Stop putting lemon, sugar, toothpaste or baking soda on your face


People use lemons for exfoliation and to lighten dark marks, but they are bad news because they are highly acidic, with a pH of 2. They will mess with the natural pH of the acid mantle and can irritate the skin. Also, because the citric acid content in lemons varies from fruit to fruit, you don’t really know how strong of a treatment you’re putting on your face; not to mention that citrus oils are potentially phototoxic, meaning that when you make contact with daylight with lemon on your face, the irritation will only increase, possibly to the point of chemical burns.


The uneven, jagged edges of sugar crystals will tear at your skin cells and disrupt your lipid barrier right quick, leaving you vulnerable to dryness and flakiness. After you’ve irritated your skin by scratching at it, the disruption of the lipid layer will only make it take longer to heal. If you want to make your skin soft and smooth, sugar will have the opposite effect in the long run.


Not only is it too harsh of a scrub, but it is also extremely basic (in the pH-of-9 way, not in the thirsty-haters way), so it will knock all the power out of your acid mantle, making your skin more basic than acidic. So basically, baking soda will tear your skin up and then strip it of its first line of defense against bacterial infection.


The first beauty magazines I ever read recommended this as a spot treatment for acne. And in a sea of acne treatments marketed to teens that are way too harsh and quickly strip the lipid barrier, I can understand why toothpaste seems like a gentler option. Still, this is misguided advice because most toothpastes are very basic in pH, so they mess with the acid mantle--the opposite of what you want to do when killing acne bacteria is your aim. Also, they contain a whole bunch of ingredients that aren’t doing your skin any favors. The surfactants that make it foam up and the flavorings that keep it minty fresh? Irritants. All of them.

Now click here to read the full post and suggested alternatives to the above mentioned ingredients.

Tanzania's strong economic growth shows signs of trickling down - World Bank

PRESS RELEASE

DAR ES SALAAM, Tanzania, May 7, 2015 – Sustained rapid economic growth and concerted efforts around national strategies to alleviate poverty have led to a decline of approximately one percentage point per year in the rate of poverty in the country between 2007 and 2012, constituting the first significant reduction in 20 years.

The latest World Bank ‘Tanzania Mainland Poverty Assessment’ confirms earlier findings by the Government’s 2012 Household Budget Survey (HBS) that the basic needs poverty rate declined from around 34 percent to 28.2 percent during that period.

“The reduction in poverty is important news that should be applauded,” says Philippe Dongier, Country Director for Tanzania, Burundi and Uganda. “But what is more important is for the country to accelerate the trend further so as to address the important challenges that still remain. The majority of Tanzanians remain close to the poverty line. In fact, more than 70 percent of the population lives on less than US$2 per day. There is a lot of work ahead to improve the living standards of all Tanzanians.”

“There are emerging signs of pro-poor growth,”
adds Dongier. “These can be seen in the improved levels of education, access to basic services and ownership of land and other assets among poor households. In addition, the economic returns to the poor’s economic activities have also increased, particularly outside agriculture.”

Among other key findings, the Assessment shows a reduction in the level of deprivation of those who remained in poverty as well as a slight decline in inequality at the national level. But despite these positive changes, the number of poor remains high, particularly in rural areas, and the welfare disparity between the geographic regions is widening.

Poverty declined more rapidly in Dar es Salaam than in the rest of the country. The capital city has experienced the highest poverty reduction at a rate above 70 percent between 2007 and 2012, while rural areas registered a reduction of only 15 percent.

Even though there are emerging signs of increased participation of the poor in the growth process, they continue to suffer from lack of capacities and limited access to better job opportunities. Persistent high population growth will continue to challenge poverty reduction efforts in Tanzania. However, the investments made by the Government and its development partners to better measure and understand the determinants of poverty reduction in Tanzania are important steps towards designing improved development programs.

Mengi awazawadia milioni 1 wanafunzi 12 waliofaulu vyema


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amewatunuku wanafunzi 12 waliofaulu vizuri mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka jana wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Kisutu, Dar es Salaam, Shilingi milioni moja kila mmoja. 

Pia, alitoa wito wa kutambuliwa kwa mchango mkubwa wa walimu nchini na kutengewa bajeti ya kutosha.

Dk. Mengi alitoa zawadi hiyo ikiwa ni kutimiza kwa ahadi aliyoitoa alipokaribishwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya wanafunzi 152 waliotarajia kufanya mtihani huo mwaka jana shuleni hapo.

Wanafunzi hao walifaulu kwa kiwango cha daraja la juu ‘distinction’.

Wanafunzi hao ni na daraja la ufaulu katika mabano ni Aluna Athumani (4.0), Grace Mdachi (4.0), Brenda Kisaka (4.0), Bahati Billah (4.0), Angela Amir (3.9), Dafney Mangamba (3.7), Esther Rusimbi (3.7), Halima Mchekwa (3.7), Helen Mkangala (3.7), Clara Kabyemela (3.6), Hamida Said (3.6) na Vailet Amen (3.6).

Akitoa zawadi hizo shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam, Dk. Mengi aliwapongeza wanafunzi hao na walimu wao kwa moyo wa kujituma kwa ajili ya mafanikio ya watoto hao.

Dk. Mengi pia alitaka kutambuliwa kwa kazi kubwa inayofanywa na walimu katika kuinua maendeleo ya elimu nchini na kutaka kutengwa kwa bajeti ya kutosha kwa ajili yao na sekta hiyo kwa ujumla.

“Nawapongeza walimu….mna kazi kubwa. Leo hii hapa nchini, hakuna mtu ambaye haoni au asiyejua matatizo yaliyopo kwa walimu. Ombi langu, tufike mahali tutambue umuhimu wa walimu na elimu kwa maendeleo ya Taifa. Tukishajua umuhimu wa walimu, elimu, tutatenga bajeti ya kutosha,”  “Kama tunasema elimu ni msingi wa maendeleo, ninachoomba maneno yetu yafanane na matendo.”

Ahadi nyingine ambazo Dk. Mengi aliahidi kwa shule hiyo ambazo alishatimiza kabla ya hafla ya jana ni seti nne za runinga (flat) zenye ukubwa wa inchi 40 kila moja, mashine ya kuchapa (printer) na ya kutolea nakala.

Mary Kisaka, mmoja wa wazazi aliyehudhuria tukio hilo, alimshukuru Dk. Mengi na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano huo huku Mwalimu Tunsubilege Alexander, akitaka pongezi kwa walimu kwani wao wapo nyuma ya mafanikio ya wanafunzi.

via NIPASHE


Taarifa ya Ikulu ya Kazi ya Tume ya kuchunguza Operesheni Tokomeza

TAARIFA YA KUKAMILIKA KWA KAZI YA TUME YA UCHUNGUZI WA MALALAMIKO YALIYOTOKANA NA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI TOKOMEZA
___________________________________________


1.0 Utangulizi:

1.1 Tarehe 01/05/2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliunda Tume ya Uchunguzi kuhusu malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Aliteua Makamishna watatu ambao ni Mhe.

Balozi Jaji (Mst) Hamisi Amiri Msumi (Mwenyekiti wa Tume), Mhe. Jaji (Mst) Stephen Ernest Ntashima Ihema (Kamishna), Mhe. Jaji (Mst) Vincent Kitubio Damian Lyimo (Kamishna) na Ndugu Frederick Kapela Manyanda (Katibu wa Tume).

1.2 Operesheni Tokomeza ilikuwa Operesheni iliyobuniwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo jema na muhimu la kupambana na ujangili unaotishia urithi wetu wa wanyama pori, hususani tembo, faru, nyati, twiga, pundamilia n.k.

2.0 Hadidu Rejea kwa Tume

2.1Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;

2.2.Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa;

2.3.Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa;

2.4.Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua zilizochukuliwa na maafisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi;

2.5.Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maaafisa wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea za Operesheni Tokomeza; na

2.6.Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika kupanga na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii ili kuzuia na kuepuka malalamiko mengine kama yaliyotokea kwenye Operesheni Tokomeza.

3.0 Kukamilika kwa kazi ya Tume
3.1 Tume imekamilisha kazi yake na kukabidhi taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 10 Aprili, 2015. Kwa maagizo ya Rais tumeisoma na kuichambua taarifa hiyo vya kutosha.

Kwa hakika Tume imefanya kazi kubwa sana, na nzuri sana ya uchunguzi na uandishi wa taarifa. Kazi imefanywa kwa weledi na umakini wa hali ya juu na kwa lengo dhahiri la kutenda haki. Katika siku 265, Tume ilitembelea wilaya 38 katika mikoa 20 na kuhoji jumla ya mashahidi 259.

Mikoa iliyohusika ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya, Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mara, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Morogoro, Pwani, Tabora, Singida, Manyara, Arusha na Tanga.

3.2 Tume imejitahidi kuwahoji wote waliokuwa na malalamiko, kuwahoji mashuhuda, kuwahoji watuhumiwa, na kukusanya ushahidi wa aina mbalimbali ili ama kuthibitisha makosa pale yalipofanyika na kupendekeza hatua za kuchukua, au kujiridhisha kuwa tuhuma na malalamiko hayakuwa ya msingi.

Kazi hiyo imefanywa vizuri na kurahisisha kazi ya Serikali ya kuchukua hatua zinazostahili.

4.0 Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa

4.1 Tume ilibaini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja cha utekelezaji wa Operesheni Tokomeza iliyoanza tarehe 4 Oktoba, 2013, mafanikio mengi yalipatikana, ikiwemo:

4.1.1 Watuhumiwa 1,030 wa makosa mbalimbali yanayohusu ujangili na uvunaji haramu wa misitu walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria;

4.1.2 Kukamatwa kwa meno ya 211 yenye uzito wa kilo 522, meno ya ngiri 11, mikia ya wanyama mbalimbali 36, ngozi za wanyama mbalimbali 21, pembe za swala 46, mitego ya wanyama 134, ng’ombe 7,621 waliokuwa wanachungwa ndani ya hifadhi na misitu, baiskeli 58, pikipiki 8 na magari 9;

4.1.3 Katika kipindi cha Operesheni kulikamatwa jumla ya bunduki za kijeshi 18, bunduki za kiraia 1,579, risasi 1,964, mbao vipande 27,913, mkaa magunia 1,242, magogo 858 na misumeno 60.

4.1.4 Operesheni ilifanikiwa kupunguza kasi ya mauaji ya tembo kutoka tembo wawili kwa siku hadi tembo wawili kwa mwezi wakati wa Operesheni;

4.2 Operesheni ilisitishwa rasmi tarehe 01/11/2013 ili kupisha uchunguzi wa malalamiko yaliyojitokeza. Baada tu ya kusitishwa kwa Operesheni wafugaji wengi wamerudisha mifugo yao katika maeneo ya hifadhi yaani Mapori ya Akiba, Hifadhi za Taifa, Hifadhi za Misitu na Maeneo Oevu na ujangili ukaanza kurejea.

Aidha watuhumiwa waliokuwa wametoroka kukimbia Operesheni wameanza kurejea kwenye makazi yao.

5.0 Vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu Rejea

5.1 Tume imebaini kuwa katika utekelezaji wa Operesheni kulikuwa na matukio ya ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu Rejea. Ukiukwaji huu umesababisha madhara kwa wananchi mbalimbali ikiwemo vifo, madhara ya mwili na kadhalika.

5.2 Tume ilichunguza matukio 15 ya vifo, na kuridhika kuwa vifo tisa (9) kati ya hivyo vilisababishwa na mateso ambapo watendaji kwenye Operesheni walitumia nguvu kubwa kupita kiasi dhidi ya watuhumiwa wakati wa ukamataji au kuhoji.

Kabla ya vifo watu hao walikuwa chini ya ulinzi wa askari wa Operesheni na kuna ushahidi wa kitabibu (medical reports), ushahidi wa kimazingira na ushahidi wa kuona, unaohusisha vifo vya marehemu hao na mateso kutoka kwa askari wa Operesheni.

Tume haikupata ushahidi wa kuhusisha vifo sita (6) vilivyobaki moja kwa moja na Operesheni Tokomeza.

5.3 Tume ilichunguza madai ya mateso yaliyosababisha madhara kwenye miili ya wahusika. Walalamikaji walieleza Tume kwamba waliteswa ili waoneshe silaha au nyara zilipofichwa au wakiri kujihusisha na ujangili au ujambazi na wataje washirika wao wa mtandao wa ujangili.

Kulikuwa pia na malalamiko ya udhalilishwaji. Malalamiko hayo yalitoka kwenye wilaya ishirini na mbili (22) za mikoa mbalimbali.

Yapo matukio ambayo walalamikaji waliweza kuleta mbele ya Tume uthibitisho wa kuteswa, na walionesha makovu na kutoa vyeti vya matibabu na PF 3 walizopewa baada ya kuumia.

5.4 Tume imebaini kuwepo matendo mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea uliofanywa na baadhi ya askari wa Operesheni na maafisa wengine walioshiriki katika utekelezaji wake, ikiwemo matukio yanayoashiria rushwa na udanganyifu mbalimbali.

5.5 Tume ilishughulikia pia tuhuma za wizi, upotevu na uporaji wa mali. Walalamikaji wa kundi hili walieleza Tume kuwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni, waliibiwa au kupoteza fedha na mali zao wakati na baada ya kukamatwa au kupekuliwa na askari wa Operesheni.

Tume ilichunguza jumla ya matukio ishirini na tatu (23) ya aina hiyo na kubaini kuwa malalamiko mengi yalitokana na askari wa Operesheni kutofuata sheria, kanuni na taratibu za ukamataji, kuhoji na upekuzi maungoni mwa watuhumiwa na kwenye nyumba zao.

Kasoro zilizoonekana ni pamoja na kutoshirikisha viongozi au watu huru katika upekuzi na kutojazwa hati za upekuzi mara baada ya upekuzi. Kasoro nyingine ni askari wengi kuingia kwenye nyumba kwa wakati mmoja.

Aidha, Tume imebaini walalamikaji wengine waliongeza chumvi katika ushahidi wao kuhusu idadi ya mali na fedha zilizopotea au kuibiwa na hivyo ushahidi wao kutoaminika au kuthibitika.

5.6 Tume ilichunguza malalamiko ya kubakwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni. Matukio yaliyochunguzwa na Tume yalikuwa katika Kijiji cha Iputi, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro na Kijiji cha Mwantimba Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu na Wilayani Sikonge.

Hata hivyo wote waliodai kubakwa hawakujitokeza mbele ya Tume kutoa ushahidi wao, hivyo Tume haikuweza kuchunguza malalamiko yao.

Alijitokeza mlalamikaji mmoja Wilayani Ulanga, Morogoro, lakini Tume haikuridhika na maelezo yake, ambayo hayakutosheleza kubainisha kosa kwenye utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

5.7 Tume ilibaini kuwa wapo watuhumiwa waliofikishwa mahakamani na kutiwa hatiani na wengine kuachiwa. Tume imeona kuwa hatua hii ilikuwa sahihi kisheria. Lakini Tume ilibaini pia kuwa baadhi ya watuhumiwa hawakufikishwa mahakamani.

Badala yake maafisa wa Operesheni walijichukulia mamlaka ya kutoa adhabu kwa watuhumiwa kama vile kukamata na kuzuia mali zao, kuchoma moto nyumba na mali zilizokuwa kwenye maeneo ya hifadhi, kuua au kujeruhi mifugo iliyokutwa kwenye maeneo ya hifadhi au kuuza kwa mnada ng’ombe waliokamatwa kwenye maeneo ya hifadhi.

Hatua nyingine inayolalamikiwa ni kuchukua bunduki zinazomilikiwa kisheria.

5.8 Tume imebaini kwamba katika baadhi ya maeneo askari wa Operesheni walichoma nyumba moto kwa madai ya nyumba hizo kujengwa kwenye hifadhi.

Malalamiko hayo yalitoka katika Wilaya za Mlele na Mpanda, Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya; Wilaya za Nkasi na Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa; na Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara.

Katika uchunguzi wa matukio haya Tume imebaini yafuatayo:

Wanakijiji hawakupewa taarifa ya kutosha kuhamisha mali zao kabla ya kuchoma nyumba zao;
Baadhi ya wanakijiji walipoteza vyakula na mali zao katika zoezi hilo la uchomaji moto;
Kuna vijiji vilivyosajiliwa lakini sehemu ya vitongoji vyake viko ndani ya Hifadhi za Taifa;
Kuna maeneo ya hifadhi au ushoroba (buffer zone) ambayo hayana alama za mipaka kati ya hifadhi au ushoroba na vijiji husika;
Kuna nyumba ambazo hazikuwa kwenye eneo la hifadhi au ushoroba na hivyo zilichomwa moto kinyume cha sheria.
Baadhi ya matukio na malalamiko ya kuchomewa moto nyumba yalitokea kabla ya Operesheni.

5.9 Uchunguzi wa Tume umebaini kuwepo kwa tatizo kubwa la wafugaji kutoka nje ya nchi na wafugaji wenyeji kuingiza mifugo yao katika Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Misitu, Maeneo Oevu na Hifadhi za Taifa.

Maeneo yaliyoathirika sana na tatizo hili ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Pori la Akiba la Kigosi – Moyowosi, Pori la Akiba la Maswa, Mapori ya Akiba ya Biharamulo – Burigi – Kimisi na Pori la Akiba la Kijereshi.

Katika baadhi ya maeneo imethibitika kwamba wapo ng’ombe waliouawa kwa kupigwa risasi baada ya kukutwa ndani ya hifadhi.

Aidha, Tume imeridhika kwamba kuna ng’ombe wa walalamikaji waliokamatwa na kuuzwa kwa mnada. Uuzaji wa ng’ombe katika tukio hili haukuzingatia utaratibu wa kisheria.

5.10 Tume ilipata ushahidi kwamba katika maeneo mbalimbali askari wa Operesheni walikamata au kuchukua bunduki, risasi pamoja na vitabu vyake hata kwa silaha zinazomilikiwa kihalali.

Maeneo ambayo yalikuwa na malalamiko ya watu kuchukuliwa silaha zao ni mikoa saba (7) ambayo ni Katavi, Mbeya, Lindi, Morogoro, Tabora, Manyara na Pwani ambapo jumla ya watu sitini na mbili (62) walijitokeza mbele ya Tume kulalamika tukio hili.

6.0 Hatua Zitakazochukuliwa na Serikali

6.1 Baada ya kupitia kwa kina taarifa ya Tume, pamoja na mapendekezo ya Tume, Serikali itafanya yafuatayo:

6.1.1 Hatua za kimashtaka zitaendelea kwa shauri la mauaji ambalo upelelezi wake umekamilika na hatua za kiuchunguzi zitaendelea kwa mashauri mengine nane (8) ya mauaji ambayo upelelezi wake haujakamilika;

6.1.2 Hatua za kisheria na kiutawala zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa waliothibitika kuwatesa watu 15 wakati wa Operesheni;

6.1.3 Hatua za kiuchunguzi zinazofanywa na TAKUKURU kuhusu tuhuma za rushwa na udanganyifu zilizothibitika zitaendelea;

6.1.4 Silaha zinazodaiwa kumilikiwa kihalali zitafanyiwa uhakiki na ukaguzi wa kina kuhusu umiliki na matumizi yake na endapo hakutakuwa na sababu nyingine za kisheria za kuzuia urejeshwaji, wamiliki warejeshewe silaha zao kwa mujibu wa sheria na taratibu;

6.1.5 Mali ambazo zimethibitika kuchukuliwa wakati wa Operesheni kwa tuhuma za kuhusishwa na uvunaji haramu wa mazao ya misitu zirejeshwe endapo hakutakuwa na sababu za kisheria kuendelea kuzishikilia;

6.1.6 Serikali itafanya uhakiki wa vijiji ambavyo vimesajiliwa na vimo ndani ya hifadhi ili kutatua migogoro ya ardhi kati ya hifadhi na vijiji. Aidha, Serikali itahakikisha kunakuwa na ushirikiano wa karibu kati ya Msajili wa vijiji au mamlaka husika na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuepuka kusajili vijiji ndani ya maeneo ya hifadhi;

6.1.7 Wizara ya Maliasili na Utalii itatayarisha kanuni zitakazoweka utaratibu wa kuwaondoa watu waliovamia na kujenga makazi katika hifadhi;

6.1.8 Sheria zote zinazolinda maeneo ya hifadhi zitafanyiwa marekebisho ili kuongeza adhabu kwa kosa la kuingiza mifugo kwenye Hifadhi bila kujali uraia wa wamiliki wa mifugo hiyo;

6.2 Kwa vile Tume imejiridhisha na faida kubwa na mafanikio ya Operesheni Tokomeza, Serikali itaendelea na Operesheni kama hizo kadri itakavyojitajika ili kuokoa maliasili za Taifa, ikiwemo wanyama, hifadhi na misitu.

Hata hivyo ushauri wa Tume juu ya kuboresha upangaji, usimamizi na utekelezaji wa Operesheni hizo itazingatiwa kikamilifu.

7.0 Mawaziri Waliojiuzulu

Tume ilijiridhisha kuwa Mawaziri wote waliojiuzulu, yaani Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi, Mb., Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, Mb., Mhe. Mathayo D. Mathayo, Mb., na Mhe. Shamsi V. Nahodha, Mb.,hawakuhusika moja kwa moja na makosa yoyote ya utekelezaji kwenye Operesheni Tokomeza. Hivyo, waliwajibika kisiasa tu na hakuna hatua nyingine inayostahili dhidi yao.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Mei, 2015

Orodha ya majina yaliyopitishwa na CUF kuwania Ubunge, Uwakilishi

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, ametangaza majina ya wagombea nafasi za ubunge na uwakilishi watopigiwa kura za maoni katika majimbo yao kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CUF kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

MAJINA YALIYOPITISHWA NA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KUWANIA TIKETI ZA UTEUZI KWA NAFASI ZA UBUNGE NA UWAKILISHI ZANZIBARTaarifa na Ratiba ya Mkutano wa XX wa Bunge la X la Bajeti 2015/16

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIATAARIFA KWA UMMA

YAH: MKUTANO WA ISHIRINI WA BUNGE LA KUMI KUANZA DODOMA TAHERE 12 MEI 2015

_______________

1.0 UTANGULIZI

Mkutano wa Ishirini (20) wa Bunge la Kumi (10) unatarajia kuanza mjini Dodoma tarehe 12 Mei 2015. Mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali ndiyo utakaokuwa mkutano wa mwisho wa Bunge hili kabla ya kuvunjwa na baadaye kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015.

Hivyo, Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili mjini Dodoma ifikapo Jumapili tarehe 10 Mei 2015 tayari kuhudhuria kikao cha briefing siku ya Jumatatu tarehe 11 Mei, 2015.

2.0 SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA

Katika Mkutano huu kutakuwa na wastani wa maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na kupatiwa majibu. Aidha, kutakuwa na wastani wa maswali 56 atayoulizwa Waziri Mkuu na kuyapatia majibu kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013.

Aidha, katika mkutano huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/2014 itawekwa mezani na kufuatiwa na taarifa yenye majibu kuhusu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Hesabu za mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Baada ya hayo, Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa Wizara zote 24 wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha unaoisha pamoja na Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.

Siku ya Alhamisi tarehe 11/Juni/2015 saa 4:00 (nne) asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 itakayosomwa na Waziri wa Fedha saa 10:00 jioni. Wabunge wote mnaombwa kuwepo Dodoma.

Mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2015/2016 utaanza na utafuatiwa na kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2015 pamoja na kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2015.

3.0 SHUGHULI NYINGINE

Shughuli za Mkutano wa 20 zinatarajiwa kumalizika tarehe 27 Juni, 2015 na kuhitimishwa kwa hotuba ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge.

Ratiba kamili ya shughuli za Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Kumi itapatikana kwenye Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
DAR ES SALAAM
08 Mei 2015JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA


RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE LA BAJETI, KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016 TAREHE 12 MEI, 2015 HADI 27 JUNI, 2015 


OFISI YA BUNGE
MEI, 2015

Taarifa ya TMA kuhusu hali ya mvua kwa ukanda wa Pwani

Nakala hii na taarifa nyingine kuhusu hali ya hewa zinapatikana kwenye tovuti ya www.meteo.go.tz

Taarifa ya Waziri kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA 

TAARIFA YA MHE. PROF. MAKAME MBARAWA (MB), WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015 KWA WAANDISHI WA HABARI


TAREHE 8 MEI, 2015

Ndugu Wananchi,
Ndugu Waandishi wa Habari,


Kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kumeleta mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku. Mafanikio haya yanathibitika kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii. Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi katika jamii. Changamoto hizo ni pamoja na kuibuka kwa makosa mapya ya jinai na pia mbinu mpya za kutenda makosa ya zamani.

Ndugu Wananchi,

Makosa hayo hujumuisha uhalifu wa Mitandao ambao simu za mkononi, kompyuta au mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu huo.

Mifano ya makosa hayo ni kama ifuatavyo:

 1. Kumekuwepo na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao,
 2. Kumekuwepo na ugaidi kupitia kwenye mitandao,
 3. Kuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili,
 4. Kumekuwepo na uharibifu wa miundombinu muhimu ya Taifa kwa makusudi, Kwa mfano kukatwa kwa makusudi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. [Hii imepelekea kuisababishia Serikali na Sekta binafsi hasara na kusababisha kukosekana kwa huduma mbalimbali za kiuchumi na za kijamii]. 
Ndugu Wananchi,

Kama mnavyofahamu kwenye kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopita, Serikali ilipeleka Mswada wa kutunga sheria ya uhalifu wa mtandao (Cyber Crimes) na Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge. Madhumuni ya kutunga sheria hii kama sheria nyingine zilizotungwa na Bunge hapa nchini ni kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hasa kwenye matumizi ya TEHAMA.

Ndugu Wananchi,
Ndugu Wandishi wa Habari,


Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hii. Kuna nchi mbalimbali duniani zimetunga sheria kama hii, kwa mfano nchi ya Uingereza (UK Computer Misuse Act, 1990), India (IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime Act 2. ) Uganda (Computer Misuse Act, 2010), Korea ya Kusini (Information and Communications Network Act na Information and Communication Infrastructure Protection Act), Singapore (The Computer Misuse and Cybersecurity Act), Maturities (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003), Afrika ya Kusini, Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984) na nyingi nyinginezo.

Ndugu Wananchi sasa mmepata pahala pa kukimbilia, kwani mukitendewa uhalifu kupitia mitando sheria hii itawasaidia kupata haki zenu. Ninawashangaa sana wale wanaopinga kutungwa kwa sheria hii hapa Tanzania. Haikubaliki hata kidogo kuona Wantanzania wengine wanakumbana na uhalifu kupitia Kwenye mtandao na wachache kwa faida zao binafsi wanataka Serikali ikae kimya. Sheria hii haina tofauti na sheria za nchi nyingine nilizozitaja hapo awali. Sheria hii imetungwa kwa mazingira ya nchi yetu ya Tanzania.

Ndugu Wananchi,

Sheria hii sasa imeshasainiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kupitia hatua zote za kuiboresha. Hatua ya MWISHO ilikuwa ni ile ya marekebisho yaliyofanywa na Bunge ambapo baadhi ya vifungu vilivyolalamikiwa viliboreshwa. Kwa hivyo wananchi sasa tuipokee sheria hii na kuitumia. Sheria hii ni nzuri na itasaidia sana kuwalinda wananchi, mitandao na miundombinu yetu muhimu ya kitaifa.

Katika kuitumia sheria hii na kama ilivyo kwa sheria nyingine yoyote, patakapoonekana kuna mapungufu, marekebisho yatafanyika. Kwa hivyo kama kuna mtu yeyote mwenye maoni ya kuiboresha sheria hii anaweza kuleta maoni Serikalini hapa Wizarani. Ninarejea tena: Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Mabalozi, wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano, waandishi wa habari, wana-bloggers, na wananchi kwa ujumla kama kuna yeyote mwenye maoni ya kuboresha kifungu chochote cha sheria hii alate maoni hayo hapa Wizarani.

Serikali kupitia Wizara yangu itapokea maoni au ushauri huo, tutayatafakari na kuyafanyia kazi kwa kina. Haitosaidia sana kusema huko pembeni, jukwaa zuri la kuleta maoni ni kupitia Wizara yangu.

Ndugu Wananchi, na
Ndugu Waandishi wa Habari,


Hii haitokuwa sheria ya kwanza kufanyiwa marekebisho kama itaonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Ahsanteni na Ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.

Taarifa ya TMA kukanusha uvumi wa kuwepo Tsunami


Tangazo la nafasi za masomo na fursa za ajira • Wewe ni kijana wa Kitanzania ?
 • Unapenda kufanya kazi kama MTAALAMU WA CHAKULA NA LISHE ?

Kama jibu ni ndio, basi hii ni habari njema sana kwako.

Chuo cha NEEMA HERBALIST COLLEGE, kinatangaza nafasi za kujiunga na kozi ya CHAKULA NA LISHE katika ngazi ya cheti cha msingi yaani BASIC CERTIFICATE IN FOODS AND NUTRITION.

Kozi hii itakupa sifa na uwezo wa kufanya kazi kama MUANDAAJI NA MTAYARISHAJI WA VYAKULA-LISHE MAALUMU KWA WAGONJWA, NA WENYE KUSUMBULIWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA, kwenye maeneo mbalimbali kama vile:

1. Hotelini na kwenye migahawa mbalimbali.
2. Vituo mbalimbali vya afya.
3. Kwenye shule za chekechea, msingi na sekondari.
4. Kwenye vituo vya kulelea na kutunza watoto ( Day Care Centres )
5. Kwenye Vituo vya kutunza wazee na watu wenye mahitaji maalumu ya kiafya.
6. MAJUMBANI : Kuhudumia wagonjwa na wenye mahitaji maalumu ya kiafya waliopo majumbani.
7. Pamoja na kwenye maofisi mbalimbali.

MWOMBAJI awe na Elimu ya kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na kuendelea.

FOMU ZA KUJIUNGA

Fomu za kujiunga na kozi hii zinapatikana chuoni kwetu kwa gharama ya shilingi ELFU KUMI NA TANO TU (Tshs.15,000/=).

Tunapatikana jijini DAR ES SALAAM, katika eneo la UBUNGO nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA karibu na KAGAME HOTEL.

Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 12 JUNI 2015 saa nane kamili mchana.

ADA YA MASOMO
Ada ya masomo haya ni rahisi, na inalipwa baada ya mhitimu kuingia kazini.

KWA WAOMBAJI WA MIKOANI:
Kwa wanafunzi kutoka mikoani, Hosteli zipo kwa wanawake na wanaume.

Kwa waliopo nje ya Dar Es salaam,kupata fomu ya kujiunga na kozi hii, andika maombi ya fomu ya kujiunga na kozi hii,kupitia barua pepe yetu ambayo ni : [email protected]

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu 0765103080 au tembelea ; neemaherbalist.blogspot.com

Taarifa ya Ikulu: Matokeo ya uchunguzi wa awali kumhusu Maswi

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz               

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
     STATE HOUSE,
             1 BARACK OBAMA ROAD,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MATOKEO YA UCHUNGUZI WA AWALI KUMHUSU NDUGU ELIAKIM
C. MASWI, KATIBU MKUU, WIZARA YA NISHATI NA MADINI
_________________________________________________

 1. Utangulizi

  1. Katika mkutano wake wa 16 na 17, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine, lilijadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyotokana na Taarifa ya Ukaguzi wa Akaunti ya Tegeta Escrow uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

  1. Baada ya majadiliano, Bunge lilipitisha maazimio kadhaa yaliyoelekezwa kwa Serikali kwa ushauri na utekelezaji. Mojawapo ya maazimio hayo yalimtaja Ndugu Eliakim C. Maswi, ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kuwa amehusika kijinai au kimaadili katika miamala iliyotokea katika akaunti ya Tegeta Escrow.

  1. Wakati anahutubia Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam tarehe 22 Desemba, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema ifuatavyo:-

“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. Hivyo, nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”

  1. Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zimeshughulikiwa katika ngazi mbili tofauti. Amechunguzwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma, kisha baada ya hapo alichunguzwa pia na Kamati ya Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na mamlaka yake ya nidhamu.

 1. Sekretarieti ya Tume ya Maadili

  1. Kifungu 18 (2) (c) na (3) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kinaipa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mamlaka na uwezo wa kuchunguza tuhuma yoyote ya kuvunjwa kwa maadili ya uongozi wa umma yanayotawaliwa na Sheria hiyo. Tuhuma dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi zilizomo kwenye maazimio ya Bunge zinatawaliwa na Sheria hiyo.

  1. Katika kutekeleza majukumu yake, Sekretarieti ya Maadili ya Umma ilifanya uchunguzi wa awali na kisha kumhoji Ndugu Eliakim C. Maswi tarehe 19 Desemba, 2014.

  1. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma haijabaini kuwepo kwa maslahi binafsi katika uamuzi uliofanywa na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini wa kuruhusu fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow kutolewa. Aidha, hawakubaini ukiukwaji wowote wa maadili ya viongozi wa umma uliofanywa na Ndugu Eliakim C. Maswi. Waliona kuwa yote aliyoyafanya yalizingatia matakwa ya Sheria, ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na ridhaa ya TANESCO. Hivyo, Sekretarieti ya Maadili haikuona msingi wowote wa kuendelea na shauri la Ndugu Eliakim C. Maswi, na wamelihitimisha.

 1. Kamati ya Uchunguzi wa Awali ya Mamlaka ya Nidhamu

  1. Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa) Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu ya Makatibu Wakuu.

  1. Kwa kuzingatia Azimio husika la Bunge, na kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu Mkuu Kiongozi aliunda Kamati ya Uchunguzi wa Awali dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Kifungu cha 36 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 kinachotamka ifuatavyo:-
“Where it is necessary to institute disciplinary proceedings against a public servant, the disciplinary authority shall make preliminary investigations before instituting disciplinary proceedings.”

  1. Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni 35(2)(b) na Kanuni 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Katibu Mkuu Kiongozi alimpumzisha Bwana Eliakim C. MASWI kutekeleza majukumu yake ya kazi ya Katibu Mkuu ili kupisha uchunguzi wa awali. Uchunguzi wa awali ulifanyika chini ya Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa Umma zilizotajwa, pamoja na Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, kama ilivyorekebishwa.

  1. Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni zilizotajwa kwenye ibara 3.3 hapo juu, Katibu Mkuu Kiongozi aliteua Kamati ya Uchunguzi wa Awali na kuipa Hadidu za Rejea zifuatazo:

3.4.1 Kubainisha wajibu na madaraka halisi ya Katibu Mkuu, Wizaraya Nishati na Madini, kwenye uendeshaji wa TANESCO kwa ujumla, na hususan kwenye kufungua, kuendesha na hatimaye kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow.

3.4.2 Kubainisha na kupata maelezo ya kina juu ya kuhusika kwa Bwana Eliakim C. Maswi katika mchakato na mtiririko mzima wa akaunti ya Tegeta Escrow, tangu kufunguliwa hadi kufungwa.

3.4.3 Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo kuna jambo lolote ambalo Bwana Eliakim C. Maswi alilifanya au ambalo alipaswa  kulifanya lakini hakulifanya, linalomstahilisha achukuliwe hatua za nidhamu.

3.4.4 Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua yoyote ya mchakato na mtiririko wa tangu kufunguliwa hadi kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow, Bwana Eliakim C. Maswi alifanya  jambo lolote linalodhihirisha matumizi mabaya ya mamlaka yake kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa namna iliyosababisha hasara ya aina yoyote ile kwa Taifa la Tanzania.

   1. Kubainisha na kupata maelezo ya kina iwapo katika hatua yoyote tangu akaunti ya Tegeta Escrow ilipofunguliwa hadi ilipofungwa, Bwana Eliakim C. Maswi hakuchukua tahadhari ya kutosha kulinda maslahi ya umma na kusababisha kupotea kwa fedha za umma kwa uzembe au matumizi mabaya ya madaraka.

   1. Kubainisha iwapo kuna mahali popote katika mchakato wa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo Bwana Eliakim Chacha Maswi alifanya jambo lolote linaloashiria kitendo cha kijinai, au kukiuka maadili ya viongozi wa umma.

   1. Kuandaa taarifa ya uchunguzi wa awali kwa msingi wa Hadidu za Rejea zilizomo humu na kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, ipendekeze hatua za kuchukuliwa kwa kila eneo ambalo Kamati itabaini umuhimu wa hatua kuchukuliwa.

  1. Mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi wa Awali

   1. Kamati haijabaini kosa lolote ambalo linaweza kusababisha Ndugu Eliakim Chacha Maswi, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, kufunguliwa mashtaka ya kinidhamu kwa kukiuka Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 ikisomwa pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 kwa kuruhusu Benki Kuu ya Tanzania kutoa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

 1. Hitimisho la Uchunguzi wa Awali

  1. Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote ya kimaadili katika mchakato wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.

  1. Hali Kadhalika Uchunguzi wa Awali uliofanywa na Kamati ya Uchunguzi wa Awali iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi umebaini kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi, “hakutenda au kuhusika na jambo lolote linaloashiria vitendo vya jinai au kukiuka Maadili ya Viongozi wa Umma”.

  1. Ushahidi wa vielelezo uliotolewa kwenye Sekretarieti ya Maadili na kwenye Kamati ya Uchunguzi wa Awali umejitosheleza kuthibitisha kwamba Ndugu Eliakim C. Maswi alitenda kazi yake kwa kiwango kinachoridhisha kwa kufanya mawasiliano na mamlaka mbalimbali na kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuhakikisha na kujiridhisha kwamba kufungwa kwa Akaunti ya Tegeta Escrow kunafanyika kwa usahihi.

  1. Hakuna ushahidi wowote kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi alikuwa miongoni mwa waliopata mgao wa fedha au fadhila yoyote kutokana na kufungwa Akaunti ya Tegeta Escrow.

  1. Kwa nafasi yake ya mamlaka ya nidhamu Katibu Mkuu Kiongozi, ameridhika kuwa Ndugu Eliakim C. Maswi hana makosa yoyote aliyoyafanya katika mchakato wa akaunti ya Tegeta Escrow yanayostahili adhabu. Hivyo, mchakato wa kinidhamu, kimaadili na kijinai dhidi yake umefikia mwisho wake. Mwenye mamlaka ya uteuzi atatafakari taarifa hizi na kuamua cha kufanya kuhusu ajira yake baadaye.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
8 Mei, 2015


[video] Daraja la Tegeta linalounganisha Goba na Wazo lakatika


Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya Wazo jimbo la Kawe na kata ya Goba jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma ya umeme baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja.

Maji ya mvua yameingia kwenye matanki katika kituo cha Kobil kilichopo Afrikana na kuchanganyika na mafuta na hivyo kusababisha hitilafu katika magari.

Ofisi ya Takwimu yazungumzia ongezeko la mfumko wa bei

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Gwesigabo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kupanda kwa mfumuko wa bei wa huduma na bidhaa. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bi, Ruth Minja.

OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.3 kwa Machi mwaka huu ambapo umeongezeka kwa asilimia 0.8 kutoka asilimia 0.7 Machi, 2015.

Ongezeko hilo limechangiwa na kasi ya upandaji bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Aprili, 2015 kuongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo ya Machi, 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alisema farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili,
mwaka huu kutoka 150.50 Aprili mwaka jana.

"Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Machi mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 5.9 Machi mwaka jana, hii imetokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kinachoishia Aprili, 2015," alisema.

Alisema bei za vyakula kama mchele umepanda kwa asilimia 23.3, unga wa mihogo kwa asilimia 8.4, nyama kwa asilimia 4.9, samaki kwa asilimia 5.8 ambapo maharage yamepanda kwa asilimia 6.8 na sukari kwa asilimia 5.6.

Kwegisabo aliongeza kuwa mfumuko huo kwa Aprili, 2015 umeongezeka kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na asilimia 0.7 Machi, 2015 ambapo farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, 2015 kutoka 155.88 Machi, 2015.

"Vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa farihisi za bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 5.8, mahindi kwa asilimia 6.3, unga wa mahindi kwa asilimia 5.0, samaki waliokaushwa kwa asilimia 3.1, ambapo maharage kwa asilimia 2.9, na viazi mviringo kwa asilimia 7.0, mihogo kwa asilimia 6.4 pia viazi mviringo kwa asilimia 4.0," alisema Kwesigabo.

Aidha uwezo wa shilingi 100 kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 63 na senti 61 Aprili, 2015 kutoka Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 64 na senti 15 Machi, 2015.

Alisema mfumuko huo unamwelekeo unaofanana na nchi za Afrika Mashariki ambapo Uganda umeongezeka kwa asilimia 3.60 kutoka asilimia 1.90 Machi, 2015, Kenya umepanda kwa asilimia 7.08 Aprili, 2015 kutoka 6.31 Machi, 2015. 

Taarifa ya Dotto Mwaibale
Imeandaliwa na mtandao wa habarizajamii.com