Taarifa ya habari Channel TEN ya Juni 5, 2015
Job opportunity: Native Swahili Language Analyst

Job title: “Native Swahili Language Analyst” 

Applicant must be a Native Speaker, U.S. Citizen, Possess TOP SECRET Clearance with Polygraph. 

Job location: Maryland, USA. 

If you have all those qualifications, please contact me at [email protected]

Wanafunzi 6 na Padre wafariki ajalini Ruvuma wakitoka shambani


Kitabu cha Prof. Mbele kutafsiriwa kwa Kisomali?


Kitabu cha Prof. Mbele ambacho nilibahatika kupata nakala yake (nimepiga picha zinazoonekana hapo juu na chini) kutoka kwake mwenyewe ni moja ya vitabu muhimu sana ambacho ninawashauri watu kukisoma ili kufahamiana na namna ya kuchukuliana katika tofauti za tamaduni, mila, desturi na itikadi zetu. Kitabu hiki japo ni cha wastani kabisa kwa ukubwa katika macho ya msomaji wa vitabu vikubwa na hivyo kuweza kusomwa haraka na yeyote, hata asiye msomaji wa vitabu, kimejaa utajiri wa maarifa. 

Leo katika blogu yake ameandika kuwa huenda kitabu hiki kikatafsiriwa katika lugha tofauti na Kiingereza kutokana na maombi ya wasomaji ila wasemaji wa lugha tofauti. 
Mara kadhaa, wa-Marekani wameniuliza  iwapo kitabu changu Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kimetafsiriwa kwa ki-Swahili au wameniomba nikitafsiri. Hao ni watu ambao wameishi au wanaishi Afrika Mashariki, hasa kwa shughuli za kujitolea.

Tangu nilipoanza kupata maulizo au maombi hayo, nimekuwa na wazo la kukitafsiri kitabu hiki. Mwanzoni kabisa, kwa kuzingatia uwingi wa wa-Somali walioingia na wanaendelea kuingia hapa Minnesota, ambao nimekuwa nikiwasaidia katika kuufahamu utamaduni wa Marekani, niliwazia kumwomba mmoja wa marafiki zangu wa ki-Somali atafsiri kitabu hiki kwa ki-Somali. Ninao marafiki kadhaa wa ki-Somali ambao, sawa na wa-Afrika wengine, wamekisoma na wanakipenda kitabu hiki. Lakini bado sijalitekeleza wazo hilo.

Namtakia Prof. Mbele mafanikio katika kulifanyia kazi wazo hili ili kitabu chake kisambae katika jamii mbalimbali zaidi duniani.


Mwili wa Kamishna Malisa wapumzishwa Moshi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiweka saini katika daftari la rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimpa pole mke wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiweka saini katika daftari la rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri nchini (KKKT), Usharika wa Kinyerezi, Manford Kijalo akiwaongoza askari waliobeba mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati mwili huo ukiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akitoa heshima wakati mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa ulipokuwa unawasili katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, Aloyce Msika akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa jeshi hilo, Onel Malisa wakati mwili huo ukipelekwa ndani ya gari kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Tukio la kuuga mwili huo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

  • Picha: Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele. Mazishi hayo yamefanyika leo Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.


Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Diyosisi ya Kasikazini akiweka akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiweka Shada la Maua kwenye kabuli la Marehemu.


Gadi Maalum ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa katika Gwaride la mazishi yake.


Kabuli la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa limepambwa na mashada ya maua baada ya mazishi.


Umati wa watu waliojitokeza katika mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.


Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiimba wimbo kwenye Ibada Maalum ya kumuombea kheri Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa baada ya shughuli za mazishi kukamilika(kulia) ni Mchungaji Frank Machanga kutoka Jimbo la Kasikazini.

  • Picha zote: Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

Maana ya Ujasusi, Upelelezi, Udukuzi na hatari zake


Mpelelezi ni mtu anayekusanya taarifa za adui, mshindani wa biashara au serikali adui.

Wakati mwingine mpelelezi huyo anaweza kufanya kazi ya kumpeleleza adui ila akamgeuka basi wake aliyemtuma kwa sababu mbalimbali.

Mtu huyu huwa anakusanya taarifa hizi kwa siri kwa kuangalia , kusikiliza , kufuatilia na kutumia vifaa vingine kutokana na ukuaji wa tekinolojia lakini lengo ni lile lile kupata taarifa za siri bila mhusika , wahusika kujua kwamba taarifa zao zinachukuliwa.

Shuguli za upelelezi zimekuwepo kwa miaka mingi toka binadamu ameanza kuishi duniani na kila kipindi zinabadilika utokana na ukuaji wa binadamu kimbinu, vifaa na wahusika wenyewe.

Kutokana na kukua kwa tekinologia watu wengi wametumia tekinologia hizo kukusanya taarifa na kuacha njia za asili ya upelelezi ambazo wakati mwingine ni sahihi kabisa kwa wakati huu .

Ili jamii Fulani isonge mbele kwenye maendeo Fulani ni vizuri iwekeze sana kwenye nyenzo na vitendo vya kipelelezi na hujuma kwa kuwa na watu wazuri kila sehemu pamoja na vifaa.

Labda tujiulize sasa kwanini kuna upelelezi , kwanini watu wanakuwa wapelelezi , mtu anavutiwa kukusanya taarifa za siri za mtu au kampuni au serikali nyingine kwa njia ya siri?

Kwa kweli hakuna maana moja ya kwanini mtu anaamua kuwa mpelelezi au anaamua kusaliti wenzake kwenye upelelezi na kwenda upande wa adui lakini kuna vichocheo vinne vikuu ambavyo vinatumika kwenye shuguli hizi .

Kitu ambacho kinaweza kuwa namba moja ni hela, fedha au uchumi. Kama nchi jirani imeshindwa kabisa kuingiza wapelelezi ndani ya baraza la mawaziri ili kupata taarifa kutumia njia za kawaida basi pesa inaweza kutumika katika kuhonga watu haswa wasaidizi au mawaziri wenyewe hata viongozi wengine ili kupata taarifa wanazozitaka.

Ushindani wa viwanda na biashara kati ya nchi au kampuni unategemeana sana na fedha ambazo hutolewa kwa wapelelezi au wachunguzi wengine ili kupata siri za mshindani wake sokoni au popote.

Katika shuguli za kijeshi zinazofanywa na nchi moja dhidi ya nyingine au vikundi vya kigaidi na vya kihalifu fedha hutumika sana na mfano hao ni tunaposikia kuhusu kundi la Al Shabaab kuhonga baadhi ya polisi wa mipakani ili wavushe silaha na watu kwa ajili ya kufanya mashambulizi au wapewe taarifa mapema wakati polisi wanapofanya msako kwenye maeneo yao .

Kichocheo cha pili ni itikadi ambayo ni msimamo au mtazamo kuhusu masuala fulani ya kimaisha, dini, imani, uongozi na mengine mengi hapa kwenye itikadi ndio makundi mengi ya kigaidi yanachipukia na kupata watu wa kujiunga nao wakifuata mtizamo na misimamo ya imani yao.

Vyama vya siasa navyo vinapata wafuasi wao kutokana na hili la itikadi ingawa wengine wanaweza kuwa sio wasomi wa itakadi wala kuielewa wanafuata mkumbo mpaka wanapoumizwa au kuumiza wengine ndio wanashtuka kitu ambacho wanakuwa wamechelewa.

Kwa hiyo ili uwe mpelelezi mzuri wa kundi la kigaidi lazima uelewe itakadi yao, nchi, vikundi au vyama vya siasa na vikundi vingine vya siri.

Ili serikali na wadau wengine waweze kukabiliana na vikundi vya kigaidi ni vizuri kuwekeza sana kwenye suala la kujua itikadi za vikundi wanavyopambana navyo.

Hapa kwenye itikadi ndipo uzalendo unatakiwa kujengwa kwa vijana, watoto na wengine kwenye taasisi za elimu ili wasiweze kuangukia kwenye mikono ya wahalifu na maadui wengine kutokana na itikadi zao mfano china wana ukomunisti , nchi za magaribi wana itikadi zao na mengine mengi .

Wakati mwingine watu au mtu anaweza kuingia kwenye makubaliano na adui baada ya kukamatwa akifanya upelelezi au hata kabla lakini adui anaweza kuona yeye anafaa akampa mafunzo na mbinu nyingine ili aweze kupelelezi kwa niaba ya adui huyo mwisho wa makubaliano kama haya mara nyingi ni watu kuuwawa na hujuma nyingine nyingi dhidi ya nchi yake au watu wake wa karibu .

Mmoja wa wapelelezi maarufu kwenye suala hili anaitwa Kamanda Zig Zag, yeye alikua mfungwa kwenye gereza la Uingereza kwenye kisiwa fulani, kisiwa hicho kilivyotekwa na Wajerumani yeye akaandika barua kutaka kujiunga na jeshi la Kijerumani baada ya muda alipelekwa Ufaransa kwa mafunzo kisha akatumwa Uingereza ili akalipue kiwanda cha kutengeneza ndege za kivita. Alivyotua Uingereza akatoa taarifa kwa mamlaka za Uingereza, sasa akawa upande wa Uingereza tena akatengeneza mlipuko bandia na kuaminisha Wajerumani kwamba kweli kimelipuliwa kisha Waingereza wakamtuma arudi Ujerumani. Kwa hiyo akawa mpelelezi wa Uingereza ndani ya Ujerumani. Wajerumani walimtuma maeneo mengi Ulaya kwa kudhani anawasaidia kumbe taarifa zote zilikuwa zinaenda kwao Uingereza.
Kuna wakati mtu analazimika kufanya upelelezi dhidi ya mtu au watu baada ya nguvu kutumika au kulazimishwa ili labda asiuwawe au ndugu zake wa karibu asiuwawe mara nyingi wanaweza kutumika wapenzi na wapendwa wengine ili mtu afikie muafaka wa kufanya upelelezi dhidi ya nchi, kampuni, washirika na wengine wa karibu.

Hapa kwenye nguvu wakati mwingine mtu anaweza kusingiziwa kitu au kuingizwa kwenye kashfa au kutengenezwa uwongo ili akubali kufanya upelelezi dhidi ya wengine lakini sio kwa hiari yake .

Pia kuna suala la umuhimu au umaarufu wa mtu au uzuri wake , kuna watu wengi maarufu kama wanamuziki au wacheza mpira na warembo wanatumia fursa hiyo kufanya upelelezi dhidi ya maadui wa nchi zao au washindani wa kibiashara wanajua kwa kutumia njia hiyo wanaweza kuingia chumbani , kulala na wanaume au wanawake , kuchungulia simu au kuweka vinasa Sauti , kujua marafiki au ndugu wa karibu , mipango ya biashara na mengine mengi .

Baadhi ya watu haswa vijana wanajiingiza au wanaweza kuingizwa kwenye shuguli za kipelelezi kwa wao kupenda vile wanavyoona kwenye sinema au kusoma vitabu au kuhadithiwa na wao wanaamua kujihusisha na upelelezi lakini bila kuwa na mafunzo au mtu yoyote anayemuongoza kwenye mambo mbalimbali anayotakiwa kufanya .

Wengine wanaweza kuwa wapelelezi wazuri ndani ya polisi , majeshi na kampuni lakini hawalipwi vizuri au hawaridhiki na baadhi ya vitu matokeo yake ni kuuza siri na mikakati mengine kwa wapinzani au maadui ili kuweza kuleta mabadiliko na mengine ndani ya taasisi yake au kuiua kabisa isiwepo .

Mahusiano binafsi kati ya watu au mtu ni moja ya kichocheo kikubwa cha watu kuweza kufanya upelelezi mara nyingi yanaweza kuwa mahusiano ya kifamilia kuoleana , kuowa au kuolewa hii maarufu inaitwa HONEY TRAP na hii ni ngumu kugundulika kwa sababu ni mambo binafsi sana na yanaweza kuchukua muda mrefu kwenda vizazi na vizazi viongozi na viongozi .

Kama nilivyosema hapo juu upelelezi umeanza siku nyingi na kila jamii inategemea upelelezi ili iweze kujua mwingine ili kuweza kupambana au kushindana nae ili aweze kuwa juu kwenye mambo mbalimbali na upelelezi umebadilika kwa kiasi kikubwa sana .

Ni vizuri taasisi zetu kuwekeza vizuri kwenye upelelezi kupata vijana hodari , wapewe mafunzo ya kutosha, mishahara, motisha, vifaa na kuzidi kuwaongezea ujuzi ili kuweza kupambana katika dunia ya sasa ya sayansi na tekilologia .

Upelelezi usiishie ndani ya jeshi la polisi au JKT, au Usalama wa Taifa tu, hata vyuo vinatakiwa kuwa na wapepelelezi , kampuni za nchini zinatakiwa kuwa na wapepepezi, mashirika ya umma yanatakiwa kuwa na wapelelezi , viwanda vya ndani vinatakiwa kuwa na wapelelezi na wote hawa wanatakiwa kufanya kazi pamoja ili kuleta maendeleo kwa jamii ya watanzania .

Nchi za wenzetu zinaendelea na kuendeleza ushindani mkubwa kwenye nyanja hii, Uchina ilishtuka ikapeleka wapelelezi nchi nyingi ili wakalete tekinolojia na maarifa kwao sasa wako mbali, wakati wa vita kuu ya dunia wamarekani waliiba wanasayansi wengi wa ujerumani ambao walisaidia kujenga uwezo mkubwa wa jeshi la marekani na taasisi nyingine ndio maana ikawa mbabe wa dunia kwa kipindi kirefu .

Kumbuka kazi za upelelezi ni ngumu na zenye siri nyingi na kubwa sana, wapelelezi wengi pia wana mafunzo ya kujilinda , kupambana na kushambulia usijaribu kupambana nae kama una uhakika ni bora kutoa taarifa kwa vyombo husika wamshugulikie.

Mwisho upelelezi usitumike katika kutafuta taarifa mbaya tu, hapana, kuna taarifa nyingine nzuri zinaweza kutumika Vyuoni, Wizarani, kwenye majeshi na sehemu nyingine kwa ajili ya kuboresha au kujenga zana na vifaa vya kisasa.

LENGO LA MAELEZO HAYA NI KUFUNDISHA, UKIKAMATWA KWA KAZI HIZI UNAWEZA KUUWAWA , KUTESWA NA KUPOTEZA MENGI

  • Imeandikwa na kushirikishwa kwetu na Yericko Nyerere.

Mkristo pekee katika baraza la Saddam Hussein, Tareq Aziz afariki


MMOJA wa watu muhimu sana katika utawala wa Saddam Hussein, Tariq Aziz, amefariki dunia akiwa gerezani.

Taarifa za awali zilisema kwamba kiongozi huyo ambaye alikuwa anaonekana ndio sura ya Saddam Hussein na Mkristo pekee katika baraza la mawaziri la Saddam Hussein amekufa kwa ugonjwa wa moyo.

Akiwa na umri wa miaka 79 Aziz, alikuwa ndiye waziri wa mambo ya nchi za nje na Naibu waziri Mkuu.

Aidha alikuwa mshauri wa karibu wa kiongozi huyo wa Iraq.

Kiongozi huyo ambaye alijisalimisha kwa Wamarekani mwaka 2003 na baadaye Mahakama Kuu kumhukumu adhabu ya kifo, hakuwa amenyongwa kwa miaka yote hii.

Kiongozi mmoja alisema kwamba baada ya kukumbwa na ugonjwa wa moyo alikimbizwa hospitalini ambako alifia, lakini taarifa za awali zinasema kwamba alikufa akiwa bado gerezani.

Familia ya Kiongozi huyo ambaye alikuwa na afya mbaya kwa muda mrefu akisumbuliwa na kisukari shinikizo la damu, matatizo ya kupumua, walitaka aachiwe lakini hakuna mtu aliyewasikliza.

  • via Lukwangule Ent. blog

Mteja kuiburuza Vodacom mahakamani kwa kutomlipa milioni 100/- za promosheni

Mshindi wa mchezo wa kubahatisha wa Jay Millions, Danny Paul Njau (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu ya Vodacom kushindwa kumpa zawadi yake ya sh.milioni 100 baada ya kushinda mchezo huo. Kushoto ni mtoto wake, Erick Danny Njau.

Habari na Dotto Mwaibale — MSHINDI wa mchezo wa kubahatisha wa Vodacom Jay Millions Danny Paul Njau kupitia jina la Innocent Daniel Njau ametishia kwenda Mahakama kuishitaki kampuni ya simu ya Vodacom kwa kushindwa kumpa zawadi yake ya ushindi sh.milioni 100 baada ya kushinda mchezo wa kubahatisha wa Vodacom Jay Millions.

Njau ametoa siku saba kwa kampuni hiyo kuhakikisha inampatia fedha hizo vinginevyo atakwenda mahakama kutafuta haki yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Njau alisema amesikitishwa na danadana anazopigwa na kmapuni hiyo kushindwa kumpatia kitita chake hicho baada ya kushinda.

"Tayari nimetoa malalamiko yangu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kuhusu suala hilo lakini mpaka hivi sasa bado hajafanikiwa" alisema Njau.

Njau alisema kwamba tangu kampuni hiyo ianze kucheza mchezo huo alikuwa akishiriki kucheza kila siku na ilipofika Januari 14, 2015 saa 5:8 asubuhi kupitia simu yake alipokea ujumbe sms iliyosomeka hivi 'hongera wewe ni mshindi wa leo wa Tzs Miliioni 100 utapigiwa simu na wafanyakazi wa Vodacom. Kwa maelezo zaidi ndani ya masaa 48 ambapo alisubiri bila ya kupigiwa simu kama alivyoelekezwa.

Alisema Januari 20, 2015 alienda ofisi za vodacom na kuwaelezea kuhusu jambo hilo ambapo aliambiwa awape muda na aliporudi Januari 22 alikutanishwa na maofisa wa Jay Millions na kufanyanao kikao akiwepo mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ambapo aliambiwa kuwa eti sms hiyo ni ya kwao lakini ilitoka mapema kwenda kwake.

Njau alisema kwamba kauli hiyo ilimshangaza sana ukizingatia kuwa katika kipindi hicho cha mchezo kulikuwa na matangazo yaliyokuwa yakisema kila siku kutakuwa na mshindi mmoja wa sh.100, washindi 10 milioni 10 na washindi 100 wa sh.milioni 1 na kuwa yeye alifuata taratibu zote za kucheza mchezo huo Jay kwenda 15544 na kuona sms ya ushindi.

Alisema baada ya majadiliano na maofisa hao walimuuliza wampe sh. ngapi kwa kuwa zawadi hiyo imetoka mapema na kabla ya watu hawacheza na kuwa wao hawana pesa nyingi anayoifikiria.

Alisema hakuamini kilichokuwa kikifanywa na kampuni hiyo katika uchezeshaji wa mchezo huo na kuwa aliomba apewe muda wa kutafakari ambapo aliamua kupeleka malalamiko yake kwenye bodi ya michezo ya kubahatisha na kwenye vyombo vya habari.

Jitihada za mtandao huu kumpata mmoja wa maofisa wa Vodacom Tanzania ambaye alitajwa kuwa ni Meneja, Kelvin Twisa ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kupigwa zaidi ya mara nne bila ya kupokelewa, pia hali kama hiyo ilitokea kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas Tarimba ambaye simu yake ilikuwa imefungwa jitihada hizo zinaendelea ilikutoa fursa kwa maofisa hao kutoa ufafanuzi ili umma wa watanzania upate kujua kinachoendelea katika kampuni hiyo.

Taarifa hii imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

Agizo la TFF kuhusiana na mgogoro wa Singano na Simba

TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba.

TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.

Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.

Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Barua ya NCCR-Mageuzi ikijibu barua ya Deo Meck na mengineyo

NANJING UNIVERSITY
S.L.P1042
NANJING-JIANGSU
CHINA

3 JUNE 2015

KUMB: NCCR-M/KVT/07/15
KATIBU MKUU
NCCR-MAGEUZI
S.L.P 72474
DAR ES SALAAM

YAH: KUJIUZURU NAFASI YANGU NA KUJIVUA UANACHAMA WA NCCR-MAGEUZI


Napenda kukutaarifu kuwa nimetafakari kwa kina juu ya utofauti wa msimamo na utendaji kati yangu na Mwenyekiti wa Chama Taifa na kuona kuwa siwezi endelea kufanya kazi nae kwa sababu mbalimbali, hali hii inatokana na tofauti yetu kimtazamo juu ya uendeshaji wa Chama.
  1. Chama sio mali ya Mwenyekiti na familia yake, Chama ni mali ya wanachama wote kwa pamoja. Itakumbukwa kuwa toka mwaka 2010 Mwenyekiti wa Chama Taifa amekuwa akitenga kiasi cha shilingi milioni saba (7,000,000/= Tshs) kwa ajili ya kuhamasisha Chama na kuzichukua pesa hizo, na hakuna ziara alizofanya za kuhamasisha Chama na hakuna mrejesho aliowahi kuufanya kuhusu matumizi ya pesa hizo. Na hili unalifahamu na mara kadhaa tumetaka uhamasishaji ufanyike lakini kwa kuwa pesa za uhamasishaji kazikumbatia Mwenyekiti imekuwa ngumu kwa viongozi wengine kupata rasilimali za kuhamasisha chama, na hata tulipoomba ili kufanya ziara kuhamasisha chama bado hatukuweza kupata uwezesho.
  2. Kwa hali hiyo hali ya chama kwa ujumla imezorota sana, Mwenyekiti Taifa amekuwa Mwenyekiti wa Vunjo peke yake na chama kimelala sehemu kubwa ya nchi, hali hiyo inatupa wakati mgumu viongozi wengine na wanachama kwani inaonekana kuwa sote hatufanyi kazi ya kujenga chama.
  3. Kwa rasilimali za Chama Mwenyekiti ameshindwa kujenga chama, pia ndani ya UKAWA ameendeleza ubinafsi wake wa kuhakikisha anapata jimbo la Vunjo hata kwa gharama ya kukiangamiza chama. Ameshindwa kukitetea chama na hadi sasa wajumbe wa Chama katika kamati ya Ufundi ya UKAWA waeondolewa kwa sababu ya misimamo ya kutetea Chama na kabaki mwenyewe.
  4. Hili kama nilivyoongea kwenye kikao miaka ya nyuma, pia naliweka hapa kwa rekodi, kwamba tulipinga hila za Mwenyekiti za kuiga mambo ya kufanya taasisi ya Chama kama mali ya familia kama wanavyofanya katika vyama vingine, Mwenyekiti alihakikisha anatumia mbinu na hila ili Dada yake Mh. Nderakindo Kessy awe mbunge wa Afrika Mashariki, na kweli akawa, zaidi ya kufaidi marupurupu ya huo ubunge hatuoni mchango wake katika ujenzi wa Chama. Ni mbaya kufanya vyama vya siasa vitega uchumi vya kifamilia.

Hivyo nimeamua kujivua rasmi na kukoma kuwa Mwenyekiti wa Kitengo Cha Vijana Taifa kuanzia leo 3 June 2014, na pia kujivua uanachama wa NCCR-Mageuzi.

Pamoja na kasoro hizo, naondoka na yale mazuri niliyojifunza na nitayaendeleza mazuri hayo kwa ajili ya nchi yangu na kokote nitakapoamua kufanyia siasa zangu hapo baadae.

Pamoja na salaam,

Deo Meck
Email: [email protected]


Ushauri wa Wabunge kwa wazazi kuhusu watoto wanaopelekwa 'boarding school'


Taarifa ya habari Channel TEN ya Juni 4, 2015
Utabiri wa hali ya hewa Tanzania 06.06.2015 kutoka TMA