Resume Writing ChecklistSource: www.essaymama.com/

Mjumbe wa AU aporwa jijini Johannesburg na 'polisi bandia'

Mjumbe mmoja wa Umoja wa Afrika (AU) kutoka Nigeria, ameripotiwa kuporwa na watu waliovalia mavazi ya polisi katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mjumbe huyo kwa jina la Gabriel Gundo, alikumbwa na mkasa huo alipokuwa akisafiri kutoka uwanja wa ndege wa OR Tambo kuelekea Sandton ili kuhudhuria mkutano wa AU.

Gundo mwenye umri wa miaka 55, alisimamishwa na waporaji waliovalia mavazi ya polisi na kuporwa fedha dola 500 za Kimarekani alizokuwa amebeba pamoja na noti kadhaa za fedha za ndani ya nchi.

Msemaji wa idara ya polisi amearifu kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika kuhusiana na tukio hilo. [via TRT Kiswahili]

Mwalimu aliyezaa na mwanafunzi ajiua baada ya kumuua mtoto; Mama alaumiwa

Forwarded message:

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mnaida, ndugu Lucas iliyoko Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara amejinyonga hadi kufa.

Inasemekana kabla ya kujinyonga yeye alimnyonga kwanza mwanae wa kiume anaesoma darasa la tano halafu akajimaliza yeye.

Chanzo cha kufanya hivyo ni wivu wa mapenzi.

Miaka ya nyuma kidogo mwalimu huyo alimpa mimba binti aliyekuwa mwanafunzi ambae alimzalia mtoto huyo, baada ya kitendo hicho alimrudisha binti huyo shule akamsomesha yeye kuanzia form one hadi chuo, baadae mke wake huyo alipata kazi kama askari upelelezi, hapo ndo matatizo yalipoanzia.

Mwanamke alianza visa vya kumjengea mazingira ya kuachana nae, ikafika mahali kwa wenzake anamtambulisha kama kaka yake ili asijulikane kama ni mke wa mtu mbaya zaidi mke wake huyo alianza kumdai jamaa aseme ni kiasi gani cha fedha alizitumia kwa ajili yake ili amlipe.

Ndipo mwalimu huyo alipofikia uamuzi wa kujinyonga

Sababu za kumnyonga na mtoto kwa taarifa za watu wa pembeni ni kujenga mazingira ya kumuumiza mke wake huyo kwani kifo chake kisingeweza kumgusa kabisa huyo mke wake.

Inauma sana ila there is no way, kila dada kwa nini mnakuwa vyanzo vya matatizo? hapa simaanishi wote ila asilimia kubwa yenu huwa mkiwa na maisha duni mnakuwa wanyonge ila wanaume zenu wakijitolea mkafikishwa mlipokuwa mnapataka mnakuwa miiba.

Serious imeniuma but SINA MAANA KUWA WANAUME NI WAZURI AU WANAOFANYA HIVI NI WANAWAKE WOTE.BUT MOST OF WOMEN MNABADILIKA SANA.

Taarifa ya Habari Channel TEN Juni 12, 2015


Ofisi ya Waziri Mkuu: Pinda chukua fomu CCM kuwania Urais Tanzania 2015

Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akiwa ameshika fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12, 2015. Kulia ni Mkewe Tunu na kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Oganaizesheni), Bw. Mohammed Seif Khatib.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amechukua fomu za kuomba kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Waziri Mkuu Pinda alikabidhiwa fomu hizo leo (Ijumaa, Juni 12, 2015), saa 4:03 asubuhi kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Oganaizesheni), Bw. Mohammed Seif Khatib na saa 4:05 akaweka saini kwenye daftari la kupokea nyaraka ili kuthibitisha kuwa amezipokea.
Saa 4:07 alikabidhiwa mkoba wenye nyaraka hizo na Bw. Khatibu na saa 4:08 akaunyanyua juu mbele ya waandishi wa Habari waliokuwepo kwenye ukumbi wa Katibu Mkuu wa CCM kushuhudia akipokea fomu hizo. Kisha saa 4:15 aliingia ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kukutana na wanahabari.

Akizungumza na waandishi wa habari na wanaCCM waliofika ukumbi wa NEC kumsikiliza mara baada ya kuchukua fomu hizo, Waziri Mkuu alisema endapo atafanikiwa kuteuliwa na CCM awanie kiti cha Urais atasimamia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Uchumi ili unufaishe makundi mengi zaidi ya jamii.
“Ukuaji wa uchumi uko vizuri lakini umaskini unapungua kwa kiasi kidogo, kasi yake hairidhishi… hii ni kwa sababu ukuaji huo umegusa sekta zisizogusa maisha ya watu moja kwa moja kama za ujenzi, utalii, uchukuzi na nyinginezo,” 
alisema.
“Wataalamu wa mataifa yaliyoendelea wanatuambia ukuaji wa uchumi hauonekani sana kwa sababu unagusa maisha ya watu wachache, sasa hivi wanataka jitihada ziongezwe kwenye jamii kubwa zaidi ambazo ni wakulima, wavuvi, wafugaji, wajasiriamali na warinaasali,” 
alisema.
“Mimi naamini tukiwagusa hawa impact kubwa itaonekana, ajira zitapatikana kwani viwanda vya usindikaji vitakuwepo; kilimo kikiboreshwa kwa kutumia zana za kisasa wengi watafanya kazi hiyo ambayo hivi sasa kila mtu anaikimbia kwa sababu ya shuruba za kazi yenyewe.”


Alisema Mpango wa Kwanza wa Maendeleo na Ukuzaji Uchumi ulilenga kuimarisha miundombinu zikiwemo barabara, bandari na ndani yake kulikuwa na mpango wa kuunganisha makao makuu ya mikoa yote kwa barabara za lami ifikapo mwaka 2018.

Alisema mpango huo ulioasisiwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ni wa miaka 25 (2000-2025) lakini ilibidi Rais Kikwete augawanye katika awamu tatu za miaka mitano mitano kuanzia kwama 2011 -2015 sababu muda uliobakia ulikuwa ni miaka 15 tu.
“Kwa maoni yangu kazi iliyokwisha kufanyika ni nzuri lakini tusibweteke. Chini ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Uchumi, mambo yatabadilika na ikiwezekana hatutafika 2025 kwa sababu maji, elimu, afya vitakuwa vimeboreshwa tayari,” 
aliongeza.

Akigusia kuhusu Ilani ya CCM, Waziri Mkuu alisema hawezi kuiongelea kwa sababu bado haijatoka. “Lakini ninaahidi, pindi ikitoka na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM, na Mungu akijalia nikapitishwa na chama, sitashindwa kuitekeleza Ilani hiyo. Nina uzoefu wa Ilani zote zilizopita,” 
alisisitiza.

Alisema kufanya kazi kwa karibu zaidi na Marais wote wanne na uwepo wake kwenye Serikali za Mitaa kwa muda mrefu ni turufu pekee anayoamini itamuwezesha kuwahudumia Watanzania vizuri zaidi kwani anaifahamu nchi kwa undani pamoja na matatizo yanayowakabili Watanzania walio wengi.

Alisema anaamini Mungu peke yake ndiye ajuaye nani amemuandaa kwa ajili ya kuiongoza nchi hii na kwamba hata yeye bado anamtumaini Mungu amuongoze katika safari hiyo. “Mungu peke yake ndiye anajua nani amemuandaa kwa nafasi hii, ni siri yake. Kadri itakavyompendeza, atampa nafasi hiyo yeye amtakaye,” alisema.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L. P. 980,
IJUMAA, JUNI 12, 2015.Kansiime agoma kushuka kwenye gari aliloomba lifti mpaka...


Kinana jimboni Kyerwa

Wananchi wakimsalimia kwa shauku, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, alipowasili Uwanja wa michezo, kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Kaisho, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.

Makala ya Chahali kuhusu Dk Mwele: Ndoto kuwa mtafiti hadi mwanasayansi kimataifa, sasa mwania UraisMapema wiki hii, mwanasanyansi wa kimataifa Mtanzania, mwanamama Dokta Mwelecele (Mwele) Malecela, alitangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa kuomba ridhaa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM. Dokta Mwele ambaye hadi wakati anatangaza uamuzi huo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ana historia ya kipekee ambayo nilibahatika kuifahamu kupitia chapisho moja lililopo katika blogu hii. Hata hivyo, chapisho hilo ambalo lilisomwa na maelfu ya watu, lilikuwa katika lugha ya Kiingereza. Makala hii ni marudio ya chapisho hilo kwa lugha ya Kiswahili. Maelezo hayo yanatoka mdomoni mwa Dkt Mwele mwenyewe ila mie nimetafsiri tu kwa Kiswahili.

Ajira yangu katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ni hadithi ya bahati yenye matokeo mazuri ambayo awali haikuwa katika nia yangu. Nilijiunga na taasisi hiyo mwaka 1987 baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika stadi ya wanyama na tabia zao (BSc in Zoology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1986. Baada ya usahili mzito, nilipangiwa kufanya kazi Kituo cha Amani (Amani Centre), hususan kushughulikia ugonjwa unaofahamika kama Bancroftian Filariasis. Nilishawahi kusikia kuhusu ugonjwa huo nilipokuwa mwanafunzi UDSM chini ya uangalizi mzuri wa Mhadhiri Dokta Parkin lakini sikujua nini nitafanya kuhusiana na ugonjwa huo. Kichwani mwangu, nilitamani kufanya kazi kuhusu ugonjwa wa malaria ambao kwa wakati huo nilidhani ulikuwa eneo la kuvutia kiutafiti. Kwahiyo, lazima Nikiri kwamba nilifadhaika kujikuta nashughulikia ugonjwa wa Bancroftian Filariasis badala ya malaria, ambayo ilikuwa na nyenzo nyingi kwa maana ya vifaa na ufadhili. Hata hivyo, niliambiwa bayana kuwa lazima nishughulikie kufufua shughuli ya ugonjwa huo wa Bancroftian Filariasis hapo Amani.Nikiwa mtu ninayependa kukabiliana na changamoto, nikaanza safari ndefu ya kupita Milima ya Usambara, kuelekea sehemu hiyo inayoitwa Amani.Safari ilikuwa katika mlolongo wa kupanda na kushika vilima kama mawimbi vile hadi wakati flani sikuona watu wala makazi. Hofu yangu ilipunguzwa na mandhari mazuri, misitu ya kupendeza, na hewa ilivyokuwa mwanana kadri tulivyopanda milima. Nilipofika Amani, hofu yangu ilinirudia tena, nikijiuliza iwapo ningemudu kweli kumudu maisha katika sehemu hiyo ambayo ilikuwa kama mafichoni kwa wakati huo. Nilijifariji mwenyewe kwa kujikumbusha kwamba sehemu hiyo tayari ilikuwa na wanasayansi kadhaa, na wamemudu kuishi hapo, Kwahiyo nami ningeweza pia. Baba yangu alikuwa na msemo maarufu, ‘Ni juu yako kumudu mazingira yanayokukabili,’ na hivyo ndivyo nilivyoamua kufanya.Baada ya wiki kadhaa za mafunzo ya kuelewa mazingira, hatimaye nilipangiwa kufanyakazi katika maabara ya minyoo (helminthology laboratory) ambapo nilijifunza kuhusu parasaiti aitwaye Wuchereria Bancrofti, ambaye ndiye anayeeneza ugonjwa wa Bancroftian Filariasis. Nikajifunza kutambua hatua za awali za mzunguko wa maisha ya parasaiti huyo na mwingine aitwaye Onchocerca Volvulus. Nikajifunza kupasua mbu kwa ajili ya ucuhunguzi wa lava wa maambukizi na utambuzi wa mabara wa parasaiti mbalimbali, kama vile wa kichocho (schistosomes), minyoo ya tumboni (hookworks), trikurisi (Trichuris), nk. Wakati huo, dunia yangu ilikuwa dunia ya minyoo, na watu walioniinghiza katika dunia hiyo walikuwa miongoni mwa wajuzi wa mabara na wasaidizi wa mabara, ambao walinipatia mafunzo bora kabisa. Nathamini mafunzo hayo kwa sababu yamesaidia sana kunifanya kuwa mtu niliye sasa. Mmoja wa wasaidizi wa mabara alipendelea kunikumbusha kwamba alianza kazi mwaka niliozaliwa. Haikujalisha walivyonichukulia kama mtoto, nilichukua kila walichoniambia, na nilifurahia kila dakika. Kuna Nyakati familia yangu ilikuwa na wasiwasi kuhusu maendeleo yangu.Niliwapigia simu zile za zamani za mkonga kuwajulisha kuwa nilikuwa naendelea vema na kwa hakika ninapenda mahala hapo.
Kazi zangu za awali zilijumuisha kuchunguza uhusiano kati ya parasaiti wa eosinophilia na helminth. Pia nilichunguza matokeo ya majaribio ya maangamizi ya malaria katika maambukizi ya Bancroftian Filariasis. Pia nilifanya kazi na marehemu Profesa Chris Curtis kudhibiti mbu aina ya Culex katika mji wa Muheza kwa kutumia dawa za kuua wadudu za polystyrene beads.

Baadaye nilikwenda London, Uingereza kufanya Shahada ya Uzamili na ya Uzamifu katika Taasisi ya Magonjwa ya Kitropiki ya Chuo Kikuu cha London, ambapo nilifanyia kazi maambukizi ya filarial kwa paka. Paka hao walikuwa kwa ajili ya majaribio ya uchunguzi ambao ulikuwa muhimu kwa uelewa wa maambukizi ya filarial. Kazi niliyofanya ilikuwa kupata uelewa jinsi parasaiti wanavymudu kukwepa mfumo wa kinga ya mwili wa kiumbe aliyeambukizwa, na matokeo ya uchunguzi wangu yaligundua kuwa kuna molekyuli za kiprotini (immunoglobulins) ambazo zilikuwa zikiwakinga parasaiti husika. Hii ilisaidia kuongoza uelewa kuhusu watu wenye maambukizi ya filarial lakini hawaonyeshi dalili za wazi.

Baada ya kurudi nyumbani, nilijihusisha na kuandaa utafiti wa kuelewa kitu ambacho kwa lugha ya kitaalam kinachoitwa immunoepidemiology ya maambukizi ya ugonjwa wa mabusha.Utafiti huo uliofanyika Kingwende, Kenya na Masaika, Tanzania. Machapisho kadhaa ya kitaaluma yalitokana na utafiti huo uliotuwezesha kufahamu zaidi kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa mabusha, ambao ungetuwezesha kutafuta mbinu bora za udhibiti.Wakati huohuo, nilihusika na kuandaa mpango wa kimkakati kwa ajili ya mradi wa kutokomeza mabusha nchini Tanzania. Hii ilifuatiwa na azimio la Shirika la Afya Duniani Mei 1997 ambalo lilisisitiza kuangamizwa kwa ugonjwa huo.Uaandaji wa mpango huo madhubuti ulifuatiwa na kuteuliwa kwangu kubwa mkurugenzi wa mradi unaohusu maradhi hayo mwaka 2000. Mwaka huohuo, mradi wa kupambana na ugonjwa wa mabusha ulianzishwa katika kisiwa cha Mafia, na mchango wangu kutoka maabara hadi kwenye eneo ambapo utafiti unatafsiriwa kwa vitendo ulitimia kamili. Kuna msemo wa Kiswahili kwamba safari moja huanzisha nyingine. Kwa upande wangu, hakujawa na mwisho wa safari hii bali ni vituo tofauti tu ninaposimama kidogo lakini naendelea mwelekeo huohuo.


Mradi huo wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha ulizidi kuimarika na sasa unafanya kazi katika wilaya 53 na umewafikia watu MILIONI 13. Huku msukumo sasa ukiwa kwenye magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika, njia zilizotumika katika mpango wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha zimepanuliwa na kujumuisha ugonjwa wa kichocho, minyoo wanaosambaa kupitia udongo na trakoma. Kwa kiasi kikubwa, usaili wangu katika makao makuu ya NIMR uliniandaa kwa ajira ya utafiti na udhibiti wa ugonjwa wa mabusha lakini kama ilivyo katika maeneo mengine ya maisha, sikujua hilo kwa wakati huo. Nilipata fahari kubwa pale Rais Jakaya Kikwete alipotangaza kuwa ataanzisha mfuko maalum kwa ajili ya ugonjwa huo kuwasaidia watu wanaosumbuliwa nao. Rais alitoa tangazo hilo katika Mkutano wa kimataifa wa masuala ya afya jijini Arusha, na hii imesaidia kupanua uelewa wa madhila yanayowakabili wahanga wa ugonjwa huo nchini Tanzania na kwingineko barani Afrika. Matokeo kutoka kituo cha uangalizi Tandahimba yanaonyesha mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha umefanikiwa kupunguza maambukizi katika wilaya hiyo, na hiyo itakuwa sehemu ya kwanza ya mafanikio ya kuingilia kati maambukizi kwa upande wa Tanzania Bara.Je hii habari inayoelezea mafanikio? Ni habari kuhusu binti mdogo aliyekuwa na ndoto za kuwa mtafiti; kuhusu msichana aliyepanda vilima vya Amani kusaka ndoto yake, na ya mwanamke ambaye sasa anaishi katika ndoto hiyo kwa kufanya tafiti na kuchangia katika kukabiliana na ugonjwa ambao amekuwa akijishughulisha nao kwa takriban maisha yake yote. Labda hayo ndio mafanikio. Au waonaje?

Nina deni kubwa kwa watu wengi walioniwezesha kufanikisha safari hii, hususan baba yangu Dokta John Malecela na marehemu Mrs Ezerina Malecela ambao walinihakikikisha kuwa "ndiyo, waweza kutimiza ndoto yako."

Hapa chini ni machapisho mbalimbali ya kitaaluma

Malecela M.N. Baldwin C.I and Denham D.A (1994) Hosts antigen on the surface of microfilariae of Wuchereria bancrofti and Brugia pahangi.

Transactions
Awarded prize for best presentation

Baldwin C.I., Medieros F, Malecela M.N. and Denham D.A (1994) Humoral responses in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Parasite 1,1S

Malecela (1995): Microfilariae and the immune response in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Ph.D. thesis, University of London.

P.E.Simonsen, D.W Meyrowitsch, W.G.Jaoko,M.N.Malecela, D.Mukoko, E.M.Pedersen, J.H. Ouma, R.T.Rwegoshora, N.Masese, P.Magnussen, B.B.A Estambale and E.Michael (2001) Bancroftian Filariasis infection,Diseaese and Specific Antibody Response Patterns in a high and a low endemicity community in East Africa. Parasite Immunology 23: 373-388

Michael E., Simonsen P.E., Malecela M., Mukoko D., Pedersen E.M., Rwegoshora R.T., Meyrowitsch D.W, Jaoko W.G., (2001)Transmission intensity and immunoepidemiology of bancroftian filariasis in East Africa. Parasite Immunology No 23. Pp 373-388

Paul Simonsen,Peter Bernhard, Walter Jaoko, Dan Meyerowitsch, Mwele N.Malecela-Lazaro, Pascal Magnussen and Edwin Michael (2002) Filaria Dance sign and subclinical hydrocele in two East African communities with Bancroftian filariasis. Transactions of the Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene

Simonsen,P.E, Meyerowitsch, D.W, Jaoko W.G., Malecela, M.N., Mukoko, D., Pedersen, E.M., Ouma,J.H., Rwegoshora, R.T., Masese.N Magnussen, P., Estambale, B.B.A & Michael E. (2002) Bancroftian filariasis infection disease and specific antibody responses patterns in a high and low endemicity community in East Africa. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene Vol 66(5) pp550-559

Simonsen P.E Meyrowitsch D.W., Mukoko D, Pedersen E.M., Malecela-Lazaro M.N., Rwegoshora R.T., Ouma J.H., Masese, N. , Jaoko W.G., Michael E., (2004) The effect of repeated half-yearly mass treatment on Wuchereria bancrofti infection and transmission in two East African communities with different levels of endemicity. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene No 70 pp. 63-71

Germany closes probe into US hacking Merkel's phone allegations

Germany's top prosecutor Harald Range has decided to close an investigation into whether the United States' National Security Agency eavesdropped on Chancellor Angela Merkel's phone calls.
Prosecutors said they see no prospect of success in continuing to investigate. They noted that journalists involved in publishing Snowden's documents are entitled to refuse testimony, and argued that public statements by Snowden give no indication that he has personal knowledge of the surveillance of Merkel's phone.
via The NPR

Je wajua? Mwanao anavyotumiwa kusambaza dawa za kulevya

Je, unazijua safari zote za mtoto wako wa kiume? Je, siku za mwisho wa juma au mapumziko anakuwa kwenye mazingira yanayoeleweka? Je, hakuna wakati amelioonekana kuwa na vitu kuliko uwezo wa familia?

Basi kama hujui, watoto wadogo wenye umri wa kati ya miaka 10 na 17 tena baadhi wakiwa ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, wamebainika kuwa wanatumiwa na wauzaji wa dawa za kulevya kusambaza dawa hizo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa miezi miwili sasa unaonyesha kwamba baadhi ya vijana walioanza kutumika kusambaza dawa hizo wakiwa wadogo sasa ni wafanyabiashara wanaojitegemea. Mbali ya kutumiwa kusambaza dawa hizo zinazoangamiza nguvu kazi ya taifa, wanatumia dawa hizo.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wauzaji wa dawa za kulevya huwatumia watoto hao kusambaza dawa hizo kutoka eneo moja kwenda jingine kwa kuwa ni vigumu askari kuwatilia shaka na kuwakamata watoto, tofauti na ilivyo kwa watu wazima.

Malipo kwa watoto hao hutegemea umri wao na aina ya dawa wanazosambaza. Wanafunzi wa shule za sekondari wanaotumiwa katika usafirishaji huo hupewa malipo makubwa tofauti na watoto wa umri wa chini ya miaka 13. Malipo kwa ajili ya usafirishaji wa bangi ni kati ya Sh10, 000 na Sh15,000 na wanaosafirisha dawa za kulevya kama heroin na cocaine hulipwa kati ya Sh20,000 na 30,000.

Hata hivyo, imebainika kuwa watoto wadogo ambao wengi ni wa mtaani hawajui kama wanasambaza dawa hizo bali hudhani wanatumwa tu kupeleka mzigo na kupewa fedha.

Mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu (jina limehifadhiwa) ameleza kwamba amekuwa akitumwa na vijana wa eneo la Kinondoni kupeleka mzigo kwa watu, maeneo ya Kimara na Mbezi. “Sisi tunapewaga mzigo na kaka (jina linahifadhiwa) tunaupeleka kwa kaka (jina linahifadhiwa), halafu tukirudi anatupa hela,” alisema mtoto huyo wa umri wa miaka 13, mkazi wa Kinondoni Mkwajuni.

Ushuhuda


Mmoja wa vijana hao (jina linahifadhiwa) ambaye alianza kuuza dawa za kulevya tangu mwaka 2001 alipokuwa na umri wa miaka 13, anasema kwamba mjomba wake ndiye alikuwa akimtuma maeneo tofauti kupeleka mzigo na baada ya kumaliza, alikuwa akipewa Sh10,000.
“Mwanzoni sikuwa nikijua natumwa nini, nikawa natumwa hadi nilipokuwa na miaka 15. Siku moja nikajua ninachopeleka baada ya kumsikia mmoja wa wateja wa mjomba akisema lazima afungue kwanza ndipo niondoke, ili ahakikishe kama kweli ni mali,” 
anaeleza.
“Basi alipofungua niliona kitu kama unga unga mweupe ambao aliunusa kisha akaniamuru niondoke. Sasa wakati naondoka nikamsikia akilalamika kuwa siku hizi anapewa ‘poda’ feki,” 
anafafanua kijana huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 28.
“Nilikuwa na ‘good time’ (maisha mazuri). Nilikuwa na simu, enzi hizo, hata watu wazima hawana simu. Nilikuwa na uwezo wa kununua kitu chochote, siri yangu ilikuwa ni kutumwa tu kupeleka mzigo hapa na pale,” anaeleza kijana huyo aliyehitimu elimu ya sekondari.
“Baadaye niliamua kuhama nyumbani na kupanga nyumba, nikanunua gari na pikipiki kutokana tu na kusambaza unga, bado nilikuwa bega kwa bega na mjomba,” 
anasema kijana huyo ambaye kwa sasa anadai ameacha kazi hiyo.

Polisi

Kamishna wa Polisi Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa anasema kuwa wana usalama wake wamefanya uchunguzi na kubaini kuwa watoto na vijana wadogo wa rika tofauti wanatumikishwa kusambaza dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.
“Tumegundua kuna watu wanawatumikisha hawa watoto, tulizunguka hapa jijini na kupata taarifa kuwa watoto wa rika tofauti wanafanyishwa kazi za kusambaza unga,” 
anasema Kamishna Nzowa na kuongeza kwamba watoto hao wa umri wa hadi miaka 10 hawafanyi kazi ya kusambaza tu, bali pia wananunua dawa za kulevya kwa ajili ya matumizi yao.

Machi 2013, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema kwamba wauzaji wa dawa za kulevya wanaweka dawa hizo kwenye mikate na barafu zinazouzwa kwenye shule.

Lukuvi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika maadhimisho ya Siku ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya alisema Serikali itaanza kufuatilia biashara hizo shuleni.
“Sasa dawa hizi zinauzwa hadi kwenye vitu ambavyo watoto wanakula katika shule za msingi. Kwa mfano, hivi sasa dawa hizo zinawekwa kwenye maandazi, mikate na barafu. Ni lazima kufahamu watu gani wanauza vyakula vya aina hiyo na wana nia gani,” 
alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema kuwa watu hao wamekuwa wakisababisha vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu na alitaja baadhi ya matendo ya ajabu kuwa ni mtoto wa shule kuingia darasani akiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe, kidani chenye nyembe kifuani, misumari mifukoni, hawafungi lisani za suruali zao na wengine kutembea vifua wazi.

Uchunguzi

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili jijini Dar es Salaam maeneo ya shule kwenye wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, unaonyesha kwamba wasambazaji wa kawaida wa dawa za kulevya huitwa ‘mapusha’ wakati watoto wanaotumiwa kufanya kazi hiyo huitwa ‘masadal’. Masadal hupewa mzigo kuuza au wakati mwingine kuusambaza tu na kupewa fedha kwa ajili ya kazi ya usambazaji.
“Kwa siku unaweza kupewa mzigo wa Sh200, 000 au Sh300, 000, ukiumaliza unapewa malipo ya Sh 50,000, basi. Lakini si kila siku unaweza kupewa mzigo, inatokea siku na siku,” 
anasema mmoja wa wasambazaji hao mwenye miaka 16 eneo la Tabata.

Eneo la Kinondoni, Manyanya, Mwananyamala Komakoma kuna idadi kubwa ya vijana wadogo wanaotumiwa kusambaza ‘unga.’ Hata hivyo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura anasema kwamba khajawahi kupata taarifa za watoto wadogo kutumika kusambaza dawa za kulevya.

Walimu

Baadhi ya walimu katika shule za msingi, waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, walisema baadhi ya wanafunzi katika shule zao wana tabia sawa na vijana mitaani wanaovuta bangi.
“Wewe unaona mwanafunzi wako anatembea na vijana wavuta bangi, kwa vyovyote naye atakuwa anashiriki,” 
anasema mwalimu wa shule moja wilayani Temeke.

Mwalimu Mkuu (jina linahifadhiwa) wa shule moja ya msingi eneo la Tabata alikiri kuwa wapo wanafunzi wenye mienendo inayotia shaka na hata baadhi ya wazazi anasema wamekuwa wakifika kushtaki kutokana na mabadiliko ya watoto wao.
“Unakuta mwanafunzi kwao familia ina kipato cha chini, lakini yeye anaishi maisha aghali sana hapa shuleni; ana simu ya gharama, anavaa mavazi ya gharama na wakati mwingine anawapa wanafunzi wenzake fedha. Hapo tunapata wasiwasi huenda ameingizwa kwenye mtandao huo,”
 alisema Mwalimu katika shule moja ya jeshi jijini. 

 Mwalimu mwingine wa shule binafsi katika Wilaya ya Temeke alisema kuwa wachezaji mpira wakiwa na timu za mitaani huvuta bangi kwa kile wanachodai kuondoa nishai na kwamba wapo wanaotumia dawa za kulevya.
“Mimi naijua shule hii… hata wanafunzi wake wengine tayari wanatumia dawa za kulevya,” 
alisema mwalimu huyo.

Ripoti ya hali ya dawa za kulevya inayotolewa na Tume ya Taifa ya Dawa za Kulevya kwa mwaka 2013 inaonyesha kuwa Wilaya ya Kinondoni ina watumiaji 2, 941 wa dawa za kulevya ambao wamesajiliwa na wameanza kupata tiba ya uraibu. Kati ya hao, wanaume ni 2, 162 na wanawake ni 879. Temeke ina watumiaji 2, 963 wakati Ilala ina watumiaji wanaume 453 na wanawake 23.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa Kitengo cha Uhalifu na Dawa za Kulevya (UNODC) kwa mwaka 2013, inaeleza kuwa kuna Watanzania 176 waliokamatwa nchini China kwa kesi za dawa za kulevya. Nako Brazil kuna wafungwa zaidi ya 103 na Hong Kong kuna Watanzania zaidi ya 200 wenye kesi za dawa za kulevya, ambapo kesi 130 zimeshatolewa hukumu na kesi 70 bado zinaendelea.


Bi Monica Mbega achukua fomu CCM ya kuwania Urais wa Tanzania 2015

Monica Mbega (kulia) akifurahi pamoja na wana CCM Iringa mjini ambao walijitokeza kumdhamini kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM 


Monica Mbega: Ikulu ni zamu yangu wengine wasindikizajiWAKATI mbio za makada wa chama cha mapinduzi (CCM) waliotia nia ya kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea kushika kasi kwa kila mgombea kutumia mbinu yake ya kuwafikia wana CCM kuomba udhamini , aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega leo ameingia wilaya ya Iringa Mjini mkoani hapa kuomba udhamini na kupata wajumbe 33 huku akiwataka watanzania kutoaminishwa na mbwembwe za watia nia wenzake wanazofanya mikoani na kuwa yeye ndie Rais wa awamu ya tano baada ya Dk Jakaya Kikwete na kuwataka watia nia wenzake wamuunge mkono.

Mbega ambae alilazimika kusubiri wajumbe 30 wa kumdhamni kwa zaidi ya masaa manne katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari juu ya safari yake hiyo ya kutaka kwenda Ikulu na kudai kuwa amelazimika kuzuia viongozi wa CCM wilaya ya Iringa kutomuandalia mbwembwe zozote wala wapambe wa kumshangilia wakati wa safari yake hiyo ya kutafuta wadhamini.

Alisema kuwa kuwa anamtegemea Mungu zaidi katika safari yake hiyo ya kwenda Ikulu na ndio maana hakupenda kuweka makisio ya gharama za safari nzima ya mchakato huo wa kuelekea kupokea kijiti kwa Rais Dk Kikwete na hivyo ndio sababu ya yeye kuzunguka bila ya mpambe zaidi ya dereva anayemuendesha pekee.
"Naomba niwaelezeni wazi kuwa sina mgombea wa kumuunga mkono kati ya wote waliojitokeza zaidi ya 30 kwani naamini kuwa namba moja kati ya wote hao waliojitokeza ni Monica Ngenzi Mbega ninasema hivyo kwa kuwa nchi ya sasa inahitaji mwamanke kuongoza kwani mwenye kuweza kuvunja makundi ni mwanamke sio mwanaume tena .....mwanamke ni mwepesi wa kusamehe sio mtu wa makundi hivyo kama hivyo ndivyo ukitanguliza upendo makundi hayatakuwepo. Wapo wenye visasi vya kutoka mwaka 2005 ila sio mimi ....mimi nimetanguliza upendo zaidi....mimi ni mama nitaiunganisha nchi na changamoto inayomkabili Rais wa awamu ya tano ni jinsi na kuiunganisha nchi na mimi ndie pekee wa kuunganisha nchi hii"

Alisema kuwa iwapo watanzania wataunganishwa kuwa wamoja kuna uwezekano wa nchi kuachana na utegemezi na hivyo wananchi wake kuwa wamoja na kuweza kushiriki kujiletea maendeleo yao chini ya rais wao Mbega .

Hivyo alisema kuwa iwapo chama chake kitamteua na watanzania wakamchagua na kuingia Ikulu wategemee Tanzania mpya yenye amani ,upendo na mshikamano na uchumi bora kwa kila mtanzania kuongeza pato binafsi.

Mbega alisema kuwa tayari Rais wa nchi Dk Kikwete amepata kuueleza umma kuwa misaada ambayo nchi inapata kutoka kwa wahisani mingine ina masharti magumu na ndio maana ya baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati na kuwa iwapo yeye ataingia Ikulu atajaribu kukwepa misaada hiyo na kulijenga Taifa linalojitegemea lenyewe ili kuto kuwa na miradi isiyo kamilika kutokana na masharti magumu ya wahisani.

Alisema kuwa kikubwa kilichomsukuma kuchukua fomu ya kutia nia kuomba kuteuliwa kuwania Urais ni uzalendo wake katika Taifa wenye shauku la kuliongoza Taifa la Tanzania kama mwanamke wa kwanza toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 bila ya kuongozwa na mwanamke na kudai kuwa hakuna mgombea wa CCM ambae anajambo lake binafsi la kufanya zaidi ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
"Falsafa yangu ni kusahihisha changamoto zinazoonekana katika kutekeleza ilani hatujaweza kufanikiwa hili ....mheshimiwa Rais Dk Kikwete tunaona jinsi anavyotekeleza ilani katika sekta mbali mbali ila utasikia katika vikao vya kamati kuu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuwa kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ilani hivyo mimi nitaanzia kutekeleza changamoto kwanza .....kwani bajeti inayotengwa ndio inapaswa kusimamiwa kwanza mwelekeo mzima wa serikali yangu ni kuona tunapata Taifa la watu wanaojitegemea wenyewe"

Katika hatua nyingine Mbega ambaye aliangushwa nafasi ya ubunge mwaka 2010 na Mbunge Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) alisema kuwa bado ana nguvu ya kurudi kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini na kumshinda mbunge wa sasa mchungaji Msigwa kwani bado nguvu za kurejesha jimbo hilo CCM anazo japo hana mpango wa ubunge zaidi ya kutimiza dhamira yake ya kuingia Ikulu kama Rais aliyokuwa nayo toka mwaka 2005 na alishindwa kuingia mwaka 2010 kwa kumheshimu Rais Dr Kikwete pekee ila sasa ni zamu yake.

Pia alisema CCM bado ina nguvu zaidi katika jimbo la Iringa mjini na Tanzania kwa ujumla na iwapo suala la upendo likawatangulia watia nia wote pale wanapokosa kuteuliwa kuungana kwa upendo kumuunga mkono aliyeteuliwa kamwe suala la wapinzani kushinda litabaki kuwa ni ndoto.Monica Mbega akisisitiza kuwa hakuna zaidi yake

Monica Mbega akizungumza na wanahabari mjini Iringa leo baada ya kudhaminiwa na wanachama zaidi ya 33

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akitoa taarifa ya idadi ya wana CCM waliomdhamini Mbega

Mbega akifurahia orodha ya wana CCM waliomdhaminiBaadhi ya wadhamini wa Mbega IringaKada wa CCM mama Mwalusamba akimuombea dua Monica MbegaMonica Mbega akionyesha orodha ya wadhamini wakeWadhamini wa Mbega IringaHata mimi nimechukua fomu ya Urais :Naibu meya wa Manispaa ya Iringa ambae ni diwani wa kata ya Ilala Bw Gervas Ndaki akifurahia kushika mkoba wenye fomu ya CCM ya kuomba kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, fomu ya Monica Mbega baada ya mgombea huyo kufika mjini Iringa kusaka wadhamini 30 
 • Tumeshirikishwa taarifa hiii na Francis Godwon/Matukiodaima Blog

Makada wa CCM, wameendelea kupigana vikumbo katika ofisi za makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais. Jana ilikuwa zamu ya Balozi Augustine Mahiga na Monica Mbega aliyejitosa kimya kimya.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Monica alisema kuwa endapo atafanikiwa katika kinyang’anyiro hicho, atatekeleza Ilani ya chama na kuendeleza mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne.

‘Nitaangalia changamoto gani ambazo hazikuweza kuleta maendeleo na kuzishughulikia,” alisema. Mbega alisema atafanya hivyo kwa kutumia wataalamu wa ndani ya nchi. Nitatumia watalaamu wa kila aina katika kuiendeleza Tanzania, alisema.

Mbega alisema Serikali ya awamu ya nne imejitahidi kupambana na tatizo la rushwa na yeye akiingia madarakani, ataangalia chanzo cha tatizo hilo na kuongeza nguvu katika hilo.

Mbega alisema hivi sasa tayari vimejitokeza viasharia vya uhasama, mauaji ya albino, wizi, ubaguzi wa dini na ukabila. Alisema ili kuendelea na amani ni lazima kurejesha vitu vinavyojenga amani.

Kwa nini alikosa ubunge?

Alisema siyo kweli wananchi walimkataa, ila utaratibu wa kumpata mgombea ubunge ndani ya CCM, ndiyo ulikua tatizo.
 • via MWANANCHI: Monica Mbega ajitosa urais 

Mayai ya kware kama "kikombe cha Babu" lakini Serikali...


Miaka ya hivi karibuni kulikuwa na gumzo kubwa hapa nchini na hata nje ya nchi juu ya tiba ya kimaajabu maarufu kama ‘kikombe cha babu.’

Tiba hiyo ya kikombe ilikuwa ikitolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile kijijini Samunge Wilaya ya Loliondo. Taarifa za tiba hii zilienea kwa haraka nchi nzima hali iliyowafanya wananchi wengi kila kona kuelekeza macho, masikio na mioyo yao kwenye tiba hii.

Kutokana na uvumi wa maajabu ya kikombe cha Babu, baadhi ya watu walidiriki hata kuwatorosha wagonjwa wao hospitalini.

Wengine wakaacha matibabu na dozi walizopangiwa hospitali kwa magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale sugu na kuamua kukimbilia kikombe cha babu kwa imani, kina uwezo zaidi.

Pia, ikumbukwe kwamba kikombe hakikuwa na tiba sahihi kwani hata Serikali kupitia Wizara ya Afya na taasisi zake zilishindwa kutoa uthibitisho wa kisayansi juu ya ukweli wa tiba ile. Hivi sasa kumeibuka tiba ya ‘mayai ya kwale’ ambayo inavuma kila kona na imekuwa gumzo kila mahali. Tiba hii ni ya kimaajabu kwani uvumi uliopo ni kwamba mayai ya kwale yana uwezo wa kutibu magonjwa yote sugu.

Kasi ya kushauri wagonjwa na hata wasio wagonjwa kutumia mayai haya badala ya kwenda hospitali kwa uchunguzi wa afya zao inaongezeka na maelekezo yanayopatikana mitaani juu ya kutumia tiba hii ni ya ajabu na yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Nilishuhudia mtu mmoja akimwelekeza mgonjwa kuwa alipaswa kuyapasua mayai na kuyapondaponda pamoja na magamba yake na kisha ayanywe katika hali ya ubichi. Mwingine aliambiwa ayapasue na kisha ayakoroge pamoja na asali au maziwa kisha anywe, wengine wanaelekezwa kuyachemsha kama mayai ya kawaida na kisha kula kiini cha ndani. Uvumi huu unaenea kwa kasi mitaani.

Kutokana na kuvuma kwa tiba hii, mayai haya hivi sasa yanaonekana kusakwa kila mahali na yanauzwa kati ya Sh15,000 hadi 20,000 kwa trei.

Uvumi wa tiba hii hauna tofauti na ule uliozuka nchini juu tiba maarufu kama ‘kikombe cha Babu’. Watu wengi walikatisha matibabu kwenye hospitali mbalimbali na kuamua kwenda Kijiji cha Samunge kwenda kupata kikombe cha babu na kufanya kuwe na misururu mirefu ya watu waliokesha usiku na mchana. Hii ilizusha adha kubwa hasa kutokana na kutokuwepo na maandalizi ya vyoo hivyo watu kujisaidia ovyo vichakani.

Adha ya safari ndefu na kukaa kwenye foleni kwa zaidi ya siku tatu, kulifanya wenye afya mbaya kushindwa kuhimili na hata kupoteza maisha.

Katika mazingira haya ya kuibuka tiba za ajabuajabu ambazo hazijathibitishwa kitaalamu, ni vyema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikatoa ufafanuzi.

Isisubiri hadi watu wapoteze maisha halafu ndiyo ianze kuja na maelekezo tena yanayopingana na yale ambayo jamii inaamini. Kuchelewa kunafanya wengi wapoteze fedha na hata kuacha tiba sahihi na kukimbilia kitu ambacho kinavumishwa tu.

Serikali haipaswi kukaa kimya wakati watu wakiendelea kutibiana kwa vitu ambavyo havijathibitishwa kitaalamu.

Kama Serikali ingechukua hatua mapema, watu wasingepoteza maisha kupitia kikombe cha babu.

Uvumi huu wa tiba ya mayai ya kwale hauna tofauti na Kikombe cha Babu.

Katika ulimwengu huu wa utandawazi na soko huria, ni kawaida kusikia mambo mapya yakiibuka kila kukicha, lakini kama mambo hayo yanagusa afya zetu, hatuna budi kuwa makini na waangalifu zaidi.

Mchambuzi ni mwandishi wa gazeti la MWANANCHI (0782124410)Speed up Vodacom, Shivacom probe - MPs orderJune 8, 2015 via The Daily News, Dodoma — THE Parliamentary Committee on Industry, Trade and Economy yesterday ordered speedy investigations into the alleged multi-million scam pitting Vodacom Tanzania and its former super dealer, Shivacom.

The committee tasked the Tanzania Revenue Authority (TRA) and Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) to speed up investigations into the multimillion scam and submit the report before June 20, this year.

Shivacom has come under fire for allegedly printing duplicate airtime vouchers of 500/- and 2,000/- worth millions of shillings, when it was contracted by the telephone company to print and distribute the coupons between 2007 and 2012.

Committee Chairman Luhaga Mpina, presenting the parliamentary committee report on activities conducted by the Ministry of Finance in the current fiscal year and budget estimates for the 2015/2016 financial year during the ongoing sessions of the National Assembly here, asked the two state agencies to hasten the forensic investigations.

Mr Mpina noted with concerns that the two companies have been hesitant to provide information to the government regarding the matter.

"If it is proved that Shivacom printed the duplicate vouchers, it should be subjected to criminal charges since the act is a fraud. It should as well be compelled to pay Value Added Tax (VAT) for the vouchers it sold to the market.

"Vodacom on its part, if proved that it evaded taxes during the period, it should be obliged to pay the due taxes during the period it conducted business with Shivacom," Mr Mpina said.

He went on to note that since Vodacom has produced credit notes and some of the duplicated vouchers with a value of 74m/-, it was evident that there were traces of fraud in the multimillion contract.

"Between 2008 and 2012, Vodacom paid taxes amounting to 118bn/- and yet the value of the 500/- and 2,000/- vouchers was 925bn/-; meaning that the mobile operator should have paid 166bn/- in VAT on these two categories of vouchers alone. "It seems Vodacom does not want to cooperate with the government to pin Shivacom since by doing so might unravel other cases of tax evasion," Mr Mpina charged.

During the five-year contract spanning the year 2007 and 2012, reports have it that the mobile operator incurred a loss of 675b/-, while the government was denied of taxes to the tune of 121bn/- from the 500/- and 2,000/- vouchers.

Subscribers were on the other hand cheated of their money as they bought vouchers which were duplicated and thus unable to use them. Vodacom terminated the contract with Shivacom in July 2012, but it has never come out in public to apologise to its subscribers.

Not sure what Android phone to buy? This Google tool can help


Google has launched a website, android.com/phones/whichphone aimed at helping people pick out a new Android device.

The page asks you to answer 12 questions about how you plan to use your device, and then uses that information to make a suggestion.

Google will ask what you plan to use your device for such as taking photos, social media, or staying fit etc. After each selection, you'll be taken through some questions for that specific task. For example, when you choose "listening to music," Google will ask how many hours per day you plan on listening, and whether on speakers or through headphones. 

After selecting at least three interests, you can then choose which carrier you plan to go with (this step is optional). Finally, Google will offer up suggestions on which phones you may be interested in, with side-by-side comparisons of each specifiction sheet. [via Android Central]


Call for abstracts: New voices in Global Health 2015

The New Voices in Global Health (NVGH) initiative promotes the active participation of young scientists in the World Health Summit (WHS). It is supported by the M8 Alliance of Academic Health Centers, Universities and National Academies. The NVGH is aimed at empowering research, policy and advocacy initiatives among future leaders in global health, who are invited to send in abstracts of their scientific work and ideas.

Selected candidates will present their work in a special poster exhibition, thus playing an active role in the WHS. Abstracts will be published digitally at www.worldhealthsummit.org.

Deadline for applications is July 31, 2015.

Africa Research Excellence Fund Research Development Fellowships

New Programme of Research Development Fellowships funded by the Medical Research Foundation’s Africa Research Excellence Fund

The Medical Research Foundation has recently established the Africa Research Excellence Fund (AREF) to nurture excellent health research by Africans, in Africa with impact for Africa. The AREF is pleased to announce its first programme of AREF Research Development Fellowships.

This is a new opportunity intended to benefit outstanding early-career African researchers. The Programme is designed to enable talented, African researchers who have been awarded their PhD in the last four years to develop their own research ideas and funding proposals. Each AREF Fellowship will support a placement of up to nine months in a leading research organisation in Europe or South Africa.

The deadline for receipt of applications is 1600 hours (GMT) on 8 July 2015. Our first awards will be announced in November 2015.

Ratiba ya kuanza na kumaliza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


BlackBerry considering Android for next smartphone


According to news posted at REUTERS, BlackBerry is considering equipping an upcoming smartphone with Google Inc.'s Android software for the first time, an acknowledgement that its revamped line of devices has failed to win mass appeal, according to four sources familiar with the matter.

The move would be an about-face for the Waterloo, Ontario-based company, which had shunned Android in a bet that its BlackBerry 10 line of phones would be able to claw back market share lost to Apple's iPhone and a slew of devices powered by Android.

The sources, who asked not to be named as they have not been authorized to discuss the matter publicly, said the move to use Android is part of BlackBerry's strategy to pivot to focus on software and device management. BlackBerry, which once dominated smartphone sales, now has a market share of less than 1 percent.

The 100 highest-paid athletes in the world

Ndamukong Suh

Forbes released it's 2015 rendition of the top-100 highest-paid athletes in the world on Wednesday

Here's the top-20:
 1. Floyd Mayweather Jr. (boxing): $300 million
 2. Manny Pacquiao (boxing): $160 million
 3. Cristiano Ronaldo (soccer): $79.6 million
 4. Lionel Messi (soccer): $73.8 million
 5. Roger Federer (tennis): $67 million
 6. LeBron James (basketball): $64.8 million
 7. Kevin Durant (basketball): $54.1 million
 8. Phil Mickelson (golf): $50.8 million
 9. Tiger Woods (golf): $50.6 million
 10. Kobe Bryant (basketball): $49.5 million
 11. Ben Roethlisberger (football): $48.9 million
 12. Rory McIlroy (golf): $48.3 million
 13. Novak Djokovic (tennis): $48.2 million
 14. Zlatan Ibrahimovic (soccer): $39.1 million
 15. Lewis Hamilton (racing): $39 million
 16. Ndamukong Suh (football): $38.6 million
 17. Fernando Alonso (racing): $35.5 million
 18. Gareth Bale (soccer): $35 million
 19. Jon Lester (baseball): $34.1 million
 20. Derrick Rose (basketball): $33.9 million

The full list is available at Forbes Magazine