Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 12, 2015

Mulenda achukua fomu ya CCM ya kuwania Urais wa Tanzania 2015

Mkurugenzi wa Kampuni ya High Quality Consultancy Limited (HQCL) Leonce Mulenda juzi alifika katika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho ili kukiwasilisha katika kinyang'anyiro cha kumpata Rais wa Tanzania mwaka huu.

Gazeti la MwanaHALISI Online linaripoti kuwa Leonce Mulenda, ujio wake wa kuchukua fomu ulikuwa wa kushtukiza. Hakutangaza nia wala kuweka taarifa zake wazi mapema kwani hata kwenye ratiba ya leo jina lake halikuwemo, bali lilingizwa baadaye.

Amefika mchana wa saa nane, na kukabidhiwa fomu yake kasha akazungumza kwa kifupi akisema, iwapo atapata nafasi hiyo atahakikisha CCM inakuwa imara.
“CCM haitakuwa joka la mdimu, tutahakiksha Serikali inatekeleza ilani yake na watumishi wa umma wakati wote wataongozwa na sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa,”
alisema.

Mulenda ameongeza kuwa, kinyume na hilo mtumishi huyo atakuwa anajichimbia kaburi lake.

Amesema, serikali yake kupitia ilani ya CCM, itakuwa ni sikivu, makini na inayojali shida za watu huku akijinasibu kuendeleza elimu.

Peter Nyalali achukua fomu ya CCM ya kuwania Urais Tanzania 2015

Peter Nyalali, mtoto wa Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, hayati Francis Nyalali majira ya saa 7:00 mchana wa juzi alifika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dodoma na kukabidhiwa fomu yake ya kuomba kuteuliwa na CCM ili kuwania Urais wa Tanzania mwaka huu.

Gazeti la MwanaHALISI Online linaripoti kuwa Nyalali ambaye si maarufu katika medani za kisiasa kama ilivyokuwa kwa baba yake mzazi, naye alipata muda wa kuzungumza na waandishi wa habari, akisema kugombea nafasi hiyo ni haki yake kikatiba, anataka kukuza demokrasia pamoja na kuleta mabadiliko chanya katika nyanja mbalimbali.

Amesema alikuwa afisa mwandamizi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) hadi mwaka 2007, alipomuomba Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama atoke nje ya jeshi ili alitumikie Taifa katika nafasi nyingine.
“Mwaka 2010, niligombea ubunge Temeke, nikashika nafasi ya tatu. Mwaka huohuo nikagombea uspika lakini chama kikaona nipishe nafasi hiyo kwa kuwa ilikuwa zamu ya mwanamke,”
amesema.

Alipoulizwa sababu za kuamua kugombea nafasi ya juu zaidi, Nyalali amesema alipogombea ubunge alipata kujua mahitaji ya Watanzania ni nini.

Akijibu kwa nini hakutangaza nia mapema kabla ya kuchukua fomu ili afahamike kama walivyofanya makada wenzao, Nyalali amesema siasa ni sayansi na kwamba siyo wote wanaomchagua rais.
“Watanzania wengi wananifahamu, nina kundi kubwa na nianaomba vyombo vya habari vinitangaze,”
amesema.

Tofauti na wagombea wengine wanaoongozana na makundi ya watu na msafara wa magari, Nyalali alifika makao makuu ya CCM kuchukua fomu yake, akitumia usafiri wa gari ndogo ya kukodi (taksi).

Tumia Coca-Cola na aluminium foil kuondoa kutu kwenye chuma [hapa kuna video]

Inashauriwa kutumia:

  • Diet Coke ili kuzuia kunata kwa sababu Coke ya kawaida ina sukari inayosababisha kunata.
  • Aluminium foil ili kuzuia mchubuko kwenye chuma unachoondoa kutu.

Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 11, 2015


CAG asema Wananchi wanalaumu "hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wafujaji au wanaotumia mamlaka vibaya"

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (aliyesimama) akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria na Ofisi yake katika kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za nchi. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Bibi Felista Tirutangwa na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Ofisi ya Rais, Bw. Stephene Likunga (Kulia).

Ofisi ya CAG yaendesha mafunzo kwa taasisi wadau wa usimamizi wa sheria


Na Mwandishi wetu

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imeendesha mafunzo ya siku moja ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria juu ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na jinsi ya kuitafsiri yanayofanyika katika Hoteli ya Den France jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad alisema kuwa mafunzo yanalenga kuwapa ufahamu juu ya ripoti za ukaguzi ambazo Ofisi yake inazitoa, na jinsi ya kuzitafsiri na kushughulikia masuala ya maadili yanatokana na ripoti za ukaguzi.

Prof. Assad aliongeza kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa kuzingatia Kifungu cha 27 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008, kama ilivyofanyiwa mabadiliko na Sheria ya Fedha Na. 10 ya mwaka 2010.

Kwa mujibu wa kifungu hiki, kinawataka wakaguzi wanaofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara tu wanapobaini kuwepo kwa viashiria vya ulaghai/kugushi au rushwa wanapokuwa wanafanya ukaguzi kutoa taarifa kwa CAG.

Kifungu kinaongeza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akithibitisha kuwepo wa viashiria hivyo anapaswa mara moja kuvitaarifu vyombo vya dola vya uchunguzi na nakala ya taarifa hiyo kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.
“Kifungu hiki kinaeleza vyombo hivyo vya dola (DCI/PCCB) kufanya uchunguzi wa kitaalamu juu ya tuhuma hizo na kukamilisha zoezi la uchunguzi ndani ya siku 60 tangu siku ya kwanza. Mara baada ya kumaliza uchunguzi huu vinapaswa kuwasilisha ripoti yao kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa ajili ya maamuzi ya hatua za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa. Mkurugenzi wa Mashitaka anapaswa kwa mujibu wa kifungu hiki kumtaarifu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu juu ya hatua alizochukua,” 
Prof. Assad alifafanua.

Washiriki wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri wakimsikiliza kwa makini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (aliyesimama). Mafunzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam.


Prof. Assad alisema kuwa utekelezaji wa kifungu hiki kwa sasa unaendelea ingawa wakuu wa Taasisi wadau waliona ni vyema kuwepo na mpango maalumu wa utekelezaji wake. Kwa mujibu wa CAG, mpango huu utaongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa matakwa ya sheria ya ukaguzi.

Prof. Assad aliongeza kuwa licha ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kupongezwa kutokana na utendaji kazi wake, hata hivyo, kumekuwa na malalamiko kuwa hakuna hatua za kuridhisha zinazochukuliwa. 
“Kwa mujibu wa maoni ya wananchi wa kawaida, hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaobainika kufuja mali za umma au kutumia mamlaka yao vibaya kama ripoti hizo zinavyokuwa zinaonesha,”
alisisitiza.

Prof. Assad aliongeza kwa kuzingatia maoni hayo, mafunzo hayo yanategemea kuboresha ufanisi katika utendaji kazi kwa washiriki wa mafunzo. Aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo wakiwa sehemu ya wadau katika maendeleo ya Tanzania hawana budi kusimamia uwajibikaji na kusimamia utawala bora ili kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi.

Prof. Assad aliongeza kuwa mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
“Naishukuru sana USAID kwa kufadhili mafunzo haya kwani yanachochea uelewa wa namna bora ya kutafsiri ripoti za ukaguzi na kushughulikia masuala ya maadili yanatokana na ripoti hizo,” 
aliongeza Prof. Assad.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Ofisi ya Rais, Bw. Stephene Likunga alimuomba CAG kuendelea kutoa mafunzo hayo kila wakati ili kuwaongezea uwezo wataalam wanaotumia Taarifa za Mkaguzi Mkuu.
“Tunaomba mafunzo haya kuwa endelevu ili kuwa tija katika kuchambua kwa kina taarifa zako kwa kina kwa faida ya umma,” 
alisema.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri.


  • Taarifa hii tumeshirikishwa na SAIDI MKABAKULI - NAOT

MUCOBA FC yatwaa kombe la Muungano Mufindi

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita katikati akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wa mashindano ya kombe la Muungano Mufindi timu ya Mucoba Fc ,wa kwanza kulia ni mratibu wa mashindano hayo aliyestaafu rasmi Daud Yassin na mdau mkubwa wa soka mkoa wa Iringa Feisal Asas

Na MatukiodaimaBlog  -- MASHINDANO ya kombe la Muungano Mufindi yamefikia tamati baada ya timu ya benki ya wananchi wilaya ya Mufindi (MUCOBA FC) kuibukwa mabingwa wa fainali ya mashindano hayo kwa kuigagadua (kuifunga) timu ya Academ kutoka Dodoma kwa jumla ya magoli 2-0.

Huku mratibu wa mashindano hayo Daud Yassin akitangaza kustaafu rasmi nafasi yake hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 19 hivi sasa.

Mratibu huyo aliweza kuwaaga rasmi wapenzi wa mpira wa miguu katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa wa shule ya msingi wambi mjini Mafinga. 

Yassin aliwashukuru wadau wote wa soka waliomsaidia kwa namna moja au nyingine kwa miaka 19 aliyoratibu mashindano hayo.

Alisema pia anawashukuru viongozi mbalimbali, chama cha soka wilaya ya Mufindi, chama cha soka mkoa wa lringa, shirikisho la soka nchi TFF, na ZFA kwa kuonyesha ukaribu wao kwa kipindi chote cha mashindano hayo.

Pia aliwaomba radhi wadau wote ambao walikwazika kwa utendaji wake endapo alikosea katika utendaji wake na kuwa haikuwa makusudi yake kuwakwaza .

Amesema kwa sasa hatajihusisha na mambo ya soka tena katika wilaya hiyo kwani kazi aliyoifanya kwa kipindi cha miaka hiyo 19 ni kubwa na wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa umetangazwa zaidi kupitia mashindano hayo.

"Nimejifunza mengi mwaka huu mambo yalikuwa magum sana japo anawashukuru wale waliomsaidia kufanikisha na kuwa atawaandikia rasmi kuwashukuru.....Wakiwemo viongozi wa kisiasa mbunge wa kaskazini Mahamudu Mgimwa na mjumbe wa NEC na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini kwa kumsaidia kufanikisha mashindano hayo kwa mwaka huu "

Mgeni rasmi katika fainali hiyo mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita mbali ya kumshukuru mratibu huyo wa kombe la Muungano Mufindi ,Yassin pia alipongeza wadau wote ambao wameyafikisha hapo mashindano hayo na kuwa wilaya ya Mufindi imeweza kutangazwa vilivyo kupitia soka.

Hivyo aliwataka wadau wa soka wilaya ya Mufindi kuangalia uwezekano wa kuendeleza mashindano hayo baada ya mratibu wake kustaafu rasmi na kuwa akiwa mkuu wa wilaya hiyo atahakikisha mashindano hayo yanaendelea japo ushauri wa mratibu huyo utaendelea kuhitajika zaidi.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza timu ya Mucoba Fc ilipata zaiwa ya kombe kubwa, pesa taslim kiasi cha Tsh milioni 5, jezi seti nne na medali, wakati mshindi wa pili Dodoma Academy ikipata kiasi cha Tsh milioni 2.5, seti tatu za jezi pamoja na medali wakati mchezaji bora akipata kiasi cha Tsh 500,000.Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita akikabidhi kombe kwa mabingwa timu ya MUcoba FCMkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita akikabidhi kombe kwa mabingwa timu ya MUcoba FCMratibu wa kombe la Muungano Mufindi Daud Yassin akitangaza kustaafu nafasi yake hiyoMabingwa wa mashindano ya kombe la Mungano Mufindiwashindi wa pili wa mashindano ya kombe la Muungano Mufindi timu ya Dodoma Academ wakipita kuvishwa medali na Feisal Asas

Mwalimu wa timu ya Mabingwa wa fainali ya Muungano Cup akipongezwa

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Francis Godwin

Shughuli za watu ndani ya ziwa lenye mawimbi makali, ziwa NyasaMtoto mkazi wa Rupindu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe akicheza kando ya ziwa nyasa wakati mawimbi makali yakipiga