Msasani Tower kazi iliyofanywa na SUMA JKTKoplo Mhandisi Lazaro Masanja kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akitoa rai kwa wananchi na Taasisi kutumia Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (SUMAJKT) kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa gharama nafuu. Nyuma ni jengo la kitega uchumi cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ‘Msasani Tower’ lililopo Msasani jijini Dar es Salaam ambalo limejengwa na kampuni ya ujenzi ya JKT (NSCD).

--- Georgina Misama.

Mahojiano na Linda 'LB' Bezuidenhout - Pt II (mwisho)Karibu katika sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout

Ameeleza mengi kuhusu kazi yake na familia kwa ujumla.

Anavyokabiliana na kazi zake, changamoto za afanyalo, tuzo alizopata nk.

Na pia, kaeleza kuhusu mtazamo wake juu ya waTanzania (hasa wa Diaspora) na ushauri kwa kinamama wote

KARIBU

Taarifa ya kukamatwa wenye bendera ya CHADEMA na vifaa kadhaa

(picha via gazeti la MTANZANIA)

MNAMO TAREHE 24.04.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MTAA WA SOGEA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, VIJANA WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. MATHEW ANGANILE MWAFONGO @ RASI (27) MKAZI WA TUNDUMA NA MWENZAKE AITWAYE SALEHE TABULEI SICHALWE (22) MKAZI WA MAJENGO TUNDUMA WALIKAMATWA NA POLISI BAADA YA WANANCHI WA ENEO HILO KUWATILIA MASHAKA KUWA NI WAHALIFU, HII NI KUTOKANA NA MVAO WAO AMBAO ULIKUWA UMEFICHA SURA ZAO.

VIJANA HAO WALIKUWA WAKITUMIA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.855 CDQ AINA YA T-BETTER NA WALIKUWA NA BEGI MOJA AMBALO MMOJA WA VIJANA HAO ALIKUWA AMELIVAA MGONGONI.

POLISI WALIPOWAPEKUA KATIKA BEGI HILO WALIKUTA VISU VIWILI, MANATI MBILI, MAWE AROBAINI YA KURUSHWA KWA MANATI NA NATI NNE ZA KURUSHWA KWA MANATI, KOFIA MBILI ZA JESHI, BUTI JOZI MBILI, MIWANI MIKUBWA INAYOTUMIWA NA POLISI KATIKA MISAFARA, SHEEN-GUARD JOZI NNE (VIFAA MAALUM VYA KUVAA KWENYE MAGOTI NA VIWIKO VYA MIKONO), MAKOTI MAWILI MAREFU, VIFAA VYA KUFANYIA MAZOEZI YA “PUSH UP” NA KAMBA YA KUFANYIA MAZOEZI YA KURUKA.

AIDHA KATIKA BEGI HILO KULIKUTWA PIA T-SHIRT MOJA YA CHADEMA, BENDERA MBILI NDOGO ZA CHADEMA, KITAMBAA/KILEMBA KIMOJA NA BARUA TATU ZA KUWATAMBULISHA WATUHUMIWA KWENDA KUTOA MAFUNZO KWA RED BRIGADE HUKO MAENEO YA KATA YA CHITETE, MSANGANO NA KAMSAMBA WILAYANI MOMBA.

KATIKA KUHOJIWA, WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KUWA WANAENDA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WA RED BRIGADE KATIKA KATA HIZO TAJWA HAPO JUU. KUTOKANA NA MATISHIO TULIYONAYO YA USALAMA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU NCHINI, WATUHUMIWA HAO WALIFIKISHWA POLISI MKOA KWA MAHOJIANO ZAIDI NA BAADA YA UCHUNGUZI, JALADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAWASHUKURU WANANCHI KWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KIUSALAMA KWA KUTOA TAARIFA HARAKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA HARAKA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA PALE WANAPOTILIA MASHAKA MTU/WATU AU VITENDO VYA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE HARAKA IWEZEKANAVYO.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

[update] Brigedia Jenerali Hashim Mbita atangulia mbele ya haki


Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Aprili 28, 2015 - saa 10 Alasiri baada ya swala.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.

Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania, bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

  • via Michuzi blog


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
 STATE HOUSE,
 1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), Chama cha TANU na Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Africa – Liberation Committee of the African National Unity (OAU), Brigedia Hashim Mbita, kiongozi ambaye Rais Kikwete amemwelezea kama mmoja wa viongozi ambao wameifanyia nchi yetu mengi na kwa miaka mingi.

Rais Kikwete ambaye amepokea taarifa za msiba huo mara ulipotokea asubuhi ya leo, Jumapili, Aprili 26, 2015 wakati alipoingia tu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kuongoza maelfu kwa maelfu ya wananchi kuadhimisha miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ameuelezea msiba huo kama msiba wa simanzi kubwa.

“Ni wachache katika nchi yetu wanaoweza kulinganishwa na Mzee Hashim Mbita kwa kiwango cha utumishi uliotukuka, wa miaka mingi na usiokuwa na kasoro. Katika utumishi wa Serikali alipata kuwa Mwandishi wa Habari Mkuu wa Idara ya Habari na pia kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais kabla na baadaye kuwa Balozi wa Tanzania katika Zimbabwe. Kazi zote alizifanya kwa ufanisi mkubwa sana,”amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Katika Chama cha TANU alikuwa Katibu Mtendaji wa Chama na katika Jeshi letu makini, Mzee Mbita alipata na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali, yote mambo makubwa kweli kweli.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini ilikuwa katika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika ambako Mzee Mbita alikamilisha utumishi wake kwa kusimamia shughuli nzito ya kuwasaidia ndugu zetu Kusini mwa Afrika kwa miaka 20 mfululizo, miongo miwili, na kuweza kupata uhuru wao. Hakuna mpigania uhuru katika Mozambique, katika Zimbabwe, katika Namibia, katika Angola na hatimaye katika Afrika Kusini ukiondoa nchi nyingine kama Cape Verde, asiyejua mchango wa Mzee Mbita. Wote hawa amewatumia vizuri, kwa ufanisi, kama mlezi, kama kiongozi, kama kamanda hadi wakafanikisha kazi ya ukombozi. Huu ni mchango mkubwa kweli kweli.”

Ameongeza Rais: “Kitendo chake cha mwisho cha utumishi, kilikuwa kuongoza shughuli za Mradi wa Hashim Mbita wa Kuweka Kumbukumbu za Harakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika na Kuenzi Viongozi Wakuu (Hashim Mbita Project to Honour Outstanding Leaders), kazi ambayo nayo aliifanya kwa uwezo na ufanisi mkubwa na ripoti yake tukaizindua mwaka jana pale Victoria Falls, Zimbabwe wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).”

Ilikuwa kwenye Mkutano huo wakati Zimbabwe ilitangaza kumpa Mzee Mbita Nishani ya The Royal Order Munhumutapa yenye kutambua mchango wake katika harakati za ukombozi wa Zimbabwe. Mzee Mbita amekuwa raia wa sita wa kigeni, na wa kwanza asiyekuwa rais, kupata heshima hiyo ya juu kabisa ambayo hutolewa na Taifa la Zimbabwe kwa wageni ambao wamechangia Uhuru wa Zimbabwe.

Viongozi watano wa mwanzo kupata Nishani hiyo, mwaka 2005, walikuwa ni Marais na Viongozi Waanzilishi wa Kundi la Nchi za Frontline States dhidi ya Ukoloni na Ubaguzi wa Rangi, Marehemu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Kenneth David Kaunda wa Zambia, Marehemu Sir Seretse Khama wa Botswana, Marehemu Samora Moises Machel wa Mozambique na Marehemu Augustinho Neto wa Angola,

Ameongeza Rais Kikwete: “Mzee Mbita ametibiwa ndani na nje ya nchi na kila alipolazwa hapa nchini nilikwenda kumwona hospitali. Majuzi tu nilikwenda kumwona kwenye Hospitali ya Jeshi letu pale Lugalo na tukazungumza vizuri sikujua itakuwa mara yangu ya mwisho kuzungumza naye. Naungana na familia ya Mzee Mbita katika kuomboleza kifo na msiba wa Mzee wetu huyu. Nawaomba watambue kuwa msiba wa Mzee Mbita ni msiba wetu sote, msiba wa taifa letu ambalo limepoteza busara yake wakati tulipokuwa tunahitaji zaidi.”

Ameongeza Rais: “Tayari nimeagiza Serikali na Jeshi washirikiane na familia ya Mzee Mbita katika kuandaa matanga na mazishi ya Mzee wetu huyu. Wakati tunaendelea na maandalizi, nawaomba wanafamilia wawe na utulivu na subira kwa kadri tunapopitia kipindi hiki kigumu na kwa pamoja tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma kuiweka peponi roho ya Mzee Hashim Mbita. Amin.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
26 Aprili, 2015 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji  familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo Aprili 27, 2015.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikiti wa Mtoro, baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha
maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo Aprili 27, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mtoto wa Marehemu Bw. Iddi Mbita kuhusu taratibu za mazishi walipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es Salaam jioni ya leo April 27, 2015.


[video] Sherehe za Kitaifa za Maadhimisho ya Muungano 2015
Mapitio ya magazeti ya Aprili 26, 2015 katika Tv


Uandikishaji Vitambulisho vya Taifa waanza Ruvuma
SERIKALI Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma imewahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha katika ya Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na NIDA ili waweze kupata vitambulisho hivyo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru (DC) Bw. Chande nalicho wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo Mjini hapa.

DC Nalicho alisema kuwa miongoni mwa faida za vitambulisho hivyo, ni pamoja na kila Mtanzania kutambuliwa na vile vile kitambulisho hicho kuwa msaada mkubwa kwa mtu binafisi.

Alisema wito huo ameutoa kwa wakazi wa wilaya yake kwa vile wilaya yake ipo pembezoni mwa mipaka kati ya Tanzania na Msumbiji na kuwepo kwa vitambulisho hivyo vizitasaidia mamlaka husika kuwatofautisha wananchi hao kutokana na muingiliano uliopo miongoni mwao.

“kitambulisho hicho ni muhimu hasa kwa upande wetu Tanzania, maana wenzetu nchi jirani ya Msumbiji tayari wamekwisha andikishwa na kupatiwa” 
alisisitiza DC, Nalicho.

Awali akitoa taarifa za uanzishwaji wa zoezi hilo, afisa wa Nida wa Wilaya ya Tunduru Bw. Anafi Nachungu alisema kuwa NIDA itafanya zoezi hilo la utambuzi na usajili wa watu Wilayani humo kwa kuanzia kwa watumishi wa serikali na baadaye zoezi hilo litaingia kwa wananchi wa kawaida.

Alisema zoezi hilo ambalo limeanza April 24 mwaka huu kwa kujaza fomu na kuchukua alama za vidole vya Mkuu wa Wilaya hiyo limepangwa kutekelezwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu ambao unatarajiwa kuishia mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Bw. Nachungu aliendela kufafanua kuwa katika kipindi hicho yeye kwa kushirikiana na wasaidizi wake Bi. Dainas Mossi na Sarvatory Majengo wamejipanga na kuhakikisha kuwa zoezi hili ambalo lilikwama kuanza mwezi Agosti 2014 linakamilika kwa wakati.

via DemashoNews blog

Taarab music fans wajinoma na Jahazi @DarLive

Mzee Yusuf akiimba ndani ya Dar Live

MASHABIKI wa taarab nchini jana walipata walichokitaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Katika onyesho la jana, Kundi la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf lilimwaga burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki kibao waliofurika katika ukumbi huo ambao una kila aina ya ‘mafuraha’ ikiwa ni pamoja na makulaji na vinywaji licha ya hali ya hewa kujenga tishio la mvua kila mara.

Mashabiki wakiserebuka huku wakiwa na picha ya Mzee Yusuf.

Leila Rashid akipagawisha mashabiki.

Mashabiki wakiserebuka kwa raha zao.

Wanenguaji wa Jahazi wakipozi mbele ya kamera.

Shabiki akimtunza pesa Hadija Yusuf.

Musa Musa akilicharaza gitaa.


Shabiki aliyetaka kuingia bure ukumbini baada ya kutaitiwa na walinzi.


Fatma Kassim akiimba.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na: Issa Mnally/GPL

Zanzibar Diaspora yailabua 7:1 Tanganyika na kubeba Kombe la Muungano

Watanganyika

Katika shamrashamra za kusherehekea Miaka 51 kuungana Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Timu ya Zanzibar Diaspora​ nchini Marekani imeifunga bao 7-1 jirani zake timu ya Tanganyika USA.Tanganyika na Zanzibar kama ishara ya MuunganoAbdulghan Ali Himid akipokea tunzo la uchezaji bora

Ally akishangilia Ushindi wa ZADIAMwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Omar Ally
 
 
 
Kocha Seif Ameir wa Timu ya Zanzibar Diaspora Nchini Marekani wapili kushoto akipata picha na wachzaji wa Zanzibar Diaspora 


Kutoka shimoni Kariakoo hadi Marekani: Yasin Kapuya, Mwandishi vitabu, mweleza Rais Mwinyi maudhui ya vitabu vyake vya kumkwamua mwananchiMwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akimwelezea Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ya jinsi gani vitabu vyake vinavyoweza kumkwamua mwananchi wa hali ya chini na kumfikisha juu katika kumboreshea maisha mapya. Akijitolea mfano wake mwenyewe alipoanzia shimoni Kariakoo mpaka kufika nchni Marekani na sasa kualikwa katika mikutano mikubwa ya kutoa semina ya jinsi gani unavyoweza au kampuni inavyoweza kuwa namba moja katika sekta ya biashara.Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akichangia jambo na Katibu Mkuu wa Rais mstaafu Bwn. Abdallah Makame (kulia) aliokua akiongea na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi siku ya Ijumaa April 24, 2015 jijini Washington, DC nchini Marekani.Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakishikilia bango la kitabu chake kipya kitakachotoka hivi karibuni.Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akimkabidhi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi moja ya vitabu vyake.Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akiagana na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. 

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na: Vijimambo na Kwanza Production 

Rais Mwinyi afunga kikao cha Mabalozi wa Heshima, MarekaniRais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akiongea na Mabalozi wa Heshima kuwashukuru kwa kuipenda na kuitangazaTanzania nchini Marekani na kuwaasa wasichoke kwa wao wamekua chachu ya maendeleo ya nchi aipendayo Tanzania.Rais mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiingia katika chumba cha mkutano cha Nyerere ndani ya mjengo wa Ubalozi Washington, DC siku ya Ijumaa April 24, 2015 kulikokuwa na kikao cha Mabalozi wa heshima kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Liberata Mulamula kwa ajili kuongelea masuala mbalimbali zikiwemo changamoto za utalii na uwekezaji nchini Tanzania na jinsi gani ya kukabiliana nazo.

Mbali na Mabalozi hao wa heshima na marafiki zao wengine waliohudhuruia kikao hicho ambacho kilikuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano, ni wawakilishi wa Taasisi za Diaspora za Kitanzania zinazopigana kusaidia maswala ya uwekezaji na Utalii kwa nchi yao Tanzania. 

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliongozana na mkewe Mama Sitti Mwinyi.

BALOZI LIBERATA MULAMULA AONGOZA MKUTANO


Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwemo Mabalozi wa heshima wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani.Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Mabalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha kuongea nao.Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani anyoamtambulisha mbele ya mabalozi wa heshima na kwamba yeye Rais mstaafu ndiye aliyefanya mageuzi ya mfumo wa uchumi Tanzania tunaoendelea nao hivi sasa.Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani akifungua mkutano wa Mabalozi wa Heshima uliofanyika siku ya Ijumaa April 24, 2015 Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mkutano huo ulizungumzia uwekezaji na Utalii zikiwemo Changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo. Pia katika mkutano huo uliokua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano uliudhuria pia na Viongozi wa Taasisi za Diaspora wa Tanzania ambao wanaguswa na kuiona nchi yao ikipiga hatua ya maendeleo katia sekta ya uwekezaji na Utalii.Abdul Majid mwanaDiaspora Mtanzania anayeishi California nchini Marekani akielezea huduma kwa wateja bado ipo kiwango cha chini nchini Tanzania na jinsi gani ikiboreshwa inavyoweza kunua uchumi wa Tanzania.Balozi wa Heshima Mhe. Kjell Berch akichangia na kuelezea majukumu ya Balozi wa heshima.Rais wa East Africa Diaspora Business Counsil Benedict Kazora ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas akichanganua na kutoa maelezo yanayoweza na kurahisiha maswala ya uwekezaji na kukosoa baadhi ya makampuni yanavyowekeza Afrika kwa kujinufaisha yenyewe.Karen Hoffman Rais wa The Bradford Group kutoka New York akielezea sekta ya Utalii na utangazaji wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani.Balozi wa Heshima Mhe.Cemil Teber kutoka New Mexico akichangia jambo.Balozi wa Heshima kutoka Ohio Mhe. Patrick Griswold akielezea sekta ya uwekezaji na changamoto inazokutana nazo huku akitoa mfano wake mwenyewe alipokua meneja mkuu wa General Tire miaka ya nyuma na tangia alipoondoka kiwanda kikafa na sasa anatarajiwa kwenda tena Tanzania kujaribu kukifufua upya kiwanda hicho.Mkutano wa Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Heshima ukiendeleaWakati wa chakula.Mbalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi zinazotangaza Utalii na uwekezaji Tanzania wakimsuikiliza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.Picha ya pamoja.Mayor De Andre Windom wa mji wa Highland Park jimbo la Michigan akipata picha na Rais mstaafu Ali Hassan MwinyiBalozi wa Tanzania nchini Marekani akimuaga Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi wakati walipokua waiondoka baada ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kumaliza kufunga kikao cha Mabalozi wa Heshima Ubalozini hapo.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Vijimambo na Kwanza Production