Bodi ya Mikopo yaanza kupokea maombi: Mwongozo 2015/16


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) siku ya Ijumaa, Mei 1, 2015 imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.

Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).

Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.

“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.

Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.

Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Zuio la kuvuta sigara, tumbaku katika maeneo ya umma

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 2, 2015
East African Community statement on Burundi

The Secretary General of the East African Community Amb. Dr. Richard Sezibera commends the Government of Burundi on the preparations undertaken so far towards the General Elections to be held in May, June and July 2015.

The Community wishes the People of Burundi free, fair and peaceful elections and calls upon all friends of Burundi to offer their support to the success of the electoral process.

The Secretary General notes that Burundi has made substantial progress in establishing and maintaining peace and stability in the last decade and the forthcoming elections provide an opportunity to consolidate and enhance the country’s social and economic development.

He further recalls that on March 09, 2015 all political actors signed a code of good conduct in which they committed to refrain from pursuing violence in the electoral process.

The EAC notes that the attainment of peace and stability in Burundi amounts to peace and stability in the entire region and urges all regional and international stakeholders to actively engage in the attainment of these objectives.

The Secretary General notes with concern that some Barundi are seeking refuge in neighboring countries due to fear of election related violence. He commends Partner States that receive them and urges the International Community to offer support.

He further urges the Government of Burundi and all actors to ensure that the electoral process does not lead to humanitarian crisis.

Maadhimisho ya Mei Mosi 2015 Kilimanjaro

Mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa zao la Kahawa ncini cha TACri ,Jeremiah Magesa akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi namna ambayo kituo hicho kinavyo saidia katika upatikanaji wa mbegu bora ya zao la Kahawa.Wafanyakazi wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro wakipita na gari lao mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu chaUshirika mjini Moshi.Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCLwakipita katikamaonesho ya Mei Mosi

Chuo cha wauguzi Kibosho pia walipita mbele ya mgeni rasmi kuonesha nini wanafanya katika sherehe hizo za Meio Mosi.


Moja ya mtambo inayotumika kunyunyiza dawa katika Kahawa ikioneshwa mbele ya mgeni rasmi.

Kampuni ya Swissport pia walikuwepo kuonesha kazi wanayofanya katika viwanja vya ndege.Kassim Mwinyi akitoa maelezo kuhusu kampuni ya Panone inavyosaidia katika utoaji wa huduma ya mafuta.

Mwakilishi wa kampuni ya Bia Tanzania, Pudensiana akitoa maelezo kuhusu kampuni hiyo.Magari ya kampuni ya TBL yakipita mbele ya mgeni rasmi.Baaadhi ya wa wafanyakazi wakifuatilia maonesho hayo.Afisa Masoko wa Hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA )Antypas Mgungusi akitoa maelezo juu ya ofa iliyotolewa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kilele cha Shira kwa gharama za Kiasi cha sh 25.000ikijumuisha kiingilio hifadhini,usafiri wa kwenda na kurudi ofa inayotaraji kuanza rasmi Mei 15 mwaka huu.


Halmashauri ya manispaa ya Moshi wakionesha shughuli mbalimbali wanazofanya pamoja na kikombe cha mshindi wa pili wa usafi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akikabidhi kikombe cha ushindi wa nafasi ya pili katika usafi pamoja na cheti kwa mgeni rasmi kaimu mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Novatus Makunga katika shrehe za Meio mosi zilizofanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika.

Bodi ya Kahawa Tanzania TCB pia walikuwepo katika sherehe hizo.Watengenezaji wa Highlife Gin pia waipita kutangaza bidhaa zao mele ya mgeni rasmi.
Kampuni ya SBC watengenezaji wa kinywaji cha Pepsi na jamii yake pia walipita kuonesha vinywaji vinavyo tengenezwa nakampuni hiyo.Kampuni ya Sukari ya TPC ilitia fora baada ya kuingiza mitambo yake inayotumika katika kilimo,kunyunyiza dawa pamoja na kupakia miwa wakati wa uvunaji.

 

hata hivyo vijana walikosa uvumilivu wakalazimka kukimbilia miwa iliyoachwa uwanjani hapo kwa ajili ya maonesho.

Wafanyakazi wakiimba wimbo wa Solidarity katika shrehe hizo.
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga/Kanda ya Kaskazini. 

[video] Rais Kikwete alipoimba "Mimi msafiri bado niko njiani..." na kusema "nisingekuwa Rais, ningekuwa Bongo Fleva"


Jana wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi, Rais Kikwete alijaribu kuimba mstari katika mashairi ya wimbo 'Mimi msafiri" (wimbo wa King Kiki akiwa na Orchestre Safari Sound a.k.a Wana-OSS) na kisha akasema "ah, kama nisingekuwa Rais, nadhani na mimi ningekuwa Bongo Fleva. Sauti yangu si mbaya sana, ingawaje sitawashinda akina Ali Kiba, na akina Diamond na wenzao huko, lakini na mimi rekodi zangu zingenunuliwa."

Unaweza kumsikiliza kwenye video iliyopachikwa hapo chini, na pia unaweza kumsikiliza King Kiki kwa kubofya hapa.


Official Notice: ESRF gets new Executive Director


[video] Mei Mosi 2015: Kauli ya Rais Kikwete kuhusu nyongeza ya mishahara na punguzo la kodi


Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Mei Mosi 2015, ameahidi kuongezeka kima cha chini cha mishahara (kutoka 265,000 hadi kufikia 315,000), ikiwa uchumi utaimarika.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, Rais Kikwete pamoja na mengi aliyoyasema, amewataka waajiri kuendelea kutekeleza sera ya ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi, kulipatia ufumbuzi tatizo la mifuko ya jamii, ushiriki wa wananchi katika kujiandikisha kupiga kura na malipo kwa madeni ya waalimu.

Katika hotuba hiyo Rais Kikwete ameeleza kuwa moja ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani ni kuanzishwa kwa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, ambao utatumika kulipa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia wakiwa kazini. Amesema mfuko huo utaanza kufanya kazi mwezi ujao na tayari Mkurugenzi wake amekwisha teuliwa.

Kuhusu suala la kima cha chini cha mshahara pamoja na kiwango cha kodi ya mapato katika mishahara, Rais Kikwete amesema kuwa serikali inaendelea kuyafanyia kazi, na huenda katika bajeti ijayo mambo hayo yakawezekana.

Sikiliza sehemu ya hayo yalivyotamkwa kwenye video iliyopachikwa hapo juu.


FeDe leo Mei Mosi na makandokando ya Mfanyakazi


Grooveshark shuts down due to license, copyright issues


Wakudata leo katika mizani ya Mei Mosi


Mkondo wa maji waangusha basi Arusha


Imetokea asubuhi leo, kilometa kama 80 kutoka Mto wa Mbu. Hakuna majeruhi yeyote. Chanzo cha ajali ni mkondo wa maji.
Taarifa via WhatsApp.


Salamu za Mei Mosi kutoka kwa Kafulila

SALAMU ZA KAFULILA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI.

Nimependa kutoa maoni yangu eneo moja kuhusu maslahi ya wafanyakazi leo.

Wafanyakazi wa tanzania wanaumizwa sana katika kodi kuliko wafanyakazi wa nchi zote za afrika mashariki

Wastan wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni 18%, Uganda11%, Kenya 6.8%, Burundi 10.3 %na Rwanda 5.6%. ( global tax comparison report 2014-WB)

Wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani kwa mujibu wa ripoti hiyo ni 16.2%. Kwa takwimu hizi sio tu kwamba wastani wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni kubwa kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki bali ni zaidi ya wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani.

Ikumbukwe chama tawala Tanzania asili yake ni harakati za wafanyakazi na wakulima wadogo na ndio tafsiri ya alama ya jembe na nyundo kwenye bendera ya CCM. Hivyo ni aibu chama kilichoasisiwa na wafanyakazi leo kinaongoza kunyonya wafanyakazi kwa kodi kubwa kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki.

Nashauri wafanyakazi waombe CCM iondoe nembo ya nyundo kwenye bendera yake kwani ni kejeli kwa wafanyakazi. CCM kwasasa ipo kwa maslahi ya wafanyabiashara wakubwa wasio waaminifu. Hao ndio wanafaidi uchumi kwa misamaha ya kodi na ukwepaji mkubwa wa kodi.

Ni maoni yangu kwamba kodi ya mshahara inapaswa kushuka kwa 50%. Itoke 18%mpaka9% wastani kwa kuanzia.

Kwa mujibu wa taarifa za TRA mwaka jana, tukishusha kodi hiyo kutoka wastani wa 18-9% tutapoteza mapato kiasi cha 704 billion.

Ni maoni yangu kwamba mapato hayo yanaweza kufidiwa kwa kutekeleza sheria ya kodi ya majengo ambayo mpaka sasa utekelezaji wake ni 3% na tunakusanya 25 billioni. Hii maana yake tukiteleleza kwa 100% tutakusanya zaidi ya 800 billion.

Nawatakia heri wafanyakazi wote Tanzania siku hii muhimu.

David Kafulila (MB)

Moja ya mabango ya leo katika sherehe za Mei Mosi


Rais katika hotuba yake, Rais Kikwete amesema ujumbe wote wa mabango yote umemfikia, "hata wa mashemeji zangu, ukioa Mwalimu..." akatamka mambo kadhaa ambayo Serikali imeyapanga na yanaendelea kukamilika, kisha akasema, "Shemeji zangu baada ya kufanya hayo, nina uhakina ninawaacha pazuri."