Ujumbe wa Prof. Mwandosya kuhusu mbio za Urais 2015

Baba wa Tgaifa, Hayati Julius Nyerere (katikati) akizungumza na Profesa Mark Mwandosya walipokutana enzi hizo.

Marafiki zangu, ndugu zangu, watanzania wenzangu, salaam!

Kwa muda mrefu, na kwa njia mbalimbali za mawasiliano, mmekuwa mkinidadisi mbona kimya kuhusu mwaka 2015? Pamoja na kwamba mara nyingi mlitaja mwaka tu, lakini niliwaelewa. Wengi mliushangaa ukimya wangu.

Pamoja kwamba ukimya ni haiba yangu na ni karama aliyonitunuku Mwenyezi Mungu, Muweza wa yote, baadhi yenu niliwajibu 'Ukimya Una Kishindo'! Sina uhakika kama yafuatayo ni kishindo, lakini ni taarifa rasmi kutoka kwangu.

Kwa staili ya siku hizi tunajitokeza na kutamka: tutatangaza nia siku hii au ile. Kwa kusema hivyo tayari tumetangaza nia! Basi nami kwa staili hiyo hiyo nawataarifu kwamba, majaaliwa, natarajia kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya wanaCCM wenzangu wanichague ili niwe mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natarajia kutangaza nia hiyo Jijini Mbeya, jumatatu, tarehe 1, saa 4 asubuhi, katika ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.

Wale mtakaoweza kufika karibuni, na ninyi ambao hamtaweza kufika basi tutakiane heri.

Kubwa zaidi Mwenyezi Mungu atujalie kwa yote na rehema zake nyingi ziwe juu ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.

CCM yashinda Uenyekiti Himo, KilimanjaroMsimamizi wa Uchaguzi na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza wakati wa kutangaza matokeo katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika uchaguzi huo kutoka vyama mbalimbali vya siasa.Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo Hussein Jamal akizungumzamara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi huo uliofanyika katika shule ya walemavu wa usikivu eneo la njia Panda.

Baadhi ya viongozi waliofika kushuhudia Uchaguzi huo.Mkurugenzi wa wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akitoa ufafanuzi katika uchaguzi huo.Baadhi ya madiwani walioshiriki uchaguzi huo.Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Morris Makoi akisalimia mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo.Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza wakati wa kufunga kikao cha uchaguzi huo.Dc Makunga akipeana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Moris Makoi mara baada ya kuzungumza katika uchaguzi huo.

  • Taarifa ya Dixon Busagaga Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Mei 30, 2015


Taarifa ya habari Channel TEN, Mei 29, 2015