Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 23, 2015

Wakudata: Wachumba 38...Public notice to the Dodsal Group Dubai


 • Notice to All Expatriates
 • Notice to Mr. Rajen Kilachand, The Chairman of Dodsal Group Dubai
 • Notice to Dr. Jogendra Nath Sahu, Dodsal Group Dar es Salaam
 • Notice to Milembe Company
 • And whomever concerned directly or indirectly.

My Name is Bishop Charles Gadi the servant of the Almighty God.

Due to your evil doings, I declare that you have made me your God and that for the evil you did in my farm I will not even need any help from God Almighty, because in Joshua 6:26 the word of God says “cursed is he who will build this town (Jericho/Dodsal Group) again. He will lay its foundations by expense in death of his first born son, and will erect its gates by the expense in death of his last son. God has given me this authority over people who don’t want to obey laws and authority of the country.

I am giving all of you 72 hours to close your plant AND LEAVE THE PREMISES.

If you will not heed to this order TO CLOSE AND LEAVE after the allotted time, these things will follow:
 • All external expatriates working in the plant will go back to their nations insane
 • All other workers working in the plant will be hopeless in everything.
 • After 72 hours the plant will not be there.
 • I will be the last man to be wronged with such a great evil by the chairman of Dodsal Group Mr. Rajen Kilachand.
 • You wrongly believe that your money can by everything including human rights and human life, this time you will not succeed.
 • You promised me through a letter in September 2014 that you will pay me before starting drilling. But now you have drilled 3000m (3km) deep, sleeping in hotels with your companions, enjoying yourselves without a consent from the owner. You have prevented me from doing any development on my farm for 2 years, littered the place with human and chemical waste, plus destroying the vegetation. Up to now you are not showing any efforts to negotiate with the owner of the farm. Only in this country you may do such things and sleep comfortably, but not in any other country.
 • Within 71 hours, anything can be done including negotiations between you and the owner, but after 72 hours I emphasis nothing can be done, Neither God, nor me will be able to change the situation.
 • God who introduced me in Hyderabad India by heavy rainfall and Thunderstorm on 6th June 2015, the same will introduce me to you. For my reference refer: Heavy rainfall in Hyderabad/ABN News (06-06-2015)-YouTube - http://www.youtube.com/watch?v=6Ssv6jRdmFA

So from Tuesday 23rd to Thursday 26th June 2015 at 4:00 pm you need to vacate the premises and leave it clear.

God has magnified his WORD above his Name.

BISHOP CHARLES GADI

Google is 'increasing transparency' for you to see 'invalid activity deductions'


According to a post published at Google Adsense blog by their Product Manager, Justin Chu, Google is now making it possible to learn more about the differences between estimated and finalized earnings.
Starting with May’s payment history, you’ll be able to see the invalid activity deductions that cause these differences. For example, if your estimated earnings were $1,100 and your finalized earnings were $1,000, you now have a better view into how your estimated earnings break down into invalid activity and finalized earnings.

Further, they said that the difference is mostly caused by invalid activity on your site, i.e. accidental clicks, deducted from finalized earnings and:
If there is a large difference between your estimated earnings and your finalized earnings, make sure to review these tips. To prevent invalid activity on your site, pay special attention to your site design andtraffic acquisition. If you see unusual levels in invalid activity, we encourage you to notify us by using theInvalid Clicks Contact Form.

Mwandishi wa Guardian atangaza kuwania Ubunge kupitia CHADEMA

MWANDISHI wa gazeti la The Guardian Gerald Kitabu amejitosa katika kinyang’anyiro cha ubunge katika Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kitabu ambae ni mshindi wa tuzo ya uandishi wa habari ya SADC ambayo hutolewa kwa mwandishi bora anaeandika habari za maendeleo na mazingira katika nchi za jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, alichukua fomu hizo hapo katika ofisi za Chadema jimbo la Nsimbo zilizopo katika kijiji cha Songambele, Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi.

Kadhalika, mbali na kushinda tuzo ya SADC, mwandishi huyo pia hivi karibuni alishinda tuzo mbili kubwa katika nafasi ya kwanza, moja ikiwa ya TANAPA (2013), na nyingine ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) (2014) katika kipengele cha mazingira.

Akizungumza na mamia ya wafuasi wa chama hicho pamoja na wananchi wa jimbo la Nsimbo waliokusanyika katika ofisi za chama hicho jimboni hapo, amesema amesukumwa na uzalendo wake kwa jimbo hilo kutokana na changamoto kadhaa zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na usimamizi mbovu wa rasilimali, mikataba ya hovyo isiyojali maslahi ya wananchi na taifa ikiwemo mikataba ya uwekezaji katika kilimo, na rushwa hali ambayo imepelekea huduma duni za jamii kama vile maji, barabara, afya na elimu.
“Miaka michache iliyopita, kuna mkataba mmoja wa Katumba na Mishamo ulisainiwa kati ya viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na mwekezaji wa kampuni ya AgriSol kutoka Marekani. Katika mkataba ule wa miaka 99, ikitokea kuna mgogoro kati yao na mwekezaji, unawalazimu wananchi husika kwenda kusikiliza kesi Uingereza hali ambayo wananchi maskini hawawezi kumudu gharama za usafiri na mawakili wa kuwasimamia ” 
alisema Kitabu.

Aidha, alizitaja kero nyingine kuwa ni kukithiri kwa aina mbalimbali za ushuru wa mazao ambao unaishia mifukoni mwa wajanja wachache hali ambayo ina lalamikiwa sana na wakulima na wafanya biashara hapa mkoani.
“Soko la Mkoa lina vibanda 356 na meza 284. Kila banda linalozwa ushuru wa sh. 15,000/- kwa mwezi, wakati meza moja inatozwa sh. 300 kwa siku ambayo ni sawa na sh.9,000 kwa mwezi. Hii ina maana kwamba jumla ya mapato yote kwa mwezi ni zaidi ya shilingi milion 7 na nusu. Cha ajabu pamoja na mapato makubwa, soko linazidi kuwa kongwe na chafu hata kufikia hatua ya kukimbiwa na baadhi ya wateja wastarabu wakiwemo baadhi ya watalii wanaokuja kutembelea Hifadhi ya taifa ya katavi” 
amesema.

Amesema endapo atapitishwa na chama chake kipaumbele chake kitakuwa kuweka mipango thabiti inayotekelezeka ikiwemo ufuatiliaji wa mikataba mibovu na usimamizi wa rasilimali zilizomo kama vile madini.
“Nina imani na chama changu ambacho kipo mbele kupiga vita ufisadi wa aina yoyote, tukiweza kupiga vita rushwa na tukasimamia vizuri rasilimali zetu na mapato yatokanayo na ushuru, maendeleo ya haraka yatapatikana katika jimbo langu na Mkoa kwa jumla” 
amesema.

Aidha,amesema Mpanda ina vipaji vingi, atahakikisha kuwa michezo ya aina yote inapewa kipaumbele ili kuinua vipaji vilivyokuwepo hapo awali.

Katika zoezi hilo la kuchukua fomu, wafuasi wa chama hicho, akina mama na vijana walimchangia pesa ya kuchukua fomu jumla ya sh.250,000.

 • via MwanaHALISI Online


Mwanri 'atoka povu' Bungeni

Serikali yamwagiza mmiliki wa Slipway kusitisha shughuli zote za ujenzi
Na Devotha Kihwelo — SERIKALI imemtaka mmiliki wa hoteli ya Slipway kusitisha shughuli zote za ujenzi zinazoendelea pembezoni mwa bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakili wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Manchare Heche alisema amri hiyo imetoka kwa Waziri wa Mazingira baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wanaozunguka hotel hiyo.

Alisema wamempa barua juzi kwa ajili ya kusitisha ujenzi uliokuwa unaendelea katika hoteli hiyo ya kuchukua vifusi na kuingiza baharini ili kupata nafasi kwa kuongeza majengo katika eneo la bahari.

Alisema endapo atakaidi kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitafuata na kupelekea kuifungia kabisa kwa kutoendelea na huduma za hoteli ndani ya nchi.
“Agizo limetoka kwa waziri ili mmiliki wa hoteli hii aachane na shughuli zote za ujenzi katika eneo hiili kutokana kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira na kuharibu eneo la bahari kwa kujaza mawe na vifusi vya michanga”,
alisema Heche.

Aidha Heche alisema mmiliki wa hoteli hiyo anapeleka vifusi pamoja na mawe makubwa katika bahari kwa kutumia katapila pindi maji yanapohama nyakati za asubuhi.

Alisema Slipway amekiuka sheria za bahari na wizara kwa kutofuata taratibu na vibali vya kufanya hivyo na kupelekea serikali kutupiwa lawama na wananchi mabazo zinafanywa na watu wachache.

Heche alisema wamefanya hivyo iwe fundisho kwa wamiliki wote wenye tabia ya kujichukulia maamuzi kwa madai serikali haiwezo kuchukua hatua yoyote dhidi yao.

Kutokana na kitendo alichofanya mmiliki huyo cha kujaza mawe na vifusi katika bahari itaundwa kamati kwa taasisai zote zinazohusika na maswala ya bahari kwa ajili ya kujadili swala hilo na endapo hawataridhishwa na watapeleka shauri mahakamani.

Alisema kutokana na kauli hiyo ya waziri watamfuatilia kwa karibu ili kufahamu kama bado anaendelea na shughuli hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafuriko katika maeneo yanayozunguka hoteli hiyo.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa sharti la kutotaja majina yao, wafanyabiashara wa eneo hilo walisema awali hawakufahamu vifusi hivyo vinakazi gani katika eneo hilo lakini waligundua kuwa vinapelekwa baharini na kushindwa kusema kwa kuhofia kufukuzwa.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa wamiliki wa maduka ya vitu vya asili alisema wamechoshwa na vifusi hivyo kwa madai kuwa imekuwa shida pindi mvua zinaponyesha kwani hukosekana sehemu ya kupita kutokana na tope pamoja na maji kutuama katika njia za maduka yao.
“Kwakweli maeneo haya imekuwa kero kwa ajili ya vifusi pamoja na magari yanayo kushusha kukosa njia pindi mvua zinaponyesha na sio sisi tu hata majiranai na watalii wanaokuja hapa wamekuwa na wakati mgumu sana pindi mvua zinapo nyesha”
Alisema mmoja wa watu hao.

Gazeti hili lilipojaribu kumtafuta mwanasheria wa hoteli hiyo kuzungumzia swala hili halkipokea simu na mwisho akazima kwa kuondoa usumbufu.

Mjengwa na Dk Salim kwenye 'Nyumbani na Diaspora'


Ndugu zangu,

Tangu nikiwa kijana mdogo wa Sekondari nimekuwa na ndoto ya siku moja kukutana na Dk Salim na kufanya nae mazungumzo ya kina na ya ana kwa ana. Fursa hiyo niliipata majuzi hapa.


Hakika, Dk Salim ni mmoja wa Watanzania waliotufanya, enzi hizo tukiwa shuleni, tutembee tukijivunia kuwa Nchi Yetu ni moja ya ' Mataifa Makubwa' kwenye siasa za dunia. Ni kupitia watu wa aina ya Dk Salim, Tanzania ilikuwa na sauti ya kusikilizwa duniani.

Na hakika, mazunguzo niliyoyafanya na Dr Salim hivi karibuni ni moja ya mazungumzo muhimu niliyopata kuyafanya ya kuweka kwenye kumbukumbu. Ilikuwa ni kama mwanafunzi aliyekutana na mwalimu aliyekuwa akimtungia maswali, na sasa mwalimu na mwanafunzi wanatafsiri kwa pamoja maana ya majibu ya maswali yale.

Ndugu zangu,

Naweza kabisa kumwelezea Dk Salim kwa maneno manne; Kiongozi, Mzalendo, Mwanamapinduzi na Shujaa.

Ndio, ni Kiongozi mzalendo, mwanamapinduzi na shujaa wa Afrika. Nyongeza muhimu; ni mtetezi wa haki za wanyonge wa dunia. Aliyaanza mapambano ya kuipigania Afrika na wanyonge wa duniani akiwa na miaka 22 tu.

Am hakika amestahili kuwa na nishani ya utumishi uliotukuka si kwa Tanzania tu, bali kwa bara zima la Afrika.

Dk Salim alinisimulia mengi; sikiliza kidogo hapa kwenye kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora'

Taarifa nzima ya Habari Channel TEN, Juni 22, 2015

Baraza la Maulamaa lamteua atakayekaimu nafasi ya Mufti Mkuu wa Tanzania

BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limemtangaza Sheikh Abubakar Ally kuwa Sheikh Mkuu na naibu Mufti baada ya kifo cha aliyekuwa mufti wa baraza hilo Sheikh Shaban Simba.

Uteuzi huo ulifanyika jana mkoani Bagamoyo mara baada ya baraza la Ulamaa lenye wajumbe 7 kukaa na kumteua Sheikh Ally kushika wadhifa huo.

Akitangaza uteuzi huo katika ofisi za makao makuu ya BAKWATA jijini Dar es salaam jana, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Suleiman Lolila alisema baraza la Ulamaa lilikaa jana likiwa na wajumbe nane ili kumteua Naibu Mufti.

Uteuzi huo ulifanyika kwa kupiga kura ya siri ambapo kati ya wajumbe wote waliohudhuria, Sheikh Ally alipata kura zote nane na hivyo kuteuliwa na kushika wadhifa huu ambao atadumu nao kwa kipindi cha siku tisini ambazo ni sawa na kipindi cha miezi mitatu.

"Kwa mujibu wa katiba yetu ya BAKWATA, Mufti akifariki dunia baraza la Ulamaa linatakiwa likae na kumteua naibu Mufti na Sheikh mkuu ambaye anatakiwa kudumu kwa kipindi cha miezi mitatu na kusimamia mchakato wa kumpata Mufti, " alisema Lolila.

Alisema kazi kubwa iliyopo kwa hivi sasa ni kuandaa mazingira ya uchaguzi na kumteua Mufti katika kipindi hiki cha miezi mitatu.

Akizingumza mara baada ya uteuzi huo, Sheikh Ally alisema amefurahi kuteuliwa kusikia wadhifa huo na yupo tayari kuitumikia jumuiya ya waislam na kuendeleza yale yote mema aliyoacha Mufti Simba na kusimamia vyema mchakato wa kumpata Mufti mpya.

"Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kuwa kwa kipindi hiki cha miezi mitatu tunampata Mufti atakayetuongoza baada ya kufiwa na mpendwa wetu Mufti Simba, " alisema Sheikh Ally.

Alisema kuwa ataendeleza umoja na mshikamano uliopo baina ya waislam pamoja na kuifanyia marekebisho katiba iliyopo ili Iweze kukidhi mahitaji yaliyopo na kuwaunganisha waislam kwa pamoja.

Akizingumzia uteuzi huo, Sheikh Hamid Jango amabaye pia ni Mjumbe wa baraza la Ulamaa, Alisema yeye aliamua kumpigia kura Sheikh Ally kutokana na anavyomfahamu na pia yeye bado ni kijana hivyo ataleta mabadikiko makubwa katika baraza hilo.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, Sheikh Ally alikuwa mjumbe wa baraza la Ulamaa kabla hata ya mwaka 2000 na pia aliwahi kuwa naibu Mufti kabla ya mabadiliko ya katiba yaliyoondoa wadhifa huo.

Wakati anateuliwa Kuwa naibu mufti, alikuwa Naibu Kadhi mkuu namba moja Kati ya wawili.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIUTEUZI WA KAIMU MUFTI MKUU WA WAISLAM TANZANIA


Muda mfupi baada ya aliyekuwa mmoja wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa la BAKWATA Sheikh Abubakar Zuberi, kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DK. Willibroad Slaa amemtembelea nyumbani kwake kumpongeza na kumtakia majukumu mema akimhakikishia ushirikiano kama jirani na kiongozi.


Sheikh Abubakar Zuber ambaye ametangazwa leo kukaimu nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa dini ya Kiislam kwa siku 90 hadi hapo atakapochaguliwa Mufti Mkuu kwa mujibu wa taratibu za dini hiyo, anaishi Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jirani na zilipo Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA.

Mbali ya kumtakia kila la heri, Katibu Mkuu Dk. Slaa amemuahidi Mufti Sheikh Zuberi kuwa CHADEMA iko tayari wakati wowote kutoa ushirikiano atakaouhitaji katika kutimiza wajibu wake huo.

“Shehe Zubeir, jirani yangu napenda kutumia fursa hii kukupongeza sana kwa namna ambavyo wenzako wamekupatia imani kubwa na kukuteua ili uwaongoze Waislam kiroho. Ni imani kubwa ambayo binafsi naamini utaweza kuitumikia wakati mkiendelea kusubiri taratibu zingine za uchaguzi.
“Nitumie fursa hii pia kusema tukiwa majirani zako hapa Mtaa wa Ufipa, tukiwa viongozi ambao tunao wanachama, wapenzi na wafuasi wetu wenye dini tofauti wakiwemo Waislam, naomba kukuhakikishia ushirikiano kutoka kwetu wakati wowote katika kutimiza majukumu yako haya makubwa na nyeti.

“Shehe wangu kwa muda wote tumeishi pamoja hapa tukiwa majirani… ukitimiza wajibu wako uliokuwa nao nasi tukiendelea kutimiza majukumu yetu katika jamii ya Watanzania, nakutakia kila la heri katika kuwatumikia na kuwaongoza kiroho Waislam wa Tanzania,” alisema Dk. Slaa nyumbani kwa Sheikh Zuberi leo mara baada ya uteuzi wa Kaimu Mufti Mkuu wa Waislam kufanyika.

Imetolewa leo Jumatatu, Juni 22, 2015 na;

Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Viongozi wa Wamasai, mbele ya UNESCO, wakubali kuacha ukeketaji

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) akimpongeza Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli kwenye semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro.

VIONGOZI wakuu wa jamii ya Kimasai wa Afrika Mashariki wameridhia kuachana na mila potofu zimezopitwa na wakati ikiwemo vitendo vya ukeketaji kwa wasichana wa jamii ya kimasai ambavyo vimekuwa vikiwaathiri wasichana hao kwa kiasi kikubwa.

Kauli ya kusitisha vitendo hivyo ilitolewa juzi Wilayani Ngorongoro na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na msaidizi wake kutoka Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni walipokuwa katika semina ya elimu ya afya ya uzazi, kupinga vitendo vya ukeketaji pamoja na mimba za utotoni.

Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Afrika Mashariki, Olaiboni Simeli alimueleza Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) na Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues kuwa jamii hiyo ya wamasai imeridhia kuacha mila zilizopitwa na wakati na itaendelea kushiriki kuelimisha jamii yao zaidi juu ya madhara ya mila hizo potofu ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni.
"...Tunaishukuru UNESCO kwa kuendelea kutoa elimu hii kwetu juu ya mila potofu nasisi tunaungana nanyi kuendelea kutoa elimu kwa jamii yetu kupinga ukeketaji na ndoa za utoto tumeelezwa athari nyingi zinazowapata wasichana wanaokeketwa...kwanini tuendelee na mila zinazoleta madhara kwa watu wetu? Tushirikiane kupiga vita hivi," 
alisema Olaiboni Simeli akizungumza mbele ya Bi. Rodrigues.

Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Naimado Olaiboni alisema hakuna haja ya jamii ya kimasai kuendelea na mila zilizopitwa na wakati ilhali mila hizo zikiendelea kuwaathiri wamasai na kuwabakiza nyuma kimaendeleo katika nyanja mbalimbali. "...Tutaendelea kushirikiana nanyi kupinga ndoa za utotoni kwa kuwa tumeelezwa madhara yake na wataalamu leo," alisema Naimado Olaiboni.

Naye Mkuu wa Shirika la UNESCO na Ofisa Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania, Bi. Rodrigues alisema anapenda kuona Jamii ya Kimasai inaendeleza mila na tamaduni zao lakini zile nzuri ambazo hazina chembe ya kiunyanyasaji kwa makundi yote. Alisema ukeketaji kwa wasichanga unamadhara makubwa kwa jamii hiyo hivyo haina budi mila hizo kupuuzwa ili kumlinda mtoto wa kike na madhara yanayomkumba anapofanyiwa vitendo hivyo.
"...Napenda kuona Wamasai wanaendeleza mila na tamaduni zao lakini ziwe nzuri na zisizo na chembe ya ukatili wala unyanyasaji, tuangalie ni namna gani tunaziendeleza na kubaki katika uhalisia wetu...nawahakikishia tutashirikiana kuhakikisha hili linafanikiwa kwenu,"
 alisema Bi. Rodrigues akizungumza katika semina hiyo.

Aidha aliwashauri jamii ya Kimasai kupunguza kuwa na idadi kubwa ya watoto na wake ilhali mume akishindwa kuihudumia familia hiyo jambo ambalo limeendelea kuchochea umaskini wa familia hizo vijijini kwani watoto wamekosa mahitaji ya msingi katika familia na kujikuta wakiishi kwa taabu.

Aliwataka Wamasai pia kupinga ndoa za utotoni kwani mabinti wadogo wanapoolewa wanakosa fursa ya elimu pamoja na kuunda familia bora kutokana na uduni wao katika masuala ya afya ya uzazi kiujumla na madhara yanayowaandama katika maisha yao. 
"...Ndoa za utotoni nazo ni tatizo katika jamii yetu, tuzipige vita maana mtoto mdogo anapoolewa haweza kuunda familia bora na wala uzazi wake hauwezi kuwa bora...,"
 aliongeza Bi. Rodrigues.

Zaidi ya wanasemina 210 kutoka Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili, Aoliani Magaidulu wakiwemo viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari na wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii Wilayani Ngorongoro wamenufaika na semina hiyo ya jitihada za kuelimisha jamii juu ya mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Susana Koillah, Mama Shughuli na mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika semina hiyo akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) kabla ya kutafsiri mada yake kwa wanasemina.
Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Mathias Herman (kushoto) akitoa maelekezo kwa wana semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi shule za sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.


Kutoka kushoto ni Mshauri na Mkufunzi wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii kutoka UNESCO Tanzania, Rose Haji pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na UNESCO juzi.

Baadhi ya washiriki wa semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakifuatilia mada kwenye semina hiyo.

Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Emanyata Ololosokwani na Mwenyekiti warsha hiyo, Ole Daniel akitafsiri kwa lugha ya kimasai mada ya Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) alipokuwa akiwasilisha.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) akimsikiliza Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli (kulia) kwenye semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) wakichangia mada mbalimbali

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

Susana Koillah, Mama Shughuli na mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika semina hiyo akisisitiza jambo. Kulia ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni (kushoto) akichangia mada katika semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro. Wengine ni wasaidizi wa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli wakishiriki semina hiyo.

Baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania wakiwapongeza viongozi wa jamii ya kimasai, Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni mara baada ya semina kumalizika.

Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni wakipiga picha za kumbukumbu na baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania baada ya semina kumalizika. Kulia ni Ofisa Mradi Elimu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Jennifer Kotta akijiandaa kuwapongeza viongozi wakuu wa jamii ya kimasai Afrika Mashariki na Tanzania walioshiriki semina hiyo.

Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Mathias Herman (kulia) akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni (kushoto) mara baada ya semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, wakuu shule za sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com, Ngorongoro

World Tourism Expo Sanganai/Hlanganani Zimbabwe yafumbua macho WatanzaniaModewjiblog team, Harare — TIMU ya watanzania walioenda kuhudhuria maonesho ya utalii nchini Zimbabwe wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza uendeshaji wa sekta ya utalii.

Walisema katika ziara yao hiyo wamegundua kwamba Wazimbabwe kuanzia wanapompokea mgeni hadi anapofika hotelini wanaonesha kujali hali ambayo mgeni hawezi kusahau hata kidogo.

Aidha amesema kwamba hata mipangilio ya kwenda kwenye vivutio inafanyika katika hali ambayo huwezi kusahau hata kidogo.

Kutokana na mazingira hayo, wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza namna ya kupokea na kuishi na wageni na kuwatengenezea taswira ambayo hawatakaa wakisahau.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog yaliyofanyika mjini Harare siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani (World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers jijini Harare.

Solomon amesema ingawa hali ya Tanzania si mbaya, watendaji katika viwanja vya ndege na mahotelini wanaweza kuangalia namna Wazimbabwe wanavyojali kazi zao na tabasamu zao nyakati zote kwa wageni .

“Si kwamba kwetu kuna shida lakini unaona watu wanavyojituma hapa” alisema Esther Solomon na kuongeza kuwa aliona jinsi walivyojipanga vizuri na wafanyakazi walikuwa na uelewa wa hali ya juu.

Esther aliongoza kundi la watu watano wa Kitanzania walioalikwa na mamlaka ya utalii Zimbabwe (ZTA) kuhudhuria maonesho hayo.Tanzania iliweka banda lake pia katika maonesho hayo ya siku tatu yaliyomalizika juzi.

Makampuni ya mawakala wa utalii aliyoambatana nayo katika safari hiyo ni pamoja na Tanzania Travel CompanyCordial Tours and TravelMberesero Tented Camp na Best Northern Tours and safaris .

Alisema safari yao Zimbabwe pamoja na ushiriki wao katika maonesho pia walifika katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini yakiwemo maporomoko ya Victoria.

Aidha walipewa nafasi ya kukagua sehemu za malazi kwa ajili ya wageni.

Alisema katika maonesho hayo wamefanikiwa kupata wageni wengi wanaoulizia namna ya kufika Tanzania na pia ushirikiano wa makampuni katika sekta ya utalii.

“ Watu wengi wamekuja kututembelea. Na wengi ni watu weusi. Mwamko wao wa kutembelea vivutio ni mkubwa.” Alisema Esther na kuongeza kuwa wamebaini kwamba ipo haja ya watanzania kuhimizwa kutembelea vivutio kwani hata nchini Zimbabwe wanaotembelea vivutio ni wananchi wenyewe.

Alisema wengi waliofika katika banda la Tanzania waliulizia namna ya kufika visiwa vya Zanzibar na pia mbuga za Tanzania.

Aidha mawakala wengi waliulizia namna ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utalii katika bara la Afrika.

Asilimia 80 ya watalii nchini Zimbabwe wanatoka bara la Afrika na waliobaki ndio wanatoka nje ya bara hili.
Pichani juu na chini ni Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.Wageni mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii zinazofanywa na kampuni yake kwa wageni waliofika katika banda la Tanzania wakati wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare.Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (wa pili kulia) akitoa maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho nane ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.


Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel ya nchini Tanzania, Joseph Waryoba (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Zambia, Felix Chaila aliyembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers ambayo yamemalizika juzi.


Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tanzania Travel Company ambayo pia imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.Timu kutoka Tanzania ambayo imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare ikiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba, Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (kulia).

 • Picha na taarifa tumeshirikishwa na Zainul Mzige wa modewjiblog


Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 22, 2015


Taarifa nzima ya Habari Channel TEN, Juni 21, 2015

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 22, 2015