Mdahalo wa WanaCCM wawania Urais 2015: Mufuruki ataja maswali 4 yaliyowakimbiza


Siku moja baada ya kuahirishwa kwa mdahalo wa waliotangaza nia katika nafasi ya urais CCM, imebainika kuwa viongozi hao wangepaswa kujibu maswali magumu manane yanayohusu uchumi, utawala bora na utawala wa sheria. Hata hivyo mgombea Balozi Amina Salum Ali pekee ndiye aliyejitokeza.

Baadhi ya wagombea waliokuwa wametajwa kuhudhuria mdahalo huo wa moja kwa moja kupitia televisheni ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta.

Akizungumzia utaratibu wa mdahalo huo ulioandaliwa na Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini ( CEOrt), Mwenyekiti wake Ali Mufuruki alisema, kila mtangaza nia alitakiwa kujibu maswali manne ya uchumi na manne ya utawala bora na utawala wa sheria na ya aina moja.

 1. Maswali ya uchumi waliyotakiwa kujibu ni namna gani mgombea anaweza kupunguza ongezeko la vijana kukosa ajira, umaskini na uvunjifu wa amani.
 2. La pili lilikuwa, ‘Ukitilia maanani kwamba sekta ya kilimo ndiyo tegemeo kuu la maisha kwa asilimia 80 ya Watanzania pia ina uwezo wa kipekee wa kubadilisha uchumi, ni hatua gani utachukua kama utateuliwa kuwa rais?’
 3. La tatu liliuliza, ‘je, kama ukiteuliwa kuwa rais utafanya nini kuhakikisha uchumi wetu unakua na manufaa yake yanakuwa shirikishi na tofauti kati ya maskini na matajiri haiwi kubwa kiasi cha kuhatarisha amani katika nchi yetu?’
 4. Jingine lilipaswa kuulizwa, Ukiwa kiongozi atakayekuwa ofisini wakati huu wa uwekezaji katika sekta ya gesi asilia, utachukua hatua gani kuhakikisha matumaini ya utajiri na maisha bora waliyonayo Watanzania kwa sekta hii yanatimia?’

Watangaza nia hao walitakiwa kueleza pia iwapo wanakubali kwamba Tanzania haiwezi kufikia malengo yake ya maendeleo bila kuwekeza katika miundombinu. ‘Kama unakubali, utatumia mbinu gani kupata fedha hizo nyingi zinazotakiwa katika kuwekezaji kwenye miundombinu?’

Kwa upande wa utawala bora na utawala wa sheria, walitakiwa kueleza ni vipi watachukua hatua kuhakikisha usimamizi mbovu wa masilahi ya nchi, rushwa na upuuzwaji wa sheria unadhibitiwa.

Pia, walitakiwa kueleza watachukua hatua gani kuhakikisha ujangili unatokomezwa nchini, watakomeshaje upotevu mkubwa wa mapato unaotokana na ukwepaji kodi na watatumia njia gani kuhakikisha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa.

Hata hivyo, Mufuruki alisema kuwa hadi kufikia juzi mchana watangazania watatu pekee ndiyo walikuwa wamethibitisha ushiriki wao na baadaye Sumaye na Nyalandu wakitoa udhuru.

Watangaza nia wengine, walionekana kuomba radhi kupitia mitandao ya kijamii wakidai kuvurugwa na ratiba ya mdahalo huo ambao awali walielezwa ungefanyika asubuhi kabla ya kuahirishwa.Wanaojinadi CCM kwa Urais wa Tanzania wanafanya kazi ya bure


Wakati makada wanaotangaza nia na kuchukua fomu kugombea urais kupitia CCM wakiendelea kujinadi kwa kutaja sifa mbalimbali za rais ajaye, chama hicho kimesema hayo yote ni kazi bure kwa kuwa chenyewe kina vigezo vyake 13 ambavyo kitavitumia kumpata mgombea wake wa nafasi hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana huku wasomi na wachambuzi wa siasa wakisema sifa hizo na ahadi wanazotoa wagombea hao si rahisi kutekelezeka ndani ya mfumo uliopo wa chama hicho.

Mangula, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ndogo wa maadili, alisema: 
“Kila mtu anatoa sifa zake anazozipenda. Ohh nataka mgombea ajaye awe hivi… lakini chama chetu kimetaja sifa 13 za mgombea urais. Mtu anayetaka kuwa mgombea kupitia CCM lazima awe na vigezo hivyo.

Mangula alisema kifungu cha tano cha kanuni za uteuzi wa wagombea wa CCM, kinaipa jukumu Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) kuzingatia mambo kadhaa muhimu wakati wa uteuzi wa mgombea katika nafasi ya urais.

Aliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni uzito wa nafasi hiyo, haja ya kulinda na kuendeleza mshikamano miongoni mwa wanaCCM, haja ya kupanua demokrasia ya ndani katika kuwapata wagombea na hali halisi ya nyendo za ushindani wa kisiasa nchini.

Vigezo 13 vya urais


Mangula alitaja vigezo vya mgombea urais CCM kuwa ni uwezo mkubwa wa kuongoza nchi kwa kutumia uzoefu katika uongozi wa Serikali, umma au taasisi, awe mwadilifu, mwenye hekima na busara.
“Unapimaje hekima?”
“Unapima kwa kuangalia yale mliyokubaliana kama ameyatekeleza kama mlivyokubaliana.”
aliuliza Mangula na kujibu mwenyewe.

Alivitaja vigezo vingine kuwa ni elimu ya chuo kikuu au inayolingana na hiyo, upeo mkubwa wa kudumisha na kuendeleza Muungano, umoja, utulivu na mshikamano wa kitaifa, wepesi wa kuona mbali, asiyeyumbishwa na mwenye uwezo wa kuona mbali kuhusu masuala nyeti na muhimu kwa Taifa kwa wakati unaofaa.

Vigezo vingine ni upeo mkubwa na usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa ili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi na dunia yote, asiwe mwenye hulka ya udikteta au ufashisti, bali awe mtu mwenye kulinda Katiba, utawala bora, kanuni na taratibu za nchi.


Mangula alisema mgombea urais wa CCM anapaswa kuwa mtetezi wa wanyonge wa haki za binadamu na mzingatiaji wa maendeleo ya watu wote. Pia asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wa mtu binafsi. Pia mgombea lazima awe mstari wa mbele katika kuzifahamu, kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza sera na ilani ya uchaguzi ya CCM, awe mpenda haki na jasiri wa kupambana na dhuluma na uonevu.

Alisema anatakiwa asiwe mtu anayetumia nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali, awe ni mtu anayekubalika na wananchi, makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa viongozi na asiyevumilia uzembe wa majukumu au wajibu aliokabidhiwa ili kuinua nidhamu ya kazi tija na ufanisi.

Kutafuta wadhamini

Mangula alisema katika kipindi ambacho wagombea hao wanatafuta udhamini, chama kinafuatilia kila wanachofanya na kuweka kumbukumbu zitakazosaidia kupata wasifu wa mgombea husika.
“Wakati huu wa kutafuta wadhamini, kila kilichofanywa na mwanaCCM anayetafuta wadhamini 450 kitaingia katika kumbukumbu za tathmini ya mgombea mtarajiwa,” 
alisema.

Mangula aliziagiza kamati za maadili za wilaya kukutana mara moja baada ya wagombea kujaza majina ya wadhamini wilayani na kuwajadili.
“Mihtasari iletwe mara moja makao makuu ya chama ili kamati ya maadili ya taifa itumie taarifa hizo za tathmini ya wilaya katika jumla ya kumbukumbu za kila mgombea mtarajiwa,” 
alisema.

Kampeni marufuku

Katika hatua nyingine; Mangula alipiga marufuku watia nia hao au mawakala wao kufanya vitendo vyovyote vinavyoonekana dhahiri kuwa ni sehemu ya kampeni za kuwania nafasi wanayoitafuta kabla muda wa kampeni.

Alitaja vitendo vinavyoashiria kampeni kabla ya wakati kuwa ni pamoja na utoaji wa misaada ambayo dhahiri ina lengo la kuvutia kura.
“Kanuni hii haitamhusu rais, mbunge, mwakilishi na diwani ambaye yupo madarakani,” 
alisema Mangula.

Mangula alieleza kuwa katika kipindi cha mchakato huo, CCM itatumia kanuni za uteuzi wa wagombea wake katika vyombo vya dola zilizotolewa na NEC ya CCM toleo la 2010. Pia alisema miiko ya shughuli za uchujaji na uteuzi inawataka wagombea hao kutofanya kampeni za kupakana matope dhidi ya wenzao.

Kauli za wachambuzi
Wakati mchakato wa kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala ukiwa umepamba moto, baadhi ya wanasiasa, wanataaluma na wananchi wa kawaida, wamesema kati ya wanaCCM takriban 24 waliokwishajitokeza, hakuna mwenye uwezo wa kuvunja mfumo mbovu wa utawala uliopo, hivyo wanayoahidi si rahisi kuyakamilisha.

Makada waliojitokeza ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Balozi Amina Salum Ally.

Pia, wamo Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Balozi Ally Karume.

Wengine ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Ofisi wa Rais (Kazi Maalumu) Profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa Sospter Muhongo.

Katika foleni hiyo pia wapo Mkurugenzi wa Kampuni ya Forecast Enterpreneurship, Boniphace Ndengo, Leonce Mulenda, Peter Nyalali, Wakili Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Godwin Mwapongo, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na leo wakitarajiwa, Dk Mwele Malecela na Balozi Augustine Maiga.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa katika kutafuta kiongozi wa juu wanatakiwa kuangalia mfumo mzima wa uongozi ambao CCM imeshauharibu.
“Hata wakipata kiongozi mzuri kiasi gani, mfumo wao hauwawezeshi kutekeleza mabadiliko. Wananchi wajue mapema kati ya waliotangaza nia ni nani atathubutu kuuvunja mfumo uliopo?...hakuna. Tunapozungumzia mabadiliko ya kimfumo ni kuanzia ngazi ya taifa hadi katika vijiji,” 
alisema Nyambabe.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim aliyesema kati ya wote waliojitokeza hakuna anayemuona anafaa kutokana na kushindwa kuainisha namna atakavyovunja mfumo mbovu wa uongozi uliopo.
“Hakuna mgombea aliyezungumza atafanyaje kuuvunja mfumo huo hii ni kwa sababu utawaharibia hata wale watakaohusika kuwavusha katika kile wanachokitafuta.
“Binafsi sijapata kiongozi ambaye ataivusha Tanzania miaka 10 ijayo. Sijamwona mwenye ujasiri wa kuvunja mfumo mbovu uliopo na angekuwapo tayari angekuwa ameshazungumzia namna kuuvunja,” 
alisema Salim.

Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam, Daniel Kitwana alisema watangaza nia wote hawawezi kutekeleza mambo wanayosema kwa kuwa watalazimika kufuata mfumo wa chama, ambao umeshindwa.

Aliongeza kuwa hata waliotangaza kuwa watawaletea maendeleo wananchi kwa kuwa wanachukia rushwa hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa watakapoingia madarakani watamezwa na mfumo wa chama hicho.

Ukanda

Kuhusu kitendo cha wagombea wengi kutangazia nia katika maeneo walikotokea, Salim alisema kutatengeneza tatizo la ukanda na ukabila ambao utaleta matatizo siku zijazo kwa kuwa kiongozi atakayepita ataanza kulipa shukrani kwanza eneo alikotokea.

Mkazi wa Tabata, Dar es Salaam, Hijja Omary (28) alisema kitendo cha makada wengi kujitokeza kuwania urais kunatokana na kukosa kiongozi msimamizi na ni sawa na kukosekana baba kwenye nyumba, hivyo kufanya kila mtoto kujiona anaweza kuongoza.
“Sioni kama kulikuwa kuna haja ya msururu wote huu wa watu kutangaza nia ya kuwania urais. Naweza kusema kinachotokea sasa ni vurugu. Maana licha ya kuwapo kwa sera za CCM, kila kada anayetangaza nia anatangaza sera yake. Kwa hali hii sioni kama kuna kiongozi wa kweli hapa,” 
alisema.

Katibu wa Kanda ya Dar es Salaam, Umoja wa Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGOSCO), Moses Kyando alisema kinachosikika ni matumizi ya lugha za kuwavutia wananchi, ili viongozi hao waingie madarakani, lakini wakishapata nafasi hawatafanya walichoahidi.
“Sidhani kama kuna jambo jipya, wengi hawana jipya. Kwa mfano kwenye elimu tumeshuhudia mfumo wa kutoa matokeo ya mitihani ukibadilishwa, mara wanasema Matokeo Makubwa Sasa (BRN), lakini hakuna kinachofanyika,” 
alisema Kyando.

Kada mkongwe wa CCM, Ibrahim Kaduma alisema kujitokeza wagombea wengi ni jambo zuri kwa kuwa kunatoa fursa kwa wananchi kumchagua wanayemwona anafaa.


Hata hivyo, alisema Watanzania hawana haja ya kuwa na wasiwasi wa rais ajaye kwa kuwa Mungu amekwisha waandalia kiongozi atakayeisaidia nchi kutimiza mipango yake ya maendeleo... “Mungu atafanya hivyo atatuonyesha mambo makubwa na magumu tusiyoyajua, atatupa mtu atakayeweza kutumia vizuri rasilimali tulizonazo.”

Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Ameir Manento alisema ameona mabadiliko ndani ya CCM katika mchakato huo, hasa kwa kutoa uhuru wa kutosha kwa watangaza nia, wakiwamo wanaotaka kujitangaza tu.
“Kuna wengine wanataka kufahamika majimboni tu, ukimuuliza ‘una nia kweli’? Anakwambia ana nia, lakini wanataka kufahamika tu,” 
alisema Jaji Manento.

Imeandikwa na Nuzulack Dausen, Goodluck Eliona na Sharon Sauwa via MWANANCHI.

Kibosho Kindi wanyakua kombe la Lucy Oweya Cup 2015Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya (CHADEMA)akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kibosho Kilima kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.Mratibu a mashindano hayo Charles Mchau akisalimiana na wachezaji.


Mgeni rasmi katika fainali hiz katibu wa CHADEMA kanda ya kaskazini Aman Golugwa akisalimiana na wachezaji.Mbunge Lucy Oweya akiwa ameambatana na mgeni rasmi Aman Golugwa mara baada a kukagua timu hizo.


Mgeni rasmi katika mashindano ya Lucy Owenya Cup yaliyoshirikisha timu za jimbo la Moshi vijijini, Amani Golugwa akizungumza na timu zilizoingia fainali za Kibosho Kindi na Kibosho Kilima.

Manahodha wa timu hizo mbili wakipeana mikono kusalimiana.Timu ya Kibosho Kindi wakiomba Dua.Timu ya Kibosho Kilima wakiomba Dua.Waamuzi wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu hizo mbili.Timu ya Kibosho Kindi katika picha ya pamoja.Timu ya Kibosho Kilima katika picha ya pamoja.

Baadhi ya mashabiki waliohudhulia mchezo huo.Mchezo ukiendelea.Moja ya timu iliyoshiriki mashindano hayo Sangiti Sekondari wakifuatilia mchezo wa fainali.Meza kuu wakifurahi mara baada ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha mwisho ambapo timu ya Kibosho Kindi iliibuka na ushindi wa bao 3 kwa 1.Mashabiki wa timu ya soka ya Kibosho Kindi wakifurahia ushindi huo.Mashabiki wa timu ya soka ya Kibosho Kindi wakichukua taswira na muandaaji wa mashindano hayo.Baadhi ya timu zilizoshiriki mashindano hayo.Mdhamini wa mashindano hayo Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindabo hayo na bingwa kupatikana.Mgeni rasmi katika mashindano hayo Katibu wa Chadema Kanda ,akizungumza wakati wa kufunga rasmi mashindano hayo na kukabidhi zawadi kwa washindi.Mgeni rasmi, Golugwa akikabidhi cheti kwa Mbunge Lucy Owenya kama ishara ya chama hicho kuthamini mchango wake katika kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo.Mgeni rasmi Amani Golugwa akikabidhi zawadi ya kikombe kwa nahodha wa timu ya Kibosho Kindi mara baada ya kufanikiwa kutwaa kikombe hicho kwa mara ya kwanza katika mashindabo ya Lucy Oweya Cup 2015.Mashabiki wa timu ya Kiboshi Kindi wakifurahia na kikombe chao.

 • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga 

Brazil scholarships for Tanzanians for 2015-2016

The Government Republic of Brazil is offering scholarships for qualified Tanzanians under the programme Brazilian Exchange Program for Undergraduate Students (PEC – G) for academic year 2015/2016
1.0 Financial Conditional of Scholarships

The Scholarship will Cover:-
  1. Tuition fee;
  2. Purchase of air tickets;
  3. Allowance money should be catered for solely by the students themselves.
2.0  PEC – G Conditions for Application
(i) Be a Citizen and resident of Tanzania
(ii) Age between 18 to 23 years old by December 31, 2015.
(iii) Have completed high school at the average of equal or above 60% (grade C).
(iv) Have obtained the certificate of proficiency in Portuguese.
(v) Applicants who have not concluded high School on the date of Application may present their certificate of conclusion in the moment of enrollment in the assigned Brazilian Higher Education Institution (Result slip).
(vi) Have obtained the certificate of proficiency in Portuguese as a Foreign Language Celpe – Bras exam.
(vii) Applicants from Countries where there is no  Celpe -  Bras exam must take the exam in Brazil in sole opportunity, upon the conclusion of the Portuguese as a Foreign Language preparatory course to the Celpe – Bras exam, in an accredited Higher Education Institution .
(viii) Applicants who fail the Celpe – Bras exam taken if Brazil will not be able to participate in PEC – G.  Their registration will be considered invalid and their staying in Brazil will be  terminated.

3.0  Who cannot apply to PEC – G
 1. Brazilian Citizens, even those holding Dual Nationality;
 2. Holders of any temporary or permanent Visa to Brazil;
 3. Those who have completed high school in Brazil,
 4. Those who have been selected in previous – editions of PEC – G and who, having not presented at the Brazilian IES at the time of enrolment, fail to provide a justification until the deadline for enrolment.
 5. Those with a high school final overall average and official language average inferior 6o%.
 6. Applicants from Countries  where the Celpe-Bras exam can be taken who do not hold the Celpe bras Certificate.
4.0  Requirement documents
(i)Completed application form with endorsement from the  Ministry of Education  and Vocational training;
(ii) Certified copy of birth certificate
(iii) Photocopy of biodata page of passport
(iv) Certified copies of O-Level and A-level Secondary educational certificates or Diploma Certificate with B+ Grade,
(v) Transcripts of secondary school results/Diploma, and
(vi) Medical certificate mentioning that student is free of contagious diseases.
(vii) Original and copies of the candidates and both parents Birth certificates
(viii)Original of certificates of physical and mental health issued within the last three months before application.
(ix)Original of statement of financial responsibility (TRF) in Portuguese accompanied by proof of the signatory income attesting the capacity to fulfil the commitment made. Or application
(x). Original of statement of commitment for application (TCL) it is mandatory to fill in the Portuguese version

Note
 • Applicants from countries where there is no celpe- Bras-exam must take the exam in Brazil in a sole opportunity, upon the conclusion of the Portuguese as a foreign language preparatory course to the celpe-Bras-exam, in an accredited Higher Education Institution (HEI)
 • The statement of financial responsibility (TRF) declares that the applicant counts with at least one source of income able to funds his /her trip to Brazil and his return to their home country, as well as installation and maintenance in Brazil throughout the duration of the course.
 • The registration for the programme can be accessed in the link http.www.dce.mre.gov.br/en/pec/pecg.php
 • Selected Candidate will be notified by September 2015
5.0 Address for forwarding of completed application Forms
Permanent Secretary
Ministry of Education and Vocational Training
Office No.34 Director of Higher Education –Registry
7 Magogoni Street
Code 11479
P.O.Box 9121
Dar es Salaam

The deadline 30/06/2015  at 10:00am 

Tanzania - Germany Postgraduate Training Programme 2015: PhD and Masters Degrees in Germany

Second CALL FOR APPLICATIONS

The Tanzania Commission for Universities (TCU) is pleased to announce the second call for application of PhD and Masters Scholarships for the 2015 Cycle of Tanzania - Germany Postgraduate Training Programme. This training programme which is funded jointly under the Tanzanian Government through the Ministry of Education and Vocational Training and the German Academic Exchange Service (DAAD), aims in particular, to impact on capacity-building in Tanzanian Universities through staff development. Scholarships will be awarded to candidates who qualify to undertake PhD or Masters degrees in Germany.

Eligibility Criteria

The applicant must:

a)Be a citizen of the United Republic of Tanzania;

b)Be an academic member of staff in a private accredited or public Tanzanian university;

c)Have at minimum, a bachelor degree second class upper division or equivalent;

d)Hold a good Masters degree having obtained an equivalent of a B+ grade or above from a recognized university institution (for PhD applicants only);

e)Have obtained the Masters degree not more than within the past 6 years (for PhD applicants only);

f)Be willing to undertake a 6 months German language course in Germany.

Mode of Application:

Interested eligible applicants wishing to apply for the scholarships may download the application documents at: http://www.tcu.go.tz/index.php/program-fees-scholarships/18-programs-awards/75-daad-forms

Soft copies and hard-copies of duly filled-in application forms and other documents must be addressed to:

Executive Secretary,
Tanzania Commission for Universities,
Garden Road, Mikocheni, Near TPDC Houses,
P. O. Box 6562, Dar es Salaam

Tel: 22 27772657; Fax: 22 2772891

E-mail: [email protected]

Applications end on Friday 31st July, 2015 at 15:30 hours.

Mkulima kutoka Kasulu aenda kuchukua fomu za CCM za kuwania Urais Tanzania 2015

KATIKA hali isiyo ya kawaida mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Eldoforce Bilohe (43)leo alitinga makao makuu ya Chama cha Mapindizi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kuteuliwa kuwa mgombea bila kuwa na ada huku akiwa amebeba maji ya chupa kwapani.

Bilohe ambaye alisema elimu yake ni ya darasa la saba aliwasili makao makuu ya CCM muda wa saa 5:40 asubuhi na kuelekea Ofisi ya kupokelea wagombea ndani ya ofisi baada ya kuwapita waandishi wa habari wakiwemo wapiga picha waliokuwa wamejipanga kumsubiria lakini aliwapita waandishi bila kumtambua kuwa ni mgombea.

Akiwa amevaa suruali ya khaki na fulana yenye rangi ya kijani na njano alionekana kuduwaza watu wengi ambao walikuwa wakiwasuburi wagombea ambao walikuwa wakichukua fomu jana.

Akiwa kati ya watu waliokuwa kwenye orodha ya kuchukua fomu,  Bilohe alikuwa amebeba chupa ya maji kwapani baada ya kufika na kupokelewa na maafisa ambao walimtambua kuwa ni mgombea na ndipo wapiga picha waligutuka na kuanza kupiga picha.

Kisha aliingia ndani ya ofisi ya kuchukua fomu na alitoka baada ya muda mfupi na kuanza kuhojiwa na waandishi wa habari.

Alisema amefika Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuteuliwa kuwa mgombea lakini kwa sababu ambazo hazijazuilika ameambiwa akachukue fedha.
“Nilipogiwa simu wakati niko benki ya CRDB nikiwa kwenye foleni nikisubiri kuchukua fedha ndiyo nikakimbia kuja hapa”
 alisema

Alisema amekuwa mwanachama hai wa CCM tangu mwaka 2003 na elimu yake ni ya m msingi na ana uzoefu kutokana na kuwa katika chama kwa muda mrefu.
“Nimekuja kama nilivyo kwa sababu sijawahi kuwa na makundi unayoyaona wewe, mimi ni mwanachama wa kawaida kama wanachama wengine” 
alisema

Alisema ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kuamini kama anaweza.

Kwa Mujibu wa mujibu wa moja wa maofisa wa Chama ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema Bilohe amerudisha si kwa sababu hana hela kuna vigezo ambavyo havijafikiwa ikiwemo barua ya utambulisho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya aliyotoka.
“Hajakamilisha taratibu za kumwezesha kuhukua fomu” 
alisema.

Hata hivyo taarifa zilizopatikana baadaye zilisema kuwa tayari mkulima huyo ameshalipa gharama za ada ya fomu kiasi cha Sh. 1,000,000 na atachukua fomu yake kesho saa kumi jioni.

Bi Moza afanikisha kumpeleka mwanaye India kwa matibabu

Bi Moza akiwa akimshindikiza mtoto wake Moh'd Saidi, nchini India kwa matibabu

Bi Moza Moh'd Khamis anapenda tena kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliochangia kwa hali na mali kwa mtoto wake Moh'd Said Moh'd, kwenda kufanyiwa matibabu ya upandikizaji wa figo, nchini India.

Mapema asubuhi ya  Jumanne Juni 9, 2015, Bi Moza aliongea na blog ya SwahiliVilla ili kutoa taarifa kwa kukamilika safari yake ya kwenda nchini India pamoja na kutaka tumuombe dua za kumtakia kila la kheri katika safari hiyo.

Moh'd Said Moh'd ameondoka siku ya Jumanne Juni 9, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu yake.

Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers Network (DMV) na Watanzania wote waishio nchini Marekani, kumtakia kila la kheri ndugu yetu Moh'd Said Moh'd katika matibabu yake huko nchini India.M/Mungu amjaalie wepesi katika safari yake na ampe afuweni na mafanikio katika mipangilio yote matibabu yake. Ameen.

 • Taarifa kutoka kwa Abou Shatry/SwahiliVilla blog

MJUMITA wazindua Mkuhumi ulioimbwa na Mrisho Mpoto, Afande Sele na Dayna

Mjumbe wa kikosi Kazi cha Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi),Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Julitha Masanja (kushoto) akiwa ameshikilia CD na DVD alizozizindua jua ambazo zina nyimbo maalum wa Mkuhumi ambao hupambana na uharibifu wa mazingira Dar es Salaam jana. Pamojanae ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (Mjumita), Rahima Njaidi

WATANZANIA wametakiwa kuwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wa masuala muhimu ya kijamii kwakuwa wasanii hao wanamvuto mkubwa kwa wananchi.

Hayo yalisema jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira uliojulikana kama ‘Mkuhumi’.

Wimbo huo ulioimbwa na wanamuziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Dayna Nyange pamoja na msanii nguli wa kughani mashairi Afrika Mashariki, Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA), Rahima Njaidi alisema, wameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa ni rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii.

Alisema lengo kuu la wimbo huo ni kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi), kupitia fedha zinazotolewa na nchi zenye viwanda.

“Watu wengi tunapoenda kusikiliza muziki kuliko kusoma, kwa maana hiyo kama tungeweka elimu hii kwenye vipeperushi isingekuwa rahisi kwa watu wote kupata ujumbe, lakini tunategemea kupitia muziki huu tutawafgikia watu wengi,” alisema.

Alisema wimbo huo umetayarishwa chini ya usimamizi wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Mkuhumi ili kuwafikia wadau ili kwa pamoja waweze kuchukua tahadhari na kupunguza shughuli zinazochangia kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.

“Kupitia wimbo huu jamii itapata uelewa utakaosaidia kuhamasisha jamiikutumia rasilimali za misitu kwa njia ya uendelevu na kujipatia faida,” alisema Njaidi.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Mjumbe wa Kikosi kazi cha Mkuhumi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Julitha Masanja ambaye alipongeza kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo ya Mjumita.

“ Mjumita inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote kwani inasaidia kutunza misitu ya asili ambayo imekuwa na changamoto kutokan ana shughuli za binadamu,”alisema Masanja.

Mjumbe wa kikosi Kazi cha Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi), kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Julitha Masanja akikabidhi DVD kwa wanahabari,Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili nchini, Bettie Luwuge akifafanua jambo juu ya mradi huo.Mtaalam wa IRA, Edmund Mabhuye akiwasilisha mada juu ya mabadiliako ya tabia nchi na ongezeko la hewa ukaa.Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi akizungumzia uzinduzi huo Dar es Salaam leo.Wanahabari n mbalimbali wa kifuatilia maelezo juu ya miradi ya hiyo ya uhifadhi mazingira.

Dk Slaa ziarani nchi za UlayaKatibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini Jumamosi Juni 06, 2015 kuelekea Bara la Ulaya ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nane.

Akiwa ziarani Dk Slaa anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambapo pia atakutana na jopo la wataalamu wa masula ya uchumi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika kupata mifumo sahihi na kujenga taasisi za kusaidia uwajibikaji na kusukuma maendeleo ya watu katika nchi za Afrika hususan zile zenye rasilimali nyingi kama Tanzania ili kuziepusha na kile ambacho kimezikumba nchi nyingi duniani yaani ‘laana ya raslimali’ (resource curse).

Aidha, akiwa na viongozi wa nchi za Ulaya, Dk Slaa atajadiliana nao kuhusu hali ya Demokrasia, utawala bora na hali ya haki za binadamu nchini hasa kwa kipindi hiki ambapo Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba. Katika ziara hiyo, viongozi hao wa Ulaya watapata fursa ya kujadiliana na Dk. Slaa hali ya siasa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dk. Slaa ameambatana na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene.

Itakumbukwa kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa amekwensa ziarani barani Ulaya akiwa ametoka kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kagera, Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa mfumo wa BVR huku pia akiwahamasisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuhakikisha wamejiandikisha.

Alitumia pia ziara hiyo kukagua maandalizi ya chama katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Dk. Slaa atarejea nchini tarehe 15.06.2015.

Wazanzibari waishio Marekani waendelea kutafuta maendeleo na ustawi wa jamii Zanzibar


Tulipokuwa skuli tulifundishwa kuwa, ili tuendelee tunahitaji mambo manne: Ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Jumuiya ya Wazanibari Waishio nchini Marekani (ZADIA) inauelewa fika umuhimu wa maneno hayo ya hekima, na ndio maana uongozi wake bora, kwa kutambua jukumu lake, daima umekuwa mbioni katika kutafuta na kubuni mbinu za kusaidia maendeleo nyumbani Zanzibar.

Kwa vile kuwa na watu tu haitoshi kuleta maendeleo ya nchi, ndio maana ZADIA imelipa kipaumbele swala la afya na ustawi wa jamii, kwani bila kuwa na watu wenye afya bora hatuwezi kufikia maendeo.

Kwa mantiki hiyo, kama ilivyoelezwa siku zilizopita, uongozi wa ZADIA ulifanya mawasiliano na Shirika la Pure Ultrasound la nchini Marekani na kufikia makubaliano ya kimsingi ya kuwapatia wataalamu wa Zaznzibar vifaa vya Ultrasound na mafunzo ya kuvitumia vifaa hivyo.

Na kama inavyokumbukwa, ujumbe wa shirika hilo tayari umeshatembelea Zanzibar katika hatua za awali za kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuisadia Zanzibar katika uwanja huo.

Katika kufuatilia hatua za utekelezaji wa makubaliano hayo, Mwenyekiti wa ZADIA Bwana Omar Haji Ali, kwa mara nyengine alikutana na uongozi wa Pure Ultrasound mnamo tarehe 18 Mei, 2015.

Katika mkutano huo, pande hizo mbili zilikubaliana kuwa Pure Ultrasound itatuma mtaalamu wake wa ngazi za juu Visiwani Zanzibar mara tu baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mtalaamu huyo atakaa Zanzibar kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja kwa ajili ya kufanya utafiti wa kimkakati kuhusu mahitaji ya vifaa vya tiba katika hospitali za Zanzibar, pamoja na mafunzo yanayohitajika kwa wataalamu wetu katika fani hiyo.

Upande wa Pure Ultrasound, unaomba kama ikiwezekana, wakati mtaalamu wao atakapokuwa Zanzibar akutane na uongozi wa ngazi za juu wa Wizara ya Afya, kuanzia Waziri, Naibu wake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya. Aidha, wanaomba kukutana na Mkuu wa Kitengo Cha Huduma Za Dharura (Director of Emergency), wakuu wa Hospitali zote, watunga sera za afya pamoja na Wakuu wa vitengo vya Upasuaji (Surgery)

Baada ya tarehe ya kuwasili mtaalamu huyo nyumbali Zanzibar kupangwa, ZADIA itawasiliana na Wizara husika kwa ajili ya maandalizi ya lazima kwa ujumbe huo.

MAPENDEKEZO

ZADIA inatambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kutokana na hali hiyo, ilipendekeza ujumbe wa Pure Ultrasound ufike Zanzibar kabla ya kipindi cha kampeni rasmi za uchaguzi kuanza, na kwamba wataalamu watakaoleta vifaa na na kutoa mafunzo ya jinsi ya kuvitumia wafike baada ya uchaguzi kumalizika. Kwa hali hiyo, tunaomba Maofisa waliotajwa katika taarifa hii, wapangiwe, au wajipangie ratiba zao ili zitoe nafasi ya kukutana na mtaalamu huyo.

ZADIA inapiga mbwiru tu, goma kubwa liko mikononi mwa Uongozi Bora wa Wizara husika. Hivyo, basi, ni vyema kuitumia nafasi hii ikiwezekana kuwepo na mapatano ya mpango huu kuendelezwa kila baada ya kipindi fulani.

Aidha, tuzithanmini juhudi na mchango wao. Kwani katika mkutano na Ndugu Omar, walitoa maelezo ambayo kana kwamba yanaonesha kuwa walidharauliwa, kwa vile mjumbe wao aliyekuja mara ya mwanzo hakupata nafasi ya kukutana na Waziri wa Afya.

Wahenga walisema: "Abebwaye hujikaza". Kwa hivyo, ZADIA inapendekaza kuwa, ili kuwahamasisha wahisani hao, Serikali ya Zanzibar ichangie japo kidogo katika gharama za mtaalamu huyo wakati atakapokuwa akiendeleza utafiti wake, kama vile malazi na chakula.

SHUKURANI

Pure Ultrasound imeelezea shukrani zakeza dhati kwa ukarimu ulioonneshwa na watu wa Zanzibar wakati wa ziara ya mjumbe wake Bi Trisha mwezi April mwaka huu. Halkadhalika mjumbe huyo alitoa shukrani na pongezi maalum kwa Dakta Omar Ali Juma kutokana na umahiri aliouonesha katika taaluma yake. Hivyo basi, Pure Ultrasound itafurahi sana iwapo Dk Omar atakuwa na mtaalamu wao Bi Abiola wakati wa ziara yake Visiwani Zanzibar. Tusisahau kumtayarishia zawadi ya kanga, kwani Bi Trisha zilimvutia sana.

Tupo pamoja kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar.

Ziara ya Kinana katika picha Bukoba VijijiniKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili Bukoba Vijijini kuendelea na ziara yake katika mkoa wa Kagera kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa huo leoWandesha bodaboda wakiwa wamejipanga kwenye eneo la mapokezi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Bukoba Vijijini kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, leoKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana kwa furaha na Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini, Profesa anna Tibaijuka, wakati wa mapokezi yake kuingia wilaya ya Bukoba Vijijini leo, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa iani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera, leo.Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akimuaga, Kada wa CCM, Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela, wakati wa mapokezi ya Kinana, kuingia wilaya ya Bukoba vijijini leoKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Mjumbe wa NEC, ambaye mewahi pia Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Mzee Justine Kamaleki, wakati wa mapokezi ya Kinana kuingia katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia ukumbi wa Bandari, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Bukoba Vijijini, tayari kwa kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini leoMwenyekiti wa CCM wilaya ya Bukoba Vijijini, akitoa utangulizi kumkaribisha kuzungumza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika kikao hicho cha ndani. Kushoto ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza na Mjumbe wa NEC, Nazir KaramagiKatibu wa CCM wilaya ya Bukoba Vijijini akisoma taarifa ya wilaya hiyo wakati wa kikao hichoBaadhi ya wajumbe wakimsikiliza Kinana kwenye kikao hichoBaadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hichoKada wa CCM , Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini, Jakson Msome akisalimia baada ya kutambuliwa na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera (kulia)Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye Kikao hicho kabla ya kuendelea na ziara yake katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo. Kinana amewataka viongozi wote kutokuwa na wagombea wao mioyoni katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pia amewataka wapambe wa viongozi kuacha umbea wa kuuza maneno kutoka huku kwenda kule kwa sababu hali hiyo ni chanzo cha fitina miongozi mwa viongozi na wanachama

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi cheti cha CCM, mhitimu katika Chuo Kikuu cha St. Augustine, Amosi Joseph, wakati wa mkutano huo, leo. Jumla ya wahitimu 120 ambao ni wanachama wa CCM walitunukiwa vyeti hivyo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufukia mtaro wa bomba la maji, alipokagua ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Ibwera, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, leoKatibu wa Mradi huo wa Maji, Hassan Omar akimweleza Kinana malalamiko ya wanajiji hicho cha Ibwera kuhusiana na mradi wa maji wa kijiji hicho kuchelewa kukamilika ambapo kwa mujibu wa barua aliyomuonyesha kutoka kwa wasimamizi wa mradi huo, ulipasw auwe umekamilika tangu mwaka jana.

Wananchi wa Kijiji cha Rukoma, wakitangulia mbele ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Katibu Mkuu huyo alipowasili katika kijiji hicho leo, kufungua tawi lao la CCM na kufanya mkutano wa hadhara, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.Katibu Mkuu wa CCM akiwasili kwenye Ofisi mpya ya CCM katika Kijiji cha Rukoma, tayari kwa kuizindua leo.Vijana wa kijiji cha Rukoma wakiwa na furaha ya aina yake wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji hicho leoKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leoKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia katika Ofisi hiyoKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza wakitoka katika Ofisi hiyo.Kijana akiwa amekwea mti kuhakikisha anamuona Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati anahutubia Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini leoKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuhutubia mkutano huo katika kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini leoMbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza akieleza mchango wake aliofanya katika utekelezaji wa ilani ya CCM wakati wa mkutano huo wa Kinana katika Kijij cha Rukoma leo.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kijiji cha Rukoma, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi baada ya kumaliza hituba yake katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba VijijiniKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsikiliza kijana ambaye ni mkulima wa kahawa, baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake katika Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera. Kijana huyo alimweleza kuhusu changamoto wanazopambana nazo wakuliza wa zao hilo husuasan bei ndogo.Wananchi wa Kijiji cha Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, wakimshangilia Kinana alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leoMkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela akizungumzana wananchi katika mkutano huo wa Kinana uliofanyika Kijiji cha Katoro. Mongela amewataka wananchi wote kujiandiksha katika daftari la kudumu la wapigakura, lakini kuwa macho na wageni kutoka nchi jirani ambao baadhi yao wamekuwa wakijaribu kujiandikisha katika daftari hilo, kinyume cha sheriaKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshukuru Sheikh Yassin Baruan wa Kijiji cha Katoro, baada ya kumkabidhi fedha ya mafuta ya magari kusaidia katika ziara ya Katibu Mkuu huo katika kukagua uhtekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera na kwingineko nchni.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo katika Kijiji cha Katoro, wilaya ya Bukoba Vijijini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini leoKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jason Rweikiza wakishikana mikono na makatibu wa CCM waliopo Kata za jimbo hilo, kama ishara ya Katibu Mkuu huyo kuwakabidhi baiskeli makatibu hao, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Katoro wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leo.

 • Picha na maelezo tumeshirikishwa na Bashir Nkoromo