Watangaza nia mnaitania Serikali au mko 'serious'?


"WATANGAZA NIA" MUNAITANIA SERIKALI AU MUKO "SIRIAZI"?


Kwa kipindi cha kama mwaka mmoja nimekua miongoni mwa watu wanaofuatilia kwa karibu kinachoendelea kuelekea uchaguzi mkuu wa wabunge na rais wa mwaka 2015. Kila nipatapo muda hujitahidi kumfualitia kila aliyeonesha nia ya kutaka kuwa kiongozi bila kujali ni udiwani, ubunge au urais. Ninawafuatilia kujua historia zao, kujua mawazo na mitizamo yao, kujua uwezo wao, kujua misimamo yao juu ya mambo ya msingi ya kitaifa na mengine mengi. Kwa kuwa hadi sasa wengi wa walionesha kwa uwazi kutaka uongozi wa nchi yetu hasa katika ngazi ya urais ni wanachama cha mapinduzi (CCM), nimekua makini zaidi kusikiliza kauli zao wanazozitoa kwa njia yoyote ile ili kuona wana mtazamo gani juu ya hali ya nchi yetu kwa sasa na wana mawazo gani mbadala ambayo wanadhani yataleta mabadiliko katika taifa letu.

Katika kuwasiliza wengi wa wanaotarajia kuteuliwa na chama chao kugombea nafasi ya urais, nimevutiwa na jambo moja kubwa ambalo ni utata au sintofahamu kati ya wanachokisifia kama mafanikio na wanachokiona kama matatizo wanayokusudia kuyatatua. Nimesema utata kwa sababu inakua ngumu kuelewa wanasifia nini, wanakosoa nini na wanataka kubadilisha nini. Ingawa kila mmoja amekua na mambo yake ambayo anayapa uzito wa kipekee, naweza kuweka mawazo yao katika ujumla bila kuwataja kwa majina kusema nani kasema nini. Ukiwasikiliza vema utaona kila mmoja wao anaonesha kwamba kuna mambo mengi hayajakaa sawa katika nchi. Utaona wanavyolalamika kuhusu ubovu wa mifumo iliyoko na kwa jinsi gani imeshindwa kukidhi mahitaji ya wakati na wananchi kwa ujumla wao. Baadhi ya malalamiko yao au mambo ambayo wanadhani yamekosa wa kuyatatua ni haya yafuatayo:
 • Nimewasikia baadhi yao wakionesha kwamba serikali na nchi inahitaji mabadiliko makubwa na kuna haja ya kufumua kila mfumo ulioko na kuweka mpya ikiwa ni pamoja na kubadili viongozi na watumishi ndani ya taasisi na idara za serikali kama namna ya kuleta tija
 • Nimewasikia karibu wote wakiongelea tatizo kubwa la ajira kwa vijana. Tatizo hili limepewa umuhim wa kipekee na wengine wameliona kama ajenda yao kubwa ya kutafuta nafasi ya kuteuliwa. Wanalalamika kwamba vijana wanasoma lakini hawana ajira na hawasikilizwi. Ingawa wengi wao ni sehemu ya serikali iliyoko nimewasikia wakionesha kwamba serikali imeshindwa kutatua tatizo hili
 • Nimewasikia wakielezea tatizo kubwa la rushwa katika nchi yetu. Wengi wa watarajiwa hawa wanalalamika kwamba nchi imeoza kwa rushwa na haki imepotea
 • Nimewasikiliza watarajiwa hawa wakieleza jinsi gani rasilimali za nchi hazitumiki vizuri kusaidia wananchi na kunufaisha taifa
 • Nimewasikia wakilalamika kwamba mfumo wetu wa elimu umeharibika na hauna mwelekeo na kiwango cha elimu yetu kimeshuka. Wanatuahidi kwamwba ndoto zao zikifanikiwa wataleta muharubaini wa elimu na kuifanya kuwa ya daraja la kwanza
 • Nimewasikia wakilalamika juu ya wizi wa mali za umma na ufisadi uliokithiri nchini
 • Nimewasikia wakiongelea kushuka kwa maadili na uminifu kwa watumishi wa umma 
 • Nimewasikia wakisema nchi imekua legelege na mambo yanachukuliwa ovyoovyo tu
 • Nimewasikia wakisema wanatamani wapewe nafasi wafanye maamuzi maana serikali iliyoko haifanyi maamuzi (magumu na mepesi) na hivyo kufanya mambo mengi kutotekelezeka
 • Nimewasikia wakiongela tatizo la huduma za kijamii kama maji, afya na usafiri. Wanaonesha ni kwa jinsi gani huduma hizi hazidhirishi na hakuna wa kuzitatua
 • Nimewasikia wakiongelea tatizo la uchumi na wana mawazo ambayo wanadhani yatabadilisha hali ya uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja

Sina tatizo na mambo haya iwapo waheshimiwa watarajiwa hawa wameyaona na wanadhani yanahitaji mtu sahihi kama wao kuyatafutia ufumbuzi. Tatizo langu liko katika mambo mawili:

Moja: ni ukweli kwamba watarajiwa hawa wote wako chama kinachoongoza serikali na wengi wao ni wajumbe wa vikao na mikutano ya maamuzi ya chama. Ninachojiuliza, haya mambo wamewahi kuyasema ndani ya chama chao? Mambo haya wamewahi kuyaelezea kwa mzigo na uzito huuhuu kwenye chama na serikali yao kama wanavyoonesha kwetu? Nini kilitokea?
 • Wengi wa watarajiwa hawa ni sehemu ya serikali na wenye nafasi kubwa ya maamuzi na kuleta mabadiliko. Haya wanayolalamika kuwa hayatendeki ndio hasa tuliyotegemea wayafanye kama majukumu yao ya msingi. Kwa nini hawayafanyii kazi sasa na wanadhani hadi wawe viongozi wakuu wa nchi ndio yatafanyika?
 • Labda na hili pia sio shida na huenda wana maelezo na sababu za msingi kwa nini mawazo na mipango yao haitekelezeki katika mazingira ya sasa ingawa ningetamani sana kujua sababu zao. Nijue walifanya nini kikawa kigumu kwao na kitakwendaje kuwa kirahisi baadaye.

Mbili: iwapo jambo la kwanza ni sahihi kwao au la, nina la pili linalonisumbua zaidi. Ukiwasikiliza watarajiwa hawa, utashangaa wanapokuwa katikati ya maelezo yao au mwishoni ghafla wanabadili kauli na kuanza kuisifia serikali iliyoko kwamba imefanya mengi na makubwa sana. Kama vile hiyo haina uzito wa kutosha, utawasikia wakimtaja Rais kwamba katenda mambo mengi sana makubwa na mazuri. Watamsifika kwamba kaipasiha nchi kimaendeleo na utendaji wake hauna mfano. Utawasikia wakisema pengo lake halitazibika na atakumbukwa daima.

Nini kunawakuta watarajiwa hawa? Kwa nini wanakua na kuali za kujichanganya? Inawezekanaje mtu ukuwa na malalamiko gunia nzima juu ya mambo ambayo unadhani yangefanywa na serikali au kusimamiwa na Rais aliyeko madarakani na wakati huohuo ukaanza kumsifia kwamba kafanya na anafanya mambo makubwa? Nini kinatokea? Huwa wanakumbuka kwamba bado hawajakabidhiwa bendera na kwamba kuna chama na kiongozi wake mkuu ambao wameshika mpini na wao wako kwenye makali?

Watarajiwa hawa huwa wanamaanisha nini? Kwa nini wasiwe wa kweli na wawazi tu katika yale wanayoyasimimia? Kwa nini wasiwe wazi tu kusema serikali na kiongozi wake wameshindwa kazi na ndio mana mambo yako jinsi yalivyo na hivyo wao wanakuja kubadilisha? Au kwa nini wasituambie tu kwamba serikali na Rais wetu wametenda miujiza na kuleta maendeleo makubwa na wao hawana jipya ila wanakwenda kusimamia tu yale ambayo kayafanya na kuendeleza mipango Rais anayoiacha?

Ninategemea wanapoanza kutangaza nia zao rasmi, watakumbuka kuliweka hili sawa na watupe kauli zisiyotukanganya, tututania wala kutudanganya. Zaidi sana wasimtanie Rais wetu na serikali yake. Tunaweza kuwaelewa tu na wanapotaka kutupeleka bila kumuhusisha yeye na serikali anayoiongoza.

Mwalimu MM
[email protected]

Mratibu Mkazi wa UN na Waziri wa Mambo ya Ndani wazuru eneo la mapokezi ya wakimbizi Kigoma

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma, eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Modewjiblog Team

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katikati ya wiki wametembelea eneo la mapokezi ya Wakimbizi kutoka Burundi lililopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Walipofika katika eneo hilo la mapokezi waliojionea huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula duniani (WFP), Shirika la afya duniani (WHO) pamoja na Shirika la UNFPA linaloshughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.

Wakimbizi wengi waliofika eneo hilo walikuwa na afya dhoofu kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu.

Kutokana na hali hiyo baadhi yao ilibidi wapatiwe huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya makazi yaliyotengwa kwa Wakimbizi ikiwemo kambi ya Nyarugusu iliyopo katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Hata hivyo kambi hiyo ya Nyarugusu ina uwezo wa kuchukua sio zaidi ya Wakimbizi 50,000 lakini sasa ina Wakimbizi zaidi ya 48,000 kutoka Burundi na 60,000 kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo.

Aidha Waziri Chikawe alisema kuwa Serikali imetenga eneo maalum ambalo litajengwa kambi mpya itakayojulikana kama Nyarugusu B ambayo itakuwa ni mahususi kwa Wakimbizi kutoka Burundi.

Mh. Chikawe alisema kuwa kambi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu kutoka hivi sasa, ili kuwatenganisha Wakimbizi kutoka Congo na Burundi.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaoandikisha Wakimbizi wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto) walipotembelea uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.Mmoja wa watoa huduma kwenye kituo cha muda cha Wakimbizi katika viwanja vya Lake Tanganyika akipuliza dawa ya kuua wadudu kwenye mifereji inayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi waliokuwa kwenye foleni ya kupanda mabasi kuelekea kambi ya Nyarugusu kwenye makazi maalum yaliyotengwa na Serikali ya Tanzania yanayohudumiwa na Shirika linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi ya Umoja wa mataifa. Wanne kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.Foleni ya Wakimbizi kutoka Burundi kuelekea kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la IOM kuwapeleka kwenye eneo maalum la kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakishuhudia baadhi ya Wakimbizi wakipakia kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM tayari kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (aliyeipa mgongo kamera kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiagana na baadhi ya Wakimbizi wanaoelekea kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutokea katika kituo cha muda cha mapokezi na huduma za afya kilichopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.Baadhi ya wakina mama na watoto zao wakiwa wamejipumzisha ndani ya viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Wahudumu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiwapulizia dawa maalum kwenye mikono na miguu kwa ajili ya kuua bakteria kabla ya kuingia ndani ya mabasi na kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakielekea kutembelea mabanda mbalimbali ya huduma za afya yaliyopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika yanayotoa huduma kwa Wakimbizi wanaowasili kabla ya kupekwa kambini.Pichani juu ni baadhi ya watoto wakipatiwa matibabu ndani ya kituo cha muda kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.Wazazi na watoto wakiwa kwenye hema maalum, huku nwengine wakiwa kwenye dripu za kuongezewa maji mwilini.

Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wakisafisha mikono yao na kupuliziwa dawa maalum katika viatu mara baada ya kutembelea mahema yenye wagonjwa mbalimbali Wakimbizi kutoka Burundi wanaopatiwa matibabu kwenye kituo cha muda kilichopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.Baadhi ya watoto wakijiliwa na kujifaraji kwa kucheza mpira katika kituo maalum cha kupokelea Wakimbi wanaotafuta hifadhi nchini Tanzania wakitokea nchini Burundi katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.Pichani juu na chini ni familia za Wakimbi wakiwa wamejipumzisha kwenye kituo cha muda katika viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Sehemu ya eneo la uwanja wa Lake Tanganyika.

Hotuba ya Rais Kikwete kwa Walimu alipofungua Mkutano wa CWT Arusha


HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA TAREHE 26 MEI, 2015 MJINI ARUSHA

Ndugu Gratian Mukoba, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania, TUCTA;
Mhe. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Mheshimiwa Gaudencia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira;
Mheshimiwa Celina Kombani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma;
Mheshimiwa Hamis Majaliwa, Naibu Waziri – TAMISEMI;
Mheshimiwa Margaret Sitta, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Jamii;
Mhe. Felix Daud Ntibenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha;
Ndugu Msulwa, Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania;

Ndugu Nicholaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania, (TUCTA);
Ndugu Ezekiel Oluoch, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania;
Ndugu Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Walimu Tanzania;
Mke wangu Mama Salma Kikwete;
Ndugu Walimu;
Wageni waalikwa;
Shukurani
Nakushukuru sana Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Ndugu Gratian Mukoba na viongozi wenzako wa CWT kwa kunialika na kunipa heshima kubwa ya kufungua Mkutano wenu Mkuu. Nawapongeza kwa maandalizi mazuri ya mkutano.  Kufanikisha mkutano wa Wajumbe 1,200 si kazi ndogo hata kidogo. Hivyo basi unapofanikiwa ni jambo linalostahili pongezi.  Hongereni sana. Pia nikushukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wananchi wote wa Mkoa huu kwa mapokezi mazuri na kwa kukubali kuwa wenyeji wa mkutano huu.  Mmekuwa wenyeji wema. Hongereni sana.
Pongezi kwa CWT
Ndugu Rais
Ndugu Waalimu;
Natoa pongezi kwa viongozi wa Chama cha Waalimu wanaomaliza muda wao kwa kazi kubwa nzuri waliyofanya na kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.  Mmeifanya vyema kazi ya kutetea haki na maslahi ya walimu. Tumejionea jengo kubwa na zuri la kitega uchumi lililojengwa Ilala, Dar es Salaam. Jengo hili lijulikanalo kama Mwalimu House limependezesha sana eneo la Ilala na jiji la Dar es Salaam.  Kama kwamba hiyo haitoshi hivi karibuni tumepokea habari nyingine njema za kuanzishwa kwa Benki ya Waalimu itakayojulikana kama Mwalimu Bank. Mafanikio haya na mengine mengi ambayo sikuyataja, yanafanya CWT kuwa moja ya vyama vya wafanyakazi mahiri na makini nchini licha ya kuwa ndicho Chama kikubwa kuliko chote chote. Hongereni sana viongozi na wanachama wa CWT.
Risala ya Chama cha Waalimu
Ndugu Rais
Ndugu Waalimu;
Nimeisikia na kuipokea risala yenu nzuri mliyoiwasilisha kwangu muda mfupi uliopita. Nawashukuru kwa risala yenu imeainisha mafanikio, mliyopata, changamoto zinazowakabili na muhimu zaidi mmetoa ushauri muafaka kuhusu namna bora ya kuzitatua. Ni risala inayotoa fursa ya kujadiliana na kushirikiana na yenye lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano ya pande zetu mbili. Ni risala inayoonyesha kuwepo kwa kushirikiana, kustahamiliana na kuaminiana kati ya walimu na Serikali yao. Sisi sote inatupa funzo kuwa, pale panapokuwepo na uhusiano mzuri na ushirikiano kati ya walimu na Serikali, haliharibiki jambo. Hata yale mambo ambayo pengine yalionekana magumu, tumeweza kuyatatua kwa pamoja. Hatuna budi kuendeleza hali hii ya mahusiano kati yetu siku zote.
Risala yenu pamoja na mambo mengine imeibua masuala tisa. Masuala hayo ni kuhusu madaraja ya walimu; posho ya kufundishia; madeni ya walimu; uhaba wa nyumba za walimu; utoaji wa elimu bora; mabadiliko ya mafao ya pensheni; ukaguzi wa shule; Sekta ya Elimu katika BRN; na mapungufu ya kiutendaji katika kuhudumia walimu. Mambo yote haya ni ya msingi sana na yanastahili kupatiwa majawabu muafaka. Yapo ya kisheria, ya kisera na ya kimfumo. Napenda kuwahakikishia kuwa nimeyapokea na tutayafanyia kazi mambo yote kama kawaida yetu.   Kama mlivyosema katika risala yenu, baadhi ya mambo yanahitaji kukaa mezani kujadiliana na kushauriana zaidi. Tutafanya hivyo. Nitajitahidi kwa yale yanayowezekana niwe  nimeyatatua kabla ya kumaliza muda wangu wa uongozi. Kwa yale ambayo yanahitaji muda mrefu, nitahakikisha kuwa kabla ya kukabidhi ofisi niwe nimeyawekea msingi mzuri ili iwe rahisi kwa Rais ajaye baada yangu kuyakamilisha.
Hatua za Serikali Kushughulikia Madai ya Waalimu
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
Kwa uchache, nitapenda kuzungumzia hatua ambazo Serikali imechukua na inazoendelea kuchukua kushughulikia madai ya waalimu.  Kama mlivyoainisha katika risala yenu, Serikali ninayoingoza  imefanya jitihada kubwa sana kupanua fursa za watoto wetu kupata elimu na sasa tumeelekeza nguvu zetu katika kuboresha elimu inayotolewa. Kwa ajili hiyo, tumeongeza shule za msingi kutoka 14, 257 mwaka 2005 hadi 16, 343 mwaka 2014, na kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka milioni 7.54 hadi milioni 8.23. Shule za Sekondari, zimeongezeka kutoka 1,745mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014  na kuongeza wanafunzi kutoka 524, 325 hadi milioni 1.8 kati ya mwaka 2005 na 2015. Hali kadhalika, idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka 2015, na kufanya idadi ya wanafunzi kuongezeka kutoka 40, 719 hadi200, 986 katika kipindi hiko.
Sote tunafahamu kuwa shule na elimu haikamiliki pasipo na waalimu na pasipokuwa vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Upanuzi huo mkubwa ulilazimu kupanua vyuo vya ualimu. Idadi ya vyuo vya ualimu vya cheti na stashahada vimeongezeka kutoka 52 mwaka 2005 hadi 126mwaka 2015. Upanuzi huu ukiongeza na ule wa vyuo vikuu umewezesha kuongeza idadi ya waalimu wa msingi na sekondari kutoka 153, 767mwaka 2005 hadi 301,960 mwaka 2015. Hii imewezekana kutokana pia na uamuzi wetu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi waliochagua kusomea ualimu, na kuwahakikishia ajira pale wanapomaliza masomo yao.
Serikali imefanya jitihada pia za kuboresha maslahi ya waalimu kadri uwezo uliporuhusu. Hatukuweza kutoa nyongeza kubwa kwa wakati mmoja lakini tumeongeza mara kwa mara.  Kati ya 2005 – 2015 kumekuwepo na ongezeko la kianzio cha mshahara cha Mwalimu mwenye cheti, Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu na wale wenye elimu ya shahada.  Watumishi wa kada nyingine za Serikali wenye elimu ya viwango hivyo, huanza na mshahara wa chini ya ule wa waalimu. Nafahamu kuwa kiwango hiki bado hakitoshi, lakini ukweli ni kuwa hakuna upungufu wa dhamira kwa upande wa serikali, ila kikwazo ni kutokuwepo na uwezo mkubwa kimapato kwa upande wa Serikali. Ukizingatia kuwa walimu ni asilimia 52.7 ya watumishi wa Serikali, hivyo, ongezeko katika mshahara wa waalimu linaleta mabadiliko makubwa sana katika bajeti ya Serikali. Kwa ajili hiyo hatukuweza kutoa nyongeza kubwa kwa wakati mmoja lakini tumeongeza mara kwa mara mpaka tumefikia hapa tulipo leo.  Na katika bajeti hii tutaongeza tena. Hivyo nitawaacha mahali penye unafuu ukilinganisha na tulikotoka.
Tumeendelea pia kushughulikia kero nyingine za waalimu ikiwemo madeni na madai yenu. Deni la waalimu lililopokelewa lilikuwa shilingi bilioni 53, 185,440,406 lililohusu waalimu 70,668. Baada ya uhakiki uliofanyika kwa kuhusisha Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali, jumla ya shilingi bilioni 23, 233, 654, 025 zililipwa kwa waalimu 29,243. Serikali imeshatoa ahadi ya kulipa ifikapo mwezi Agosti mwaka huu madai mengine ya waalimu 7,169 yenye jumla ya shilingi bilioni 9, 285,283,600 ambayo uhakiki wake umekamilika. Aidha, madai ya walimu 30,807yenye jumla ya shilingi bilioni 17,346, 593, 468 hayakuweza kulipwa kutokana na kukutwa na dosari za msingi za kihasibu na kiutaratibu. Wametakiwa kurekebisha kasoro zilizoonekana.
Jambo la kururahisha katika ukaguzi na uhakiki huo wa madeni ni kule kushirikishwa kwa Chama cha Walimu. Kwa pamoja tumethibitisha palipokuwa sahihi na pasipokuwa sahihi. Inasikitisha kupata taarifa za kuwepo vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali na walimu vinavyochangia kuzalisha madeni bandia. Vitendo vyao hivyo ndivyo vinavyofanya madai yachukue muda mrefu kulipwa kwa kulazimika kuweko na uhakiki wa ziada. Naungana nanyi katika pendekezo lenu la kutaka watumishi hawa kuwajibishwa, maana ndio mzizi wa fitna kati ya waalimu na Serikali. Nimekwishaeleza mamlaka husika kufanya hivyo bila ajizi.
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
          Tumeshughulikia lile dai kubwa la waalimu la marekebisho ya muundo wa utumishi wa waalimu (Teacher’s Service Scheme). Tumepitisha Muundo mpya wa Waalimu ambao umeanza kutumika toka Julai 1, 2014. Nimesikia kuwa utekelezaji wake haukuweza kuanza kote nchini mara moja, napenda kuwahakikishia kuwa katika mwaka ujao wa fedha tutahakikisha kuwa Waalimu wote watakuwa wamefikiwa. Sambamba na hili la Muundo, tumekwishapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya kuanzisha Tume ya Utumishi wa Waalimu (Teachers Service Commission) ambao tayari umesomwa kwa mara ya kwanza. Mawasiliano yanaendelea na Ofisi ya Spika ili Muswada huo ujadiliwe katika Bunge hili la Bajeti.  Tunafanya hivyo pia kwa Muswada wa kuanzisha Bodi ya Taifa ya Taaluma ya Waalimu (Teachers Proffessional Board). Nimepokea maoni yenu ya kutaka uangaliwe uwezekano wa Bodi hii kuwa sehemu ya Tume ya Utumishi wa Waalimu badala ya kuwa na vyombo viwili tofauti. Hoja yenu ya kutaka kupunguza utitiri wa vyombo vinavyoshughulikia maslahi ya waalimu ina mashiko. Ushauri wenu umepokelewa, tutautafakari na kuufanyia kazi.
          Napenda kuwahakikishia kuwa madai yenu mengine ikiwemo nyumba za waalimu, motisha kwa waalimu, mazingira ya kufanyia kazi, mafunzo vikokotoo vipya vya pensheni na masuala mengine mliyoibua katika risala yenu tutayashughulikia na tutawapeni taarifa. Pia nitaelekeza mamlaka zinazohusika kukutana na uongozi mpya wa Chama chenu baada ya uchaguzi mkuu wenu kuyajadili masuala hayo na kuyatafutia majawabu.
Napenda kusisitiza kwenu kwamba mimi na wenzangu Serikalini tunawathamini sana na kuwapenda waalimu kwa dhati ya mioyo yetu. Sisi tunatambua nafasi ya Mwalimu katika maendelo ya mtu binafsi na taifa kwa jumla.  Hakuna badala yake. Hivyo basi tunatambua wajibu wetu wa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Tumefanya  jitihada kutimiza wajibu wetu. Pale panapojitokeza matatizo yoyote si makusudio yetu. Kitendo cha makusudi na anapojulikana mtu huyo atawajibishwa ipasavyo. Wakati mwingine matatizo yanayowakuta hutokana na watu wetu kuelemewa na mzigo kutokana na ukubwa wa kada yenu katika utumishi wa umma ambapo  ni  asilimia 52. 7.
Kwa ukubwa huu, mnaweza kuelewa ni changamoto kiasi gani zinazojitokeza katika kushughulikia masuala yenu. Ndio sababu hatuchoki kutafuta muundo bora wa kushughulikia matatizo yenu. Ninachoomba kutoka kwenu ni uvumilivu na uelewa wenu na kuwaomba mtupime kwa dhamira yetu na utayari wetu wa kuyashughulikia madai yenu na si kwa idadi ya changamoto zinazojitokeza.
Uchaguzi Mkuu wa CWT
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
          Moja ya Agenda kubwa ya Mkutano wa leo ni Uchaguzi Mkuu. Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi mliochaguliwa katika ngazi ya Tawi, Wilaya na Mkoa ambao kwa pamoja mmeunda Mkutano Mkuu huu. Nawapongeza kwa kuuendesha uchaguzi wa ngazi za chini vizuri maana natambua kuwa haikuwa kazi ndogo kutokana na ukubwa wa nchi yetu, na hamasa ya waalimu kisiasa.
          Nawapongeza sana viongozi wote waliojitokeza kugombea nafasi za uongozi wa ngazi ya Taifa. Naamini nyote mnatosha kwa nafasi mnazoomba.  Naomba mkumbuke kuwa si kila mtu aliyeomba atashinda.  Nafasi si nyingi kiasi hicho. Hivyo basi, wale ambao kura hazitatosha safari hii, watumie uzoefu walioupata katika uchaguzi huu kujinoa zaidi kwa chaguzi za miaka ijayo. Haitakuwa vizuri iwapo wale ambao hawatafanikiwa kushinda, wataendeleza nongwa na kuwa chanzo cha kuvunja mshikamano mzuri mlionao katika Chama cha Walimu. Kama nilivyosema awali, sisi sote tunawaangalia waalimu kama kioo cha maadili na upevu katika jamii yetu. Naamini hamtatuangusha.
          Nawapongeza na kuwashukuru sana viongozi wanaomaliza muda wao kwa ushirikiano wenu mkubwa mliotupatia sisi   katika Serikali katika kipindi chenu cha uongozi. Kwa pamoja tumeweza kutatua changamoto nyingi za waalimu na kujenga madaraja kati yetu yaliyozaa mahusiano mazuri ambayo ndio msingi wa kutatua madai ya waalimu kila yalipojitokeza. Ni matumaini yetu kuwa viongozi watakaochaguliwa, wataendeleza pale mlipoishia na muhimu zaidi uhusiano mzuri na ushirikiano na Serikali. Sisi tunaahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano unaostahili. Ni jambo lenye maslahi kwetu sote.
Hitimisho
Ndugu Rais na
Ndugu Waalimu;
          Hii ni fursa yangu ya mwisho kukutana na kuzungumza na viongozi wa CWT nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya hapo nitakuja kumsindikiza Mwalimu mwenzenu akija mkutanoni. Hivyo, sina budi kutumia fursa hii pia kuagana nanyi na kupitia kwenu kuagana na Waalimu wote nchini. Nirudie tena kuwashukuru sana kwa mchango wenu mkubwa katika maendeleo ya elimu nchini. Kwa kweli mnajitoa sana na mnafanya kazi kubwa ambayo inaonekana na wote. Napenda kuwatia moyo kuwa msilegeze uzi bali muendelee na moyo na wito wenu huo. Nitawakumbuka sana waalimu katika maisha yangu baada ya kustaafu uongozi, kwa msaada wenu na ushirikiano wenu. Nimewapenda, ninawapenda na nitaendelea kuwapenda ‘Shemeji’ zangu.        
   Nawatakia Uchaguzi Mkuu na Mkutano Mkuu mwema.
Akhsanteni kwa kunisikiliza!

Wanaopaswa kuwa gerezani nao wanatafuta urais?


Ndimara Tegambwage katika blogu yake aliyochapisha habari iliyonukuliwa hapo chini anasema,
Rafiki yangu amenipelekea andishi hili. Nimelisoma. Naona niliweke hapa nawe uweze kulisoma. Haya!

Na Lawrence Kilimwiko*

NANI wanataka kuwa rais nchini Tanzania? Wana nini? Historia yao ikoje? Wanaishi maisha ya kiwango gani? Wana mali kiasi gani au ni masikini kiasi gani? Wanalipa kodi au ni wakwepa kodi?

Nani anafahamu yeyote anayetaka kugombea urais ili atupe taarifa na ikiwezekana atusaidie kujibu maswali yaliyoulizwa hapo juu?

Tanzania inaingia katika uchaguzi mkuu wa 2015 ikiwa katika mazingira yanayohitaji uchunguzi na uchambuzi wa aina ya kipekee.

Kuna watuhumiwa wa makosa makubwa, ukiwemo ukwapuaji Benki Kuu (BoT) wa zaidi ya shilingi bilioni 290. Unaitwa kashfa ya EPA. Kuna uwindaji haramu wa tembo na faru na usafirishaji nje ya nchi wanyama hai kutoka mbugani. Kuna uzawadiaji mikataba kama ule wa Richmond wa kufua umeme wa dharura ambao, hata hivyo, haukupatikana.

Kuna wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya ambao Rais Jakaya Kikwete aliwahi kuliambia taifa kuwa ana orodha yao wote; lakini hajawahi kuiweka wazi hadi leo.

Kuna wezi wa fedha za umma kupitia akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya BoT. Hata watumishi wa ikulu wako kwenye orodha ya waliochotewa mamilioni ya shilingi.

Je, miongoni mwa wote hawa na wengine, hakuna anayetaka kugombea urais? Hakuna ambao wamejichomeka kwenye ulingo wa siasa ili kuepuka kushitakiwa; na sasa wanatafuta urais ili kuficha zaidi sura na ukwasi wao unaotokana na wizi, ukwapuaji na ujambazi kiuchumi?

Tanzania haiwezi kuwa tofauti. Angalia Italia. Silvio Berlusconi, waziri mkuu wa zamani wa Italia, ni mmoja wa mamilionea wa ki-Italia aliyekuwa akimiliki utajiri wa thamani ya dola za Marekani 6.2 bilioni.

Historia yake inaonyesha kuwa alianza maisha akiwa mchezadisko kwenye vilabu vya pombe na vingine. Baadaye alisoma na kuhitimu sheria mwaka 1961.

Biashara zake zimo katika maeneo kadhaa kuanzia kampuni ya ujenzi, televisheni kubwa ya Telemilano na nyingine mbili, kampuni ya uchapaji magazeti ya Giomele, redio, Shirika la habari la Rai pamoja na kumiliki klabu maarufu ya kandanda ya A.C.Milan.

Mwaka 1993 Berlusconi alianzisha chama cha siasa cha Forza Italia na kujitumbukiza kwenye siasa.Alitambua mapema kabisa kuwa ili aweze kufanikisha malengo yake; na hasa kukwepa mkono wa sheria kutokana na kufanya biashara nyingi haramu, ilikuwa muhimu kwake kuingia katika siasa – ili apate mahali pa kujikinga.

Njama hizo zilimsaidia sana Berlusconi kukwepa mkono wa sheria kutokana na makosa ya kukwepa kodi, udanganyifu, rushwa na hata ngono. Kwa ufupi, maisha ya Berlusconi yamejaa mchanganyiko wa sifa na kashfa.

Alikuwa waziri mkuu wa Italia kwa vipindi vitatu, na mtawala aliyekumbwa na kashfa nyingi na hata kuhukumiwa kwenda jela. Lakini hakuwahi kutumikia jela kutokana na kujificha kwenye kichaka cha siasa.

Hata hivyo, baada ya kukwepa kwenda jela kutokana na makosa ya rushwa, ubakaji, kukwepa kodi na udanganyifu; hatimaye alijikuta akining’inizwa baada ya kutiwa hatiani na mahakama kwa kosa la kukwepa kulipa kodi mwaka 2013.


Kama hiyo haitoshi, alihukumiwa pia adhabu ya miaka saba jela kutokana na kufanya ngono na “kahaba” aliye chini ya umri wa mtu mzima. Adhabu hiyo, hata hivyo, ilibadilishwa na kuwa ya kutumikia jamii kwa mwaka moja kutokana na umri wake mkubwa – miaka 77.

Hiki kilikuwa kitu kipya kabisa kwa raia wa Italia ambao walifikia kuamini kwamba Silvio Berlusconi haguswi na mkono wa sheria kutokana na ukubwa kisiasa na utajiri wake.

Nchini Tanzania, wenye utajiri mkubwa walianza kwa kujipenyeza kwenye michezo kupitia vilabu vikubwa. Ukweli ni kwamba kelele za wanachama na mashabiki wa klabu, huweza kumsetiri mwizi na hata kuhakikisha kuwa hakabiliwi na mkono wa sheria.

Baada ya kugundua mbinu hiyo inafanya kazi, inawezekana sasa kuna waliojiingiza katika siasa, tena kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) au vyama vingine.

Siyo siri kwamba wizi na ufisadi wote uliotajwa hapo juu, umo nchini Tanzania. Siyo siri kwamba wizi mkubwa umewahusu viongozi wa serikali ambayo inaongozwa na CCM.

Siyo siri kwamba miongoni mwa wanaotaka kugombea urais, Oktoba mwaka huu, tena kupitia CCM, wamo watuhumiwa wakuu wa ama hujuma, wizi au ukwapuaji mabilioni ya shilingi kupitia wizara ya fedha na BoT.

Ripoti ya hivi karibuni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa fedha za serikali (CAG); inaonyesha kuwa serikali inatumia vibaya fedha inazopewa; inapoteza fedha, na watumishi wake waliokabidhiwa dhamana kuu, wanatafuna fedha kama njugu kutoka shamba la bibi!

Ni kula! Kula! Kula! Ni kula faida na ziada; na hatimaye kula mbegu; kana kwamba mwakani hakuna kupanda!

Kinachostua wananchi wengi wapenda nchi yao, ni kuona waliotajwa na CAG – na huwataja mwaka hadi mwaka – kuwa watuhumiwa ubadhilifu, wezi moja kwa moja, wakwapuaji na, au waandaa mipango ya uhujumu uchumi; ni miongoni mwa wanaotangulia kutangaza kugombea urais na ubunge.

Yuko wapi mwandishi wa kuwaanika hao? Yuko wapi mwandishi wa kuwahoji?

Kwa wizi wa waziwazi alioanika CAG, kuna wanaopaswa kuwa jela wakati huu au wakati wa uchaguzi, Oktoba. Serikali inayowaajiri, inayowakinga, inayostahili kuwafukuza au kuwakamata na kuwashitaki, iko kimya.

Ni serikali hiyohiyo ya chama hichohicho, inayotuhumiwa na kushutumiwa na CAG ambayo inasimamia upatikanaji rais kutoka miongoni mwa watuhumiwa - Chama Cha Mapinduzi.

Katika mazingira haya, hakika hakuna kulala – kwa upande wa CCM na serikali yake. Wanataka kuhakikisha kuwa anapatikana mgombea na labda baadaye, rais atakayefunika kombe ili mwanaharamu apite.

Wanataka rais aendelee kutoka katika chama chao – CCM – kilichojaa viongozi wa serikali wanaotuhumiwa na kushutumiwa kwa wizi na ufisadi wa viwango mbalimbali; kuanzia kijijini hadi ikulu.

Wanataka kuendelea kujenga kinga kwa wahalifu wanaowafahamu, waliowaweka madarakani, waliowalea na watakaoendelea kulinda, kuhifadhi na hata kuenzi genge la wezi wa tunda la jasho na damu ya Watanzania.

Chama Cha Mapinduzi kinaweza kufananishwa na mtu mmoja aitwaye Robert Mugabe, rais wa Zimbabwe, ambaye aliapa kufia ofisini kwa hofu ya kukamatwa na kushitakiwa, pale tu atakapotoka ikulu.

Kuiba fedha za umma, kushiriki kuiba, kuruhusu kuiba na, au kunyamazia kuiba, ni kosa kubwa kimaandili, kisiasa na kisheria.

Wizi usioadhibiwa, au usiokemewa; na badala yake ukawa wizi wa kuendeleza kwa “gharama yoyote ile,” alimradi mtu amebaki madarakani; ndio unafanya vyama na watawala watake kufia madarakani; kama inzi anavyofia kwenye kidonda. Hawaoni usalama wao nje ya madaraka ya dola.

Watajipitisha makanisani, misikitini, misibani, kwenye harusi na matanga; wakijifanya wacha-Mungu na wenye kuwahurumia wasumbukao kwa njaa, maradhi na kiu; wakiwalaghai watu kwa vitenge, kanga, pilau au kofia za chama au ahadi za ajira, ili wapate kubaki madarakani.

Hakika, Watanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuacha ngonjera za kuthamini “uasisi” na “kuleta uhuru.” Siyo siri kwamba vyama vilivyopigania uhuru Afrika na kwingineko, vingi viliingiliwa na kirusi cha wizi na ufisadi na hatimaye kuangushwa na umma.

Tanzania siyo kisiwa! Watanzania wanaona, kusikia na kunusa. Kama mwizi wa mali yao hakamatwi, basi wasiomkamata wasiwaombe kura ya kuendelea kutawala. Au wakiwaomba kura, basi wawakatalie.

CCM haikuundwa ili ilee wezi, iwatukuzwe na iwaweke madarakani. Hapana! Kwa kauli za Mwalimu Nyerere, iliundwa kulinda na kudumisha uhuru wa nchi na raia wake; kusimamia haki na maendeleo ya wakulima na wafanyakazi, kuhakikisha kuwa matumizi ya utajiri wa taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi, na hasa jitihada za kuondosha ujinga, maradhi na umaskini.

Kama walioahidi na wanaopaswa kuamini hayo ndio wenye serikali inayoanikwa na CAG kuwa ni badhilifu kupindukia; basi wameandika barua ya maombi kwa umma wakitaka kufukuzwa kazi. Watafukuzwa!

Kuwafukuza kazi ni kutowachagua; lakini kwanza ni kuwataka wagombea wao, hasa wanaotaka urais, kutaja walikopata fedha wanazomwaga misibani, michezoni, misikitini na makanisani; na jinsi watakavyozirejesha.

Isemwe tu basi, kwamba CCM bado ina nafasi ya kujisahihisha kwa kuwaengua wagombea urais, ubunge na udiwani – wote wasio waadilifu – wahujumu, wezi, matapeli, walafi, wababaishaji na mafisadi.

Kama hilo litaigharimu kushindwa katika uchaguzi mkuu huu, isiwe hoja. Wakae pembeni. Wajipange upya na kurudi kwenye misingi walioyiacha, ndipo warejee kwenye kinyang’anyiro wakiwa wasafi na wenye sifa ya kushindana na hata kushinda.

*Lawrence Kilimwiko ni mshauri wa habari na mwandishi wa vitabu kutoka asasi ya Interlstar Consults, Dar es Salaam: [email protected], Mob. 0754 321308.

Fikra Pevu: Lowassa kawaleta pamoja ‘Fisadi Papa’ na ‘Fisadi Nyangumi’?

Menyekiti wa chamacha wamiliki wa vyombo vya habari nchini, MOAT, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, (kushoto), akijadili jambo na Mkurugenzi wa New Habari 2006 Limited, Rostam Aziz, walipokutana kwenye kikao cha MOAT kujipanga na kujadili namna ya kukabiliana na mpango wa serikali wa kuwasilisha muswada wa habari kwa mara ya pili. (wavuti.com imechukua picha hii kutoka kwa: Khalfan Said / K-VIS blog)

Ama kweli wahenga walisema, “Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime, siku wakipatana chukua kapu ukavune mazao yako shambani.”

Hivyo ndivyo ninavyoweza kusema kila ninapolifikiria tukio la Mei 26, 2015, siku ambayo wafanyabiashara wawili maarufu hapa nchini, Dk Reginald Mengi na Rostam Aziz walikutana, wakakumbatiana, wakaa meza kuu moja na kunywa kahawa na kula vitafunwa pamoja.

Ulikuwa ni mkutano baina ya wamiliki wa vyombo binafsi vya habari nchini, kupitia umoja wao, MOAT na waandishi wa vyombo vya habari vya ndani na nje, ndio uliowakutanisha pamoja wafanyabiashara wawili hawa.

Pamoja na mambo mengine, walizungumzia hisia zao kuhusiana na miswada miwili inayotazamiwa kuwasilishwa na Serikali bungeni ili kuwa sheria kamili, miswada hiyo ni ule wa Huduma za Vyombo vya Habari na wa Haki ya Kupata Habari.

Inajulikana kwamba wafanyabiashara hawa wawili, mbali na kuwa na biashara zao nyingine, wote wanamiliki vyombo vya habari vikubwa katika nchi hii, hivyo kuwafanya wawe wadau wakuu wa tasnia ya habari. Hivyo linapoibuka suala lolote linagusa maslahi mapana ya vyombo vya habari, kama ilivyo kwa miswada hiyo miwili, lazima jambo hilo liwaguse.

Mojawapo ya maswali yanayosumbua vichwa vya baadhi ya wadadisi wa mambo walioshuhudia tukio hilo la Mei 26, 2015, ni endapo miswada hiyo miwili ya Serikali ndiyo iliyowaleta pamoja wafanyabiashara hao au ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu?
Itakumbukwa kwamba Aprili 23, 2009, Dk Mengi, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, alitaja kwa majina orodha ya wafanyabiashara watano wa hapa nchini na kuwatuhumu vikali, akidai kwamba hao ni ndio Mafisadi papa, miongoni mwa mafisadi wasiozidi wala kupungua 10 wanaoshiriki kuyumbisha utawala wa Rais Jakaya Kikwete kutokana na vitendo vyao vya kifisadi.

Katika madai yake hayo, Dk Mengi alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema: “Nchi hii ina mafisadi ambao kila kukicha wanaiyumbisha nchi…hawazidi hata kumi. Lakini kuna watano ambao ni mafisadi papa. Ukitokea kupingana nao kutokana na ufisadi wao, wanakuona wewe ni adui.”

Baada ya hapo, Dk Mengi alitaja majina ya ma mafisadi papa hao, wakiongozwa na Rostam Aziz, akidai ni pamoja na wafanyabiashara wengine wakubwa na maarufu hapa nchini ambao ni Tanil Somaiya, Yussuf Manji, Jeetu Patel na Subhash Patel.

Mei 2, 2009, siku 10 tu baada ya Dk Mengi kutaja majina ya wafanyabiashara hao, Rostam aliitisha mkutano na waandishi vyombo vya habari vya ndani na nje na kuvunja ukimya wa muda mrefu, kwa kumtuhumu Mwenyekiti Mtendaji huyo wa IPP kwa kumwita kwamba ni fisadi nyangumi, huku akidai kuwa na vielelezo kibao alivyodai kuwa angeviwakilisha kwa Jeshi la Polisi ili waanze kumchunguza dhidi ya vitendo vyake vya kifisadi.

Katika kipindi hicho cha misuguano baina ya wafanyabiashara hao wawili, kiasi cha kupachikana majina ya mafisadi papa na mafisadi nyangumi, Rostam alikuwa bado ni Mbunge wa Igunga na pia Mjumbe wa Kamati Kuu pamoja na Halmashauri Kuu ya CCM.

Takriban miaka mitatu baadaye, baada ya Rostam Aziz kudaiwa na Dk Mengi kwamba amekuwa akishiriki katika vitendo vinavyoiyumbisha nchi hii, kwa maana ya Julai 13, 2011, mwanasiasa huyo aliamua kujiuzulu ubunge huo wa Igunga pamoja na nyadhifa nyingine zote hizo alizokuwa nazo ndani ya CCM, akisema dhamira yake ya dhati ya kuachana na siasa uchwara (gutter politics) za ndani ya chama chake hicho na kutumia muda wake kushughulika na biashara zake.

Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, na tayari michakato mbalimbali, ikiwemo ya baadhi ya makada wa CCM na vyama vingine vya upinzani kuonyesha nia zao za ama kuutaka urais, ubunge au udiwani.

Rostam Aziz ambaye Julai 13, 2011 alidai kwamba anaachana na siasa uchwara za ndani ya CCM, ameibuka tena akidaiwa kuratibu mikakati ya mmoja wa wenye mitandao yao ya urais ndani ya chama hicho hicho alichokituhumu kwa kuendekeza siasa uchwara.

Kwa kuwakumbusha tu wana-CCM na Watanzania kwa ujumla wao, Rostam ndiye aliyeratibu na kuongoza ‘mapinduzi’ ya kimfumo ndani ya CCM mwaka 2005/2006, kwa kukiondoa chama hicho mikononi mwa wananchi wanyonge, kwa maana ya Wakulima na Wafanyakazi kama msingi mkuu wa Chama na kukiweka mikononi mwa matajiri.

Kila mwana-CCM na kila Mtanzania, akiwemo Mwenyekiti wa CCM mwenyewe, Rais Kikwete, anatambua ni kwa kiasi gani ‘mapinduzi’ hayo yaliyoratibiwa na kuongozwa na Rostam Aziz yalivyokiathiri chama hicho kiasi cha kuponea chupuchupu mwaka 2010.

Ni baada ya fedheha hiyo Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete, aliwataka wote waliochangia chama chake kikose haiba mbele ya umma wa Watanzania wachukue uamuzi mgumu wa kujivua gamba, na kwa shinikizo kubwa Rostam Aziz akatangaza kujivua gamba na hadi sasa ndani ya CCM kumetulia.

Sisi wengine tunapoona Rostam huyo huyo akipitia mlango wa nyuma wa CCM, akiwa na mgombea wake wa urais mgongoni, hatuwezi kuwa na tafsiri nyingine zaidi ya kwamba hili ni jaribio lake jingine la pili la kutaka kufanikisha ‘mapinduzi’ yaliyoshindwa mwanzo kutokana na wana-CCM Itikadi kusimama kidete dhidi ya wana-CCM Maslahi ambao sasa wamejipanga kwa nguvu zote kurejea tena ulingoni.

Rostam Aziz anafahamika kwa wengi wanaofuatilia siasa za nchi hii kama ‘kingmaker.’ Kwa hali hiyo, wanaomfahamu hawawezi kushangazwa na matukio ya sasa ya kumuona akihangaika huku na kule katika kuhakikisha kwamba yule atakayepitishwa na CCM kuwa mgombea urais au yeyote nje ya chama hicho, anakuwa ni yule atakayemrahisishia kufanya biashara zake, ziwe halali au haramu.

Bali watashangazwa na matukio ya kumuona Dk Mengi akijiweka karibu na mwanasiasa-mfanyabiashara huyo katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Tunajua, wote waliomo ndani ya Team Lowassa inayoongozwa na Rostam Aziz, wameshaahidiwa uwaziri, ukuu wa mikoa, ukuu wa wilaya, ukuu wa taasisi mbalimbali za umma na mashirika ya umma kama vile PPF, NSSF na kadhalika.

Je, Dk Mengi, kwa uamuzi wake huu wa sasa, kukumbatiana, kukaa meza kuu moja na kunywa kahawa na kula vitafunwa pamoja na Rostam Aziz, ambaye takriban miaka sita tu iliyopita walikuwa ni mahasimu wakubwa kiasi cha kupachikana majina ya fisadi papa na fisadi nyangumi, naye ameahidiwa nini na Serikali hiyo ijayo ya akina Rostam Aziz?

Je, Dk Mengi ameahidiwa kupewa upendeleo wa kipekee wa kupatiwa vitalu vya gesi na mafuta? Sisi wengine tunalazimika kuhoji hivyo kwa sababu Dk Mengi anatambulika ndani ya jamii ya wanyonge wa nchi hii kama mtu wao wa karibu wa kuwafariji katika madhila yao ya umasikini.

Kila mwaka Dk Mengi amekuwa akiandaa chakula cha pamoja na kula nao wanyonge wa nchi hii, wengi wao wakiwa walemavu. Ofisi zinazomilikiwa na Rostam Aziz katika jiji la Dar es Salaam, baadhi yake zinajulikana. Hakuna hata ombaomba wa mjini anayekanyaga kwenye ofisi zake kwa sababu anajua hata akienda kuomba hatapewa hata senti tano.

Je, uhusiano huu mpya wa Dk Mengi na Rostam Aziz, uliowafanya wazike tofauti zao na uhasama wao, umebeba siri gani? Kama nguvu ya kisiasa ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, katika mbio zake za kuusaka urais zinaweza kumfanya Dk Mengi awe swahiba mkuu wa Rostam Aziz, basi siasa za nchi hii zimefika mahali patamu! Yetu ni macho na masikio, tusubiri.


Maadhimisho ya "Siku ya Afrika", Washington DCBalozi wa Misri nchini Marekani Mhe. Mohamed Tawfik akiongea kufungua sherehe ya African Union iliyofanyika siku ya Alhamisi May 28, 2015 katika hotel ya JW Marriott, Washington DCBalozi wa Morocco nchini Marekani Mhe. Rashad Bouhlal akiongea machahce.Msemaji mkuu wa sherehe ya siku ya Afrika Mhe. Donald Tetelbaum.Mchungaji Jesse Jackson akiongea kwenye sherehe ya siku ya Afrika.Maureen Umeh mfanyakazi wa kituo cha luninga cha Fox News DC akisherehesha sherehe ya siku ya Afrika.Mambalozi wa Afrika nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamojaWageni waalikwa wakifuatilia hotuba.Mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Githae.

 • Tumeshirikishwa na Kwanza Production

In summary: Things to know about student loans in the USA


I thought it's worth sharing Ben Allred (Sr. Loan Officer at Waterstone Mortgage Corp.,) tips about students loans. The message reads as follows:

Not sure how you (or your kids) will pay for college? You might be planning on a combination of savings, scholarships and grants, but it doesn't hurt to understand your options for student loans too.

Where can students get a loan?

There are two main categories of student loans:
 • Federal loans -- Federal government loans with fixed interest rates. Repayment isn't required until after graduation.
 • Private loans -- From a bank or other entity, these loans often have variable rates. Repayment may begin while the student is still in school.

Federal or private -- which is best?

Experts generally recommend applying for federal loans first because they typically come with lower interest rates and more flexible repayment options. The first step is to complete the Free Application for Federal Student Aid (FAFSA), and then to consider three types of federal loans:
 • Federal Direct Loans -- Unsubsidized loans are available to all students, regardless of financial need. These loans start accumulating interest as soon as they are received. Some students may qualify for subsidized loans, which cover the interest while the recipient is in school.
 • Federal PLUS Loans -- Geared to graduate and professional degree students, or parents of students pursuing undergraduate degrees, a PLUS loan requires a credit check.
 • Federal Perkins Loans -- These are need-based, government-funded loans administered by the college or university. The amount available to an individual student depends on how much is still available at the school, so apply early.

How to "fill in the gaps." 

Federal loans may not be enough to cover all education costs. In that case, a private loan may help. The school's financial aid office can help identify the available options, but they generally fall into three categories:
 • State agency loans (for residents or students enrolled at a school in the state)
 • Traditional bank loans (credit check and co-signer are typically required)
 • School loans (administered by the school, often with fixed rates)

With all of these alternatives, it may be tempting to borrow too much. Students should consider the earning potential of their major before borrowing, and take only what can be repaid within a reasonable timeframe (usually about 10 years).

That way, student loans won't end up as a burden; instead, they'll be a smart investment in the future.

Picha: Faraja Nyalandu akijiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura

Faraja Nyalandu akijiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura kijijini Pohama Singida. Pembeni ni mmoja ya wasimamizi wa kituo akimpa maelekezo

Alama za vidole zikichukuliwa ikiwa ni mojawapo ya taratibu katika kujiandikisha kama mpiga kura

Faraja akikabidhiwa kitambulisho cha mpiga kura mara baada ya kukamilisha taratibu za kujiandikisha