Lighter moment: Masawe on his deathbed...


Masawe is on his deathbed and knows the end is near. The nurse, his wife, his daughter and 2 sons, are with him. He asks for 2 witnesses to be present to record his last wishes, and when all is ready he begins to speak: 

"My son, "Lelo, I want you to take the Sea-view and Upanga Apartments."

My daughter "Manka, you take the Oyster-bay Hotel, Masaki apartments and the mansion on Haile Selasie avenue."

My son, Matayo, "I want you to take the offices in town, PPF towers and Diamond Jubilee towers."

Anastazia, my dear wife, "please take all the residential buildings in Mbezi beach, Shanty Town and Njiro Hill"

The witnesses are blown away as they did not realize his extensive holdings, and as Masawe slips away, the nurse says, "Anastazia, your husband must have been such a hard-working man to have accumulated all this property."

She replies, "Property? Ni ruti za kuzungusha maziwa!"
  • Lighter moments via WhatsApp

10 Misconceptions about English

Mwanafunzi ajinyonga baada kukutwa na barua ya mapenzi

MWANAFUNZI wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mwagiligili, iliyopo Misungwi, mkoani Mwanza, Rahel Emmanuel (13), amekutwa amekufa baada ya kujinyonga ndani ya nyumba ya Mwalimu wake Mkuu, John Msusa.

Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Msusa alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa sita mchana.

Alisema kabla ya kifo hicho, mwanafunzi huyo ambaye ni mtoto wa shemeji yake, aliyeanza kuishi naye tangu akiwa mdogo alikutwa na karatasi katika madaftari yake iliyokuwa na maneno ya mapenzi na alihojiwa ofisini na kuruhusiwa kwenda nyumbani kumpikia mtoto chakula, ndipo akajinyonga.

“Huyu mwanafunzi alikamatwa na kipande cha karatasi katika madaftari yake kilichokuwa na maneno ya mapenzi, tulimhoji ofisini na kumruhusu kwenda nyumbani kumpikia uji mtoto aliyekuwa analia, sasa alipofika nyumbani kwangu alifanya uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ndani ya nyumba tunayoishi.
“Hatujui alifikiria nini hadi kuchukua uamuzi wa namna hiyo, hili suala tunawaachia vyombo vya dola ili kuchunguza zaidi,” 
alisema Msusa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwagiligili, Herman Paulo, alikiri kutokea tukio hilo na alisema alichukua uamuzi wa kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Misasi na walifika na kufanya uchunguzi na kuruhusu mwanafunzi huyo kuzikwa jana katika Kijiji cha Kanyerere.

Pia Ofisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Misungwi, Efram Maginge, alisema wamepata taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo, aliyekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuhitimu mwaka huu.

Polisi wilayani Misungwi nao wamethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na walisema hakuna wanayemshikilia.

Mapitio ya magazeti katika Tv, Mei 13, 2015Basi la wanafunzi lagonga lori; Mwalimu alaumiwa

Lori la mchanga likiwa limepinduka baada ya ajali 
Ajali hiyo imetokea jioni ya jana eneo la Boma Mbuzi, Pasua katika barabara iendayo kiwanda cha sukari TPC, na kuhusisha magari mawili -- Toyota Hiace yenye namba za usajili SU 37299 mali ya Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) lililogongana uso kwa uso na tipa la mchanga lenye namba za usajili T 202 BFT -- na kusababisha tipa hilo kupinduka.

Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa barabarani aliyefika katika eneo la tukio, aliyepata majeraha makubwa ni dereva (mwanafunzi) ambaye jina lake halijafahamika na aliwahishwa kupata matibabu.

Kwa upande wa dereva wa lori hilo bwana Victor ambaye amepata mshituko katika mguu wake wa kulia, ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni dereva wa Hiace kuingia kwa kasi katika barabara hiyo akitokea upande wa kushoto wa barabara hiyo hivyo na kushindwa kulimudu gari na hatimaye kulifuata lori hilo.
Mimi nilikuwa nikipandisha kutokea upande wa Serengeti (breweries) kwa kawaida nilitegemea dereva wa Hiace angesubiri nipite kwani nilikuwa upande wake wa kulia lakini cha kushangaza aliingia bila kutoa ishara na gari ilipomshinda alikuja upande wangu, nilijaribu kumkwepa lakini ilishindikana kwani alishakaribia sana na baada ya kugongana, gari langu lipinduka kutokana na uzito wa mchanga niliyokuwa nimebeba.

Hali ya tafrani ilizuka mara baada ya mwalimu wa VETA kumueleza askari wa usalama wa barabarani waliofika eneo hilo kuwa yeye pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakitokea upande wa mjini jambo lililopingwa vikali na mashuhuda wa ajali hiyo kitendo kilichopelekea askari kuwatuliza wananchi hao ambao walitaka kumpiga mwalimu huyo.

Akizungumza na mwandishi wetu huku akiwa haoneshi ushirikiano wa kutosha, Mwalimu aliyekuwa akiwasimamia wanafunzi hao wa VETA (hakutaja jina) alieleza kuwa ndani ya Hiace kulikuwemo na wanafunzi ishirini akiwemo aliyejeruhiwa (dereva).
“Huyu mwalimu ndiyo mwenye makosa. Huwezi kumruhusu mwanafunzi aingize gari barabarani katika hali kama ile” 
alieleza bwana Hamis Mbwana mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.

Hadi mwandishi wa habari hii anaondoka katika eneo la tukio, gari maalum kwa ajili ya kuvuta na kuondoa magari hayo lilifika ili kuruhusu shughuli nyingine za matumizi ya barabara kuendelea.Kushoto ni dereva wa lori akiongea na askari wa barabarani. Aliyefunga mikono kifuani ni mwalimu wa VETA aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi katika hiace iliyohusika katika ajali.Utingo wa lori akikusanya mchanga uliomwagika baada ya ajali
Askari wa barabarani akijaribu kuwatuliza wananchi walitaka kumpiga mwalimu wa VETA

Sababu ya Tanga kushindwa kuuza machungwa Ulaya yatajwa


TANZANIA imeshindwa kuuza matunda aina ya maembe na machungwa katika soko la nje kutokana na kushindwa kudhibiti ubora wa matunda yanayozalishwa na wakulima wakiwemo wa wilaya za Muheza, Korogwe, Kilindi na Handeni mkoani Tanga.

Hayo yamebainishwa na Mtafiti wa Mazao ya Kilimo wa Kituo cha Mikocheni, Dk. Zuberi Seguni wakati akiwasilisha mada kuhusu Nzi Mvamizi wa Matunda kwenye mkutano wa kikosikazi ngazi ya mkoa kilichofanyika jijini Tanga jana.

Amesema kuwepo wa nzi huyo nchini kunasababisha Tanzania kuwekewa karantini ya kuuza matunda nchi za nje ambazo zina masoko yanayotoa bei kubwa ya matunda, na kwamba katika wilaya ya Muheza yenye uzalishaji mkubwa wa machungwa kumekuwa na uharibifu wa kati ya asilimia kati ya 50 hadi 80 kwa msimu.
“Wilaya ya Muheza ambayo inazalisha wastani wa tani 100,000 za machungwa kwa mwaka, asilimia 20 huharibika na kusababisha hasara ya kiasi cha sh. bilioni 2.5 kila mwaka”
“Kabla ya kuingia kwa Nzi Mvamizi kutoka nchini Sri Lanka mwishoni mwa mwaka 2003, ieleweke kwamba tunao nzi wa asili ambao nao walikuwa tatizo kwenye maembe lakini uharibifu wao ulikuwa kati ya asilimia tano hadi kumi kiwango ambacho hakikuwa na athari kubwa kwa wakulima kwa sababu machungwa na maembe hayakutumika kama zao la kibiashara kwa wakati huo,” 

Akielezea kuhusu nzi huyo alisema, hutaga mayai ndani ya tunda ambayo baadaye hugeuka funza wanaoishi kwa kula nyama ya tunda hilo na kusababisha tunda kudondoka kabla ya kukomaa.

Dk. Seguni alisema jitihada za utafiti huo ikiwemo elimu kutolewa kwa wakulima wa matunda zimeleta mafanikio makubwa katika kumdibiti nzi huyo na sasa uharibifu kwa msimu umekuwa kati ya asilimia 10 hadi 20.

Awali, Mkuu wa wa mkoa wa Tanga, Magalula Said akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda aliwataka wakulima kuendeleza usafi wa mashamba na kuziagiza Halmashauri husika kutenga bajeti kwa ajili ya kununua sumu ya kuangamiza Nzi Wavamizi ambayo itauzwa kwa wakulimwa kwa bei nafuu.
  • Taarifa ya Anna Makange

Mbatia na Mrema wakutana Kanisani Mamba Kotela katika kumbukumbu ya Askofu Stephano MoshiMbunge wa kuteuliwa na rais,Jmaes Mbatia akizungumza jambo na mbunge wa jimbo la Vunjo, Augustino Mrema mara baada ya kukutana kwa mara ya kwanza jimboni humo katika ibada ya kumbukumbu ya Askofu wa kwanza wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini iliyofanyika mwishoni mwa wiki.Kanisala la KKKT, Usharika wa Mamba Kotela ilokofanyika ibada hiyoMbunge Mbatia akiingia Kanisani humo.Ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshi unaofanyika kando ya Kanisa la usharika huo.Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bishop Moshi wakiwa katika ibada hiyo.Viongozi mbalimbali wa dini pia walikuwepo.

Mbunge Mrema akiwa ameketi na mbunge mwenzake Mbatia wakifuatilia ibada hiyo.

Askofu mstaafu Dkt Martin Shao akizungumza wakati wa ibada hiyo.

BabaAskofu Dkt Frederick Shoo akiongoza ibada hiyo ya kumbukumbu ya miaka 29 ya kifo cha aliyekuwa askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini, Stephano Moshi.

Askofu mstaafu Dkt Erasto N. Kweka akimzungumzia marehemu Baba Askofu Stephano Moshi jinsi alivyo mfahamu.

Baba Askofu Dkt Shoo akitoa hotuba yake.Ikafika wakati wa kuchangia ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshi na aliyealikwa mwanzo alikuwa ni Mbunge wa jimbo hilo Dkt Mrema.Dkt Mrema akimtizama mkewe Rose Mrema wakati akitoa pesa kwa ajili ya mchango wa harambee ya kuchangia taasisi hiyo ambapo alitoa kiasi cha sh 500,000/=Baadae ikafika zamu ya Mbatia ambaye alipata nafasi ya kuzungumzakido huku akieleza kuwa tayari amekwisha changia kiasi cha Sh mil 10/= kwa ajili ya shule ya sekondari ya Bishop Moshi na pia alitoa kiasi cha sh mil 2/= kwa ajii ya ujenzi wa taasisi hiyo.Baba Askofu, Dkt Shoo akimhukuru Mbatia kwa mchango anaoendelea kutoa kwa kanisa.

Baba Askofu Dkt Shoo akizindua rasmi jengo la kuweka kumbukumbu za Askofu wa Kwanza wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Stephano Moshi.

Baba Askofu Dkt Shoo akiingia katika jengo hilo.Baba Askofu Dkt Shoo akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu.Askofu mstaafu, Dkt Martin Shao akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu.

Baba Askofu, Dkt Shoo akiweka shada la maua katika kaburi la askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini na kufanya maombi katika kaburi hilo.Mbunge wa kuteuliwa na rais, James Mbatia akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu ya askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaslazini mStephano Moshi .

Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia akiweka shada la mauakatika kaburi la Askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya kasakzini ,hayati Stephano Moshi.Mbatia akizungumzajambo na askofu msataafu Dkt Martin Shao mara baadaya kumalizika kwa ibada hiyo.
Maaskofu wastaafu, Dkt Erasto Kweka na Dkt Martin Shao wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumbu kumbu ya Askofu wa kwanza wa KKKT, Stephano Moshi.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga

Uingereza imefanya uchaguzi mkuu - Tanzania twajifunza nini?

Sehemu ya Tatu
Sehemu ya pili ya makala hii nilionesha mambo mawili makubwa, moja ni  umuhim wa siasa na uongozi wa serikali ya Uingereza kwa nchi kama Tanzania na kwa jinsi gani tunaathirika kwa njia moja au nyingine na aina ya uongozi ulioko. Pili nilionesha mambo kadhaa kuhusu kampeni za uchaguzi wa Uingereza ambayo twaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu hawa na kuzifanya kampeni zetu za uchaguzi mkuu kuwa na tofauti na mazoea yetu. Leo nataka niongelee jambo la mwisho ambalo twaweza kujifunza  na ambalo nimeamua kulipa uzito wa kipekee kutokana na umuhim wake. Nini chanzo cha sera tunazouziwa na wanasiasa wakati wa kampeni?

Wazanzibari Canada wachangia walioathiriwa na mvua Tanzania

Wanajumuiya ya ZANCANA katika picha ya pamoja baada ya ibada ya dua maalum ya kuwaombea walioathirika na mvua za masika nchini Tanzania

Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Canada (ZANCANA), imechangisha zaidi ya Dola 1500 za Canada kwa ajili ya waathirika wa hali ya hewa nchini Tanzania.

Katika taarifa yake ambayo Swahilivilla imeipata nakala yake, ZANCANA imesema kwamba mnamo tarehe 9 Mei, 2015, jumuiya hiyo iliandaa mkutano maalum wa wanachama wake katika jiji la Toronto nchini Canada.

Mkusanyika huo uliofanyika katika ukumbi wa ZANCANA, ulifunguliwa kwa ibada maalum ya kuwaombea na kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki waliokumbwa na maafa ya hali ya hewa katika maeneo ya Pemba, Unguja na Dar-es-Salaam.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, baada ya ibada, mawaidha na dua, kilifuatia chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya uchangishaji wa fedha kwa lengo la kuwasaidia wahanga wa mvua za masika katika maeneo ya Unguja na Dar, na waathirika wa kimbunga katika eneo la Kisiwapanza kisiwani Pemba.

Taarifa ya ZANCANA imemalizia kwa kusema kuwa, bado michango inaendelea kupokelewa, na kuwaomba wale wote wenye moyo na uwezo kuchangia kwa kupitia accounti inayopatikana katika tovuti yao ya www.zancana.org

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na SwahiliVilla blog

Hotuba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mei 12, 2015

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akilihutubia Bunge
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akilihutubia Bunge

HOTUBA YA KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE.FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9), ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Mwaka 2013)
_________________________________

Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni Mei 12, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia Bungeni siku ya Jumanne, Mei 12, 2015
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia Bungeni siku ya Jumanne, Mei 12, 2015

UTANGULIZI


1.            Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba kutokana na Taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2014/2015 na Mwelekeo kwa Mwaka 2015/2016. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mafungu ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka 2015/2016.

Bunge la Bajeti 2015/2016
Maelezo ya Dismas Lyassa: Nia rasmi ya kugombea Ubunge Kilombero

Kutokana na magari kusitisha shughuli zao kutoka Ifakara kwenda vijijji mbalimbali vya Kilombero wananchi wengi wamekuwa wakitembea kwa miguu kama hivi, hapa ilikuwa ni eneo la Ihenga linalounganisha kata za Mofu na Ifa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Wanahabari

Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.

Nimekuwa nikitembelea vijiji na kata mbalimbali za Wilaya ya Kilombero. Hivi karibuni nilitembelea kata zote za wilaya, nilizungumza na wananchi, wengi wao walinishauri kugombea Ubunge. Wananchi wanaamini kuwa kwa pamoja tutaweza kuendeleza vema gurudumu la maendeleo kwa kasi zaidi.

Wananifahamu kama mtoto wa masikini mwenzao niliyewahi kuzunguka mitaani kupiga picha ili kuendesha maisha, mtoto wa masikini niliyewahi kuwa na ofisi ya kusafisha viatu vya watu eneo la Ubungo Maziwa kwa mzee Mrisho ili niweze kupata nauli ya kwenda shule wakati huo nasoma Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Maisha nayafahamu vizuri na nina uchungu nayo, natamani kushirikiana na wananchi ili kuepukana na maisha duni. Katika maisha yangu kutokula au wakati fulani kutembea kwa miguu kwenda chuo CBE na kurudi nyumbani Ubungo Maziwa (nilikuwa naishi kwa dada), lilikuwa ni jambo la kawaida, kwani maisha yalikuwa magumu mno.

Sauti ya wananchi wa Kilombero

Kilio cha wananchi pamoja na mambo mengine ni kwamba wanahitaji kiongozi kijana mwenye nguvu za kuongoza, kiongozi mwenye ujuzi wa namna ya kuongoza na kutawala, kiongozi ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. Kiongozi ambaye anajua namna ya kuongoza, siyo namna ya kuhonga au kuwalisha yamini wapiga kura, kwani wanachohitaji watu wa Kilombero ni maendeleo, siyo zaidi. Hawahitaji kiongozi ambaye ni maarufu kwa kutembelea magari ya kifahari, wanahitaji huduma za kijamii kama shule, hospitali na wao wenyewe kusaidiwa namna ya kubuni miradi ya maendeleo.

Elimu yangu ya juu ni Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala (Postgraduate Diploma in Leadership and Governance), kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma-Dar es Salaam niliyohitimu Aprili 22, 2014. Hata hivyo nje ya elimu nimekuwa nikishughulika na masuala ya kijamii kupitia kufanya mikutano ya ana kwa ana na jamii katika masuala ya ujasiriamali, uchumba/ndoa na kadhalika.

Mojawapo sababu za wananchi kuamini kwamba ninaweza kushirikiana nao kwa ufanisi ni rekodi ambazo wananchi wenyewe wanazo juu yangu, kwani nimekuwa nao karibu katika mambo mengi ya maendeleo ikiwamo kushirikiana nao moja kwa moja au vikundi vyao hasa vya walemavu, kina mama, vijana na kadhalika kama mshauri wao katika suala zima la namna ya kuviendesha na kuwaunganisha na taasisi au watu wa kusaidiana nao.

Kwa hivi sasa maeneo kadhaa ya Kilombero yanasaidiwa na mashirika mbalimbali yakiwamo ya nje, baadhi yake ni kutokana na jitihada zangu….nje ya uandishi wa habari, pia nimekuwa nikimiliki kampuni ya kuwaunganisha watu na vyuo vya nje ya Global Source Watch (GSW), ambayo imekuwa ikinipa fursa ya kujuana na watu wengi wa nje.

Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo
-(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Mofu, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Juni 26, 1976. Nimewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi ikiwamo the Guardian Limited kama mwandishi wa kujitegemea, Uwazi kama Mhariri, Leo ni Leo kama Mhariri wa Makala, Mwananchi kama Mwandishi wa makala baadaye mhariri wa jarida la ndani ya biashara, the Media Project (Marekani) kama mchangiaji nk.

Kwa sasa ni Kiongozi wa Utafiti hapa nchini (National Lead Researcher) wa taasisi ya kimataifa iitwayo Global Integrity yenye makazi yake Marekani, pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanahabari, lakini maamuzi haya ya kugombea ubunge ni yangu binafsi hayana uhusiano wala hayataingiliana na sehemu yoyote ninayofanyia kazi.

Nimewahi kutembea katika nchi mbalimbali kwa lengo la kwa kusoma na kutembea, baadhi yake ni Marekani, Kenya, Uganda, Dubai, Thailand, India.

OMBI KWA WASAMARIA WEMA

Napenda kuchukua fursa hii pia kuwaomba wasamaria wema kuangalia namna ya kusaidiana na wananchi wa Kilombero kwani wakati huu njia nyingi hazipitiki kwa sababu barabara zimejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Magari yamekuwa hayapitiki katika maeneo mengi ya Kilombero kwa sasa.

Kwa mfano sehemu kubwa ya barabara ya kutoka Ifakara kwenda Mofu haipitiki, kiasi kwamba wagonjwa wamekuwa hawawezi kubebwa kupelekwa Ifakara ambako ndiko pekee kuna hospitali ya Wilaya, St Francis. Wapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakibebwa kwa kutumia baiskeli na hata pikipiki, jambo ambalo limekuwa gumu hasa kwa wajawazito.

Magari ya abiriia hasa Noah zilizokuwa zikifanya safari kutoka na kuingia Ifakara kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Kilombero yamesitisha safari kutokana na barabara kujaa maji. Yapo magari machache hasa ya mizigo ambayo nayo yanafika baadhi ya vijijini kwa shida yakiwa yamebeba mizigo na abiria hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi.

Mvua zimeathiri pia kilimo, kwani mashamba mengi yamefurika maji, huku kukiwa na njaa kwa baadhi ya wanavijiji. Hivyo nachukua fursa hii kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kusaidia wananchi wakiwamo wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mlimba, Chisano, Chita, Mkula, Sanje, Uchindile na Utengule

Imetolewa leo tarehe 12, Mei 2015,

na Dismas Lyassa
(Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM)
0754 49 8972/0712183282


Dismas Lyassa akizungumza na baadhi ya vijana katika kijiji cha Ihenga ambao wamekuwa wakifanya shughuli za kuvusha watu baada ya barabara kujaa maji, picha ya mpiga picha wetu

Dismas akiteta na jambo na mkewe Rightness, nyuma ni mtoto wao Grace, picha na mpiga picha wetu

Inspekta wa Polisi atoa ushahidi katika kesi ya mauaji ya albino

SHAHIDI wa sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa ushahidi wake leo hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Mbele ya Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014, shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na mawakili wa serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.

Hata hivyo, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya vidhibiti kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi hilo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.

Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.

Daniel Mbega,
brotherdanny.com
Mwanza

Majambazi Ruvuma yapora Wavietnam milioni 42/=

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi limevamia jengo la kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL lililopo Msamala manispaa ya Songea mkoani Ruvuma na kuwajeruhi walinzi wawili kwa kuwapiga na kuwanyang’anya silaha aina short gun kisha kupora pesa taslimu shillingi milioni 42 mali ya kampuni ya VIETTEL.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tuko hilo lilitokea jana majira ya saa 8:45 usiku ambako walinzi wawili wa kampuni ya ulinzi ya Lukuba walikuwa wanalinda jengo ambalo wafanyakazi wa VIETTEL wanaishi.

Alisema kuwa walinzi hao wakiwa eneo lao la kazi walipigwa kwa kutumia vipande vya nondo vilivyowajeruhi kichwani. Kisha, majambazi hayo yaliingia ndani kwenye vyumba wanapoishi maafisa ambao ni raia Vietnam na kuwanyang’anya kitita cha fedha zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya nyumba hiyo kabla ya kukimbia na kutokomea kusikojulikana.

Aliwataja walinzi walionyang’anywa silaha wakiwa lindoni kuwa ni Joseph Ndunguru (23) mkazi wa eneo la Bombambili, Songea na Joseph Goliama (31) mkazi wa Mahenge, Songea. Maafisa wa kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL ambao wote ni raia wa Vietnam kuwa ni Vubach Khiem (31), Trandinh Nhat (32), Nguyen Minh Hoan (30), Le Then Phuoc (34) na Nguyen Van KhoI (55).

Alisema kuwa majeruhi walitibiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Songea na baada ya kuruhusiwa, hivi sasa wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
  • Taarifa ya COSMAS MULIRIYE, SONGEA via Demasho News

Rais Kikwete ateua Mkurugenzi Upelelezi na Idara ya Intelijensia ya Jinai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).

Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.

Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015.

Verizon buys AOL for $4.4 billion


The strongest mobile network in the USA and one of the top broadband providers Verizon Communications says it will buy the online pioneer American Online (AOL) for about $4.4 billion. The transaction will be completed this summer, and AOL will become a wholly owned subsidiary of Verizon [click here for Verizon's full statement and here for AOL memo].

It looks like Verizon is banking on the idea that, instead of watching Tv, people stream more media online using portable gadgets thus supplying content as it can through AOL will increase advertisement and revenue. 

AndroidPolice notes: 
But it's not really the content that Verizon wants. It's the advertising business. AOL makes money through traditional banners as well as ads embedded into video, including those streamed on mobile devices. Under CEO Tim Armstrong, a former Google sales executive who will stay on board following the acquisition, AOL introduced an automatic platform that allows marketers to bid on ad space. The company has since seen continued revenue growth.

AOL shifted from providing Internet to a media giant. It owns The Huffington Post, Engadget, TechCrunch, AOL.com amongst many other sites.

Rais Kikwete arejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara Algeria

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers Jumatatu May 11, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga wenyeji wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers Jumatatu May 11, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Marubani na Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Tassili la Algeria baada ya kuwsili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi alipowasili kutoka Algeria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salam Suleiman Kova, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda alipowasili kutoka Algeria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria.
Picha taarifa: Ikulu