Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 11, 2015Leo: 7 Strategies for dealing with 'toxic people'


By Leo Babauta via ZenHabits

Are there people who constantly criticize you, tell you that you can’t do things, make you feel bad about yourself, even yell at you?

These are toxic people.

Dealing with them is never easy, but it’s such a difficult problem that it’s worth looking at some strategies you might consider.

I was reminded of this problem by a reader recently, who asked, “What if toxic people are my family? How do I shut them out? What if I can’t find the courage to rise above them?”

I have to confess, there aren’t any easy answers. I’ve used a number of strategies in my life, and I’ll share what I’ve tried:
  1. Practice self-compassion when you’re feeling bad. This is always my first step these days, as I’ve learned how useful this method is. Think about it: if you’re feeling bad because of someone else’s behavior, you might show your anger or irritation in your actions and words, and that only makes that person more likely to be toxic. Your bad feelings are not only horrible for you, but for the situation. So try this when you notice you’re feeling bad from someone else’s actions/words: turn inward and notice your feelings, instead of avoiding them. What do they feel like in your body? After a minute, try creating a feeling of love towards yourself. Wish yourself happiness, and an end to your suffering. Wish yourself a life of joy and peacefulness. This won’t magically cure the pain, but it’s a good place to start. 
  2. Talk to other people. I’ve found that when I’m hurting, I often don’t want to admit it to other people, but then when I talk to someone about it, I inevitably feel better. So take the plunge and talk to someone. Share your feelings, ask for them to listen, maybe even give advice. The advice doesn’t matter so much as the connection and listening. 
  3. Practice empathy and compassion. Try practicing the same compassion method towards the person who frustrates you. In your heart, wish them happiness. See that they’re also going through difficulties, like you are, and that’s why they act that way. Wish for an end to their suffering. Wish them a life of joy and ease. 
  4. Talk to the toxic person. Once you start to feel more compassionate towards the other person, talk to them. Yes, they might not act in a compassionate and peaceful way towards you, but you can be the better person. You can see that they’re suffering in some way, and are acting inappropriately because of that suffering. Try connecting with them, sharing that you’re having a hard time, asking for their support. This might not always turn out well, but if you do it in a spirit of connection, they might be open to this discussion. 
  5. Model the behavior you want to see. Often I get mad at other people for getting mad at me, and then I’m doing the same thing they are, behaving badly because they behaved badly. Even if I feel it’s their fault, my behavior escalates the situation. So I try to show how to deal with frustration, try to be compassionate with them, try to show a positive way of dealing with things. And often that can have a great effect, even if it’s not immediate. 
  6. Find more positive friends. If all of this isn’t working, it helps to find other people who are more aligned with the way you want to live. People who are creative, entrepreneurial, self-sufficient, excited about things, positive, healthy, happy. Find them in your local running club, yoga or crossfit class, Toastmasters, volunteer organizations. Find them online in various positive communities. Take the plunge and reach out, develop relationships. Buy someone tea or coffee and start a friendship. One by one, nurture the relationships that have a positive influence in your life, and be a positive influence in theirs. I’ve done this in my life, and it’s made a huge difference. 
  7. Cut them out. It’s a harsh thing, but when family members aren’t supportive of me, if they’re constantly critical and angry … and none of the above works … I will just stop seeing them as much. I’ll do my own thing. See other friends. That’s harder to do, of course, when they live with you, but even then you can go out for a run, take a hike and see nature, meditate, create. Don’t let the thinking about toxic people be the thing you focus on all day — put your mind in more peaceful, creative, positive places.

"Jina langu lisiporudi ndani ya chama, nitampigia kampeni Profesa Mwandosya"


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kama CCM haitampitisha kuingia tano bora, atampigia kampeni kwa moyo wa dhati Profesa Mark Mwandosya iwapo ataingia fainali ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.

Membe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya waliojitokeza kumdhamini.

Alisema unapozungumzia viongozi waadilifu nchini, Profesa Mwandosya ni namba moja, kwani amekuwa kiongozi mwenye maadili ya uongozi na mwenye upendo wa dhati kwa wengine.

“Natamka hili kwa moyo wangu wa dhati, jina langu lisiporudi ndani ya chama, nitampigia kampeni Profesa Mwandosya. Sina tatizo lolote hata wakisema mimi nimuachie Mwandosya nipo tayari, kwani ndiyo viongozi wanaotakiwa kama yeye kwa sasa kuongoza nchi yetu,”
alisema.

Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mmoja wa wagombea urais kwa tiketi ya CCM. Wagombea wengi wamekuwa wakieleza kuwa wameamua kuingia kwenye mbio hizo kwa kuwa hawajaona mgombea mwenye sifa zaidi yao.

Wakati akitangaza nia ya kugombea urais mkoani Lindi, Membe alisema: “Nimetafakari sana kuhusu urais nimeona niombe. Nimejilinganisha na watu wengine wote wanaotia nia, na baada ya kumpitia mmoja baada ya mwingine, nimeona Lindi tuna nafasi ya kuchukua na kuwa na kiongozi wa juu Tanzania.”

Na baada ya kuzungumza kwa kirefu aliuhoji umati akisema, “nani kama Membe?” na kujibiwa “hakuna”.

Kuhusu mipango yake kwa Mkoa wa Mbeya, alisema anatarajia kuboresha huduma za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa kuwa ni kitovu cha uchumi.

Awali katibu wa CCM wa mkoa, Alhaji Mwangi Kundya alisema jumla ya wanachama 877 walijitokeza kumdhamini Membe licha ya kwamba wanaotakiwa ni 30 tu.


Nyimbo za Ngoma Africa Band za kumuaga Rais Kikwete


Ujerumani, Kuliungua shoka mpini ukabaki!

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani, wapekaua nyimbo mbili mpya za kumuaga Rais Jakaya Kikwete atakayemalizaa muda wake wa awamu ya nne mwishoni mwaka huu, 2015.

Nyimbo hizo zipo katika single CD iliyopewa jina la "LA MGAMBO" ambayo nyimbo mbili (1) " La Mgambo J.K anamaliza Kazi..."(rumba) na (2) J.K Tunatamba Nae (Dance) ni utunzi wa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja, akiimba kwa kushirikiana na Afande Chris-B ambaye pia ni mcharaza solo gitaa mahiri nayetisha katika upigaji wa gitaa lake.

Katika kunogesha nyimbo hizo, kikosi kizima cha Ngoma Africa band aka FFU kimeifanya CD hiyo mpya ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete kuwa na mdundo unaotingisha kimataifa!

Kamanda Ras Makunja na Afande Chris-B wanaichana mistari katika nyimbo hizo na kusindikizwa na mlio wa muziki unaotingisha anga kwa kumrusha hewani Rais Jakaya Kikwete na kuifanya bendi hiyo kuwa bendi ya mwanzo kumtungia Rais Jakaya Kikwete nyimbo za kumuaga.

Wasiliana nao at [email protected] 

Wimbo wa kwanza


Wimbo wa pili


Taarifa kutoka kwa "Msema Kweli"

Picha za Rais Kikwete alipokutana na Watanzania The Hague, UholanziWatanzania waishio Uholanzi walikusanyika siku ya Jumatatu Juni 9, 2015 katika hoteli ya Crowne Plaza jijini The Hague kukutana na kumsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa nchini humo kwa mwaliko wa Mfalme Willem-Alexander

Mwalimu ajeruhiwa na wafugaji walioingiza mifugo eneo la shule

CHAMA cha Walimu Tanzania CWT wilayani Kahama, kimewaonya vikali wananchi wanaovamia maeneo ya shule kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha kuwepo uvunjaji wa amani kati ya jamii na walimu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Kahama,Victor Tandise,baada ya kumtembelea nyumbani Mwalimu Mashaka Mziba wa shule ya Msingi Bumbiti Kata ya Mondo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Mwalimu Mziba anatibisha majeraha makubwa aliyojeruhiwa baada ya kupigwa vibaya na wachungaji wa mifugo waliovamia eneo la shule na kulisha mifugo yao na baada ya kuwatoa alishambuliwa kwa kipigo hali iliyosababisha kujeruhiwa.

Kufuatia hali hiyo Tandise amesema ili kuepuka hali hiyo wananchi wanapaswa kuheshimu mipaka ya shule kwakuwa maeneo hayo ni mali ya wana jamii ambayo haipaswi kuingiliwa ovyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ya Mondo said hamad amewataka Maafisa watendaji wa Vijiji na Kata kuhakikisha wanaimarisha ulinzi wa amani katika maeneo ya watumishi wa serikali ikiwemo makazi ya walimu.

Katika tukio hilo watuhumiwa wote waliomshambulia Mwalimu huyo wametoweka na kutelekeza mifugo yao ipatayo 58 iliyokuwa imeingizwa kwenye shamba hilo la shule ingawa mmiliki wake amejitokeza na upelelezi unaendelea.

New Book: 'The Story of Swahili' by John M. Mugane


The Story of Swahili — 2015

By John M. Mugane

Swahili, or more properly Kiswahili, was once an obscure littoral dialect of an East African Bantu language. Today more than one hundred million people use Swahili, making it one of the few truly international languages: Swahili is to eastern and central Africa what English is to the world. How this came about and why, of all African languages, it happened only to Swahili is the story that John M. Mugane sets out to explore.
The remarkable adaptability of Swahili has allowed Africans — and others — to tailor the language to their needs, extending its influence far beyond its place of origin. The Story of Swahili calls for a reevaluation of the widespread but fallacious assumption that cultural superiority, military conquest, and economic dominance determine the prosperity of any given language.
The Story of Swahili is about where languages come from, where they are now, and where they are headed, using the success of Swahili as a convenient point of entry. As a language that arose from contact between peoples from diverse cultures, Swahili is an excellent conveyor of the history of communities in eastern and central Africa as well as their associations throughout the Indian Ocean world. It is also a vibrant, living language that continues to adapt to the changing demands of global trade, technology, and communication.
Find more about the book at ohioswallow.com


First seen at the Udadisi blog

Chikawe ahukua fomu za kuwania Urais Tanzania 2015


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ameongeza idadi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaoendelea kuchukua fomu katika Makao Makuu ya Chama hicho huko Dodoma, kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kupewa tiketi ya kuwania Urais wa Tanzania mwaka huu.

Pichani juu ni Chikawe akionesha kabrasha lake baada ya kukabidhiwa fomu husika.

Serikali kuziadhibu shule zitakazotoza ada kwa fedha za kigeni

Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Betty Machangu akitoa hoja Bungeni Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Serikali itazichukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia Shule na vyuo vyote vya elimu nchini, vitakavyobainika kutoza ada kwa fedha za kigeni bila idhini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anne Kilango Malecela (Mb) alipokuwa akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bungeni leo.

Katika swali lake, Mhe. Rita Kabati (Mb) alitaka kujua ni shule ngapi na vyuo vya Elimu hapa nchini ambavyo vimeruhusiwa kutoza ada kwa fedha za kigeni.

Mhe. Malecela amesema serikali haijawahi kutoa kibali cha kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa shule au vyuo isipokuwa kwa shule zile zilizoanzishwa kwa ajili ya kuhudumia watoto wa mabalozi, maofisa wa ubalozi na wanafanyakazi kutoka mataifa ya nje walioko nchini, ambazo hutumia mtaala wa kimataifa na kutoza ada kwa fedha za kigeni.

Amezitaja shule zinazotoza ada kwa fedha za kigeni kuwa ni Dar es Salaam Internationa School, International School of Tanganyika, Haven of Peace International School na Laureate International School and Educational Trust Fund.

Mhe. Malecela amesema kuwa nyaraka na miongozo ya elimu iliyowahi kutolewa na Kamishna wa Elimu kwa lengo la kusimamai utekelezaji wa sera ya elimu haijawahi kutoa kibali cha kutoza ada kwa fedha za kigeni.

Amesema hata waraka wa elimu Na. 10 wa mwaka 1998 unaohusu “mabadiliko ya ada kwa shule na vyuo vya ualimu vya binafsi na walaka wa elimu Na. 19 wa mwaka 2012 unaohusu “ongezeko la ada kwa shule zisizo za serikali” zilitoa viwango vya ada kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu vya binafsi kwa fedha za kitanzania kuzingatia kuwa utoaji wa elimu ni huduma na si biashara.

Amesema kuwa hata utozaji wa ada katika vyuo Vikuu unaodhibitiwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), viwango vya ada vinavyotakiwa kutozwa ni kwa fedha za kitanzania tu. Lengo ni kumuwezesha kila mtanzania kupata elimu stahiki bila kikwazo.Selasini, Mrema wamtaka Rais Kikwete amwajibishe Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro

Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mhe. Joseph Selasini, akiwaonyesha waandishi wa habari mkataba wa ubia kati ya Raia wa China na anayedai ni mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.

Georgina Misama, MAELEZO - Dodoma

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameombwa kumwajibisha mara moja Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwn. Leonidas Gama kwa kutumia vibaya madaraka yake na kujiingiza kwenye biashara chafu ya kupora na kuwapa wawekezaji wageni ardhi ya wananchi mkoani humo. Ombi hilo limetolewa leo na Mbunge wa Rombo, Mkoani Kilimanjaro Mhe. Joseph Selasini alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari wa Bunge, Mjini Dodoma.

Aidha, Mhe. Selasini ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imchunguze mkuu huyo wa mkoa pamoja na watendaji wote wa serikali ambao amedai wametumia madaraka yao vibaya, kuwatapeli wananchi ardhi na kutumia isivyo halali fedha za Halmashauri za Wilaya ya Rombo shilingi million 168 kuanzisha kampuni binafsi.

Amesema Mkuu huyo wa Mkoa aliilazimisha halmashauri ya Rombo kutoa fedha hizo shilingi millioni 168 kuwalipa fidia wanaushirika wa Lokolova waliotoa kwa hiyari yao, kwa Rais Jakaya Kikwete ardhi heka 140 kwa ajili ya kujenga soko la kisasa.

Amesema hata hivyo, bwana Gama ameshiriki katika kuanzisha kampuni binafsi ya ubia ya kujenga na kuendesha soko hilo inayomilikiwa na wananchi wawili raia wa China na Mtoto wa Mkuu huyo wa Mkoa. Kampuni hiyo imeanzishwa bila kushirikisha Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ambayo alitoa fedha za kulipa fidia wala wananchi wa rombo.

Amesema wakati alipokwenda China kuwatafuta wawekezaji hao, Bwn. Gama alitumia fedha za Halmashauri ya Rombo na nembo ya serikali ya mkoa imetumika katika kuanzisha kampuni hiyo binafsi.

Mhe. Selasini amesema pia kuwa, Bwn. Gama amefuta ushirika wa Lokolova na kuunyang’anya ardhi uliokuwa nayo eka 2100 ingawa Waziri Mkuu ameagiza ushirika huo urejeshwa. Mhe. Selasini aliyeambatana na Mbunge wa Vunjo, Mhe. Augustine Mrema amesema kuwa, kuna tetesi kwamba kampuni hiyo binafsi imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kulipa fidia lakini shilingi milioni 168 zilizotolewa na Halmashauri ya Rombo haijulikani zimefanyiwa nini. Mbunge huyu amesema yeye hapingi uwekezaji katika jimbo la Rombo lakini anataka uwekezaji huo uwe shirikishi wananchi waukubali na wawe wabia au wanufaike na ajira zinazotokana na uwekezaji huo.

Ushauri huo ulitolewa pia juzi na Waziri kivuli wa Wizara wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Halima Mdee wakati akiwasilisha bajeti ya kambi ya upinzani. Pia Mhe. Mrema amewasilisha leo Hoja binafsi kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, Spika, Mheshimiwa Anna Makinda amesema kama alivyoahidi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Ardhi juzi kuwa hawezi kulitolea jibu suala hilo mpaka ufanywe uchunguzi kupata ushuhuda na wabunge hao wawe wavumilivu ili wizara iweze kulifuatilia suala hilo.

Foods containing artificial trans fats that's to be avoided


The process that makes partially hydrogenated oils creates “trans” fats that aren’t found in nature. The resulting oil works beautifully in donuts and pie crusts, for frying oil, and to make margarine. Because it can stand in for “unhealthy” saturated fats, it became extremely popular, and is only recently being phased out. (Those saturated fats turned out not to be so unhealthy, but that’s another story.)

By the way, there is a family of trans fats that are found in nature, especially in dairy products. These, including conjugated linoleic acid, seem to be somewhere between harmless andbeneficial. That complicates labeling because you can’t make everything trans fat free, nor should you try to. When we’re talking about the “bad” trans fats, we mean the artificial kind in partially hydrogenated oils.

These trans fats have been linked to heart disease, and possibly diabetes and obesity. It’s hard to say for sure if trans fat is the culprit, since it tends to be part of a diet that includes a lot of junk food, like fried foods and mass-produced cupcakes. It’s possible that trans fat isn’t as bad as everyone is making it out to be, but it makes this list because nobody is defending it.

The USDA has trans fat on their naughty list (they were one of the “solid fats” in SoFAS—saturated fat was the other—and are still on the list of things to avoid in the new guidelines). The World Health Organization concurs. Meanwhile, anybody in favor of “natural” foods, from paleo to vegan and beyond (Food Babe: check) recommends avoiding them and the processed foods they’re part of.

5 THINGS ABOUT TRANS FATS AND THE FDA'S PROPOSED PHASE OUT


WASHINGTON (AP) -- There are a lot fewer trans fats in the nation's food than there were a decade ago, but the Obama administration is moving toward getting rid of them almost entirely.

The Food and Drug Administration says Americans still eat about a gram of trans fat every day, and phasing it out could prevent 20,000 heart attacks and 7,000 deaths each year.

The FDA originally proposed in November 2013 to phase out trans fats over time. The agency says it will make a final decision by June 15.

Five things to know about trans fats and the government's proposed effort to get rid of them:

---

WORST KIND OF FAT: Scientists say there are no health benefits to trans fats, which are used in processing food and in restaurants, usually to improve texture, shelf life or flavor.

Trans fats can raise levels of "bad" cholesterol and lower "good" cholesterol, increasing the risk of heart disease, the leading cause of death in the United States. Trans fats are widely considered the worst kind for your heart, even worse than saturated fats, which also can contribute to heart disease.

The fats are created when hydrogen is added to vegetable oil to make it more solid, which is why they are often called partially hydrogenated oils.

---

NO BLANKET BAN: To phase the fats out, the FDA made a preliminary determination in 2013 that trans fats no longer fall in the agency's "generally recognized as safe" category, which covers thousands of additives that manufacturers can add to foods without FDA review. Once trans fats are off that list, any company that wants to use them would have to petition the agency to allow it. That would phase them out almost completely, since not many uses are likely to be allowed.

FDA officials said the agency may phase the fats out more quickly for some foods than others, depending on how easy it is to find substitutes.

---

WORST OFFENDERS: Think baked goods, microwave popcorn and fried foods. Over the years, trans fats have been most plentiful in foods like frostings, which need solid fat for texture, or in those that need a longer shelf life or flavor enhancement. Popular foods that have historically contained trans fats are pie crusts, biscuits, microwave popcorn, coffee creamers, frozen pizza, refrigerated dough, vegetable shortenings and stick margarines.

Trans fats also have been used by restaurants for frying. Many larger chains have stopped using them, but smaller restaurants may still get food containing trans fats from suppliers.

---

MOST OF IT IS ALREADY GONE: The Grocery Manufacturers Association, the main trade group for the food industry, says that food manufacturers have voluntarily lowered the amounts of trans fats in their products by 86 percent since 2003. Food companies are using other types of oils to replace them.

That reduction was helped along by FDA's decision to force labeling of trans fats on food packages in 2006. There have also been local laws, like one in New York City, banning the fats. Retailers like Wal-Mart have reduced the amount they sell.

---

INDUSTRY PLANS TO ASK FOR EXCEPTIONS: The Grocery Manufacturers Association is working with food companies on a petition that would ask the FDA to determine if there is a "reasonable certainty of no harm" from some specific uses of the fats. A spokesman for the group would not specify what the industry plans to ask for, but said the FDA encouraged food companies to submit a petition.

The advocacy group Center for Science in the Public Interest first petitioned FDA to ban trans fats nine years ago. The group's director, Michael Jacobson, praised the industry's efforts so far in reducing the fats but said federal action is necessary.

A phase out would be "the single most important thing the FDA has done about the healthfulness of our food supply," Jacobson said.

---
BY MARY CLARE JALONICK
ASSOCIATED PRESS
Follow Mary Clare Jalonick on Twitter: http://twitter.com/mcjalonick

Dk Hassy Kitine atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania 2015

KADA wa Chama cha Mapinduzi na Waziri wa zamani Dk Hassy Kitine jana alichukua fomu za kuwania Urais na kusema akikosa Rais haumwi hata kidogo kwanza hakuutaka wamemlazimisha tu.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu alisema ameamua kugombea Urais kutokana na kulazimishwa ndiyo maana hata akikosa hawezi kuumwa, hivyo alilazimika kuingia kwenye siasa kutokana na shinikizo la watu waliomtaka kuwa kiongozi. Alisema yeye si kama wagombea wengine wanaosema kuwa wameoteshwa ili kuweza kugombea. .
“Nikiukosa Urais siwezi kuumwa hata kidogo kwanza sikuutaka wamenilazimisha tu”
“Sikuwahi kuoteshwa kugombea Urais”
“Sikuoteshwa wala kufanya chochote nilifikiria kuendelea na utaalam tu kwani nilisoma nikiwa yatima ila nilipata presha za kunitaka niwe kiongozi.
“Nikinyimwa urais siumwi hata kidogo ni presha za watu tu hata mkininyima na sijawapa hela yoyote sawa, lakini hakuna thamani ya fedha unaweza kuipa kura yako, kura yako ina thamani zaidi ya fedha”

Aidha alisema Rais anayekuja awe na uadilifu wa asili:
"mtu fisadi na mla rushwa anaonekana tu."
Aliwataka Watanzania kumchagua kwani ni msomi aliyesoma nje ya nchi. Anasema aliwahi kumwambia baba wa Taifa kuwa akisoma na kurudi nchini atakuja kufundisha na aliporudi kweli alifundisha.
“Mimi ni msomi niliyetaka kuandika vitabu lakini nilipata msukumo wa kugombea Urais.”
“Mimi sio mwanasiasa nilikuwa ni mtaalam wakaja wanasiasa wakanishawishi nigombee Ubunge.”
“Nimeamua kugombea ili kusaidia kuijenga nchi” 
alisema.

Alitaka wagombea wote kupimwa afya zao na kufanyika kwa midahalo katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza:
“Nikiwa Rais nitapitisha sheria wabunge wazungumze lugha zote mbili, ni lugha ambazo zinatumika kimataifa”.
“Ni lazima viongozi wajue Kiingereza vizuri na si kubahatisha bahatisha tu

Rais Mkapa alimteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Utawala Bora na baada ya Tume ya Jaji Warioba kumchunguza juu ya mianya ya rushwa, jambo hilo lilimsikitisha na kujiuzulu. 
“Wanaochukua rushwa hawasemi wanasema watu wengine, nachukia sana rushwa na ufisadi.
Alisema alikuwa Mkuu Usalama wa Taifa kwa muda mrefu na anayechukia rushwa na kwamba watu hawamchukii kwa sababu ana sura mbaya bali kutokana na tabia yake ya kusema ukweli.

Alisema sasa nchi inavurugwa na mambo ya kipuuzi na sasa Watanzania wamekuwa wabaya zaidi ya wanyama.

Amekuwa mwanachama wa CCM tangu akiwa shuleni, na kati ya wanafunzi waliofukuzwa na Baba wa Taifa.

  • Taarifa ya Sifa Lubasi, Dodoma


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 10, 2015

Baada ya kutatua mgogoro wa maji, Nassari akaribishwa kwa sherehe

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwahutubia wananchi wa kata ya Leguruki na King'ori baada ya kufanikiwa kuvunjwa kwa bodi ya maji uliokuwa ikihudumia vijiji 15 katika jimbo hilo. 

WANANCHI wa vijiji vya Leguruki na King’ori katika wilaya ya Arumeru wameandaa sherehe kubwa kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari baada ya kutatua mgogoro wa maji uliodumu kwa muda mrefu katika vijiji 15 vya wilaya hiyo.

Sherehe hiyo iliyoenda sanjari na shughuli za kimila ilishuhudiwa mbunge huyo pamoja na mkewe Anande Nnko wakivishwa maazi ya kimila pamoja na kukabidhiwa rungu huku mkewe akikabidhiwa kibuyu pamoja na ijiti cha kimila.

Uamuzi wa wananchi hao unatokana na Mbunge Joshua Nassari kutatua mgogoro kwa kuunda timu ya viongozi wa dini, mila, vijiji na kuamua kuwapeleka Dodoma na kukutana na Waziri wa Maji, Waziri wa Tamisemi na Waziri wa Nishati na Madini kwa ajili ya mazungumzo.

Safari ya viongozi hao ndio iliyozaa kuvunjwa kwa iliyojiita bodi ya maji yaliyofadhiliwa na shirika la OIKOS East Africa kwa vijiji 15 katika wilaya hiyo huku ikiwalipisha wananchi kwa lita.

Mbali na kutozwa fedha kwa wananchi hayo bodi hiyo pia ilidaiwa kusababisha baadhi ya wananchi kuwekwa rumande kwa hila huku mbunge huyo akipambana na kufanikiwa kuwatoa.

Katika sherehe hiyo viongozi wa mila na dini walimsimika Nassari huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkno katika mapambano ya kupigania wananchi wa Meru ili kuondokana na hali ya umaskini.

Akizungumza katika hotuba yake, Nassari alisema Bodi ya Maji imevunjwa na kauli ya Waziri wa Maji: "wananchi ndio wenye Mamlaka ya mwisho kimaamuzi."
“Linapokuja swala la namna bora ya kuchangia na sio kulipia, ikizingatiwa mradi huu ulijengwa kwa nguvu za wananchi bila malipo yeyote kwa miaka 3 wananchi wanapaswa kupata huduma hii ya maji”
alisema Nassari.

Nassari alitumia sherehe hiyo kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa huku yakiombewa na kuwekwa wakfu ili yakawe sehemu ya uponyaji kwa watu wa Arumeru Mashariki.

Wananchi wamekiri kwa umoja wao "hawajawahi kupata Mbunge Kama Nassari baada ya Japhet Kirilo.
Mamia ya wananchi wakimsikiliza mbunge Joshua Nassari wakati akizungumza katika mkutano huo.Mbunge Joshua Nassari alitumia pia mkutano huo ,kukabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa katika jimbo la Arumeru Mashariki. 
Mbunge Joshua Nassari akiwa na mkewe Anande Nnko wakati wa sherehe ya kimila iliyoandaliwa na wananchi katika jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wa maji uliokuwepo katika baadhi ya vijiji .

  • Taarifa kutoka kwa Dixon Busagaga

Gama azungumzia taarifa ya kudadali ardhi iliyotolewa Bungeni na Mdee

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akizungumza na wanahabari (hawako pichani) juu ya tuhuma zilizoibuliwa bungeni dhidi yake.

SIKU moja baada ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kumlipua mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama kwa madai ya kufanya udalali na ufisadi katika uporaji wa ardhi ya wananchi ,mkuu huyo amejitokeza mbele ya wanahabari na kukanusha tuhuma hizo.

Katika utetezi wake Gama alirejea kauli yake aliyoitoa miaka sita iliyopita ya kuwa yeye ni msafi huku akiitupia mzigo halmashauri ya wilaya ya Rombo tuhuma za kiasi cha shilingi mililioni 500/= zilizotajwa kutolewa wawekezaji wa Kichina kama fidia kwa wananchi katika ardhi kilipojengwa kiwanda cha kutengeneza Saruji.

Alisema tuhuma zilizotolewa Bungeni dhidi yake si za kweli na kwamba ni za kisiasa huku akitaja sababu ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni kutokana na juhudi zake za kupambana na Pombe haramu katika wilaya ya Rombo pamoja na urejeshwaji wa wafanyabiashara katika Soko la Kati la mjini Moshi.
“Nataka niwaambie hii ni siasa,zipo issue nyingi zilizochangia kuibuka kwa haya mambo ,lakini nawaambieni mbili tu,Issue ya kwanza Pombe Rombo,na msimamo wangu juu ya Pombe Rombo ndio imeza hii,la pili nisoko la Moshi mjini,watu wana agenda zao kwenye soko hilo, wananchi wamerudi pale, imewaumiza watu.”
“Watu walitaka Pombe ya Gongo iharalishwe, mimi nimesema hadharani anayetaka pombe ya Gongo ihararishwe si mwenzetu mu mshughulikie kwa maana si mwenzetu sasa hili limeleta nongwa”
alisema Gama.

Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo ,Gama amekiri mtoto wake aliyetajwa kwa jina la Mayunga Leonidas Gama kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda hicho huku akihakikisha kiwanda hicho kinajengwa katika mkoa wa Kilimanjaro badala ya Bagamoyo kama walivyopendelea
wawekezaji hao.
“Kiwanda cha saruji kinachojengwa pale Rombo, nilikuwa na uwezo wa kukipeleka popote ninapotaka mimi, lakini mimi binafsi ndiye niliyefanya juhudi kiwanda kile kijengwe Kilimanjaro, mimi binafsi na wala sio mtu mwengine, nimefanya juhudi hizo kwa lengo la kuongeza ajira kwa wananchi na kuinua uchumi wa mkoa huu”,
“Historia ya Kiwanda hiki iko wazi, na nililipeleka hadi kwenye kikao cha ushauri wa mkoa (RCC), nanaomba nieleweke kwamba, ni juhudi zangu na za mtoto wangu, nilitamka kwenye kikao kile na wala sikuficha, mtoto wangu ambaye ametajwa yeye ana rafiki yake wa kichina, wala si kweli kwamba hii kampuni mimi nimekwenda kuichukua China kwa gharama za serikali.”

Alisema katika kikao hicho (RCC), Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walishiriki katika kikao hicho na kwamba baada ya mvutano ndipo makubaliano yakawa kiwanda kijengwe wilaya ya Rombo
“Toka siku ile mimi kama mkuu wa mkoa nikakabidhi madaraka wilaya yaRombo,kwa hiyo shughuli zote za ujenzi ,shughli zote za kutafuta viwanja ziifanywa na halmashauri ya wilaya ya Rombo na siyo Gama”
alisema Gama.

Alisema waliolipa fidia na kununua viwanja ni halmashauri ya wilaya na hata eneo kilipojengwa kiwanda hicho ni mali ya halmashauri ya wilaya ya Rombo na si cha mwekezaji kama inavyoelezwa.
“Nimeelezwa kweye tuhuma kuwa nimepewa milioni 500,hii ni hadithi ya kisiasa ,sijapokea kiasi hicho cha fedha wala sikijui,hata hizo hisa 20,000 nilizoambiwa ninazo kwa kweli sina, kama ningekuwa nazo ni haki yangu kwa sabau sijavunja sharia lakini sin ahata hisa moja.”
alisema
Gama.

“Swala mtoto wangu kuwa na hisa si dhambi na ni haki yake kisheria, kwa sababu yeye ndiye aliyewatafuta hao watu na ni rafiki zake, wala si mimi niliyewaleta kama amenunua hisa huko ni hiari yake,mimi sina hisa kama Gama, sijapokea milioni 500/= kama gama,mimi si dalali na kama ni
udalali wa ardhi hiyo itakuwa ni halmashauri ya wilaya ya Rombo na si gama.”

Alipoulizwa endapo kama halmashauri ya wilaya ya Rombo itakuwa inamiliki sehemu ya hisa katika kampuni hiyo kutokana na utolewaji wa ardhi yake ,Gama alisema wenye majibu ni halmashauri ndio watakuwa wanajua ni mikataba gani wameingia na wawekezaji hao.

Kuhusu eneo la Uwekezaji wa soko la Lokolova, Gama alisema ameshangazwa na kauli za kuwa yeye ni fisadi wa ardhi katika eneo hilo wakati makubaliano ya kuanzishwa kwa soko la kimataifa na ji mdogo wa kibiashara ulipitishwa katika kikao cha RCC ambacho pia Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema alihudhuria na kusifia mpango huo.

Sakata la Kiwanja cha Mawenzi, Gama alisema yeye kama mkuu wa Mkoa, alichokifaya ni kuishauri Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kufuata Sheria za umilikishwaji wa Ardhi ili kuepusha Halmashauri kufilisiwa kwa kukiuka taratibu.

Juzi wakati akiwasilisha bungeni maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti yay a wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2015/2016, msemaji mkuu wa kambi hiyo Halima Mdee alimrushia tuhuma Gama za kuhusika katika kutumia fedha za serikali kwenda nchini China kutafuta watu wawili wanaotajwa kama wawekezaji.

Katika taarifa hiyo Mdee alidai katika hali isiyo ya kawaida nay a kushangaza watu hao katika ardhi iliyokwisa lipiwa fidia kwa fedha za umma ,ilianzishwa kampuni binafsi ya Jun Tu Investment International Company Ltd .

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga

Niambie Live Show EP 4

Omby Nyongole, Henry Kente na Salma Moshi

Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.

Ni Niambie Live...

KARIBU


Taarifa ya habari Channel TEN Juni 9, 2015 na Asubuhi Njema Juni 10, 2015