MMjengwa: Watangaza nia na sanaa ya kuhutubia... (II)

Ndugu zangu,

Naomba nianze na tungo hii fupi...

"SINA sauti nzuri ya kuimba, siwezi kucheza muziki watu wakanistaajabia.
Najua siwezi kuchora. Najua siwezi kuandika kitabu kikapata tuzo.
Maneno yangu si ya kurembesha sana, yanatoka moyoni.
Kipaji nilichojaaliwa si kikubwa na wala si cha upekee duniani.
Lakini, wote waliojaaliwa vipaji si sharti wang'ae wakaonekana."

Basi, ukiachilia mbali itikadi, siasa inahusu pia sanaa ya mawasiliano. Kwa mwanasiasa, kama huiwezi sanaa ya kuwasiliana na wananchi, basi, ni sawa na mtu anayejiita fundi mekanika , lakini hawezi kushika spana.

Watanzania tunashuhudia sasa wagombea watarajiwa wa nafasi mbali mbali za uongozi wa kisiasa wakitangaza nia zao. Wanafanya hivyo hadharani, ama kwenye viwanja vya michezo, kumbi za mikutano au sebule za nyumba zao. Kubwa, hawafanyi kwa siri.

Na huu ndio msimu wake haswa. Lakini, kwa baadhi yetu tuliopata bahati ya kusoma vitabuni na hata kuishi na kushuhudia kampeni za chaguzi mbali mbali za ndani na nje ya mipaka yetu, kuna mapungufu tunayoyaona. Mapungufu ambayo, yumkini wengine walio ndani ya vuguvugu la kisiasa kwa sasa hawayaoni. Ni hao wagombea watarajiwa wenyewe.

Hapa nitajikita kwenye eneo la mawasiliano ya mwanasiasa kwa wapiga kura. Kuna watakaokubaliana nami, kwamba kuwa mwanasiasa ni jambo moja, na kuwa na uwezo wa kuwasiliana na wapiga kura ni jambo jingine kabisa.

Hadi ninapoandika makala haya, na kwa uzoefu wangu mdogo kwenye sanaa ya mawasiliano na hususan sanaa ya kuongea mbele ya hadhara, naliona tatizo kubwa kwa baadhi ya watangaza nia kwenye eneo hili.

Kwamba, bila wao wenyewe kujua, ukweli kuna wanaotumia fedha nyingi na kupata mavuno haba kwa makosa ya kiufundi kwenye kujipanga kwenye eneo hili la sanaa ya mawasiliano kwa umma. Nimesema jana, kuwa ningeweza kabisa kutoa ushauri wa bure, kwa ninayoyafahamu, ili kuwasaidia wanasiasa hawa, iwe wa kutoka chama tawala au upinzani, ili, kama Watanzania wenzangu, waweze kufanya vema zaidi kwenye kufikisha ujumbe wao kwa Watanzania, jambo ambalo, kwa masikitiko makubwa, nimeshuhudia watangaza nia wenye ' kupotea' jukwaani bila kujua kuwa wameshapotea. Nafurahi, kuwa tayari jana ile ile, kuna walionitafuta niwasaidie.

Na anayepotea jukwaani yawezekana akawa amenunua hata muda wa televisheni wa saa zaidi ya mbili na kwa gharama kubwa. Alichoshindwa ni kupata wa kumshauri vema namna ambavyo, angeweza kutumia dakika 45 tu za kuwa ' Live' kwenye runinga na kutoa hotuba ya kutangaza nia ambayo ingewaacha watu wengine wakipiga kuta kwa ngumi wakitamani uchaguzi uwe juma lijalo ili wamalize kazi.

Hiyo ndio sanaa ya mawasiliano. Imekuwepo tangu enzi za Wayunani, wakiita ' Retorik'. Na hakika, ni ushauri wa bure kutoka kwangu, kuwa kwa mtangaza nia yeyote, atenge bajeti ya kununua muda wa kuwa ' live' kwenye runinga na redio japo kwa saa moja. Na kwamba asilifanye tukio la yeye kuongea likazidi saa nzima. Hapo kutakuwa na dalili zote za mtangaza nia ' kupotea' na pengine ' kujizamisha' mwenyewe kwenye bahari ya taarifa nyingi na zenye kumchanganya msikilizaji. Msikilizaji hapaswi kumsikiliza mtangaza nia na akafikia kufikiria mambo mengine nje ya yale anayozungumza mtangaza nia. Hivyo, kuna haja ya mzungumzaji mkuu kuwa na mbinu za kumbakisha msikilizaji wake kutoka sekunde ya kwanza mpaka anapomaliza kuzungumza.

Ni kwa namna gani?

Mzungumzaji mkuu anapaswa kujua mbinu za kuingia ' uwanjani' na kuwafanya mashabiki washangilie. Kujua anawezaje kubaki mchezoni huku akihakikisha mara kwa mara anajua wapi atazipiga ' kanzu' na kutuliza mpira huku akiwaacha washabiki wakilipuka kwa furaha. Hii ina maana ya uwezo wa mzungumzaji kujua namna ya kuingia kwenye mazungumzo yake na wanaomsikiliza. Ajue, kuwa maneno yanapashwa moto pia, tena taratibu. Hupaswi kuanza na moto mkali. Mzungumaji hapaswi kuanza na kulalamika! Ajue pia namna ya kupangilia hoja zake na wapi pa kuweka kituo kupisha wasikilizaji wake washangilie. Na ukiona pale ambapo walipaswa kushangilia hawakushangilia, basi, mzungumzaji ujue kuwa kuna hesabu kwenye mtiririko wako wa hoja haziko sawa, au , umeshindwa kujua uongee nini kwenye hadhira gani.

Na kuzungumza ni kama kupiga muziki. Kuna midundo ndani ya hotuba. Ndio maana, unaweza kuona mzungumzaji anaongea na watu wakitingisha vichwa. Ni kama wanacheza ndani ya hotuba.

Mzungumzaji anapaswa kuzitambua rasilimali zinazomzunguka wakati akitoa hotuba yake. Unapopewa jukwaa uongee ni fursa kubwa. Na unapokuwa na fursa ya kuwafikia Watanzania kwa mamilioni ni jambo adimu sana. Bahati mbaya, wengi hushindwa kuzitumia fursa hizo na huku wakiwa wamezigharamia kwa mamilioni ya shilingi. Ni mahali hapa, wenye kuzipata fursa hizo walipaswa kuomba hata ushauri. Mathalan, mzungumzaji anashindwa hata kutambua kuwa viungo vya mwili wake ni moja ya rasilimali hizo. Kujua namna nzuri ya kutumia lugha ya mwili. Unamwona mzungumzaji akiwa amesimama jukwaani mahali pamoja wakati hajawa hata Rais au Mbunge, hilo ni tatizo. Huo ndio wakati wa kushika kipaza sauti na kutembea jukwaani ukiongea na hata kushuka chini kwa wanaokusikiliza kutengeneza ukaribu nao.

Mzungumzaji, kama ni mtangaza nia na unataka kuomba kura kwa Watanzania wanachama wa chama chako na wasio wanachama wa chama chako. Basi, ukweli hapo ni kuwa, unaotaka kuwafikia walio wengi si wanachama wa chama chako. Hivyo, kosa kubwa la kwanza utakalolifanya ni kutanguliza maslahi ya chama chako badala ya nchi yako. Hapo chama chako ni tiketi tu, na kwamba sera zake ama ilani yake ya uchaguzi ndio unayoamini kuwa itawasaidia walio wengi wasio wanachama wa chama chako. Hivyo, kwenye shughuli ya kutangaza nia kumruhusu DJ kucheza nyimbo za chama chako ni sawa na kuamua kwa makusudi kupunguza idadi ya wasio na vyama ambao wangeweza kukuunga mkono katika harakati zako. Lengo la kwanza la mtangaza nia liwe ni kuwafikia wasio wanachama wa chama chake, na mara nyingi, wasio wanachama wa vyama vya siasa.

Hakika, ili eneo la sanaa ya mawasiliano ni pana mno. Nitaendelea na chambuzi hizi. Na anayetaka ushauri wa bure awasiliane nami;

0754 678 252, [email protected]
NB: Hii ni sehemu pia ya makala yangu Raia Mwema.

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 3, 2015
Kamani atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania 2015

Titus Kamani
Dk Titus Kamani -Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, ametangaza nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuomba uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili agombee urais Oktoba mwaka huu, huku akiahidi kusimamia vyema rasilimali na kukuza uwekezaji.

Dk. Kamani ambaye pia ni Mbunge wa Busega mkoani Simiyu, ametangaza nia hiyo leo katika mkutano wa ndani uliofanyika kwenye ukumbi wa grand hall jijini Mwanza na kuhusisha makada mbalimbali wa CCM kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini.

Amesema kuwa ataendeleza kazi za viongozi waliotangulia, hivyo kipaumbele chake ni kuhakisha kusimamia uchumi wa taifa.

Dk. Kamani ameahidi kuwa endapo akipata ridhaa ya kuwa Rais, atahakikisha anaweka mazingira rafiki ya wawekezaji kutoka nje, kuimarisha huduma ya maji vijijini na miundombinu ya barabara.

Ametaja vipaumbele vingine kuwa ni kuimarisha mshikamano wa uongozi unaowashirikisha wananchi katika matumizi ya rasilimali za nchi, kujenga huduma ya maji vijijini na kuimalisha umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kuimalisha mawasiliano ya kisiasa, jamii na kiuchumi.

Kwa mujibu wa mtangaza nia huyo, endapo vitu hivyo vitasimamiwa na kulindwa, vitawezesha taifa kupiga hatua kimaendeleo na kukuza uchumi wa taifa ambao unaonekana kuyumba hivi sasa.

Kilimo na Mifugo

Dk. Kamani amesema asilimia 80 ya Watanzania walio wengi wanategemea kilimo na kwamba hiyo ni moja ya mipango yake mikubwa ambayo ataingia nayo Ikulu kuhakikisha inawekwa mipango mizuri kwa wakulima.

“Kama tutashindwa kuwekeza katika kilimo hatutafanikiwa na hata kama tutakuwa na gesi, hivyo ni lazima tukawawezesha wakulima kwa kuwatafutia njia nzuri ya kufanya shughuli zao.

“Nikipata nafasi hiyo, ni dhumuni langu kuona hata Mkuu wa Wilaya anasimamia, hiyo ni pamoja na kwenda shambani kukagua mazao ya wakulima na kiasi wanachovuna,” amesema Kamani.

Katika Mifugo, amesema Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na mifugo wengi, lakini imekuwa na tatizo kubwa la malisho na kwamba ni wajibu wake akiingia Ikulu atahakikisha malisho yanaboreshwa.

Pia, kuhakikisha idadi ya viwanda vya kusindika ngozi na nyama vinaongezeka ili kuongeza ajira kwa vijana ambao hawana kazi, pamoja na kutafuta maeneo yamayofaa katika kufanyia kazi hiyo.

Usimamizi mbovu wa rasilimali

Kwa mujibu wa Dk. Kamani, usimamizi mbovu uliopo serikalini, umekuwa ukichangia kushuka kwa uchumi hivyo, akiwa Rais atahakikisha anaisimamia kikamilifu kwa manufaa ya taifa.

Amesema mara nyingi Watanzania wamekuwa wakilalama juu ya viongozi wa ngazi ya juu kushindwa kuchukua maamuzi magumu katika mambo ya rushwa, kitendo ambacho kinatakiwa kuimarishwa.

Hata hivyo, amesema endapo akiwa Rais, atahakikisha anajenga uwezo kwa watumishi na viongozi kuchukua maamuzi magumu pindi kunapogundulika kumefanyika ubadhilifu.

Pia amesema atahakikisha anasimamia urasmu uliopo serikalini unazibitiwa kwa nguvu zote jambo ambalo litaweza kuliletea taifa maendeleo na kukuza uchumi kwa kila mtanzania.

Rushwa na kodi

Dk. Kamani amesema, akiwa rais, tatizo la rushwa linakomeshwa pamoja na kusimamia ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo.

Amesema atasimamia watu wanaoshindwa kulipa kodi, kudhibiti kodi sumbufu kwa wafanyabiashara na kutilia mkazo vita vya rushwa kwa watumishi wa umma na viongozi serikalini.

“Endapo utashindwa kudhibiti vitu hivyo, utasababisha nchi kuyumba kimaendeleo, hivyo basi kila mamlaka inapaswa kushiriki katika kupambana na vitendo vya rushwa.

“Kama kiongozi ni lazima nisimamie udokozi wa nguvu za wananchi unaofanywa na watumishi wasiokuwa waaminifu kwa watanzania wenzao, pamoja na kuboresha mazingira kwa wafanyakazi,”amesema.

Wasifu

Dk. Titus Kamani alizaliwa mwaka 1955 katika kijiji cha Mkula Wilaya ya Busega mkoani Simiyu (zamani Wilaya ya Magu- Mwanza), akiwa mtoto wa tano kuzaliwa katika familia ya watoto 10.

Alianza safari ya elimu ya msingi mwaka 1965 hadi 1968 na kuendelea na katika shule ya msingi Bwiru na kuhitimu mwaka 1971.

Alihitimu elimu ya sekondari mwaka 1979 na kupata alama za kumwezesha kuendelea na masomo ambapo mwaka 1981, Dk. Kamani alihitimu masomo ya kidato cha tano na sita.

Kwa mujibu wa sheria, kipindi hicho alijiunga na kuhitumu Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kambi ya Bulombora mkoani Kigoma kati ya mwaka 1981 na 1982.

Kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu, Dk. Kamani alifanya kazi kama Afisa Mifugo msaidizi katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kati ya mwaka 1982 na 1984, hiyo ilikuwa ni kwa mjibu wa Azimio la Musoma lililowataka vijana wa kiume kufanya kazi kwa miaka miwili kabla ya kujiunga na chuo.

Baada ya hapo, Dk. Kamani, alijiunga na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro mwaka 1984 na kufanikiwa kuhitimu mwaka 1987 na kutunukiwa shahada ya wa mifugo.

Dk.Kamani amekuwa kada wa 10 wa CCM kutangaza nia ya kutaka kugombea urais tangu chama kilipofungua milango. Wengine waliokwaishatangaza nia ni Makongoro Nyerere, Luhaga Mpina, Prof. Sospeter Muhongo, Edward Lowasa, Mwigulu Nchemba, Steven Wasira, Prof. Mark Mwandosya na Balozi Ali Karume.


Wabunge waijia juu Serikali kuhusu deni la bilioni 17 katika hospitali ya Apollo, India


CCM yaanza leo kutoa fomu kwa wanaoomba kuteuliwa kuwania Urais Tanzania 2015; Dk Seif Khatib aeleza utaratibuKatibu wa Halmashauri kuu ya CCM, Idara ya Oganezesheni Dk Mohamed Seif Khatib amepewa jukumu la kukabidhi fomu kwa wanaonuia kugombea Urais wa Tanzania 2015 kwa tiketi ya chama hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma kuhushu ratiba pamoja na mambo mengine, aliwataja watakaoanza kuchukua fomu kuwa ni Prof. Mark Mwandosya akifuatiwa na Stephen Wasira, Edward Lowasa, balozi Amina Salum Ali na  kisha Charles Makongoro Nyerere.


Dondoo za mkutanoni wakati Sumaye alipotangaza nia

Sumaye akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia ya Urais wa Tanzania.


DONDOO YA HOTUBA YA MHESHIMIWA SUMAYE AKITANGAZA NIA YA KUWA RAIS WA TANZANIA 2015 ALIYOITOA KILIMANJARO HOTEL PAMOJA NA MASWALI NA MAJIBU YAKE KWA WANAHABARI. JUNI 2, 2015.


Nimetangaza nia hapa Dar es salaam sio kwasababu sina kwetu, ni kwasasababu nafasi ninayoitafuta ni ya kuongoza watanzania wote.

Nimejiandaa kupokea kijiti kutoka kwa Rais Kikwete mnamo mwezi Oktoba iwapo chama changu kitaridhia, kwa kuwa nafasi ya Urais ni nafasi kubwa hatuhitaji kukimbizwa au kuswagwa kama mbuzi.

Mtu anayetaka nafasi ya Urais lazima ajipime, ajitafakari kwamba anatosha katika mambo yafuatayo.
Kiafya, kiakili, kimaadili na kifhamira na lazima asipungukiwe hata moja kati ya hayo na mtaka Urais yeyote lazima awe tayari Umma umpime katika hayo.

Watanzania wanataka Rais Mtiifu na Mwaminifu, anayefikiri na kushaurika na atakayetuwekea maslahi ya taifa mbele na sio maslahi yake binafsi.
Tunataka Rais mwenye uwezo wa kusimamia uchumi na kuondoka matabaka na pengo kati ya walionacho na wasio nacho.


Tumekuwa na malalamiko mengi juu ya sekta ya elimu, tunataka Rais ajaye ashughulikie suala hili na sio kushusha alama za ufaulu ili wanafunzi wengi waonekane wamefaulu.

Nimesikia wagombea wenzangu wakizungumza kuhusu rushwa, lakini kama upo serikalini na kuna rushwa kwanini hawaelezi wamepigana nayo kiasi gani?

Tunashuhudia watawanya rushwa na fedha wakisema eti watakomesha rushwa kwa kisingizio cha kupewa na rafiki zao lakini tujiulize nani anaweza kutoa fedha bila kujua atazirudishaje?

Nimeshangaa sana mtu anasema eti hatutaki kiongozi masikini yaani unashindwa kusema tu "tunataka Rais tajiri" hii ni hatari sana mtu anayesema yeye si tajiri na hataki Rais awe masikini.

Mimi nimejipima, nimetafakari na nimejiridhisha kuwa natosha, bahati nzuri watanzania wananijua na sifa ambazo watanzania wanazihitaji kwa Rais wao mimi ninajitosheleza.

Nilikuwa mbunge tokea 1985, nimekuwa Naibu waziri, nimekua waziri na nimekuwa waziri mkuu kwa miaka 10 kama ni jeshini tunasema mimi nimepanda kwa ranks and files na kama kuna mtu mwingine kati ya waliojitokeza ananizidi kwa hizo sifa nipo tayari kumpisha(anashangiliwa)...

Mimi si mpenda vyeo, Rais aliponiita na kuniambia nimekuteua kuwa waziri mkuu nilikataa nikamwambia naomba uteue mtu mwingine, Rais akakataa, hii inakuonyesha mimi si mpenda vyeo.

Ni mimi niliyekuwa kinara wa utekelezwaji wa mambo yote makubwa yaliyofanywa na awamu yetu ya tatu.


Tulikuza uchumi na kuondoa inflation kutoka asilimia 27 mpaka asilimia 4, ndio maana hakuna mfumuko wa bei uliotokea.

Mapato ya serikali ilikuwa bil.27 lakini ilipanda mpaka bil. 280
Mishahara ilikuwa kima cha chini 17 elfu lakini tulipambana na kuondoa suala hilo.
Tulipambana na kuhakikisha madeni yote sugu yanakomeshwa.

Umeme unakata, watu wanatania na kusema ni richmond hiyo.

Tulisimamia uchumi seriously mpaka tukapata msamaha wa madeni kutokana na appreciation tulivyokuwa tukikuza uchumi.

Tuliunda tume ya Warioba ipambane na rushwa.

tulianzisha kura ya maoni kwa wala rushwa ili wananchi wakapige na kuwataja wala rushwa kisha ambaye jina linatokea mara nyingi PCCB.

Mhe. Sumaye anataja idadi ya waliofukuzwa, na kusimamishwa kazi kutokana na rushwa, wengine wanasema tu lakini hawasemi waliikabili vipi rushwa.

Nilifanya maamuzi bila uoga, nilivunja halmashauri ya jiji la Dar es salaam na kuliboresha jiji kwa kiasi chake. Nilipandisha mapato ya jiji kutoka milioni 800 mpaka bilioni 800 mpaka 900.

Inshalah nikijaliwa kuwa Rais majiji yetu yataboreshwa zaidi.
Wakati tunaingia watoto wrngi walikuwa wakikaa chini lakini tuliongeza madawati kwa kasi sana mpaka tukafikia kipindi tukawa na akiba.

Leo hii tuna televisheni ya taifa kwa kuwa nilisimamia ikapatikana ambapo kwa miaka yote ilishindikana.

Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, watu wanatuhumu eti tuliuza mashirika ya umma.
Kwanza sera ya ubinafsishaji iliundwa kabla ya Mkapa kuingia madarakani na sisi tulisimamia sera ya chama leo hii eti tunalaumiwa.
Wafanyakazi wa mashirika ya umma hawakulipwa mpaka mwaka mzima kwa kuwa viwanda na mashirika yalikuwa hayapati faida zaidi ya hasara.

timu ya wataalamu(si wanasiasa) iliendesha mchakato wa ubinafsishaji na ni asilimia 20 tu ya mashirika yaliyonuniliwa na wageni, mengi yalinunuliwa na Watanzania.

Ubinafsishaji upo hata marekani, ndio maana kampuni kama General Motors imenunuliwa na wageni kutoka China na maeneo mengine.

Nimekumbana na mambo magumu kwa miaka kumi, ikiwemo ukame wa 1997 ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania mto Ruvu uliacha kupeleka hata tone moja baharini, tulipambana kwa kuchimba visima zaidi ya 300 Dar ndio watu wa Dar wakaweza kujisitiri.

Mvua za elninho pia zilitutikisa sana, reli nyingi ziling'olewa lakini tulipambana na kutumia hata wanajeshi wetu kuzijenga upya.

Leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita, serikali ipo wapi?
Nilifika kuamulia ugomvi wa makabila Tarime na nilishuka na helicopter katikati ya mapambano huku kila upande ukiwa umeshika silaha.

"Mimi nasema, kama kuna mtu amepikika kuliko mimi aseme, nimpishe. Na kama ni Afya ninayo.

NITAFANYA NINI NIKIWA RAIS?

Kwangu, Suala la uchumi ndio litakuwa la kwanza.
Huwezi kuboresha elimu, Afya, wala amani bila nchi kuwa na uchumi imara.

Tatizo la uchumi wetu tunaangalia takwimu badala ya uhalisia. Nitqshughulikia na kuwekeza katika kilimo, sipingi.kuwa na matrekta lakini hata kipindi cha Mwalimu yalikuwemo lakini hayakusaidia kukuza kilimo.

Leo tunasikia wakulima wanauza mazao yao kwa bei ya kutupa kwahiyo lazima tuwatafutie soko la uhakika.

Lazima tuimarishe viwanda vyetu na kuvilinda viwanda vyetu vya ndani.
Kuna viwanda vinauza nguo nzuri kabisa lakini tunaingiza kutoka nje tena bila kuchukua kodi. Hili ni lazima zikome.

Mimi kipaumbele changu kitakuwa ni uchumi na kupitia ukuaji wa kilimo mambo mengi yataimarika.

Nitaboresha huduma za jamii (afya na elimu).
Nitarudisha shule za vipaji maalumu ili vijana wenye uwezo mzuri kutoka shule za serikali, sasa hv shule zinazofanya vizuri za binafsi zinataka kupunguzwa nguvu.

Nitapunguza idadi ya robo tatu ya wanaoenda kutibiwa nje kwa kuboresha hospitali zetu.

Jambo lingine ninaloahidi ni kupambana na maovu ikiwemo rushwa. Mimi ni "zero tolerance katika rushwa na nina moral authority.

Nitaunda vyombo vya uchunguzi lakini pia nitaanzisha mahakama maalumu ya kushughikia masuala haya na hakika sitamuangalia mtu usoni wala cheo chake.

Mwisho, nasema "komesha rushwa, jenga uchumi na huu ndio motto(kauli mbiu) yangu.

Waandishi wa habari sambazeni taarifa hizi na watanzania watupime kwa uwezo wetu wa kujenga hoja na kutatua matatizo yao.

Ahsanteni.

Anaruhusu maswali kama yapo.

MC anasema maeneo mengi ya nchi hii umeme umekatwa.

Ibrahim Yamola Tanzania Daima anauliza. "Katika awamu uliyoongoza ziliibuka kashifa kama Meremeta, uuzwaji.wa NBC, Rada na uuzwaji wa mgodi wa Kiwira haya yalikushindaje?

Mwandishi wa mwananchi anauliza
"umekuwa ukinukuliwa kuwa CCM ikipitisha mla rushwa utajitoa, jee watanzania wategemee kukuona nje ya CCM?.

Mariam Mziwanda wa Uhuru anauliza.
"Eleza mali unazomiliki ili watanzania wajue na pia tuambie nani anakupa homa miongoni mwa wagombea unaogombea nao.

SUMAYE ANAANZA KUJIBU.1. Kuhusu kashfa zilizojitokeza, kwanza niseme ni kweli mimi nilikuwa mshauri wa Rais.
kuna vitu vimeitwa kashfa lakin mimi sioni kama kashfa mfano, NBC si kashfa, hii benki haikua ikitoa kodi yoyote hazina, gavana wa benki alitoa tahadhari kuwa kwa madeni ya NBC ukipanga noti za elfu kumi zinazidi urefu wa mlima Kilimanjaro.
Ubinafsishwaji wake ulitangazwa lakini pia haikuuzwa yote na ndio iliyozaa NMB ya leo.

Hakuna mwehu aliyekaa na mwenzake wakauzina NBC hotelini. Hakuna.

Zingine zote zinafanana. Rada, ndege ya Rais na mengineyo.

Nchi ilikuwa haikuwa na rada, Museveni alitaka kugongana na ndege zingine na kuna mashirika makubwa yalitaka kuondoa ndege zao Tanzania kwa kuwa ndege zilikuwa zikitazamwa kwa macho
Kama kuna mtu alifanya wizi na tulipotoka ndio wamebainika washughulikiwe.
Kiwira ilikuwa hivyo hivyo, bahati mbaya Mkapa akaingia na akatoka baada ya siku tatu.

Pili. Sitaungana na wala rushwa, nitatoka ndani ya CCM kama CCM watapitisha mla rushwa na siamini kama chama hiki kitachagua mla rushwa.
Sijajiandaa kutoka lakini iwapo watapitisha mla rushwa nitatoka kwa kuwa siwezi kuungana na wala rushwa.

Tatu, ninatajwa kuwa tajiri. muda unatoa jawabu, tujiulize hivi huo utajiri nilionao nataka kwenda kuulia mbinguni.

Mnakumbuka Mtikila alinitukana lakini akaja akasema watu wasafi nchi hii ni Sumaye, Warioba na Mwakyembe.
Walionituhumu
 nilipomaliza uongozi niliwaburuza kortini na nikashinda na fedha nilizopata kama fidia nilisomesha nyie wana habari.

"Hivi ningekuwa mla rushwa ningejitokezaje kuikemea rushwa?"

Kwa waliojitokeza sasa hivi hakuna hata mmoja ambaye ni tishio kwangu.

MASWALI YANARUHUSIWA TENA.

Pendo Omari (mwanahalisi online).
Tumekwama kwenye mchakato wa katiba, unawaahidi nini wananchi ambao maoni yao yaliyotupwa?

Mwandishi wa Mtanzania anauliza. "inasemekana unamiliki ardhi kubwa, hili lipoje?

Saed Kubenea anauliza.

"Ukiwa serikali ndio nyumba za serikali ziliuzwa, unasemaje kuhusu hili?

ANAJIBU

Kuhusu katiba mpya. Tangu mchakato unaanza nilisema usimamizi ni muhimu kuliko hata katiba kwasababu hata ikiwa nzuri wasipokuwepo wasimamizi wazuri mambo yatakwenda hovyo.

Suala la Ardhi, wapo watanzania wengi tu wenye ardhi kubwal kuliko mimi.

Gazeti liliandika nina ardhi kubwa na siliendelezi, sikuiendeleza kwa kuwa bado sijapatiwa hati.

Sisi wengine tumejikita kwenye kilimo hatutakiwi kuandamwa, tunafanya kile tunachokihubiri ili tuone na tu experience adha wanazokumbana nazo wananchi.

Kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali, Rais alishauriwa na cabinet na akakubali.

Kuna tume tatu zilifanyia kazi suala hili kwa muda tofauti na zote zilikuja na mapendekezo kuwa nyumba za serikali ni nyingi na serikali inagharamia fedha nyingi kuzikarabati na hivyo tuwauzie watumishi wa Umma.

Tulikuwa na nyumba nyingi mfano Breweries na bandari walikuwa na nyumba zaidi ya elfu moja.

Nyumba nyingi zilinunuliwa mpaka na wananchi wa kawaida, Rais alishituka kuona ghorofa zinainuka Oysterbay zilipokuwepo nyumba za serikali.
Rais akasema lazima paper iandikwe wauziwe wafanyakazi waliokuwa wakiishi humo na hakuna kuuzwa mpaka baada ya miaka 25, na gvt valuer akafanya tathimini na watumishi wa serikali wadogo kabisa wakauziwa.

Kuhusu kupambana na rushwa kubwa.

Hakuna rushwa amabyo ni kubwa kuliko Rais, huwezi ukapewa Urais alaf ukasema kuna rushwa kubwa.

Nyie nipeni Urais halafu mtaona ninavyowashughulikia wala rushwa.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akiwa na mke wake Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.

Taarifa ya NEC: Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura kwa wakazi wa Geita, Simiyu, Mwanza, Shinyanga

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA 

MIKOA YA GEITA, SIMIYU, MWANZA, NA SHINYANGA. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mikoa mine (4) ya Geita, Simiyu, Mwanza na Shinyanga kuwa itaendesha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kvra kutumia Teknolojia ya liometric Voters Registration'.

Zoezi hilo la Uboreshaji litanzia tarehe 02/06/2015 hadi 04/07/2015. Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji katika Kata zote za Mikoa hiyo mine iliyotajwa. Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-. 
 • Waliotimiza umri wa Miaka 18 na watakaotimiza Miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba 2015. 
 • Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura iii kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura. 
 • Wote ambao wanazo sifa lakini hawajawahi kujiandikisha 
 • Wananchi wanatakiwa kwenda kujiandikisha kwenye vituo vya kujiandikisha vilivyoko ndani ya Kata zao. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwasisitiza wananchi wote katika Mikoa hiyo minne kujitokeza kwa wingi ill waweze kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwani ndiyo hatua muhimu ya kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu na kuchagua viongozi wao. Uandikishaji utafanyika kwa muds vra siku saba (7) kwa kila kituo. 

JITOKEZE SASA NENDA KAJIANDIKISHE 

Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam 

Taarifa ya Wizara ya Uteuzi wa Wajumbe wa TPA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA UCHUKUZI 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Yah: KUTEUA WAJ UMBE WAPYA WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA) NA KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA UJUMBE WA SASA 


Kwa mamlaka aliyopewa kwa mujthu wa Kifungu Na. 6, Kifungu kidogo cha 2 (b) cha Sheria ya Bandari Na. 17 ya mwaka 2004, Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Samuel J. Sitta (Mb) amewateua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuanzia tarehe 2 Juni, 2015:
 1. Dkt. Tulia Akson — Mhadhiri Mwandamizi, Chuo cha Sheila Tanzania; 
 2. Injinia Musa Ally Nyamsingwa — Mhandisi wa Ujenzi, Norplan Consultants; 
 3. Ndugu Donata S Mugassa — Mtaalam wa Manunuzi na Mjumbe wa Bodi ya PSPTA; 
 4. Ndugu Haruna Masebu — Mkurugenzi Mkuu Msataafu wa EWURA; 
 5. Injinia Gema Modu — Mhandisi wa Elektroniki, Bodi ya Wahandisi Tanzania; 
 6. Dkt. Francis Michael — Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dsm; 
 7. Ndugu Crescentius Magori — Mkurugenzi wa Mipango (NSSF); na 
 8. Nd. Flavian Kinunda — Mkuruganzi wa Masoko Mstaafu, Mamlaka ya Badari Tanzania.

Lengo la uteuzi huu ni kuleta tija na ufanisi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Uteuzi huu unatengua uteuzi wa wajumbe wa sasa wa Bodi hiyo kuanzia tarehe 2 Juni, 2015. 

Wizara inawashukuni wajumbe wanaoondoka kwa kazi waliyoifanya wakati wakiwa wajumbe iNa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Tunawatakia kila la kheri katilca shughuli zenu nyingine za ujenzi wa Taifa letu. 

Kwa wajumbe wapya, Wizara inawatakia kila la kheri katika jukumu zito walilokabidhiwa la kusimamia shughuli za Bandari yetu ambayo ni muhimu katika uchumi wa Taifa letu. 

Imetolewa na Wizara ya Uchukuzi 
2 Juni, 2015

Mbunge Dk Ndugulile anusurika ajalini; Amlilia Mwaiposa waliyezungumza saa chache

Dk Faustine Ndugulile
Dk Ndugulile

Mbunge wa Kigamboni, Daktari Faustine Ndugulile ametaarifu kwenye blogu yake kuhusu ajali aliyoipata na kunusurika kifo huku akihuzunishwa siku moja baadaye kwa msiba wa Mbunge mwenziye waliyezungumza siku moja kabla ya kifo chake. Ujumbe wake unasomeka ifuatavyo:

Jana na leo si siku nzuri kwangu. Nikiwa njiani kuja Dodoma, nilipata ajali. Namshukuru Mungu niko salama lakini gari imeharibika sana baada ya kugongwa na Lori la aina ya Semi-trailer. Gari lilivutwa kurudi Dar nami niliendelea na safari ya Dodoma.

Nilipofika Dodoma, Mbunge wa kwanza kuonana naye alikuwa Mhe. Eugene Mwaiposa wa Ukonga. Tulikutana kwenye geti la kuingilia mjengoni. Tuliongea na kutaniana kuhusu michakato ya uchaguzi kwenye majimbo yetu.

Baada ya Bunge kuanza jioni alikuja akakaa kwenye kiti changu na kuongea na Mhe. Esther Bulaya. Aliniomba namba za simu za Waziri mmojawapo nikampa na alipohitimisha maongezi yake na Mhe. Bulaya alirudi kitini kwake. Hii ilikuwa kwenye saa kumi na moja jioni. Alionekana mzima na mwenye afya.

Leo asubuhi nikapata taarifa kuwa Mhe. Mwaiposa ametutoka. Nilishtuka sana.

Nitamkumbuka Mhe. Mwaiposa Kwa ushirikiano wake katika Umoja wa Wabunge wa Dar Es Salaam.  Umetangulia Mhe. Mwaiposa, nasi tuko njiani. Kapumzike kwa amani.

Dkt Faustine Ndugulile MB
Mbunge wa Kigamboni

Niambie Live Show: Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi

Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi
Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi


Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.

Ni Niambie Live....

KARIBU

Prof. Muhongo: Mwenye kuweza kuikwamua Tanzania ni mimi

* Atangaza nia kwa kutoa takwimu za umasikini na utajiri
*Asema viwanda, gesi, umeme utaipaisha Tanzania

Habari kutoka kwa Mwandishi wetu, Musoma

WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.

Pamoja na mambo mengine, Muhongo alitumia muda mwingi kutoa takwimu hali ya umasikini na utajiri kwa wananchi wa Tanzania, bila kusahau baadhi ya nchi ambazo zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kujikita kwenye kuzalisha wataalamu na watafiti, akiwamo yeye, ambaye si tu ni Profesa, bali pia amebobea kwenye nishati kwa miaka mingi.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya wanachama wa CCM na Watanzania katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria, Musoma Mjini, Profesa Muhongo alisema kwamba anayo tiba ya umasikini wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba anatumia utaalamu wake kwa kusimamia mambo ya gesi, mafuta, umeme, bila kusahau elimu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wake.

“Nchi ina upungufu mkubwa wa takwimu hali inayowafanya viongozi washindwe kujua namna gani wanaweza kuondoa umasikini na kero zinazowakumba wananchi wake, hivyo hata wale wanaosema wanataka uongozi, hawajui wangapi wenye uhitaji.
“Ukiacha takwimu ambayo kwa Dunia ya sasa ni lazima, nchi yetu lazima ijiamini, kuongeza ushindani, kuongeza upendo, bila kusahau rushwa ambayo kwa uhakika inapaswa kupigwa vita kwa vitendo ili nchi yetu isonge mbele,” 
alisema Muhongo.

Kuhusu uchumi, Profesa Muhongo alisema kwamba ni aibu Tanzania kupitwa kiuchumi na Mataifa waliyokuwa nayo sawa, akitolea mfano wan chi za Brazil, China, India na Kenya ambao wao wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye elimu na utafiti.

Alisema nchi ikiwa na watafiti, wananchi wao hawataishi kwa mashaka, huku akisema endapo atapitishwa kuwania nafasi hiyo na kuwa rais wa Tanzania, atahakikisha kwamba anakuza uchumi wan chi kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 10 na 15 kwa kipindi cha miaka mitano hadi 10 ya urais wake.
“Nimeweza kufanya kazi ya gesi na mafuta kwa miaka kadhaa kwenye nchi mbalimbali, hivyo hakika kama chaguo ni wataalamu, basi mimi nastahili kwa sababu sioni mwingine mwenye uwezo wa kutangaza kuondoa kero za Watanzania na jinsi atakavyoziondoa.
“Ndio unaweza kusema utaondoa umasikini kwa wananchi au kuongeza mishahara, lakini ili hilo liweze kufanikiwa kwa vitendo, ni lazima pia katika kipindi cha uongozi wako uweze kukuza uchumi wako kwa kiasi kikubwa, bila hivyo hakuna kitu,” 
alisema Muhongo.

Aidha Profesa Muhongo alisema kwamba Duniani kote nchi zimepiga hatua kwa kuwekeza kwenye wataalamu na viwanda, hivyo Tanzania inapaswa kuangalia namna ya kuwekeza kwenye sekta hizo, bila kusahau sekta ya elimu yenye umuhimu mkubwa.

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alisema kwamba akiwa Waziri wa Nishati na Madini, ndio mtu ambaye alifanikiwa kwa vitendo kutekeleza ilani ya CCM kwa kuhakikisha kwamba vijiji vingi vinapata umeme kwa kuongeza bajeti na kusimamia kwa vitendo wakala wa umeme vijijini (REA).

Alisema kusudio la kuhakikisha kwamba wananchi wake wanaendelea kupata umeme kwa bei nafuu ni kati ya mambo anayoona yanafaa kuongezewa chapuo na usimamizi wa aina yake, hivyo mwenye uwezo wa kulitatua hilo ni yeye.
Rais Kikwete akiwa Ufini


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi Dorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa Finland Dorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyoRais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.

akipokea zawadi ya jezi ya timu ya taifa ya Finland ya basketball

Kikwete akitoa zawadi ya mchoro wa Tingatinga kwa viongozi wa kampuni ya KONE


Kikwete akitembelea bandari ya HelsinkiRais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli NiinistoRais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli Niinisto

Rais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli Niinisto
Rais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli Niinisto

Shukurani:

 • Picha: Ikulu, 
 • Video: StarTv


Taarifa Waajiri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi


Mstaafu Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania afariki


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kuanzia Mwaka 1996 hadi 2002, Onel E. Malisa kilichotokea leo Alfajiri tarehe 2 Juni, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dares Salaam.

Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu linaendelea kuratibu taratibu zote za kuaga na mazishi ya marehemu. Hivi sasa msiba upo nyumbani kwake Kinyerezi, Jijini Dar es Saalam. Aidha taarifa kamili kuhusiana na msiba huu mtaendelea kufahamishwa baada ya mipango yote kukamilika.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi;

AMINA

WASIFU WA MAREHEMU

Marehemu alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kidia mwaka 1951 – 1954 na baadae Shule ya Msingi Kidia Juu (Kidia Upper Primary School) mwaka1955 – 1958. Alihitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne mwaka 1974 katika Shule ya Sekondari Mawenzi akiwa mtahiniwa wa kujitegemea (Private Candate). Aidha, alisoma Cheti cha Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1975 – 1976 na baadaye Shahada ya Kwanza ya Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1977 – 1980.

Marehemu ajiunga na Jeshi la Magereza mwaka 1964 baada ya kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Chuo Ukonga, D’Salaam yaliyofanyika kuanzia Januari - Julai, 1964. Ndani ya utumishi, alipata fursa ya kuhudhuria Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili (Advance Course) Chuo Ukonga, D’Salaam kuanzia Aprili – Julai, 1967 na Mafunzo ya Uongozi wa Juu (Gazetted Course) kuanzia Februari – Mei, 1974.

Kutokana na utendaji wake wa kazi, marehemu aliwahi kutunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-

• Afisa Magereza Daraja la Tatu mwaka 1964
• Afisa Magereza Daraja la Pili mwaka 1965
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Nne mwaka 1967
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Tatu mwaka 1971
• Mrakibu Msaidizi wa Magereza mwaka 1975
• Mrakibu wa Magereza mwaka 1976
• Mrakibu Mwandamizi wa Magereza mwaka 1978
• Kamishna Msaidizi wa Magereza mwaka 1982
• Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza mwaka 1984
• Kamishna wa Magereza mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Magereza mwaka 1996 – 2002

Aliwahi kufanya kazi katika vituo mbalimbali vikiwemo Gereza Butimba - Mwanza, Isanga - Dodoma, Wami Vijana - Morogoro, Chuo cha Usalama Moshi, Gereza Songwe - Mbeya, Chuo Ukonga - D’Salaam na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, D’Salaam.

Aidha, marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Magereza kama ifuatavyo:-

• Mkufunzi Mkuu Chuo Ukonga mwaka 1975
• Mkuu wa Chuo Msaidizi, Chuo Ukonga mwaka 1981
• Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1983
• Mkurugenzi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1984
• Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Makao Makuu mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza mwaka 1996 – 2002 alipostaafu kazi.


Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake. Baadhi ya mambo aliyoyafanya ni kama ifuatavyo:-

• Alianzisha na kuimarisha mahusiano baina ya Jeshi la Magereza na Magereza ya nchi nyingine Afrika na duniani.
• Alikuwa mmojawapo wa Makamishna wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Nchini (Law Reform Commission)
• Alikuwa mshauri kwenye Maboresho ya Jeshi la Magereza pamoja na Sera ya Taifa ya Magereza.
• Kama hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani aliweza kushauri na kusimamia kutungwa kwa Sheria zifuatazo:-

- Sheria ya Bodi ya Parole
- Sheria ya Huduma kwa Jamii (Community Service)

Nishani alizotunukiwa akiwa kazini ni:-

• Nishani ya mstari wa nyuma
• Nishani ya Utumishi mrefu
• Nishani ya Utumishi uliotukuka

Hata baada ya kustaafu kazi, marehemu aliendelea kutoa mchango wake kwa kushauri mambo kadhaa pamoja na kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya Jeshi na Taifa. Kutokana na mchango wake huo alitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2015.
Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza, tunatoa salamu nyingi za rambirambi kwa Mke, Watoto na Ndugu wa Marehemu kwa msiba huo mkubwa uliotufika.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

Mbunge aaga dunia

Kwenye blogu ya CCM kuna ujumbe unaosomeka ifuatavyo:

Eugen Mwaiposa
Eugen Mwaiposa

Taarifa zilizotufikia sasa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa amefariki dunia leo mjini Dodoma.

Blogu nyingine zimeeleza kuwa, Mbunge huyo ameaga dunia akiwa amelala nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.

Naibu Spika, Job Ndugai amelitangazia Bunge kuwa marehemu Mwaiposa alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Mwili wake utaagwa kesho mara baada ya familia yake kuwasili Dodoma.

Bunge limeahirishwa hadi Jumanne ya tarehe 4 Juni 2015.Taarifa ya habari Channel TEN, Juni Mosi, 2015
Mwanachuo Mzumbe atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania 2015


Hamasa ya wanaCCM kutangaza nia ya kuwania urais imemwibua mwanafunzi Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Maliki Malupu (34).

Malupu alitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM akiahidi kushughulikia suala la elimu, afya, kilimo na michezo huku akijua kuwa umri wake haujatimia miaka 40 inayotakiwa kikatiba.

Akitangaza nia hiyo mjini Morogoro jana, Malupu alisema kutokana na uaminifu na uadilifu wake, ameamua kuwania nafasi hiyo pamoja na mambo mengine kwa kuwa ni haki yake kikatiba.

Alipoulizwa atatimizaje nia yake hiyo bila kuwa na sifa kikatiba, alisema vifungu vya katiba vinavyotaja umri vina utata, hivyo ameamua kuingia kuvitafutia suluhisho.
“Unajua ibara ya 39 (1) (b) inasema lazima utimize miaka 40, lakini ibara (d) inasema mtu mwenye sifa za kuwa mbunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi anaweza kuwania urais,” 
alisema akifafanua kuwa yeye ana sifa hizo.

Akieleza sababu nyingine zilizomsukuma kuwania urais, Malupu alisema kuwa ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa kikamilifu kwa kuwa muda mrefu imekuwa ikichezewa na baadhi ya viongozi.

Alisema muundo wa sekta hiyo unapaswa kurekebishwa kwa ama kufutwa au kuondoshwa utaratibu wa kupanga viwango vya ufaulu wa GPA kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari katika mitihani ya kidato cha sita na cha nne.

Alisema utaratibu huo haufai kwa kuwa hautoi matokeo ya kuboresha maarifa kwa wanafunzi, pia unawaathiri wanafunzi kisaikolojia katika kujitofautisha wao na wanafunzi wa elimu ya juu.
“Nitahakikisha naboresha mitalaa kwa masomo ya kidato cha nne na cha sita ili kuleta weledi wa kina na wa kutosha, nitaboresha mazingira ya watumishi sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na stahiki za walimu wa msingi hadi vyuo,” 
alisema.

Katika mkutano wake wa saa 1.30, Malupu alisema atahakikisha anadhibiti suala la maprofesa kuacha kazi yao ya weledi na kukimbilia katika siasa na ataboresha stahiki zao na mishahara kwa kuwalipa vizuri wanaofundisha vyuo vya Serikali na binafsi bila ubaguzi wowote ili kuimarisha sekta ya elimu ngazi vyuo vikuu.

Malupu alisema ataitazama sekta ya kilimo kwa kuongeza vyuo vikuu vya kilimo ili kuleta tija ya kilimo katika sekta hiyo na Serikali yake itakuwa na mkakati mahsusi wa kutoa elimu na mitaji kwa wakulima wanaofanya kilimo chenye tija na kilimo cha kujikimu. Katika afya, Malupu alisema kuwa atahakikisha suala la afya linasimamiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja kuwapatia wazee huduma bure na kwamba zahanati, vituo vya afya na hospitali zinapatiwa vifaatiba vya kutosha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Malupu pia alizungumzia wananchi wanaoishi katika visiwa vya Ukerewe mkoani Mwanza na Mafia mkoani Pwani kuwa wamesahaulika, hivyo akiteuliwa na baadaye kuchaguliwa atahakikisha anakifanya kisiwa cha Ukerewe kuwa mkoa unaojitegemea ili kuwapunguzia wananchi umbali wa kufuata huduma Mwanza.
“Wananchi wa Visiwa vya Mafia na Ukerewe wanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa huduma za kimkoa kutokana na mazingira ya kijiografia na wamesahaulika kwa kiasi kikubwa,” 
alisema.

Katika hotuba yake hiyo, Malupu aliwataka vijana kutokata tamaa na kujitokeza kugombea nafasi za udiwani, ubunge na urais pamoja na kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kutumia haki hiyo ya kikatiba kwa kupiga kura.

Michezo

Akizungumzia uboreshaji wa sekta ya michezo, Malupu alisema atahakikisha anaanzisha vituo vya kulea vipaji katika mpira wa miguu vitakavyowawezesha vijana kuibua vipaji na kuwapa elimu ya msingi kuhusu mpira wa miguu ili kuinua soka la Tanzania. Pia, aliahidi kuboresha sekta ya filamu na muziki kwa ujumla kwa kuwawekea vijana utaratibu maalumu ili waweze kujitengenezea ajira za kudumu.

Polisi na nyumba

Aliahidi kulipatia Jeshi la Polisi nyumba za shirika la nyumba ili kuondokana na wanazokaa ambazo hazilingani na hadhi walionayo...
“Nia yangu ni kuhakikisha askari polisi wanakaa katika mazingira salama na yenye hadhi yao siyo kama ilivyo sasa,” 
alisema.


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 2, 2015
(?) Wanaounda Kamati Kuu ya CCM itakayopitisha majina 5 ya wawania Urais Tanzania 2015

Hii ndio Kamati Kuu (CC) ya CCM itakayopitisha majina matano ya wagombea Urais kwa ajili ya kupigiwa kura na NEC kupata mgombea mmoja.

1. Jakaya Mrisho Kikwete 
2. Dk. Ali Mohamed Shein 
3. Phillip Japhet Mangula 
4. Abdulrahman Kinana 
6. Dk. Mohamed Gharib Bilal 
7. Mizengo Kayanza Peter Pinda 
8. Balozi Seif Ali Iddi 
9. Anna Semamba Makinda 
10. Pandu Amir Kificho 
11. Rajab Luhwavi 
12. Vuai Ali Vuai 
13. Nape Moses Nnauye 
14. Mohammed Seif Khatib 
15. Zakhia Hamdan Meghji 
16. Asha Rose Migiro 
17. Sophia Simba 
18. Sadifa Juma Khamis 
19. Abdallah Majura Bulembo 
20 Jenister Mhagama 
21. William Lukuvi 
22. Steven Masatu Wasira 
23. Emmanuel John Nchimbi 
24. Pindi Chana 
25. Jerry William Silaa 
26. Adam Kimbisa 
27. Shamsi Vuai Nahodha 
28. Hussein Ally Mwinyi 
29. Maua Daftari 
30. Samia Suluhu 
31. Salim Ahmed Salim 
32. Makame Mbarawa 
33. Hadija Abood

Nafasi zilizo wazi:

34. Anna Kajumulo Tibaijuka (ametolewa kutokana na kashfa ya Escrow) 
35. Salmin Awadhi (amefariki)

Kabla ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012 wenyeviti wastaafu (Taifa) na makamu wenyeviti wastaafu (taifa) walikuwa wajumbe wa kamati kuu. Kwa sasa wana nafasi yao kama Baraza la Ushauri ambalo wajumbe wake ni hawa wafuatao:

 1. Ally Hassan Mwinyi - Mwenyekiti 
 2. Pius Msekwa - Katibu 
 3. Benjamin William Mkapa - Mjumbe 
 4. Amani Abeid Karume - Mjumbe 
 5. Dk. Salmin Amour - Mjumbe

Hawa wazee wa Baraza la Ushauri wana nafasi yao katika ushauri kwa kamati kuu kuhusu wagombea Urais. Vikao vyao havina kalenda hukutana tu pale linapokuwa jambo muhimu na mahususi linalohitaji mawazo yao.

Maamuzi ya Kamati Kuu ni kwa consensus (busara/common sense), sio kura.


Prof. Mwandosya atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania 2015

Nianze kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,muweza wa yote kwa rehema nyingi alizotushushia kutuwezesha kuifikia siku hii ya leo.

Kwani hatukustahili zaidi ya wengi waliotutangulia mbele za haki.Nawashukuru ninyi nyote mliofika kuungana nami katika siku hii muhimu katika kukuza,kuimarisha na kuendeleza demokrasia ndani ya Chama chetu,Chama Cha Mapinduzi.

Wazee wangu, Waheshimiwa Maaskofu, Viongozi wa Dini na madhehebu mbalimbali,Waheshimiwa viongozi wa kimila,Waheshimiwa Machifu,akina mama,vijana,WanaCCM wenzangu,Viongozi wa vyama vya siasa,Wananchi,Wana Mbeya,Nawashukuru,Asanteni sana kwa uwepo wenu.

Ndugu zangu,
Kwa muda mrefu na kwa njia mbalimbali za mawasiliano mmekuwa mkinidadisi Mbona kimya kuhusu mwaka 2015? Pamoja nna kwambamliutaja mwaka tu, lakini niliwaelewa.

Wengi mliushangaa ukimya wangu.Pamoja na na kwamba ukimya ni sehemu ya haiba yangu na daima nimeupokea kama ni karama aliyonitunuku Mwenyezi Mungu,Muweza wa yote,baadhi yenu niliwajibu " Ukimya una Kishindo"! Kuhusu Sultan Qabus wa Oman,mwandishi mmoja maarufu aitwae Robert Kaplan amemwelezea ifuatavyo: Ni mtu mkimya, mpole, hapendi kuzungumza na waandishi wa habari mara kwa mara, hapendi habari zake ziandikwe kwenye magazeti mara kwa mara,lakini ameibadilisha nchi ya Oman kutoka makundi hasimu ya makabila na kuwa taifa linaloheshimika na linaloendelea kwa kasi sana na kuwa mfano wa kuigwa...." Sijifananishi na Sultan Qabus, la hasha.Isipokuwa najaribu kusisitiza kwamba mara nyingi ni bora katika maisha kuwa mjenga hoja na mtendaji makini kuliko kuwa mpayukaji na maamuzi ya papo kwa papo yenye matokeo hasi na yenye hasara kwa taifa. Nimeenda nje kidogo ya mada yangu!

Kwa staili ya siku hizi wagombea watarajiwa huwa tunajitokeza na kusema : tutatangaza nia siku hii au ile! Nadhani tunawashangaza na mtuwie radhi.Kwani kwa kusema hivyo tunakua tayari tumetangaza nia!Basi nami kwa staili hiyo hiyo naomba kutangaza rasmi mbele ya kadamnasi hii kama mashahidi,kwamba kwa unyenyekevu mkubwa, nitaomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natarajia kuendeleza rasmi safari niliyoianza leo kwa kuchukua fomu za maombi hayo pale Dodoma,Makao Makuu ya CCM, jumatano, tarehe 3 Juni,2015, saa 4 kamili,barabara.

Kipindi cha mpito kutoka awamu moja ya uongozi kwenda awamu nyingine kingekuwa kigumu sana kwa nchi nyingi hasa nchi zetu za kiafrika. Mifano iko wazi.Majirani zetu wamepata shida.Lakini waasisi wetu Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume wametujengea misingi imara.

Tuna kila sababu ya kuwashukuru na tuna kila sababu ya kujivunia misingi hiyo. CCM haijayumba na CCM haitayumba.

Baadhi ya wanachama inawezekana wameyumba. Hebu tuzirudie Ahadi za mwana CCM: binadamu wote ni ndugu zangu na AFrika ni moja, nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma, rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa, cheo ni dhamana sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu binafsi, nitajielimisha kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote, nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu, nitakuwa mwanachama mwaminifu wa ccm na raia mwema wa Tanzania na Afrika nzima.

Nitasema kweli daima fitna kwangu ni mwiko. Hii ndiyo CCM na atoaye ahadi mbele za Mwenyezi Mungu ndiye Mwana CCM,na si vinginevyo.

Ahadi ya mwanaCCM ya kuondoa umaskini inanipa nafasi ya kuelezea na kusisitiza kipaumbele muhimu sana cha serikali iliyodhamiria kuwaondoa wananchi wake kutoka lindi la umasikini ni kukuza uchumi,uchumi wa kisasa,uliojikita katika misingi ya sayansi na teknolojia na kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kama kichocheo cha maendeleo hayo.

Kama sayansi na teknolojia ndio msingi wa uchumi wa kisasa basi naweza kusema,tena kwa unyenyekevu mkubwa kwamba aliye mbele yenu ndiye pekee mwenye ujuzi,uelewa,na uzoefu wa masuala haya. Ninalotaka kusisitiza hapa ni kwamba kukuza na kusimamia uchumi ndio utakuwa kipaumbele namba moja.Jenga kwanza uchumi imara na mengine yatafuata.

Uchumi imara unajengwa hasa pale panapokuwa na lengo la kitaifa.Lengo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ni Tanzania kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Lengo hilo liliwekwa mwaka 2000. Tudhamiria sasa kwamba ifikapo mwaka 2030 Tanzania iwe nchi za juu zenye kipato cha kati(High Middle Income),na kwamba ifikapo 2050 Tanzania iwe nchi iliyoendelea.

Tunawezaje kuyafikia malengo hayo? Tunawezaje kukuza uchumi na ukuaji huo uwe endelevu?Hili ndilo swali.
 1. Kilimo cha kisasa na cha kisayansi kupitia matumizi zaidi na bora ya mbolea; kuendeleza utafiti kwa kuboresha miundombinu,vifaa,na kuendekeza rasilimali watu;kuboresha mifumo na aina ya mikopo kwa wakulima wadogo;kuboresha barabara za vijijini; kuendeleza ujenzi wa maghala kwa ajili ya kutunza nafaka;kuwa na migumo ya uhakika ya masoko ya mazao;na kuhakikisha kiwanda cha kimkakati cha mbolea itokanayo na gesi asilia kinajengwa haraka iwezekanavyo.
 2. Kuanzisha na kuendeleza viwanda,kwa kuanzia viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao na rasilimali asili
 3. Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula.
 4. Kuendelea kusimamia kutengemaa kwa uchumi mpana
 5. Kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa ndani na kutoka nje
 6. Kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ipasavyo kwa kufungua fursa nyingi za utalii wa ndani na utalii katika sekta ya kusini.
 7. Kuongeza tija katika utendaji wa kazi kwa kuthamini kazi(kufanya kazi kwa bidii,kwa uadilifu,na kwa kujituma), kusimamia kanuni,maadili na miiko ya utumishi wa umma na kuufanya utumishi wa umma usiwe wa mazoea tu bali wa ushindani unaopimika katika kutoa huduma kwa wananchi.Hii itakwenda sambamba na kulinda haki na kuboresha msilahi ya wafanyakazi.
 8. Kuchukia,kuzuia na kupambana na ufisadi na rushwa. Kuondoa vikwazo vinavyoonekana kuwepo kwa matabaka mawili ya wananchi; wale wanaoshughulikiwa na takukuru moja kwa moja,na wale ambao kibali kinahitajika kuwashtaki,kwa kuipa Takukuru uwezo wa kisheria kufanya kazi bila kuingiliwa na chombo chochote,wakati huohuo kuhakikisha haki za wananchi wema zinalindwa kupitia chombo cha kusimamia malalamiko (ombudsman).
 9. Kuendeleza na ikibidi kuimarisha uhuru wa Benki Kuu na uhuru wa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi,mifuko ya jamii,bima.
 10. Serikali kuwa injini ya ukuaji wa uchumi lakini kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi,mtu mmoja,vikundi vya wajasiriamali,saccos,na kampuni binafsi kuchochea ukuaji wa uchumi.

Uchumi unapokua,basi serikali itakuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza vipaumbele katika maendeleo ya jamii: Elimu,maji safi na salama,afya, na miundombinu.

Kuhusu elimu,lengo litakuwa ni kuboresha mitaala ili iendane na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ngazi zote;kuhakikisha kila mtanzania ana nafasi sawa ya kujiendeleza kielimu kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu; kuendeleza elimu ya ufundi na kilimo; kuandaa na kutekeleza mipango kwa hatua kuifanya elimu ya msingi ifikie kidato cha pili, cha nne na hatimaye kidato cha sita;kuongeza wingi wa udahili wa wasichana katika katika ngazi ya elimu ya juu;kuboresha hali na ari ya utendaji wa kazi kwa walimu,ikiwa ni pamoja na ujenzi nyumba za kuishi na kuongeza ujira.

Katika maeneo mengine ya huduma za kijamii,lengo la serikali litakuwa ni kutekeleza sera zilizopo na kuhakikisha malengo yanatekelezwa na yanapimika.Katika kuleta afya bora kwa wananchi lengo litakuwa ni kuweka mizania katika kuzuia na kupambana na magonjwa.

Uchumi hauwezi kukua pasipokuwa na amani na utulivu. Amani usalama na utulivu ni tunu.Waasisi wetu wametujengea msingi wa tunu hii.

Viashiria vya kupotea kwa amani vinaanza kuonekana kutoka ndani na nje.Hali inahitaji kuimarisha vyombo vyetu vya usalama katika maeneo yote hususan mafunzo,vitendea kazi,vifaa, miundombinu na silaha za kisasa.Hatimaye ulinzi wa nchi unaanzia mwananchi mwenyewe.

Nafasi ya Zanzibar katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni kubwa. Hii inatokana na asili na haiba ya nchi zenye visiwa,Zanzibar ikiwa mojawapo. Historia ya Zanzibar inatukumbusha hili.Kwani katika karne ya kumi na tisa Zanzibar iliongoza eneo lote la Afrika ya Mashariki kiuchumi na maendeleo,ukuondoa biashara ya utumwa.

Ilisemekana Ikipigwa zumari Zanzibar wanacheza ngoma maziwa makuu. Kila linalowezekana litafanywa kuondoa kabisa hali inayoweza kuikwaza Zanzibar kufikia uwezo wake mkubwa kiuchumi.Muungano utaimarika na uchumi wa Tanzania utakuwa kwa kasi zaidi.

Nahitimisha na suala muhimu la uzalendo.Kwa tafsiri isiyo rasmi,Uzalendo ni upendo kwa nchi. Tumeanza kushuhudia kupungua kwa uzalendo. Upungufu huo unajionesha katika kuenzi tamaduni za nje,kubeza juhudi za maendeleo yaliyopatikana, viongozi kutoa matamshi yanayo kebehi nchi wakiwa nje ya nchi,kutojivunia historia yetu iliyojikita katika michango ya mashujaa wetu.

Hawa ni pamoja na wale waliopambana na wakoloni,akina Kinjeketile, Mkwawa , Mirambo,Chaburuma na wengineo ambao walitoa uhai wao kulinda na kutetea heshima ya mwafrika dhidi ya ukoloni.Aidha waasisi wa TANU,Hayati Mwalimu Nyerere,Sykes,Mzee Kawawa, na wenzao;Waasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Hayati Abeid Amani Karume na wenzake akina Mzee Thabit Kombo,Kanali Seif Bakari,Hais Darwesh,Edington Kisasi,Yusuf Himid,Said Washoto na wengineo;ambao walionesha upendo na uzalendo wa hali ya juu.Vilevile tuna mashujaa wa ukombozi wa Kusini mwa Afrika akina George Magombe na Hashim Mbita.Tutaendelea kuenzi, kuthamini,na kuiendeleza michango mikubwa ya Marais wetu wastaafu,Mzee Aboud Jumbe, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Idris Abdukwakil,Dr Salmin Amour,Dr Amani Abeid Karume,na Mzee Benjamin William Mkapa. Kipekee napenda kuwashukuru Marais wetu wa sasa; Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mheshimiwa Dr Ali Mohamed Shein.ambao wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha uchumi na umoja wa nchi yetu. Daima nitaenzi mchango wao. Tujivunie nvhi yetu na Kwa pamoja tutaenga nchi tunayoitaka.

Balozi Ali Abeid Karume atangaza ni ya kuwa Rais wa Tanzania 2015Mwanadiplomasia mashuhuri visiwani Zanzibar, Balozi Ali Karume ametangaza nia ya kuchukua fomu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Balozi Karume alitangaza nia yake hiyo jana katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja na kuahidi kuwa iwapo chama chake kitampitisha na kupata ridhaa ya kuingia Ikulu, atatoa uhuru wa kujieleza kwa wananchi wake na uhuru wa kuikosoa Serikali bila ya kuvunja sheria na katiba ya nchi.

Alitumia muda mwingi kuelezea historia na uzoefu wake wa uongozi ndani ya chama na Serikali na kuwataka Watanzania kutokurupuka kumchagua rais kama watataka maendeleo endelevu.

Balozi Karume alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ya urais, baada ya kujipima na kuona ana sifa na uwezo wa kuliongoza Taifa la Tanzania na akawakumbusha wagombea wenzake umuhimu wa kuwa na kiongozi atakayeweza kujenga umoja na kudumisha amani miongoni mwa Watanzania.

“Ni wakati wa kufikiria na kutukuza utaifa wetu, badala ya Utanganyika na Uzanzibari,” alisema Balozi Karume katika mkutano wake huo uliochukua takriban saa moja na nusu.

Kwa mujibu wa Balozi Karume, urais unahitaji kiongozi mwenye sifa na uadilifu atakayepiga vita vitendo vya ubadhirifu na kukemea rushwa ili kujenga Taifa lenye kufuata misingi ya sheria na utawala bora.

“Uongozi si suala la majaribio, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuwa makini na watu ambao walishawahi kupewa uongozi na kushindwa kutokana na kukosa uadilifu,” alisema Balozi Karume.

Hata hivyo, alisema kwamba atahakikisha anaendeleza mipango yote ya maendeleo iliyoanzishwa na Rais Jakaya Kikwete na kukabiliana na kero mbalimbali zinazowakabili Watanzania hasa suala la umaskini, maradhi na elimu.

Vipaumbele vyake

Akizungumza katika shamrashamra za kutangaza nia hiyo, Balozi Karume alisema lengo lake ni kuwania nafasi hiyo ya juu serikalini ili kupokezana kijiti na kuendeleza mambo yote mazuri yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete.

Balozi Karume alitaja kipaumbele chake cha kwanza kuwa ni uhuru wa watu wote. “Kila mtu ana haki ya kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo yake kuwa muumini wa dini au chama chochote cha siasa tena bila kubughudhiwa na mtu mwingine.

“Mkombozi wa mwananchi ni kuimarisha kilimo kwanza, elimu baadaye, huwezi kusoma huku ukiwa na njaa na hilo ndilo lengo nikipata ridhaa ya kuwa Rais wa Muungano” alisema Balozi Karume.

Alisema Tanzania ili iweze kujenga uchumi imara, inahitaji kiongozi mwenye mbinu na uwezo wa kupambana na rushwa na ufisadi kwa vile ndiyo adui wakubwa wa maendeleo yake.

Alisema kuwa atahakikisha Watanzania wanapata uhuru wa kuchagua chama wanachotaka, uhuru wa kuabudu dini wanayotaka na kufanya biashara katika mazingira bora pamoja na kufungua milango ya uwekezaji yenye masilahi kwa Serikali na wananchi wake.

Alisema uhuru atakaousimamia pia utahusu uhuru wa kujituma na kufanya biashara bila kuwekewa vikwazo, kwani nayo ni haki ya msingi ya wananchi wa Tanzania.

“Uhuru wa kujituma ni muhimu sana kwa kila mtu siyo mtu anataka kuuza njugu wewe unamwambia huna leseni… leseni kwani anataka kuendesha gari? Mtu akitaka kuendesha gari ndiyo mdai leseni, lakini siyo kuuza njugu lazima watu wapewe uhuru wa kujituma,” alisema Balozi Karume.

Balozi alieleza kuwa atasimamia uhuru wa kuepukana na njaa kwa kusimamia uanzishwaji wa viwanda ili kusindika mazao na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuziongezea thamani.

Karume alitumia muda mwingi kuelezea historia ya nchi na CCM akieleza kuwa ni muhimu kwa wanachama hao kuwachagua viongozi wenye uelewa mzuri wa kimataifa na siyo watu ambao wanasindikiza na kutia aibu mbele ya mabalozi wa nchi za nje.

“Hatutaki mtu wa okay, sir au yes sir! Tunataka mgombea urais ambaye anaelewa mambo ya kidiplomasia na anajua kuzungumza na mataifa mbalimbali siyo anakwenda Ulaya anashindwa kuongea badala yake anaitikia tu yes sir,” alisema.

Balozi Karume amewataka wanachama wa CCM kuwachagua viongozi kwa vigezo vya uwezo na uadilifu na siyo kwa sababu wamekaa muda fulani katika matawi na mashina ya chama hicho tawala, huku akielezea jinsi gani wao walivyopikwa katika chama hicho.

Aidha, aliwapiga vijembe wenzake waliotangulia akisema wapo baadhi ya wagombea ambao wametangaza anataka kuunda Tanzania mpya jambo ambalo alisema haliwezekani kwani Tanzania ni hiyohiyo na haiwezi kuwa nyingine.

Alisema watu waliosema hawatakubali kilimo kwanza na badala yake watawekeza kwenye elimu wamekosea, kwani ingawa elimu ni muhimu, kilimo nacho bado ni muhimu pia.

Ilivyokuwa ukumbini

Balozi Karume aliwasili katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati mkoani Unguja saa 9:45 jioni akiwa ameambatana na Zainabu Shamori ambaye amewahi kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba na Kusini Unguja.

Pia, Zainabu amewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar wakati wa uongozi wa Rais Amani Abeid Karume na aliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Baada ya Balozi Karume kuwasili katika ukumbi huo alipokewa na wapambe wake ambao ni wanachama wa CCM na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakiimba na kushangilia kwa kupiga makofi muda wote.

Balozi huyo alipopanda jukwaani, kundi la watu waliokuwapo ukumbini ambao idadi yao haikufika 100, waliendelea kuimba na kushangilia kwa kupiga makofi. Hata hivyo, hapakuwapo na shamrashamra za ngoma.

Licha ya uchache wao, watu hao walionekana wenye furaha na kumshangilia Balozi Karume kwa kila neno alilokuwa akisema hasa pale alipoelezea namna atakavyopambana kuondoka rushwa na ufisadi unaoitafuta Serikali na kudhoofisha uchumi.

Huku akiendelea kushangiliwa, Balozi Karume alisema kwamba Rais mstaafu Karume, ambaye ni kaka yake, alisema kuwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu ni vizuri apatikane rais mwenye uzoefu wa kimataifa.

“Rais alisema ni vizuri apatikane rais ambaye atakuwa ametembea nchi mbalimbali ili ajue uzoefu wa mataifa mengine yanayofanya kazi,” alisema Balozi Karume.

Balozi huyo aliongeza kuwa uzoefu wa kimataifa ni sifa muhimu kutokana na kasi ya maendeleo ya kiuchumi inayoendelea duniani hivi sasa.

Katika mkutano huo wa Balozi Karume, hakuna viongozi maarufu waliopo madarakani au wastaafu waliomsindikiza kama ambavyo imekuwa kwa baadhi ya wanasiasa wanaotangaza nia ya kuwania nafasi ya kuteuliwa na vyama vyao kugombea urais.

Siyo mara ya kwanza

Balozi Karume aliwahi kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2000, lakini alijitoa katika hatua za awali na kumwachia Rais Karume, pia mwaka 2005 na mwaka 2010, aligombea urais wa Tanzania Bara.

Wakati akiondoka ukumbini baada ya kutangaza nia jana, Balozi Karume alitumia muda mwingi kusalimia wanachama waliokuwapo ukumbini kwa kuwapa mikono.


Charles Makongoro Nyerere atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania 2015


Mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Charles Makongoro, ametangaza nia ya kuwania urais, akisema anaomba kibali kuisaidia CCM iache rushwa, kuparaganyika na atakapoingia madarakani, ili asiwaangushe Watanzania, anahitaji chama imara kisicho na shaka kama ilivyo sasa.

Akitangaza nia hiyo nyumbani kwao Mwitongo, Butiama jana, Makongoro alisema kutokana na CCM “kubakwa na vibaka,” inawavunja moyo wanachama na inawakatisha tamaa Watanzania, hivyo inahitaji kiongozi anayewarudishia matumaini.
“Sisi ndiyo wazalendo tunasema mnapotaka kutupora hiki chama sisi tupo, turudishieni na mnapoturudishia kipitishie kwa Makongoro Nyerere mna uhakika chama hiki hakipotei siyo kumkabidhi kibaka,” 
alisema Makongoro.

Kabla ya kutangaza nia hiyo alisema, “nitangaze nisitangaze?, Nitangaze nisitangaze,” akajibiwa na watu waliohudhuria hafla hiyo ‘tangazaaa...’.

Makongoro aliyesema Sh1 milioni za kuchukulia fomu anazo hivyo haitaji kuchangiwa, alikataa kusoma hotuba iliyoandaliwa kwa ajili ya kutaja vipaumbele vyake atakapoingia madarakani na kuwashangaa wenzake waliotangaza nia kwa kutaja vipaumbele, kuwa wanafanya faulo kwa sababu ilani ya chama haijatoka.

Alisema wametangaziwa na chama kuwa ilani itakuwa tayari Julai na kwamba hawezi kutoa kipaumbele vyake halafu baadaye vitofautiane na vitakavyobainishwa na chama ili asije kulaumiwa.
“Nipo hapa kukiri kwamba sehemu kubwa ya tatizo la CCM ni kutofuata utaratibu, ukiona kuna kazi inaombwa kwa kufuata utaratibu na wanaoomba hawafuati utaratibu hawa washtukie mapema, hawafai,”
“Ukiona mtu anayeomba kazi na hafuati utaratibu huo ilhali akiujua, ujue siku ukimpa kazi biashara ya kwanza akifika pale ni kufuta utaratibu huo na kuweka wa kwake ili akae mpaka awe mfalme wa nchi hii, usimpe!”
alisema Makongoro.

Makongoro alisema kibaya zaidi viongozi wa CCM ambao wameshiriki kuweka utaratibu huo ndiyo wanahusika na kwamba, ingawa kikao chake hakikuwa cha kuwataja kwa majina walioshiriki kuvunja utaratibu huo lakini hana jinsi lazima awataje.

Aliwataja baadhi ya wagombea waliokwishatangaza nia ndani ya chama hicho akisema wamekiuka utaratibu kwa kutoa ahadi wakati ilani ya chama hao haijapitishwa na mkutano mkuu.
“Wewe (anamtaja mgombea) ni mjumbe wa NEC umeshiriki na unajua kuwa rasimu ya ilani itapitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM, wewe unatangulia kimbelembele, nakuuliza wewe nani?”

Makongoro alimpiga kijembe mgombea mwingine akisema hana wasiwasi na uadilifu wala uwezo wa kiongozi huyo lakini hazingatii msamiati wa kung’atuka kwa kuwa amekuwapo ndani ya Serikali kwa muda mrefu.

Kijembe kwa Rais Kikwete

Kuhusu mtifuano miongoni mwa wanaCCM na tuhuma za ufisadi dhidi a viongozi wa chama na Serikali, Makongoro alisema yote hayo yanatokana na kosa la Rais Kikwete kuwapenda isivyo kifani marafiki zake ambao huishia kumvunjia heshima.
“Kosa la Rais Kikwete ni kuwapenda sana marafiki zake. Kwa bahati mbaya baadhi ya marafiki zake hao ni vibaka. Kibaka ni kibaka tu hata akipewa gari la Serikali na kupeperusha bendera ya Tanzania, bado ataendelea kuwa kibaka tu,” 
alisema Makongoro bila kutaja majina.

Alisema haoni haya kukiri kuwa wamo vibaka ndani ya CCM kwa sababu hata vyama vya upinzani navyo vina vibaka wao.
“Ni kujidanganya kusema hakuna vibaka ndani ya CCM wakati wapo na wanatumia fedha zao, nyingine walizopata kwa wizi kukivuruga chama,” 
alisisitiza Makongoro.

Kuhamia upinzani 1995

Akizungumzia uamuzi wake wa kuhamia upinzani mwaka 1995 alikogombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini na kushinda kupitia Chama cha NCCR – Mageuzi, Makongoro alisema mizengwe, rushwa na chama kugeuzwa kuwa cha matajiri na wenye fedha ndicho kilichomkimbiza na alipata baraka zote kutoka kwa baba yake Mwalimu Nyerere.
“Watu wataanza kusema kuhusu mimi kuhamia upinzani na baadhi eti wanadai nina laana ya kukihama chama alichoasisi baba yangu. Hivi kweli mie naonekana kama mtu mwenye laana? Hivi naonekana kama mtu mlevi mimi?”
“Mizengwe kwenye kura za maoni ndani ya CCM na matumizi ya fedha kununua uongozi ndivyo vilinifanya kuhamia upinzani baada ya wazee waadilifu ndani ya CCM kunishauri nihame ili wanipe fursa ya kutumikia wananchi wa Arusha kupitia nafasi ya ubunge,”
 alisema Makongoro.

Alisema baada ya kutangaza nia kugombea ubunge wa Arusha Mjini mwaka 1995, huku akitiwa moyo na wazee na wanachama wengi, alijikuta akikimbiwa na viongozi wote wa chama kila alipofanya ziara ya kujinadi katika kata zote 17 za jimbo hilo wakati huo.
“Walionishauri kutoka CCM kwenda NCCR-Mageuzi ni wazee na waasisi wa CCM. Kabla ya kuhamia upinzani, nilimwarifu Mwalimu Nyerere na kupata baraka zake zote,” 
alisisitiza Makongoro.

Alisema ingawa alipanga kuhamia upinzani bila kumweleza Mwalimu Nyerere, mke wake, Jaji Aisha Nyerere ndiye aliyeshurutisha kupata kwanza baraka za mwasisi huyo wa Taifa ikabidi yeye na mkewe wafunge safari hadi Dodoma kumtaarifu Mwalimu Nyerere uamuzi huo huku akiwa na hofu ya kutopokewa wazo lake, ingawa matokeo yalikuwa kinyume na hofu yake.
“Nilihama CCM kwenda upinzani siyo kwa kupenda, bali nililazimishwa,” 
alisema.

Maradhi ya CCM

Alisema:
“CCM kinaugua maradhi ya kukaa madarakani kwa muda mrefu na dalili za maradhi hayo ni kuteua wagombea bila kujali matakwa ya wananchi.”

Alitaja dalili nyingine kuwa ni viongozi wa CCM kuzungumza maneno yasiyolingana na matendo yao.
“CCM iongoze kwa matendo badala ya maneno. Chama kinanuka rushwa. Taifa linanuka rushwa. CCM ichukue hatua na kutokomeza rushwa na ufisadi unaotishia kuangamiza taifa letu.
“Nikipata ruhusa ya chama changu na kibali cha wananchi, nitaanza safari ya kuwaambia vibaka turudishieni chama chetu. CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi, waturudishie chama chetu.”

Kununua nyumba Ulaya, Dubai

“Wapo waliotangaza nia ambao wanajinasibu kununua nyuma Dubai na sehemu kadhaa huko Ulaya na kwingineko. Wasijidanganye kwa sababu wakiharibu huku na kukimbilia huko watambue watakuwa wakimbizi tu. Hapa ndipo petu sote,” 
alisema.

Alisema hata utajiri wanatuambia hivi sasa wameupata wakiwa ndani ya CCM kwa sababu baadhi yao walikuwa maskini walipojiunga na utumishi wa chama cha Serikali.
“Fedha zote, nyingine halali na nyingine haramu wamezipata ndani ya CCM. Sasa hawa waliotajirika kwa kuwamo ndani ya CCM wanataka kukipore chama hiki kutoka mikononi mwa wananchi walio wengi. Haiwezekani waturejeshee chama chetu,” 
alisema Makongoro.

Makundi ndani ya CCM

Akizungumzia makundi ndani ya CCM, hasa nyakati za uchaguzi, Makongoro alisema anayachukia makundi ya siku hizi kwa sababu yanakivunja chama kutokana na wahusika kutoyavunja uchaguzi unapomalizika.
“CCM hivi sasa ina makundi. Kila mgombea ana timu yake na msingi mkuu wa timu hizi ni fedha na wanaojiunga nayo wanafuata fedha. Leo hii nikiwa na hela hata walioko kwa wagombea wengine wananifuata.
“Binafsi sina kundi na ninayachukia sana haya makundi kwa sababu yanakivuruga chama chetu. Wenye fedha wageuka wafugaji wa watu badala ya mifugo. Yaani wenye fedha siku hizi wanamiliki watu wakiwamo wajumbe wa halmashauri kuu. Haiwezekani,”
 alisema Makongoro

Mkono yuko na Makongoro

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye alisema watia nia waliokuwa wanamfuata ili awaunge mkono kuanzia sasa “bye bye”, watambue yupo na Makongoro Nyerere.

Mkono alisema wapo wengi waliokuwa wakitaka kujua aliopo kati ya watia nia ya urais,
“Mmesikia mengi, Simba wa Butiama amekohoa hakuna mwingine. Makongoro ndiye aliyenifanya mimi kuwa mbunge, amenitembeza kijiji kwa kijiji mngenishangaa kusikia niko kundi jingine,”
“Nitajitolea kwa hali na mali, nitamtembeza Makongoro nchi nzima, wale waliokuja kwangu bye bye niko kwa Makongoro.”

Alisema Makongoro ni miongoni mwa vijana waliolelewa katika maadili ya itikadi za uongozi na pia ametoka katika jiko la viongozi wa ngazi kubwa tangu ukoloni.

Mkono alisema Makongoro akiongoza nchi, kuna uhakika wa kuwa katika mstari mmoja mnyoofu kwani hana hofu yoyote kwa Watanzania katika kuendesha gurudumu la maendeleo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Samwel Kiboye alisema Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuadhimisha sikukuu haitoshi, bali wafanye hivyo kwa kumkabidhi kijana wake Makongoro fimbo ya kuwaongoza.
“Tukimkabidhi kijana wa Baba wa Taifa viatu vya baba yake tutakuwa tumemuenzi kiuhakika Baba wa Taifa hili, kwanza kijana huyu ni mwadilifu na pia ni kiongozi shupavu kwani mifano yake tunayo na tulishaionja wakati akiwa mwenyekiti wa mkoa huu,” 
alisema Kiboye.

Kiboye alisema Makongoro ni kati ya viongozi ambao hawana harufu ya ufisadi, ubadhilifu wa aina yoyote wala si mla rushwa hivyo endapo atapewa nafasi ataongoza katika misingi ya kuleta mafanikio na kuondokana na kero zinazochangia kuondoa uzalendo wa nchi.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy – Rose Bhanji alisema anaamini Makongoro ndiye kiongozi anayetakiwa kuvaa viatu vya Baba wa Taifa kulingana na sifa alizonazo katika utendaji wake wa kazi katika nafasi alizowahi kushika na aliyopo hivi sasa ya ubunge wa Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Butiama, Yohana Mirumbe alisema wanachama wa wilaya hiyo kwa pamoja wako tayari kumuunga mkono Makongoro katika kugombea nafasi ya kuwa mgombea wa CCM katika nafasi ya urais.

Mirumbe alisema lengo ni kutaka kiongozi atakayeweza kumalizia kazi itakayoachwa na rais aliyepo madarakani ya kuongoza nchi na kuiweka katika hali ya kusaidia wananchi kuondokana na hali ngumu ya maisha.

Apewa kifimbo

Mwenyekiti wa ukoo wa Burito ambaye pia ni Chifu wa Kabila la Wazanaki, Japhet Wanzagi alisema Makongoro kutangaza nia hakukosea, bali ni historia ya ukoo aliotoka kuwa na karama za kuongoza tangu enzi za ukoloni kabla ya uongozi wa kisiasa.

Chifu Wanzagi alimkabidhi kifimbo Makongoro akitaka Watanzania kumsikiliza na kumwelewa.
“Ukoo huu umekuwa ukitoa viongozi na kuaminiwa na jamii. Makongoro anatoka ukoo wa kichifu, ukoo huu hata siku moja haufanyi kitu kwa kubahatisha au kujaribu,”
“Kama tungekuwa na shaka na Makongoro, tusingekubali asimame, kwa sababu angetushushia heshima kwa jamii, Watanzania, Afrika na Dunia.”
Taarifa kuhusu Prof. Muhongo kutangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania 2015

Leo ni zamu ya Profesa Sospeter Muhongo kutangaza nia ya kuomba kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kurithi mikoba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. 

Profesa Muhongo anatangaza nia yake leo mjini Musoma, kwenye Ukumbi wa Open University Hall, kuanzia saa 10 jioni.

Call to attend DFID Tanzania Supplier Briefing on "Working with DFID"

MMjengwa: Watangaza nia na sanaa ya kuhutubia...

Ndugu zangu,

Kuongea mbele ya hadhara yaweza kuonekana kuwa ni jambo jepesi, lakini, hakika ni kazi ngumu.

Nimefikiri kuandika haya baada ya kufuatilia hotuba za watangaza nia zinazoendelea.

Ninachokiona, ni kuwa wengi tuna hofu ya kutoa hotuba. Kuna ambao, iwe kwenye sherehe ya harusi au hata kipaimara, akiombwa asimame atoe hotuba yumkini atatamani ardhi ipasuke, atumbukie asionekane. Ni hofu ya kuzungumza mbele ya hadhara. Hata mimi huwa na hofu ya kuongea mbele ya hadhara, lakini, nimejitengenezea mbinu za kupambana na hofu hiyo kila ninapotakiwa nisimame kuongea. Utazifahamu kadri utakavyonifuatilia kwenye makala haya, labda nawe kuna utakachojifunza kutoka kwangu.

Lengo langu hasa ni kukupa vidokezo mbalimbali, ushauri na uzoefu mpya kwa wewe ambaye, siku moja, upende usipende, utalazimika usimame uongee mbele ya hadhara; yaweza kuwa ni kwenye harusi ya binti yako au mwanao. Mathalan, wengine hawajui, kuwa baba mkwe hupaswi kutoa hotuba ndefu kwenye harusi ya mwanao. Ongea kwa dakika tano tu, zinatosha. Anayeoa ni mwanao, si wewe baba!

Hivyo, ni imani yangu makala haya yatakusaidia wewe unayejiona ni mzoefu sana kwenye kuongea mbele ya hadhara, na hata wewe unayetaka kuanza kujifunza kuongea mbele ya hadhara. Ufanye nini, kwa maana utumie mbinu gani. Ujiandae vipi, na ni kwa namna gani unaweza kujifunza kwa mifano ya wazungumzaji mahiri hapa duniani mfano wa Barack Obama, Julius Nyerere, Martin Luther King na wengineo.

Sanaa ya kuhutubia au kuongea mbele ya hadhara ni ya kale. Ni tangu enzi za Wayunani miaka 2500 iliyopita. Hata wakati huo, waliosemwa kuwa mahiri wa kuhutubia ni wale walionyesha kuwa na vitu vitatu; Haiba ( ethos), Uelewa ( Logos) na Hisia kwa maana ya uwezo wa kuivaa hotuba na kuamsha hisia ( Pathos). Lengo la mzungumzaji, hata enzi hizo lilikuwa ni kuelimisha,kuamsha mjadala, kuhamasisha, kupandikiza hisia, kuburudisha na hata kupamba kwa maneno. Iliitwa ' decorum' na ndio asili ya neno Decoration- Mapambo.

Hata wakati huo, kulikuwa na watu ambao kazi yao ilikuwa ni kuandika hotuba. Waliitwa ' Logografer'. Kwa Kigiriki ' Logo' ikiwa na maana ya neno na grafer ni kuandika. Kwamba neno linaandikwa, tena kwa kupambwa! Na bila shaka, ndio hapo wakaja wengine kazi yao ikawa kupiga picha- Fotografer- Kuandika kwa picha! Si inasemwa, kuwa picha moja maneno yaweza kuwa elfu moja.

Na kwa mwanasiasa kuwa na uwezo wa kuhutubia ni jambo muhimu sana. Siasa ni kuongea, na mwanasiasa huongelei chumbani au sebuleni kwako na familia yako. Unatakiwa utoke uongee hadharani watu wakusikilize na wakupime uwezo wako wa kiuongozi. Huwezi kuchagua siasa na kupuuzia hotuba.

Na kwenye kuongea mbele ya watu mzungumzaji unatakiwa ujue mambo matatu ya msingi; 1. Nini unataka kusema. 2. Tukio linahusu nini. 3. Hadhira yako ni ya watu wa aina gani.

Kwa kufuatilia hotuba za Watangaza Nia zinazoendelea kuna yaliyo mazuri na mapungufu ambayo nimeyaona kutoka kwa waliozungumza hadi sasa. Nitakuwa nikichambua haya kwa kutolea mifano ya niliyoyaona na kuyasikia hadi sasa.

Sitapenda kutaja majina ya wanasiasa wakati nikitoa mifano.
Nitakuwa tayari pia kutoa ushauri wa bure kwa yeyote yule anayetaka kuchota uzoefu mdogo kwenye eneo hili la sanaa ya mawasiliano; awe ni mwanasiasa wa chama tawala, upinzani au hata raia wa kawaida anayetaka kupata mbinu za kuhutubia zimsaidie kwenye eneo lake la kazi, au hata anapojiandaa kutoa hotuba kwenye harusi ya bintinye au mwanawe!

Nitumie ujumbe mwenyekiti wako...

0754 678 252

Maggid,
Iringa.