Wanajeshi 12 waliojaribu kupindua Burundi wauawa, 35 wajeruhiwa, 40 wakamatwa


Wanajeshi 12 waliohusika na jaribio la mapinduzi wameripotiwa kupoteza maisha katika mapigano yaliyozuka kati yao na vikosi vya serikali nchini Burundi.

Ofisi kuu ya ulinzi wa taifa hilo ilitoa maelezo katika kituo cha RTNB na kufahamisha kuuawa kwa wanajeshi hao huku 35 wakijeruhiwa na 40 kukamatwa. Wanajeshi wa vikosi vya serikali walioripotiwa kujeruhiwa ni nane.

Mmoja wa wahusika wakuu wa mapinduzi, Jenerali Cyrille Ndayirukiye aliyewahi kuwa mkuu wa jeshi alitangaza kutofanikiwa kwa jaribio hilo la mapinduzi. Viongozi watatu wa jeshi waliohusika na jaribio la mapinduzi waliripotiwa kutiwa mbaroni.

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 18, 2015

[update] Waziri ajibu swali kuhusu kuugawa mkoa wa Morogoro

UPDATE/TAARIFA MPYA 19 Mei 2015

MBUNGE wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga (CHADEMA), ameitaka Serikali kuingilia kati mgogoro ambao unaonekana kukua kati ya majimbo ya Ulanga Mashariki na Ulanga Magharibi. 

Kiwanga alitoa pendekezo hilo bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza akitaka kujua ni lini mgogoro wa ugawaji majimbo katika mkoa wa Morogoro utatatuliwa.

Awali katika swali lale la msingi, Kiwanga alitaka kujua ni lini serikali itatangaza kuugawa mkoa wa Morogoro kwa kuzingatia maombi na mapendekezo ya RCC ya tangu mwaka 2013, na kuhoji ni lini serikali itaridhia mapendekezo ya kugawa jimbo la Kilombero kwa majimbo mawili ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kasim Majaliwa amesema kuwa suala ya kugawa mkoa wa Morogoro liliibiliwa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichokutana 10 Januari mwaka jana.
“Katika kikao hicho ilipendekezwa uanzishwe mkoa mpya wa Kilombero na kuanza mchakato wa kitaalam ufanyike ikiwa ni pamoja kuwasilisha mapendekezo hayo Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI).
“Hadi sasa pendekezo hilo halijapitishwa katika vikao vya kisheria ili kuwezesha serikali kufanya maamuzi kwa kuzingatia vigezo na maoni ya vikao vya kisheria,” 
alieleza Majaliwa.

Kuhusu mgogoro ambao aliutaja Kiwanga katika majimbo ya Ulanga Mashariki na Magharibi, amesema kuwa serikali itahakikisha inaingilia kati ili kuutatua.

via MwanaHALISI online


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia, akijibu swali lililolulizaw na Wabunge wengi kuhusu kuugawa mkoa wa Morogoro, alisema hajapata maombi ya kutaka mkoa huo ugawanywe.

Alilieleza Bunge juzi katika majumuisho yake kuwa mkoa utakaogawanywa ni wa Mbeya.

Serikali ilitumia bilioni 1.9/= kukabiliana na vurumai za gesi Mtwara


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia, alilieleza Bunge juzi katika majumuisho yake kuwa serikali ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 1.9 kukabiliana na vurumai zilizokuwa zinapinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar, zilizotokea mkoani Mtwara.

Fedha hizo zilitumika kuweka kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mkoani humo kwa ajili ya kudhibiti hali hiyo.

Alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na Kambi ya Upinzani kuwa Halmashauri ya Mtwara Mikindani ilipata fedha nyingi kuliko kiasi cha bajeti iliyoombwa wakihoji iwapo zimetolewa kwa vile Waziri wa Tamisemi ni mwenyeji wa mkoa huo.

Alieleza kuwa walipewa fedha za ziada nje ya bajeti ili kujenga kikosi cha JWTZ kudhibiti vurumai zinazotokana na gesi. [NIPASHE]

Athari za wakimbizi zaanza: Shule zafungwa, wanafunzi hawasomi


Kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Burundi na kusababisha kufurika kwa waomba hifadhi nchini hususani mkoa wa Kigoma, kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu imejaa na kusababisha shule zilizopo ndani ya kambi hiyo kufungwa kwa muda.

Akizungumza na NIPASHE juzi katika kambi hiyo, mkuu wa kambi hiyo, Sospeter Boyo, alisema uwezo wa kambi hiyo kwa sheria za kitaifa ni kuhifadhi wakimbizi 50,000 lakini kwa sasa ina watu 54,706 ambao ni wazamani.

“Kwa kawaida kambi hii ina uwezo wa watu 50,000 kulingana na taratibu za kimataifa, lakini mpaka sasa ina wakimbizi 54,706...hivyo baada ya kuanza kuwapokea waomba hifadhi wapya Aprili 29, mwaka huu, tumepata wapya 16,808 hadi juzi,” 
alisema Boyo.

Alisema, hata hivyo licha ya kufunga shule zilizopo kambini hapo, lakini wataendelea kuwapokea wageni hao kutokana na serikali ya mkoa kutafuta eneo lingine litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wakimbizi wengi zaidi.

Alisema kwa sasa wamefunga shule ili majengo hayo yaweze kutumika kuwahifadhi wahamiaji wapya wanaowasili kila siku kutoka kitongoji cha Kagunga wilayani Kigoma, wanaokochukuliwa na meli ya Mv Liemba.

Hata hivyo, alisema huduma zote muhimu zinapatikana vizuri kambini hapo kuanzia chakula, maji, afya pamoja na watoa huduma wa mashirika mengine kuwapo kambini hapo.

Aidha, alisema kambi hiyo inakusudiwa kuwasiliana na viongozi wa dini wa makanisa na misikiti ndani ya kambi hiyo ili kuweza kusitisha huduma zao kwa muda, kwa lengo la kuwaweka waomba hifadhi hao ambao kwa sasa wamekuwa wengi.

Afisa Uhamiaji mfawidhi wa Kagunga, Boniface Mayala, alisema mpaka jana waliongozeka wakimbizi 108 na kufikisha idadi ya walioingia mpaka sasa kufikia 90,000. 
“Zaidi ya 11,000 tayari wamesafirishwa kwenda mjini tayari kupelekwa kambini kwa ajili ya uhifadhi,” 
alisema Mayala.

Benki ya Dunia inaingilia mradi wa mabasi ya haraka Dar?

  
Kampuni ya wazawa itakayoendesha mabasi yaendayo haraka (DART), jijini Dar es Salaam imeanzishwa na inatarajiwa kuanza kutoa huduma hizo Septemba, mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia, alilieleza Bunge juzi kuwa ubia huo wa usafirishwaji unaoundwa na kampuni ya UDA na wasafirishaji wa daladala iitwayo UDART.

Alieleza kuwa UDART imesaini mkataba wa huduma ya mpito ili kuanza kuhudumia wateja.

Waziri Ghasia aliwataka wamiliki wa daladala kununua hisa kwenye kampuni hiyo ili washiriki katika mradi huo wa usafirishaji.

Mapema wiki hii akitoa mchango kwa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbunge wa Igalula (CCM), Athumani Mfutakamba, alisema Benki ya Dunia (WB) inapinga wazawa kumiliki na kuendesha mabasi ya DART.

Mfutakamba alisema ni lazima wazawa wachukue jukumu hilo hata kama WB haitaki na kushauri kuwa kampuni za kigeni zisimamie ukataji tiketi na muda wa mabasi kufika na kuondoka vituoni.

Mbunge huyo alisema hata kama WB watagoma kutoa fedha zinazohitajika kukamilisha mradi wa DART, serikali inaweza kuwasiliana na kampuni ya bima ya China ili kutoa mkopo kukamilisha kazi ya miundombiu iliyobakia.

Jana Waziri Ghasia alisema serikali itaendelea kuwahimiza wazawa kuunganisha nguvu ili kuwa wamiliki wa mradi huo wa usafirishaji.Mozambique, Tanzania scrap entry visasMozambique and Tanzania on Sunday signed a Visa Waiver Agreement on diplomatic, service and ordinary passports extending to 90 days the period of stay in the territory of each country against the previous 30 days of the initial agreement, APA reports.

According to state-controlled Radio Mozambique, the agreement was signed in Dar es Salaam, the economic capital of Tanzania, after the meeting between Mozambican President Filipe Nyusi and President Jakaya Kikwete.

Nyusi arrived in Tanzania on Sunday at the start of his three-day official state visit.

The Mozambican Interior Minister Basilio Monteiro, and the Tanzanian minister of Foreign Affairs and International Cooperation, Bernanrd Membe, signed the deal on behalf of both countries.

According to Monteiro, the agreement aims to make more fluid cooperation by facilitating the free movement of people and goods in both countries because there is an understanding in this sense at the level of the Southern African Development Community, (SADC).

The agreement will help to increase trade between the two countries.

We know that people in the provinces of Cabo Delgado and Niassa are very close and there are Tanzanians on the other side of the Mozambican boarder with Tanzania, therefore, the populations of these provinces very close 
Said Monteiro, pointing out for example that the Unity Bridge which is under construction to link the two countries will enable Commercial flow, transit and the mutual benefits to countries.

Nyusi, in turn, said that the memorandum of understanding formalises a practice that already exists between Mozambique and all countries of the SADC region.

M.Mndeme: Nalilia jiji la Dar

Nalilia Jiji la Dar es Salaam
Mwaka jana kulipotokea mafuriko makubwa jijini Dar es Salaam yaliyoleta madhara ya kuaharibu mali na kupoteza maisha ya watu wengi, niliandika makala kwa mheshimiwa Rais Kikwete kama sehemu ya mchango wangu kwa taifa langu.  Kwa kuwa ni ngumu sana kupata nafasi ya kuchapisha makala katika magazeti yetu ya Tanzania, nilitafuta nafasi katika mitandao kadhaa na kuiweka makala hii ili isomwe na watu wengi. Kwa kuwa sikubahatika kupata anunani ya barua pepe inayotumiwa na Rais wetu au wasaidizi wake, nilitafuta mawasiliano ya barua pepe ya viongozi kadhaa wa juu wa serikali walio karibu na Rais na kuwatumia wao binafsi na kuwaomba wasome ushauri wangu. Niliamini watamfikishia ujumbe.

Binti wa miaka 9 amwokoa Mama yake kwa kupambana na mamba kwa nusu saa

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa ameonesha ujasiri wa kipekee kwa kumwokoa mama yake mzazi, Magreth Ibrahim (50) kuuawa na mamba baada ya kupambana na mnyama huyo kwa zaidi ya nusu saa.

Mama huyo mkazi wa kijiji cha Karema, mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda, kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda mjini Mpanda kwa matibabu baada ya mkono wake kunyofolewa na mamba aliyemshambulia wakati akifua kando ya Mto Ikola.

Akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima aliyemtembelea hospitalini hapo masaibu yaliyomsibu, alisema anamshukuru sana binti yake mwenye umri wa miaka tisa aliyeweza kuokoa maisha yake licha ya kuwa amenyofolewa mkono na mamba huyo.

Akisimulia mkasa huo, Magreth alieleza kuwa juzi akiwa anafua kando ya mto Ikola ghafla mnyama huyo aliibuka majini na kumpiga usoni na mkia wake.

“Mamba huyo aliibuka ghafla mtoni na kunichapa usoni na mkia wake nami nikaangukia majini ndipo aliponidaka mkono wangu na kunivutia mtoni ….binti yangu aliyekuwa jirani yangu alipoona niko karibu kuliwa na mamba kwa ujasiri aliweza kukabiliana naye …
Alinishika mkono mwingine na kunivutia nje huku akipiga kelele kumtisha mnyama huyo ili aniachie hatimaye akaunyofoa mkono wangu na kutokomea nao mtoni ….” 
alieleza.

Aliongeza kuwa watu waliokuwa wakifua mtoni hapo wengi wao wakiwa wanawake walifika eneo la tukio ambapo wakiwa na binti yangu walimvuta na kumtoa nje na baadae wakamkimbiza hospitalini mjini Mpanda kwa matibabu.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Dk Joseph Mkemwa amethibitisha kuwa hali ya mama huyo inaendelea kuimarika baada ya kupatiwa matibabu.

Kwa upande wake, Mwamlima amepiga marufuku wakazi wilayani humo kuoga au kufulia katika mito na maziwa ili wajiepushe na visa vya kusambuliwa na mamba.
  • Taarifa kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo

Kinondoni yatekeleza agizo la Rais la kuondoa maji


Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini dar es Salaam imeanza utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete kuondoa kwa kutumia pampu maji yaliyozingira makazi ya wananchi katika maeneo ya Tegeta Basihaya, Nyaishozi, Bunju na Mbweni pamoja na kuanza kuchimba mtaro ili maji hayo yaelekezwe baharini.

Agizo hilo la Rais alilitoa wakati wa ziara yake wiki iliyopita alipojionea athari za mafuriko ambazo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 12 pamoja na nyumba kadhaa kuanguka na nyingine kuzingirwa na maji. Zaidi ya nyumba mia tatu zimefurika maji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa agizo la Rais, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik akiambatana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amesema zoezi la uchimbaji mtaro limeanza ambapo nyumba kadhaa zilizojengwa kuzuia mikondo ya maji zitavunjwa.

Kwa upande wake, Mwenda amesema mafuriko hayo yalichangiwa na baadhi ya wananchi kujenga katika mikondo ya asili ya kupitishia maji huku wengine wakiziba kwa makusudi njia za maji.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamesema licha ya mvua kupungua bado wamelazimika kuzikimbia nyumba zao kutokana na kufurika maji ambayo hayana dalili ya kukauka.

Taarifa ya Channel TEN

Taarifa ya habari ya Channel TEN Mei 17, 2015
Taarifa ya habari ya Channel TEN Mei 16, 2015
Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 17, 2015


10 Most reliable car brands in USA

From a car dealer's view, listed below in ascending order are 10 most reliable car brands in the United States of America:10. Mercedes-Benz: Mercedes is helped by long model runs for their most popular vehicles; a multitude of models that share the same engines and transmissions; and finally, a quality initiative that made long-term customer satisfaction a priority. We should note that Mercedes-Benz and the next competitor are surprisingly close to each other in terms of long-term quality.9. Scion: The average Scion will typically cost less than half of a Mercedes and yet the long-term reliability is surprisingly similar. This is a common theme we find in our results. Paying more does not necessarily mean you’re going to get a premium return when it comes to long-term reliability.8. Mitsubishi: This was a complete shocker. However, Mitsubishi has benefited from long model runs over the past ten years, and much of what they sell is devoid of the unproven electronics and technologies that have hurt other brands. Four-cylinder models are particularly strong in terms of long-term reliability.7. Acura: Honda’s Acura division is helped by four-cylinder models such as the Acura RSX and Acura TSX, which are ranked among the highest quality vehicles in the study. The poor reliability of transmissions for V-6 models throughout the late-90s and early 2000s pulled down the overall rankings of both brands.6. Chevrolet: While Chevrolet cars have routinely averaged middling to mediocre reliability, Chevrolet trucks and full-sized SUVs have rightly earned their reputation as workhorses. The Corolla-based Prizm and the Chevrolet Corvette are the best Chevy cars when it comes to long-term reliability.5. Infiniti: Six of the top 10 Inifiniti models are ranked among the top 15 percent in overall quality. The Infiniti QX4, an SUV based off Nissan Pathfinder, has enjoyed particularly long periods of trouble-free ownership, as have the G37 and M35.4. Honda: The entire Honda line-up has offered excellent long-term reliability with two notable exception: V-6 Accords and Odysseys. The frequency of bad transmissions for the Odyssey, and the Accord from 1998 thru 2002 was enough to pull them well outside the top rankings of reliable vehicles, although four-cylinder Accord models continue to be ranked among the top.3. GMC: Once again it’s the full-sized American truck and SUV that makes all the difference for domestic manufacturers. The same strong showing in full-sized trucks is also true for Ford. For GMC, it’s the Sierra truck, Suburban SUV, and Savanna full-sized van that are true standouts.2. Lexus: Lexus has three of the top seven ranked vehicles when it comes to long-term reliability. This includes the Lexus LX which is ranked at #1 along with it’s sister model, the Toyota Land Cruiser. Lexus is also the only brand in the study that offers excellent long-term reliability for every single model they sell.1. Toyota: There are certain weeks when the Toyota Camry will offer more high-mileage trades than all European models… combined. Part of Toyota’s dominance comes from having two of their models, the Camry and Corolla, represent nearly half their sales. However as Lexus offers three of the top 10 vehicles when it comes to long-term reliability, Toyota nails four more spots. The Land Cruiser, 4Runner, Sequoia and Avalon are all top ranks, with the Corolla and Camry firmly in the top 3 percent of reliable models.

Source: Yahoo

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi awasili Tanzania kwa ziara rasmi

Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Jumapili, Mei 17, 2015. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.

Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais Filipe Jacinto Nyusi akipokea shada la maua.

Rais Filipe Jacinto Nyusi akikagua gwaride la heshima

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wakiangalia ngoma

Rais Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu jijini Dar es Salaam katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama Rais wa Msumbiji

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wakishangiliwa na mamia ya wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kumlakiRais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi na ujumbe wake katika mazungumzo rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Waziri wa Masuala ya Ndani wa Msumbiji wakitiliana saini mkataba wa makubaliano mbele ye marais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji
Picha: IKULU[audio] Majadiliano ya Uchaguzi Mkuu na hatma ya TanzaniaMakala-sauti ya Evarist Chahali

House for rent in Mikocheni B, Sangara StreetA 3 bed room and 2 bath - one is Master bed room is available for rent at Sangara Street in Mikocheni B, Dar es Salaam.

All rooms have AC including a heater in the Master bed room.

It has a kitchen, dining, garage and boys quarter.

The house is fenced and fortified by electrical wire. It's in a peaceful and elite neighborhood.

For more info., call 0763514988.

Below are pictures of the house, please click to enlarge.
Fremu 2 za biashara zinapangishwa Tabata

Fremu mbili za biashara zinapangishwa Tabata - Kimanga, Dar es Salaam.

Bei ni shilingi laki moja kwa mwezi.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0763514988.