Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 14, 2015
Ofa ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa watalii wa ndani Afrika Mashariki

Ukiwa katika hifadhi hiyo utafurahia mandhari mbalimbali za mlima Kilimanjaro

IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani ya kipindi cha miaka 10 huku asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni wazawa.

Asilimia hiyo inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda Mlima huo kwa muda wa siku moja hali inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi zetu ili kujionea urithi tuliopewa na Mungu.

Mhifadhi utalii wa KINAPA,Eva Mallya alisema katika kuhamasiosha utalii wa ndani ,KINAPA imeandaa zoezi maalumu ambalo litadumu kwa muda wa siku nne kwa watanzania walio walio karibu na mlima kuweza
kuupanda kwa muda wa siku moja na kurudi.

“Tumeandaa zoezi rahisi kwa kila mmoja mwenye nafasi aweze kupanda,sehemu kubwa itakuwa ni kwa kutumia gari ambapo walio tayari watachukuliwa na gari hadi eneo fulani kabla ya kutembea umbali mdogo na kutizama uwanda wa Shira katika mlima Kilimanjaro.”alisema Mallya.

Alisema zoezi la uandikishaji kwa ajili ya watakao penda kupanda katika mlima huo tayari limeanza katika vituo vilivyoko jirani na Duka la Maua mkabala na Rafiki Supermarket ,Hosptali ya rufaa ya KCMC na njia Panda ya Himo.

Mallya alisema mpandaji atapaswa kujitegemea kwa Sweta na Jacket kwa ajili ya baridi ,suruali raba pamoja na chakula huku mhusika akitakiwa kulipia kiasi cha sh 15,000 kama kiingilio cha hifadhini.

Kwa upande wake afisa masoko wa KINAPA,Antypas Mgungusi alisema safari ya kupanda mlima Kilimanjaro imekuwa ikitumiwa na baadi ya watalii kufanya matukio ya kihistoria ikiwemo kufunga ndoa na wengine
kuadhimisha siku zao za kuzaliwa wakiwa kileleni.

“Imezoeleka kuwa watu wanapokuwa na matukio yao yakiwemo ya mikutano,au Honey moon baada ya ndoa na siku za kuzaliwa wamekuwa wakifanya sherehe zao mijini,lakini kuna maeneo mengine kama haya ya
hifadhi kufanyia mambo hayo”alisema Mgungusi.

Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kwa kuhifadhi barafu kwa kipindi cha mwaka mzima licha ya kupitiwa na mstari wa Ikweta huku ukiwa ndio mlima pekee uliosimama peke yake ukilinganisha
na milima mingine duniani.

Mhifadhi utalii katka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akizungumza juu ya ofa iliyotangazwa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima huo kwa siku moja na kurudi hadi kilele cha Shira.

Afisa masoko wa KINAPA, Antypas Mgungusi akisistiza jambo wakati akizungumzia juu ya ofa ya safafri ya kupanda Mlima Kilimanjaro huku akishauri wenye sherehe zao kutumia nafasi hiyo kupanda Mlima huo kwa ajili ya kufanya sherehe zao,alitaja sherehe ambazo zinaweza fanyika katika hifadhi hiyo ni pamoja na wale wenye kukumbuka siku zao za kuzaliwa wanaweza fanya hivyo wakiwa kileleni,lakini pia kwa wale wanaoenda Honey Moon baada ya ndoa pia wameshauriwa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha ofa.Baadhi ya watalii wa ndani wakielekea katika kilele cha Shira safari ambayo inatajwa asilimia 70 wanaenda kwa usafiri wa gariWengine wanaweza pia kupanda na watoto wao.Hivi ndivyo safari ya mwisho huwa.Njiani utakutana na uoto mbalimbali wa asiliZipo tenti kwa ajili ya watalii wanaoendelea na safari.Waliofanikiwa kufika kilele cha Shira hawakusita kuonesha furaha zao kwa kucheza .

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga


Tume ya mipango yatembelea Bandari ya Salama


Pichani ni meli ikipakua shehena ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.


Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.


Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Wapili Kushoto) akizungumza wakati ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) na wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.


Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Ugeni huo uliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto).


Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya upakuaji wa mafuta kwa ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.


Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza wakati walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.


KILIFAIR 2015 - Kilimanjaro Tourism & Industry Fair


KILIFAIR 2015 is here with over 140 exhibitors from Tanzania, Zanzibar, Kenya and more. The fair has the character of a networking event for the tourism industry, in combination with a community fair to attract local people, families & expats. Get to enjoy the international food court, cultural maasai dances, African art & crafts and may more. Also get to participate on the 5 km/ 10 km Moshi Club FUN RUN for 5,000 Tsh.
Entrance: 1 day ticket 6,000 Tsh (3000 Tsh kids) | 3 day ticket 12,000 Tsh

When: 5th- 7thJune 2015 
 
Where: Moshi Club Ground, Moshi

For more, visit: www.kilifair.de

Mbeya Urban tops districts in EA for learning; Kenya outperforms Tanzania, Uganda

Top district in East Africa for learning outcomes is Mbeya Urban in Tanzania, but overall Kenya outperforms Tanzania and Uganda
Assessment reveals wide disparities within and between countries

13 May 2015, Dar es Salaam, Kampala, Nairobi: Many children across East Africa are not learning basic literacy and numeracy skills. Only two out of ten pupils (20%) in the third year of primary school can read and do basic mathematics at Standard (or Grade) 2 level. By the time they reach the last year of primary school, one out of four East African children (24%) still have not acquired these skills.

These findings were released by Uwezo, a program of Twaweza, in a report entitled Are our children learning? Literacy and numeracy across East Africa. Data on learning outcomes, school conditions and households were collected in 2013 in every district across the region through citizen-led household-based assessments. Learning outcomes are assessed among children aged 6 to 16 through tests set at Standard (or Grade) 2 level.

When considering all children aged 10 to 16, whether in or out of school, results are also poor. In Kenya 64% passed both one literacy and a numeracy test, in Tanzania 48% and in Uganda 36%. This means that, even in Kenya, the best performing country, less than 7 out of 10 of all children (aged 10-16) have mastered Grade 2 literacy and numeracy skills.

The best performing district in East Africa is Mbeya Urban in Tanzania. However the rest of the top ten is populated by Kenyan districts, which dominate the upper ranks. Tanzanian districts tend to fall in the middle ranks and Uganda districts are consistently ranked near the bottom. The best performing Ugandan district is ranked 82 in the region. Seven out of the bottom ten places are taken up by Ugandan districts.

Wealth also appears to influence learning outcomes: in all three countries, there are large gaps between different wealth groups.
·         In Kenya, seven out of ten pupils aged 10 to 16 (70%) in non-poor households, and four out of ten pupils (44%) in ultra poor households passed one literacy and numeracy test
·         In Tanzania, just under six out of ten pupils aged 10 to 16 (55%) in non-poor households, and four out of ten pupils (39%) in ultra poor households passed one literacy and numeracy test
·         In Uganda, four out of ten pupils aged 10 to 16 (42%) in non-poor households, and two out of ten pupils (24%) in ultra poor households passed one literacy and numeracy test
Despite the larger disparities in Kenya, ultra poor households in the country still, on average, perform better than non-poor households in Uganda.

The report also shows that learning outcomes have stagnated since Uwezo began collecting data in 2009/2010. East African children continue to face a crisis in the education system with no significant changes in learning outcomes over the last four years (up to 2013). Enrollment trends are similarly unmoving but have been high since the introduction of universal primary education in the three countries.

Uwezo metrics are used to assess progress against the Education for All goals. These goals were agreed with a 15-year timeframe in 2000 and cover both access to and quality of education. Overall, there are no significant changes in any of the metrics used to assess the goals in the four years that Uwezo data have been collected. However, enrolment is high with all three countries having over 90% enrolment rates. Similarly gender parity has been achieved in the three countries in terms of access and quality. There are no marked differences in access to schooling between boys and girls. Sadly boys and girls perform equally poorly in terms of learning outcomes. However these are national averages and so conceal geographical variation. Similarly, they do not consider any gender differences in primary school completion or secondary school enrolment.

The three East African countries remain a long way from “recognized and measureable learning outcomes [being] achieved by all.” However, children do seem to be learning general knowledge or life skills: in all three countries, by the fourth round of data collection (2013), at least nine out of ten children could answer the bonus general knowledge question.

Dr John Mugo, Director of Data and Voice at Twaweza observed “The large disparities between and within countries, particularly along socio-economic lines, suggest that the region may be becoming more divided. In addition the lack of meaningful improvements in learning outcomes over the three rounds of Uwezo assessments point to a lack of strong action to tackle our education crisis.”

Aidan Eyakuze, Executive Director of Twaweza, added “The progress made to increase access and gender parity is to be commended. However we must ensure that the national figures do not hide local variations. Although this does not mean we need to abandon or ignore access issues, these data clearly show that the core focus for East African education over the coming years should be about quality and ensuring that children are in school and learning.”

Uwezo assessed more than 325,000 children aged 6 – 16 in just under 150,000 households in 366 districts in Kenya, Tanzania and Uganda. In addition data were collected from over 10,000 public primary schools.
---Ends---
The full report, including samples of the tests used, is available at www.twaweza.org

Kiwango cha chini cha pensheni Zanzibar kuwa shilingi elfu sitini

Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee akionesha Mkoba wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 jana katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Unguja, Zanzibar.

Hayo yamesemwa katika sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha wa Zanzibar kama ifuatavyo:

73. Mheshimiwa Spika, kundi jengine muhimu kwa jamii yetu ni Wazee. Kundi hili pia lilipewa umuhimu maalum tokea Mapinduzi yetu matukufu kwa kupatiwa makaazi na matunzo maalum. Taarifa ya Sensa ya mwaka 2012 inaonesha kuwa Wazee waliofikia miaka 65 na zaidi ni asilimia 2.8 ya watu wote wa Zanzibar. Hawa ni wazee wetu ambao wameshatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu, ulezi wa vijana na watoto na sasa wamefikia umri wa kusaidiwa. Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wazee wanaohitaji msaada wa matunzo ya Serikali imekuwa ikipungua kutoka Wazee 223 mwaka 2010 hadi Wazee 148 mwaka 2015. Hali hii inamaanisha kuwa wengi wa Wazee wetu wanatunzwa na jamii, hasa watoto na jamaa zao. Baadhi ya Wazee hawa ni wale waliotumikia Serikali wakati wa ujana wao na kwa sasa ni Wastaafu na wanategemea kipato cha Pencheni.

74. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko ya udogo wa kiwango cha chini cha Pencheni kinachotolewa sasa. Serikali iliahidi kukiangalia kiwango hicho kwa kadiri hali itakavyoruhusu hasa kwa kuzingatia kuwa mara kadhaa kumekuwa na marekebisho ya mishahara kwa Wafanyakazi wa Serikali ambayo hayakuhusisha pencheni.

Kwa mwaka wa fedha 2015/16, Serikali inakusudia kupandisha kiwango cha chini cha pencheni kutoka TZS 40,000 kwa mwezi za sasa hadi TZS 60,000.

Marekebisho haya yamelenga zaidi kwa wale ambao wanapokea kiwango cha chini cha pencheni.

75. Mheshimiwa Spika, baadhi ya nchi duniani zina utaratibu wa kulipa pencheni kwa wazee hata kama sio wastaafu wa Serikalini. Katika nchi za jirani kama vile Mauritius , utaratibu huu umetumika kwa miaka kadhaa sasa. Serikali kwa kusaidiana na Taasisi ya kuwasaidia Wazee ya "Help Age International" imefanya utafiti na kuzingatia uzoefu wa nchi nyengine katika kutunza Wazee. Kwa sasa Serikali inakamilisha taratibu za kuwatambua Wazee wote waliofikia miaka 70 na zaidi kwa lengo la kuwapatia vitambulisho vyao pamoja na taratibu nyengine. Zoezi hili litachukua sio zaidi ya miezi 10.

Nina furaha kulitangazia Baraza lako tukufu kuwa kuanzia tarehe 1 April mwaka 2016, Serikali itaanza kulipa pencheni kwa Wazee wote waliofikia umri wa miaka 70 (universal pension).

Pencheni hiyo itatolewa kwa Wazee waliofikisha umri huo bila ya kujali kipato chake na italipwa kwa kiwango cha TZS 20,000 kwa mwezi. Jumla ya TZS 1.65 bilioni zinatarajiwa kutumika kwa ajili hiyo.

Hotuba nzima inapatikana katika tovuti ya Baraza la Wawakilishi: www.zanzibarassembly.go.tz

Balozi mpya wa Malawi nchini Marekani atembelea Ubalozi wa TanzaniaBalozi mpya wa Malawi, Mhe. Nector Mhura akipokelewa na Afisa ubalozi Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi.Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Malawi Nector Mhura.Balozi wa Malawi nchini Marekani akiweka saini kwenye kitabu maalum cha wageni.


Balozi wa Malawi nchini Marekani, Mhe. Nector Mhura akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha.Balozi wa Malawi nchini Marekani, Mhe. Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya.Balozi wa Malawi nchini Marekani, Mhe. Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya, kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Liberata Mulamula na Afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme.


Picha: Kamera ya Ubalozi.

Sehemu ya III ya kipindi cha ‘UBISHI’

Wiki hii bwana Costantine Magavilla anaongelea maana nyingine ya shule. Je unajua maana nyingine ya shule zaidi ya kusoma. Pata undani kwa kutembelea www.magavilla.com videos au kwa kubofya pleya hapo chini.
Usikose kufuatilia vipindi hivi vinavyolenga kuelimisha, kukuhamasisha utazame upya maisha yako upateujasiri wa kubadili fikra na kufanya yako kila wiki siku ya Jumanne.

Bwana Costantine Magavilla ni mwandishi wa kitabu kiitwacho Life and You  na ni mhamasishaji maarufu Tanzania katika makongamano mbalimbali kuhusiana na maendeleo binafsi na mabadiliko ya kibiashara. Ni mdau mkubwa wa masuala ya masoko hususan katika kutangaza biashara na miongoni mwa kazi zake ni kuwahamasisha vijana kujituma na kuchangamkia fursa.

Mwisho wa taarifa.

Imetolewa na Mancom Limited kwa mawasiliano zaidi tuandikie kupitia

[email protected] au [email protected]

Imetolewa Mei 13, 2015

Mgahawa wafungwa kwa kuuza nyama ya binadamu

Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa baada ya viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.

Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruzika damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo, pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!

Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya nailoni "Rambo".

Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo, seti ya maguruneti na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.

Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo, watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka, hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.

Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .

Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema, baada ya kupata staftahi, akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili u nusu alistaajabu mno. "Sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila," na kwamba ilikuwa ghali sana.

Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binadamu tu.

[video] EAC Summit discussion on the situation in Burundi

Serukamba alianzisha upya Bungeni sakata la "Escrow"

Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) amefufua bungeni kashfa ya uchotwaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow kiasi cha shilingi bilioni 306, iliyofunguliwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akisema, hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo ni ubaguzi na usanii usikubalika.

Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2015/16, katika eneo la utawala bora, Serukamba amesema: 
“hii staili inayojaribu kutumika ni ya kizamani ya kusafisha watu kiaina, imepitwa na wakati”.
“kama Balozi Sefue anasema Maswi na mawaziri hao ni safi, basi atwambie Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), Prof. Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), William Ngeleja (Geita), uchafu wao ni upi wakati walipata mgawo halali?

Chenge, Ngeleja na Victor Mwambalaswa (Lupa), walivuliwa uenyekiti wa kamati za Bunge baada ya kuthibitika kuwa walipokea mgawo wa fedha hizo kutoka kwa mmoja wa wamiliki wa IPTL, James Rugemalira bila kutangaza maslahi kama sheria ya maadili ya viongozi wa umma inavyotaka.

Katika mtiririko huo, mawaziri Tibaijuka, Muhongo na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema walijiuzulu kutokana na kashfa hiyo huku baadhi ya watendaji katika mamlaka mbalimbali za serikali wakifikishwa mahakamani na kwenye Baraza la Sekretarieti ya Viongozi wa Umma.

Akizungumza kwa masikitiko kuhusu uamuzi huo wa Ikulu, Serukamba alishauri kuwa, 
“Chenge, Ngeleja, Werema, Mwambalaswa na mawaziri wengine waliowahi kujiuzulu kama sehemu ya uwajibikaji nao wasafishwe na kurudishwa katika nafasi zao.”
“Bunge hapa tuliomba ripoti ya oparesheni tokomeza lakini haijawahi kuletwa ila anajitokeza katibu mkuu kiongozi kusafisha baadhi ya watu. Huu ni usanii wa kuwasaidia watu wachache na kuumiza wengine kwa malengo binafsi. Hatuwezi kuwa na serikali yenye “double standards”.
“Lazima wakina Chenge, Tibaijuka na wengine wote mawaziri waliojiuzulu huko nyuma kwa kashfa ya Richmond nao waundiwe tume wasafishwe kama wakina Maswi, vinginevyo mna ajenda binafsi ya kujisafisha,”
amesema.

Serukama ameongeza kuwa, wako watumishi wa Ikulu wenye tuhuma za escrow lakini bado wanaendelea kubaki kazini huku watumishi wengine wa umma katika taasisi nyingine wakifikishwa mahakamani kwa jambo hilohilo na hivyo kuhoji:
“hii ni serikali gani yenye ubaguzi wa aina hiyo?
Kama ni kuunda Judicial Inquiry (Tume ya Kimahakama), basi ifanyike kwa watuhumiwa wote. Hiki si Chama Cha Mapinduzi tunachokijua. Sasa kinachofuata hata hao mliowapeleka mahakamani kwa suala hilo watawashinda kutokana na uamuzi huu wa kusafisha baadhi ya watu.
“Katibu Mkuu Kiongozi anasema hiyo ripoti ya tokomeza hawezi kuileta bungeni badala yake anaisoma nusu nusu na kuwasafisha baadhi ya watu. Huu ni ubaguzi na labda tuambiwe kuna watu mnaowalenga lakini haitawezekana,”
alisisitiza Serukamba huku akishangiliwa.

Waziri wa Ulinzi auawa hadharani kwa tuhuma za uhaini

Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un aliamuru kuuawa kwa risasi Waziri wake wa Ulinzi kwa tuhuma za uhaini na kutomuheshimu, imesema leo Jumatano asubuhi Idara ya ujasusi ya Korea Kusini.

Kwa mujibu wa maafisa wa Upelelezi nchini Korea Kusini, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini, Hyon Yong-Chol, aliuawa mwishoni mwa mwezi Aprili mbele ya mamia ya viongozi vigogo wa Korea Kaskazini kwa kutumia bunduki inayodungua ndege ya kivita.

Waziri huo wa ulinzi aliteuliwa kwenye wadhifa huo mwaka mmoja uliyopita, na alituhumiwa na Kim Jong-un wa kukaidi amri zake katika maadhimisho ya kijeshi, na kutofuata maelekezo ya yake.

Tangu kifo cha baba yake Kim Jong-il na kuingia kwake madarakani mwaka 2011, Kiongozi huyo kijana wa Pyongyang ameripotiwa kuwanyonga baadhi ya washirika wake.

Jaribio la kumpindua Rais nchini Burundi

*UPDATE/TAARIFA MPYA:

Inaripotiwa kuwa uchaguzi mkuu wa Burundi umeahirishwa kwa muda usiojulikana. Vyama vyote vya siasa vya Burundi vitaitwa kujadili mezani kwa amani na kisha utaitishwa mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kupitia mapendekezo ya mkutano huo wa vyama vya siasa ili kufikia maafikiano.

 --- MWISHO WA TAARIFA MPYA ---

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.

Hayo yanajiri wakati Pierre Nkurunziza anashiriki Jumatano wiki hii mkutano wa kikanda wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Burundi.

Burundi imekua ikishuhudia maandamano ya raia wakipinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza. Kwa muda wa majuma kadhaa mitandao ya kijamii imekua imefungwa, lakini baada ya mapinduzi hayo mitandao hiyo imefunguliwa.

Kituo cha redio RPA ambacho kimekua kimefungwa tangu maandamano hayo yaanze, kimeanza kupeperusha matangazo yake baada ya mapinduzi hayo, hata redio za kibinafsi mbili ambazo ni Bonesha Fm na Isanganiro, ambazo matangazo yake yalikua hayasikiki mikoani na katika baadhi ya maeneo ya nchi jirani, kwa sasa matangazo ya redio hizo yanasikika.

Mapema Jumatano asubuhi, raia kutoka wilaya zote za mji wa Bujumbura walikua wakijaribu kuingia mjini kati Bujumbura, bila mafaanikio. Lakini kuna kundi la wanawake na wasichana ambao wamefaulu kuingia kwenye eneo la Uhuru mjini Kati Bujumbura.

Hata hivyo Ikulu ya rais imetangaza kupitia akaunti yake ya twitter kuwa mapinduzi hayo yamefeli, baada ya jeshi kuingilia kati na kudhibiti hali ya mambo. Hata hivyo raia wameingia kwa wingi mjini kati Bujumbura baada ya kusikia tangazo hilo, huku askari polisi wakionekana kuingia katika makambi yao.

Wakati huo huo wanajeshi wengi wameonekana wakiizingira redio na televisheni vya taifa pamoja na uwanja wa ndege wa Bujumbura.  [Taarifa ya RFI Kiswahili]


  • Taarifa ya picha ifuatayo ni kwa mujibu wa BBCKiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare
18:37 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ameamrisha wanajeshi kuzuia rais Nkurunzinza kutua Burundi

18:30 Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya kurejea kutoka Tanzania amesema msemaji wake Willy Nyamitwe.


Wananchi waendelea kusheherekea Bujumbura kufuatia tangazo la ''Mapinduzi''
18:25 Generali Niyombareh ametoa amri kwa majeshi kuungana na kulinda viwanja vya ndege kote nchini humo

18:20 Generali aliyeongoza ''Mapinduzi'' leo asubuhi amewataka maafisa wa jeshi na polisi kufanya kazi kwa pamoja ilikulinda usalama wa nchi hiyo.


Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza

18:15 Viongozi wa kanda ya Afrika wametaka makundi hasimu kutulia na kukubali hali ya kikatiba Kurejea

18:10 Esipisu amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta anaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba

Maafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura


18:07 Msemaji wa rais wa Kenya Manoah Esipisu amesema kuwa viongozi wanataka hali ya kawaida irejee huko Burundi


Rais Uhuru Kenyatta akiwa Tanzania

18:06 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

18:05 Rais amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:01 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.


Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''

18:01 Viongozi hao wanakutana dar es salaam kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi

18:01 Rais Jakaya Kikwete amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:00 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

17:55 Msemaji wa rais Nkurunzinza ameiambia BBC kuwa asilimia 95 ya taifa hilo ingali salama na wala hakuna tashwishi.


Manuari za kijeshi zingali barabarani mjini Bujumbura

17:50 Manuari zaidi zaonekana barabarani mjini Bujumbura

17:45 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.

17:30 Msemaji wa rais Nkurunziza,Willy Nyamitwe ameiambia BBC kuwa rais huyo angali madarakani na kuwa hajaondolewa madarakani


Raia wakiwazoma maafisa wapolisi ambao awali walikuwa wakikabiliana nao

17:22 Redio ya taifa ya Burundi inasema kuwa rais Nkurunzinza angali Madarakani na kuwa hakujakuwa na ''mapinduzi''


Raia wakikumbatiana katika bustani la uhuru Bujumbura

17:20 Maafisa wa jeshi wanaolinda kituo cha taifa cha redio wamewaonya watangazaji wasitangaze kuwa kuna ''mapinduzi''

17:05 Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema kuwa waandamanaji wamefululiza hadi kwenye vituo vya polisi na magereza yaliyokuwa na mahabusu waliokamata kwa kuandamana na kuwaachilia huru


Wanajeshi ya Burundi wakijaribu kutuliza hali Bujumbura

17:00 Redio ya taifa inasema kuwa bado rais Nkurunzinza angali madarakani.

16:50 Kituo hicho cha redio cha ''African Public Radio'' kinapeperusha tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya rais Nkurunzinza


Raia wanasherehekea ''kupinduliwa'' kwa Nkurunzinza

16:40 Redio iliyokuwa imefungwa na serikali ya rais Nkurunzinza kwa kupeperusha habari za maandamano imefunguliwa upya.

16:30 Mwandishi wa BBC Cyriac Muhawenay aliyeko Bujumbura anasema raia wanaonekana kuwa na furaha.

16:20 Picha za raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi


Vifaru vya kijeshi katikati ya mji mkuu Bujumbura

16:08 Watu wanaonekana wakininginia kwenye vifaru vya jeshi

16:05 Afisi ya urais nchini Burundi imetangaza kwenye mtandao wake wa twitter kuwa ''hali ni Shwari''


Raia wakishangilia ''mapinduzi''

16:00 Majeshi wameonekana nje ya kambi za kijeshi mjini Bujumbura

15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani.


Raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi Bujumbura

15:55 Mwandishi Sonia Rolley, wa Radio France International anasema kuwa halaiki ya raia wamefika nje ya kituo hicho wakishangilia matukio hayo


Waandamanaji Bujumbura

15:50 Waandamanaji wanasemekana kuambatana na wanajeshi kuelekea katikati ya mji mkuu wa Bujumbura

15:45 Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.


Waandamanaji Bujumbura

15:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Maud Julien anasema kuwa Miili ya watu watatu imeonekane katika barabara za Bujumbura

15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.


Raia wanashangilia mjini Bujumbura

15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea Burundi.

15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.


Maafisa wa jeshi la Burundi wanaonekana wakiweka usalama

15:20 Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.


Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu

15:05 Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madarakani.

Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi


Polisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.


Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh

Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.

Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.


Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.

Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''


Kwingineko:

  • Picha na video ya askari mwanamke akishambuliwa na raia (bofya hapa).
  • East African leaders condemn coup bid in Burundi at summit

DAR ES SALAAM (Reuters) - East African leaders condemned an attempted coup in Burundi on Wednesday by a general who declared that he had deposed President Pierre Nkurunziza for seeking to run for a third term in office.

The summit's host, Tanzanian President Jakaya Kikwete, made the statement after a meeting of leaders from the five-nation East African Community, which also groups Kenya, Rwanda, Uganda and Burundi. A Tanzanian Foreign Ministry official said Nkurunziza had not attended the discussions and had left Tanzania for Burundi.

Major General Godefroid Niyombare, who had declared he had deposed Nkurunziza, said in Burundi that the airport in the capital Bujumbura and other border crossings were closed.

(Reporting by Fumbuka Ng'wanakilala; Writing by Edmund Blair; Editing by Kevin Liffey)
2015-05-13 17:43:03