Dk Mwele Malecela, Nicholaus Mtenda wawania Urais wa Tanzania 2015


MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu Dk Mwele Malecela mtoto wa Makamu wa zamani wa CCM John Malecela ni miongoni mwa wana CCM ambao wamejitosa kugombea urais kupitia CCM.

Dk Mwele kesho amepangiwa na CCM kuchukua fomu za kuomba kugombea urais. Ratiba ya CCM iliyotolewa jana Makao Makuu ya chama hicho mjini hapa inaonesha kuwa licha ya Dk Mwele, mwingine ambaye atachukua fomu hiyo kesho ni Nicholaus Mtenda ambaye pia amejitokeza kuomba kugombea urais kupitia CCM.

Dk Mwele katika maisha yake mengi kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa mtumishi katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambako alianza kazi akiwa kijana na akapanda hadi kuwa mtafiti mkuu na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Licha ya kukulia katika familia ya mwanasiasa maarufu nchini, lakini Dk Mwele hajawahi kujitokeza hadharani kushiriki kwenye masuala ya siasa. Kama akichukua fomu hiyo kesho, atakuwa ni mwanamke wa pili kuomba kuteuliwa na CCM kugombea urais kumrithi Rais Jakaya Kikwete.

Mwanamke mwingine ni Balozi Amina Salum Ali wa Zanzibar. Jana Waziri wa Malisili na Utalii, Lazaro Nyalandu na wanachama wengine wawili wa CCM walichukua fomu za kuwania urais. Nyalandu alikuwa wa kwanza kufika katika ofisi za CCM kuchukua fomu akiwa amefuatana na familia yake na wafuasi wake kadhaa.

Baadaye alifuatiwa na mwanachama mwingine wa CCM, Peter Nyalali, ambaye ni Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na kufuatiwa na mwanachama wa chama hicho kutoka wilaya ya Muleba, Leonce Mulenda.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Nyalandu alisema hatua hiyo ni ishara ya yeye kuanza safari ya ndoto yake ya kuchukua majukumu ya urais kwa lengo la maendeleo ya nchi hii chini ya misingi aliyoianzisha Baba wa Taifa, hayati, Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa upande wa Nyalali, alisema atalenga katika kuimarisha uchumi kwa kuzingatia Katiba ya nchi na ya chama na kuleta mabadiliko chanya ndani ya CCM na kwa Watanzania ambao wamekuwa hawanufaiki na fursa zilizopo nchini.

Kwa upande wa Leonce Mulenda, alisema atahakikisha Katiba ya Chama na maamuzi yanatekelezwa kama inavyotakiwa na kuwa chama imara kitakachosaidia serikali isiwe legelege.


Somo la lishe kwa watoto wenye miezi 6+

(picha: Ash Correia via Pinterest)

MAZIWA ya mama kwa mtoto ni chakula pekee na kinachofaa hasa kwa mtoto mchanga mwenye umri kuanzia mwezi sifuri mpaka miezi sita.

Ushauri wa kitaalamu unapendekeza mtoto mwenye umri huu asipewe chakula kingine chochote zaidi ya maziwa ya mama. Hii ni pamoja na maji ya kunywa ambayo hayaruhusiwi kupewa mtoto huyo.

Makala hii inazungumzia chakula cha ziada au kijulikanacho kama chakula cha kulikiza anachopaswa kupewa mtoto mwenye umri zaidi ya miezi sita na kuendelea. Hata hivyo pamoja na kupatiwa chakula cha kulikiza ifahamike kuwa, ni muhimu mtoto huyu aendelee kupatiwa maziwa ya mama, pia katika umri huu wa zaidi ya miezi sita mtoto anaweza kutumia maziwa mengine yoyote yakiwemo maziwa ya mgando (mtindi).

Mtoto atapatiwa chakula cha kulikiza endapo atafikia umri wa zaidi ya miezi sita. Chakula cha ziada hapa kinatolewa kwani kwa wakati huo maziwa ya mama pekee hayatoshi kumpatia mtoto virutubisho vyote kwa ajili ya ukuaji wake na pia katika umri huu mtoto anaweza kula kwani utumbo wake unaweza kumengenya na kufyonza vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Pamoja na kumuanzishia vyakula vingine ni lazima mtoto aendelee kunyonya maziwa ya mama mpaka atakapotimiza miaka miwili au zaidi (Labda katika hali maalumu mfano kama mama anaishi na maambukizi ya VVU ambapo lazima afuate ushauri wa wahudumu wa afya). Jinsi mtoto anavyokua kiasi cha chakula anachopewa lazima kiongezeke ili kuweza kufikia mahitaji yake ya kilishe.

Chakula kizuri cha kumuanzishia mtoto ni kile ambacho kina:-
  • Wanga, mfano uji wa nafaka kama mahindi, mtama, mchele, ngano, viazi, muhogo n.k.
  • Vyakula viongezavyo nguvu kwa wingi kama mafuta, siagi, sukari na karanga (kwa kiasi).
  • Vyakula vyenye protini kwa wingi, kama vile karanga, maharage, soya, maziwa, mayai.
  • Mboga mboga na matunda kama mboga za kijani, karoti, na matunda ya aina mbalimbali.

Vyakula hivi vinapaswa kuandaliwa katika hali inayorahisisha kula na kufyonzwa, chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na salama, chakula kisicho na vitu vigumu kama mifupa, vitu vinavyoweza kusababisha mtoto akapaliwa, pia chakula hakipaswi kuwa na viungo na chumvi nyingi.

Pamoja na kwamba kuna umuhimu wa mtoto kupata makundi yote ya chakula bora , hta hivyo siku za mwanzoni uandaaji wa chakula unapaswa kuwa wa aina moja katika mlo na si kuchanganya vyakula vingi kwa mara moja. Hii itamsaidia kuzoea kwa urahisi.

Siku za mwanzo chakula hiki ili kufikia mahitaji ya nishati, protini, vitamini na madini ya kutosha chakula cha mtoto lazima kiandaliwe kwa mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kutoka kati makundi yote ya vyakula.

Kwa mfano unaweza kuchukua chakula kimoja kutoka katika kundi la nafaka, mizizi na ndizi, halafu ukachukua kingine kutoka katika kundi la jamii ya mikunde na asili ya wanyama na hivyo hivyo katika makundi ya mbogamboga, matunda na mafuta.

Mtoto aanze kupewa chakula kidogo kidogo kwani wakati huo bado utumbo wake ni mdogo hauwezi kuhimili chakua kingi. Jinsi mtoto anavyokua kiasi cha chakula na milo iongezeke.

Kwa mfano anapoanza kulikizwa apewe kijiko kimoja mpaka viwili vya chakula laini mara mbili au tatu kwa siku, halafu mitano wakati mtoto anapokuwa na umri wa miaka miwili.

Mtoto akifikisha miezi minane na kuendelea huwa anapenda kushika mwenyewe, hivyo anaweza kupewa vyakula vya kushika kama chapati au andazi, akifikisha miezi tisa mpaka 24 anaweza kula vyakula vya familia na apewe milo mitatu mpaka mitano kwa siku na nyongeza ya vitafunwa angalau viwili.

Chakula cha kwanza kilichozoeleka kwa kuanza kulikiza ni uji, na ndizi au viazi vilivyopondwa. Lakini nishati na viinilishe vingine vilivyopo kwenye uji ni kidogo kwa kuzingatia kuwa kuna kiasi kikubwa cha wanga kwenye nafaka mfano mahindi, mtama au ulezi.

Hata hivyo, kuna changamoto wakati wa uandaaji wa mlo unaotokana na nafaka. Mfano ni wakati wa uandaaji wa uji ambapo kiasi kikubwa cha maji huhitajika kwa kuchanganywa na unga, uchanganyaji huu hufanya unga kuvimba na hivyo kukulazimu kuongeza maji ili kuufanya uji uwe mwepesi.

Hali hii hufanya kiasi cha nishati na virutubisho kupungua, hivyo ili mtoto apate virutubisho itamlazimu kunywa kiasi kikubwa cha uji wakati haiwezekani kwani utumbo wake bado hauwezi kuchukua kiasi kingi cha uji hivyo mtoto anabaki amekunywa kiasi kidogo cha uji na sehemu kubwa ya uji huo ni maji.

Ili kuufanya uji uwe na kiasi cha kutosha cha nishati na virutubishi tunashauriwa kutumia nafaka ya aina moja na kuongeza vyakula vingine kama maziwa, unga wa karanga na mafuta.

Pia inashauriwa kutumia unga wa nafaka zilizochachushwa au zilizooteshwa kwani zenyewe hazivimbi hivyo hutumia maji kidogo na unga mwingi. Faida nyingine ya nafaka zilizooteshwa au kuchachushwa ni kwamba uyeyushwaji na ufyonzwaji wake tumboni ni unafanyika kwa urahisi sana.

Baada ya kutengeneza chakula cha mtoto uangalizi na upendo wakati wa kula ni muhimu sana kwani mara nyingine watoto wanakula vizuri kunapokua na uangalizi wa wazazi.

Hakikisha wakati wa kula unakua wakati wa furaha huku ukimhimiza mtoto wako kula na kuonyesha kuwa chakula ni kitamu ili afurahie tendo la kula na kujifunza aina za vyakula.

Wakati wa milo mikuu ya familia hakikisha unakaa na mtoto meza moja huku akiwa na chakula chake peke yake ili kuhakikisha anakula chakula cha kutosha na ili ashike mwenyewe kwa chakula anachoweza kufanya hivyo.

Wakati wa ulishaji mlishaji asiwe na haraka wakati wa kumlisha mtoto kwani mara nyingine watoto hupenda kula na kucheza.

Pamoja na kwamba, wakati wa kula mtoto huyu anapenda kula na kucheza kuna vitu ambavyo vinawenza kumvutia vinakua mbali, kwa mfano TV.

Pia ni muhimu mtoto alishwe akiwa na njaa usisubiri mpaka alie njaa na wala asilishwe akiwa amechoka au akiwa na usingizi. Epuka ulishaji wa kulazimisha kwani utamfanya mtoto kuwa muoga wakati wa kula na kumfanya apoteze hamu ya kula.

Wakati wa ulishaji kama mtoto ana kiu apewe maji lakini sio kiasi cha kujaza tumbo kwani atashindwa kula vizuri.

Ufuatiliaji wa ukuaji na maendeleo ya mtoto ni muhimu sana kwani husaidia kugundua mapema kama mtoto ana tatizo la lishe au hakui vizuri na kuchukua hatua mapema. Hivyo ni vema kumpeleka mtoto Kliniki kama alivopangiwa.

Makala ijayo tutaangalia namna ya kuotesha na kuchachusha nafaka na kutengeneza uji kwa ajili ya mtoto.

  • Imeandikwa na Juma Nziajose, Mtaalamu wa Lishe na Afisa Tabibu- 0718 962336 via MwanaHALISI Online

Get extra information on WhatsApp messages


You’re probably so busy chatting with your pals that you don’t realize you can uncover a bit more information about when your messages we’re delivered and seen. On iOS just swipe left on a particular chat entry to see when it was delivered and when it was read.

The process is slightly more involved on Android, but not much: Tap and hold on a particular message, then tap the Info button (an “i” in a circle) to get the relevant screen. If want to know exactly to what extent your friends are ignoring you then you can find out here.

BlackBerry updates BBM for Android with Private Chats, Message Editing


Here’s what’s new according to the BlackBerry blog post:

Private Chats:
In a private chat, your contact’s name is hidden, and new message notifications are turned off. Your chat is automatically deleted after a short time, or when you end the private chat.

Edit Message
The perfect complement to message retraction, Replace provides you with the power to edit a sent message.

Publish in Feed:
Share status updates faster, right from your BBM feed.

Facebook launches a smaller version of it's app for developing countries

Here is the update from the co-founder of Facebook, Mark Zuckerberg:


We just launched Facebook Lite, a new app designed to serve people a faster experience on slower mobile networks and Android phones around the world.

We built Facebook Lite to be faster, more reliable and very data efficient even when internet bandwidth is at a minimum. The app is less than 1 MB in size and takes just a few seconds to download.

We’re starting to roll out Facebook Lite across Asia, Africa, Latin America and Europe, and it will be available in the Play store. We’re going to keep working to serve the entire world, and we'll keep building tools for people in every community until we're all connected.

Android users can get it now at Google Play

Wananchi watoa maoni kuhusu ombi la MUWSA kubadili bei ya majiViongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira mjini Moshi, MUWSA wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (hayupo pichani) wakati wa utolewaji wa maoni juu ya bei mpya ya huduma ya maji.

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Moshi waliofika katika ukumbi wa Hindu Mandal kwa ajili ya kutoa maoni.

Mkuu wa mkoa a Kilimanjaro, Leonidas Gama akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na EWURA.

Mkaguzi wa hesbu wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na maji taka mjini Moshi, MUWSA, Benson Maro pamoja na Meneja rasilimali watu wa MUWSA, Michael Konyaki wakichukua kumbukumbu wa yale yaliyokuwa yakizungumzwa katika mkutano huo.Meneja fedha wa MUWSA, Joyce Msiru akichukua kumbukumbu wa mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa katika kikao hicho kulia kwake ni kaimu mkurugenzi wa MUWSA, Mhandisi Patrick Kibasa.Kamu mkurugenzi wa MUWSA, Mhandisi Patrick Kibasa akitoa hoja juu ya mapendekezo ya bei mpya ya utolewaji wa huduma mpya ya maji.Watumishi wa MUWSA, Idd Semkunde na Jacob Ollotu wakifutilia mkutano huoMkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA, Sharry Raymond.Mhandsi, Patrick Kibasa akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

Baadhi ya viongozi kutoka manispaa na watumiaji wa huduma ya maji wakifuatilia kwa makini.Baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano huo.

Mmoja wa wananchi waliofika kutoa maoni yao aliyefahamika kwa jina la Maulid Darabu akiwasilisha maoni yake katika mkutano huo.

  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Dixon Busagaga

Meya Jafary aipa kompyuta Shule ya Msingi PasuaMwenyekiti wa shule ya msingi Pasua Shaban Machivya akizungumza wakati wa kikao cha wazi kilichofanyika katika shule hiyo.Baadhi ya wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya msingi Pasua wakimsikiliza Mwenyekiti wa shule hiyo Shaban Machivya (hayupo pichani)

Mwenyekiti wa shule ya msingi Pasua, akisisitiza jambo katika mkutano huo.Msathiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa kikao cha wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi, Jafary Michael akimkabidhi mwenyekiti wa Shule ya msingi Pasua Shabani Machivya msaada wa kompyuta kwa ajili ya shule hiyo.Kompyuta zilizotolewa na msathiki Meya wa manispaa ya Moshi, Jafary Michael kwa ajili ya shule ya msingi Pasua.Baadhi ya wazazi waliofika katika mkutano wa wazazi na shule,Mstahiki Meya akizungumza.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon BusagagaZiara ya Kinana huko Muleba

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Anna Tibaijuka, baada ya kuwasili Kijiji cha Kyamkwikwi, wilayani Muleba mkoani Kagera leo, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa cha Bumbile wilayani Muleba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, jana, Juni 7, 2015. 

Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka

Kinana akisalimia wananchi

Kinana akikagua ujenzi wa gati katika ziwa Victoria, katika eneo la Kyamkwikwi wilayani Muleba mkoani Kagera, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa cha Bumbile wilayani Muleba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, Juni 7, 2015

Nape Nnauye akiielekeza boti eneo la kutia nanga ili Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wasafiri nayo kwenda Kisiwa cha Bumbile.

Kinana akipanda boti kutoka kijiji cha Kywamkwikwi kwenda Kisiwa cha Bubile

Kinana na Nape (kulia) wakiwa na Profesa Anna Tibaijuka wakati safari ilipoanza kwenda Kisiwa cha Bubile

Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba

Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika kijiji cha Katunguru, wilayani Muleba

Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Kijiji cha Katunguru.

 Charles Mwijage, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera

Prof. Tibaijuka akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini

 Kinana, akihutubia wananchi

Japan hands over building to Michakaini 'A' Primary School

The rear view of the newly constructed Classroom block.

By Our Correspondent

The Government of Japan which has been extending support to local communities in various sectors including health, education and water supply under the Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP) scheme since 1991, over the weekend has handed over two-storey Classroom Block at Michakaini 'A' Primary School in Chakechake town, South Pemba Region

The building which cost about US Dollars 159,037 is a response to a request by the Parents Committee of Michakaini A Primary School to ease congestion at the school.

The building which was constructed under the GGHSP scheme was handed in the presence of Hon. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba – Chairman of the Civic United Front (CUF) andHon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah – Regional Commissioner, South Pemba Region.

Speaking during the handover ceremony at Michakaini ‘A’ Primary School Ambassador of Japan, Masaharu Yoshida said Reconstruction of a Two-storey Classroom Block at Michakaini A Primary School in Chakechake Town, South Pemba Region; it is another contribution from Japan to the people of Tanzania.
“This project was recommended to us by Professor Ibrahim Lipumba, chairman of the Civic United Front (CUF), and I’m happy that he is here today to witness this handing over ceremony.” 
He lamented.

Narrating a sad story of the school he said situation at Michakaini „A‟ primary school, where pathetic with more than 1,300 pupils sharing only 12 classes, an average of 110 pupils in one class.

Due to the shortage of classes, the school decided to divide the pupils into two sessions, the morning session and the afternoon session.

However, even after two sessions, the average number of pupils per class was still very high at about 58 pupils per class.
"In some classes, the number was more than 80 pupils per class. These pupils could not get lectures of good quality and supervision. I’m glad that after our intervention, whereby the Government of Japan extended a grant assistance of US$ 159,037 (by then approximately equivalent to 250 million Tanzanian shillings), three classrooms, which were old and in a very bad condition, were demolished and the two-storey classroom block with a total of seven classrooms was constructed."
he said.

With these new classrooms, the average number of pupils per class is expected to be at 44 pupils per class.

Therefore, this project will help to create better condition that almost reaches the teacher-pupil ratio of 1:40 recommended by Primary Education Development Plan (PEDP III).

The ambassador believed that the new block will improve the quality of education and supervision to all pupils and will help their dreams to come true.

He also reiterated that the Government of Japan would like to provide continuing support for basic human needs in Tanzania.
The front view of the newly constructed Classroom block.Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida posing with from left Chaiman of Parent Committee of Michakaini Primary School, Mr. Nassor HArith Mohammed, Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, Headteacher Ms. Neema Mwalim Khamis, Secretary of the Committee and Head Teacher, in front of the newly constructed classroom block.Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, posing with Michakaini primary school pupils in front of the newly constructed classroom block.Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, during the Handing over ceremony.Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, during the Handing over ceremony.Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida congratulates Eng. Mansour Kassim, during the Handing over ceremony. Also in the phor Prof. Ibrahim Lipumba.