Cheka kidogo: Teja na Babu...

MZEE: Kijana wangu unaweza kunielekeza mtaa wa Kiyungi?

TEJA: Dah babu sijawahi kuusikia mtaa huo

Baada ya dakika chache yule Teja akaanza kumuita yule babu aliyekuwa kaenda mbali kidogo na babu wa watu akajikongoja akarudi...

TEJA: Babu nimemuuliza rafiki yangu kama anaujua mtaa wa Kiyungi

BABU: Asante sana kijana wangu, nashukuru sana kwa msaada, anasema uko wapi?

TEJA: Hata yeye anasema hajawahi kuusikia.

Leo kuna BBQ na mechi ya Muungano huko MD
Mechi ya Muungano itachezwa Jumamosi Aprili 25, 2015 kati ya timu ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani chini ya udhamini wake People's Bank of Zanzibar (PBZ), wadhamini mechi hii tangu mwaka jana.

Mechi inatarajiwa kuanza saa 12 jioni na kutakuwa na BBQ kuanzia saa nane mchana. Timu zote zipo kwenye mazoezi makali zikijiwinda na mpambano huo.

Anuani ya uwanja ni 8001 Walker Mill Road, District Heights, MD, 20747.Jukwaa la watazamaji

Shule na intaneti, Serikali kuzifuta kampuni zisizofikisha mawasiliano vijijini

Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa

MIKAKATI ya serikali ya kutoa wataalamu wengi wa sayansi imeendelea kutetekelezwa kwa kasi, ambapo imetia saini mikataba kusambaza huduma za mtandao kwenye shule mbalimbali nchini.

Mikataba hiyo iliyotiwa saini jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, iko miwili ya kupeleka huduma za mawasiliano vijijini na kuunganisha mtandao wa intaneti katika shule utakaogharimu sh. bilioni 26.28.

Katika mikataba hiyo, serikali imeonya kuwa itazifuta kampuni ambazo zitashindwa kutekeleza makubaliano ya kufikisha mawasiliano kwa wakati katika vijiji 480 vilivyoainishwa.

Onyo hilo la serikali linatokana na kampuni hizo kushindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba wa kupeleka huduma za mawasiliano vijijini, ambapo nyingi zimetekeleza kwa asilimia 50 tu.

Akizungumza wakati wa kutia saini mikataba hiyo, Profesa Mbarawa alisema awamu ya tatu ya kupeleka mawasiliano vijijini utahusisha kata 102 ambapo vijiji 480 vitanufaika nayo.

Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ulihusisha kata 52, ambao ulitekelezwa mwaka 2013 na umekamilika kwa asilimia 99.05 na awamu ya pili ilihusisha kata 86 na ulitakiwa kukamilika mwaka jana na hadi sasa umetekelezwa kwa asilimia 50.

“Awamu ya kwanza kuna kata nne kati ya 52 ambazo bado hazijamazilizika, jambo ambalo halikubaliki na kama mtu ameshindwa kutekeleza mkataba wake afungiwe na katika hili sitakubali,” alisema.

Mkataba wa mradi huo ambao utahusisha kata 102 na kugharimu sh. bilioni 14.02 umesainiwa kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF) na kampuni za utoaji huduma za mawasiliano.

Kampuni zilizotia saini mkataba wa utoaji huduma ya mawasiliano kwa awamu ya tatu na idadi ya kata katika mabano ni Tigo (42), Vodacom (36), TTCL (19) na Airtel (5).

Alisema bado kuna changamoto kubwa ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini, hivyo kuzitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatekeleza mikataba ili kila mwananchi apate huduma popote alipo.

Waziri huyo alisema katika kuhakikisha huduma ya mawasiliano inawafikia wananchi wote, serikali ilianzisha utoaji wa ruzuku kwa kampuni zinazotoa husika ili kupeleka mawasiliano kwenye maeneo yenye uchumi hafifu.

Alisema serikali kupitia UCAF itatoa ruzuku ya asilimia 100 ambayo inatolewa kulingana na eneo yakiwemo maeneo ya mipakani ambayo ni lazima yawe na mawasiliano wakati wote ili kuimarisha ulinzi na usalama.

Alisema UCAF ilianzishwa mwaka 2006 ambapo hadi mwaka 2010 anaingia katika wizara hiyo hakukuwa na kazi yoyote iliyotekelezwa ambapo alilazimika kubadilisha uongozi jambo ambalo limeleta mafanikio na sasa mawasiliano yanaendelea kufika kwa wananchi.

“Ni mafanikio makubwa yaliyopatikana itakuwa kichekesho kwa waziri atakayekuja ashindwe kufanya vizuri zaidi, na akishindwa kuna tatizo kwa sababu sasa teknolojia imebadilika,” alisema.

Awali, Mtendaji Mkuu wa UCAF, Mhandisi Peter Ulanga, alisema mbali na kutia saini mkataba na kamapuni za mawasiliano, pia waliingia mkataba na kamapuni ya Avanti inayotoa huduma za mtandao wa intaneti kwa ajili ya kuziunganishia shule 250 za serikali. 

Pia alisema wataanzisha vituo 25 vya kufundishia walimu wa masomo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, mradi unaotarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya UCAF, Profesa John Nkoma, aliwaomba wananchi wabadilike na kutumia huduma ya intaneti kwa faida na si vinginevyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. John Mngodo, alisema huduma ya kuunganisha intaneti katika shule za serikali itasaidia kuboresha elimu.

  • KHADIJA MUSSA via gazeti la UHURU

[video] Kauli ya NEC kuhusu tetesi za Kura ya Maoni kufanyika pamoja na Uchaguzi Mkuu

[video] Kauli ya NEC kuhusu tuhuma za kuandikisha wapiga kura kwa kuanza kwenye ngome za CCM

[video] Kauli ya Mbowe kwa IGP na Msajili wa Vyama vya SiasaINSPEKTA Generali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu amepiga marufuku vikundi vya ulinzi vya vyama vya siasa ambavyo vina muonekano na muundo wa vyombo vya usalama, kwani ni kinyume cha katiba na sheria ya nchi.

Vilevile, amevitaka vyama hivyo kuhakikisha vinafuata muongozo uliotolewa na Ofisi ya Msajili wa vyama hivyo na kama vikienda kinyume jeshi litapambana navyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi uliokuwa ukijadili namna ya kuondoa vikundi hivyo au namna ya kuboresha shughuli za uendeshwaji wa vikundi hivyo.

Alisema wamejadiliana na vyama hivyo na kwamba ofisi ya msajili imetoa muongozo ambao wanatakiwa kufuata katika kutekeleza ili waweze kufanya kazi zao kwa utaratibu unaotakiwa.

IGP Mangu alisema Katiba na sheria za nchi haziruhusu vikundi hivyo kuwepo, kwani jukumu la kulinda raia na mali zao ni la Jeshi la Polisi, hivyo vinaingilia kazi ya jeshi hilo.

“Katika mkutano huu tumekubaliana kuwa vyama vinatakiwa kufuata muongozo kutoka Ofisi ya Msajili na kama watashindwa kufanya hivyo basi sisi jeshi tuko tayari kupambana nao,”alisema IGP Mangu.

Mangu alisema mkutano huo utawasaidia kupata uelewa pole pole lakini kinachotakiwa hadi kufikia wakati wa uchaguzi mkuu vikundi vyote visiwepo.

Alisema suala la chama kuwa vikundi vya vijana vyenye misingi ambayo haivunji Katiba ya nchi ni sahihi lakini kinyume cha hapo hawezi kuvumilia hali hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mziray alisema kuna vyama ambavyo vimekuwa na vikundi vya ulinzi na kuvitaja kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF).

Mziray alisema historia inaonesha kuwa vikundi hivyo vilikuwa wakati wa chama kimoja hivyo kinachoonekana sasa ni vikundi hivyo kufanya kazi ya Polisi jambo ambalo ni kinyume cha taratibu, sheria za nchi na katiba.

Alisema uwepo wa vikundi hivyo ni kinyume cha sheria hivyo katika mkutano huo wanajaribu kuviangalia kama undeshwaji wa vikundi hivyo kama ni sahihi au si sahihi.

“Unajua vikundi hivi vipo miaka mingi tatizo ni wakati huu vinaonekana kuwa na mitizamo tofauti jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi,” alisema Mziray.

Mziray alisema vyama vya siasa vinatakiwa kufuata mapendekezo yaliyotolewa kama wakishindwa jeshi litashughulika nalo.

Mbali na hayo, alisema katika mkutano huo vyama viwili ambavyo ni Chadema na CUF havikuhudhuria lakini ujumbe utawafikia na watatakiwa kutekeleza.

Aidha, Mziray alilitaka Jeshi la Polisi kusimamia misingi ya sheria katika utekelezaji wa majukumu yake kwani kinyume cha hapo ndipo migogoro inabuka kila kukicha.

Mziray alisema kitendo cha katiba za vyama vyao kubainisha vikundi hivyo na msajili kuvikubalia isiwe ni sababu ya kuruhusu migongano hiyo. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ally Vuai alisema wao hawana vikundi vya ulinzi ndani ya chama.

Alisema kuwa vijana wao hawawaandai kijeshi ila kuwa vijana bora kiitikadi na kuwa na mwamko wa kujua siasa.

“Sisi hatuwafundishi kuwa magaidi ila tunawafundisha kuwa vijana bora ila kuna muonekano wa mavazi ambao jeshi wakiona wanaweza kutia shaka, lakini kama tatizo ndiyo hilo tunaweza kurekebisha,” alisema Vuai.

Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliwataka viongozi wa vyama kusoma sheria za nchi na kuzielewa ili wasizivunje kwa kisingizio cha kujilinda.

Mutungi alisema ofisi yake itahakikisha inawapatia elimu viongozi wa vyama ili kuhakikisha wanatambua mipaka yao ya kisheria katika kuunda vikundi hivyo.

Msajili huyo alisema ni jukumu la vyama na Jeshi la Polisi kujipanga na kukaa pamoja ili waweze kufikia muafaka kuhusu changamoto ambazo zinawakuta na si kuingia kwenye migongano.

“Unajua kinachotokea hapa ni kukosekana kwa uaminifu katika pande hizi mbili lakini wakati wa kutambua kuwa katiba na sheria za nchi zinataka nini ni huu ili kuepuka migogoro,” alisema.
CUF yanena

Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya, alisema hawawezi kufuta kikundi chao cha ulinzi (Blue Brigade) kwani kinatumika kulinda ulinzi wa mali za chama na viongozi wake.

“Polisi wenyewe wanalalamika hawatoshi kutoa ulinzi kwa wananchi wote, lakini pia sisi kama CUF hatuwezi kuacha kutoa ulinzi mathalan kwa mwenyekiti wetu, Profesa Ibrahim Lipumba. Na hili limo kwenye katiba yetu.

“Kikundi hiki hakipo kupambana na watu, na kama kuna mahali kimefanya kosa kichukuliwe hatua…kwanza uamuzi uliofikiwa ni wa kidikteta kwani hatujashirikishwa,” alisema Kambaya.
CHADEMA.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema kikundi chake cha ulinzi cha Red Brigade kitaendelea kuwepo hadi pale haki itakapotendeka.

Alisema lengo la kikundi chao cha ulinzi ni kulinda viongozi, mali za chama na wanachama wao katika mikutano kwani Jeshi la Polisi limeshindwa kuwajali CHADEMA na kuegemea upande wa CCM.

Mbowe aliongeza inaonekana hiyo ni hofu ya uchaguzi mkuu hasa kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka jana, upinzani umeshinda maeneo mengi.

Alisema kuwa Jaji Mutungi ana uwezo wa kufuta vikundi hivyo kwa mamlaka aliyonayo, lakini hawezi kufuta yaliyoko moyoni kwa watu katika kujilinda.

“Haki ikitendeka katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa siasa za Tanzania, hakutakuwa na sababu ya kuwa na vikundi hivyo.

“Leo (jana), tumezindua mafunzo ya vijana wa CHADEMA yanayohusu ulinzi na usalama ambapo uzinduzi utaendelea kufanyika kila mahali,” alisema Mbowe na kuongeza kama polisi wamejitosheleza kwa nini kuna polisi jamii.

Mbowe alisema hawakuonekana kwenye kikao hicho kwa sababu ya majukumu mengine ya kichama nje ya Dar es Salaam.

  • via gazeti la Jamboleo