7 wafariki kwa kuangukiwa na daraja lililokuwa linajengwa


Watu saba waliokuwa ndani ya teksi siku ya Jumapili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na daraja ambalo bado lilikuwa halijakamilika kujengwa katika jiji la Kano huko kaskazini magharibi Nigeria.

Malam Ibrahim, shahidi wa ajali hiyo, sehemu ya daraja iliangukia gari hilo ilipokuwa likipita chini yake.

Msemaji wa polisi Magaji Musa Majia aliyesema kuwa polisi walitumwa eneo la ajali hiyo iliyotokewa saa kumi na moja jioni.

Majia alisema kuwa sehemu ya gari ilinaswa chini ya daraja hilo lililoanguka na kwamba waathirika walikuwa wameshafariki wakati wafanyakazi wa uokozi walipowasili eneo hilo.

Shahidi mwingine, Ahmed Kaka alisema kuwa iliwachukua wafanyakazi wa uokozi takriban saa mbili u nusu kuwatoa maiti.

Wabomoa kaburi, wakamvua maiti nguo, wakachukua mikoba


Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamebomoa kaburi la Napegwa Kishaluli (75) mkazi wa Mailimoja Kibaha mkoani Pwani aliyezikwa Aprili 20 mwaka huu na kumvua nguo zote pamoja na kuchukua mikoba aliyokuwa amezikwa nayo.

Tukio hilo lilitokea Aprili 24 mwaka huu katika Kata ya Tangini jirani na soko la Loliondo ambako baada ya mazishi kaburi hilo liliwekewa mlinzi kwa muda wa wiki moja.

Mkataba wa mlinzi huyo ulipomalizika aliondoka na siku iliyofuata kaburi hilo lilivunjwa.

Watu wa karibu na familia ya marehemu wamesema kuwa baada ya mazishi ulikuwapo uvumi kwamba marehemu alizikwa na vitu vya thamani zikiwamo fedha, simu, pete na mikufu ya dhahabu pamoja na nguo zenye thamani kubwa.

Hata hivyo, taarifa zinasema marehemu Kishaluli alizikwa na mikoba miwili ya nguo na vitu vyake vingine na kwamba kabla ya kifo chake aliagiza azikwe na vitu vyake.

Akizungumza na Mwandishi wetu jana,ndugu wa marehemu,Bartholomew Mwanjile alisema baada kuzika walilazimika kuajiri mtu wa kulinda kaburi hilo la ndugu yao kwa wiki moja lakini siku moja baada ya mkataba kumalizika kaburi hilo lilivunjwa.

“Tuliweka mlinzi alinde kaburi hilo kwa wiki moja tukiamini litakuwa limekauka kwa sababu lilitengenezwa kwa zege.
“Tuliamini watu wenye nia mbaya watashindwa kulivunja jambo ambalo limekuwa kinyume kwa vile baada ya muda huo kumalizika kaburi lilibomolewa na watu wasiojulikana ambao waliamini ndani ya mikoba hiyo kulikuwa na fedha,” 
alisema Mwanjile.

Mwanjile alisema baada ya kuvunja kaburi hilo majambazi walifungua jeneza na kupekua ndani kwa kuligeuza na kuliweka tofauti na lilivyokuwa awali, baada ya kumvua marehemu nguo zote na viatu alivyokua amevalishwa na hata soksi nazo walichukua.

Alisema tukio la kuvunjwa kwa kaburi hilo limetokea baada ya uvumi kuwa ndugu yao alizikwa na nguo na vitu vingine zikiwamo fedha, kiasi cha Sh milioni 8, cheni ya dhahabu,simu za gharama na kompyuta mpakato (laptop), jambo ambalo si la kweli.

“Tulimzika ndugu yetu na mikoba ya nguo zake ambazo aliagiza kabla ya mauti kumkuta na kaburi tulijenga kwa zege lakini tukashauriana tuweke mlinzi, hapo ndipo watu wakaanza kutia shaka wakadhani kuna vitu vya gharama jambo ambalo si kweli,” 
alisema Mwanjile.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamedi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea na watakaobainika watachukuliwa hatua za sheria.

 • via gazeti la MTANZANIA

[audio] Nitagombea Ubunge Shinyanga Mjini - M/Kiti BAVICHA Taifa

Moto wateketeza ghala la Oil Mills la Kahama

Muonekano wa ghala hilo lilivyoathiriwa na moto huo

Bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, katika ghala la kuhifadhia bidhaa za kampuni ya Kahama oil mills wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo William Matonange, amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni kulipuka kwa baadhi ya bidhaa zenye asili ya kulipuka zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala hilo.Aidha meneja huyo amesema bidhaa zilizoteketea zilikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 huku jengo likiwa lenye thamani zaidi ya shilingi bilioni moja.

Akifafanua zaidi amesema moto huo unasadikiwa ulianza usiku wa manane ambapo uligundulika majira ya saa tisa usiku ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha zimamoto ambao walifika na kuanza kuuzima ambao ulidumu kwa masaa sita.Hata hivyo Matonange amelipongeza jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa juhudi za kuimarisha ulinzi katika zoezi la kuzima moto kutokana na wananchi walikuwa na lengo la kuvamia kiwanda hicho kwa ajili ya kwenda kupora mali wakati jeshi la zimamoto likiendelea na zoezi la kuuzima moto huo.

Kwa upande wake, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha amesema uchunguzi unaendelea hivyo taarifa zaidi zitatolewa baada ya wataalam kutoka kitengo cha bima kufanya uchunguzi wao.

 • via KijBibi bog by Bundala William

Taarifa ya ajira mpya ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara


Bofya linki zifuatazo kupakua makabrasha yenye orodha ya majina:

 1. Ajira za Walimu wa Cheti (Shule za Msingi) 2015.
 2. Ajira za Walimu wa Sayansi wa Shahada na Stashahada kwa Mwaka 2015.
 3. Ajira za Walimu wa Masomo ya Sanaa na Biashara Ngazi ya Shahada na Stashahada.

Au kutumia linki za JamiiForums kwa uharaka zaidi.

Kitabu: Tanzania na Propaganda za Udini - I. N. Shariff


“Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenyekupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala.”

Mwanachuoni wa Chuo Kikuu Cha Rutgers, New Jersey, Marekani, Ibrahim ni msomi wa Sanaa, Tarikh (Historia) na Fasihi ya Kiswahili.

Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.
Kitabu hiki “Tanzania na Propaganda za Udini” kina milango mitatu na sahifa 152

Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.

Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.

Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.

Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.
Kitabu hiki “Tanzania na Propaganda za Udini” kina milango mitatu na sahifa 152.

Prof. Ibrahim Noor Shariff
Mlango wa Kwanza unahusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.” Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.

Mlango wa Pili unazungumzia “Propaganda za Siasa za Chuki na Athari Zake.”Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, kuuza na kumiliki watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi, na kumezwa na Tanganyika 1964.

Katika Mlango wa Tatu “Tanzania na Propaganda za Udini Shuleni“ mwandishi, ambae ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata, kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa. Hapohapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli. Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.

Prof. Ibrahim Noor ana hadharisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta balaa kubwa kuliko mauwaji ya Zanzibar ya 1964. Watakaoumia na chuki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania. Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha mambo Tanzania, kwa mfano:
a) Wahishimiwa Memba /Wabunge Tanzania
b) Memba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
c) Mawaziri wa Serikali ya Muungano wa Zanzibar
d) Wakubwa wa Makanisa na Wakubwa wa Vyama vya Kiislamu
e) Wakubwa wa Vyama vya Siasa
f) Wakubwa wa Magazeti
g) Wakubwa wa TV na Radio
h) Na kabla ya wote hao waliotangulia ni mimi na wewe wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema

Kitabu kinauzwa:

DAR ES SALAAM

 • Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema, Phone: 0773 777 707
 • TAMPRO, Magomeni Area along Morogoro Road, Adjacent to Kinondoni Municipal, Plot no. 169 Block R, Kinondoni Dar es Salaam. Phone: 0222172182
 • KEF “Kalamu Education Foundation”, Magomeni– Kinondoni District, Dar es Salaam. Phone: 0776 525 268


ZANZIBAR

 • Masomo Bookshop, behind the Central Market, Zanzibar, Phone: 0242 232652

Wagiriki 3 wakamatwa Tanzania kwa cybercrime

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi.

Polisi wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo:

 1. FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.

 2. ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876.

 3. PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS, Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.

Watu hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.

Katika upekuzi watu hao wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:

 1. Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa “Inspector General of Police DSM”

 2. Nyaraka mbalimbali za kughushi za Polisi Tanzania zinazowasaidia kwa lengo la kupata malipo ya bima nje ya nchi ambazo zina mihuri ya kughushi.

 3. Zimepatikana Kompyuta Mpakato (Laptops) zipatazo tisa ambazo watuhumiwa hawa huzitumia kwa ajili ya mawasilisano pamoja na uhalifu huo wa kimataifa.

 4. Zimekamatwa laini za simu za mkononi (Cheap) za kampuni ya simu ya Airtel ambazo baadhi zimetumika na nyingine hazijatumika.

 5. Aidha, zimekamatwa kadi mbalimbali za benki (Credit Cards) zipatazo 13 zinazotumika kutoa fedha, kuingiza fedha, au manunuzi mengine za ATM.

 6. Pia watuhumiwa hao wamekamatwa na vitabu vitano vyenye kumbukumbu za majina, anwani, pamoja na namba za siri za wateja mbalimbali wa mabenki mbalimbali kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Kenya, Uingereza na Nigeria.

Uchunguzi ziadi unaendelea kuhusu raia hao watatu kutoka nchi ya Ugiriki ili kubaini mtandao wao na kugundua matukio mbalimbali ambayo wameyafanya.

TAHADHARI KWA WANANCHI NA WAGENI WENGINE

Pamoja na kuibuka na wimbi hili la wezi wa mtandao bado ni salama kuweka na kutoa fedha katika mabenki hapa nchini. Hata hivyo kutokana na wimbi hili la wizi kwa njia ya mtandao, ni muhimu sasa kuzuia uhalifu wa aina hii kwa ushirikiano kati ya wamiliki wa mabenki na wateja wao.

Jeshi la Polisi linashauri (pamoja na maelekezo mengine ya benki) njia sahihi ya kwanza ya kuzuia ni kuhakikisha kwamba miamala yote inayofanyika katika akaunti za benki ni lazima ifahamike kwa mteja kwa njia zifuatazo:

 1. Mteja ajulishwe kwa simu ya mdomo ili kuthibitisha muamala.

 2. Mteja atumiwe ujumbe kwa kila muamala unaofanyika kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kumjulisha mteja kiasi kilichotolewa, kiasi kilichoingizwa au makato au maingizo yoyote kwa muda ule ule.

Aidha tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na wasikubali kutoa nambari za akaunti zao kwa watu wasiohusika au nambari zao za siri hata kwa mtu ambaye ni ndugu wa karibu sana.

Mara baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

Orodha ya vyama vitakavyofutiwa usajili Serikalini


Mwenyekiti amlaumu Msajili kubadili ACT-Tanzania kuwa ACT-Wazalendo

Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama Siasa Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha ACT-Tanzania na kuwa ACT-Wazalendo bila ya kufuata utaratibu. Kulia ni Katibu Muenezi wa chama hicho, Fredy Kisena na Katibu Mkuu wa chama hicho, Leopold Mahona.

MWENYEKITI wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas Kadawi Limbu amemlalamkia Msaji wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mtungi kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la chama hicho na kuwa ACT-Wazalendo.

Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.

"Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu mwenendo wa chama hicho. Alisema Limbu

Aliongeza kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za kubadilisha jina la chama hicho kwani haiwezeka na haiingii akilini kubadilisha jina la chama kwa kipindi kifupi na haraka kiasi hicho.

"ACT-Tanzania ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi aanzishe chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania.

Alisema ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye nia hofu na kumpatia mtu madaraka ya kioongozi mkuu na kubadilisha jina lake huku msajili wa vyama akishuhudia.

Alisema msajili wa vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama hicho tarehe 20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho kilichobadilishwa jina akiwa katika zaira ya kichama mikoani aliyoianza tarehe 10-4-2015 huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ATC-Wazalendo.

Limbu alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia mbaya na chama cha ATC-Tanzania.

Taarifa ya Dotto Mwaibale
Imeandaliwa: www.habarizajamii.com

Rais Kikwete ametua Gamaha kuwa Balozi nchini Burundi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: [email protected]
Barua pepe: [email protected]
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600

                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
                  11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

Balozi Gamaha anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.

-Mwisho-

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

27 Aprili 2015

Win APO Award to Dubai for the Africa Energy ForumPRESS RELEASE

DAKAR, Senegal, April 27, 2015/ -- APO (African Press Organization), the sole press release wire in Africa and the global leader in media relations relating to Africa, announced today that entry is now open for the 2015 APO Energy Media Awards (#APOEnergyMediaAward).

APO will offer transport, accommodation and perdiem for the first-place winner to attend the Africa Energy Forum held in Dubai from 8-11 June 2015, as well as one year of access to over 600 airport VIP lounges worldwide.


The Africa Energy Forum (AEF) is the only international Forum focused on power generation for Africa with attendance restricted to stakeholders (investors, consultants, developers, ministries, utilities, regulators etc.) from the power sector.

APO Energy Media Awards celebrates brilliant and inspiring stories about Energy in Africa. The subject matter may comprise a single topic or a variety of subjects, including – but not limited to – oil, gas, electricity, geothermal energy, hydropower, solar energy, wind power, nuclear, coal, biomass and more.

APO Energy Media Awards is open to African journalists and bloggers, whether directly employed or freelancers, working in the continent of Africa who have produced a story that has been broadcast or published in English, French, Portuguese or Arabic in the form of a printed publication, a television feature, a radio story, a website or a blog whose primary audience is based in Africa.

Stories are judged on content, writing, analysis, creativity, human interest and community impact.

Stories must have been broadcast or published between January 1, and April 30, 2015.

All stories must be submitted in electronic format:

a) Print: upload the scan(s) of the published article.

b) Radio: upload the SoundCloud link (SoundCloud is an online audio distribution platform that enables its users to upload and share sounds they have created themselves – https://soundcloud.com).

c) Website: upload the URL.

d) TV: upload the YouTube link.

TV material must first be uploaded to YouTube and radio material to SoundCloud. If you are not a member of these sites, you will need to sign up in order to upload the video or radio material. Once you have obtained the link, you must enter it in this online entry form when inputting your story details.

Online Entry Form is available here

The deadline for entries is 1 May 2015.

The finalists will be announced on 6 May 2015.

The winners will be announced during the Africa Energy Forum in Dubai.

Follow APO on Twitter.com

Follow the hashtag: #APOEnergyMediaAward

Hotuba ya Prof. Lioba kwenye Mkutano wa IV wa CHAUKIDU