Lowasa achangisha milioni 234/= kwa nusu saa; Lema achangia

Edward Lowasa na Sheikh Mkuu wa BAKWATA mkoani Arusha, Shaaban Juma katika hafla ya harambe ya ujenzi wa msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha (via Arusha 255 blog) Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa amemwakilisha Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na kufanikiwa kuchangisha shilingi milioni 234 ndani ya dakika thelathini katika harambee ya msikiti wa Patandi huko Tengeru jijini Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini, Godlbess Lema (CHADEMA) naye alimuunga mkono Lowasa kwa kutoa shilingi milioni moja.

Kwa mujibu wa Jamii blog Lowasa aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Arusha, Josephat Lobulu kwa kusimamia amani ya mkoa huo.

Alisema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote:
“Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya dini, kabila au rangi, lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii. Bila amani hakuna utalii Arusha.”


Mgombea anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris akiwa anasalimiana na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa baada ya kumkabidhi shilingi milioni sita kwaajili ya ujenzi wa msikiti Patandi


Diwani Mathias Manga akiwa anawasilisha mchango wa rafiki yake wa karibu Husein Gonga wa shilingi milioni saba
Kada maarufu wa chama cha CCM,Violet Mfuko katikati akiwa na diwani viti maalum Vick Mollel wakiwa wanamshangilia mgeni rasmi


Kushoto ni mtia nia jimbo la Arumeru mashariki Solomon Sioi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima wakifatilia jambo katika harambee hiyo

SAM_2672


Wananchi wamsikiliza Lowasa


Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wakeLowasa asalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuuLowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti mkubwa jijini Arusha

Rais Nyusi kuzuru Tanzania na kulihutubia Bunge

Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi anatarajia kuwasili nchini Tanzania Mei 17 mwaka huu kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine anatarajia kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.

Akitoa taarifa ya ziara hiyo leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki amesema kuwa Rais Filipe Nyusi atawasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 17, 2015 majira ya saa sita.

Amesema mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais huyo atalakiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, kupata mapokezi ya burudani ya ngoma za asili na kukagua gwaride la heshima litakaloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na baadaye kupigiwa mizinga ishirini na moja.

Mhe. Sadiki amesema kuwa mara baada ya shughuli ya mapokezi ya Rais huyo uwanja wa ndege ataelekea Ikulu ambako atapokewa rasmi na mwenyeji wake,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na baadaye viongozi hao wawili watakua na mazungumzo ya faragha.

Amesema Mei 18, 2015 Rais Filipe Nyusi atafanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Msumbiji waishio nchini Tanzania na kisha kuendelea na ziara yake Visiwani Zanzibar ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.

Ameeleza kuwa baada ya kukamilisha ziara yake kisiwani Zanzibar Mei, 19 mwaka huu, Rais Filipe Nyusi ataelekea mjini Dodoma ambako atakutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Rais Jakaya Mrisho Kikwete yalipo Makao Makuu ya Chama cha hicho na baadaye ataelekea Ukumbi wa Bunge kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema, Mhe. Filipe Nyusi atahitimisha ziara yake na kurejea nchini kwake Mei 19, 2015 na kuwaomba wananchi hususan wakazi wa jiji la Dar es salaam kuwa wavumilivu kutokana na usumbufu utakaotokana na baadhi ya barabara zikiwemo Nyerere, mzunguko wa Kamata, Barabara ya Sokoine ,Luthuli na Barabara ya Kilwa kufungwa mara kwa mara kupisha msafara wa kiongozi huyo.
  • Taarifa ya Aron Msigwa - MAELEZO

Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Nyussi
Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Nyussi 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 17 Mei, 2015 kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Rais Nyusi atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Rais Nyusi atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21.
Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Nyusi atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji.
Baadaye siku hiyo ya Mei 17, Mhe. Rais Nyusi atakutana kwa mazungumzo na Mabalozi kutoka Nchi za Afrika waliopo hapa nchini mkutano utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.
Mhe. Rais Nyusi ambaye ataongozana na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Msumbiji atahutubia Kongamano la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara wa nchi hizi mbili ambalo litafanyika tarehe 18 Mei, 2015 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Aidha, siku hiyo ya tarehe 18 Mei, Mhe. Nyusi atapata fursa ya kukitembelea Chuo cha Diplomasia kinachotambulika kama “Tanzania-Mozambique Centre for Foreign Relations” kilichopo Kurasini ambacho kilianzishwa mwaka 1978 kama mradi wa ubia ili kuendeleza mahusiano ya kindugu ya muda mrefu kwa lengo la kutoa mafunzo ya diplomasia na masuala ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.
Mhe. Nyusi atakutana na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini kabla ya kuelekea Zanzibar ambako atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia kuzungumza na raia wa Msumbiji waliopo Zanzibar.
Akiendelea na ziara yake hapa nchini, Mhe. Rais Nyusi ataondoka Zanzibar tarehe 19 Mei, 2015 kuelekea Dodoma. Akiwa Mkoani humo atatembelea Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mhe. Rais Nyusi atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mhe. Rais Nyusi anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 19 Mei, 2015 na kuondokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kurejea Msumbiji.

Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Dar es Salaam.16 Mei, 2015

Zilipendwa: Vijana Jazz - Bujumbura

Anatafutwa mtengeneza tovuti/website


Baadhi ya watu wamekuwa wakiniuliza endapo ninamfahamu yeyote anayetengeneza blogu/tovuti na gharama zake.

Binafsi sifahamu ila kwa kuwa hili ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara, tafahali yeyote anayefanya kazi hii au anayemfahamu anayeifanya, acha jina na mawasiliano kwenye kisanduku cha maoni hapo chini ili iwe rahisi kurejea (reference) kwa yeyote anayehitaji huduma hii.

Natanguliza shukurani.

Mapitio ya magazeti katika Tv, Mei 16, 2015
[audio] Bungeni: Nassari alivyomsema Nyalandu

Waziri Nyalandu akiwa amemmbeba mmoja wa askari aliozungumzia Nassari katika audio iliyopachikwa hapo chini

Huko Bungeni: Ole Sendeka amwagia sifa Lowasa

Tafadhali bofya video iliyopachikwa hapo kumsikiliza...Tume ya MIpango yatembelea EPZA na kujionea 'jeans made in Tanzania'Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mhandisi Keneth Haule (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Abel Shirima (Kushoto), Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), na Bw. Omary Abdallah (Wapili Kulia).Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (katikati) akizungumza na Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (kushoto) wakati Bibi Mwanri na ugeni wake walipotembelea Ofisi za Mamlaka kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (kulia).


Bibi Lilian Kalengo (Kulia), mwakilishi wa Kiwanda cha Tooku Garments akiwaonesha suruali ya jeans wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho ni moja ya viwanda 12 vilivyoanza uzalishaji katika Ukanda wa huo.Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia moja ya suruali zinazotengezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.Mmoja wa mabinti wa Kitanzania walioajiriwa na Tooku Garments akiwa kazini.Wakina dada wakiendelea na kazi ya utengenezaji wa suruali za jeans zinazotengenezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.


Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na SAIDI MKABAKULI

Taarifa ya JWTZ kuhusu uvumi wa usaili

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitishwa na taarifa za uvumi zilizotolewa kuenea kwenye mitandao ya kijamii face book, whatsapp na twitter zikieleza kuwa JWTZ inafanya usaili leo tarehe 15 May 2015 katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa wale waliosoma fani ya Computer science, IT, Electronics na Mechanical Engineering.

JWTZ linapenda kuwajulisha wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo si za kweli ni uvumi, JWTZ lina utaratibu wake wa kuandikisha Jeshini ambapo hutoa taarifa katika vyombo vya habari kwa utaratibu ulio sahihi.

Aidha, Jeshi linaendelea kusisitiza wananchi kuwa halina akaunti za mitandao hiyo na ni kinyume cha sheria kusambaza ujumbe kwa kutumia jina au nembo ya JWTZ watakao bainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963.

Hali ilivyo mpakani mwa Burundi na TanzaniaRais Nkurunziza kulihutubia taifa; Jenerali Niyombare akamatwaKiongozi aliyeongoza mapinduzi yaliyoshinidikana nchini Burundi kutaka kumpindua rais Pierre Nkurunziza, amekamatwa na yuko chini ya ulinzi wa polisi, yeye pamoja na maofisa wengine aliokuwa nao.

Taarifa hizi zimethibitishwa na maofisa wa juu wa jeshi la Burundi, ambao wamesema Niyombare na wenzake walijisalimisha kwa hiari kwa vikosi vya Serikali na kwamba sasa wako chini ya ulinzi wakisubiri hatua nyingine kuchukuliwa.

Mapema usiku wa kuamkia leo, Jenerali Nyombare alitangaza kushindwa kutekeleza mapinduzi aliyoyapanga na kwamba atajisalimisha yeye pamoja na wanajeshi wengine waliokuwa wanamsaidia.

Hatua hii imekuja baada ya wanajeshi walioasi kuzidiwa uwezo na wanajeshi watiifu kwa Serikali ya rais Nkurunziza, ambapo toka juzi walikuwa wanawania kuchukua kituo cha taifa cha Televisheni na Redio.

Jaribio hili la aina yake, limemalizika ndani ya saa 48 baada ya hapo awali kuwepo taarifa kuwa haijulikani ni nani hasa ambaye alikuwa anaumiliki wa Serikali baada ya kushuhudia maandamano ya wananchi wanaopinga rais Nkurunziza kuwania muhula watatu wa urais.

Jenerali, Godefroid Niyombare mwenye miwani ambaye jaribio lake la mapinduzi limeshindikana na kukamatwa
REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Jenerali Niyombare, anasema kuwa
"Tumeamua kujisalimisha, na nimatumaini yetu kuwa hawatatuua". 
Alisema Niyombare.

Kiongozi mmoja wa juu wa Polisi nchini Burundi, amethibitisha kujisalimisha kwa wanajeshi hao, ambapo ameongeza kuwa jenerali Niyombare pamoja na wanajeshi wengine wanaomuunga mkono wamekimbia na wanatafutwa.

Msemaji wa jenerali Niyombare, Zenon Ndabaneze akizungumza na shirika la habari la AFP amethibitisha wanajeshi wao kujisalimisha baada ya yeye mwenyewe kukamatwa na wanajeshi wa Serikali, ambapo pia naibu wake Niyombare, Cyrille Ndayirukiye na wenzake wengine pia wamekamatwa.
"Tumeamua kujisalimisha, tumeweka chini silaha zetu, tumewapigia simu Wizara ya Mambo ya Ndani kuwataarifu kuwa hatuna silaha tena". 
Alisema Ndabaneze saa chache kabla ya kukamatwa kwake.

Mwandishi wa RFI idhaa ya Kiingereza, Danniel Finnan aliyeko mjini Bujumbura, Burundi, amesema kuwa hali kwa sasa imerejea kwenye hali yake ya kawaida licha ya maandamano ya hapa na pale katika baadhi ya maeneo, ambako pia kumesikika milio ya risasi.

Katika hatua nyingine, msemaji wa rais Nkurunziza, amethibitisha kuwa kiongozi wake amerejea mjini Bujumbura usiku wa kuamkia leo na kwamba leo Ijumaa anatarajiwa kulihutubia taifa kupitia njia ya televisheni.

Wakati jaribio hili linafanyika, rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania, ambako alienda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati, lakini akashindwa kushiriki baada ya kupokea taarifa za jaribio la mapinduzi.

Taarifa zaidi kutoka jijini Bujumbura zinasema kuwa mashirika ya kiraia yametoa wito kwa wananchi kujitokeza tena barabarani kushiriki kwenye maandamano zaidi ya kupinga rais Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Machafuko yaliyoshuhudiwa nchini Burundi kwa takribani majuma matatu sasa, yametokana na hatua ya rais Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu licha ya shinikizo la kimataifa kumtaka asigombee.

Juma hili wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini dar ee Salaam, Tanzania, walilaani mapinduzi yaliyofanyika nchini Burundi, na kutaka uchaguzi mkuu usogezwe mbele na pia kuheshimiwa kwa mkataba wa Arusha unaotaka rais wa Burundi kuwania urais kwa mihula miwili pekee.

Taarifa ya Wizara: Vyama vinavyokusudiwa kufutwa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

ORODHA YA VYAMA VYA KIJAMII VINAVYOKUSUDIWA KUFUTWA


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI INATOA KUSUDIO LA KUVIFUTA VYAMA VIFUATAVYO CHINI YA KIFUNGU CHA 17 CHA SURA 337. VYAMA HUSIKA VINAPEWA SIKU 21 KUANZIA TAREHE 15 MEI, 2015 KUWASILISHA UTETEZI WAO KWA MSAJILI WA VYAMA KWA NINI VYAMA HIVI VISIONDOLEWE KWENYE ORODHA YA VYAMA

ORODHA YA VYAMA VYENYE MADENI MAKUBWA YA ADA YA MWAKA NA AMBAVYO HAVIJALETA TAARIFA YA UKAGUZI WA FEDHA YA KILA MWAKA
NA.
NAMBA YA USAJILI
JINA LA CHAMA
TAREHE YA USAJILI
MAHALI CHAMA KILIPO
1
SO. 9845
ELIMISHA
20/4/1999
DAR ES SALAAM
2
SO. 9849
FOR GREEN ENVIROMENT AND WASTE MANAGEMENT ASSOCIATION
20/4/1999
DAR ES SALAAM
3
SO. 9856
TUGEME WOMEN GROUP
6/5/1999
DAR ES SALAAM
4
SO. 9864
TAUSI DEVELOPMENT ASSOCIATION
DAR ES SALAAM
5
SO. 9865
THE HISTORICAL ASSOCIATION OF TANZANIA
13/5/1999
DAR ES SALAAM
6
SO. 9870
CHAMA CHA MAENDELEO NGANJONI
12/5/1999
DAR ES SALAAM
7
SO. 9874
LUCHENGELEGWA DEVELOPMENT ASSOCIATION
22/11/1999
DAR ES SALAAM
8
SO. 9875
KIKUNJA DEV ELOPMENT ASSOCIATION
11/9/1999
DAR ES SALAAM
9
SO. 9880
KIKUNDI CHA KUJIENDELEZA DSM
19/8/1999
DAR ES SALAAM
10
SO. 9881
THE SOLAR INNOVATIONS OF TANZANIA
19/8/1999
DAR ES SALAAM
11
SO. 9882
TANZANIA INITIATIVE FOR WORLD SOLIDARITY
31/5/1999
DAR ES SALAAM
12
SO. 9837
CHAMA CHA HIARI CHA NEEMA SITAKISHARI
19/4/1999
DAR ES SALAAM
13
SO. 10437
THE D'SALAAM LABOUR CENTRE
24/5/1999
DAR ES SALAAM
14
SO. 10058
MVITA DEVELOPMENT AND WELFARE ASSOCIATION
16/5/2000
DAR ES SALAAM
15
SO. 10068
AFRICAN RELIEF COMMITTEE OF KUWAIT
8/10/1999
DAR ES SALAAM
16
SO. 10055
SHARIFU SHAMBA ILALA EQUITABLE COMMUNITY DEVELOPMENT FOUNDATION
2/10/1999
DAR ES SALAAM
17
SOO. 10062
WOMEN ACTION FOR DEVELOPMENT
13/10/1999
DAR ES SALAAM
18
SO 10070
COMMUNICAITON OPERATORS ASSOCIATION OF TANZANIA
8/10/1999
DAR ES SALAAM
19
SO. 10079
TANZANIA NATIVE NETWORK
27/10/1999
DAR ES SALAAM
20
SO. 10081
MOTHERLAND TANZANIA
11/10/1999
DAR ES SALAAM
21
SO. 10088
TANZANIA TWINS RELIEF ASSOCIATION
22/11/1999
DAR ES SALAAM
22
SO. 10098
MBURAHATI BARAFU SOCIEITY FOR DEVELOPMENT
22/12/1999
DAR ES SALAAM
23
SO. 10093
KILIMAHEWA DEVELOPMENT SOCIETY
11/10/1999
DAR ES SALAAM
24
SO. 10100
TEMBONI DEVELOPMENT ASSOCIATION
22/11/1999
DAR ES SALAAM
25
SO. 10106
EASTERN AND SOUTHERN AFRICAN UNIVERSITIES RESEARCH PROGRAMME
8/7/1988
DAR ES SALAAM
26
SO. 10114
THE HUMAN RESOURCES DEVELOPMENT IN WATER AND SANITATION
7/12/1999
DAR ES SALAAM
27
SO. 10115
KIJITO WOMEN GROUP
22/11/1999
DAR ES SALAAM
28
SO. 10135
SOGO ECONOMIC DEVELOPMENT FOUNDATION
29/10/1999
DAR ES SALAAM
29
SO. 10137
MAMPATA AND KINAMBEU DEVELOPMENT ASSOCIATION
22/11/1999
DAR ES SALAAM
30
SO. 10144
THE HOPE AND MERCY CHARITABLE GROUP
7/12/1999
DAR ES SALAAM
31
SO. 10147
CHAMA CHA MAENDELEO TARAFA YA MVOMERO NA TURIANI
20/11/1999
DAR ES SALAAM
32
SO. 10197
FOOD SECURITY PROMOTION CENTRE
22/11/1999
DAR ES SALAAM
33
SO. 10193
YOUTH ADVISORY DEVELOPMENT ASSOCIATION
21/12/1999
DAR ES SALAAM
34
SO. 10178
YOUTH AND DEVELOPMENT AFRICA
29/12/2000
DAR ES SALAAM

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
14 MEI 2015