactly? It’s “one” plus “one” of each color! 

See more at oneplus.net blog

Chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini: Wamalawi 390 waondoka; Seneti ya Nigeria yaomba mfalme wa Kizulu afikishwe ICC

Nchini Afrika Kusini kumetokea ghasia na purukushani dhidi ya raia wa kigeni ambapo huvamiwa na kuendeshewa kipigo hadi kufariki. Makundi ya raia huvamia maduka ya wageni na kupora mali ziliomo. Baadhi ya wazawa hutuhumu wageni kuwa wanapora ajira zao, kufanya uhalifu na kuyapa gharama mashirika ya kiutu nchini mwao.

Ghasia hizo zilisababisha mamia ya raia wakigeni kuondoka.

Hivi majuzi, raia 390 wa Malawi walioponea chupuchupu mashambulizi hayo walipokelewa kwa vilio walipowasili mjini Blantyre. Mabasi 6 ya abiria yanaarifiwa kuwasili mjini humo na raia 390, miongoni mwao wakiwa wanaume na wanawake wa kati ya umri wa miaka 18 – 30 na wazazi wenye watoto wachanga.

Waziri wa Mawasiliano wa Malawi Kondwani Nankhumwa alisema, ‘Tumefurahia kuona raia wetu wako salama. Raia wengine zaidi watawasili nchini siku baadaye.’ Waziri huyo alijumuika na ndugu na jamaa wa karibu wa raia hao ili kuwapokea katika uwanja wa kitaifa wa Blantyre.

Baada ya kuwasili salama salmini nchini Malawi, raia waliokuwa na majeraha walifikishwa katika hospitali ya Queen Elizabeth Central (QECH).

Nako nchini Nigeria, Baraza la seneti nchini humo limomba mfalme wa Kizulu afikishwe katika mahakama ya jinai ya Kimataifa (ICC) iliyopo The Hague, Uholanzi kutokana na mashambulizi yalionendeshwa dhidi ya raia wa kigeni waliopo nchini Afrika kusini na kusababisha vifo vya watu saba.

Mfalme wa Kizulu, Goodwill Zwelithini amekana kuwa kauli yake ndiyo sababu ya raia wa kigeni kushambuliwa hadi kuuawa nchini humo wiki mbili zilizopita.

Kabila la Wazulu ni kabila kubwa nchini Afrika kusini ambapo linakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 11 na huwa wakitekeleza na kuheshimu maombi hutoka kwa Mfalme wao.
David Mark, msemaji wa Seneti nchini Nigeria alifahamisha kuwa unyama wanaoendeshewa raia wakigeni nchini Afrika Kusini ni jambo lisilokubalika hata kidogo na kuomba mfalme Goodwill afikishwe mahakamani.

Msemaji huyo alifahamisha kuwa haiwezekani kamwe kwa kiongozi kusimama katika hadhara nakusema kuwa raia wa kigeni wanapaswa kuondoka, matamshi haya yamechochea chuki na ni jambo lisilokubalika. Alisema Afrika Kusini inapaswa kuwafunza raia wake historia na kukumbuka msaada wa Nigeria kwa Afrika kusini katika kipindi cha ubaguzi wa rangi "apartheid".

Cheka kidogo... Mume ataka kumsaidia mkewe...


Mume karudi nyumbani, akamuliza mkewe, nikusaidie nini? Mke akajibu, chukua huo mfuko, menya viazi nusu kisha uviinjike... ndivyo hivyo vinavyoonekana pichani.

Johns Hopkins undergrads win funding for bright new venture in Tanzania

In Tanzania for an internship last summer, Miguel Dias found himself spending a lot of time in smoke-filled rooms. Residents would often cook indoors using charcoal, and the smoke would saturate the small spaces. Not accustomed to it, "in just five minutes, I'd already feel faintish," said Dias, a Johns Hopkins University sophomore studying biomedical engineering.

Around the same time, Violet Ayoub, his internship director, told him about a relatively new innovation happening in Kenya—smokeless fuel briquettes made from agricultural waste. Several developing countries were experimenting with the briquettes as a cheaper, healthier, more environmentally friendly alternative to charcoal.

Using his engineering knowledge, Dias took his own approach to the technology, designing a new briquette-burning kiln model from an oil barrel. Ayoub let him set it up in extra space behind the headquarters of her NGO, Visions For Youth. With that, the two of them recognized a new venture in the making.

That venture, called Bright Energy Africa, now has recognition on a larger scale—and startup money to begin producing the briquettes. Last month, Dias and the team he recruited back at Hopkins—fellow Whiting School of Engineering sophomores Samantha "Yu" Wang and Yadel Okorie—were among the winners of the 2015 Social Venture Challenge at the Clinton Global Initiative University.

The competition received nearly 200 applications, and two dozen teams earned awards. The Hopkins team got $5,000 in seed funding, the highest amount awarded, along with ongoing networking and mentorship opportunities with industry leaders.The big picture for Bright Energy Africa is ambitious: an enterprise that could create hundreds of jobs in Tanzania, with micro-franchises of the briquette centers set up in rural communities. Ultimately, Bright Energy Africa could be "100 percent owner-controlled in Tanzania," Dias says.

The briquettes could help preserve the environment, reducing the deforestation required for creating charcoal and wood fuel and making use of discarded farm products that are currently just burned. The smokeless briquettes could also improve health, reducing carbon monoxide and other harmful byproducts of the current cooking methods. "It'd be a very big impact on their lives," Dias says.

When he returned to Baltimore at the end of last summer, Dias turned his focus to the business plan. Okorie, a mechanical engineering major, helped on the financial side, and Wang, an electrical engineering major, worked on marketing. From Tanzania, Ayoub contributed through email and Skype sessions.

For the next several months, the goal is to use the $5,000 in seed funds—which Dias says goes a long way in Tanzania—to get the pilot production plant up and running in Arusha. The team is also working on other fundraising angles and entering other competitions.

The Social Venture Challenge, hosted by the Resolution Project, is an international business plan competition for undergraduates that is designed to inspire solutions to pressing social issues. The Hopkins team received its award last month at the annual Clinton Global Initiative University conference, held at the University of Miami in Coral Gables, Florida.

Sophomores Yadel Okorie, Miguel Dias, and Samantha (Yu) Wang

Alexander Forbes eyes Ghana, Tanzania


SA’s largest retirement fund administrator, Alexander Forbes, has announced it is working on making an acquisition in Ghana within a year.

A successful deal in Ghana will expand Alexander Forbes’s footprint to seven African countries. The expansion would also be in line with the company’s plans to leverage off the pension reforms in countries such as Ghana and Tanzania.

"Tanzania is probably in the short to medium term. Ghana is more short term. The idea is to buy businesses that are small and leverage them with the brand (Alexander Forbes) and technology as well as the skills and grow that," Alexander Forbes Afrinet (rest of Africa network) MD Luendran Pillay said in an interview on Monday following the announcement of the company staff black economic empowerment deal.

Mr Pillay said the business Afrinet was acquiring in Ghana would potentially be in the employment space as well as consulting and actuarial space.

With a presence in Ghana there is an opportunity for Alexander Forbes to pursue business opportunities from its South African clients that do business in the West African country.

Mr Pillay said the company had done work in Ghana on a fly-in, fly-out basis, and that had given it an opportunity to test the market and the regulatory environment.

He added Alexander Forbes’s entry strategy in the rest of Africa was pension-fund reform in an Anglophone footprint.

It also involved leveraging off the existing infrastructure to support the African businesses.

Over the past three years about 10% of the company’s staff component in the rest of Africa received training in SA.

The staff training was important to embed the skills, technology, culture, risk and compliance measures that Alexander Forbes espoused.

As the company makes acquisitions it will also seek to grow the businesses organically.

As an example, Mr Pillay said the company was piloting the rollout of its retail client offering in countries such as Namibia, Botswana and Kenya.

Meanwhile, Alexander Forbes announced on Monday it was issuing 2.9% (about 39-million shares) of its issued share capital as part of an employee share-ownership plan aimed at promoting broad-based black economic empowerment.

Black women participants are expected to receive 70% of the distribution.


Uandikishaji wanaotaka kujiunga 'Tanzania Bloggers Network'

Uandikishaji Wanachama 'Tanzania Bloggers Network' (TBN), 22/04/2015

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama mhitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN.

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Kitabu 'The 7 Habits of Highly Effective People' kwa Kiswahili chazinduliwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.

UWEKEZAJI mkubwa unatakiwa kufanywa katika eneo la raslimali watu, kama taifa hili linahitaji kuondokana na malalamiko kuhusu maendeleo na ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu wakati akizindua tafsiri ya kiswahili ya kitabu cha “The 7 Habits of Highly Effective People” kilichoandikwa na Mmarekani, Stephen Covey.

Hii inakuwa tafsiri ya kwanza ya kitabu hiki kwa lugha za asili zinazotumika bara la Afrika .

Alisema malalamiko mengi kuhusiana na taifa kuwa na raslimali nyingi na umaskini kuendelea kuwepo yanatokana na kutoendelezwa kwa raslimali watu kwa lengo la watu kujitambua, kutambua wanachotaka na kusababisha kiwepo.

Alisema inasikitisha kuona kwamba watanzania wengi wanalalamika kuhusu hali ngumu kumbe ilhali wao huenda ndio wakawa sababu za matatizo hayo ya ukosefu wa maendeleo.

Alisema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika kwa kuwa vitabu hivyo vina tafiti nyingi za miaka mingi ambazo watanzania wakitumia kwa muda mfupi watafanya mabadiliko katika maisha yao.

Alisema uwapo kwa tafsiri ya Kiswahili kwa moja ya vitabu vyenye sifa kubwa duniani katika masuala ya menejimenti na ambacho kimekuwa katika 20 bora za vitabu duniani kwa miaka 20, kutasaidia watanzania wengi kujiangalia na kujifunza kuwa na dira na nidhamu ya kutekeleza yale ambayo wanayafikiria.

Alisema kwamba ari ya kusoma kazi mbalimbali kutasaidia watanzania kuwa na upeo mpana wa kujituma na kuwa na nidhamu ya malengo wanayostahili ya kufikia kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa.

Tafsiri hiyo ya kitabu ambayo imewezeshwa na Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) na imeandaliwa taasisi ya ushauri wa masuala ya maendeleo ya raslimali watu (NFT).

NFT ambayo makao makuu yake yapo mjini Kampala, Uganda ina matawi Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Wajibu wake mkubwa taasisi hiyo ni kukabilina na changamoto mbalimbali za wafanyakazi kwa kutoa mafunzo yenye kutengeneza manufaa kwao na kwa menejimenti ya uhuru na kutegemeana katika kufanikisha maono ya taasisi husika.

Kutumika kwa kitabu hicho chenye kurasa 380 kwa kuangalia tabia zenye manufaa kunatokana na haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi na ushirikishaji wenye lengo la kuchochea kutegemeana katika kuleta ufanisi.

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege.
Mwezeshaji wa Franklin Covey, Alice Levora akichambua kwa ufupi tabia 7 zilizomo kwenye kitabu hicho kwa wageni waalikuwa (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi rasmi.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia) na Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa (wa pili kushoto) pamoja na wadau wengine wakifuatilia uchambuzi wa kitabu hicho.Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wageni waalikwa.Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika.Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati wa kutafsiri kitabu hicho.Pichani ni kikundi cha burudani kutoka Tanzania House of Talent (THT) wakitumia sanaa "Choreograph" kuzindua rasmi kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Sasa kimezinduliwa rasmi.Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akipokea kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia). Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida MutasaMgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akionyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Vida Mutasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege, Mkurugenzi wa NFT Consult, Nambie Kiwanuka pamoja na Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong.Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania.Mratibu wa shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People"kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kutoka JB's PR & Events, Babbie Kabae akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani).Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni maafisa rasilimali watu na wadau kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.


 • Taarifa hii tumeshirikishwa na Zainul Mzige/Modewjiblog.