Maswali magumu kumhusu Jaji Augustino Ramadhani


NIANZE makala hii kwa kuomba radhi kutokana na kushindwa kuwaletea makala katika toleo lililopita. Hiyo ilitokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Ninaomba pia kutumia fursa hii kuwatakia ndugu zangu Waislamu mfungo mwema wa mwezi Mtukukufu wa Ramadhani.

Katika makala ya hii nitaendelea kuzungumzia kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu. Na zaidi nitaelemea katika nafasi ya urais, hususan mchakato unaoendelea ndani ya chama tawala, CCM, ambapo hadi wakati ninaandaa makala hii, makada 37 wa chama hicho wameshajitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho kuwapitisha kuwania nafasi hiyo.

Lakini kabda sijaingia kwa undani, pengine ni muhimu tukumbushane kuwa wakati idadi ya makada 37 (ambayo huenda ikaongezeka) ni ya kihistoria, suala la kushtua zaidi ni ukweli kwamba miongoni mwao ni pamoja na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mawaziri kamili saba, bila kujumuisha manaibu waziri.

Nimekumbushia suala hili kwa sababu ni vigumu kufahamu serikali yetu muda huu inaendeshwaje, hasa ikizingatiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete nae amekuwa katika safari za mara kwa mara nje ya nchi (wakati ninaandika makala hii yupo nchini India).

Ukiondoa Makamu wa Rais, ambaye anakuwa kaimu Rais wakati Rais anapokuwa nje, licha ya majukumu ya kiwaziri, Waziri Mkuu na hao mawaziri wengine pia ni wabunge. Katika hili ni vigumu kufahamu wanamudu vipi kugawa muda wao kwa majukumu yao ya kiserikali, kiubunge na hayo ya kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais.

Hata hivyo, si vigumu kudhani kwamba kwa muda huu, akili na nguvu kubwa kwa makada wote waliotangaza nia zitakuwa zimeelekezwa kwenye kinyang’anyiro cha Urais. Kwa kiasi gani hilo linaathiri utumishi wao kwa umma, ni vigumu kwa sisi wengine kufahamu.

Nikirejea kwenye suala la makada wa CCM kutangaza nia zao kuwania urais, jina lililosikika zaidi wiki iliyopita lilikuwa la Jaji Mkuu wa zamani, Augustino Ramadhan. Japo jina lake lilishawahi kutajwa huko nyuma kama mmoja wa watu ‘wanaoweza kuokoa jahazi,’ lakini kwa kiasi kikubwa habari zilizosikika huko nyuma zilionekana kama tetesi tu pasi uthibitisho.

Angalau mara mbili, gazeti hili la Raia Mwema lilibeba habari zilizohusu uwezekano wa Jaji Ramadhani kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Binafsi, kwanza ninaheshimu uamuzi wa Jaji Ramadhani kwani ni haki yake ya Kikatiba kuchukua uamuzi huo. Hata hivyo, tayari kuna baadhi ya wananchi walioshtushwa kumsikia Jaji huyo akielezea kuwa amekuwa mwanachama wa CCM tangu miaka ya sitini.

Kwanza ninadhani alipitwa tu kutoa kauli hiyo kwa sababu CCM iliundwa mwaka 1977 baada ya TANU na ASP kuungana. Kwahiyo, hakukuwa na CCM miaka ya sitini.

Jaji huyo alieleza kuwa alijiondoa CCM mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya sheria, ambapo mfumo wa vyama vingi uliruhusiwa na hiyo kupelekea watumishi wa umma kutoruhusiwa kuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Japo Jaji Ramadhan anasema alijiondoa CCM wakati huo, kuna wanaokwenda mbali zaidi na kutaka uthibitisho katika suala hilo. Sote tunaijua Tanzania yetu, na kwa hakika tunawafahamu vema viongozi na wanasiasa wetu. Ni kwa mantiki hiyo, kuna wanaotaka uthibitisho kuwa kweli Jaji huyo alijiondoa CCM na kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa katika utumishi wake, ikiwa ni pamoja na Ujaji Mkuu.

Na kauli hiyo ya uana-CCM wake, kwa namna flani, imerejesha tena suala la hukumu iliyotolewa na Jaji huyo kwa kushirikiana na majiji wengine dhidi ya kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila aliyetaka mahakama itamke kuwa sheria inayozuwia mgombea binafsi ni kinyume cha Katiba.

Pasi kuingiza kiundani katika kesi na hukumu hiyo, binafsi ninaichukulia hukumu hiyo kuwa moja ya hiba (legacies) kuu za utumishi wa Jaji Ramadhani.

Kwa baadhi yetu tunadhani Jaji huyo angebaki shujaa kwa demokrasia kwa sababu mfumo wa sasa unaolazimisha wawania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa pamoja na urais kuwa wanachama wa vyama vya siasa unatupunja fursa ya kupata viongozi wa kisiasa wazalendo lakini wasiotaka kujihusisha na vyama vya siasa.

Hata hivyo, ili kumtendea haki, ni muhimu kutambua kuwa hukumu hiyo haikuwa maamuzi binafsi ya Jaji Ramadhani bali licha ya kuwahusisha majaji wengine pia, ilikuwa ni ya kisheria na sio hisia binafsi.

Lakini kwangu, licha ya dalili zinazoonekana wazi kuwa kana kwamba CCM imeshapata mgombea wake urais kufuatia uamuzi wa Jaji Ramdhan kutangaza nia, nina wasiwasi kidogo kuhusu ufanisi wake.

Kubwa zaidi ni ukweli kwamba Idara ya Mahakama, ambayo licha ya Jaji Ramadhan kuitumikia muda mrefu bali pia aliwahi kuwa mkuu wake kwa maana ya ujaji mkuu, imeendelea kuwa moja ya taasisi sugu kwa rushwa. Takribani kila ripoti inayotolewa kuhusu tatizo la rushwa katika taasisi mbalimbali za serikali nchini mwetu, Idara ya Mahakama haikosekani, na tena ikishika nafasi za juu.

Mara baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kuwania Urais, Jaji Ramadhan aliwaambia waandishi wa habari kuwa atatumia uzefu wake kupambana na ufisadi. Swali la msingi: uzoefu upi? Huohuo ulioshindwa ukiondoa Idara ya Mahakama katika orodha ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa?

Kwa upande mwingine, Jaji Ramadhan alikuwa mjumbe wa ‘Tume ya Warioba’ iliyokusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba. Sote twakumbuka yaliyomsibu Jaji Joseph Warioba na baadhi ya wasaidizi wake kupigania sio tu kazi nzuri iliyofanywa na tume yao bali pia mustakabali wa Katiba mpya.
Kwanini Jaji Ramadhani amekuwa kimya sana katika suala hilo? Je ukimya wake ulitokana na kufahamu kuwa siku moja angeomba kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM?

Na katika hilohilo, kwa vile mapendekezo ya Tume hiyo iliyomshirikisha Jaji Ramadhani yalikuwa muungano wenye muundo wa serikali tatu, je kwa vile CCM ambayo jaji huyo anaiomba ridhaa ya kumteua awe mgombea wake ina msimamo wa serikali mbili kama ilivyo sasa, hilo si tatizo angalau kimsimamo na kimtizamo?

Hadi muda huu, Jaji Ramadhani ni Rais wa Mahakama ya Afrika kuhusu haki za binadamu. Sihitaji kuorodhesha matukio lukuki ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania lakini miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na ukatili unaofanywa na Jeshi la Polisi na rushwa (naam, rushwa sio tu adui wa haki bali pia inachangia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu).

Je Jaji Ramadhani amekuwa wapi wakati ukiukwaji wa haki za binadamu ukiendelea kushamiri na kuwa kama umehalalishwa na Katiba yetu? Ni nani anaweza kusimama hadharani na kuwaambia Watanzania kuwa ‘Urais wa Jaji Ramdhani katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika umechangia hili na lile katika kutetea au kudumisha haki za binadamu nchini Tanzania’?

Niwe mkweli, binafsi ninamwona Jaji Ramadhani kama Rais Kikwete alipojitambulisha mwaka 2005 kuwania urais na hatimaye kushindwa nafasi hiyo.

Alionekana mtu mwadilifu, aliyeitumikia nchi kwa muda mrefu, na pengine kubwa zaidi, msafi (asiye na kashfa). Sifa hizo zinalingana na tunazosikia kuhusu Jaji Ramadhan. Je, kwa mfano, kuwa msafi ni sawa na kuwa na uwezo wa kuongoza nchi?

Lakini la mwisho kuhusu kada huyo ni taarifa za awali kuwa amekuwa akiombwa na baadhi ya wana-CCM kuwania nafasi ya urais (kuna wanaodai kuwa ndio mtu pekee anayeweza kumudu ‘kumzuia’ Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa asiingie Ikulu, na wengine wanasema Jaji huyo ndio ‘msafi zaidi’ kuliko makada wengine wanazowania nafasi hiyo).

Swali la msingi: je hao waliomwomba (kama ni kweli) hawafanyi hivyo kwa maslahi yao binafsi? Na je, kumwomba huko (kama ni kweli) hakutopelekea urais wa Jaji Ramadhan (iwapo atashinda) ukaishia kuwa kama ‘deni la kwa wanamtandao’ lilivyouandama utawala wa Rais Kikwete?

Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha tena Watanzania wenzangu kuwa ni muhimu tujiulize na kuwauliza wawania urais maswali magumu ili tusije kuishia kujiulaumu huko mbeleni.

Nchi yetu ipo katika wakati mgumu; umasini wa kupindukia huku ufisadi ukizidi kuimarika, uhaba mkubwa wa uzalendo, utovu mkubwa wa maadili ya uongozi ikiwa na pamoja na uhuni katika matumizi ya fedha za umma, shilingi inayporomoka kama ipo kwenye mashindano ya marathoni na kadhalika.

Tunahitaji rais ambaye si tu anajua matatizo yetu bali pia ana uzalendo na uwezo wa kukabiliana nayo. Hatuhitaji Rais msafi lakini mwoga wa kupambana na maharamia wanaoibomoa nchi yetu kila kukicha.

Hatuhitaji mtu anayeahidi kupambana na rushwa ilhali hana mfano japo mmoja wa jinsi alivyowahi kupambana na rushwa.
 • Makala ya Evarist Chahali katika gazeti la RAIA MWEMA

[video] Mkulima azungumza kuhusu fomu alizochukua CCM kuwania Urais Tanzania 2015

Kada wa CCM, Elidephonce Bilohe (43), mkulima anayeomba kupitishwa na chama chake kuwania urais, amesema anatumia usafiri wa mabasi ya umma kuzunguka mikoani kusaka wadhamini.

Bilole alisema ameshafika mikoa tisa ambayo ni Dodoma, Kigoma, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Morogoro na Dar es Salaam, tangu alipochukua fomu hiyo Juni 9.

“Huko kote nimekuwa nikienda kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria na daladala. Kwa kweli nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa makatibu wa CCM, nawashukuru sana,” alisema.

Bilohe alisema atakwenda mikoa 15 tu kama inavyotakiwa na chama chake, tofauti na watiania wengine ambao baadhi wamekwenda zaidi ya mikoa 20.

“Kwenda mkoa mmoja natumia siku mbili ama tatu kufika na kupata wadhamini. Gharama ni nyingi sana, lakini kwa kuwa nimeshaamua kuwatumikia Watanzania nitakwenda,”alisema.

Alisema Watanzania wamekuwa wakimtia matumaini katika safari yake hiyo na kuwaomba wamuombee ili aweze kuifanikisha kwa mafanikio.

“Naomba Watanzania wenzangu mniombee katika safari hii. Nitawavusha kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi,” alisema Bilohe aliyejiunga na chama hicho mwaka 2003.

Alisema kuwa atazirudisha fomu hizo Juni 30 au Julai Mosi kulingana na ratiba yake ya kukusanya wadhamini.

Jumla ya makada 39 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo na Bilohe ndiye mgombea pekee aliye na elimu ndogo ya darasa la saba, tofauti na sheria ya nchi inayotaka mgombea wa nafasi hiyo ya juu kisiasa awe na shahada.

Bilohe ni mmoja wa makada wachache waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM ambao hawajawahi kushika madaraka makubwa serikalini au ya kisiasa.


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 25, 2015

Taarifa ya Habari Channel TEN Juni 24, 2015


Taarifa ya kifo cha Mariamu-Mwajuma Musisa (Nee Mzige)DK. ALI MZIGE wa Mikocheni, Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha Dada yake MRS MARIAMU-MWAJUMA MUSISA (NEE MZIGE) kilichotokea Raleigh, North Carolina Marekani tarehe 21-06-2015. Mwili wa marehemu utaletwa Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Tutatoa taarifa zaidi mwili utakapowasili. Kwa mawasiliano tafadhali mpigie Yussuf Mhiro 0754-609-338 / 0714-979-014.Usoma taarifa hii tafadhali wajulishe ndugu jamaa na marafiki wa Ukoo wa Humbi Ziota na Musisa. Au Kaka wa Marehemu DK. ALI A. MZIGE 0713 410 531, 0754 495 998.

Inna Lillahi, wa inna ilaihi ra'ajiun.

Bobby Jindal isn't his real name


His real name isn't Bobby — it's a nickname inspired by "The Brady Bunch"

Jindal was born Piyush Jindal in Baton Rouge in 1971 to parents who had immigrated just months earlier from India. When he was 4, he asked to be called "Bobby" after one of the brothers on the popular family sitcom.

Raised Hindu, Jindal converted to Christianity in high school after a friend shared his faith with him. He would read his Bible with a flashlight in his closet, hiding his conversion from his parents.

"I read the words of Jesus Christ, and I realized that they were true," Jindal said in a 2014 commencement address at Liberty University. "I used to think that I had found God, but I believe it is more accurate to say that He found me."

Rais Kikwete akutana na Mengi


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) Dkt Reginald Mengi wakiongea na kubadilishanma mawazo Ikulu, Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kutunuku nishani kwa watumishi wa umma na wananchi waliofanya vyema na kwa uadilifu kwenye sehemu zao za kazi. Dkt Mengi alikuwa mmoja wa watu mashuhuri walioalikwa hapo Ikulu.Rais Kikwete akutana na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picjha ya kumbukumbu na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Picha: Ikulu

Tanzania passport renewal - Taarifa ya Jumuiya ya TanzaSeattle


Jumuiya ya Tanzaseattle kwa kushirikiano na wenzetu wa Portland na Idaho tulipitisha wazo la kushirikiana kumleta Ofisa wa Uhamiaji kutoka Ubalozi wetu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania uliopo Washington DC.

Watanzania mbalimbali wa maeneo tajwa wamejitokeza kujiandikisha kwa ajili ya zoezi hili. Ada ya malipo kwa ajili ya kumleta ofisa wa ubalozi kila mshiriki ni US $45. Jumuiya inatoa shukrani za dhati kwa wale wote ambao wameshawasilisha ada hiyo. Pia Jumuiya inawaomba wale wote ambao bado hawajawasilisha ada zao wafanye hivyo haraka ipasavyo kupitia akaunti ya Tanzaseattle KeyBank # 477991002247 (Tafadhali weka risiti ya malipo). Au wanaweza kuwasilisha malipo ya pesa taslim (cash) siku ya kufanyika zoezi hili. (Never too late).

RATIBA NA ADA YA MALIPO YA PASIPOTI (United Republic of Tanzania Passport).

Jumamosi TAREHE 27/6/2015 - Kuanzia saa Tatu asubuhi (9am) - Kumaliza saa Kumi na moja jioni (5pm).

Jumapili TAREHE 28/6/2015 - Kuanzia saa Tatu asubuhi (9am) - Kumaliza saa Kumi na moja jioni (5pm)

 • Ada ya malipo ya Pasipoti kwa kila Muombaji ni US $50
 • Ada ya malipo ya Posta kutumiwa Pasipoti ni US $20
 • Malipo haya kwa ofisa wa Ubalozi yatalipwa kwa MONEY ORDER siku ya Kujiandikisha.
 • Vitu vinavyohitajika kwa Muombaji.
 • Kopi Tano za Picha( Passport size 2 by 2 with Light Blue Background)
 • Kopi ya Pasipoti-Ukurasa wa kwanza (First Page) na Ukurasa wa Mwisho (Back Page)
 • Kopi ya Identification Card i.e Driver Licence
 • Kwa ambao watafanya maombi kwa ajili ya watoto wao wanaombwa kuja na Kopi ya Cheti cha Kuzaliwa cha Mtoto pamoja na Kopi ya Cheti cha kuzaliwa cha Baba au Mama wa Mtoto.

Anuani ya Pahala ni:
411 156th Ave Ne,
Bellevue WA 98007


Common Landmark to the address location is Crossroad Mall in Bellevue WA.

Kwa wale wageni wanaweza kuwasiliana na wafuatao pindi kutatokezea tatizo la kupotea njia.
 1. Emil Muta: 206 291 8835
 2. Haji R. Haji 206 302 9404
 3. Jimmy Mkude 206 499 7054
 4. Abdul Dola aka (Mayor of Seattle) 206 422 3050.

TUNAOMBWA TUZINGATIE MUDA ULIOPANGWA.

Jumuiya ya TanzaSeattle inapenda pia kuwatakia Kheri na Baraka waislamu wote kwa kutekeleza mfungo wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani. Kheri na Baraka kwa Watanzania wote.

Ahsanteni Sana.

Kwa niaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Tanzaseattle.

Wenu,

Katibu Tanzaseattle- Haji Rajab Haji.

Vyuo 3 vilivyovutiwa usajili na 16 vilivyoshushiwa hadhi na NACTE

NACTE yavifutia usajili vyuo vitatu (3) na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita (16)


Dar es Salaam, 24 Juni 2015 — Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf B. Rutayuga alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE.

“Kwa kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa,” alieleza.

Kaimu Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi vilivyopewa maelekezo ya kufanya marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yabainishwa. Hata hivyo alisema hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake.

“Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukuliwa hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbali mbali,” alifafanua

Vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information Technology cha jijini Dar es Salaam pia chenye namba za usajili REG/EOS/014.

Taassi/vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kushindwa kutiza mashart ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam, Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.

Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC – Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.

Kuhusu NACTE

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

Hatua zilizochukuliwa kuhusiana na mjamzito aliyejifungulia bafuni


MJAMZITO aliyefahamika kwa jina la Rotha Bujiku, amejifungulia bafuni karibu na zahanati ya kijiji baada ya kudaiwa kufukuzwa na wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo, kwa maelezo kuwa anajifungua kila mwaka.

Tukio hilo lilitokea wilaya ya Maswa katika mkoa wa Simiyu juzi majira ya saa 2 asubuhi baada ya mjamzito huyo kufika katika zahanati hiyo kwa lengo la kupata huduma ya kujifungulia kwa wataalamu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililovuta umati wa watu, mjamzito huyo alikataliwa kupokewa na muuguzi wa zamu aliyetajwa kwa jina la Constansia John.

Ilielezwa kuwa muuguzi huyo alikataa kumpokea kwa madai kuwa mjamzito huyo alishapewa maelekezo tangu awali kuwa anatakiwa akajifungue katika hospitali ya wilaya ya Maswa kwani amekuwa akizaa watoto kwa mfululizo.

Inaelezwa kwamba, wakati Rotha akiugulia maumivu ya uchungu, muuguzi huyo alimpigia simu ya mkononi Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Leticia Kachumi kumjulisha hali hiyo na alipofika alitaka mjamzito huyo aondoke katika eneo hilo na atafute usafiri ili aweze kufika katika hospitali ya wilaya kama alivyoelekezwa katika siku za nyuma.

“Leticia alipofika hapo zahanati baada ya kupigiwa simu na Constansia, licha ya kumuona anaendelea kulalamika kutokana na uchungu alimwamuru aondoke eneo hilo mara moja na atafute usafiri wa kumfikisha hospitali ya wilaya iliyoko umbali wa kilomita 36, kwani walishamweleza kuwa amekuwa akizaa mfululizo na hiyo ni mimba ya kumi na moja,” alisema shuhuda, Kundi Mageni.

Kutokana na hali hiyo, mjamzito huyo alilazimika kuondoka zahanati hapo bila msaada wowote na baada kufika karibu na nyumba iliyoko na zahanati hiyo, alikwenda katika bafu la nyumba ya jirani ambalo halina sakafu na kujifungulia humo na baadaye kusaidiwa na wasamaria wema waliosikia sauti ya mtoto.

“Kwa kweli huyu mama amejifungulia katika mazingira machafu na hatarishi kwa afya yake na mtoto aliyemzaa. Kwa kweli hili ni tukio la kusikitisha. Huwezi kuamini wauuguzi hao ambao ni wanawake kumtendea mwenzao ukatili wa kiasi hiki,” alisema Pili Kidesela, Diwani wa kata ya Shishiyu (CCM).

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Jonathan Budenu aliyefika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo, alisema kitendo kilichofanywa na wauguzi hao ni kinyume cha maadili ya kazi yao na hivyo ni lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wote waliohusika.


HATUA ILICHUKULIWA BAADA YA TUKIO HILO [imenukuliwa]

SAKATA LA MAMA MJAMZITO, ROTHA BUJIKU KUTIMULIWA NA WATUMISHI WA ZAHANATI YA SHISHIYU WILAYA YA MASWA MKOA WA SIMIYU NA KISHA KUJIFUNGULIA KATIKA BAFU AMBALO LILIKUWA NA MAZINGIRA MABAYA LIMECHUKUA SURA MPYA BAADA YA MGANGA MKUU WA WILAYA DR JONATHAN BUDENU KUWAHAMISHA WATUMISHI WOTE WA ZAHANATI HIYO KAMA IFUATAVYO:
 1. MGANGA MFAWIDHI WA ZAHANATI HIYO,Bw CHACHA AMEHAMISHIWA ZAHANATI YA BUGARAMA.
 2. MUUGUZI,LETICIA KACHUMI AMEHAMISHIWA KITUO CHA AFYA MWASAYI.
 3. MHUDUMU WA AFYA,COSTANSIA PAUL AMEHAMISHIWA ZAHANATI YA MAGEREZA MALYA.


Baba wa Taifa angekuwepo leo hii angesema hivi...


Kijana mwingine kuchukua fomu ya Urais kesho


CUF wasusia Kikao - Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 24, 2015


Call for applications: Economic Justice Institute

ECONOMIC JUSTICE Institute
Theme: Economic Justice in Africa: Globalization, the State and Civil Society
Date: 7 – 18 September 2015
Venue: Durban, South Africa
Application deadline: 1st of august 2015
CODESRIA is a Pan-African membership research organization established in 1973 with the broad goal of promoting the work of African and Diaspora social scientists. In partnershipwith the OSISA Economic Justice Programme CODESRIA is pleased to announce the organization of an Economic Justice Institute in Durban, South Africa from September 7-18, 2015. The theme of the Institute is ‘Economic justice in Africa: globalization, the state and civil society,’ and it will be held on the margins of the World Social Science Forum in Durbanco-hosted by HSRC and CODESRIA and whose theme is "Transforming global relations for a just world”. CODESRIA invites applications for participation in the institute from scholars, researchers, practitioners and civil society activists from the SADC region working in the areas of social and economic justice, resource governance, property rights, commodification and extension of markets, climate justice, agriculture and other issues in the broad area of sustainable development.
The discourse on sustainable economic development and related policy drivers is changing at a fast pace as the world grapples with multiple levels of turbulence involving climate change, economic and financial crises, growing income inequalities and food insecurity. Over the past 20 years notable broad frameworks for dealing with these and other challenges in a rapidly evolving global environment have included the United Nations’ Agenda 21 aimed at ensuring the achievement of sustainable development, and the Millennium Declaration and Development Goals (MDGs) aimed at improving life for the world’s poorest and most vulnerable by 2015. As the deadline for achieving the targets for the MDGs approaches, global transformations challenge long held beliefs and theories about the political economy of development,  call on practitioners involved in  developing a new global framework on the Post 2015 and Sustainable Development Goals to rethink e dominant approaches to development issues.
These shifts in policies bring with them complex challenges and new forms of struggles for socio-economic and cultural rights to which social and economic justice actors must be equipped to respond.
There is no doubt that Southern Africa needs fresh approaches to sustainable development that go beyond the traditional neo-liberal strategies of macro-economic stability and market friendly reforms. Laying institutional and social foundations for structural changes that will facilitate sustainable development, ensuring inclusive and pro-poor policies that explicitly take into account issues of gender, class and the structural causes of unsustainable and unequal development and empowering  civic actors to push for alternative frameworks should be priorities as countries develop their Post Rio+20 Sustainable Development frameworks, Post 2015 MDG frameworks, Green Economy National and Regional Strategies as well as policy responses to the prevailing financial and economic crises.
Unfortunately, in this work the commitment towards developing a transformative development agenda has not always coincided with the capacity for innovative thinking on sustainable development
Civil society activists need to upgrade skills, knowledge and strategies that challenge and critique dominant approaches to development.
The goal of the Economic Justice Summer School is to ‘cultivate a shared understanding of alternative sustainable development approaches and provide analytical tools that enable social and economic justice researchers, practitioners and activists to interpret real world conditions in a rigorous manner’
The institute will focus on tapping into participants’ experiences as a foundation for learning with a view to developing critical thinking skills, deepening subject matter knowledge and facilitating tools for advocacy. It will also draw on the expertise of leading scholars and practitioners. The specific objectives are to:
·         Support the development of knowledge and skills necessary to facilitate change and inclusive sustainable development in the region and deepen critical thinking amongst practitioners, activists and key policy makers around current issues on economics and sustainability
·         Strengthen the interaction and engagement between networks and CSOs working on economic justice related issues in SADC and sharpen their advocacy in this area

Issues covered by the institute will include development and sustainability, power, control and access to resources, resource commodification and market expansion, the evolving African state, its location in global political economies and the challenges of sustainable development,  representation, accountability and political mobilization, the environment, and climate change and prospects for transformative change in Africa. 
Application Procedures
Applications for the position of resource person should include:
1.    An application letter;
2.    A curriculum vitae;
3.    Two (2) published papers;
4.   A proposal of not more than five (5) pages in length, outlining the issues to be covered in the proposed lectures.

Applications for laureates should include:
1.    A letter indicating institutional or organizational affiliation;
2.    A curriculum vitae;
3.    A two or three pages application letter including an analysis of the relationship between the candidate working area and the problematic and concerns raised by the theme of the Economic Justice Summer School;
4.   Two (2) reference letters from scholars, researchers or activists  known for their competence and expertise in the candidate’s working area, including their names, addresses, telephone numbers and email addresses.
5.    A copy of the passport.

Application Deadline
The deadline for the submission of applications is 1rst of august 2015. Selected applicants will be notified in the first fortnight of August 2015. 

Submission of Applications
All applications or requests for additional information should be sent to:

Economic Justice Summer School
CODESRIA
Avenue Cheikh Anta Diop x Canal IV
BP 3304, CP 18524, Dakar, Senegal
Tel.: (221) 33 825 98 21/22/23
Fax: (221) 33 824 12 89
For more information, please visit: http://www.codesria.org/
Be updated via Twitter: http://twitter.com/codesria

Find out if you will be able to install Windows 10 in your device


There was a confusion in the past few days about an article regarding the upcoming Windows 10. The following a clarification as posted on Windows blog:

...Windows 10, whether you get it on 7/29 or whether you got it in a preview form through the Windows Insider Program is intended to be installed on Genuine Windows devices.
 • Do you want to continue as a Windows Insider and keep getting preview builds after 7/29?
 • Or do you want to upgrade your Genuine Windows 7 or Windows 8.1 system that has been getting Windows 10 Insider Preview builds to the 7/29 release and stop being an Insider?

“I want to continue as a Windows Insider!” If you want to continue as a Windows Insider past 7/29 there is nothing you need to do. You’re already opted in and receiving builds in the Fast or Slow ring depending upon your selection. This is prerelease software and is activated with a prerelease key. Each individual build will expire after a time, but you’ll continue to receive new builds so by the time an older prerelease build expires you’ll have received a new one. Since we’re continuing the Windows Insider Program you’ll be able to continue receiving builds and those builds will continue to be activated under the terms of the Windows Insider Program. We provide ISOs for these builds for recovery from any significant problems, but they are still pre-release software. As part of the program we’ll upgrade Insiders to what is for all intents and purposes the same build as what other customers will get on 7/29, but that will be just another build for Insiders, and those who stay in the program will simply get the next build after as well.

I want to opt out of the Windows Insider Program on 7/29.” If you decide to opt-out of the program and upgrade to the 7/29 build you will be subject to exactly the same terms and conditions that govern the offer* that was extended to all Genuine Windows 7 and 8.1 customers. This is not a path to attain a license for Windows XP or Windows Vista systems. If your system upgraded from a Genuine Windows 7 or Windows 8.1 license it will remain activated, but if not, you will be required to roll back to your previous OS version or acquire a new Windows 10 license. If you do not roll back or acquire a new license the build will eventually expire.