Apple creates an app to help you switch from Android phone


In the past, Apple created a step-by-step guide teaching defectors how to move their digital content from Android to iOS, but it took that idea a step further this year.

With the next update of its mobile software, iOS 9, Apple will launch a new app called Move to iOS.

The app will help transfer users' contacts, message history, camera photos and videos, web bookmarks, mail accounts, calendars, wallpaper between their phones — wirelessly and securely. It will also suggest that new iPhone users download any free apps that they had on their Android device.

As a kicker, the app even instructs users that they can recycles their old Androids for free at any Apple store. [Source of this info: businessinsider.com]

You can also read more at: Apple.com

Ziara ya Kinana huko KamachumuKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amezungukwa na umati wa wananchi, alipohutubia mkutano wa hadhara, leo katika mji mdogo wa Nshamba, jimbo la Muleba Kusini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika mkoa wa Kagera

[video] Waziri Lukuvi akitaarifu Bungeni gharama mpya za kulipia ardhi


[audio] Lissu akijibu kuhusu mgombea Urais Tanzania 2015 kutoka UKAWA na CCM

Tundu Lissu akiongea katika kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo amejibu swali aliloulizwa kuhusu ukimya wa kundi la UKAWA katika kutoa mgombea Urais wa Tanzania 2015.

Pia, amejibu swali aliloulizwa ikiwa UKAWA wanahofia wanachama wa CCM ambao tayari wameshatangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania 2015.

*Audio hii inasikika vizuri kiasi kwenye 'desktop computer'Apple Music coming to Apple TV and Android phones soon


Apple Music, the company's new take on streaming music will be available to Android starting June 30 in over 100 countries.

Apple Music is a worldwide live radio station from Apple broadcasting 24 hours a day.

Running $9.99 a month (with the first three months free) and families of up to six people sharing a membership for $14.99 a month, it offers streaming music from Apple's vast music catalogue, as well as access to your own personal collection of ripped CDs and purchased digital music. It also offers personal recommendations and a new "Beats 1" 24/7 international radio station led by popular DJs.

To find out more, read Apple's announcement

Ziara ya Rais Kikwete nchini Uholanzi katika pichaRais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo na muhtasari wa ziara yake toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe Wilson Masilingi baada ya kuwasili The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Shell Bw. Ben van Beurden jijini the Hague, Uholanzi leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Shell Bw. Ben van Beurden jijini the Hague, Uholanzi leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Bert Koenders jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katikati wakati Waziri wa Zanzibar Mhe Ramadhani akigonganisha glasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Mark Rutte jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mfalme Willem Alexander katika kasri la Kifalme la Noordeinde jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mfalme Willem Alexander katika kasri la Kifalme la Noordeinde jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kuongea na Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Uholanzi jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Picha ya pamojaRais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mhe Mark Rutte jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.

  • Picha: Ikulu

A 3-minute video explaining Hormones and Gender Transition

With Caitlyn Jenner’s recent transition in the news, more attention is being paid to the transgender community. A big part of gender transition is hormone replacement therapy (HRT). This week, Reactions talks about the chemistry of HRT and what happens when the body undergoes major shifts in estrogen and testosterone — two very powerful hormones.Mihogo labda mpende tu...


Taarifa ya habari Channel TEN ya Juni 7, 2015


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 8, 2015[video] Polisi yawatawanya kwa mabomu Wanachuo wa KIU Dar

Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya wanafuzi wa Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mgomo kwa ajili ya kushinikiza kupatiwa majibu juu ya usajili wa kozi ya Famasia.Makala za Simon Kivamwo za mapambano dhidi ya saratani ya utumbo

Tanzanian Muslim Community Washington DC yasisitiza mshikamano

Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo, Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC

Tanzanian Muslim Community Washington DC na vitongoji vyake nchini Marekani (TAMCO) imesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamao wa kijamii miongoni mwa wanajumuiya hiyo na Watanzania kwa ujumla wanaoishi katika maeneo hayo.

Hayo yameeelezwa na Mwenyekiti wa TAMCO Ndugu Ali Muhammed Shafi alipokuwa akizungumza na Swahilivilla pembezoni mwa "Siku Ya Familia" iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo, Siku ya Jumamosi June 6, jijini Washington DC.
Lengo kubwa la siku hii ni kuwakusanya pamoja wanachama wa jumuiya yetu na Watanzania wengine wanaoishi katika eneo hili hata kama si wanachama wa jumuiya yetu, kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa Familia na mshikamano wa kijamii", 
alisema Ndugu Shafi, na kuongeza kuwa ni nafasi nzuri ya kujuana khususan kwa watoto.

Aliendelea kusema kuwa mkusanyiko huu ambao hufanyika mara moja kila mwaka una lengo pia la kufanya matayarisho ya mwezi Mrukufu wa Ramadhan, ambapo wanajumuiya huchangisha fedha kwa jili ya futari ya pamoja kwa mwezi mzima wa Ramadhani.
"Tayari TAMCO imeshaandaa kumbi maalum kwa ajili ya futari ya pamoja kwa muda wa mwezi mzima wa Ramadhani na matayarisho yote yameshakamilika, tunachosubiri ni kumkaribisha mgeni huyo Mtukufu" 
alisema Bwana Shafi, na kuwatolea wito wanajumuiya ambao bado hawajatoa ada zao za uanachama kufanya hivyo, ili kurahisisha na kufanikisha malengo ya jumuiya hiyo.

Akizungumzia malengo ya baadaye ya jumuiya hiyo, Bwana Shafi alisema kuwa wana lengo la kufungua madras kwa ajili ya watoto wanaoish Washington na maeneo ya karibu, ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu,malezi na mafunzo halisi ya Kiislamu.

Aliwatolea wito wanajumuiya kuitumia fursa ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kuongeza Ibada na Imani ndani ya mwezi huo na katika maisha kwa ujumla.

Siku Ya Familia ya TAMCO (TAMCO Family Day), hufanyika kila mwaka ambapo wanajumuiya hiyo na wengineo hukutanika pamoja kwa siku nzima, ambapo pamoja na mambo mengine, hutoa nafasi kwa watoto kucheza, kufurahi kujuana na kujenga urafiki tangu wakiwa wadogo.

Mwenyekiti wa Tanzanian Muslim Community Ndugu Ali Muhammed ShafiNyuma kabisa aliekuwa muasisi wa zamani wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala akiwa na Shamis Alhatry, kushoto, Kulia ni Mwenyekiti wa ZADIA, pa moja na Mganga katika sharehe ya familia Day Siku ya Jumamosi June 6, waIslamu Washington DCBaadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo, Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DCMwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Omar Haji Ally (kulia) akibadilishana mawazo na aliekuwa muasisi wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala, kwenye sharehe ya familia Day Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC

Picha taarifa: Abou Shatry

GOLA Foundation kuwaondoa watoto mitaani ArushaAfisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha Mwantumu Dossi akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani, katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo Elisha Maghembe

Habari picha: Woinde Shizza, ARUSHA -- Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation ,Elisha Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watoto wa mitaani walioko jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya malezi lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya
elimu waliyoikosa kwa muda mrefu.

Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha malezi kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa na kuchukuliwa na wazazi wao.

Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda mrefu hujitumbukiza katika majanga ya matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya vitendo visivyofaa hivyo ameitaka jamii ishirikiane kutatua tatizo hili ambalo ni janga kwa taifa.
“Tunapofika mtaani kuwaondoa watoto hawa wa mtaani tunakutana na changamoto nyingi ikiwemo kukosa ushirikiano na watoto wenyewe na pia wengine wanatumkishwa na ajira katika umri mdogo na baadhi ya watu hivyo kufanya zoezi hilo kuwa gumu” 
Alisha Elisha

Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini A Mwantumu Dossi alifika katika kituo cha kufikia cha malezi ya watoto wa mtaani kinachomilikiwa na Gola Foundation amesema kuwa Halmashauri ya jiji itaangalia namna ya kushirikiana kutatua changamoto za watoto wa mitaani.
“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu nimefika apa kujionea na kama Jiji kuna mkakati Mahususi wa kuwaondoa watoto wa mitaani utakaoanza 2015-2016” 
alisema Mwantumu

Mwenyekiti wa Baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassan Omari alisema kuwa juhudi za kuwaondoa watoto wa mitaani katika mazingira magumu na hatarishi zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu pamoja na serikali kwani watoto ni taifa linalotegemewa kesho.