Tamko la Waziri Nyalandu kuhusu shutuma za Mbunge Nassari

Mhe. Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonjwa waliofuata huduma katika zahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru, alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu tozo ya ushuru wa magari na wagonjwa wanaopita katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini.

Nimesikitishwa sana na kauli ya Mhe. NASSARI ambayo ameongea kwa kudhalilisha utendaji wangu serikalini. Naomba Mh Nassari afahamu kuwa kunikashifu pasipo kueleza masuala ya kisera au ya kiutendaji ni kupungukiwa na busara ya kawaida kwa kiongozi aliyepaswa kuwawakilisha wapiga kura wake kwa hoja.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mh Nassari aliniita Jimboni kwake Arumeru Mashariki akiniomba nitatue tatizo lililohusu wananchi wa Jimboni kwake waliokuwa wanahitaji matibabu katika hospitali ambayo ilikuwa sharti upitie ndani ya hifadhi ili ufike kutibiwa. Nilikwenda kuwaona wagonjwa na kuitembelea hospitali hiyo na kulitatua tatizo hilo siku hiyo hiyo. Kwangu kama Waziri, halikuwa suala la kufanyia siasa suala la afya za watanzania, pamoja na yeye kuwa Mbunge wa upinzani.

Nilimheshimu na kukubali wito wake kwa niaba ya wananchi. Nimewatembelea na kuwatia moyo maaskari wetu nchi nzima na kuwapelekea vitendea kazi. Nimefurahi pamoja nao na kulia pamoja nao. Nimeenda kuwafariji Familia za wapiganaji wetu waliopoteza maisha kwa kuuawa wakilinda raslimali za Taifa, watu ambao Mh Nassari anawabeza. Tumepambana na ujangili na tunaendelea kuushinda. Tumeleta magari, silaha, ndege, helicopters, na raslimali nyingi ili kulinda raslimali za Taifa. Busara haisomewi ila ni kumshukuru Mungu akusaidie kujua matumizi ya ulimi. Nimesikitishwa sana na kauli za uongo na kuzusha za Mh Nassari.

Rais Kikwete 'amkaba' Makonda

Rais Kikwete alipozuru maeneo ya Tegeta na Mkwajuni jijini Dar es Salaam, 'amemkaba' kwa maswali Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitaka kujua hatua zinazochukuliwa kwa ajili ya kuyaweka vyema mazingira ya makazi ya wananchi Wilayani Kinondoni kutokana na athari za maji yaliyotokana na wingi wa mvua zinazonyesha.Jamani! Albino mwingine mtoto akatwa mkono Katavi


Jamaa amwambia Rais "nisaidie buku 2 tu Baba mzazi"


Katika dakika ya 1:25 umesikia maneno yaliyonong'onwa?


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 15, 2015
Taarifa ya msiba MDV na Tanzania

Rama Kamguna wa Beltsville, Maryland nchini Marekani anasikitika kutangaza kifo cha mpendwa mama yake mzazi kilichotokea mkoani Morogoro, Tanzania Mei 14, 2015.

Mipango ya mazishi inafanywa na marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu Mei 18, 2015.

Kupeana pole na kufarijiana ndio ustaarabu wetu, hivyo upatapo nafasi usisite kujumuika na mfiwa nyumbani kwake Beltsville, Maryland kwa anwani:

3588 Poweder Mill Road,
Apt # 301,
Beltsville, MD 20705.

Kwa maelekezo na maelezo zaidi unaweza kupiga simu

Rama Kamguna 202 459 3839

Ali 202 378 0095

---
Ujumbe kutoka kwa Luke Joe/Vijimambo blog

Utaratibu wa uteuzi wa wagombea ndani ya CHADEMA kwa Uchaguzi Mkuu 2015


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU

UTARATIBU WA UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza utaratibu wa uteuzi wa wagombea wake watakaokiwakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu. 

Aidha, kupitia mkutano na waandishi wa habari, Chadema pia imetangaza namna watia nia wa nafasi mbalimbali watakavyochukua na kurejesha fomu huku pia kikiweka wazi gharama za fomu kwa kila ngazi ya uteuzi yaani udiwani, uwakilishi, ubunge na urais 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalim amesema kuwa utaratibu huo wa uteuzi katika ngazi ya ubunge na uwakilishi utahusisha hatua tatu katika ngazi ya jimbo/wilaya husika na hatua moja katika ngazi ya kitaifa huku ule wa udiwani ukiwa na sehemu mbili katika kata na moja wilayani/jimboni.


“Kupitia mkutano wetu nanyi ndugu wanahabari, tunapenda kuutarifu umma wa Watanzania hususan wanachama wetu, wapenzi na wafuasi wote wenye sifa za kuwania uteuzi kupitia CHADEMA kuwa kwa kuzingatia matakwa ya katiba ya chama na kukuza demokrasia tukilenga kuhakikisha tunapata wagombea waadilifu, wenye uwezo wa kuwatumikia watu na wanaokubalika na wapiga kura, chama kimepanua wigo wa kupata maoni ya uteuzi,”alisema Mwalim.


Akirejea maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama kilichoketi Mei 3 na 4 jijini Dar es salaam, NKMZ Mwalim amesema kuwa chama kimepitisha utaratibu huo utakaotumika kupata maoni na hatimaye kufanya uteuzi wa wagombea watakaosimama kugombea nafasi hizo tajwa kupitia CHADEMA katika ushirikano wa vyama vinavyounda UKAWA.


Mwalim ameutaja utaratibu huo utakaotumika katika nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani, kuwa ni:

Ubunge/Uwakilishi

1. Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo

Mkutano huu utafanyika kwenye kila jimbo la uchaguzi na utafanyika siku moja kwenye eneo moja ambalo ni makao makuu jimbo au eneo ambalo litaamuliwa na vikao vya chama. 

Washiriki watatakiwa kuwapigia kura moja wagombea ambao wamejitokeza ndani ya chama na kura hiyo itakuwa ya siri .


NKMZ amesema kuwa wasimamizi wa mikutano hiyo maalum ya kura ya maoni watatakiwa kuwa watu ambao hawana ‘maslahi’ kwenye uchaguzi huo yaani wasiwe wagombea au wasiwe na mgombea ambaye wanamuunga mkono kati ya wanaogombea nafasi hiyo.


Kila mgombea atapewa fursa ya kujieleza mbele ya wapiga kura kwa dakika tano (5) na ataulizwa maswali yasiyozidi matatu kutoka kwa washiriki.


Kura zitapigwa mwishoni baada ya wagombea wote kumaliza kujieleza mbele ya Mkutano Maalum wa Kura ya Maoni , na kila mgombea atakuwa na haki ya kuweka wakala wa kuhesabu kura zake.
Matokeo ya kura hizi yatawasilishwa kwenye Kikao Cha Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya kabla ya kufanya kikao chake cha uteuzi.
Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Kura ya Maoni Jimbo/Wilaya :

(i) 
Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Jimbo
(ii) Wenyeviti wote wa kata za wilaya /jimbo
(iii) Makatibu wote wa kata za wilaya/jimbo
(iv) Makatibu waenezi wote wa kata za jimbo/wilaya
(v) Wenyeviti na makatibu wa Mabaraza yote ya Chama Jimbo/Wilaya
(vi) Wenyeviti wa Mabaraza yote katika Kata za wilaya/jimbo
(vii) Makatibu wa mabaraza yote ya kata katika jimbo/wilaya
(viii) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji, Mitaa na Vitongoji watokanao na Chama kwenye Jimbo.
2. Wagombea kujipigia kura wenyewe 

Wagombea wote wapewe fursa ndani ya Mkutano Maalum ya kujipigia kura wenyewe na kila mmoja apige kura tatu, kura moja iwe yake binafsi na kura nyingine mbili atakiwe kuwapigia wagombea wengine waliopo.
Matokeo ya kura hizi pia yatawasilishwa Kamati ya Utendaji na pia Ofisi ya Katibu Mkuu. 

3. 
Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya

Kamati ya Utendaji ya Wilaya /Jimbo itafanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 7.4.10 (q).
Kamati ya Utendaji itatakiwa kupiga kura za awali na kuwasilisha taarifa yake pamoja na Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba ya Chama kwa ajili ya uteuzi mwisho.
Utaratibu wa kuendesha vikao vya Kamati ya Utendaji Jimbo/Wilaya utazingatia Katiba na Kanuni za Chama.

Udiwani 

Katika nafasi ya udiwani Mwalim amesema kuwa kuwa utaratibu utakaotumika ni ule ule kama ilivyo katika nafasi ya ubunge isipokuwa hapa itakuwa katika ngazi ya kata kama ifuatavyo;

1. 
Mkutano Mkuu Maalum wa Kata/Wadi

Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Kura ya Maoni kata/wadi:


(i) 
Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Kata
(ii) Wenyeviti wote wa matawi katika kata
(iii) Makatibu wote wa matawi katika kata
(iv) Wenyeviti wote wa mabaraza ya wazee, wanawake na vijana katika kata
(v) Diwani wa Chama wa Kata/Wadi, Diwani wa Viti Maalum, Mbunge/Mwakilishi anayeishi katika kata husika.
(vi) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Wenyeviti wa Kamati za Mitaa au Shehiya wanaotokana na Chama katika kata.
(vii) Wenyeviti wa Serikali za Vitongoji, Mitaa na wajumbe wa serikali hizo katika kata wanaotokana na CHADEMA.
2. Wagombea kujipigia kura wenyewe

3. 
Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya
Mwalim ameongeza kuwa tofauti na kwenye nafasi ya ubunge na uwakilishi ambayo uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Kamati Kuu ya Chama, kwenye ngazi ya udiwani uteuzi utafanywa na Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA.

“Lakini pia hapa kwenye udiwani, mkutano mkuu maalum wa kata ambao utawapigia kura za maoni wanaowania uteuzi wa udiwani, mbali ya kujumuisha wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa, utahusisha pia wajumbe wote wa serikali katika vitongoji, vijiji na mitaa wanaotokana na CHADEMA katika kata husika. Unaweza kuona tunavyopanua wigo wa demokrasia.


“Jambo jingine ambalo tungependa kusisitiza kwa wote watakaojitokeza kuchukua fomu ni kuhakikisha wanazingatia utaratibu wa katiba ya chama, kanuni za uendeshaji chama na miongozo yetu na nyaraka mbalimbali za kiutendaji. Watambue kabisa kuwa kati ya mambo ambayo hatutakubali yatokee kwenye chama hiki ni vitendo vya rushwa kusaka nafasi. 

“Tumeshasema na tunarudia tena kusisitiza kuwa watoa rushwa na wapokea rushwa hawana nafasi ndani ya CHADEMA. Tumekuwa wakali katika hili. Yeyote atakayebainika kuvunja kanuni za chama katika zoezi hili ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa hatutakuwa na msalie mtume katika kuchukua hatua stahiki ndani ya chama pamoja na vyombo husika vya kiserikali kuchukua hatua za kisheria,”amesisitiza Mwalim. 


Gharama za fomu, utaratibu wa kuzichukua na kuzirejesha


Kuhusu gharama za kuchukua fomu za uteuzi huo, Mwalim alisema kuwa baada ya Kamati Kuu kuamua tarehe za kuchukua na kurejesha fomu za uteuzi wa ndani ya Chama na mfumo mzima wa kuwapata wagombea ilikasimisha mamlaka kwa sekretarieti ya chama kufanya maamuzi na kuidhinisha kutolewa kwa fomu pamoja na gharama zake.


Amesema kuwa sekretarieti ya chama taifa imeelekeza kuwa fomu zitaweza kuchukuliwa eneo lolote lile yaani kwenye ngazi zifuatazo; Taifa, Mkoa, Wilaya na Jimbo kwa upande wa fomu za ubunge na kwa upande wa udiwani fomu zitaweza kuchukuliwa kwenye ngazi ya wilaya, jimbo na kata.


Aidha ameongeza kuwa fomu hizo pia zitapatikana mitandaoni kupitia website ya chama; www.chadema.or.tz, kwa ajili ya wale wote ambao kwa sababu moja ama nyingine wanaweza kushindwa kufika katika ofisi za chama. 


Amesisitiza kuwa kuwa fomu hizo ni lazima zirejeshwe kwenye Ofisi ya Jimbo au Kata ambayo mgombea anagombea na ndipo atapaswakulipia gharama za fomu husika.


Kwa upande wa Ubunge wa Viti Maalum, NKMZ amesema kuwa fomu zao zitalipiwa moja kwa moja kwenye Akaunti ya BAWACHA Taifa ambayo ipo kwenye fomu husika, hivyo wagombea wa nafasi hiyo watalazimika kuambatanisha fomu zao na risiti ya kibenki (Pay Slip) ambayo inaonyesha kuwa wamelipia fomu hizo. 


Gharama za fomu hizo ni kama ifuatavyo;


· Urais ni Tsh. 1,000,000/=
· Ubunge/Uwakilishi wa Jimbo ni Tsh. 250,000/=
· Ubunge Viti Maalum ni Tsh. 250,000/=
· Udiwani wa Kata ni Tsh. 50,000/=
· Udiwani wa Viti Maalum Tsh. 50,000/= 

Imetolewa leo Alhamis, Mei 14, 2015 na;

Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Changamoto zilizopo katika kuboresha usimamizi wa fedha za umma


 Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.

PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake.

Mratibu wa Mradi huo ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo.

Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi.

Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu.  

Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma.

Mradi pia umefanikiwa kuimarisha ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini, kutumika kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya kuingiza mahitaji ya Mpango wa miaka mitano na kugawa rasilimali na pia kuchapishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali hivyo kuongeza kiwango cha uwazi.

Mengine ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 badala ya sheria iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo mengine imeiweka PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi, na kubaki na shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma. Vile vile sheria imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya ununuzi wa umma.

"...Kujenga uwezo wa watumishi katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Kwa mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu, wakaguzi, wachumi; maafisa wa ununuzi...kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kulitumikia taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya mfumo wa IFMS ili kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa mfumo wa kusimamia mali za serikali (Asset tracking software) katiak ofisi  zote za kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali." 
Alisema Mratibu huyo.

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua ya 3 ya AFROSAE, uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5 ulibadilishwa na kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi kuliko ule wa mwanzo, Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda serikali za mitaa na kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa fedha toka serikali kuu kwenda kwenye LGAs.

Mratibu alibainisha kwa sasa Ofisi ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo wa IFMS, na hivyo kuongeza ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya kimataifa ya International Public Sector Accounting Standards Cash Basis (IPSAS).

Mradi wa PFMRP ulianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika serikali na taasisi zake, huku ikitekelezwa sambamba na programu nyingine za kitaifa katika sekta ya umma.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.

Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.

Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.

Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.

Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.

Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP.

Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP.
Call for applications: The Hubert H. Humphrey Fellowship Program

The Public Affairs Section of the United States Embassy in Dar es Salaam is seeking qualified candidates for the Hubert H. Humphrey program. Online applications are now available starting April 9, 2015. Deadline for submitting applications will be no later than June 1, 2015. Only successful candidates will be called for interviews scheduled for mid-June, 2015.

Details can be found at this link: tanzania.usembassy.gov/humphrey_fellowships2.html

Balozi wa Finland, @SinikkaAntila azindua Kituo cha Msaada kwa Wahanga wa Ukatili KilimanjaroMkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) akimpokea Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka aliyefika kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.Watoa ushauri wa shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO)wakiimba wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara wakati akitembelea majengo ya kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ambayo yamejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo chini ya shirika la UKUMBIMjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya KWIECO ,Clement Kwayu akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Loe Rose Mbise wakai wa sherehe ya uzinduzi wa kituo hicho.Mkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro (KWIECO) Elizabeth Minde akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Katika kituo hicho wahanga watapatiwa malazi ya muda na huduma zingine za kijamii km matibabu, chakula, msaada wa kisheria, mafunzo ya ujasiriamali n.k

Katibu tawala wa mkoa a Kilimanjaro ,Martha Ufunguo akitoa salama za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia,mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje chini ya shirika la UKUMBIMjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa KWIECO,Jaji Aishiel Sumari akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi, Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka.
Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza kwa niaba ya wadau wa Kwieco wakati wa sherehe hizo.

Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akikata utepe kuashiria kuazna kutumika kwa majengo hayo.Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara baada ya kufungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo hicho.Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akiwa katika picha ya pamoja na watoa ushauri.

Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka alikabidhi kitabu cha "Politics of Gender "kwa mkurugenzi wa Kwieco ,Elizabeth Minde.

Maeneo mbalimbali ya kituo hicho.

Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga

Allegedly, Doctor left cell phone in patient’s abdomen

Ramallah: A Jordanian gynaecologist is alleged to have accidentally left his cell phone in his patient’s abdomen during a Caesarian section in April this year.

Hanan Mahmoud Abdul Karim, 36, was admitted to a private hospital in Amman for the operation on April 24, according to the Jordanian media. During the procedure, the gynaecologist somehow misplaced his mobile phone in the woman’s abdomen.

Majeda Abdul Hamid, the patient’s mother, told the media that after Hanan gave birth to a 4.8 kilogram baby boy she was discharged from hospital, and later the family started noticing her abdomen vibrating.

“My daughter suffered serious pains and could not move. I brought her back to the hospital where she was treated but nothing was done for her,” the mother was quoted as saying.

Hanan was then admitted to the casualty department of Al Bashir public hospital in Amman where X-rays revealed a foreign object in her abdomen. Physicians in Al Bashir hospital operated on Hanan and removed the phone.

Hanan’s case echoed in the Jordanian parliament, where the parliament member Salim Al Bataynah urged the Jordanian government to resign as a result of this scandal. “In countries which show respect to their nations, and following such scandals, governments usually resign,” he was quoted as saying. “The parliament should show responsibility and be on the level of the case.”

Jordanian Health Ministry spokesman Hatem Al Azrae said Hanan’s story was “baseless and a fabricated one”, but also stated that the ministry is carefully following it.

[update] Hospitali ya AMI yafungasha virago...


Madalali wa Mahakama Kuu jana waliondoa na kukamata mali za Hospitali ya African Medical Investment Ltd (AMI) maarufu kama Trauma Center ya Msasani Jijini Dar es Salaam, baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango kwa zaidi ya miezi 26, inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.6.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa kampuli ya MEM Auctioneers and General Brokers Limited iliyopewa kazi ya kukamata mali hizo, Elieza Mbwambwa alisema walikuwa wanatekeleza amri ya Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara kilichoamuru mali hizo zikamatwe ili kupigwa mnada kwa ajili ya kulipa deni lao la pango na kisha kuondolewa kwenye jengo na kumkabidhi mmiliki ambaye ni Navtej Singh Bains.

Alitaja mali zilizokamatwa kuwa ni pamoja na magari matatu ya kubebea wagonjwa, vitanda maalum vya kulaza na kuwahudumia wagonjwa, gari ndogo aina ya Mark II, mashine mbalimbali kama kompyuta, printa, microwave, viti, meza, makochi na hata vitambaa na mashuka ya hospitali.
“Japokuwa mahakama ilitoa amri ya kukamatwa mali zote baada ya kikomo cha notisi ya siku 14, ambayo imeisha jana, mdai amefanya ubinadamu wa kutuomba kama madalali wa mahakama, kuondoa na kukamata vitu ambavyo havitumiki na wagonjwa waliolazwa.

“Tumewapa hospitali ya AMI notisi nyingine ya kuwahamisha wagonjwa kabla ya Mei 22 mwaka huu, kisha tutaondoa kila kitu chao na kumkabidhi mwenye jengo, jengo lake. Tulichofanya ni kuorodhesha mali zote ambazo bado zinatumika na wagonjwa hawa. Wagonjwa wapya hawataruhusiwa kupokelewa tena.
“Endapo hawa waliolazwa hawatahamishwa na hospitali, sisi tutafanya utaratibu wa kuwahamishia katika hospitali zingine,” 
alisema Mbwambwa. 
 
Alitaja mashine ambazo zimeachwa kwa ajili ya kuwapa huduma wagonjwa kuwa ni City-Scan, X-ray na mashine nyingine ambayo ni muhimu katika kuchunguza maendeleo ya afya ya mgonjwa.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo, Lawrence Ochola alisema bado madaktari wanaendelea kuwahudumia wagonjwa waliolazwa na kwamba hawezi akasema zaidi ya hayo.

Hatua hii ya kufukuzwa kwenye jengo imefikiwa baada ya mabishano ya muda mrefu ya kisheria baina ya AMI na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa jengo hilo, Navtej Singh Bains.

Taarifa zaidi inasema kwamba akaunti za Benki za Hospitali hiyo ya AMI katika Benki ya EXIM zilizoambatanishwa na Mahakama zilikutwa zikiwa zimefungwa na fedha zote zikiwa zimetolewa.
Amri ya kufurushwa kwa AMI ilitolewa wiki Mei 7 mwaka huu na kusainiwa na Makamu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hatua hii sasa inafanya kufungwa kwa Hospitali ya AMI, licha ya rufaa zake za kujaribu kuzuia kufukuzwa, huku ikiwaacha wateja wake katika hali ya sintofahamu.

Baadhi ya ndugu na jamaa wa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo walionekana wakifanya taratibu za kuanza kuwahamisha wagonjwa wao, huku uongozi wa hospitali ikionekana kukaa kimya.
Hatua hii ya kufukuzwa kutoka kwenye jengo inatokana na hospitali hiyo kushindwa kutimiza amri ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyoamuru kulipwa kwa dola za kimarekani milioni 1.6 mahakamani pamoja na kodi ya kila mwezi ya kiasi cha dola za kimarekani 64,000 kila kufuatia mgogoro wa kodi ya jengo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa AMI Plc, Theunis Botha, ambaye pia ni Mkurugenzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya AMI Tanzania, aliwasilisha ombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa imefilisika.

Katika shauri hilo la ufilisi lililofunguliwa wiki iliyopita kwa Msajili wa Mahakama Kuu, kampuni hiyo inadai kuwa imekuwa ikikumbana na hasara za mabilioni ya shilingi jambo lililofanya kuwepo kwa madeni yaliyokithiri ambayo kwa sasa yako nje ya uwezo wa kampuni kulipa.

“Mlalamikaji (AMI) anadai alipata hasara halisi ya Dola za kimarekani 1.146 katika mwaka uliomalizika Februari 28, 2013, huku kwa mwaka uliomalizika Februari 28, 2014, mlalamikaji alipata hasara ya Dola za Kimarekani 775,000,” inasomeka sehemu ya hati ya malalamiko.

AMI Tanzania inamilikiwa na Kampuni mama ya AMI Plc ya London ambayo iliondolewa kwenye Soko la Hisa la London Februari 2014 baada ya jaribio la kuuza mali zake zilizopo Maputo, Msumbiji bila kibali kutoka kwa wanahisa.

Inaelezwa kuwa kampuni hiyo ilitakiwa pia kufanya malipo kwa taasisi mbalimbali, zikiwemo Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na watu na kampuni binafsi.

Kwa mujibu wa shauri hilo, ukichukulia thamani ya mali za kampuni na kiasi cha fedha zinazodaiwa na wadai, kulikuwa hakuna njia ya kuweza kupata fedha za kutosha kuwalipa sambamba na kutekeleza majukumu yake.

Pia kuna kumbukumbu zinazoonesha kuwa Lancet Laboratory (T) Ltd iliwasilisha ombi la dharura dhidi ya kufungiwa kwa Hospitali ya AMI ikiwa inaidai hospitali hiyo zaidi ya Sh milioni 150.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa wadai mbalimbali wako njia panda kutokana na deni kubwa la Dola za Kimarekani milioni nne wanaloidai hospitali hiyo. Wadai wakubwa ni pamoja na mmiliki wa jengo Bains, madaktari, wafanyakazi, TRA, wasambazaji wa dawa na wasambazaji wengine.


Taarifa za awali zilichapishwa majuma kadhaa yaliyopita. Bofya hapa kurejea.
Mbunge ahoji matangazo ya Bunge kukatwa TBC redioni na kuacha Tv tu

Ni kiwa nini redio Tanzania inarusha matangazo wakati wa maswali na majibu tu wakati mwaka jana Naibu Waziri, Juma Nkamia aliahidi kurekebisha hilo.

Amehoji kama ni kweli Serikali ina nia ya dhati ya kuwaeleza Watanzania kinachojiri Bungeni, iweje matangazo yanakatwa redioni na kuacha kwenye televisheni peke yake? Amesema runginga inatizamwa na watu kama asilimia 10 hivi na kati ya hao, wengi wao wapo kazini, hawawezi kutembea na tv. Amesema wakulima na wafugaji walio wengi na wafanyakazi wanatembea na kusikiliza redio katika shughuli zao. Amesema hata kwenye foleni wakiwa wanarejea makwao, watu husikiliza redio siyo kutizama runinga hivyo wanakosa kufuatilia kinachoendelea Bungeni kwa sababu matangazo yanakatwa.

Pamoja na hayo, pia amezungumzia suala la ajali linalochangiwa na ubovu wa barabara.

World's 1st dual-screen always-on smartphone is here!


YOTAPHONE

  • The world's first dual-screen always-on smartphone is here! Fully personalizable always-on screen. Hands-free messaging and mail. Reading time up to 100 hours. Full Android functionality on both screens. The smart-phone future. Now.
  • YOTAPHONE 2 measures battery life not in hours but in days. Five days’ reading on a single charge. 2 days’ basic smartphone functions with the YotaEnergy app. Forgot your charger? It doesn’t matter.
  • Android screens can be almost impossible to read in bright sunlight. YOTAPHONE’s EPD screen is perfectly readable even in the brightest sunshine: fiction, Facebook, Twitter, news, RSS-feeds, blogs, mail, messaging and absolutely everything else.

Read more: yotaphone.com