Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 29, 2015
Serengeti voted the Best Safari Park of AfricaSafariBookings.com has published the definitive list of Africa’s best safari parks. The in-depth study analyzed more than 3,000 reviews from safari tourists and industry experts alike. After careful consideration, Serengeti National Park in Tanzania was rated the best safari park of Africa.

In total 3,008 reviews were collected via the SafariBookings website. The 2,234 user reviews were contributed by safari tourists from 63 countries. To complement these user reviews, reputable guidebook authors (working for Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint) teamed up in the SafariBookings Expert Panel and wrote another 774 expert reviews.

The analysis of these reviews resulted in the list of Africa’s top 50 safari parks. With an average rating of 4.89 out of 5, Serengeti came out first and was crowned Africa’s Best Safari Park.

It is important to note that the reviewers who have been on multiple safaris rated the Serengeti 16% higher than any other park. The guidebook authors from the Expert Panel also rated the Serengeti highest. These veterans tend to be more critical in their reviews because they can compare the Serengeti to a host of parks they’ve visited in various countries. Regardless, the Serengeti came out on top, justifying its first place all the more.

Source: www.safaribookings.com

Mbinu mpya ya kusafirisha dawa za kulevya kwa kutumia taulo

Wafanyabiashara wanaposafirisha dawa za kulevya kama heroine au cocaine huziweka kwenye mfumo wa kimiminika kisha taulo wanalitumbukiza kwenye maji ya dawa na kuanika kwenye jua.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzoa, alisema hayo katika mahojiano maalum na gazeti la NIPASHE Jumapili.

Alisema taulo husafirishwa kama nguo nyingine na wanapofika nchi husika huliloweka kwenye maji na kulikamua ili kutoa dawa hizo.

Alisema mbinu hiyo ilibainika kupitia mkutano uliofanyika nchi ya Seychelles wiki iliyopita ambapo moja ya washirika kwenye mapambano hayo aliielezea kama changamoto mpya.

Alitaja mbinu nyingine inayoendelea kutumiwa kuwa ni usafirishaji wa vibashirifu ambavyo ukamataji wake huhitaji kutumia mbwa. Alisema baada ya Mtanzania kukabiliwa na kesi za namna hiyo, walizungumza na Afrika Kusini ambapo wengi huvipeleka huko ili nao wabadili njia za ukamataji.

Alisema mbinu nyingine ni kubadili uelekeo wa usafirishaji ambapo kama alikuwa anaenda Afrika Kusini atapita nchi nyingine kupoteza ushahidi na kwenda alikokusudia.

Kuhusu sheria mpya, Kamanda Nzoa alisema, itaanza kutumika wakati wowote ambapo mshitakiwa atakapokutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha.

Kamanda Nzoa alisema Rais Jakaya Kikwete, ameshaisaini sheria hiyo na itawahusu wenye tabia ya kuwakodishia nyumba wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ambao mara baada ya kukamatwa hudai hawajui chochote.  

Alisema baada ya changamoto nyingi kujitokeza dhidi ya vita hiyo, wameamua kubadilisha sheria.
“Sheria ya sasa tofauti na mwanzo, itakuwa haionyeshi thamani ya mzigo aliokutwa nao mhusika, mzigo uwe mdogo au mkubwa wote kifungo ni cha maisha jela,” alisema.

Alifafanua, tofauti nyingine ya sheria ya sasa na ya zamani, hii mpya imeongezwa vibashirifu vya kutengenezea dawa hizo ambavyo ni moja ya mbinu za wasafirishaji zinazotumika kusafirisha dawa hizo.


Orodha ya "watangaza nia CCM 2015" waliochukua na kurejesha fomu

Antony Chalamila (66), mwania Urais wa Tanzania 2015 akiwa ni mwanachama wa 41 kuchukua fomu ya kuomba kupitishwa na CCM kuwania kiti hicho, hapa akitembea kwa mguu kutoka ofisi za chama hicho hadi stendi ya mabasi kutafuta usafiri wa kumrudisha mkoani Morogoro. Kwa taarifa zake zaidi, bofya hapa kusoma gazeti la MWANANCHI

Wakati vikao vya uteuzi wa kada atakayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika nafasi ya urais vikitarajia kuanza wiki ijayo mjini Dodoma, imebainika kuwa mikoa ya Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kuwa na makada wengi waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa mikoa hiyo ambayo ni Mwanza, Geita, Kagera, Mara, Simiyu na Shinyanga ina makada tisa wa CCM waliochukua fomu kuomba kuteuliwa na chama chao kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Makada hao ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira, Mbunge wa Afrika Mashariki, Charles Makongoro Nyerere, Mbunge wa Kuteuliwa, Prof. Sospeter Muhongo (Mara) Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (Geita), Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk. Titus Kamani (Simiyu), Balozi wa Urusi, Patrick Chokala, Mbunge wa Sengerema , William Ngeleja , Luhaga Mpina (Mwanza), na mtoto wa marehemu Jaji Francis Nyalali, Peter Nyalali (Kagera).

Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ina wagombea saba na Kanda ya Kaskazini inafuatia kwa kuwa na wagombea sita waliojitosa katika kinyang’anyiro hicho.

Makada wa CCM waliojitokeza katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof Mark Mwandosya, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, na Musa Mwapango (Mbeya), Mkurugenzi Mstaafu wa Usalama wa Taifa, Hassy Kitine, Dk. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Fedha mstaafu, Monica Mbega (Iringa).

Kanda ya Kaskazini makada wa CCM waliojitosa kuwania urais ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (Arusha), Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha Rose Migiro , Dk.Muzzamil Kalokola, Litha Ngowi na Hellen Elinawinga (Kilimanjaro), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (Tanga).

Kanda ya Kati inafuatia ikiwa na wagombea watano ambao ni Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangallah (Tabora), Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (Singida), na Dk. Mwele Malecela (Dodoma).

Wagombea kutoka visiwa vya Zanzibar ni Balozi Amina Salum Ali, Makamu wa Rais, Dk.Mohamed Gharib Bilal, Balozi Ali Karume na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustine Ramadhani. Aidha, Kanda ya Kusini ina makada wawili ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (Lindi).

Kanda ya Magharibi imekuwa ya mwisho kutokana na kuwa na kada mmoja aliyechukua fomu ambaye ni mkulima Lidephonce Bilohe (Kigoma).

Hata hivyo, wapo makada wengine waliojitokeza ambao ni Amos Siyatemi, Samwel John, Leonce Mulenda, Boniface Ndengo, Maliki Marupu na Veronica Kazimoto.

Hadi kufikia jana, takwimu zinanyesha makada 40 wameomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti hicho, Vikao vya CCM vitaanza Julai 5, mwaka huu mjini Dodoma na Julai 11 kutafanyika mkutano mkuu kwa ajili ya kuchagua kada mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.

Kanda ya Mashariki ya Pwani inahusisha mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Mkoa wa Pwani ambapo hadi sasa hakuna aliyejitokeza. ZANZIBAR

Kwa upande wa Zanzibar hadi sasa, makada wa CCM wanaoiomba nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Balozi Amina Salum Ali, Balozi Ali Karume na Jaji Mkuu mstaafu Augustine Ramadhani.

Makanda wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Amos Robert Siyatemi, Musa Mwapango, Peter Isaiah Nyalali, Leonce Nicholas Mulenda, Boniface Thomas Ndengo na Lidephonce Bilohe.

Kada wa CCM, Helena Elinawinga akionyesha begi lenye fomu za kuomba kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM, baada ya kukabidhiwa jana katika makao makuu ya chama hicho, mjini Dodoma. (Picha na Edwin Mjwahuzi)

FORMER Prime Minister Frederick Sumaye is on Monday scheduled to return his nomination forms for presidential bid on the ruling Chama Cha Mapinduzi at the party's headquarters here.

The CCM Secretary for Organisation, Muhammed Seif Khatib, said the number might increase taking into account that the deadline for returning the forms is near.

He said unlike when they were picking up the forms, there was a clear schedule but when returning it is done according to who finished his/her assignment the earliest.

The number of candidates seeking nomination has reached 42 and the deadline set for returning forms is July 2, though he said there will be no penalty for those who will fail to do so.

Others who have returned forms are as of yesterday include Minister for Transport, Samwel Sitta, Vice-President, Dr Mohammed Gharib Bilal, Makongoro Nyerere, Dr John Magufuli, Stephen Wassira, Ambassador Ali Abeid Karume, Dr Titus Kamani, Boniface Ndengo, Mathias Chikawe, Prof Sospeter Muhongo, Ambassador Amina Salum Ally, retired Chief Justice Augustino Ramadhani, Leonce Mulenda and Prof Mark Mwandosya, the Minister in the President's Office (Special Duties).

Those who are yet to return their forms include Prime Minister Mizengo Pinda, Minister for East Africa, Dr Harrison Mwakyembe, retired Prime Minister, Frederick Sumaye and Ex-premier Edward Lowassa.

Others are Dr Asha-Rose Migiro, Monica Mbega, Dr Mwele Malecela and Ritha Ngowi, the Minister for Natural Resources and Tourism, Lazaro Nyalandu, the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Bernard Membe, Deputy Minister for Finance Mwigulu Nchemba, Deputy Minister Communication, Science and Technology, January Makamba.

Others are Sengerema member of Parliament William Ngeleja, Nzega MP, Dr Hamis Kigwangala, Dr Hans Kitine, Ambassador Augustino Mahiga, Prof Sospeter Muhongo, a farmer from Mjimtala village in Kasulu District, Kigoma Region Wil Eldefonce Bilohe.

Also waiting to return the forms before the July 2 deadline are Kisesa Member of Parliament Luhaga Mpina, Amos Siyantemi, Godwin Mwapongo, Peter Nyalile, Joseph Chaggama, Ambassador Patrick Chokala and Mzumbe University student Amos Robert and Maliki Malupu.

TERDO yatoa Ripoti ya Tathmini kwa wananchi kuhusu "watangaza nia CCM"

TERDO yatoa Ripoti ya Tathmini juu ya watangaza nia wa CCM kwa kutumia maoni ya wananchi juu ya vipaumbele mbalimbali walivyotoa.Rais Kikwete awavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 Magereza

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Casmir Minja akimkarisha Rais Jakaya Kikwete (kushoto) katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufunga mafunzo ya uofisa wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo. Maafisa 104 wa kozi hiyo walihitimu mafunzo hayo na kuvishwa vyeo hivyo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.


Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Casmir Minja akitoa hotuba yake kabla ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo. Katika hotuba yake CGP Minja alisema jeshi lake linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu mkubwa wa nyumba za askari na maafisa Magereza.


Kikosi cha gwaride wa Askari wa Jeshi la Magereza la zamani (askari jela) likionyesha jinsi kipindi cha zamani jeshi hilo lilivyokuwa linafanya gwaride lake katika sherehe na shughuli mbalimbali za Jeshi hilo. Tukio hilo lilifanyika kabla ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo katika sherehe iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride liloandaliwa kwa ajili yake na wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kabla ya kuyafunga mafunzo ya Cheo cha Mrakibu Msaidiziyaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.


Rais Jakaya Kikwete (wakumi kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Maafisa wa Jeshi la Magereza, wahitimu pamoja na wageni waalikwa, baada ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi pamoja na kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa ajili ya kuzungumza na askari, maafisa wa Jeshi la Magereza pamoja na wageni waalikwa na baadaye kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema Jeshi hilo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa Magereza.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia), akimkarisha Rais Jakaya Kikwete kuketi baada ya kukagua gwaride la wahitimu 104 wa kozi ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kabla ya Rais huyo kuyafunga mafunzo hayo katika sherehe iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.


Rais Jakaya Kikwete akimvisha muhitimu Amina Lidenge, Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya wenzake 104 waliomaliza mafunzo hayo katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo baada ya kuyafunga aliweza kutembelea mabanda na kuonyeshwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza, wageni waalikwa na wananchi wakati akiyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshihilo na kuwatunukia vyeo vya Warakibu Wasaidizi 104. Katika hotuba yake Rais Kikwete aliwapongeza wahitimu hao kwa kutunukiwa vyeo hivyo, na pia aliwataka maafisa wa Jeshi hilo wafuate sheria kwa wawatendea haki Mahabusu na Wafungwa katika magereza nchini.

Kikosi Maalumu cha Ukakamavu cha Jeshi la Magereza (KMKM) kikimuonesha Rais Jakaya Kikwete na wageni waalikwa (hawapo pichani) jinsi kikosi hicho kinapokuwa kazini wakati wanapopambana na wahalifu wa aina tofauti. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Kikosi cha Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) katika sherehe ya ufungaji wa mafunzo hayo ya Cheo cha Mrakibu Msaidizi yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wahitimu 104 walivishwa cheo hicho. Ufungaji wa mafunzo hayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo Rais KIkwete alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.


Rais Jakaya Kikwete akiiangalia bilinganya wakati alipokuwa anatembelea mabanda yenye bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Jeshi la Magereza nchini. Rais Kikwete alitembelea maonyesho hayo maalumu yanayofanyika kila mwaka katika Siku ya Magereza, mara baada ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo, katika tukio lililofanyika Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Kilimo wa Jeshi hilo, Yesaya Kitundu. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.

Picha zote: Felix Mwagara / Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Saluti ya Kinana kwa wakazi wa Mwanza

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapigia saluti maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza. (Picha: Bashir Nkoromo)

Rais Kikwete awapokea vijana waliosafiri kwa baiskeli km 830 kumpongeza

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda(2) mmoja wa Wapanda baiskeli wawili kati ya wanne waliofunga safari kwa baiskeli kwa kilomita 830 kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam kwa madhumuni ya kumpongeza Rais jakaya Mrisho kikwete kwa uongozi bora ulioleta maendeleo na mabadiliko mengi katika miaka yake 10 ya uongozi kwenye viwanja vya Ikulu Dar es sSlaam Jumapili Juni 28, 2015. Wapanda baiskeli wenzao wawili wamerudi jijini Mbeya kwa ajili ya Uzinduzi wa Albamu yao ya muziki ya kuhamasisha kuhusu mambo muhimu ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Bw. John Mwaipyana (27)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia kitabu maalumu alichopewa na kiongozi wa msafara Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25) na Bw. John Mwaipyana

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia kitabu maalumu alichopewa na kiongozi wa msafara Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25) na Bw. John Mwaipyana

Kiongozi wa msafara Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25) (kulia) na John Mwaipyana (27)

Kiongozi wa msafara Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25) (kulia) na John Mwaipyana (27)

Rais jakaya Mrisho Kikwete akimwangalia Bw. John Mwaipyana (27) akionesha uwezo wake wa kucheza sarakasi kwa baiskeli aina ya Phoenix.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru na kumpongeza Kiongozi wa msafara Bw. Wiseman Mwakyusa Luvanda (25


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru na kumpongeza Bw. John Mwaipyana (27).


Picha: Ikulu

Rais Kikwete afunga mafunzo kwa maafisa wa jeshi la Magereza
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la wahitimu 104 wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam jana Juni 27, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Megereza Amina Juma Lidenge kwa niaba ya wahitimu wenzake 104 wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku cheto Mwanafunzi Alyefanya Vizuri Katika Masomo ya darasani Inspekta Saidi Jacob Seni wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015


p9: Rais Kikwete akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja ithabati rasmi kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo cha Ukonga iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015


Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe akipogea ithabati rasmi kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo cha Ukonga kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015


Rais Jakaya Mrisho kikwete akifunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015


p10: Askari Magereza wa enzi za Mkoloni wakionesha ukakamavu wao mbele ya Rais Kikwete wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na maafisa wanaoshughulikia kitengo cha SACCOS cha Magereza kwenye banda la maonesho ya sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam Juni 27, 2015p3: Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja wakifurahia samani katika banda la maonesho ya sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam jana Juni 27, 2015

Rais Jakaya Mrisho kikwete na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja wakiwa na Wakuu wa Jeshi la Magereza wa nchi za SADC na Kenya waliohudhuria sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam Juni 27, 2015
Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja wakiwa na wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam Juni 27, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu wa Magereza Wastaafu. Kutoka kulia ni Mhe. Augustine Nanyaro, Mhe. Nicas Pius Banzi, Kamishna Generali Mkuu wa sasa John Minja, Rais Kikwete, Alhaj Jumanne Mangara, Mzee John Mwanguku, na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji Mstaafu Mama Aziza Mursali sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam Juni 27, 2015.

Picha: IKULU

Taarifa ya Habari ya Juni 27, 2015 Channel TEN


Mapitio ya magazeti ya Juni 28, 2015 kwenye Tv