Mmiliki ailaumu DAWASA kuvunja jengo lake Mbezi-Makonde


Mmiliki wa jengo moja lilipo Mbezi Makonde Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ameilalamikia mamlaka ya maji safi na taka Dar es salaam - DAWASA kwa kuvunja nyumba yake ya biashara bila taarifa wala malipo.

Mmiliki yuyo, Zureha Salim amedai kuwa miaka miwili iliyopita DAWASA walihitaji eneo la mbele ya nyumba hiyo kwa ajili ya kupitisha bomba kubwa la maji hatua ambayo hawakukubaliana nayo na kufungua kesi mahakamani na kusimamisha uvunjaji wa jengo hilo hadi pale uamuzi utakapotoka.

Katika hali ya kushangaza majira ya saa 12 jana jioni walifika askari pamoja na watendaji kutoka DAWASA na kuwatoa na kuanza kuvunja jengo hilo huku wao wakidai kuwa kesi yao ilitakiwa kusikilizwa mwezi julai.

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 7, 2015
Taarifa ya habari Channel TEN ya Jumamosi, 06.06.2015Kima cha chini kwa wafanyakazi majumbani 100,000/=


SERIKALI imesema kuwa, wafanyakazi wote wa majumbani wanatakiwa kulipwa mshahara wa kima cha chini kwa mujibu wa mkataba.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohammed (CUF).

Mbunge huyo aliihoji serikali na kutaka itoe kauli kuwa, ni kiasi gani cha mishahara ambacho wanatakiwa kulipwa wafanyakazi wa majumbani licha ya wafanyakazi hao kunyanyaswa na waajiri wao.
“Najua kila mmoja hapa ana mfanyakazi wa nadani lakini wafanyakazi hao wamekuwa wakinyanyaswa na wakati mwingine kulipwa mishahara kidogo.
“Sasa naitaka serikali ieleze, wafanyakazi hao wanatakiwa kulipwa kiwango gani cha mshahara kwa mwezi,” 
amehoji Mbarouk.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Kuruthum Mchuchuli (CUF) alitaka kujua serikali itapeleka lini mkataba Na 189 bungeni unaohusu kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani ili uridhiwe na Bunge.

Akijibu maswali hayo Makongoro amesema, wafanayakazi wote wa ndani wanatakiwa kulipwa mshahara wa Sh. 100,000 kwa mwezi kama kiwango cha chini cha mshahara.

Makongoro amesema, wafanyakazi wa ndani wanatakiwa kutoa taarifa pale ambapo wanakuwa wanaonewa au kunyanyaswa.

Amesema, pamoja na mchakato huo wa kuridhia mkataba Na 189 unawahusisha wafanyakazi wa majumbani 
“wafanyakazi hawa kama walivyo wafanyakazi wengine, wote wanaendelea kulindwa na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na 6 ya mwaka 2004.”

Call for Applications: 2015/6 PhD Scholarships at HEARD/UKZN

Under the supervision of Professor Nana Poku and with the generous support of SIDA/ NORAD, HEARD is offering up to four fulltime PhD Research Scholarships in any of the following key areas of strategic focus Sexual and Reproductive Health; Health Systems Strengthening and Economics of Critical Enablers in HIV Programming.

Award of the HEARD PhD Research Scholarship is conditional on candidates meeting the requirements for PhD registration at the University of KwaZulu-Natal, and on participating in a compulsory training component during the first year of study. The training component will be conducted over four two-week blocks during the first year of study. Candidates will produce a thesis related to one of HEARDs priority research nodes, as detailed above. The Scholarship programme emphasizes the mastery of quantitative and qualitative methods for understanding policy problems and for devising, evaluating and/or implementing policy solutions.

The intention of providing PhD scholarships is to produce expertly qualified graduates to advise or to be part of influential policy making organisations in Africa. During their PhD, students will be strongly encouraged to present their work at international meetings.

The value of each scholarship is R270, 000 and will be paid in tranches over three years. Tranche payments will be conditional on research progress. Successful candidates will be based in Durban, South Africa, for the duration of the scholarship, with the exception of the time during which they may undertake field research elsewhere.

Applications are invited from citizens of all African countries. Female candidates and, in the case of South Africa, those from previously disadvantaged backgrounds, are especially encouraged to apply.

Click here for more information.

Zambian High Commissioner instructs Tanzania's Police to detain diplomat over "Personal Differences"?

Zambia's High Commissioner to Tanzania has allegedly instructed a Tanzanian diplomats to detain a fellow diplomat she had personal differences with and not allow him access to his family. Yosi Miti, first secretary to Tanzania, has since spent the last four nights in the holding cell of Julius Nyerere International Airport after that country's immigration authorities detained him on instruction from the Zambian mission.

Miti, who was until his recall, the first secretary for trade at the Zambian High Commission in Tanzania, was detained around 01:00 hours on Tuesday upon his arrival from Zambia.

Miti had travelled to Tanzania to see his 72-year-old hypertensive mother who is still living with the rest of his family at his official residence in Dar-es-salaam.

When contacted, the Minister of Foreign Affairs, Harry Kalaba, said the matter was being sorted out.

Tanzanian immigration officials disclosed to local media that Mr. Miti was being detained at the airport because of instructions from the Zambian mission not to allow him entry into that country.
The officer said an attempt was made to have him released on Wednesday but officials from the Zambian High Commission's office insisted that he be detained.
"We are working on instructions; it's your government who wants him detained. Actually we have no interest in this matter. We are shocked that your country can treat diplomats in the manner you are doing. It is shameful,"
"There was an instruction not to allow him entry into Tanzania and we detained him here at the airport holding cells. 
said the official.

And around 07:00hrs in the morning we asked him to have a chat with the high commission officials who informed him that there was an instruction not to allow him entry because he was no longer a diplomat accredited to Tanzania. 
With us here we are just following instructions,"
 said the official.

When asked where the instructions were coming from, the immigration official said the instructions were given by High Commissioner Judith Kapijimpanga in her letter to the Immigration Office not to allow Mr. Miti entry into that country.

The officials said they were still waiting for fresh instructions before taking action on whether he could remain in detention or have him deported back to Zambia.
"Please we have not allowed him entry into the country because we have specific instructions from Zambia not to allow him into Tanzania. He has been with us for the past four days. Actually since Monday in the night he has been with us here at the Julius Nyerere International Airport," 
said an immigration official.

Ministry of Foreign Affairs officials could not comment on the matter saying instructions have been given to the permanent secretary in the ministry to deal with it.


Kagera wamzomea Kinana, yeye kasema wamepewa elfu 10, 10 waacheniNi katikati ya hotuba yake katika mkutano wakati akielezea kuhusu ilikofikia Serikali katika kushughulikia suala la meli iliyoharibika na ahadi ya meli mpya.

[video] Wimbo wa Rose Mhando, Upendo Nkone, Mwaitege, Mwaipaja 'wakimuuza' Mwigulu Nchemba

MMjengwa: Unapokwenda kuhutubia, fikiri Kkhusu sauti yako

Ndugu zangu,

Mada hii kuhusu sanaa ya kuhutubia, ama kujieleza mbele ya watu inazidi kupata wafuatiliaji zaidi. Nami, naingiwa na ari zaidi ya kuliandikia jambo hili, hususan pale ninapopokea simu kutoka kwa Mtanzania anayefikiria kuwania Udiwani na ananiomba nimshauri juu hili la sanaa ya mawasiliano.

Leo tujikite kwenye eneo la sauti. Wagiriki wa kale waliita ' Prosodi'. Duniani hapa kuna sauti nyingi kama ilivyo wingi wa wanadamu. Sauti zina midundo yake. Kuna sauti nene, nyembamba, nzito, na hata ya mikwaruzo. Mzungumzaji ni vema ukajijua una sauti ya namna gani.

Wengi hupuuzia umuhimu wa sauti unapoongea mbele ya hadhara. Katika hili, Rais aliye madarakani, Jakaya Kikwete yuko makini sana. Anaelewa umuhimu wa sauti.

Kuna mtu ameniambia, kuwa JK husisitiza sana uwepo wa vifaa vya kutoa sauti vitakavyomfanya asikike vema.

Sauti ni muhimu sana kwenye hotuba. Mzungumzaji anaweza kupangilia hoja zake vema lakini akaangushwa na sauti, ama kutoka vifaa vya kupazia sauti vilivyopo, au yeye mwenyewe kutokuwa makini juu ya namna ya kutumia vema sauti yake.

Sauti hufanyiwa mazoezi pia. Unaweza kwenda bustanini au kando ya bahari na kuifanyia mazoezi sauti yako. Usimame tu na kuongea kwa sauti kama vile unaongea na watu wengi. Fanya mazoezi kujua wapi unaweka vituo. Kasi ya sauti yako na mengineyo. Mazoezi si ya mpira tu, hata sauti kwenye hotuba. Kuna misuli ya koo yenye kuhitaji mazoezi. Na mapafu pia. Usipoyafanyia mazoezi ndipo hutokea mzungumzaji akaonekana kuishiwa hata pumzi za kuongea. Hotuba nayo huathiriwa.

Mzungumzaji sharti ajue, kuwa ni sauti gani atumie kulingana na anachokiongea. Kuna mahali kwenye hotuba unatakiwa uweke sauti ya msisitizo. Kuna mahali iwe nzito kidogo. Kuna mahali iwe ya unyenyekevu, kwa maana laini kidogo. Kuna mahali unatakiwa kuongea kwa sauti ya huzuni.

Huwezi kupewa kipaza sauti utangaze tukio la msiba ukaanza na kutamka kwa sauti; : Jamani ee, jamaa yetu ndio keshakufa tena, sasa tujipange kwa taratibu za mazishi!" Hivyo sivyo wanavyotarajia kusikia waombolezaji.

Hapa Julius Nyerere ni mfano mzuri wa kutumia sauti husika kwa tukio husika. Alasiri ile ya Aprili 12, 1984, siku shujaa wa Watanzania, Edward Sokoine alipofariki kwa ajali ya gari, mimi nilikuwa natembea kwa miguu nikitoka shuleni Tambaza Sekondari. Pale maeneo ya Kinondoni ' A' nikasikia wimbo wa taifa ukipigwa. Enzi hizo ukisikia wimbo wa taifa unapigwa redioni mchana ni lazima ufuatile kujua kuna nini. Nikasogea kwenye redio kwenye moja ya maduka.

Wimbo wa taifa ulipomaliza ikasikika sauti ya Julius Nyerere, Rais wa Nchi. Kutoka sekunde ya kwanza aliongea kwa sauti ya pole pole na iliyochanganyika na huzuni.Tuliomsikiliza tukafahamu Rais ana habari mbaya kwa Taifa. Nakumbuka alianza kwa kutamka..:

"Ndugu zangu Watanzania, leo kunako majira ya saa..." Kilichofuatia ni sehemu ya historia yetu.

Huu ni mfano wa kutumia sauti muafaka kwa tukio husika.

Ni muhimu saa pia, kuwa unapokuwa jukwaani, sauti iendane na lugha ya mwili. Unapozungumza jambo la huzuni, basi na sura nayo ionekane hivyo, hupaswi kuonyesha sura ya kuchangamka. Au kuweka mikono mfukoni ( Kama mwenyekiti wenu hapo pichani). Hupaswi wala kurusharusha mikono. Hapo ni mahali hata pa kukunja mikono yako kifuani.

Mada hii ni endelevu..

Kwa ushauri wa bure, namba yako hiyo chini..
0754 678 252

Maggid

[picha] CHADEMA Arusha, CCM Kagera


Profesor Jay akihamsisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIO MATUMAINI"


Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amewataka watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa Miaka Mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura"Pia ametambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake


Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akitambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake


Umati wa wananchi waliouthuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha


Mjumbe wa Kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum Mh Grace Kiwelu amewataka Wanawake kuwa Chachu ya mabadiliko kwa Taifa letu."MUDA WA KUDANGANYWA KWA KANGA UMEPITA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI OCTOBER TUPATE UHURU WA UHAKIKA,WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZA"
Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ambaye pia ndiye aliyeteuliwa na Chadema Kanda Ya Kaskazini kuwa kiongozi wa kampeni za Hamasa ya kujiandikisha kanda ya kaskazini amewaambia wananchi wa Arusha kuwa safari ndio imeanza sasa kuelekea majimbo yote 33 ya kanda ya kaskazini kuhakikisha Watanzania wanajiandikisha kwa wingi ili October tufanye maamuzi sahihiMbunge wa Rombo Joseph Selasini" WATANZANIA WENZANGU HUU NDIO MUDA MUAFAKA WA KILA MMOJA WETU KUJIANDIKISHA ILI IKIFIKA OCTOBER TUWE TUNAFANYA MAAMUZI YA UHAKIKA NA SIO SAFARI YA MATUMAINI"Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mh Pauline Gekul awatakwa Watanzania kujiandikisha na kuhamasishana kwa wingi wetu kwa kutumia simu mitandao ya kijamii vikao vya kijamii ili ifikapo October tuiondoe CCM madarakani.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Cecilia Daniel Paresso amewataka Vijana na Akina Mama kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili ikifika October waweze kufanta maamuzi ya UHAKIKA na sio ya maamuzi ya MATUMAINI


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Rebecca Mgodo amewataka wananchi kusoma nyakati"NDUGU ZANGU MIAKA YA MATESO KWA WATANZANIA SASAS IMEFIKA MWISHO, TWENDENI KWA UMOJA WETU TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURATUITOE CCM MADARAKANI"-Mgodo


Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda Ya Kaskazini Mh Israel Natse akiwaongoza viongozi na Wabunge wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuingia uwanjani huku wakiwapungia wanachama na wapenzi wa CHADEMA waliofika uwanjani vya kilombero 

  • Picha: Woinde Shizza

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia Mkutan wa hadhara leo, kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba leo, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana mkoani Kagera.

 Mbunge wa Bukoba mjini Hamis Kagasheki akihutubia wananchi atika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba mkoani Kagera.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Mbunge wa Bukoba mjini, Hamis Kagasheki (kulia), baada ya Mbunge huyo kuhutubia wananchi atika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba mkoani Kagera 06.06.15.

  •  Picha: Bashir Nkoromo


Eden Hills College kuanza rasmi Julai; Itatoa cheti na diploma ya urembo na mitindo

Kwa kile kinachoweza kuelezwa kama ukombozi wa tasnia ya urembo na mitindo Tanzania, chuo cha eden hills wakishikiliana na weqa-Women Engineering Institute vilivyopo kibaha mkoani pwani wameanzisha kozi ya masuala ya urembo na mitindo kwa ya diploma na certificate. Kozi hiyo inawalenga wanaume na wanawake wa rika zote wenye elimu ya angalau kidato cha nne au zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo mbalimbali vya habari msemaji wa Eden Hills College ambacho kina usajili rasmi wa serikali kupitia Baraza la Usimamizi na Usajili wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini (NACTE) usajili namba PWF/060 muhula wa kwanza utaanza rasmi mwezi Julai 2015 sambamba na kozi za ufundi za Civil Engineering, Electrical Engineering na Laboratory Technician ambazo chuo kimetenga nafasi maalumu kwa wanawake.

Aidha eden hills college imeanzisha kozi hizo za urembo na mitindo kwa lengo la kuinasua tasnia ya urembo na mitindo nchini ambayo hadi sasa imedhihirika imekwama na haikuwi kutokana ukosefu wa taalumu hiyo miongoni mwa washiriki, waandaaji na wadau mbalimbali. Tofauti na ilivyo katika nchi nyingine dunia ambako urembo na mitindo ni taaluma inayosomewa kama taaluma zingine za kijamii na kisayansi, hapa Tanzania tasnia ya urembo na mitindo imekuwa ni kama kapu bovu ambalo linakusanya wenye sifa na wasiyo na sifa bila kuzingatia taaluma za wahusika.

Tunaamini wakati sasa umefika, tena wakati sahihi wa kuunganisha nguvu zetu kama taifa, taasisi za elimu na hata mtu mmoja mmoja katika kuifanya tasnia ya urembo na mitindo kuwa ni fani ya kitaaluma naya kuheshimika kama ilivyo katika mataifa mengine duniani. Ni dhahili kwamba taaluma ya urembo na mitindo ikizingatiwa na kupewa uzito unao stahili na mamlaka zote zinazo stahili basi tasnia ya rembo na mitindo itatowa mchango mkubwa katika kukabiliana na tatizo la ajira na ukuwaji wa uchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Lakini pia itasaidia kumaliza udumavu na migongano ya mara kwa mara ambayo inajitokeza baina ya waandaji, washiriki na mamlaka husika nchini ambayo tumekuwa tukiishudia.

Kama chuo kimejipanga kimbinu na kimkakati kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa ni moja ya mataifa kiongozi naya kuigwa na mataifa mengine duniani katika ubora wa kitaaluma na mafanikio ya tasnia hii kitaifa na kimataifa. Pamoja na kozi za urembo, mitindo na ufundi, chuo hiki pia kinatoa kozi mbalimbali za biashara, uongozi na utawala, ualimu, afya ya jamii, utalii na maliasili na uandishi wa habari na diplomasia.

Ni malengo ya chuo pia kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa ni kitovu cha urembo, mitindo sambamba na utalii miongoni mwa nchi za afrika mashariki na bara la afrika kwa ujumla.

Chuo kinatoa wito kwa asasi mbalimbali zinazo jihusisha tasnia za urembo na mitindo zikiwemo Lino International ambao ni waandaaji wa mashindano Miss Tanzania, Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant Limited ambao nia waandaaji wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania, Compas Communication Limited waandaaji wa Miss Universe Tanzania, Afrika Tourism Promotion Centre waandaji wa mashindano ya Miss Tourism University World na hata Baraza la Sanaa la Taifa kushirikiana na sisi katika kuleta mapinduzi ya tasnia ya urembo na mitindo nchini kutoka kuwa fani ya hovyo hovyo hadi kuwa fani ya kitaaluma na kuheshimika.

Ni matarajio ya chuo kuwa ushirikiano huu utapelekea kuweka taratibu na kanuni za mashindano ambazo hazita ruhusu washiriki wasiyo na taaluma kushiriki katika mashindano ya urembo na mitindo. Katika kipindi hiki cha mageuzi ya fani hii ambapo kozi za certificate zitachukua mwaka mmoja na kozi za diploma zitachukua miaka miwili chuo kimejipanga kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa gharama nafuu na hata udhamini kupitia baraza la sanaa la Taifa au taasisi za uandaaji wa mashindano mbalimbali ya urembo na mitindo nchini na ili kukabiliana na tatizo la kuwa na wakufunzi wasiyo na taaluma ya urembo na mitindo katika kambi mbalimbali za mashindano hayo chuo kimejipanga kutoa kozi maalumu za muda mfupi kwa wale wote wenye nia ya kuwa wakufunzi kwenye kambi mbalimbali.

Taratibu za uzinduzi wa kozi hiyo mahususi zinaendelea ikiwemo kuwapata mawaziri wa wizara ya habari, vijana, michezo na utamaduni, na wizara ya maliasili na utalii kuwa wageni rasmi katika huo utakao fanyika mapema mwezi julai 2015 chuoni eden hills college mlandizi kibaha.

BY MASAKA . E. MASAKA

Nchemba achukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais Tanzania 2015


Mh.Mwigulu akiwasili makao makuu ya CHAMA CHA MAPINDUZI mjini Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Tanzania mwaka 2015.Mh:Mwigulu akisaini kitabu cha wagombea Urais kupitia CCM.
Mh:Mwigulu Nchemba na Mke wake Bi. Neema Mwigulu wakifurahia kukabidhiwa nyaraka mbalimbali za kufanikisha mchakato wa kutafuta wadhamini nchi nzima kuelekea hatua ya pili ya mchujo wa wagombea Urais ndani ya CCM.Mwigulu Nchemba akimtambulisha mke wake Bi. Neema Ngure kwa umma wa Watanzania kuwa ndiye FIRST LADY ajaye wa Tanzania.


Mh:Mwigulu Nchemba akiwa anateta na mtu mwenye ulemavu mara baada ya kupokea nyaraka za kuanza safari ya kuwania Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Nje ya ukumbi wa NEC  Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi, Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Mkewe Bi. Neema wakilakiwa na mamia ya Wananchi waliojitokeza kuwasapoti hii leo wakati wa uchukuaji wa fomu ya kuwania Urais wa JMT kwa tiketi ya CCM.Sehemu ya Wananchi waliojitokeza kumsapoti Mh: Mwigulu Nchemba wakati wa uchukuaji wa fomu ya kuwania Urais wa JMT.


Mh: Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi waliofika kumsapoti wakati wa uchukuaji wa fomu ya kuwania Urais wa Tanzania mwaka 2015.

  • Picha na maelezo tumeshirikishwa na Festo Sanga

Kinana ahani msiba wa marehemu LuangisaKatibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera), Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa mapema leo asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Katibu Mkuu Ndugu Kinana na baadhi ya maofisa wa chama na ndugu na jamaa wa marehemu wakishiriki sala ya pamoja na kumuombea marehemu Mzee Samuel Luangisa nyumbani kwake Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani KageraKatibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel Luangisa nyumbani kwake mapema leo asubuhi,Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.

  • Picha: Michuzi Jr, Bukoba

Lowassa vs Membe; It is unpredictable race! - Kambota


The presidential race within the rulling Chama Cha Mapinduzi is centred on two cadres Edward Lowassa and Bernard Membe. The two figures and their followers are optimistic that they will be choosen to represent the party in presidential contest against UKAWA.

As time approaches, the winner of this race is yet to be known and the situation turns critical every second! While every one sketches his priority to Ikulu, fans are eager to know who will be selected to fly over the CCM flag on 25th October, 2015.

While Lowassa insists on “Education first”, on his side Membe holds “Integrity” as his roadmap to power, it is unpredictable who will be a winner at the end of this race, so unpredictable, let’s wait it to
reveal!

By Nova Kambota (political analyst) based in Dar es Salaam, 0712 544237, [email protected], www.novakambota.wordpress.com

[audio] Maswali ya wananchi kwa Ngeleja alipotangaza nia ya Urais wa Tanzania 2015

Bofya kitufe cha pleya kusikiliza...

[video] Kauli ya Kinana kuhusu mdahalo kwa WanaCCM wanaonuia Urais Tanzania 2015