Picha: ACACIA Bicycle Challenge IlivyofanaAfisa mkuu wa uendeshaji wa Acacia Mishel Ash akiwa tayari kwa mbio hizo.Washiriki wa mbio za wafanyakazi wa Acacia wakiwa tayari kuanza mbio hizo ambazo zilikuwa zimepewa jina la “Fun race”

Mmoja wa wafanyakazi wa Acacia aliyeshiriki mbio maalumu kwa wafanyakazi wa Acacia, akifurahia mara baada ya kufanikiwa kumaliza mbio hizo.Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akimkabidhi zawadi Mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanaume, Masunga Duba kutoka shinyanga.

Washindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanaume na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Washindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanaume na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Makamu wa rais wa Kampuni ya Uchimbaji wa dhahabu ya Acacia, Deo Mwanyika (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Acacia, Mishel Ash, (wa pili kutoka kushoto) ambaye pia ni kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu. 

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 16, 2015

Maoni ya Wasomi katika kumpata Rais #TanzaniaElection2015

(image: web2.ges.gla.ac.uk)

WACHAMBUZI wa masuala ya kisiasa, wamekosoa mbwembwe zinazofanywa na baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotangaza nia ya kuomba uteuzi wa kugombea urais kupitia chama hicho, wakisema sio kipimo cha ama wanafaa au la.

Mhadiri Mwandamizi wa Chuo cha Tumaini, Dk. Azavel Lwaitama, anasema pamoja na hekaheka kubwa za wagombea lakini zipo njia za kuthibitisha kufaa au kutofaa kwake.
“Kwanza tujue anatoka chama gani? Chama hicho kina sifa gani lakini pia je aliwahi kutetea maslahi ya umma alipokuwa kwenye uongozi? Na wala si kupelekwa na upepo wa hekaheka zao,” 
anasema.

Dk. Lwaitama anasema, kipindi hiki kila mgombea anataka kuwaonesha wananchi kwamba anafaa lakini pia kwa wananchi wanapaswa kuonesha kuwa wamekomaa.
“Wagombea hawa pamoja na kujitokeza kwa mbembwe lakini tuwapime. Je, ni wasafi kwa kiasi gani? kwanini wanatumia nguvu kujitangaza? Malamiko ya wananchi katika chama hicho aliyateteaje? 
amehoji.

Anasema, wapo wanaojitokeza kutaka kugombea lakini hao hao chama wanachotaka kugombea tayari kimewaita fisadi na chama hakijawasafisha na kimetembea nchi nzima kutaka avue gamba, 
“na wakimpitisha mtu wa namna hii mimi nitawashangaa sana.”

Dk. Lwaitama anasema, wananchi wanapaswa kukumbuka ni kwa namna gani wanaojitokeza walipambana na hoja zinazohusu matatizo yao katika jamii.

Anasema, wapo waliokuwa na nafasi ya kukemea ufisadi ndani ya serikali lakini wakakaa kimya na kwamba, watu wa namna hii kama walikuwa serikalini walishindwa, ni kipi kinachoweza kuwafanywa wananchi wawaamini?
“Rushwa ndio changamoto kubwa, sarafu inashuka, rasilimali zinaporwa, wananchi wanahangaikia huduma za jamii na huyu anayekuja leo kutoka chama hicho alipaswa kuonesha kuchukia kwa vitendo lakini walaa!
“Hao hao walipokuwa ndani walishindwa kukemea rushwa inayosababisha umasikini lakini huku nje wanapiga kelele kwamba wanachukia rushwa,”
 amesema na kuongeza: 
“Mtu wa namna hii hata akija na punda ili kudanganya wananchi, hafai na wala hakuna kuangalia sura. Kama mtu hatukumwona akisimamia ajenda za wananchi, huyo hafai kabisa,” 

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine-Mwanza (SAUT), Dk. Francis Ng’atigwa, anasema, kitu kinachoweza kuwaweka wasaka madarasa hao ni kubeba ajaenda za vyama vya na sio zao binafsi.

Anasema kuwa, sera ndio zinazoonesha vipaumbela kwa wagombea hao na si kitu kingine. 
“Wananchi wanahitaji kusikia sera na sia ajenda binafsi za wagombea. Naamini wagombea wanaobeba ajenda zao binasi watapotea kwa kukosa ‘support’ (kuungwa mkono),” 

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro, Bagesi Gaddafi, anasema jambo la msingi kwa wanansiasa ni kujua matatizo ya wananchi na si kutumia fedha, vitisho na ghiliba isipokuwa ni kuonesha uwezo halisi.

Anasema kuwa, haamini kama Watanzania bado wapo kwenye giza kwa kufuata mkumbo ama mdundo wa sauti unakovuma pasipo sababu.
“Sidhani kama tupo kwenye zama hizo, zama za sasa ni zama za kuchanganua mambo. Kwa bahati nzuri vyama vya upinzania vimekita mizizi kwa kiwango cha kutosha,” 
anasema Gaddafi.

Mhadhiri huyo anasema kuwa, siasa za Tanzania kwa sasa zina sura tofauti. 
Sura iliyopo ni ya kuhoji na kutaka majibu ya hapo kwa hapo.
“Unaweza kuona tu uchaguzi wa Serikali za Mitaa matokeo yake, angalia watu wa vijijini wanavyokesha kusubiri kuandikwa katika daftari la wapiga kura, hapa ndio unaweza kutathmini tuelekeako,”
amesema.

Uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais umepangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, na tayari makada wa vyamba mablimbali wanaendelea na hekeheka za kutangaza nia pamoja na kuchukua fomu kuomba kuteuliwakuwa wagombea.


Kipanya amwuliza Baba yake ikiwa ilani ya CCM inatekelezeka...


Mapera, maparachichi... hakuna kama vya asili nyumbani!


Picha kutoka kwa mdau aliyeko huko Kilimanjaro.Why and How to to disable Windows 8.1 SmartScreen

While searching for tip on how to disable the 'smart screen' on Windows 8.1 because it was just annoying, I also learned something.

Over at kioskea I found how to turn this feature off (listed below), but also that,
...a computer security expert [said], the SmartScreen filter also informs Microsoft about the software downloaded and installed on Windows 8.1. During this process, the data transfer (over HTTPS) between your computer/tablet running Windows 8.1 and Microsoft's servers can be intercepted by hackers.

STEPS ON HOW TO TURN IT OFF

Go to go to:
  1. Control Panel 
  2. System and Security 
  3. Action Center 
  4. Security (scroll down to "Windows SmartScreen" then click below where is says, "Change settings" a pop up will appear, in it select "Don't do anything (turn off Windows SmartScreen)". Click OK and you're done.Tanzania agrees $800 million loan from S. Africa and China for reserves and budget gap

image: pt.tradingeconomics.com

Tanzania agreed $800 million of loans from Rand Merchant Bank and China Development Bank Corp. to bolster its foreign-exchange reserves, as the country shores up a weakening currency, and plugs the budget deficit.

Talks with Johannesburg-based Rand Merchant Bank to raise as much as $600 million and $200 million from China Development Bank are being completed, said Joseph Masawe, the Bank of Tanzania’s head of economic research and policy. RMB will raise the money through a private placement, while CBD will finance the loan from its own balance sheet, he said.

“We are expecting about $800 million and we think before the end of this month we should be able to receive from both banks,” Masawe said in a phone interview Monday from Dodoma, the capital. “We have finalized the details and we are hoping this will improve the supply of foreign currency.”

Tanzania’s shilling weakened 21 percent so far this year and is Africa’s worst-performing currency, after Ghana’s cedi. Last year, foreign donors including the World Bank and the U.K. said they would withhold $558 million of budget aid because of a corruption scandal in the energy industry.

The budget deficit is expected to widen to 4.2 percent of gross domestic product this year from 4 percent last year, according to Paarl, South Africa-based NKC African Economics. The government is reducing its reliance on budget support to 3 percent of total revenue in the fiscal year that begins on July, from 7 percent in the current year, NKC said in an e-mailed research note.

Tanzania’s central bank sold $339 million to lenders from January to April to support the shilling, it said on May 4. A 13 percent slump in gold shipments to $1.4 billion in the year through to March and the government’s “external obligations” contributed to the shilling’s decline, Masawe said.

While the central bank says it has enough resources to defend the currency, it has “scaled down sales” of foreign currency to banks.

“About 65 percent of the currency depreciation is due to strengthening of U.S. dollar and 35 percent is attributed to internal factors and speculation by banks,” Masawe said.

Mifano ya uandishi wa Kiswahili usio sahihi


Makosa yanayojitokeza katika magazeti mengi ya Kiswahili ni kutokana na waandishi kutokuwa makini na wengine kutokuwa na ujuzi wa kutosha katika sarufi na fasihi ya Kiswahili. Kwa kuwa makosa haya yanaendelea kujitokeza, makala zangu zina nia ya kupunguza makosa hayo kwa kunukuu sentensi chache kwenye magazeti na kutoa maelekezo. Nimeweza kunukuu sentensi chache lakini kwa uchunguzi wa kina yako makosa mengi sana ya upatanishi wa kisarufi, matumizi mabaya ya lugha ya Kiswahili, maendelezo ya maneno mengi ambayo yanatokana na athari ya lugha za asili. Sentensi hizi chache ni mfano tu lakini kwa kweli makosa tunayosoma ni mengi. Hebu soma sentensi zifuatazo:

“Jukwaa la Wanarukwa lina dhumuni la kuhamasisha watu kuchangia sekta za kilimo, siasa, elimu, uchumi, utamaduni na jamii.”

Waandishi wengi huwa hawaelewi kuwa wanatakiwa kuwa waangalifu wanapotumia kiambishi cha awali cha ‘ma’ mbele ya baadhi ya maneno wanafanya makosa. Kwa mfano liko neno madhumuni halina umoja. Neno dhumuni halipo katika msamiati wa Kiswahili fasaha. Hivyo neno ‘dhumuni’ halikutumika kwa usahihi. Kwa usahihi lingekuwa neno madhumuni. Madhumuni hutumika katika umoja na wingi. Dhumuni linalazimishwa na wasiokuwa weledi wa lugha hii. Hivyo ni sahihi kuandika,

“Jukwaa la Wanarukwa lina madhumuni ya kuhamasisha watu kuchangia sekta ya kilimo, siasa, elimu, uchumi, utamaduni na ustawi wa jamii.”

“Mtizamo wa aina hii ni batili na hauwezi kuleta matunda mazuri.”

Hapa tena mwandishi anaandika kama wanavyozungumza watu ambao hawafuati misingi ya uandishi bora. Kuna wakati tunasikia watu wakisema, ‘Mtizamo wangu ni tofauti na wako’. Hata hivyo, wakati wa kuandika tunatakiwa kuandika neno sahihi ambalo ni ‘Mtazamo’. Hivyo iandikwe kwa usahihi,”Mtazamo wa aina hii ni batili na hauwezi kuleta matunda mazuri.”

“Keshokutwa Ijumaa hatma ya madiwani wanane wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliotimua na waliotimuliwa itajulikana mjini Dodoma”.

Neno keshokutwa haliunganishwi na kuwa neno moja bali ni maneno mawili tofauti. Vilevile tunaandika hatima na wala siyo hatma kama tunavyozungumza. Hapa tena tuchanganya lugha ya mazungumzo na ile ya kuandika. Vilevile maneno waliotimia na waliotimuliwa yalivyoandikwa ni makosa. Sahihi ni kutumia neno moja tu la waliotimuliwa. Kwa hiyo kwa usahihi ingeandikwa,

“Kesho kutwa Ijumaa hatima ya madiwani wanane wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliotimuliwa itajulikana mjini Dodoma.”

“Umati wa watu wakifatilia juu ya maiti zilizoingizwa hospitalini hapo.”

Kwa Kiswahili fasaha kuandika “ juu ya” ni makosa. Ilitakiwa kuandikwa kwa kutumia neno “kuhusu’ hivyo isomeke,

“Umati wa watu wakifuatilia kuhusu maiti zilizoingizwa hospitalini hapo.”

Mtindo wa kutumia lugha ya mazungumzo hauna budi kuepukwa katika uandishi. Wako wasemaji wanaotumia ‘kufatia’ lakini sahihi ni ‘kufuatia’. Pia ‘zikiingizwa’ iandikwe ‘wakiingizwa’. Kwa mila na utamaduni wa Mwafrika tunatumia maiti hawa na siyo maiti hizi kwa heshima ya marehemu.

“Nadhani unakumbuka tukio la mfanyabiashara aliyeuliwa juzi kati.”

Matumizi ya maneno ‘juzi kati’ yanakanganya na kwa kweli hayaleti maana kabisa. Ni bora angeandika bila kuongeza neno ‘kati’. Kwa mfano: “ Nadhani unakumbuka tukio la mfanyabiashara aliyeuliwa juzi.

“Watoto wake wawili mapacha John na Anthony walikuwa wamesimamia biashara ya baba yao.” Yako mazoea ya watu wengi tena kwa asilimia kubwa ya Watanzania hawaelewi tofauti baina ya mapacha na pacha. Kwa usahihi neno linalofaa ni ‘pacha’na siyo ‘mapacha’. Maana ya watoto pacha ni watoto waliozaliwa kutokana na mimba moja. Pia inawezekana kuwa na ndizi pacha au vidole pacha kwa maana ya vidole au ndizi kushikana. Hivyo hatusemi watoto ‘mapacha’ bali watoto pacha.

“Anasema idadi inayodahiliwa ni kidogo ikilinganishwa na nchi za jirani.”

Ningependa kufafanua maana ya maneno mawili ambayo yanayotumika vibaya. Maneno haya ni dahili na sajili. Maana ya kudahili ni kudadisi jambo, kutaka kujua habari za watu kwa kuulizauliza. Kwa wanafunzi wanaoomba kujiunga na vyuo au shule, hatua ya kwanza ni kuwadahili. Baada ya kupata taarifa kamili kuwa wana sifa zinazofaa, ndipo wanasajiliwa. Kwa hiyo kusajili ni hatua ya mwisho baada ya uchunguzi kukamilika na hivyo kuorodheshwa kwa majina na sifa zao katika daftari la kudumu. Wanafunzi waliosajiliwa wameorodheshwa katika daftari la kudumu na hivyo huwa ni wanafunzi kamili wa chuo husika.

Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kusahihishana na kuelimishana kadri siku zinavyosonga mbele

[email protected]

Tanzania, Malta zatiliana saini kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia

Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi na Christopher Grima Malta wakitia sahihi hati za kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya Mabalozi. Wanaoangalia utiaji sahihi ni Tully Mwaipopo Afisa Mwandamizi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Bw. Alan Cordina, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Malta

Na Mwandishi Maalum, New York

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malta zimekubaliana kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina yao.

Wawakilishi wa Kudumu wa mataifa hayo mawili katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi wa Tanzania na Christopher Grima wa Malta ndio waliotia sahihi hati za kuridhia kuanzishwa kwa uhusiano huo na ambao utakuwa katika ngazi ya Mabalozi.

Wakizungumza mara baada ya utiaji sahihi hati hizo, wawakilishi hao wameelezea kuwa kuanzishwa kwa uhusiano huo ni hatua muhimu sana katika kukuza na kuendeleza ushirikiano na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili na watu wake.

Tanzania imekuwa ikinufaika kwa ufadhili wa nafasi za masomo kutoka Malta kwa watumishi mbalimbali wakiwamo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara nyingine.

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Mwakilishi wa Kudumu wa Malta katika Umoja wa Mataifa, Balozi Christopher Grima wakipongezana mara baada ya kutia sahihi hati walizoshika za kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya Mabalozi. Hati hizo baadaye ya zitawasilishwa rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.


Vatican indicts its own former ambassador for sexually abusing minors; US archbishop quits for cover-ups

VATICAN CITY (AP) — The embattled archbishop of St. Paul and Minneapolis and his deputy resigned Monday after years of pressure, an indication Pope Francis is making good on his promise that no one is above the law when it comes to covering up for clergy who sexually abuse children.

Archbishop John Nienstedt and Auxiliary Bishop Lee Anthony Piche stepped down after Minnesota prosecutors charged their archdiocese with having failed to protect children from unspeakable harm by a pedophile priest who was later convicted of molesting two boys.

Separately, the Vatican indicted Jozef Wesolowski, its own former ambassador to the Dominican Republic, on charges of sexually abusing minors in the Caribbean country and possessing child pornography. He will be the highest-ranking Vatican official ever to stand trial for a sex crime.

The developments came days after Francis approved the creation of a new tribunal inside the Vatican to hear cases of bishops accused of failing to protect minors, answering years of criticism that top-ranked churchmen have long been immune to punishment for ignoring or covering up for priests who rape and molest children.

It's not clear if the tribunal — once it becomes functioning — would handle the cases of Nienstedt and Piche, since they are no longer in office.

They quit under the code of canon law that allows bishops to resign before they retire because of illness or some other "grave" reason that makes them unfit for office.

Earlier this month, prosecutors charged the Archdiocese of St. Paul and Minneapolis as a corporation with having "turned a blind eye" to repeated reports of inappropriate behavior by the priest. The complaint did not name any individuals.

The charges came two years after diocesan canon lawyer-turned-whistleblower Jennifer Haselberger alleged widespread cover-up of clergy sex misconduct in the archdiocese, saying archbishops and their top staff lied to the public and ignored the U.S. bishops' pledge to have no tolerance of priests who abuse.

Haselberger, who was Nienstedt's archivist, accused the church of using a chaotic system of record-keeping that helped conceal the backgrounds of guilty priests who remained on assignment.

She said she repeatedly warned Nienstedt and his aides about the risk of keeping accused priests in ministry, but they took action only in one case. As a result of raising alarms, she said she was eventually shut out of meetings about priest misconduct, and later resigned.

Call for Applications: 2015/6 PhD Scholarships at HEARD/UKZN

Under the supervision of Professor Nana Poku and with the generous support of Sida/ NORAD, HEARD is offering up to four fulltime PhD Research Scholarships in any of the following key areas of strategic focus Sexual and Reproductive Health; Health Systems Strengthening and Economics of Critical Enablers in HIV Programming.

Award of the HEARD PhD Research Scholarship is conditional on candidates meeting the requirements for PhD registration at the University of KwaZulu-Natal, and on participating in a compulsory training component during the first year of study. The training component will be conducted over four two-week blocks during the first year of study. Candidates will produce a thesis related to one of HEARDs priority research nodes, as detailed above. The Scholarship programme emphasizes the mastery of quantitative and qualitative methods for understanding policy problems and for devising, evaluating and/or implementing policy solutions.

The intention of providing PhD scholarships is to produce expertly qualified graduates to advise or to be part of influential policy making organisations in Africa. During their PhD, students will be strongly encouraged to present their work at international meetings.

The value of each scholarship is R270, 000 and will be paid in tranches over three years. Tranche payments will be conditional on research progress. Successful candidates will be based in Durban, South Africa, for the duration of the scholarship, with the exception of the time during which they may undertake field research elsewhere.

Applications are invited from citizens of all African countries. Female candidates and, in the case of South Africa, those from previously disadvantaged backgrounds, are especially encouraged to apply. Click here for more information.

About the PhD Scholarship Programme

The HEARD PhD Scholarship Programme was initiated for the first time early in 2009 with 14 scholarships being offered until 2012. One of the objectives of the scholarship programme is to provide students with a comprehensive academic experience and an enriching study environment as well as academic supervision and guidance. In this respect, funding to attend local HIV and AIDS conferences has been allocated each year.

HEARD anticipates that the students will return to their countries to take up senior positions in the health sector and government. In this way they will be not only instrumental in working to curb the AIDS epidemic, but will also have input into a broad range of fields covering health promotion and broader regional socio-economic development. HEARD's intention is that they be among the intellectual, civil and political leaders of the future. In fact, one of the conditions of receiving the scholarship is a commitment from the students to remain on the continent for at least two years after graduating. In this way HEARD is confident that the programme will contribute to fostering African scholarship.

Programme Contact: Cailin Hedderwick

More/Source: www.heard.org.za

Dk Migiro, Chagama, Malupu wachukua fomu CCM ya kuwania Urais Tanzania 2015


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, hivyo kufikisha idadi ya makada 36 wa chama hicho wanaowania urais, lakini pia akiwa mwanamke wa nne kuthubutu kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.

Mbali ya Dk Migiro, wengine waliochukua fomu ya kuwania urais ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anayesomea Shahada ya Uzamili katika Utumishi wa Umma, Malick Malupu (34) na Joseph Chagama (45) ambaye ni kada wa chama hicho.

Dk Migiro ambaye alikuwa ameongozana na mumewe pamoja na mwanasiasa mkongwe nchini, na Mbunge wa viti maalum, Anna Abdallah, alisema CCM imetoa fursa kwa wanachama kujitokeza ili kupata ridhaa ya kuongoza kumtafuta kiongozi wa nchi.

Pia waliojitokeza watatoa fursa kwa wanawake vijana na wasichana kusimama mabegani mwao.
“Tunaishukuru CCM kwa kufanya wengi tujitokeze kwa kuweka mazingira ya kufanya wengi zaidi wajitokeze,” 
alisema kada huyo aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini, kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), nafasi aliyoitumikia hadi mwaka jana aliporejea nchini na kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Alisema wanaCCM wamejitokeza huku akiwataka wanachama wa CCM wengi zaidi kujitokeza kumdhamini.

Alipohojiwa nini vipaumbele vyake, alisema Ilani ya CCM ndiyo dira kwani hata ilani inayotengenezwa sasa imebeba maeneo mengi, kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea, sekta ya uzalishaji, miundombinu, mazingatio maalumu kuhusu muungano.
“Ilani itakuwa imefanya tathimini na kuweka mikakati ya kuendeleza yaliyofanyika.”

Alisema akipata ridhaa nyenzo yake itakuwa ni ilani ya CCM kwani hata taarifa ya Benki ya Dunia inaonesha uchumi umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6.4 hadi asilimia saba.

Alisema hali hiyo inaashiria kuna maendeleo, kukua kwa uchumi ni kiashiria cha jitihada za serikali.
Dk Migiro alisema ikipatikana fursa ya kuongoza atatumia ilani ya CCM kwani ni nyenzo kubwa katika kufikia maendeleo ya kweli; “Pamoja na ilani msingi utakuwa kuhakikisha manufaa ya mafanikio hayo yanafikia wananchi walio wengi, kazi iliyo mbele itakuwa ni kuhakikisha wananchi wengi wananufaika,” alisema.

Kwa upande mwingine, alitoa masikitiko yake kutokana na kifo ha Mufti wa Tanzania alitoa pole za dhati kwa Watanzania wote na kwa familia yake.

Alisema uwezo wa mtu kiutendaji haupimwi kwa umri japo ana umri wa miaka 34, bado anaona ana nafasi ya kuwa mgombea.

Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 39 (1) (b) (d) kinasema mtu anayestahili kushika nafasi ya Urais awe ametimiza miaka 40.
“Katiba inatakiwa mgombea awe ametimiza miaka 40 kwa tafsiri ya Kiswahili lazima mgombea awe na miaka 40 na asizidi au kupungua na kwa tafsiri hiyo hata wale wagombea wengine waliovuka miaka 40 hawana sifa,” 
alisema.

Alisema Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliiwakilisha nchi kwenye baraza la Umoja wa mataifa (UN) akiwa na umri wa miaka 33. Alisema hata alipohojiwa alisema kuwa asipimwe kwa umri bali kwa utendaji wake na pingamizi hilo likaondolewa.

Malupu alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ataboresha kilimo. Alisema sekta ya kilimo ni sekta mama inatakiwa kupewa msukumo mkubwa.

Pia alisema atapandisha hadhi vyuo vya kilimo ili viweze kutoa wataalamu wengi zaidi ambao watakwenda kutoa msukumo mkubwa kwa wakulima na kuongeza uzalishaji. Malupu alisema atahakikisha sekta ya elimu na michezo zinakuwa bora.

Alipohojiwa ni wapi alipopata fedha za kulipia fomu alisema miongoni mwa waliomchangia fedha za kuchukua fomu ni wanachama wa upinzani na aliongeza kuwa, ameamua kugombea nafasi hiyo ili aweze kutumikia watanzania kwani ana uzoefu kwenye uongozi ambapo miongoni mwa nafasi anazoshikilia mpaka sasa ni nafasi ya Uenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Morogoro.

Chagama ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema akichaguliwa na chama chake na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania, atarekebisha mfumo wa utekelezaji wa haki, huku akiahidi jambo atakaloanza nalo kuwa ni kushughulikia suala la ajira kwa vijana na kurekebisha mfumo wa utekelezaji wa haki.

Akizungumzia elimu yake, alisema alipata shahada yake ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Bugema, Uganda, huku shahada ya pili akiipata katika Chuo Kikuu cha Wales, Lampeter nchini Uingereza na shahada ya tatu alisoma Chuo Kikuu cha Surrey, Uingereza ingawa hakuweza kuhitimu kwa kile alichosema ni kutokana na tatizo la kimazingira.
“Mimi ni mtaalamu wa jinai na ninaweza kusimamia haki, unapofikiria uchumi wa nchi lazima kusimama kwenye mstari na wananchi wajue haki zao,” 
alisema na kuongeza kuwa, wananchi wana matumaini na CCM hivyo anaamini ni miongoni mwa wanaofaa kwa Urais wa nchi.

US Court: Spouse can't protest visa denial to husband

WASHINGTON (AP) -- A California woman can't challenge the government's decision to deny a visa to her spouse from Afghanistan, the Supreme Court ruled Monday.

The justices ruled 5-4 that Fauzia Din, a naturalized U.S. citizen, had no basis to protest after the visa petition she filed for her husband was rejected in 2009.

Din's husband had worked as a clerk in the Afghan government when it was controlled by the Taliban. But the U.S. Embassy in Pakistan offered no factual explanation for refusing his visa request, other than to cite a law giving officials broad discretion to deny visas based on "terrorist activities."

Din argued that the rejection triggered her spousal rights under the Constitution and that she deserved to know the specific reason for the denial.

But Justice Antonin Scalia, writing for three justices, said even assuming that marriage is a fundamental right, Din has not been forbidden from getting married.

"Those right-to-marry cases cannot be expanded to include the right Din argues for - the right to live in the United States with one's alien spouse," Scalia said.

Justices Anthony Kennedy and Samuel Alito agreed with the outcome, but wrote separately to say that it was not necessary to decide whether marriage is a right protected by the Constitution. He said the government satisfied due process when it notified Din's husband he was denied under the law's anti-terrorism ban.

A dissent from the court's four liberal justices said Din should have prevailed on her constitutional claims. Justice Stephen Breyer said Din had "the kind of liberty interest" that deserves protection under the Constitution.

A decades-old legal doctrine gives the government broad power to deny visas and courts have long held that noncitizens have no constitutional right to seek an explanation. Din was trying to get around that legal barrier by asserting that her marriage was affected by the decision.

A federal judge threw out Din's case, but the 9th U.S. Circuit Court of Appeals reversed, finding that Din had a right to get a fuller explanation for the visa denial based on her marital rights.

The government said visa rejections are confirmed with an advisory opinion from the State Department and all denials are reported to Congress, which provides additional oversight.

At the end of his opinion announcement, Scalia mistakenly referred to his longtime colleague and friend, Justice Ruth Bader Ginsburg, as Justice Goldberg. After colleagues alerted Scalia to his mistake, he apologized to Ginsburg. "Sorry about that, Ruth," Scalia said.

Watuhumiwa 2 wa ujambazi Dar wauawa wakipambana na Polisi


Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata bunduki nne, moja ya kivita aina ya AK 47 pamoja na bastola tatu, baada ya kupambana na majambazi waliokuwa na pikipiki ambao kwa kipindi kirefu walikuwa wakiendesha vitendo vya unyang'anyi na mauaji ya kutumia silaha.

Aidha katika sakata hilo majambazi wawili waliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kukaidi amri ya kuwataka kujisalimisha na kuanza kurusha risasi kwa askari waliokuwa katika harakati za kuwatia mbaroni.

Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 15, 2015


Taarifa ya Habari ya Channel TEN Juni 14, 2015Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 14, 2015

Wapanda baiskeli waanza safari Mbeya - Dar kumpongeza Rais Kikwete


Kitabu maalum cha wapanda Baiskeli kutoka Mbeya ambacho atakabidhiwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kukamilisha safari yao km 830 kutoka Mbeya hadi Dar es salaam


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwapa nasaha wapanda baiskeli watatu kabla ya kuelekea Jijini Dar es salaam kwa kutumia Baiskeli kwa ajili ya kumuunga mkono na kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kutimiza miaka 10 ya uongozi wake.
Mmoja wa wapanda Baiskeli akionesha mbwembwe za uendeshaji wa baiskeli kabla ya kuanza safari mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
Wapanda Baiskeli wakianza safari ya kuelekea Dar es salaam kutokea Mbeya wakiadhimisha kauli mbiu yao waliyoiita 'Asante JK kumaliza miaka 10'.
Mmoja wa wadhamini wa wapanda Baiskeli hao Sambwee Shitambala kupitia kampuni yake ya Shitambala Advocate and Company akiwaaga wapanda baiskeli hao ambao wanatarajia kutumia siku nane kuelekea Jijini Dar es salaam kukutana na Rais Jakaya Kikwete kumpongeza kwa kutimiza miaka 10 ya uongozi wake.


Taarifa ya TFF kuhusu mechi ya Tanzania vs Misri na Kuanza kwa usajili


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 – 0 na wenyeji Misri.

Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 – 0.
Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy (64) na Mohamed Salah (69).

Stars ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbdonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.

Mara baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.

Tanzania: Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.

Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.

USAJILI WA WACHEZAJI KUANZA JUNI 15

Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2015/2016) unaanza Juni 15 hadi Agosti 6 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.

Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 7 na 14 mwaka huu. Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 15 hadi 19 mwaka huu.

Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 17 na Septemba 8 mwaka huu. Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Septemba 8 hadi 14 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 15 na 17 mwaka huu.

Wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania, usajili wa mtandao wa FIFA wa TMS utakuwa wazi kuanzia kesho (Juni 15) hadi Septemba 6 mwaka huu. Klabu zinazosajili wachezaji kutoka nje zinatakiwa kufanya hivyo kupitia akaunti zao za mtandao wa TMS.

Kwa klabu ambazo hazina akaunti ya TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo ya TMS, na baadaye kuombewa akaunti hizo FIFA.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 22 mwaka huu).

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu, wakati Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Ajali ya basi Iringa yaua watu 23WATU 23 wamefariki papo hapo huku wengine 34 wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka wakati likijaribu kuyapita magari mengine katika kijiji cha Kinyanambo A, eneo la Changarawe, Wilayani Mafundi mkoani Iringa.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:45 Juni 14,2015, wakati basi hilo likienda Njombe kutokea Iringa katika barabara kuu ya Iringa - Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Pudenciana Protace amesema kuwa, magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T916 AQM lililokuwa na tela T965 BEH Mali ya kampuni ya Bravo Logistics ya jijini Dar es Salaam na basi aina ya Fuso lenye namba za usajili T927 CEF la kampuni ya Another G.
“Wakati basi hilo lenye uwezo wa kupakia abiria 65 likiwa linatokea Iringa kuelekea Njombe, lori hilo lililokuwa likiendeshwa na Rogers Wales mwenye miaka 39, Msambaa mkazi wa Mwanza lilikuwa likitokea barabara kuu ya Mafinga kuelekea Iringa.”


Kamanda ACP Protace amesema madereva wote wawili wa magari hayo, Nicholaus Nagura (30) mkazi wa Makambako aliyekuwa akiendasha basi na Rogers Wales 'Mdue' (35) mkazi wa Mwanza aliyekuwa akliendesha lori wote wamefariki.

Aidha amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi Nicholas Magula (30) aliyekuwa akiyapita magari mengine kisha basi hilo kuligonga kwa ubavuni lori hilo na kupinduka.

Alisema kuwa kati ya watu hao 23 waliopoteza maisha wanaume ni 16 wakiwapo watoto 3 na wanawake ni 7, huku majeruhi hao 34 wanaume ni 18 na wanawake ni 16 na kati yao watoto wakike ni wawili. Kamanda ACP Protace amesema hali za majeruhi 30 zinaendelea vizuri ila 4 hali zao ni mbaya.

Alisema miili ya marehemu na majeruhi ilikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi ya mjini Mafinga, mapema baada ya ajali hiyo kutokea.

Alisema miili 12 ya watu waliokufa imekwishatambuliwa na kuwataja kuwa ni pamoja na Lucas Pancras, Blasto Samila, Dickson Luvanda, Albert Silla (askari wa Ruvu JKT), Eva Mbalinga, Khadija Mkoi (4), Clemence Mtati, Mohammed Lalika, Castory Mwakiamba, Damiana Myala na Silo Nziku ambao wote walikuwa katika basi hilo na dereva wa lori, Rogers Wales.

Alitaja majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa katika basi hilo kuwa ni pamoja na Emma Lupembe (35), Veronica Simba (20), Shafia Ally (24), Mariam Mbise (23), Anita Makwela (24), Benitha Sagara (18), Bertha Mkoi (27), Rahel Mavika (18), Selina Fulgensi (23), Maria Mwenda (17), Ndipako Mbilinyi (28), Alexander Mkakazi (28), Meshack Kibiki (44), Simoni Jumbe (22), Jerry Lutego (36), Enock Kanyika (18) na Yusuph Lulandala (22).

Wengine ni Deogratias Kayombo (21), Petro Mwalongo (21), Paul Chahe (21), Kennedy Msemwa (28), Emmanuel Anthony (21), Mode Shilazi (21), Godfrey Kanyika (39), Boniface Bosha (20), Ambiana Meshack (35), Martha Kanyika (30), Melika Tonga (2.5), Yusuph Luhumba (34) na Damiana Kuyala (42).

Protas alisema majeruhi wengine wanne, wanaume wawili na wanawake hawajatambuliwa majina yao kwa sababu walikuwa hawaongei.

Nikiwa Rais nitavivua viatu hivi...


Kifo cha Mufti Simba; Rais Kikwete, CHADEMA watuma salam

Mufti Sheikh Issa Bin Shaaban Simba


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Sheikh Issa Bin Shaaban Simba.

Marehemu Mufti amefariki leo 15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure).
"Kifo kinaleta huzuni, hata hivyo Kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele". 
Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.

"Nawaombea subra wana familia, ndugu, jamaa, waislamu wote na wana jamii kwani Mufti alikua kiongozi katika Jamii yetu'” Rais amesema na kueleza kuwa "Kamwe mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa Ujumla na hakika sote tutamkumbuka" ameongeza.

Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka 1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.

Rais amemuelezea Marehemu Mufti kama mwalimu katika jamii ambaye alikua na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka
"Amekua mwalimu imara na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika uislamu na jamii kwa ujumla, hakika tutamkumbuka siku zote" 
Rais Kikwete ameongeza.

Shekhe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa na uzoefu mkubwa ndani ya BAKWATA na aliwahi kukaimu nafasi ya mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.

Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahali pema Peponi, Amina.

Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM

15 Juni, 2015


----------


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

(CHADEMA)

SALAAM ZA POLE NA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUFTI MKUU SHEIKH SIMBA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za msiba wa Mufti Mkuu wa Tanzania Tanzania, Sheikh Issa Shaaban bin Simba, Kiongozi Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kilichotokea asubuhi ya leo kwa maradhi ya sukari na shinikizo la moyo.

Akitoa salaam za pole na rambirambi kwa waumini wa madhehebu ya Kiislamu na Watanzania wote kwa ujumla baada ya kupata taarifa za msiba huo, Mwenyekiti wa CHADEMA (T), Freeman Mbowe amesema kuwa Mufti Mkuu Simba atakumbukwa kwa namna aliyosimama kama kiongozi wa dini kupitia kauli zake mara kwa mara akisisitiza ushirikiano ndani ya jamii ya Watanzania bila kujali tofauti zao katika itikadi za dini.
“Mara kwa mara Mufti Mkuu Simba amesikika akiwaambia Watanzania, si Waislam pekee aliokuwa akiwaongoza kiroho, hata wale wanaoamini katika madhehebu tofauti, umuhimu wa kudumisha ushirikiano miongoni mwa dini mbalimbali na makundi mengine katika jamii ikiwa ni mojawapo ya misingi ya kuimarisha umoja wa taifa letu.”

“Naungana na Waislam wote nchini katika wakati huu wa kuomboleza kifo cha kiongozi huyu wa kiroho. Kwa niaba ya niaba ya uongozi wa CHADEMA, wanachama, wapenzi na wafuasi, natoa salaam za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, BAKWATA, viongozi wa kiroho nchini na Watanzania wote ndani na nje ya nchi walioguswa na msiba huu mzito.”

“Mwenyezi Mungu awatie nguvu wote na kuwafanyia wepesi katika wakati huu mgumu wa majonzi ya msiba wa Mufti Mkuu Simba,” 

amesema Mbowe

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji’un.

Imetolewa leo Jumatatu, Juni 15, 2015 na;

Idara ya Habari na Mawasiliano- CHADEMA.

-----------

MWILI wa Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unatarajiwa kusafirishwa kesho mkoani Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Alhad Mussa Salum amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu , viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.

Amesema marehem alikuwa akisumbuliwa na sukari, Shinikizo la Damu (BP) pamoja na Figo. Hata hivyo amesema kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam na mauti ya Mufti yamekuja majira ya saa moja leo.

Salum amesema marehem anatarajiwa kuzikwa Alhamis mkoani mkoani Shinyanga.

Prof. Mwandosya mkoani Kilimanjaro kupata saini za wadhamini


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais(Kazi Maalum) Prof, Mark Mwandosya mara baada ya kufika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaro wakati akiwa njiani kutafuta wadhamini.Prof, Mark Mwandosya akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Angela Kairuki walipokutana katika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaro.Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimpatia kipaza sauti Prof Mwandosya asalimie wajumbe waliokuwa katika ukumbi huo.Profesa Mwandosya akizungumza katika ukumbi huo.Prof Mwandosya akitoka katika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaromara bada ya kusalimia.
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Dixon Busagaga 

[video] Rais Kikwete aaga AU kwa kuhutubia kwa Kiswahili

 Rais Jakaya Mrisho kikwete akipanda jukwaani tayari kuhutubia na kuaga rasmi wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siasa ya nchi za nje na misingi mikuu ya kuongoza mahusiano ya Tanzania na nchi za kigeni hayatabadilika hata baada ya yeye kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, mwaka huu, 2015.

Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kuwa yeye anaondoka madarakani lakini Tanzania waliyoizoea na kuijua itabakia pale pale na kuwaomba viongozi hao kumpa ushirikiano mkubwa mrithi wake kama walimpa yeye.

Rais Kikwete ametoa uhakikisho huo mara mbili leo, Jumapili, Juni 14, 2015, wakati alipohutubia kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Wakati wa mkutano ujao wa kawaida wa AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, Januari, mwakani, Tanzania itakuwa na Rais mpya, Rais wa Tano.

Aidha, Rais Kikwete amerudia kauli na msimamo huo wa Tanzania wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Hassan Sheikh Mahmoud ambako kiongozi huyo wa Somalia amemjulisha Rais Kikwete kuwa angependa kutembelea Tanzania baadaye mwaka huu.

Alisema Rais Kikwete kuwa misingi ya siasa za nchi za nje za Tanzania na misingi mikuu ya kuongoza mahusiano yake na nchi za nje yaliwekwa tokea Uhuru na hasa tangu kutungwa wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania mwaka 1972 na tokea wakati huo hajapata kubadilika kama kama wamebadilika viongozi mara nne sasa.
“Hatujapata kubadilisha misingi hiyo inayoelekeza kuwa mahusiano yatajengwa kuanzia nchi za jirani, zikifuatiwa na nchi za Afrika, nchi marafiki duniani na nchi nyinginezo.”
“Sina shaka kabisa kuwa misingi ya siasa za nje na misingi mikuu ya uongozi wan chi yetu itabakia ile ile isipokuwa kama Rais ajaye atatoka chama kingine. Kitakachobadilika ni staili ya uongozi tu lakini misingi ya uongozi itabadilia pale pale kwa sababu ni misingi mizuri, ni misingi ya busara ambayo imeongoza nchi yetu vizuri kwa miaka mingi.”

Ameongeza Rais Kikwete: 
“Ni matumaini yangu kuwa Watanzania tutachagua kiongozi mzuri atakayeendela kutoa kipaumbele cha juu kwa masuala ya Afrika pamoja na uanachama na ushiriki wetu katika Umoja wa Afrika. Haya ni miongoni mwa misingi mikuu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania tangu uhuru mpaka sasa. Nawaomba mumpe ushirikiano mkubwa kama mliopnipatia mimi na hata kuzidi.”Waziri wa Nchi (OR) Ikulu na utawala bora Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini Zanzibar akisalimiana na katibu Mtendaji wa SADC Dkt.Stergomena Tax wakati wakisubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete ahutubie na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. 


Mamia ya wanahabari wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Shehemu ya wajumbe wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini.


Wajumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika uliofunguliwa Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Rais wa Visiwa vya Comoro baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa AU Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na rais Yoweri Museveni wa Uganda baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa Somalia Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wajumbe mbalimbali baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Misri Mhe Ibrahim Mahlab baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mfalme Mswati wa Swaziland baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe maalumu wa Marekani katika Mazia Makuu baada ya kuhutubia na kuwaaga wakuu wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika Jumapili June 14, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Sandton Convention mjini Johannesburg, Afrika Kusini.