Wagonjwa wa ugonjwa usiofahamika wafikia 1,048

Idadi ya wagonja ambao wameugua ugonjwa wa ajabu uliozikumba jumla ya kata 6 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu imezidi kuongezeka kila mara, tangu kuripotiwa kutokea kwa ugonjwa huo wiki mbili zilizopita.

Mpaka jana taarifa zilizotolewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Meatu Adamu Jimisha alisema kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka wagonjwa 80 hadi kufikia 1048 ambao walifikishwa katika kituo cha afya Mwandoya.

Jimishi alitoa taarifa hiyo jana mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, iliyokuwa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Elaston Mbwilo, wakati ilipowatembelea baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo hicho cha afya pamoja na kata za, Mwabusalu, Lingeka, Mwakisandu, Tindabuligi, Pamoja na Lubiga ambazo zimekubwa na janga hilo.

Alieleza kuwa bado dalili za baadhi ya wagonjwa ambao wamekuwa waliletwa katika kituo hicho cha afya tangu kutokea kwake, zimekuwa ni zilezile kumwa kichwa, kikohozi kikavu, mwili kulegea, kuchanganyikiwa akili pamoja na kupoteza fahamu.

Aidha aliongeza kuwa wagonjwa hao wamekuwa wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani pindi wanapopata nafuu au kupona kabisa, huku akibainisha kuwa baadhi yao walikutwa na magonjwa mbalimbali kama maralia na minyoo.

Mganga Mkuu huyo alieleza kuwa wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiambatana na Timu ya Mkoa akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa, Mtaalam wa Maabara na Daktari mmoja walichukua sampuli kwa ajili ya kupeleka Nairobi kwa Uchunguzi.

Alisema timu hiyo ilipeleka vipimo hivyo tarehe 15/05/2015 kwa ajili ya kubaini aina gani ya ugonjwa, ambapo majibu alieleza kuwa timu hiyo iliahidi kutoa mwishoni mwa mwezi huu.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo waliokuwa wamefika kuwajulia hali baadhi ya wagonjwa katika kutoa hicho cha afya kuwapeleka mapema hospitali watu watakaoonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.

wa binadamu usiojulikana ambao uliripotiwa mapema mwezi Mei na kuathiri Tarafa ya Kisesa na baadhi ya maeneo ya Tarafa ya Kimali, wilayani Meatu.

Mhe. Mbwilo aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na wananchi mara baada ya kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika Kituo cha Afya cha Mwandoya.

Mhe. Mbwilo alisema kuwa kutokana na taarifa aliyoipokea kutoka kwa Daktari Msaidizi wa Kituo hicho cha afya inaonesha kuwa wagonjwa wanaopelekwa mapema hospitali na kupatiwa matibabu wanapata nafuu mapema kuliko wale waliocheleweshwa.
“Msiiwaache wagonjwa majumbani waleteni na msiwapeleke kwa waganga wa kienyeji, mkiona watu wenye dalili za ugonjwa kama walivyowaeleza wataalam waleteni haraka hapa Mwandoya wapatiwe matibabu” 
alisema Mbwilo.

Mbwilo aliwaeleza wananchi kuwa kwa mujibu wa Watalaam wa Afya ugonjwa huo hauna madhara ya kifo, hivyo akawataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida wakati Serikali inaendelea kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha ugonjwa huo.

Nao baadhi ya wananchi wakiongea mbele ya mkuu huyo wa Mkoa waliiomba Serikali kufuatilia haraka matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa na Wataalam hao ili wajue chanzo cha ugonjwa huo ambao mpaka sasa hawaujajulikana.
“Tunaomba majibu ya vipimo vilivyochukuliwa yaletwe haraka, maana mpaka sasa hivi hatujui huu ni ugonjwa gani na chanzo chake nini, Serikali itusaidie katika hili” 
alisema mmoja wa wananchi alijulikana kwa jina la Joseph.

Mhe Mbwilo alisema Serikali inaendelea kufuatilia majibu ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa na Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Mkoa wa Simiyu na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii baada ya kukamilisha taarifa zitatolewa kwa wananchi.

Dk Winnie Mpanju-Shumbusho ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi WHO

Winnie Mpanju-Shumbusho
Winnie Mpanju-Shumbusho

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dr. Margaret F. Chan amemteua Dr. Winnie Mpanju-Shumbusho kutoka Tanzania kuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani, upande wa masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu Malaria na Magonjwa yaliyosahaulika. Uteuzi huu umetangazwa rasmi na Dr. Chan wakati wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani kilichoanza tarehe 14 mpaka tarehe 26 Mei 2015, Geneva, Uswisi.

Dr. Mpanju-Shumbusho ni mtaalamu na kiongozi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika ngazi za juu za uongozi katika sekta ya Afya na Ushirikiano wa Kimataifa.

Kabla ya uteuzi huu, Dr. Mpanju-Shumbusho alikuwa Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi ndani ya Shirika la Afya Duniani upande wa Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Magonjwa yaliyosahaulika na akiwa na cheo cha Ukurugenzi wa Idara inayoshughulikia Ushirikiano wa Shirika la Afya Duniani na Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis na Malaria). Dr. Mpanju-Shumbusho pia ni mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani kwenye Bodi ya Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria na Bodi mbalimbali za kimataifa.

Hapo awali, Dr. Winnie Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya kudhibiti Ukimwi na magonjwa mengine husika katika ya Shirika la Afya Duniani (WHO), makao makuu Geneva, Uswisi.

Kabla ya kujiunga na Shirika la Afya Duniani, amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa East, Central and Southern Africa Health Community Secretariat yenye makao makuu yake, Arusha, Tanzania. Vilevile, aliwahi kuwa Mkuu wa Idara na Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Afya ya Jamii na Mgonjwa ya Watoto, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Muhimbili University of Health Science). Katika wadhifa huu, Dr. Winnie pia alikuwa mwanzilishi wa mipango mbalimbali ya Afya na taaluma na Mshauri Mkuu wa Wizara ya Afya, Tanzania upande wa Afya ya Jamii. Pia amewahi kuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali za kimataifa.

Dr. Mpanju-Shumbusho ana Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; vilevile ana Shahada ya Uzamili katika Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Tulane, Marekani na Shahada ya Uzamili katika Medicine (Paediatric and Child Health) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, vilevile ana Shahada ya Uzamifu na Shahada nyingine mbalimbali.

Akiwa Mkurugenzi na mtaalamu katika Shirika la Afya Duniani, amekuwa mstari wa mbele katika kuandaa, kuongoza na kutekeleza mipango mkakati ya Dunia ya kujenga na kuimarisha sekta ya Afya hususani katika nchi maskini na zile zinazoendelea. Mipango hii imezaa mafanikio makubwa ikiwemo kujenga uwezo wa nchi maskini kukabiliana na maradhi ikiwemo pia afya za kina mama na watoto.

Sambamba na hilo, mipango hii pia ilifanikisha upatikanaji wa madawa ya gharama nafuu katika nchi maskini ili kuweza kumudu gharama za matibabu kwa watu maskini. Nchini kwetu, Dr. Mpanju-Shumbusho ameweza kufanikisha upatikanaji wa matibabu na huduma nasaha za kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na magonjwa yaliyosahaulika.

Dr. Shumbusho ameolewa na ana watoto wawili, wa kiume na kike.

[update] Kumekucha! Katavi wakesha vituoni wajiandikishe BVRMratibu wa zoezi la uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, mkoani Mbeya bwana Constantine Mushi amewahakikishia wananchi wote wa mkoa huo kuwa wataandikishwa kama ilivyopangwa.

Mushi ameitoa kauli hiyo alipotembelea baadhi ya vituo vya kujiandikisha na kukutana na changamoto za mashine za BVR kusuasua na kukwamisha zoezi hilo linalosubiriwa na wananchi wengi mkoani humo, hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kuwa na hofu ya kutokuwandikishwa
Changamoto ya mashine ile kama tulivyoiona, ni kama vile imechemka kwa hivyo sasa opereta anaisubiria kusudi irudi katika hali yake ya kawaida. Kwa hivyo nimewaomba wananchi hapa wavumilie. Wamenisikia na wamenielewa. Kwa hiyo ninatarajia kwamba, baada ya changamoto ya mashine, ikiendelea kufanya kazi, 'speed' waliyo nayo siyo mbaya.
Kusema tutaongeza siku kwa sasa hivi ni mapema mno kwa sababu leo ni siku ya tatu, kwa hiyo kama mashine itakuwa imetengemaa, nadhani wananchi wote walioko hapa wataandikishwa na hakutakuwa na haja ya kuongeza.

Huko mkoani Katavi, wakazi wa kata ya Nsemulwa, Migizani pamoja na Nsemulwa Shuleni, usiku wa kuamkia leo wamelazimika kukesha katika vituo vya kujiandikishia katika Daftari hilo ili waweze kuwahi foleni. Wakazi hao wameiomba Serikali kuongeza mashine za BVR na siku za uandikishaji ili wote wapate fursa ya kujiandikisha.

Taarifa via TBC.

Maembe ng'ong'o


Shukurani Salma kwa picha.

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 22, 2015
Taarifa ya habari Channel TEN, Mei 21, 2015Makada 8 TLP wafutwa uanachama

Chama kimoja cha siasa nchini Tanzania, TLP kimetangaza kuwafuta uanachama wanachama wake nane, kwa madai ya kukiuka Katiba ya chama hicho.

Maendeleo ya mradi wa umeme Kinyerezi I

Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi kwa juu

Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.
Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto
alisema Mhandisi Jilima.

Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongo la Mboto.

Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Katika miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” 
alisisitiza Bibi. Mwanri.

Ili kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.

Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani ni Bibi. Florence Mwanri (katikati), Ndg, Robert Masatu na Ndg. Aloce Shayo, kwa mfuatano

Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha KinyereziTaarifa ya Oyuke Phostine

Watalii wa ndani waenda kupanda mlima Kilimanjaro; Tatizo barabara!Magari yaliyokuwa yakitumiwa na watalii wa ndani waliokuwa wakipanda kwenda kilele cha Shira yakiwa yameegeshwa baada ya kushindwa kuendelea na safari kutokana na ubovu wa barabara .


Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa eneo la kambi ya Tembo wakisubiri magari madogo ya hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya kuwachukua kuwapeleka katika hifadhi hiyo.Watalii wa ndani walilazimika kupanda magari ya aina hii ili kufika katika kilele cha Shira.

Safari ya kuelekea kilele cha Shira ikianza.

Afisa Masoko wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro Antypas Mgungusi akizungumza jambo mbele ya watalii wa ndani mara baada ya kufika Lango la Londros kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea kilele cha Shira.

Baadhi ya watalii wa ndani.Hali ya hewa katika eneo hili ni ya kubadilika .

Watalii wa ndani wakielekea katika kilele.Wengine walikuwa na furaha mara baada ya kufika katika uwanda wa Shira.Wengine waliamua kupumzika njiani.kama anvyoonekana m,wandishi James Paul wa ITV.Hatimaye magari yaliyokuwa yameshindwa kupita kutokana na ubovu wa barabara yalifanikiwa kupita na kupanda kuwachukua watalii wa ndani.
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga

Huu ushauri, msaada au nguvu za giza...


Papo kwa Hapo: W/Mkuu atupiwa swali kuhusu Mashehe wa uamsho waliopo mahabusu
Leo katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda limeulizwa swali na Mheshimiwa Muhammad Ibrahim Sanya kuhusu viongozi wa kikundi cha "Uamsho", Masheikh wanaoshikiliwa katika mahabusu ya Segerera jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuhusishwa na ugaidi huku wakifanyiwa vitendo visivyofaa kutamkwa na wengine kuwa wagonjwa kiasi cha kushindwa kufika Kisutu siku za kusikilizwa kesi zao.

Ladies, use this tip to find out if short hair will look good on you


Who knew that the angle of the jaw bone determined whether or not someone would look best with short hair or long hair?

Try it out:
Position a pencil or pen under your chin horizontally and then place a ruler under your ear vertically. Take your measurement from the intersection of the pencil and ruler. Less than 2.25" and you'd look amazing with short hair, and if it's anything more long locks will be the most flattering choice for you. 
Now you know!

Tip from www.elle.com

Balozi Amina Salum Ali atangaza kuwania Urais Tanzania 2015

Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa, Balozi Amina Salum Ali akiwa na Rais Kikwete baada ya kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Machi 30, 2015.

Wakati vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vikianza kesho, mwanasiasa mkongwe, Amina Salum Ali, amekuwa mwanamke wa kwanza wa daraja lake ndani ya chama hicho kutangaza wazi nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu nia yake hiyo, mwanasiasa huyo ambaye pia ni Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Umoja wa Mataifa (UN), alisema wanawake wamekuwa wanyonge kugombea nafasi za juu za uongozi kwa kukosa fedha, lakini sasa ni wakati mwafaka kwao kujiamini katika jamii kwani uongozi siyo fedha bali ni uzalendo, kujikubali na kujiamini.
“Nimeona nina uzalendo, ninajiamini na ninaweza kuifikisha nchi yangu katika uchumi wa kwanza kwa kutumia rasilimali zetu zikiwamo gesi, mafuta, kilimo na utalii. Ninajiamini kwamba wakati wangu umefika kuwaongoza Watanzania wenzangu kwa kushika nafasi za juu,” 
alisema mwanasiasa huyo mkongwe.

Amina ambaye aliwahi kushika nafasi za juu za uongozi Zanzibar na Tanzania Bara, ukiwamo uwaziri wa fedha Zanzibar, alisema serikali inatambua mchango wa wanawake katika jamii hivyo kupewa nafasi kubwa kama vile ujaji na uhakimu ili kuongeza zaidi ufanisi wao kiutendaji.
“Wanawake wengi wanaogopa kujitokeza wakihofia kugombea nafasi za juu za uongozi kwamba kunahitaji fedha hivyo wanaishia kuwa wanyonge. Siyo kweli, wajitokeze kwa wingi ili kitimiza ndoto za kuwajibika kwa taifa letu,” 
alisema.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, wanawake wamepigana sana dhidi ya mfumo dume na kwamba baada ya miaka 20 ya maazimio ya Mkutano wa Dunia wa Wanawake uliofanyika mjini Beijing, China mwaka 1995, hali kwa sasa imebadilika na wanawake wanapewa nafasi mbalimbali za uongozi.

Alisema sheria hazitoshelezi kumlinda mwanamke, lakini mfumo dume umepungua kwa kiasi kikubwa hata kama haijafikia asilimia 50 kwa 50.
“Jambo kubwa kwa mwanamke ni kujiamini katika mambo yote… wanawake wa Tanzania hatuna utaratibu wa kuchangiana katika harakati za uchaguzi. Utaratibu wa mwanamke kupata fedha za mitaji kwa hapa nchini bado mgumu hasa katika mabenki lakini tusiogope. Mimi nina amini ninaweza kuiongoza jamii yetu,“ 
alisema Balozi Amina.

Balozi Amina ametangaza ni ya kuwania nafasi hiyo kubwa kuliko zote nchini wakati kesho vikao vikao vya juu vya maamuzi vikitarajiwa kuanza kwa ajili ya maandalizi ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais Oktoba, mwaka huu.

Vikao hivyo ni Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec). Kesho itaanza CC na kufuatiwa na Nec ambayo inahitimisha mchakato huo Jumapili ijayo.

Baadhi ya makada wameshatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo na wengine wanatajwa.

Waliotangaza nia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba; Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba; Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangallah na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya.

Makada wanaotajwa kugombea nafasi ya hiyo kupitia chama hicho ni Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Steven Wasira; Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli; Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro na Spika wa Bunge, Anna Makinda.

Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Balozi Amina alihitimu Chuo Kikuu cha New Delhi (India) - shahada ya kwanza ya uchumi (B.A), mwaka 1079, amehitimu Institute of Management Pune, India - Diploma ya utawala wa mambo ya fedha na utafiti wa uendeshaji mwaka 1980, pia mwaka 1981 alihitimu Chuo Kikuu cha Pune, India - (Symbiosis College of management) -MBA in Marketing (Masoko) na mwaka 1983 Chuo Kikuu cha Helsinki, Finland - Diploma ya utafiti wa masoko na uuzaji wa bidhaa nje (mafunzo maalum ya PRODEC).

NYADHIFA ALIZOPITIA

Mwaka 1981 hadi 1982 Mchumi Mwandamizi -Tume ya Mipango Zanzibar, mwaka 1982 hadi 1983 Mkurugenzi Biashara za Nje - Wizara ya Biashara ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mwaka 1983 hadi 984 Katibu Bodi ya Biashara Zanzibar-Wizara ya Biashara Zanzibar.

Nafasi nyingine ni, mwaka 1984 hadi 1985, Mchumi Mwandamizi - Tume ya Mipango, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, mwaka 1985 hadi 1990- Mbunge Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, mwaka 1985 hadi 1986- Naibu Waziri wa Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1986 hadi 1989- Waziri wa Nchi ,Wizara ya Mambo ya Nje.

Nyingine ni, mwaka 1989 hadi 1990- Waziri wa Nchi Wizara ya Fedha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1990 hadi 2000 -Mbunge Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mwaka 2001 hadi 2005- Waziri wa Fedha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mjumbe wa Tume ya Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mwaka 2005 hadi 2006- Mjumbe Baraza la Wawakilishi .

Nyingine ni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mwaka 2006 - Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) kwenye Umoja wa Mataifa.

UZOEFU KATIKA CHAMA

Mwaka 1968 alijiunga na Umoja wa Vijana wa ASP (ASP Youth League) na kuendelea na uanachama hadi kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.

Mwaka 1977 alijiunga na Chama Cha Mapinduzi baada ya kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM, mwaka 2006 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi hadi alipolazimika kujiuzulu kufuatia kuteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Umoja wa Mataifa.

Nafasi nyingine katika chama ni mjumbe wa kamati mbalimbali zilizoundwa na CCM kwa kipindi chote alichokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mlezi wa chama Mkoa Morogoro.

Mlezi wa Jumuia ya Vijana Wilaya ya Mjini mwaka 1992 hadi 2006 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM hadi alipoteuliwa AU.

Taarifa SSRA kuhusu Kanuni Na.13 ya Mafao ya PensheniTAARIFA KWA UMMA

MAELEZO KUHUSU KANUNI NO.13 


UTANGULIZI: 

Kanuni ya Uwianishaji Mafao ya Pensheni ya 2014 ina vipengele 15 ambavyo vinalenga kuboresha mafao ya pensheni ya wanachama, kulinda na kutetea maslai ya wanachama, kuhuisha kiwango cha uchangiaji na malipo ya pensheni ya wanachama wa mifuko mbalimbali na kutengeneza mfumo madhubuti ya Kisheria katika kuwianisha viwango vinavyohusiana na mafao ya pensheni. Kipengele cha 13 kinatoa punguzo la asilimia 0.3 kwa pensheni ya kila mwezi kutoka kwenye mafao ya mwanachama aliestaafu kwa hiari yaani kati ya miaka 55 mpaka 59. Punguzo hili hukoma pale mstaafu anapofika miaka 60.

Tumekuwa tukipokea malalamiko kuhusu kanuni hiyo, lakini Tafsiri halisi ya kipengele cha 13 cha kanuni za uwianishaji wa mafao, ni kwamba mwanachama anayestaafu kwa hiari atapunguziwa asilimia 0.3 kwa mwezi sawa na asilimia 3.6 kwa mwaka hadi pale atakapofika umri wa kustaafu wa miaka 60. Hivyo si sahihi kusema kwamba kipengele hicho cha 13 cha kanuni kinakata asilimia 18 ya mafao ya mstaafu kwa mwaka.

Badala yake mwanachama anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 59 anakatwa asilimia 3.6 tu kwa mwaka. Mwenye miaka 58 anakatwa jumla ya asilimia 7.2 tu kwa Mwaka, Hali kadhalika mwenye miaka 57 anakatwa jumla ya asimilia 10.8 kwa mwaka. Kwa yule anayestaafu akiwa na miaka 55 atakatwa jumla ya asilimia 18 katika kipindi cha miaka mitano au miezi 60.

Hata hivyo pamoja na punguzo la asilimia 0.3 bado mstaafu wa hiari anamzidi yule anayestaafu akiwa na miaka 60 kwa asilimia 10. Bila punguzo hilo anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 55 anamzidi mwenzake wa miaka 60 kwa asilimia 28. Hii inaondoa usawa wa mafao katika hifadhi ya Jamii. Jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na vyama vya wafanyakazi na wanachama kwa ujumla.

HITIMISHO

Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama na kutoa wito kwa wanachama na wadau wengine wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na kwa watanzania kwa ujumla kuunga mkono Maboresho katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa lengo la kuboresha mafao na kuifanya sekta kuwa endelevu. 
 
Mamlaka imeanza kufanyia kazi malalamiko ya wastaafu,iwapo kuna malalamiko yoyote kutokana na utekelezaji wa kanuni hii basi wanachama wasisite kuwasiliana na Mamlaka ili yapatiwe ufumbuzi mapema iwezekanavyo.

Mwisho tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata toka kwa vyama vya Wafanyakazi pamoja na Shirikisho lao; chama cha Waajiri; vyombo vya habari pamoja na Serikali kwa ujumla.

Ikumbukwe kuwa:
Asilimia 0.3 ni kwa pensheni ya mwezi na si kwa mkupuo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mahusiano na uhamasishaji
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA
S.L.P 31846,
Simu: +255 222761683/8, 
Dar es Salaam

Kauli ya CHADEMA kuhusu ripoti ya CAG

  • Upotevu wa shilingi trilioni 1.151 Serikali kuu pekee hauvumiliki.
  • Makusanyo yote yaliyotokana na kuongezeka kwa kodi 2013/14 yameyeyuka

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ufisadi wa kutisha uliofanyika kwenye matumizi ya fedha za umma kama ilivyobainishwa kwenye ripoti za ukaguzi wa fedha kwa mwaka 2013/2014 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Wakati chama kinaendelea kuzifanyia uchambuzi wa kina ripoti zote tano ili kuweka hadharani ubadhirifu mkubwa ambao mwingi hujificha kwenye maelezo ya kitaalam, tunapenda kutoa taarifa ya awali kama ifuatavyo;
  • Wizara tatu, Trilioni 1.151 zimepotea
Katika uchambuzi wetu wa awali tumebaini kuwa kwa upande wa serikali kuu pekee zaidi ya shilingitrilioni 1.151 zimepotea au kuliwa na wajanja walioko serikalini , kiwangio hiki ni sawa na asilimia 5.231 ya bajeti yote ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2015/16 inayoendelea kujadiliwa huko Bungeni Dodoma.

Ripoti ya CAG iliyotolewa jana inaonyesha kuwa katika Serikali Kuu, Wizara tatu tu ambazo tumezifanyia Uchambuzi mpaka sasa zimepotea kiasi cha shilingi 1.151 Trilioni , wizara hizo ni;
i. Wizara ya Fedha (TRA) , Fedha zilizopotea kutokana na bidhaa ambazo zilipaswa kuuzwa nje ya Nchi ila kutokana na uzembe zikauzwa ndani ya nchi bila kulipiwa kodi zilikuwa jumla ya shilingi 836 Bilioni.
ii. Ofisi ya Waziri Mkuu, kitengo kimoja cha maafa zilipotea jumla ya shilingi 163 Bilioni.
iii. Wizara ya Ujenzi , ziliibwa jumla ya shilingi 252 Bilioni.

  • Bajeti ya mwaka 2013/14 Mapato yote ya ongezeko la kodi yameyeyuka:
Mwaka 2013/14 yalifanyika maboresho ya sheria mbalimbali za kodi wakati wa Bunge la bajeti kodi ambazo kimsingi zilimwongezea mwananchi mzigo mzito wa kulipia kodi hizo kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali na ili kuiwezesha serikali kuwahudumia wananchi wake.

Pamoja na ongezeko hilo la kodi ,ukweli mchungu ni kuwa fedha yote iliyokusanywa kutokana na ongezeko la kodi mbalimbali katika mwaka wa fedha 2013/14 imepotea yote katika wizara tatu tu za serikali kutokana na vitendo vya kifisadi, na hii ni kwa mujibu wa taarifa CAG.

Kodi zilizorekebishwa na mapato yake ni kama ifuatavyo;
a. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148; kilipatikana kiasi cha sh.48.977bilioni
b. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;kilipatikana kiasi shilingi 131.686 bilioni
c. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147; kilipatikana kiasi cha shilingi 510.017 bilioni
d. Sheria ya Ushuru wa Mafuta, SURA, 220; kilipatikana kiasi cha shilingi 155.893bilioni
e. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82 ;kilipatikana kiasi cha shilingi 28.213 bilioni
f. Sheria ya Usalama Barabarani, SURA, 168; kilipatikana kiasi cha shilingi 19.710 bilioni
g. Sheria ya Petroli (Petroleum Act) SURA, 392;kilipatikana kiasi cha shilingi 123.725 bilioni

Hali hiyo ilifanya marekebisho yote ya sheria za Kodi zilizofanywa katika mwaka huo wa fedha kuiwezesha serikali kukusanya jumla ya shilingi 1.018 Trilioni katika mwaka wa Fedha 2013/2014 na hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Hansard ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hali hii haikubaliki na haivumiliki hata kidogo. Hapa tumezungumzia Wizara tatu tu za serikali kuu bado wizara 30 na idara mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na Halmashauri na Taasisi na Mashirika ya Umma.

Ripoti hizi zimezidi kudhihirisha kwa mara nyingine kuwa matatizo yanayowakabili Watanzania ikiwa ni pamoja na umaskini, maradhi, ujinga yanaendelea kudumu kwa sababu watawala wa Serikali ya CCM wameamua yaendelee kuwepo kwa kukumbatia adui wa nne ambaye ni ufisadi.

Ripoti hizo za CAG ambazo zimeanika ufisadi katika maeneo yaliyokaguliwa ikiwemo Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma na miradi ya maendeleo, kwa mara nyingine zimedhihirisha wazi kile ambacho CHADEMA kimekuwa kikisema kwa muda mrefu kwamba ufisadi huu unaoendelea kulitafuna taifa na kuwafanya Watanzania wazidi kuwa maskini ni matokeo ya kushindwa kwa sera, mikakati na mipango ya CCM.

Wakati kasi ya ufisadi inaongezeka kutoka mwaka hadi mwaka kwenye Serikali ya Rais Jakaya Kikwete chini ya usimamizi wa CCM, ndivyo serikali hiyo hiyo inaongeza kasi ya kushindwa kusimamia UWAJIBIKAJI ambayo ndiyo moja ya nguzo muhimu katika kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanaonekana katika kuboresha maisha ya wananchi hususan kuweka fursa za kujitafutia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimaye ustawi wa jamii nzima.

Ufisadi huu hauvumiliki tena. Watanzania wasikubali kuendelea kubeba mizigo ya watawala walioshindwa kutekeleza wajibu wao. Hali ya siasa inazingirwa na sintofahamu kubwa. Uchumi unazidi kuyumba. Kijamii, maisha yazidi kuwa magumu na walioko madarakani wamelewa madaraka. Msamiati wa UWAJIBIKAJI haumo vichwani mwao tena.

Ni mwaka wa Watanzania kuamua kuachana na ufisadi huu.

Imetolewa leo Jumatano, 20 Mei, 2015;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano- CHADEMA