Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 27, 2015
Baada ya Lowasa kuzungumza, watu wa karibu wasema kwa nini Mwakyembe, Sitta wapo kimya

SIKU moja baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuzungumza na waandishi wa habari na kumbeza Rais Jakaya Kikwete, kuhusu sera ya kilimo na makada wa CCM, Samuel Sitta na Dk. Harisson Mwakyemba, sasa kibao kimemgeukia, akidaiwa kutapatapa.

Lowassa ambaye alikuwa msaidizi wa Rais Kikwete kwa miaka miwili kama msimamizi wa shughuli za Serikali kabla ya kujiuzulu kwa shinikizo la Bunge mwaka 2008 kwa kashfa ya zabuni tata ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC, alisema serikali alikosea kuanza na kilimo kwanza na kuweka elimu kando.

Pia, Lowassa alijitetea kuhusu Richmond akisema hakula hata senti moja, isipokuwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe, aliyeongoza Kamati Teule, walipika ripoti ya kashfa hiyo ili kumdhalilisha.

Kama ilivyobashiriwa kuwa, Lowassa ameibua mzozo kwa kukinzana na utaratibu wa CCM unaowataka viongozi kupingana au kukosoana kupitia vikao badala ya kufanya hivyo hadharani, baadhi ya makada wamemjibu wakisema anatapatapa baada ya kuona hana nafasi ya kuteuliwa.

Licha ya Sitta na Mwakyembe kutojitokeza kujibu chochote, lakini baadhi ya watu walio karibu nao, wamelidokeza MwanaHALISI Online kwamba, wamempuuza Lowassa kwa sababu ukweli wote kuhusu kashfa ya Richmond uko wazi.
“Tumefuatilia kauli ya Lowassa kwa waandishi wa habari, lakini tumeshauri viongozi hawa aliowakejeli wasijibu ili kuvuruga mchakato wa uteuzi kwa sababu baadhi yao wataingia kwenye kinyang’anyiro.
“Lakini kitendo cha kukebehi hata Rais Kikwete ambaye alimwamini na kumpa madaraka makubwa ya uwaziri mkuu kuwa serikali yake ilikosea kuanza na kilimo kwanza badala ya elimu, hii ni dalili tosha kwamba Lowassa anatapatapa baada ya kubaini hana sifa za kuteuliwa kugombea urais,” 
amesema mmoja wa makada aliyeomba kuhifadhiwa jina lake ili kuepusha mtafaruku ndani ya chama.

Ameongeza kuwa, “anachokifanya sasa ni visasi vya tukose wote. Huyu amekuwa serikalini na hayo anayozungumza ndizo zilikuwa sera za CCM walizozinadi wakati wakisaka urais na badaye akapewa uwaziri mkuu kusimamia hayo”.

Naye mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangalah (CCM), ambaye ametangaza nia ya kuomba uteuzi wa kugombea urais, ameandika kupitia mtandao wa kijamii akisema, “kama Kamati ilimuonea Lowassa, basi imuombe radhi na ituombe radhi Watanzania wote”.

Amekwenda mbali zaidi akisema, “kama kweli Lowassa atagombea urais 2015, itakuwaje kwenye mijadala ya uchaguzi na CCM itasimamaje kama itampitisha kuwa mgombea, kumuombea kura wakati ilimuangusha bungeni kutoka kwenye nafasi nyeti ya uwaziri mkuu?

Dk. Kigwangalah amehoji, CCM itatoa majibu gani kuhusu kwa nini ilimuita Lowassa ‘gamba’ na ikatangaza hadharani kuanza mchakato wa kuvua magamba ambao haukukamilika.
“Nilisema jana, Lowassa amefungua pandora box, na kama atatangaza kweli kuwania urais, inabidi haya mambo yawekwe wazi, yamalizwe, maana hauwezi jua ya kesho – ikitokea akawa mgombea wetu, tutaanzia wapi kumnadi na kusema ni mtu safi, muadilifu, anayechukia rushwa na ubadhirifu na kwamba anafaa kuwa Rais, wakati juzi tulisema hafai kuwa waziri mkuu na tukamtoa?
“Nilisema kuwa, CCM haipaswi ku-risk kuteua wagombea wenye mambo mengi ya kutolea maelezo kwa wananchi, ikifanya hivyo itaangushwa asubuhi ya saa nne. Watanzania wa leo siyo wa juzi” 
ameandika Kigwangalah kupitia mtandao wa Jamii Forum.

Amefafanua kuwa Lowassa kama amekana kuhusika na Richmond, sasa wanakamati inabidi wamjibu, waweke wazi, na wamjibu kwa uwazi bila kuficha.
“Maana kama alionewa ijulikane na sisi tuliohuzunishwa ama kufurahishwa na Bunge wakati ule tuujue ukweli. Yeye anasema hakuhusika na ndiyo maana Kamati ya Mwakyembe haikuona haja ya kumwita kumhoji. Ukweli tunauhitaji sana leo kuliko jana. Ukweli huu ni haki yetu,” 
amesema.


Kikao na mapendekezo ya majimbo mapya ya uchaguzi Dar

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akiongoza kikao cha RCC, Ilala Boma jijini Jumanne Mei 26, 2015. 


Kikao kilichowaleta pamoja Wabunge wote wa Dar es Salaam, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa zote tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, Watendaji wa Manispaa hizo, na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kimependekeza kuongezwa kwa majimbo zaidi ya uchaguzi kwenye jiji hilo lenye wakazi wanaokaribia milioni tano.

Majimbo pendekezwa waliyataja kuwa ni Kijichi wilayani Temeke, Chanika wilayani Ilala, Bunju na Kibamba wilayani Kinondoni.

Mapendekezo hayo uatapelekwa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), kwa uamuzi wa mwisho.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf MwendaMbunge wa Ubungo, John Mnyika, na Suzan Lyimo, (wote kutoka CHADEMA)Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustin NdungulileMbunge wa Ubungo, John MnyikaMbunge wa Kawe, Halima MdeeMkurugenzi wa Manispaa ya Kiondoni, Mussa Nati

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia MjemaSuzan LyimoWabunge wa viti maalum wa Dar es Salaam kupitia CCM, Zarina Madabida, (kushoto), na Sophia Simba, wakiteta jamboMbunge wa viti maalum kutoka Wilaya ya Temeke, Mariam Kisangi,Wakuu wa vyombo vya dola, mkoa wa Dar es SalaamMkuu wa mkoa akisikiliza kwa makini mjadala  • Picha zote: Khalfan Said via K-Vis blog

TTCL yafumuliwa katika Hotuba hii ya Upinzani iliyosomwa Bungeni

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA MOHAMED HABIB JUMA MNYAA (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA- WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

(Inatolewa chini ya kanuni za kudumu za Bunge, kanuni ya 99(9) toleo la Mwaka 2013)

Kama hutaki kansa na mengineyo, tii ushauri wa Waziri: Tusitumie plastiki kuhifadhia vyakula hasa vya moto


Uki-google online madhara ya kutumia plastiki katika kubeba ama kuhifadhia vyakula, utakutana nayo mengi ikiwa ni pamoja na kansa. Pamoja na hilo, pia wanasayansi wametahadharisha kuhusu matumizi ya vyombo vya aluminium kama vile foil papers na kontena, vinavyotumika kufungashia, kubebea na kulia vyakula mathalan mishikaki inayofungashwa hivyo al maarufu 'nyama ya foil' (bofya hapa kurejea) au chips, wali, ugali, mihogo nk. Vile vile tumeaswa kuhusu matumizi ya vyombo vilivyopakwa dawa maalumu ili kuzuia kunata, kuganda na kuungulia 'non stick' (bofya hapa kurejea).

Kwa kuwa bado haijafahamika moja kwa moja kinachosababisha baadhi ya aina ya saratani (cancer) ni vyema kuchukua tahadhari ili kujizuia tusijiweke katika hali rahisi ya kupata ugonjwa huo kwa kutumia vitu ambavyo vimeshachunguzwa na kuonekana na walakini.

Habari ifuatayo kuhusu plastiki imechapishwa jana katika gazeti la MwanaHALISI Online...


WANANCHI wameshauriwa kutotumia mifuko ya plastiki na vifungio vyake kwa ajili ya kuwekea au kuifadhi chakula na badala yake watumie vifungashio vya glasi na chuma isiyoshika kutu na vyombo vingine vya asili.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Stephen Maselle, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mkiwa Kimwanga (CUF).

Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inasema nini kuhusu tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira unaotokana na mifuko ya plastiki.

Pia, alitaka kujua kama kuna madhara yanayoweza kusababishwa na uwekaji wa chakula cha moto kwenye mifuko hiyo.

Akijibu swali hilo, Maselle amesema madhara yanayoweza kusababishwa na uwekaji wa chakula cha moto katika mifuko ya plastiki ni pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa kemikali zilizotumika kutengeneza mifuko hiyo kuingia kwenye chakula na kukifanya kuwa na sumu.

“Sumu hii yaweza kusababisha saratani, kuharibu ukuaji wa mfumo wa uzazi hususani kwa watoto ambao bado kuzaliwa, mabadiliko ya kijenetiki, matatizo ya kushindwa kuona, uyeyushaji wa chakula tumboni kuwa wa tabu au kutokamilika na ini kushindwa kufanyakazi vizuri,” alisema.

Ametaja magonjwa mengine yanayoweza kusababishwa na mifuko hiyo kuwa ni pamoja na kuharibika kwa mfumo wa utendaji wa figo na magonjwa yanayaohusiana na mfumo wa kupumulia.

Kuhusu uchafuzi wa mazingira, amesema serikali inatambua kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira unaotokana na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Maselle amefafanua kuwa, ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo yenye unene wa chini ya maikroni 30 na kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala.

How the culture of Doctors bullying Trainee Doctors is putting patient's lives at risk


Maswali na Majibu ya kina ya Prof. Lipumba kuhusu UKAWA ikishika Dola

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema wakiingia madarakani Oktoba mwaka huu, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo alipotembelea ofisi za gazeti la Jambo Leo, jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa serikali hiyo itawaunganisha Watanzania wote.

“Tuwe na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo itawaunganisha Watanzania. Suala hili la Katiba mpya, lazima likamilishwe kwa pamoja na UKAWA tutaangalia namna ya kutatua mambo yaliyopo sasa,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema lazima tuwe na Serikali ndogo hata kama kwa sasa tutaingia madarakani tukiwa na Katiba ya sasa ambayo haitambui muungano wa vyama vya siasa.

Profesa Lipumba ambaye pia ni mtaalumu wa uchumi alisema, watahakikisha wanakuwa na wizara chache na kwamba watapenda kuwepo na katiba ambayo itawaunganisha badala ya kuwagawa.

Alisema mchakato wa katiba ya sasa umewagawa Watanzania badala ya kuwaunganisha.

Mwenyekiti huyo wa CUF alisema kwa maoni yake Serikali ya UKAWA iwe na wizara 15 na hakuna sababu ya kuwa na wizara zaidi ya 20.

Alisema hawatakuwa na tabia ya kubadilisha wizara kila mara kama inavyofanyika sasa ili kuongeza ufanisi.

Profesa Lipumba alisema kuwa na serikali kubwa yenye mawaziri wengi haina tija, labda hilo linaweza kufanyika kwenye nchi ambayo imetoka katika vita.

Alisema kama nchi imetoka katika vita lazima watu wengi waingie katika serikali ili kuepuka watu kulalamika kuwa wameachwa katika utawala.

“Ukiwa unatoka kwenye vita ndiyo unaweza kuwa na Serikali kubwa ili kukidhi mahitaji ya watu wote,” alisema.

Mahojiano hayo kwa kirefu na majibu yake ni kama ifuatavyo: 

Jambo Leo: UKAWA ukiingia Ikulu ni nini kipaumbele chenu cha kwanza?

Profesa Lipumba:
Kitu tutakachozingatia hasa ni Serikali yenye uwazi, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Serikali yetu.

Uwazi ndiyo utakaosaidia katika kutatua changamoto zilizopo nchini. Mfano tayari kuna panya road, tatizo hili linatokana na kukosekana kwa ajira. Vijana hawa wanaweza kuvamia eneo na kuibua taharuki.

Kuna vyanzo vingi vya ajira iwapo tutatumia rasilimali za nchi. Nchi yetu ina vivutio vya ajira kama bandari na ardhi, tumezungukwa na nchi ambazo hazina bandari kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda, Malawi, Zambia, Rwanda na Burundi.

Tukitumia vizuri tutakuwa na soko la ajira, lakini pia tuna ardhi ya kutosha, ambapo kilimo kikiwekwa vizuri kitasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania.

Kuna maeneo mengi yanakubali kilimo cha alizeti na ufuta, na mambo yote hayo yanaweza kuongeza kipato cha Mtanzania. Sekta ya nguo na mavazi inaweza kuongeza ajira.

Sekta ya ngozi na viatu nayo inaweza kuongeza ajira. Kwa sasa nchi yenye viwanda vingi ni China.

Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inakadiriwa kuwa na ajira milioni 90, zinaweza kuhama kutoka China kwenda nchi nyingine, hivyo lazima tujipange kwa ajili ya kupanua wigo wa ajira.

Sekta ya utalii nayo inaweza kuongeza ajira na iwapo vitu vinavyotumiwa na watalii vitazalishwa nchini. Kikubwa ni kuwa na umeme wa uhakika ambao utasaidia kuongeza chachu ya ajira.

Kwa sasa gharama za maisha ni kubwa, kuna tatizo la gharama za chakula na nchi inaweza kuongeza uzalishaji wa chakula.

Tukiamua kuongeza uzalishaji wa chakula tunaweza. China wana mashamba madogo kuliko kwetu, lakini kinachotakiwa ni kuongeza tija kwenye kilimo.

Tukifanya hivyo, mkulima atapa kipato kikubwa, lakini pia uzalishaji wa mahindi utaongezeka na kwa gharama nafuu. Mishahara lazima iendane na maisha ya mfanyakazi.

Kuna suala la ajira na kupunguza gharama za maisha.

Kipaumbele kingine ni elimu na ubora wake, kwa sasa tatizo letu kubwa pamoja na kujitahidi watoto kwenda shuleni, lakini ubora wa elimu umekuwa wa chini sana na ubora wa elimu unahusiana kabisa na masuala ya ajira.

Kama watu hawana elimu bora, maana yake hata ukiwa na uwekezaji bado watu wako watakosa ajira, kwa sababu ya kutokuwa na elimu inayokidhi soko la ajira.

Hivyo, lazima mazingira ya mwalimu yaboreshwe na hata upatikanaji wa walimu lazima wawe wale wenye uwezo wa kitaaluma. Nchi ya Singapore wanaoongoza darasani kwa ufaulu wa madaraja ya kwanza, ndiyo wanaopata ajira ya walimu.

Walimu lazima wapewe motisha na hiyo itasaidia kuinua kiwango cha elimu.

Afya nalo ni eneo ambalo litapewa kipaumbele. Kwa sasa kati ya watoto 100 wenye umri chini ya miaka mitano, 42 wapo kwenye udumavu. Kimo cha watoto hakiendani na umri wao. Suala la lishe bora linatakiwa lianzie kwa wanawake na watoto, ni jambo bora na linawezekana.

Mfano, hata alipotembelea nchini Mfanyabiashara maarufu duniani, Bill Gates ambaye ni raia wa Marekani, alishangaa kuona watoto wadogo wakitaja umri mkubwa, tofauti na vimo vyao.

Alikuwa akiuliza una miaka mingapi? Anajibiwa miaka 10, wakati yeye alihisi mtoto huyo ana miaka mitano au sita.

Hivyo, ipo haja ya kuwekeza kwenye eneo la mama na mtoto tangu mimba inapokuwa tumboni. Ni jukumu la familia, lakini iko haja kwa Serikali kuwa na mikakati ya kusimamia lishe bora.

Jambo la tano ambalo linahusiana na uwajibika, uwazi na uadilifu ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumiwa vizuri. Taarifa ambazo zimeandikwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) utaona namna ambavyo kuna matumizi mabaya.

Masuala ya Richmond, Epa na Tegeta Escrow yanaonesha namna ambavyo hakuna usimamizi mzuri wa fedha za umma. Hivyo, kupambana na rushwa na kuwa na utawala bora ni jambo ambalo litapewa kipaumbele.

Makusanyo ya kodi yanapungua kutokana na kukithiri kwa rushwa. Makusanyo ya Serikali ni madogo na hivyo, hayakidhi mahitaji.

Jambo Leo:
Unasifiwa kuwa ni mwana uchumi wa kimataifa je, umeitumiaje hiyo taaluma yako ya uchumi kuisaidia nchi yako? Je, Serikali inakuomba ushauri wowote?

Profesa Lipumba:

Katika masuala haya nakumbuka zamani nikiwa Chuo Kikuu tulianzisha utaratibu wa kuwa na mkutano kila mwaka wa kujadili hali ya uchumi, nilikuwa nasimamia mikutano hiyo.

Pia, nilikuwa mshauri wa Mzee Mwinyi wakati akiwa Rais (Ali Hassan Mwinyi), pia nilipata nafasi kuwa kwenye Kamati ya Umoja wa Mataifa enzi ya Kofi Annan alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Nimefanya utafiti katika maendeleo ya nchi mbalimbali na nilikuwa nikishirikiana na Gavana wa Benki ya Uganda, ambaye sasa ni marehemu. Tulikuwa tukiangalia namna ya kukuza uchumi na kuondoa hali ya umaskini iliyokuwepo.

Mwaka 1995, Tanzania ilikuwa na matatizo ya wafadhili na wakati ule nilikuwa nafundisha chuo kikuu kimoja nchini Marekani. Nilikuwa nikisaidia kuangalia namna ya kushauri kwenye masuala ya uchumi wetu.

Tulikuja nchini nikiwa na akina Profesa Beno Ndulu (Gavana wa sasa wa Benki Kuu ya Tanzania), na tulipokuwa nchini, tuliandika ripoti iliyofahamika kama Herena iliyotumiwa na Rais wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuimarisha uchumi.

Baada ya kuingia kwenye upinzani, siku za mwanzo nilipata shida kwani, hata rafiki zangu hawakutaka hata kunisogelea na wale waliokuwa wakinisaidia nao wakaondoka.

Wakati huo, nikijiunga na upinzani nilikuwa nikienda Kiluvya kwa jamaa yangu mmoja kujisomea, lakini ilifika mahali watu wakamwendea rafiki yangu na kumuuliza hivi nyumba yako imekuwa ofisi ya CUF ? Hivyo nikawa siendi kwenye ile maktaba.

Baadaye, ikawa afadhali baada ya Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani, nilimpa rasimu ya CUF ili aitumie katika utawala wake, lakini naona hakuipitia.

Tulipendekeza kuondolewa kwa ada ya shule, lakini michango imekuwa mingi. Kwa mfano, kodi nyingi tulishauri ziondolewe. Kwa sasa ni ngumu kukaa na rais kumweleza, hivyo tunatumia wabunge. Kwa sasa sina nafasi yoyote, ila labda kuzungumza katika mijadala.

Jambo Leo:
UKAWA haipo kisheria, mgombea mtakayempitisha na ikitokea mkachukua nchi, chama alichotoka rais ndiyo kitanufaika zaidi na ruzuku, hili unalizungumziaje Profesa?

Profesa Lipumba:

Ruzuku zinatokana na kura za wabunge na si urais. Hivyo, zitajumuishwa kura za wabunge wote kuona mmepeta kiasi gani. Mkiwa mtashirikiana, itabidi mwangalie utaratibu wa ruzuku kutokana na kura za wabunge wote.

Kuweka utaratibu baada ya uchaguzi kwa kuangalia namna gani watagawana ruzuku. Kama sheria ingekuwa inaruhusu, ilikuwa ni kuunganisha vyama ili tuingie kwenye uchaguzi tukiwa na chama kimoja.

Hata hivyo, jambo hili linategemea kuaminiana na kukubabalia na kwa lolote ambalo litatokea, basi tuwe na urahisi kwa vyama kufanya mambo yao. Sheria ya sasa chama lazima kisajiliwe na wanaosajili chama lazima wawe ambao hawana chama kilichosajiliwa.

Sheria inataka ukae miezi sita na sasa ukitaka kusajili utajikuta hatuna chama, hivyo tulichoamua ni kuaminiana. Tunashirikiana, lakini wakati huo huo, tunapambana.

Jambo Leo:
Msajili wa vyama vya siasa ana rasimu ya muswada kwa ajili ya kuruhusu kisheria vyama vya siasa kuungana, mmejipangaje kushinikiza muswada huo uharakishwe kabla ya uchaguzi mkuu?

Profesa Lipumba:

Tunasibiri hiyo sheria maana kwa jinsi ilivyo, hili ni Bunge la Bajeti, kuna nafasi ndogo ya miswada mingine. Kuna tetesi kuna muswada wa vyama vya siasa, muswada wa kura ya maoni.

Kwa sasa tupo kwenye sintofahamu, maana hata uchaguzi mkuu haufahamiki. Kwa mazingira yalivyo wabunge wa CCM ni wengi wakiona kuna muswada ambao unaibana Serikali kipindi hiki cha wakati wa majeruhi, itakuwa ngumu kupita.

Majimbo ya Dar es Salaam na mengine 11 wanaendelea na majadiliano, lakini mpango wa kugawa majimbo nao umetuweka njia panda, tunauliza Dar es Salaam vipi, wanasema mchakato unaendelea.


Majimbo halisi ya uchaguzi hayajafahamika. Wilaya ya Masasi tumeambiwa kutakuwa na Halmashauri ya Masasi Vijijini, hivyo kama kuna halmashauri zaidi ya moja, hilo litaongeza kuwa, jimbo lingine la uchaguzi. Tamati itategemea namna ambavyo majimbo yatakavyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Jambo Leo:
Chama cha CUF kina nguvu zaidi Zanzibar, katika uchaguzi wa mwaka huu, chama kimejipangaje kuhakikisha kinakuwa na nguvu Tanzania Bara?

Profesa Lipumba

Mwaka 2010, tulikuwa na majimbo mawili tu, lakini tulikuwa na asilimia 10 ya kura za wabunge kwa upande wa Bara. Tunapata kura za wabunge sehemu mbalimbali.

Chama cha CUF tunaongoza katika ‘kuchakachuliwa’ Mfano mwaka 2010, nilikuwa naishi Kilongawima Kata ya Kunduchi, nilikwenda kumpigia kura mgombea wangu wa udiwani na nina uhakika nilimpigia, lakini diwani wangu matokeo akapata sifuri.

Pamoja na kura yangu niliyompigia na ingawa inawezekana yeye hakujipigia. Jimbo la Mafia 2010, CUF walishinda, lakini wakamtangaza mbunge wa CCM ameshinda na hata kusababisha mtafaruku. Maana tulishinda, lakini tukaporwa ushindi.

Wakati mwingine ili ushinde lazima upate watu wa ndani kule zinakohesabiwa kura ili hata wakiiba, wasimalize zote. Hivyo, kwa kutumia UKAWA huenda tukashinda kwa kulinda kura zetu.

Jambo Leo:
Chama cha CUF huwa mnadai kushinda uchaguzi mkuu Zanzibar, lakini mnaibiwa kura je, uchaguzi wa mwaka huu chama kimejipangaje kuhakikisha ya nyuma hayarudiwi?

Profesa Lipumba:
Hili ni suala zuri na suala gumu, kwanza Zanzibar maandalizi makubwa ya uchaguzi mkuu yamefanyika, lakini mgawanyiko ndani ya CCM na hata mchakato wa Katiba CCM walipendekeza mfumo wa mamlaka tatu na ulijadiliwa ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Walikubaliana kuwa na mfumo wa Serikali ya Tanganyika kutovaa koti la muungano na kilichotokea Dodoma ilikuwa ni sawa na usaliti. Hivyo, kwa Zanzibar, Mansul Yusuf Himid aliamua kuondoka CCM na kujiunga CUF.

Hivyo, dalili ya ushindi ni kubwa sana, kwa hiyo ni matarajio yetu hata kuiba itakuwa ngumu. Najua mbinu zinaendelea na kuna vijana wetu wamenyimwa hati za ukazi na hiyo itasababisha washindwe kupiga kura.

Bado tuna kazi kubwa ya kulinda kura. Pia, hata mwaka 2010 tulishinda, lakini tukapokonywa ushindi. Kuendelea ‘kuchakachuliwa’ kutasababisha uvunjifu wa amani. Ndiyo maana nataka kuonana na rais ili kuangalia namna ya kufanya.

Jambo Leo:
CUF kinaelezwa kuwa, ni chama cha mwambao ambapo kina mbunge Lindi Mjini na Kilwa, unalizungumziaje hili, je, mtaendelea kuwa wa pwani tu?

Profesa Lipumba:

Tuliwahi kuwa na mbunge Kagera, Kanda ya Ziwa tuna ngome kubwa, lakini tumekuwa tukichakachuliwa. Tuna madiwani tisa katika ukanda huo wa ziwa tangu mwaka 1994. Tangu mwaka huo hadi sasa bado tuna madiwani huko. Kuna majimbo kule Tabora tunakuwa katika nafasi ya pili wakati wa uchaguzi licha ya kuwa hatuvuki kutangazwa ushindi.

Lindi na Mtwara ni pazuri, Tunduru pazuri, Tanga pazuri, Pangani napo pazuri. Handeni panaimarika na Kanda ya ziwa.

Jambo Leo:
Nini faida ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa CUF katika upande wa Zanzibar? Je, mtaendelea na mfumo huo wa Serikali hata kama mkishinda?

Profesa Lipumba:

Faida ni kubwa ambayo ni kuleta amani na utulivu Zanzibar, ambayo ina faida. Sera ya CUF tangu mwaka 1995, tumekuwa tukihitaji Umoja wa Kitaifa. Sera ya umoja wa kitaifa Zanzibar ni sehemu ya Katiba. Serikali ya umoja wa kitaifa iwe kwa ngazi zote ili kuleta ufanisi wa kuwatumikia wananchi.

Jambo Leo:
Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura, ikitokea hadi Agosti mchakato haujamalizika hivyo, uchaguzi kutokuwepo au wananchi wengi kutoandikishwa, UKAWA mtachukua hatua gani katika suala hilo?

Profesa Lipumba:

Ndugu zangu tasnia ya habari ndiyo mnaouhabarisha umma. Tume ya Uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kuboresha daftari la wapiga kura mara moja au mbili.

Inasikitisha hadi sasa hawajaboresha hata mara moja na wameanza kuandikisha upya. Mnakumbuka Februari mwaka 2013, nilipewa kitambulisho cha taifa.

Rais alisema vitambulisho hivyo ndiyo vingetumika kwa ajili ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu. Alisema amezungumza na Waziri wa Fedha na makatibu wa wizara hiyo wapewe fedha za kutosha.

Hivyo, ilikuwa lazima waandikishwe wapigakura wote kwenye daftari hilo hadi Julai, tukaitwa na NEC wakasema wataanza kuandikisha Septemba na tuliambiwa uandikishaji utachukua dakika tatu kwa mujibu wa tume.

Muda walioupanga hawakuanza na wakaanza na majimbo ya mfano ya Kawe, Kilombero na Mlele huko Katavi. Utawaelezaje wananchi kwamba, hujaandikisha watu wakati suala linajulikana kwa miaka mitano.

Wameanza Njombe uandikishaji mzuri, lakini nimekwenda mikoa ya Kusini, hali sio nzuri, Kwa mfano katika Kituo cha Mahoha, watu wanakwenda kuandikisha wanatokea kijiji nambari A kilichpo kilometa 15 kutoka Mahoha.

Wilaya ya Newala, kule watu bado wana changamoto ya kuandikishwa maana idadi kubwa ya watu hawajaandikishwa. Tunduru watu zaidi ya asilimia 60, hawajaandikishwa.

BVR 8000 kama zitaingia Jumapili ya mwisho ya Oktoba itakuwa tarehe 25, siku za kampeni ni 70, hivyo Agosti ndiyo kampeni zitaanza, muda huu uliopo unahitaji kuandikisha watu milioni 23.5, ambao hadi sasa hawajafika watu milioni moja.

Sasa unajiuliza, hivi hawa watu wote wanaandikishwa sawa, watu wawe na taarifa, lakini Tabora wanaanza leo (wiki iliyopita), na viongozi wangu hawana taarifa. Hakuna ratiba ya uchaguzi hadi sasa maana hakuna chochote.

Kila wakati unamsikia rais akisema anaondoka mwaka huu, lakini Tume ya Uchaguzi kila siku inazungumzia kura ya maoni na ukiangalia sheria tayari imevunjwa, maana hakuna kinachoweza kusimamia kura ya maoni.

Tuliuliza, wakasema wanaandikisha wapigakura na kama Serikali itatoa fedha, watafanya kura ya maoni na sheria ilikuwa ikisema ipigwe ndani ya siku 114.

Vijana wanaokwenda kuandikisha wanafanya kazi kwenye mazingira magumu na kijana anaanza kazi saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni, na pale kijijini kwake na kwa wiki analipwa sh. 100,000.

Wakichoka hawawezi kuendelea itabidi wapumzike. Tunduru ambako mashine zipo, lakini fedha za kulipa vijana hazipo, kwa hiyo mashine zimekaa ndani.

Fedha walizo nazo haziwezi kuwalipa vijana wote na motisha ni ndogo. Hivyo, kwa sasa kinachotakiwa kupewa kipaumbele na Serikali ni kuandikisha watu maana bila hivyo, watu hawawezi kupiga kura.

Haiwekani wapigakura wa 2015, wakawa wachache kuliko wa mwaka 2010. Maana kinachotokea uchaguzi utaingia kasoro na watu wanaweza kwenda mahakamani kwa kueleza wamenyimwa fursa.

Hivyo, lazima Serikali itoe fedha za kutosha kukamilisha mchakato huo.

Kwa sasa tunaijulisha Serikali kuwa, lazima tuzungumzie hili ili watu waandikishwe.

Jambo Leo:
CUF kipo kwenye harakati ya kuwapata wagombea urais na huko nyuma wewe Profesa Lipumba umegombea mara nne je, uchaguzi wa mwaka huu utaomba tena kupeperusha bendera ya CUF kugombea urais?

Profesa Lipumba:

Kama UKAWA watateua mgombea urais na mimi nikabahatika kuteuliwa, nitagombea. Sina mpango wa kugombea ubunge kwa kuwa si saizi yangu.

Jambo Leo:
Chama chako kinaonekana kama cha kifalme kwamba, wale wanaotaka kugombea uongozi wa juu wa chama yaani nafasi ya katibu na mwenyekiti taifa wanaonekana walafi wa madaraka. Je, hili halioneshi kwamba, ni udikteta? Nini hatma yako ya uongozi ndani ya chama?

Profesa Lipumba:

Mwaka huu uenyekiti walikuwa watatu, mmoja alitoka Shinyanga, mwingine kijana wa hapa hapa Dar es Salaam, ambaye alijitoa wakati wa kupiga kura.

Nilikuwa sitaki kugombea mwaka 2000, akaja Wilfred Rwakatare akataka nigombee walau kwa miezi sita watatafuta mwingine, lakini hakutokea. kwa upande wa Maalimu Seif Sharrif Hamad watu hawajazi fomu, na utaratibu wetu mwenyekiti akitoka bara, katibu mkuu anatoka Zanzibar.

Hamad Rashid alitaka kugombea, lakini alitangaza kabla ya wakati, si kweli kwamba, kuna udikteta au ufalme ndani ya CUF. Rashid wakati anataka kugombea nilikuwa nje.

Jambo Leo
Hamna ukomo kwenye Katiba?

Profesa Lipumba:

Katiba yetu haina ukomo, mkiweka ukomo mnajimaliza badala ya kujiimarisha. Huwa natoa mfano wa Senegal, Rais aliyemaliza muda wake, Abdoulaye Wade, aliingia kwenye ujenzi wa chama tangu mwaka 1975 na akaja kufanikiwa kuwa rais mwaka 2000.

Hatujapata mfumo wa vyama vingi maana kipimo cha vyama vingi lazima chama tawala kikubali pale kinapoanguka. Ndiyo inaweza kupimwa.

Kwa utaratibu huu kila mwaka mbinu mpya za uchakachuaji zinafanyika. Wakati wa uchaguzi masuala ya itikadi za kidini yasiwepo. Sera za viongozi wa vyama vya siasa zisijikite kwenye dini. Tujikite kwenye utatuzi wa ajira na elimu.

Historia, shule nyingi na za misheni. Wakristo wengi wamesoma na Waislamu nao wapo waliosoma. Watu wasio na elimu bora ni kundi kubwa. Waliosoma ni wachache na wanaweza kuwa pande mbili zote, Waislamu na Wakristo, zina shida.

Pande zote zimekosa ajira na elimu bora. Makabila yote, wengi wao hawana elimu bora na afya bora. Sera za kibaguzi lazima ziondolewe.

Jambo Leo:
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, chama chenu ni miongoni mwa vyama vyenye hati chafu kutokana na ruzuku kutumika vibaya. Je, huoni kama mkipewa madaraka mataendelea kuwa wale wale wafuja fedha za umma?

Profesa Lipumba:

Matatizo yaliyojitokeza kwenye ukaguzi wa CAG, ni ukosefu wa vielelezo. Kwa mfano mnaponunua mafuta, lazima upewe EFD’s. Tunaeleza matatizo kama hayo na mengi ni vielelezo vya matumizi vya yanayofanyika.

Habari hii imeandikwa Claudia Kayombo na Said Mwishehe.Kajala katika mahojiano @SporahShow


Mnada wa mali za Ubalozi wa Marekani: Gymn equipment na Magari


UNIVERSAL AUCTION CENTRE

SINZA _ - LION STREET

MNADA --- AUCTION

PROPERTY OF: AMERICAN EMBASSY DSM

VIEWING DATE: 27-29 MAY, 2015

VIEWING TIME: 9:00AM- 5:00 PM

AUCTION DATE: 30 MAY, 2015

AUCTION TIME: 10:00AM
Wiki ya Ukombozi wa Afrika na uzinduzi Mradi wa Uhifadhi Nyaraka Urithi TanzaniaProfesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti ACT atangaza kuwania Ubunge 2015


Taarifa ya habari Channel TEN Mei 25, 2015MOAT yaunda kamati kupinga muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari kujadiliwa

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (tai nyekundu) na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari.
picha: Khalfan Said

via Channel TEN — Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini, MOAT , kimeunda kamati ambayo itaenda mjini Dodoma kwa ajili ya kupinga kujadiliwa bungeni muswada wa sheria za vyombo vya habari.

Akizungumza jijini Dar es Salam mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi amesema muswada huo unakandamiza haki na uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki ya wananchi kupata habari jambo ambalo linanyima demokrasia katika vyombo vya habari hivyo.

Dk. Mengi amebainisha kuwa ni wakati sasa kwa vyombo vya habari kuweza kupiga kelele juu ya ubovu wa muswada huo ambao unatarajia kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na katika kufanikisha hilo watatoa elimu kwa wabunge kuhusiana na muswada huo unavyokandamiza uhuru wa habari.

Mengi amesema vipengele vilivyotumika katika mswada huo ni wazi vinataka kuuwa tasnia ya habari pamoja na ajira kwa waandishi wa habari jambo ambalo sio njema kwa taifa.

Serikali imeandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha bajeti kinachoendelea mjini Dodoma ili kujadili miswada ya sheria.


Mengi, Tido Muhando, kutoka Azam TV, (katikati) na mkurugenzi wa Mwanachi Communications Limited, Francis Nanai

Mpandimizi, Nyalla, na Mkurugenzi wa Hali Halisi, Saed Kubenea

Moto wateketeza ghala la viatu


Moto mkubwa umeibuka katika ghala la kuhifadhia bidhaa za viatu aina ya Yebo Yebo lililopo mtaa wa Banda la Ngozi katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Kwa mujibu wa mashuhuda pamoja na walinzi katika ghala hilo, moto huo ulioanza majira ya saa moja asubuhi, unadaiwa kusababishwa na kiwanda cha jirani kinachotengeneza vyuma vyenye madini ya kopa.

Vikosi vya zimamoto kutoka halmashauri za jiji vilifika eneo la tukio ambapo jitihada zilifanyika katika kuudhibiti moto huo, ingawa ilichukua muda mrefu kutokana na kushindwa kuufikia moto huo ndani.

Mmoja wa wamiliki wa kiwanda hicho raia wa china amesema tatizo la tishio la kuibuka moto lilikuwepo kwa muda mrefu kutokana na kuongezeka kwa joto kali mara kwa mara ndani ya ghala hilo, hasa wakati kiwanda cha jirani kinapofanya shughuli zake.

Amesema ghala hilo limekuwa likitumika kuhifadhia bidhaa zilizokuwa tayari zimetengenezwa, hivyo umesababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Mobile to enhance the lives and livelihoods of world’s poorest farmers

Vodafone today published its Connected Farming in India report* which concludes that the introduction of six simple mobile services designed to help small-scale farmers in emerging markets could boost the farm gate incomes of 70 million Indian farmers by US$9 billion in 2020.

The Vodafone report, based on research commissioned from Accenture Strategy with support from the Vodafone Foundation, has found that the mobile services summarised below could enhance earnings by an average of US$128 a year for almost two-thirds of Indian farmers, achieving a material positive impact in communities where the average farming household lives on less than $4 a day and many farmers struggle to feed and educate their families.

India is one of the world’s largest food producers with more than 200 million people currently estimated to work in agriculture, around 100 million of them farmers and the remainder working as agricultural labourers. In India, around 62% of farmers own less than one hectare of land, significantly increasing their exposure to the effects of crop failure, pests, disease and volatile market pricing.

 Vodafone and Accenture Strategy have identified six mobile services with the potential to transform Indian farmers’ lives and livelihoods.
    ·         Agricultural information services providing early warning of weather events, information on the best times to harvest and advice on crop techniques to enhance yields. These services could increase an estimated 60 million Indian farmers’ annual incomes by an average of US$89 a year in 2020.

·         Receipt services to provide greater transparency in daily commodity supply chains, allowing farmers to raise their incomes by improving efficiency and eliminating fraud.
Payments and loans enabling
farmers to access simple and secure financial products and services using mobile money payment systems such as Vodafone’s M-Pesa, launched in India in April 2013. Access to highly cost-

·         effective micro-finance and quick and transparent electronic payment systems could provide an annual benefit of US$690 for some farmers in 2020, representing a 39% increase in their average farming income.

·         Field audit enabling auditors monitoring quality, sustainability and certification requirements to move away from paper records and adopt instead electronic reporting via tablets and mobile data, greatly enhancing efficiency and potentially increasing annual average income by US$612 for some farmers.

·         Local supply chain enabling small-scale producers to transact with local co-operatives through simple but robust information services and mobile money systems. These could boost some farmers’ annual incomes by US$271 in 2020; a 50% increase on current farming incomes.

·         Smartphone-enabled services to provide deeper functionality and richer sources of information than is possible using basic SMS and voicemail services. While smartphone penetration is currently low in rural areas in emerging market economies, average device prices continue to fall year-on-year. Advanced and affordable mobile services could lead to an increase in average annual farming incomes of US$675 for more than four million farmers in 2020.

Expansion of the Vodafone Farmers’ Club

Vodafone also announced today that it is launching its Farmers’ Club initiative in four additional emerging market countries – India, Ghana, Kenya and Tanzania. The Vodafone Farmers’ Club is a social business model which offers a range of mobile services to help farmers boost productivity. It was first launched by Vodafone in Turkey in 2009; around 25 per cent of the Turkish population work in agriculture and the Farmers’ Club programme has benefitted 1.2 million farmers, helping them to enhance crop yields and increase farm gate incomes.

 Specific Farmers’ Club services offered in each country will vary but will include information services, virtual marketplaces in which farmers can sell their produce and mobile money financial services and products. Vodafone will also develop a variant of the Farmers’ Club concept for farmers in New Zealand, a country with an advanced agricultural industry. Vodafone New Zealand is harnessing the strength of its extensive rural network to connect farms, agribusinesses and rural communities, helping to drive productivity, profitability and innovation.
 Vodafone Group Regional Chief Executive for the Africa, Middle East and Asia Pacific region Serpil Timuray, said:   “One-third of humanity relies on food grown by 500 million smallholder farmers with less than two hectares of land.  Mobile has a critically important role to play in increasing agricultural resilience and enhancing quality of life for some of the poorest people on earth. Our experience in Turkey has demonstrated how mobile services can transform farmers’ ability to increase crop yields, improve efficiency and grow farm gate incomes.

“As the global population continues to expand, farmers have an urgent need to produce ever-increasing amounts of food without destroying habitats or depleting resources in a way which is unsustainable. Smart and forward-looking initiatives such as the Vodafone Farmers’ Club concept can make a real difference in addressing the global challenge of food production and security.”