Tangazo la Polisi la kuitwa kwenye usaili kwa wahitimu 2014

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Majina pia yapo kwenye tovuti ya TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa/Wilaya iliyo karibu nawe ukatazame endapo jina lako ni miongoni mwa walioitwa. 

Usaili utafanyika katika miji ya makao makuu ya mikoa Tanzania Bara kwa tarehe zilizooneshwa kwenye jedwali lililopachikwa kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi (www.policeforce.go.tz).

Hotuba ya Rais wa Zanzibar, Dk Shein wakati wa kuvunjwa kwa Baraza la Wawakilishi

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu Ameir Kificho alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na kulifunga rasmi Baraza la nane la Wawakilishi katika ukumbi wa Baraza Chukwani jana.

Derick Magoma arudisha fomu za CHADEMA za kuomba kuteuliwa kuwania UbungeMagoma akirudisha fomu za kuomba tiketi ya CHADEMA ya kuwania Ubunge katika jimbo la Hanang.


Watuhumiwa 3 wafuasi wa Al-Shabaab wauawa katika majibizano ya risasi na Polisi Morogoro


Wananchi waliotoa taarifa wamesaidia vyombo vya ulinzi na usalama kuwakurupusha na kuwaua watu watatu -- wawili kati yao wakisadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabaab -- katika mapigano baina yao na jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Musa Marambo amesema tukio hilo limetokea Juni 24 mwaka huu katika eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu hao walikuwa wamejificha msituni.

Amesema jeshi hilo linawashikilia watu 6 kati ya 50 kwa kuhusika na tukio hilo, na msako mkali unaendelea ili kuwamamata wote wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu wa kigaidi kwani ilikutwa mikoba, majambia na bunduki aina ya short-gun katika eneo la msitu wa Njeula katika kijiji cha Mziha, Turiani, Morogoro.

Taarifa kutoka katika hospitali ya Misheni ya Turian mkoani Morogoro zinasema kuwa maiti watatu wamehifadhiwa hapo ambapo kati yao, watatu wanaonekana kuwa ni watu wasio na wajihi wa Kitanzania huku mmoja akiwa ni mtu alijyeeruhiwa vibaya na badaye kufariki akiwa hospitalini hapo.
Rais Kikwete, Makamu Dk Bilal waongoza kuuaga mwili wa Mbunge, Donald Max


Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 


Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 


Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 


Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Juni 27, 2015 kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max.

Picha: Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), Dar es Salaam.

M/Kiti, Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo.

Rais Kikwete katika hafla ya kuadhimisha miaka 2 ya kutawazwa Francis kuwa Papa


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es Salaam

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 27, 2015

Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 27, 2015


CHADEMA Moshi (V) warudisha fomu za kuwania Ubunge na UdiwaniMwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Moshi vijijini, Godlisen Maramia akipokea fomu kutoka kwa Deogratius Mushi ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini wakati aliporudisha katika ofisi za chama hicho zilizopo Majengo.

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Moshi Vijijini, Godlisen Maramia akimpongeza mtia nia Deuogratius Mushi kwa uamuzi wa kuingia katika kinya'ng'anyiri cha kuwania nafasi hiyo.Mushi akipongezwa na makada wengine wa CHADEMA waliofika kumsindikiza ofisnini hapo.Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Moshi vijijini, Godlisen Maramia akipokea fomu toka kwa Tally Kisesa ya kuwania Ubunge wa viti maalumu katika jimbola Moshi vijijini.

Mtia nia wa nafasi ya Udiwani katika kata ya Kindi, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Michael Kirawira akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi ya CHADEMA kata ya Kindi.Wananchi wa kata ya Kibosho Magharibi wakimlaki Mgombea wa nafasi ya Ubunge Deo Mushi ambaye pia ametangaza kuwania nafasi ya Udiwani katika kata hiyo.Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini,Deogratius Mushi,akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuasili katika kata hiyo.Deo Mushi ambaye pia ni mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Moshi vijijini ,akizungumza na baadhi ya wananchi katika kata ya Kibosho Magharibi .Baadhi ya wananchi waliohudhuria kikao hicho.Deo Mushi akizungumza.

Mbali na kuwania nafasi ya Ubunge, Deogratisu Mushi pia amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya udiwani katika kata ya Kibosho Magharibi na hapa akikabidhi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA katika kata hiyo Kikas Mmasi.Mwenyekiti wa CHADEMA katika kata ya Kibosho Magharibi Kikas Mmasi akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kupokea fomu ya Deo Mushi.

Tumeshirikishwa picha-tarifa hii na Dixon Busagaga

Kinana na Nape katika mbio za mchakamchaka MwanzaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiongoza mazoezi ya Jogging, yaliyoandaliwa na Vijana mkoani Mwanza leo asubuhi, kwa lengo la kujenga mwili na kukuza mshikamano miongoni mwa vijana hao. Kinana na Nape wapo mkoani humo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiongoza mazoezi ya Jogging, yaliyoandaliwa na Vijana mkoani Mwanza leo asubuhi, kwa lengo la kujenga mwili na kukuza mshikamano miongoni mwa vijana hao. Kinana na Nape wapo mkoani humo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama.Jogging ikiendeleaPius Ntiga wa Uhuru FM ambaye yupo katika ziara ya Kinana mkoani Mwanza akitokwa kijasho chembamba wakati wa Jogging hiyoVijana wakifanya amsha amsha wakati wa Jogging hiyoMkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Konisaga akiwa kwenye Jogging hiyoWashiriki wa Jogging hiyo wakiwa katika ushirikiBaadhi ya wananchi wakiwa wametoka kutazama jogging hiyomtaani jijini MwanzaKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwashukuru Vijana kwa kumshirikisha katika Jogging hiyo, ilipomalizika katika eneo la stendi ya Daladala baada ya kuanzia New Mwanza Hotel. 

Picha tumeshirikishwa na Bashir Nkoromo, Adam Mzee

Ujumbe wa leo: Amka Mtanzania - Ni wakati wa #TeamTanzania, achaneni na #TeamMatumboYaWatu

Ujumbe ufuatao nimeunukuu ulivyo kutoka kwenye kundi moja WhatsApp...

AMKA TANZANIA

Mpuuzi yeyote hufurahi mno anapomwona mtu analalamika, na mimi nasema Watanzania tulio wengi tunachukua muda mwingi mno kulalamika na si kuweka mipango, Oktoba ni kesho kutwa na tumeshamwona nani mwenzetu na nani mpuuzi, tufanye maamuzi, majitu sahiz yamekomaa na #team badala ya kupigania Nchi, hela zikiisha yalizohongwa ndo utayasikia yanalalamika shemeji katufanya hivi shemeji katufanya vile ujinga mtupu, hivi tumerogwa na nani?

Mkulima unadanganywa na sera dhaifu za kilimo kwanza, kilimo kiko kijijini pembejeo ziko Dar zinafanya nini? Kulima mnalima, masoko hakuna na wala hakuna anayejishughulisha na hilo, mtakufa njaa nyie

Kijana unapelekwa VETA kusomea ufundi, Viwanda hakuna huo ufundi unaupeleka wapi zaidi ya kuanzisha vijiwe vya kutengeneza vibatari, shtuka mtanzania

Hospitali hazina Dawa, unaenda Hospitali ya Wilaya hadi Panadol eti unaelekezwa kanunue duka lilee, hilo Duka la mtu binafsi lilipataje Dawa hospitali ikakosa?

Kila siku majitu mazima yanapiga kelele eti vijana mjiajiri, vijana mjiajiri, familia zao Baba, Mama, Mtoto, wote wajumbe wa NEC, saa ngapi watajua kama Mtaji ni tatizo? Hivi unawezaje kujiajiri bila mazingira wezeshi?

Wafanyakazi wengi wanakufa maskini kwa sababu Serikali inawanyonya mpaka kwenye mifupa, mtu mshahara 400,000/= halafu take home 290,000/=, kweli are you serious? Huko mijitu bila aibu inasema tumeongeza mafao ya wastaafu kwa 100% (kutoka 50,000/= hadi 100,000/=) kweli, yani mzee aliyelisotea Taifa lake kwa zaidi ya miaka 30 ya maisha yake leo unaona raha kumpa Mil.1 kwa mwaka is it possible, aibu huwa mmezihifadhi wapi mnapotamka mambo kama haya? Mzee huyu bila shaka hata kiinua mgongo chenyewe alipata Mil.7, leo hii Mbunge mmoja anajinyakulia Mil. 230, halafu eti majitu hata hayashtuki?

Tatizo la watanzania tumeshakubali kutenganishwa, hatuko pamoja tena, ukiona mfanyabiashara anasumbuliwa na miradi isiyoeleweka kama ile ya mashine za EFD basi wewe Mwalimu unaona halikuhusu, unapomwona Mkulima analalamika Pembejeo basi wewe Dereva wa Basi unaona halikuhusu wakati huo huo unasahau kama familia yako inategemea Kilimo, amkeni watanzania, tuzungumze kama Taifa, tunategemeana ktk mahitaji, udogo wa mshara wa Mwalimu una athari ya moja kwa moja kwako mfanyabiashara wa Viazi

Wakati wa kumwondoa asiyefaa ni sasa, kajiandikishe, mwamshe aliyelala mwambie Nchi imeshauzwa, mwambie ukweli kwamba Mwekezaji wa madini anapokuja anapewa miaka5 ya kufanya kazi bila Kodi huku mzawa akifungua kibanda cha Saluni, hata kabla hajamaliza kukipaka rangi anatakiwa aonane na TRA, mwambie mwaka jana pekee ripoti ya CAG inaonyesha zaidi Bilioni 800 zimepigwa na familia zisizozidi sita, ndo mfumo wa sasa.

Ni wakati wa #TeamTanzania, achaneni na #teammatumboyawatu