Siri ya wajasiriamali Albert & Meshack: Kilimo cha miti - Njia ya uhakika kutajirika


Makala ya Albert Sanga & Meshack Maganga, Iringa.

Miezi kadhaa iliyopita kupitia redio moja, Ofisa mmoja wa wizara ya maliasili na utalii aliulizwa swali hili, “Je, inawezekana watu binafsi kufungua mashamba ya miti na kufanya biashara hii ya kuuza miti ya mbao?”

Ofisa huyo alijibu hivi “..inaruhusiwa….hata mimi najilaumu kuwa miaka ile wakati tunapanda msitu wa serikali kule Mufindi mimi sikukumbuka kutafuta maeneo kwa wenyeji nikapanda miti. Kama ningefanya hivyo nadhani leo na mimi ningekuwa milionea”. Mahojiano yale yamenipa hamasa ya kuileta makala hii wiki hii.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu tumekuwa tukiandika makala za hamasa na ujenzi wa fikra kuhusu mitazamo yetu na uthubutu wa kufanikiwa kupitia biashara. Nikiamini kuwa wengi mmeshajenga mitazamo chanya na utayari kuhusu biashara na uwekezaji; sasa nachukua hatua mpya.

Hatua hii ni ya kuonesha na kuchambua tija (pay offs) za fursa mbalimbali za kibiashara. Si mara ya kwanza kueleza kuhusu kilimo cha miti, bali nimekuwa nikikumbushia mara kwa mara ili kutoa fursa kwa wale ambao bado hawajafikiwa na fursa hii.

Kilimo cha miti kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa. Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi.

Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa (carbon dioxide). Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Binafsi tuliichangamkia biashara hii miaka saba iliyopita na ‘We are real serious with it’. Tumejiwekea lengo la kupanda ekari ishirini kila mwaka. Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na baadae imara kiuchumi usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho.

Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (20,000). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na mbili (12,000,000). Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni ishirini na tano (25,000,000) kwa ekari moja.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi laki moja na nusu hadi mbili ka ekari moja kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki nne hadi laki sita. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu!

Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako. Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini.

Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning). Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima.

Miti hukomaa kuanzia miaka sita hadi kumi kutegemea na utunzaji unaoufanya. Hii ina maana kuwa ukichukua shilingi laki mbili unazogharimia shamba kila mwaka ukazidisha mara sita unapata shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000/=) na ukizidisha mara kumi unapata shilingi milioni mbili (2,000,000/=).

Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni kati ya shilingi milioni moja na laki mbili na milioni mbili. Ukichanganya na gharama ya kupata ardhi na kupanda miti yenyewe unapata kuwa gharama nzima hadi unavuna ni kati ya shilingi milioni milioni mbili (2,000,000/=) kwa kadirio la chini.

Hapa ili kuokoa nafasi tumeweka makadirio yaliyochanganya milinganyo ya muda wa kuvuna, eneo unalopata pamoja na thamani ya fedha katika muda husika. Gharama hizi tunazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo bila shaka wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasiya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili n.k.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Miti inasitawi maeneo mengi Tanzania, lakini ukitaka kufanya kilimo hiki watafute waliotangulia, name naamini watakusaidia katika kila hatua. Usisite hata kuwasiliana nasi wakati wowote kwa msaada na maelekezo

Watanzania tunahitaji ushindi wa kiuchumi kupitia uwekezaji!

[email protected] 0766 742 414/ 0719 127 901.
[email protected]

Sababu 10 za kubaki kwenye ajira kabla ya kujitosa kwenye ujasiriamali

By Makirita Amani -- Leo naomba niongee na wasomaji wa KISIMA CHA MAARIFA ambao bado wapo kwenye ajira ila haziwaridhishi na wanataka kuingia kwenye biashara au ujasiriamali. Kwanza nikupongeze sana kama wewe ni mmoja wa watu hawa ambao wanaona kazi pekee haitawawezesha kufikia yale mafanikio makubwa waliyopanga kufikia.

Pamoja na ajira kutokuweza kukufikiahsa katika malengo yako makubwa, pamoja na changamoto nyingi zilizopo kwenye ajira, bado ni muhimu wewe kuendelea kuwepo kwneye ajira hiyo kwa muda kabla hujaiacha na kuingia moja kwa moja kwenye ujasiriamali. Hapa nitakupa sababu kumi kwa nini nakuambia hivi.

Kabla hatujaangalia sababu hizi kumi kwanza tuangalie upotoshwaji ambao umekuwa unafanywa kwa wengi. Watu wengi wamekuwa wakiaminishwa kwamba, kama unataka kuw amjasiriamali mwenye mafanikio, basi unahitaji kuchukua mazingira hatari (risk taker). Kama upo kwenye ajira basi uachane na ajira hiyo na kuingia kwenye ujasiriamali ambapo utaweka nguvu zako zote na kuweza kupata kipato kinachoendana na juhudi zako. Maelezo haya ni ya kweli ila hayamalizii kipande muhimu sana cha maelezo hayo ambacho ni biashara zinazoanzishwa na watu ambao hawana uzoefu wowote wa biashara, kati ya kumi, nane zinakufa ndani ya mwaka mmoja mpaka miwili. Na biashara zinazoanzishwa na watu ambao walishawahi kufanya tena biashara, sita kati ya kumi zinakufa kati ya mwaka mmoja mpaka miwili.

Kuingia kwneye biashara ambayo watu nane kati ya kumi watashindwa, ni hatari kubwa sana kwa mtu yeyote, kwa sababu hii ni sawa na kuwa na uhakika kwamba unakwenda kushindwa kwenye biashara hiyo.

Nimekuwa nikishauri watu wanaoingia kwenye biashara na ujasiriamali kwa muda sasa lakini sijawahi kumwambia mtu aache kazi haraka ili aweze kuweka nguvu zake kwenye ujasiriamali. Nina sababu nyingi kwa nini sifanyi hivyo, na hapa nitakushirikisha sababu kumi.

1. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato cha uhakika. Japokuwa kazi haina uhakika sana kwa sasa, lakini angalau kwa sasa kuna kipato ambacho unakipata kwenye ajira yako. Hiki kitakuvusha nyakazi ambazo ni ngumu, hasa pale ambapo utaanza ujasiriamali ukiwa bado kwenye ajira yako.

2. Kuna nafasi nyingi za kuweza kuanza ujasiriamali hata bado ukiwa kwenye ajira yako. Tumia nafasi hizi na anza kidogo kidogo, jifunze kenye kila hatua unayoshindwa au kukosea, endelea kukuza biashara yako na ikifikia hatua ukaona sasa hapa inaweza kukupatia kipato cha kutosha kuendesha maisha yako ndio unaweza kuacha kazi.

3. Kutoa fedha kwenye biashara changa ni kuiua. Katika miezi angalau sita ya kwanza ya biashara yoyote ndio kipindi ambacho biashara yoyote inakazana kukua. Sasa kama utaondoa fedha kwenye biashara hii kwa sababu yoyote ile, unakuwa umeandika adhabu ya kifo kwneye biashara yako. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato kingine unachotegemea tofauti na biashara hiyo, hivyo kama umeajiriwa, hiki ndio kipato chenyewe.

4. Kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unapokuwa kwneye kazi ni rahisi sana kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unaweza kutengeneza wateja wengi wa huduma au bidhaa zako kupitia kazi unayofanya hivyo inakupa nafasi nzuri ya kuweza kukuza biashara yako.

5. Kufaidi huduma nyingine muhimu. Kuna huduma muhimu ambazo utaweza kuzifaidi kama utakuwa kwenye kazi. Kupitia kazi yako unaweza kuwa unapata huduma ya bima ya afya kwako na kwa familia yako. Hii inakusaidia kuokoa fedha nyingi ambazo ungezitumia kwenye huduma za afya. Japokuwa unaweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya kama mtu binafsi, bado itakugharimu kiasi kikubwa kuliko aliyeko kwneye ajira.

6. Kazi inaweza kukupa uzoefu wa biashara. Kuna baadhi ya biashara unazoweza kuanzisha ambazo zinaendana na kazi unayofanya sasa. Kwa kuwepo ndani ya kazi ile unajifunza mambo yote muhimu ya kuzingatia ili na wewe uweze kukuza biashara yako. Pia unawajua vizuri wateja ambao wanaweza kuja kuwa wateja wako pia na mambo mengine ya ndani ambayo yatakuwezesha kuendesha biashara yako vizuri.

Kuendelea kusoma sababu zilizobaki na hatua za kuchukua kama wewe ni mwajiriwa na hata kama sio mwajiriwa, jiunge na KISIMA, KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA nonyeza hayo maandishi, jaza fomu na tuma fedha ya ada ya uanachama. Kupata makala nzuri na pia kuingia kwenye group la wasap ambalo lina mijadala mbalimbali ya kukuwezesha kufikia mafanikio, lipia ada ya GOLD MEMBER ambayo ni tsh elfu 50 (50,000/=) kwa mwaka.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA
Makirita Amani
[email protected]

Options and Steps to recover Facebook account


1. Use the recovery page

Use your email address or your phone number or your full name and the name of a friend using the revovery page, then change your password (go to Home > Account Settings > General and click > Password).

2. Use "No longer have access to these?"

If you failed on the step above and you no longer have access to the email address and phone number, click the link that says, "No longer have access to these?" to start the recovery process. You will be given the option to answer your security question and reset your password. If you are able to answer your security question, you will have to wait 24 hours before you can access your account.

3. Use three trusted friends

If you can not answer your security question after following the procedure above, Facebook will let you select some trusted friends to help you recover your account. They will receive a security code from Facebook and send it to you. Once you have collected all codes from your three friends, you can submit the codes to Facebook as instructed and reset your password. More information about the whole recovery process on this page in the Facebook Help Center.

4. Report account as compromised

In the event that your account was hacked and is posting spam to your friends walls while you can no longer access it, you should click here to use the page to report  your Facebook account as compromised.

5. Inform others

In case a hacker abuses your account, let your friends know through email, phone chat/texts so they are aware of the situation.

6. Remove suspicious friends/apps

If you befriended unknown people or granted access to a malicious applications which you suspect are behind posting weird stuff on your behalf, remove them (go to > Home >Account Settings > Apps and go through the list to scan and click the X next to any friend or app you wish to remove or click "Edit" to change what the app can do.

Prof. Lipumba achukua fomu ya kuwania Urais Tanzania 2015Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 14, 2015


Recipe and Health benefits of banana flower/blossom

Both the South Asians and Southeast Asians use banana flowers as a vegetable. They use it either raw or steamed with dips. They also use those in soups, curries and fried foods. The flavor resembles that of artichoke. Like artichokes, both the fleshy part of the bracts and the heart are edible.

According to stylecraze.com the following are some of the health benefits of banana flowers:

1. Wards Off Infections:

Banana flowers treat infections, thanks to their ethanol based extracts. Banana flower inhibits the growth of pathogenic bacterias. Some of them are bacillus subtalis, bacillus cereus, and escherichia coli. Banana flower also helps heal the wounds. According to a study, banana flower extracts can also inhibit the growth of the malarial parasite plasmodium falciparum in vitro. These claims are yet to be proven.

2. Reduces Free Radical Activity:

The presence of free radicals in the body can cause serious problems. Fortunately, the extracts of methanol present in banana flower possess antioxidant properties. These flowers perfectly handle free radicals that cause damages to the body. It treats many health issues, such as premature aging and cancer. To make the full use of the antioxidant property of these flowers, include in health supplements.

3. Reduces Menstrual Bleeding:

Menstruation brings pain inmany women. Some suffer from severe PMS symptoms, while others bleed excessively. A cup of cooked banana flowers can help deal with these problems. Cooked banana flowers along with curd or yogurt increases the progesterone hormone in the body and reduces bleeding.

4. Manages Diabetes And Anemia:

Calculated intake of banana flowers reduces blood sugar levels. It also increases the total hemoglobin levels in the body. However, as with antimicrobial activity, the hypoglycemic effects of banana flowers haven’t proven clinically.

5. Rich Source Of Vitamins And Minerals:

Banana flowers contain various vitamins like Vitamin A, C, and E. They also contain potassium and fibers. This makes them an excellent health food and a source of healthy nutrients.

6. Boosts Mood And Reduces Anxiety:

Don’t reach for an anti-depressant, if you are feeling down and out! Try banana flowers instead! Since they contain magnesium, banana flowers reduce anxiety and boosts the mood. They are natural anti depressants without any side effects.

7. Helps Nursing Mothers:

New mothers face many problems when it comes to breast feeding. One of the major problems that they face is dwindling milk supply. Banana flowers boost the supply of milk that helps the new mothers feed their young better.


Ulevi ni janga si Rombo na Nyeri tu! Iran yafungua vituo 150 vya tiba dhidi ya ulevi

Iran yatangaza kufunguwa vituo 150 vya kutoa matibabu dhidi ya ulevi wa kupindukia

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la afya la Iran ni kwamba zaidi ya watu 150,000 ni walevi wa kupindukia.

Iran imechukuwa uamuzi wa kufunguwa vituo hivyo ili kupambana dhidi ya madhara ya ulevi ambayo hivi sasa yamekuwa tatizo kubwa katika jamii.

Wahusika katika shirika la afya la Iran lililifahamisha shirika la habari la Isna kuwa tatizo la ulevi wa kupindukia limekuwa tatizo katika jamii ambalo limekuja na kuibuka kwa kasi.

Alireza Norouzi ambaye ni daktari katika kituo cha kutoa matibabu kwa watumiaji wa vilevi alifahamisha kuwa, katika kituo chake kutatolewa mafunzo kwa watu watakaopewa tiba dhidi ya ulevi.

Kituo cha kwanza cha matibabu dhidi ya ulevi kilifunguliwa kwa mara kwanza jijini Tehran mwaka 2013. [via TRT Swahili]

Wasifu wa Bernard Membe

Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:


1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo:

Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.

Familia:

Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.

Siasa:

Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:

Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi: Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa:

Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uozefu:

2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – hadi sasa: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – hadi sasa: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amekuw mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.